Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Cecilia Daniel Paresso

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. CECILIA D. PARESSO (K.n.y. MHE. WILLIAM D. NKURUA) aliuliza:- Wilaya ya Nanyumbu ilianzishwa mwaka 2005 lakini mpaka sasa haina Hospitali ya Wilaya hivyo kuwalazimu wananchi kufuata huduma hiyo katika Hospitali ya Wilaya ya Masasi lakini pia kumekuwa na jitihada za kuomba kukipandisha hadhi Kituo cha Mangaka kuwa Hospitali ya Wilaya ya Nanyumbu lakini mpaka sasa hakuna mafanikio yoyote. Je, Serikali haioni umuhimu wa kukipandisha hadhi kituo hicho ili kuwa Hospitali ya Wilaya na kunusuru afya za wananchi wa Nanyumbu hasa akina mama wajawazito kwa kulazimika kupelekwa Wilaya jirani ya Masasi?

Supplementary Question 1

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa hospitali zetu mbalimbali nchini zina upungufu mkubwa wa dawa, je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha dawa za uhakika zinapatikana katika hospitali zetu nchini?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali dogo la pili, kwa kuwa MSD pia inaidai Serikali fedha nyingi, je, ni lini Serikali itahakikisha inalipa deni la MSD?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Cecilia Paresso kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tulivyoeleza hapa katika vipindi tofauti, jukumu kubwa la Serikali ni kuhakikisha tunaondoa upungufu wa dawa na vifaa tiba. Katika swali la kwanza linalosema Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba dawa zinapatikana, ni kama tulivyoeleza hapo awali kwamba jukumu letu kubwa hivi sasa ni kuhakikisha kwanza tunajielekeza zaidi katika ukusanyaji wa mapato.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika vipindi tofauti nimesema kwamba ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mifumo ya kielektroniki ni kuongeza ukusanyaji wa fedha katika hospitali, zahanati na vituo vyetu vya afya. Tutakapofanya hili kwa upana wake maana yake ni kwamba vituo vya afya vitakuwa na dawa za kutosha kwa sababu mwongozo unasema jinsi gani pesa zinazopatikana zitaenda kwenye ununuzi wa dawa na vifaa tiba.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini suala la deni la MSD Waziri wa Afya alipokuwa aki-table bajeti yake na katika mijadala mipana iliyojitokeza imejielekeza kuhakikisha deni la MSD linalipwa lengo likiwa ni MSD kuwa na uwezo wake wa kusambaza dawa. Waziri wa Afya alielezea suala hili kwa upana sana na Wizara ya Fedha ilichukua commitment ya kuhakikisha kwamba MSD deni lake linalipwa ili mwisho wa siku MSD iweze kusambaza dawa katika hospitali, zahanati hali kadhalika vituo vya afya na hospitali za mkoa.

Name

Venance Methusalah Mwamoto

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilolo

Primary Question

MHE. CECILIA D. PARESSO (K.n.y. MHE. WILLIAM D. NKURUA) aliuliza:- Wilaya ya Nanyumbu ilianzishwa mwaka 2005 lakini mpaka sasa haina Hospitali ya Wilaya hivyo kuwalazimu wananchi kufuata huduma hiyo katika Hospitali ya Wilaya ya Masasi lakini pia kumekuwa na jitihada za kuomba kukipandisha hadhi Kituo cha Mangaka kuwa Hospitali ya Wilaya ya Nanyumbu lakini mpaka sasa hakuna mafanikio yoyote. Je, Serikali haioni umuhimu wa kukipandisha hadhi kituo hicho ili kuwa Hospitali ya Wilaya na kunusuru afya za wananchi wa Nanyumbu hasa akina mama wajawazito kwa kulazimika kupelekwa Wilaya jirani ya Masasi?

Supplementary Question 2

MHE. VENANCE M. MWAMOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa swali la msingi lilikuwa linahusu kuhusu kupandisha vituo vya afya; na kwa kuwa Wilaya ya Kilolo toka ilipoanzishwa mwaka 2000 haijawahi kuwa na hospitali ya Wilaya, imekuwa na Kituo cha Afya cha Dabaga na hivyo imepelekea ili wananachi kufuata huduma za hospitali inabidi waende Ilula kilometa zaidi ya 120.
Je, Serikali sasa haioni kuna umuhimu wa kupandisha hadhi kituo hicho cha Dabaga kuwa hospitali ya wilaya?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mwamoto, Mbunge wa Kilolo kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba tupokee huo mtazamo kwamba Kilolo hakuna Hospitali ya Wilaya kwa hiyo ina maana lazima watu waende Ilula kwa ajili ya kupata matibabu. Nilieleza hapa katika vipindi tofauti kwamba mchakato wa kupandisha ama Zahanati kuwa Kituo cha Afya au Kituo cha Afya kuwa Hospitali ya Wilaya kuna utaratibu wake muhimu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, utaratibu wake unaanzia kwenye WDC kwa maana ya Mabaraza ya Madiwani mwisho wa siku unafika Wizara ya Afya ambao ndiyo wenye dhamana. Wizara wakishafanya uhakiki kwamba kituo hicho kimekidhi kuwa hospitali ya wilaya basi inapandishwa moja kwa moja kama nilivyozungumzia katika suala la wenzetu wa Nanyumbu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maelezo haya, naomba nimuelekeze Mheshimiwa Mbunge kwa sababu najua yupo makini sana katika Kamati ya TAMISEMI, ahakikishe kwamba ule mchakato wa awali unaenda na kuangalia vigezo vinafikiwa mwisho wa siku na sisi TAMISEMI tutaweka nguvu na Wizara ya Afya wataangalia vigezo vikikubalika kituo hicho cha afya kitapandishwa hadhi lengo kubwa likiwa ni kuwafikia wananchi kwa karibu zaidi. Ni kweli haiwezekani wala haiingii akilini mwananchi kutembea kilometa 100, ni umbali mkubwa sana.
Kwa hiyo, hili ni jambo la msingi na naomba mchakato uendelee kwa kufuata utaratibu unaoelekezwa, nadhani Serikali italiangalia kwa jicho la karibu zaidi.