Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Luhaga Joelson Mpina

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisesa

Primary Question

MHE. LUHAGA J. MPINA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itarejesha kwa wafugaji mifugo iliyokamatwa na TAWA, TFS na WMA ambapo Mahakama ilitoa hukumu irejeshwe?

Supplementary Question 1

MHE. LUHAGA J. MPINA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwanza suala la kuvunja sheria hapa halipo kwa sababu tayari hawa wananchi wameshashinda kesi mahakamani na Mahakama ikawapa ushindi na ikaamuru mifugo yao warejeshewe.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; Waziri wa Maliasili na Utalii wakati anahitimisha bajeti yake alisema mifugo hiyo itarudishwa mara moja; na Mheshimiwa Waziri Mkuu alipokutana na kikao cha wafugaji wote nchini aliagiza mifugo hiyo wairejeshwe lakini sasa hivi…

SPIKA: Uliza swali Mheshimiwa Mpina ulishatoa maelezo marefu sana.

MHE. LUHAGA J. MPINA: Mheshimiwa Spika, swali ninaloliuliza hapa orodha ipo Wizarani na Waziri anayo orodha kwa nini anakwepa hapa kuwalipa hao wafugaji wanyonge ambao wameshashinda kesi mahakamani na kutudanganya hapa kwamba hiyo orodha hana?

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Luhaga Joelson Mpina, Mbunge wa Kisesa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu kwenye swali la msingi ni kwamba mpaka sasa hatujapata orodha ya wafugaji ambao wanalalamika hawajarejeshewa mifugo yao. Kama ambavyo nimeeleza kwamba kesi inapopelekwa mahakamani sisi tunapeleka vielelezo tu lakini kesi inabaki kuwa ni chini ya hakimu, DPP na sisi tunakuwa kama mashahidi, kwamba tumekamata mifugo hii, baada yah apo hakimu ndio anayetoa hukumu. Aidha, hukumu inakuwa ni kurejeshewa hiyo mifugo kwa faini au mifugo kutaifishwa.

Nimesema endapo kama kuna mfugaji ambaye ana kesi ambayo inatudai sisi Wizara ya Maliasili na Utalii basi waje wizarani tutakaa pamoja tuichambue hiyo kesi na tutaweza kutekeleza kama Serikali.

Name

Festo Richard Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makete

Primary Question

MHE. LUHAGA J. MPINA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itarejesha kwa wafugaji mifugo iliyokamatwa na TAWA, TFS na WMA ambapo Mahakama ilitoa hukumu irejeshwe?

Supplementary Question 2

MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Spika, asante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Swali langu pale Makete tuna pori la Mpanga Kipengele ambalo linazunguka vijiji vya Ibaga, Ikovo, Kiimani na Kigala. Pori hili limegeuka ni mwiba kwa wananchi wa Makete kwa sababu mifugo yao imekuwa ikiingia na watu wanakamata lakini bikoni zimewekwa kwenye maeneo ya wananchi; na nililalamika hapa Bungeni na ukaniahidi Mheshimiwa Waziri utakuja.

Je, ni lini Serikali itekwenda kuweka bikoni ili wananchi wangu wawe salama katika eneo hili?

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Sanga Mbunge wa Makete, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, nimtaarifu tu Mheshimiwa Mbunge kwamba tulikuwa kwenye ziara ya Mawaziri nane ambao wanatatua changamoto hizi za migogoro ya ardhi.

Mheshimiwa Spika, nimhakikishie tu kwamba nitafika kama sio mimi basi ni Mheshimiwa Waziri kuhakikisha kwamba tunafafanua wapi mipaka ilipo ili wananchi waweze kuielewa na hatimaye tuendelee kushirikiana kulinda maeneo ya hifadhi.

Name

Esther Lukago Midimu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. LUHAGA J. MPINA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itarejesha kwa wafugaji mifugo iliyokamatwa na TAWA, TFS na WMA ambapo Mahakama ilitoa hukumu irejeshwe?

Supplementary Question 3

MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwa vile Serikali inasema itawarudishia ng’ombe wao je, itakaporudisha itawalipa na fidia?

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Esther Midimu Mbunge wa Simiyu kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, naomba nifafanue hapa nimesema hapa kwamba tunapokamata mifugo kesi zao tunazipeleka Mahakamani hukumu inakuwa kati ya Hakimu na sisi tunasimama pale kama mashahidi tu ambao tunaonyesha vielelezo. Kwa hiyo suala la kwamba tutarejesha mifugo ni pale ambapo Serikali itajiridhisha kwamba hawa wahalifu watakaoingiza mifugo yao kwenye hifadhi wanastahili kurejeshewa hiyo mifugo na tunapopeleka kesi Mahakamani tunakabidhi vielelezo vyote, kwa hiyo sisi hatukai na mifugo. Ahsante.