Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Hamis Mohamed Mwinjuma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muheza

Primary Question

MHE. HAMIS M. MWINJUMA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa maksudi wa kuwavutia Wawekezaji katika Kilimo cha zao la Muhogo Wilayani Muheza?

Supplementary Question 1

MHE. HAMIS M. MWINJUMA: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru na ninashukuru kwa majibu yanayotia moyo ya Mheshimiwa Waziri kwa niaba ya Serikali. Nina maswali mawili ya nyongeza: -

Kwanza; kwa muda mrefu kilimo cha muhogo kimekuwa kikifanywa kienyeji na kwa vile kwa sasa soko lake ni kubwa na la uhakika ni lini Serikali itaanza kuwekeza kwenye utafiti hasa kupitia kwenye kituo chetu cha TARI Mlengano ili kuongeza tija kwenye uzalishaji wa zao hili?

Swali la pili; kutokana na uwezo mdogo wa kipato kwa wananchi wengi wa vijijini Muheza, hali inayokwamisha ushiriki wao kwenye kilimo chochote kinachohitaji muda mrefu na uwekezaji mkubwa.

Je, kwa vile nimeshasema kwamba soko la muhogo sasa hivi ni kubwa na la uhakika. Serikali haioni haja ya kuhimiza kilimo cha muhogo ambacho inachukua Miezi Tisa tu kuwa tayari ili kuongeza kipato cha wananchi hawa wa vijijini? Ahsante. (Makofi)

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mwinjuma kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwanza kama nchi tuna- import wanga zaidi ya tani 8,000 kwa mwaka, pamoja na tunatumia muhogo kwa ajili ya chakula vilevile tunatumia wanga kwa ajili ya viwanda hasa kwenye maeneo ya pharmaceutical, matumizi ya nguo na viwanda vya karatasi.

Mheshimiwa Spika, nataka nimwambie kuhusu varieties sasa hivi tumeshatambua variety 10 katika utafiti ambazo zina uwezo wa kutuzalishia mpaka tani 20 mpaka 40 ambazo zimegundulika na watafiti wetu wa TARI. Hatua ya pili kumpelekea mkulima variety azalishe halafu hakuna uhakika wa soko ni jambo la hatari zaidi.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tumechukua hatua kama Wizara tumeshaanza vikao na viwanda vyote vinavyotumia wanga kuweza kutambua ubora wa wanga wanaoutaka ili tuweze kuwapelekea wakulima na tutengeneze mfumo wa contract farming ili yale yaliyotokea Muheza mwaka jana na mwaka juzi yasiweze kujitokeza tena.

Mheshimiwa Spika, nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba mwelekeo wa Serikali kuhusu muhogo ni mwelekeo wa industrial pamoja na matumizi ya chakula ndani zaidi tunataka ku-push mwelekeo wa industrial na tumeanza kuchukua hatua hizo. (Makofi)

Name

Anton Albert Mwantona

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Rungwe

Primary Question

MHE. HAMIS M. MWINJUMA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa maksudi wa kuwavutia Wawekezaji katika Kilimo cha zao la Muhogo Wilayani Muheza?

Supplementary Question 2

MHE. ANTON A. MWANTONA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, Jimbo la Rungwe wakulima wa parachichi wako kwenye kilio kikubwa sana ambapo wameambiwa wanunuzi watanunua maparachichi kupitia AMCOS, AMCOS yenyewe Rungwe iko moja, masharti yamekuwa ni magumu kwamba lazima pesa wapeleke kwenye AMCOS ndio watatununulia maparachichi hao wanunuzi wa parachichi. Ni jambo la kusikitisha sana wananchi wanalia wanunuzi wote wamekimbia wameenda maeneo ya Njombe, Mbozi na maeneo mengine, pale Rungwe maparachichi yanaozea shambani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kupata kauli ya Serikali; Je, wapotayari kuwalipa fidia wananchi ambao maparachichi yao yanaozea shambani sasa hivi? Pia tupate kauli ya Serikali wanasema nini kuhusu kilimo cha parachichi?

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mwantona Mbunge wa Rungwe kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nataka nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa sababu amekuwa akilifuatilia hili jambo, tumeongea na Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya na tumekubaliana.

Mheshimiwa Spika, avocado siyo korosho, avocado sio pamba, avocado siyo kahawa, hauwezi kulazimisha kununua avocado kwa kukusanya kwenye Chama cha Msingi, hauwezi kulazimisha avocado kuipeleka kwenye Chama cha Msingi kwa sababu ni perishable. Kwa hiyo, tumekubaliana na Mkuu wa Mkoa waufute huo utaratibu na wameshaanza kuufuta, wawaache wakulima wenye contract na wanunuzi wauze moja kwa moja kwa wanunuzi wao. Wahakikishe tu Serikali inapata ushuru wake stahiki katika njia halali na wafute tozo zote walizoziweka ambazo hazijaidhinishwa na Wizara ya Kilimo kwenye zao la avocado. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Waziri hilo katazo linafanywa lini, kwa sababu maparachichi yanaoza. Mkuu wa Mkoa hilo katazo atalifanya lini?

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, katazo hili nimeongea na Mkuu wa Mkoa siku Mbili zilizopita na tumeshakubaliana na Wizara ya Kilimo imemwandikia barua Mkuu wa Mkoa siku ya jana kumueleza haya ambayo ninayasema. Kwamba, avocado haiwezi kuuzwa kwenye mfumo ambao unataka kufanyika Rungwe.

SPIKA: Hilo limeshaeleweka mmempa maelekezo ya hilo katazo lini, kwa sababu haya mazao yanaharibika. Kwa hiyo, kama atakuja kutoa hilo katazo baada ya miezi mitatu hiyo ndiyo hoja. Katazo linatoka lini? (Makofi)

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, katazo limetoka juzi kwa simu jana limekwenda kwa barua. (Makofi)

Name

Dr. Charles Stephen Kimei

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vunjo

Primary Question

MHE. HAMIS M. MWINJUMA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa maksudi wa kuwavutia Wawekezaji katika Kilimo cha zao la Muhogo Wilayani Muheza?

Supplementary Question 3

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

Mheshimiwa Spika, kwa vile bei za miche ya kisasa ya kahawa, ya miparachichi hiyo tunayozungumza, ya migomba bei zake ni juu sana. Sijui Serikali ina mpango gani wa kutoa ruzuku kwa miche hiyo? (Makofi)

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kimei kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kuanzia mwaka ujao wa fedha tutakapopitisha bajeti hapa mtaona kwenye bajeti ya Wizara ya Kilimo inatoa guidance juu ya subsidy kwenye zao la avocado na baadhi ya mazao na mazao haya kwa muda mrefu yalikuwa hayana guidance, hayajulikani nani mzalishaji kila mtu anajizalishia barabarani.

Kwa hiyo, tunazindua guiding ya uzalishaji wa miche ya avocado na mazao ya miti na kutakuwa kama ambavyo mzalishaji wa mbegu anavyozalisha na hapo mtaona kwenye bajeti tutatenga fedha kwa ajili ya ku-subsidize uzalishaji wa miche milioni 20 kuanzia mwaka kesho kwa uwezo wa Mungu. (Makofi)

Name

Vedastus Mathayo Manyinyi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Musoma Mjini

Primary Question

MHE. HAMIS M. MWINJUMA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa maksudi wa kuwavutia Wawekezaji katika Kilimo cha zao la Muhogo Wilayani Muheza?

Supplementary Question 4

MHE. VEDASTUS M. MATHAYO: Mheshimiwa Spika, ahsante kunipa nafasi na mimi niweze kuuliza swali moja la nyongeza.

Katika nchi yetu kati ya matatizo makubwa tuliyonayo ni tatizo la ajira hasa kwa vijana wetu na tunatambua kabisa kwamba Wizara ya Kilimo ndiyo inayoweza kupunguza tatizo hili.

Je, Mheshimiwa Waziri umejipangaje katika WIzara yako kuhakikisha kwamba kilimo kinasaidia kupunguza ajira hasa kwa vijana wetu? (Makofi)

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Manyinyi Mbunge wa Musoma Mjini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, sekta ya kilimo ni sekta ambayo kweli inaweza kuajiri watu wengi sana lakini yapo mambo makubwa manne ambayo kwa muda mrefu yamewafanya vijana kutokuwa tayari kwenda kwenye sekta ya kilimo:

(i) Upatikanaji wa ardhi,
(ii) Upatikanaji wa mitaji,
(iii) teknolojia, na
(iv) soko la uhakika.

Mheshimiwa Spika, hii imewafanya vijana wengi kutokwenda huko. Kwa hiyo, kama Wizara tutakapokuja kusoma bajeti mwaka huu mtaona tuna-launch kitu tunaita ‘building a better tomorrow’ na tutaitengea fedha katika bajeti.

Mheshimiwa Spika, tunaanzisha block farm system ambako Serikali itachukua maeneo makubwa itayasafisha, itapima afya ya udongo, tutagawa block farm na kuwamilikisha vijana hayo maeneo.

Mheshimiwa Spika, kama ni eneo linahitaji fidia tutalipa sisi na yale maeneo yatakuwa owned na hao vijana ambao watakuwepo hapo na kuwaunganisha moja kwa moja na soko na kuijua afya ya udongo na mazao yatakayozalishwa kwenye eneo hilo. (Makofi)

Name

Festo Richard Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makete

Primary Question

MHE. HAMIS M. MWINJUMA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa maksudi wa kuwavutia Wawekezaji katika Kilimo cha zao la Muhogo Wilayani Muheza?

Supplementary Question 5

MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Zao la parachichi ukienda kwenye soko la nje inaonekana parachichi nyingi zinatoka kwenye nchi ya jirani, lakini uzalishaji mkubwa unafanyika Njombe na Mikoa ya Tanzania. (Makofi)

Ni lini tutatengeneza ownership ya soko hili la parachichi lionekane ni la Tanzania na siyo la nchi jirani ambao wanunuzi wengi wananunua Tanzania na wanafanya packaging kwa jina la nchi ya jirani? (Makofi)

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Sanga la nyongeza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, sababu za parachichi zetu kuwa- branded nje ni kwa sababu sisi kama nchi tumekuwa kwa muda mrefu hatuna infrastructure. Kwa hiyo, watu wanakuja kununua raw wanapeleka wanakwenda ku-brand nje.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kuanzia mwaka kesho tutatenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa common use facility tatu, moja tutaijenga Mkoa wa Iringa ambapo itafanya kazi ya sorting, grading na branding na yeyote anayenunua huko atanunua akifikisha pale ataikuta hiyo huduma inafanyika na itakuwa-branded kama produce of Tanzania.

Mheshimiwa Spika, vilevile, zipo kampuni ambazo sasa hivi zimeshaanza ku-brand parachichi yetu na kui-brand kama produce of Tanzania kama Eat Fresh na Kampuni zingine ambazo zipo katika Nchi yetu. Kwa hiyo, jambo hili lipo na Serikali tunachukua hatua kuanzia mwakani tutakuwa na common use facility tatu moja Dar es Salaam, moja Iringa na moja Kilimanjaro. (Makofi)

Name

Neema Kichiki Lugangira

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. HAMIS M. MWINJUMA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa maksudi wa kuwavutia Wawekezaji katika Kilimo cha zao la Muhogo Wilayani Muheza?

Supplementary Question 6

MHE. NEEMA K. LUGANGIRA: Mheshimiwa Spika, nashukuru.

Mheshimiwa Spika, ningependa kumuuliza Mheshimiwa Waziri wa Kilimo; Je, Wizara ya Kilimo ina mpango gani wa kuhamasisha na kuimarisha uwekezaji kwenye zao la vanilla kwa Mkoa wa Kagera? Ahsante.

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Neema Lugangira kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama Wizara zao la vanilla halikuwa kwenye map ya Serikali na kuonekana kama ni zao ambalo lina-attract na kuweza kufanyiwa kazi.

Mheshimiwa Spika, nataka tu niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge baada ya kujitokeza wanunuzi na wakulima wengi either kutapeliwa au kufanya nini, tumeanza kuchukua hatua sasa hivi na tunavyoongea sasa hivi timu yetu ya Wizara ya Kilimo iko Mkoa wa Kagera na wengine wameelekea Mkoa wa Njombe kwa ajili ya kuweza kuangalia map na kuweza kulitambua vizuri na kulitengenezea mkakati.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo kuanzia mwaka ujao wa fedha baada ya mwaka mmoja kutakuwa na mkakati rasmi wa nchi kuhusu zao la vanilla. (Makofi)

Name

Samweli Xaday Hhayuma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hanang'

Primary Question

MHE. HAMIS M. MWINJUMA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa maksudi wa kuwavutia Wawekezaji katika Kilimo cha zao la Muhogo Wilayani Muheza?

Supplementary Question 7

MHE. ENG. SAMWELI X. HHAYUMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Spika, nataka kufahamu kwa kuwa mashamba ya Murujanda, Sechet ambayo yako chini ya Mwekezaji kwa sasa uzalishaji uko chini ya kiwango na aliahidi kwamba ndani ya mwaka mmoja ataboresha.

Wizara ina kauli gani katika kuhakikisha kwamba tunapata Wawekezaji ambao wako makini au kuwapatia wana Hanang’ maeneo hayo?

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge wa Hanang’ kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli kuna mashamba yalichukuliwa na Wawekezaji mojawapo ni Ngano Limited katika Mkoa wa Manyara Wilaya ya Hanang’ na uwezo wake wa kuyatumia hauzidi asilimia 30. Aliingia makubaliano nasi kama Wizara ya Kilimo na kutuambia kwamba tumpe span ya mwaka mmoja, ataweza kufanya matumizi kwa kiwango cha asilimia 100 mpaka sasa amefeli.

Mheshimiwa Spika, hivyo, Wizara sasa hivi tunawasiliana na wenzetu wa TIC na kuwasiliana na wenzetu wa Hazina ili tumuite Mwekezaji huyu, tukae naye aweze ku- offload hekari zaidi ya 30,000 ambazo ameshindwa kuzitumia mpaka sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninatumia Bunge lako Tukufu kuwaambia Halmashauri ya Hanang’ kwamba eneo la Basutu lisibadilishwe matumizi litabaki kuwa eneo la uzalishaji wa ngano. Hili ni jambo muhimu sana na Mheshimiwa Mbunge ni Mjumbe wa Baraza la Madiwani, wahakikishe hawabadilishi eneo la Basutu kulipelekea matumizi mengine isipokuwa kwa ajili ya matumizi ya ngano. (Makofi)

Name

Sophia Hebron Mwakagenda

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. HAMIS M. MWINJUMA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa maksudi wa kuwavutia Wawekezaji katika Kilimo cha zao la Muhogo Wilayani Muheza?

Supplementary Question 8

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na unyanyasaji sana kwa wanunuzi wa parachichi wanachagua wao kusema haya yamekuwa reject, haya yamekuwa mazima.

Serikali inasaidia nini wakulima kuonesha kama kweli yale ni reject kwa sababu, wanawaonea ili wao wakapate faida zaidi? (Makofi)

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, labda tu niseme kitu kimoja kwamba ninamuomba Mheshimiwa Mwakagenda na nitumie nafasi hii kama kuna wanunuzi wowote wanatumia hiyo nafasi kwa ajili ya kuwadhulumu wakulima na kuzitaka Halmashauri zote kuhakikisha kwamba mnunuzi yeyote anayeingia kununua parachichi katika Mkoa au Wilaya husika afuate guiding na manual ambayo Wizara ya Kilimo imeitoa. Kama kuna special case kwenye maeneo maalum ofisi yetu iko wazi tunaomba hizo taarifa tutachukua hatua. (Makofi)