Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Esther Edwin Maleko
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTHER E. MALLEKO K.n.y. MHE. DKT. DAVID M. DAVID aliuliza: - Je, ni lini Benki Kuu itaweka utaratibu mzuri kwa Serikali na taasisi zake kuweka fedha katika Benki za biashara ili kuwa na mzunguko mzuri wa fedha?
Supplementary Question 1
MHE. ESTHER E. MALLEKO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, kwanini Serikali isipunguze riba inapokopesha benki za biashara ili gharama hizo ziweze kushuka na Watanzania wengi waweze kukopa.
Mheshimiwa Spika, swali la pili. Kwanini Serikali isipunguze riba inapouza hati fungani ili Watanzania wengi waweze kupeleka fedha zao katika benki hizo kama fix deposit.
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Esther Malleko kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, viwango vya riba vimepungua kwa asilimia 16.60 mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 16.41, mwaka 2022 ili kuwezesha benki kukopesha wananchi kwa riba nafuu na kupunguza mikopo chechefu.
Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, riba za hatifungani haziwekwi au kupangwa na Benki Kuu ya Tanzania bali ni matokeo ya mchakato wa mauzo na ununuzi wa hatifungani kutoka soko la fedha linaloendeshwa kwa mfumo wa soko huria. Hata hivyo, takwimu za karibuni zinaonesha kuwa riba za hatifungani zimepungua.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved