Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Khadija Shaaban Taya
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. KHADIJA S. TAYA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha Sensa ya Watu na Makazi inajumuisha takwimu za watu wenye ulemavu na aina ya ulemavu?
Supplementary Question 1
MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali na kuonyesha namna gani Serikali imejipanga kwa kutumia hizi takwimu.
Mheshimiwa Spika, kwa kutumia takwimu zilizopita, za 2010 na sasa hivi tuko 2022/2023 kwenye maandalizi ya bajeti ya Mpango wa mwaka 2022/2023.
Je, Serikali imejipangaje kupitia Wizara yake hii ya Fedha na Mipango kuondoa matatizo ya watu wenye ulemavu; kwa sababu hii Wizara ndiyo ambayo ina bajeti Kuu ya Serikali? Ahsante. (Makofi)
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Khadija Shaaban Taya, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, baada ya kukamilisha Sensa yetu tukapata takwimu sahihi na kuweza kujua idadi ya watu wenye ulamavu na aina ya ulemavu ambayo ipo nchini, tutaandaa mipango rasmi na kutoa vipaumbele ambavyo vinaweza kuingizwa hadi katika bajeti yetu kwa maslahi ya wananchi wote.
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mama Samia Suluhu Hassan haiko tayari kuacha kundi lolote nyuma, makundi yote yataainishwa katika vipaumbele vya nchi hii na kwa maslahi ya umma. Ahsante. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved