Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Zuberi Mohamedi Kuchauka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Liwale
Primary Question
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA aliuliza:- Wilaya ya Liwale ilipandishwa hadhi kuwa Wilaya kamili tangu mwaka 1975, lakini ni Wilaya ya pekee ambayo haina Kituo cha Polisi wala nyumba za watumishi wa kada hiyo:- (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga jengo la kituo cha Polisi Wilaya ya Liwale sambamba na nyumba za watumishi ambao wanaishi uraiani kwa sasa? (b) Je, ni lini Tarafa ya Kibutuka itapata kituo kidogo cha Polisi ili kulinda wafanyabiashara wa mazao ya ufuta wanaokuja Tarafani?
Supplementary Question 1
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Nasikitika sana kwa majibu ya kukatisha tamaa yaliyotolewa na Mheshimiwa Naibu Waziri. Wilaya ya Liwale ina umri wa miaka 41 leo, Serikali ya Chama cha Mapinduzi inasema haina mpango wowote wa kujenga Kituo cha Polisi pale, anaposema kwamba ni zaidi ya Wilaya 65, sidhani kama hizi Wilaya nyingine ambazo anazi-include yeye zina umri wa miaka 40. Wilaya ya Liwale ina jumla ya kilometa 66,000 na hizi tarafa anazozisema zipo umbali wa kilometa zaidi ya 60 kutoka Liwale Mjiniā¦ (Makofi)
SPIKA: Mheshimiwa Kuchauka, swali sasa!
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Spika, najenga hoja. Wilaya ya Liwale mpaka leo, nimetembelea kile kituo, mafaili yale wanafunika na maturubai, lile jengo walilopanga la mtu binafsi linavuja. Sasa ninachoomba, nipewe time frame, ni lini Kituo cha Polisi Liwale kitajengwa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, vilevile katika Tarafa ya Kibutuka, ndiyo tarafa inayoongoza kwa ufuta na wafanyabiashara wakubwa wako pale na Kata ya Lilombe sasa hivi kuna machimbo na wafanyabiashara wengi wako pale, ni lini Kata hizi zitajengewa vituo vya Polisi?
Name
Eng. Hamad Yussuf Masauni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kikwajuni
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, naomba nichukue concern ya Mheshimiwa Mbunge Kuchauka kuhusiana na unyeti na umuhimu wa kujenga kituo pale Liwale, lakini kama nilivyomwambia kwamba vituo hivi pamoja na vingine ambavyo tumepanga kuvijenga, tutavijenga kadri ya fedha zitakavyoruhusu.
Mheshimiwa Spika, hata hivyo, kwa kuwa Mheshimiwa Mbunge amezungumzia kwa uchungu kuhusiana na matatizo makubwa yaliyopo katika Wilaya yake, basi niseme tu kwamba pale ambapo tutapata fedha tutatoa kipaumbele kwenye kituo cha Liwale.
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na swali lake la pili, anauliza kwamba, katika Tarafa ya Kibutuka, ninachoweza kusema ni kwamba kama nilivyojibu katika jibu la msingi, kwamba tumejaribu kupeleka Askari katika Tarafa ile ili waweze kusaidia ulinzi kwa wakati huu, wakati tunajiandaa na ujenzi wa kituo pale ambapo fedha zitapatikana.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved