Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Neema Kichiki Lugangira
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. NEEMA K. LUGANGIRA aliuliza: - Je, Serikali imejipangaje kuhakikisha mbegu za asili zenye virutubisho zinatambulika kisheria, zinalindwa, zinahifadhiwa na kusajiliwa?
Supplementary Question 1
MHE. NEEMA K. LUGANGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali ninayo maswali mawili ya nyongeza. Swali kwa kwanza; kwa kuwa tayari ipo Sheria ya Mbegu ya Mwaka 2003 ambayo ilifanyiwa maboresho mwaka 2014, je, kwa nini Serikali ianzishe upya mchakato wa kuleta sheria mpya badala ya kuongeza kwenye hii Sheria ya Mbegu iliyopo ya mwaka 2003 utambuzi wa mbegu za asili kwa kuwa sheria hii inatambua mbegu za kisasa?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili; naipongeza Serikali imeanzisha hiki Kitengo cha Taifa cha Kuhifadhi Vinasaba vya Mimea ikiwemo mbegu za asili, lakini tokea mwaka 2005 zaidi ya miaka 15, Sheria ya National Plant Genetic Resource Act bado haijawahi kupitishwa, kwa hiyo kitengo hiki kimsingi hakina meno wala hakiwezi kutambua wala kulinda mbegu za asili ikiwemo na hivi vinasaba na ikiwemo pia kulinda hakimiliki ya mbegu zetu za asiliā¦
NAIBU SPIKA: Swali.
MHE. NEEMA K. LUGANGIRA: Je, Serikali itailleta lini Bungeni Sheria hii ya National Plant Genetic Resource ili tuweze kuhakikisha kwamba kitengo hiki kinafanya kazi ipasavyo? Ahsante.
Name
Anthony Peter Mavunde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Dodoma mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Neema Kichiki Lugangira, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nampongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwa namna ambavyo anakuwa mfuatiliaji mzuri wa masuala haya, lakini swali lake la kwanza ni kwamba, tumepokea wazo lake la maboresho ya sheria iliyopo lakini pamoja na hiyo sheria aliyouliza katika swali lake la nyongeza ni sheria ambayo ndio itakuja hasa kuja kuzitambua na vilevile kuzungumzia usajili wa mbegu za asili, ambao sheria hii mpaka hivi sasa ipo katika ngazi ya IMTC. Tunaamini kabisa taratibu zinaendelea vizuri na sheria hii italetwa hapa Bungeni ili iweze kupitishwa na basi tuwe tuna sheria ambayo itakuwa inatambua lakini vilevile ambayo itakuwa ina usajili mbegu za asili kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved