Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Regina Ndege Qwaray

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. REGINA N. QWARAY K.n.y. MHE. SAMWELI X. HHAYUMA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kufanya utafiti wa kujua sababu za kusambaa kwa maji ya Ziwa Bassuto na kuhama kwa samaki kwenye Ziwa Eyasi?

Supplementary Question 1

MHE. REGINA N. QWARAY: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi, mwaka 2020 Mheshimiwa Waziri wa Mazingira alifanya ziara kule Ziwa Bassuto na aliahidi kwamba atatuma timu ya wataalam ili waje kufanya tathmini kuona namna gani wanaweza kudhibiti madhara yanayoendelea kuwapata wananchi wa eneo hilo. Lakini kwa majibu haya ya Serikali sasa wananchi wategemee nini?

Mheshimiwa Spika, kipengele cha pili, ni lini Serikali sasa itatafuta fedha kwa ajili ya kuboresha mazingira ya Ziwa Bassuto kwa sababu wananchi wale wanaendelea kupata madhara makubwa ili kuepuka yale madhara yasiendelee kuwapata wananchi?

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza Mheshimiwa Mbunge Regina Qwaray, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali haina kauli mbili, kauli ya Serikali ni kauli moja, sasa katika hili namuomba Mheshimiwa Mbunge, twende na hii kauli ya kwamba kwa sasa hivi Serikali hatujawa na mpango wa kufanya kama vile Mheshimiwa anavyosema kwa sababu kama ambavyo tumeeleza katika jibu la msingi.

Mheshimiwa Spika, lakini kwa upande wa fedha nadhani hili sasa atupe muda tuona namna ya kukaa na kushirikiana na baadhi ya Wizara zingine za kisekta, ikiwemo Wizara ya Kilimo, Wizara ya Maji na Wizara yetu ya Mazingira ili kuona namna ambavyo tunaweza kujadili kwa pamoja na baadaye tukatafuta fedha kwa ajili ya ziwa hili.