Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Oliver Daniel Semuguruka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA K.n.y. MHE. KABULA E. SHITOBELA aliuliza: - Je, Serikali imefikia wapi kuhusu kufanya uchunguzi ili kujua chanzo cha ugonjwa wa saratani katika Mkoa wa Mwanza na Kanda ya Ziwa na ina mpango gani wa kudhibiti ongezeko la ugonjwa huo?

Supplementary Question 1

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa majibu masuri ya Serikali, ninalo swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, ni lini Serikali itaiwezesha hospitali zote za kanda kutoa huduma ya tiba ya kansa kwa asilimia 100?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa jinsi ambavyo anahangaika na matatizo ya wananchi na akinamama wa Kagera, lakini jinsi ambavyo anashirikiana na Wabunge wa majimbo kwa kuwafuata kwenye viti vyao na kuwauliza mambo ambayo wanaweza wakafuatilia kwa pamoja. Hili linaonesha ni kwa nini umeaminika miaka iliyopita na sasa unaendelea kuaminika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, labda niseme tu kwamba Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan, amenunua kifaa chenye thamani ya shilingi bilioni 18 ambacho ni kifaa pekee kwa Afrika Mashariki kwa sasa na viko vitano tu kwa Afrika ambacho kina uwezo wa kusaidia kupima kansa na kiko Ocean Road na kinazalisha mionzi ambayo ilikuwa tunaenda kuchukua Afrika Kusini. Kwa maana hiyo sasa mionzi iliyokuwa inachukuliwa Afrika Kusini hata nchi za Afrika Mashariki sasa watakuwa wanachukua hapa Ocean Road.

Mheshimiwa Spika, lakini hiyo haijatosha kwa Kanda ya Ziwa; kwa Kanda ya Ziwa tayari Serikali imepeleka shilingi bilioni 7.4 kwa ajili ya kuboresha miundombinu pale na kununua vifaa ili kuweza kutoa huduma pale kwa asilimia 100, KCMC imeshapelekwa shilingi bilioni sita kwa ajili hiyo na kwa upande wa Kanda ya Mbeya sasa hivi tukio kwenye hatua, inatakiwa ufanyike ujenzi kujenga kituo kimoja ambacho kinashughulikia kansa kwa eneo lote. Tayari michoro imeshachorwa na sasa tathmini inafanyika ili kujua sasa ni shilingi ngapi itumike hiyo kazi ianze mapema. Ahsante sana. (Makofi)