Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Joseph Zacharius Kamonga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ludewa
Primary Question
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA aliuliza: - Je, ni lini Serikali italipa fidia wananchi waliotwaliwa ardhi yao kwa ujenzi wa viwanda maeneo ya Liganga na Mchuchuma?
Supplementary Question 1
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri yaliyotolewa na Serikali, ila nina swali moja dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Serikali imekuwa na dhamira ya kutengeneza ajira maeneo haya yenye uwekezaji kwa kutenga vitalu vya wachimbaji wadogo; na kwa kuwa katika eneo lile la Mkomangāombe, eneo lote lenye makaa ya mawe limeshikiliwa na Serikali kupitia Wizara hii: Je, Serikali haioni haja ya kukaa na wachimbaji wadogo ambao wamekuwa wakiomba muda mrefu kugaiwa maeneo ya kuchimba makaa ya mawe ili nao waweze kutengeneza ajira?
Mheshimiwa Spika, ahsante.
Name
Exaud Silaoneka Kigahe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kaskazini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Zachariuz Kamonga, Mbunge wa Ludewa, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kwanza nampongeza sana Mheshimiwa Zacharius kwa ufuatiliaji kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu katika Jimbolake la Ludewa. Ni kweli dhamira ya Serikali ni kuona sasa tunashirikisha wachimbaji wadogo katika maeneo yote au katika biashara zote ambazo zinafanyika kwenye maeneo husika.
Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema, kwa sababu mradi huu ni mkubwa, kwa sasa bado tunakamilisha majadiliano na huyu mwekezaji mkubwa. Kwa hiyo, naamini atakapoanza kutekeleza na hao wengine wachimbaji wadogo nao naamini watashiriki katika kuhakikisha wanafaidika na uwepo wa mali asili au madini haya katika maeneo hayo ya ludewa.
Mheshimiwa Spika, tunalichukua hili kwa uzito wake ili kuhakikisha local content nayo inachukua nafasi yake.
Mheshimiwa Spika, nakushukuru.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved