Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Angelina Adam Malembeka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ANGELINA ADAM MALEMBEKA aliuliza: - Fursa zimetolewa kwa watu binafsi kuanzisha ranchi, mashamba na bustani za wanyamapori? Je, ni wanyama wa aina gani wanaruhusiwa kufugwa na utaratibu gani unaotumika kuwapata na Serikali ina mkakati gani kuhakikisha wanyama hao hawasafirishwi kwenda nje ya nchi?

Supplementary Question 1

MHE. ANGELINA A. MALEMBEKA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa fursa ya kuuliza maswali ya nyongeza. Kwanza nimpongeze Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri yanayoeleweka na ambayo yamenijenga zaidi.

Mheshimiwa Spika, maswali yangu mawili ni kwamba; kwa kuwa fursa kwa watu binafsi ya kuanzisha ranchi, mashamba na bustani za wanyamapori imetolewa.

Je, hadi sasa ni watanzania wangapi wamepata fursa hiyo?

Swali la pili nilitaka kujua, kutokana na utaratibu huo hadi sasa hivi Serikali imepata faida kiasi gani? Ahsante. (Makofi)

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Angelina Adam Malembeka, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwa sasa jumla ya ma-butchery 71 ambayo yamekwisha sajiliwa na yanafanya kazi na kwa ujumla sasa siwezi kujua idadi lakini wamiliki ni pamoja na kuwa na leseni na kwa sasa hivi leseni zilizosajiliwa ni 71. Lakini pia faida zake tulizozipata ni pamoja na kupokea mapato jumla ya shilingi 229,500,000; lakini pia tumeweza kuongeza ajira kwa wananchi ikiwemo Madaktari wa Mifugo ambao wanapaswa kuajiriwa kwa kila mwenye butchery au shamba, bustani au ranchi ili kuwezesha hawa wanyama kupata huduma za kitabibu. Lakini pia tumeongeza ajira katika wahudumu wanao wahudumia hao wanyamapori ambao wapo katika ranchi hizo ama bustani. Ahsante. (Makofi)