Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Neema Gerald Mwandabila

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NEEMA G. MWANDABILA aliuliza: - Je, nini mkakati wa Mahakama kutoa hukumu ya pande mbili hasa mtuhumiwa anaposhinda kesi kuepuka usumbufu kufungua kesi mpya ya kulipwa fidia?

Supplementary Question 1

MHE. NEEMA G. MWANDABILA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa mchakato uliopo unapoteza haki ya watu wengi kwa kutokupata haki zao kwa wakati, lakini wakati mwingine kwa watu wengine kushindwa kurudi Mahakamani kwa hofu na woga: Je, ni lini Serikali itakuja na sheria ambayo inatoa haki kwa wakati huo huo wa hukumu? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia swali la pili; kumekuwa na utaratibu kwa watu kufunguliwa kesi baadaye kesi hizo zinafutwa, anafunguliwa kesi nyingine mbadala; je, ni vigezo gani vinatumika kumbadilishia mtu kesi kutoka ile kesi ya awali kuja kesi ya pili? Ahsante. (Makofi)

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Neema, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, suala la kufanya marekebisho madogo ya sheria kwenye eneo hili tunalichukua na tunakwenda kulifanyia mchakato ili tuone kama kuna sababu zozote za kufanya hivyo na Bunge lako Tukufu litajulishwa.

Mheshimiwa Spika, kuhusu mabadiliko ya kesi wakati umeshitakiwa kwa kosa hili na baadaye unapelekwa kwenye kosa lingine, hilo linategemea sana mwenendo wa upelelezi ambao unaweza ukabaini uhusiano wa tukio lile na tukio lingine ambalo linakupeleka kwenye mashtaka mapya. Ahsante. (Makofi)