Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Cecil David Mwambe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ndanda
Primary Question
MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza: - Je, ni lini Serikali itafikisha umeme katika Kata mbili ambazo hazijawahi kupata umeme kabisa katika Jimbo la Ndanda?
Supplementary Question 1
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa majibu mazuri kabisa ya Waziri na tumekuwa tunafanya mjadala kwenye jambo hili.
Nimhakikishie kwamba Mkandarasi tayari yupo site, kwenye Kata ya Mpanyani hajaanza kazi imeanza Kata ya Msikisi, Je, ni lini Mkandarasi huyu ataanza kazi pia katika Kata ya Mpanyani ili kuweza kufanya kazi yake kwa wakati tuliokubaliana?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili Kitongoji cha Ndolo kilichopo kwenye Kata ya Ndanda kiko mita 200 tu kutoka Shule ya Sekondari ya Ndanda lakini kitongoji hiki kimekosa umeme kwa muda mrefu sana.
Sasa niombe Mheshimiwa Waziri utoe maelekezo kumwelekeza Engineer wetu wa Mkoa Ndugu yetu Fadhili kwamba ni lini atapeleka umeme kwenye Kitongoji cha Ndolo kwa sababu kipo mjini kabisa lakini hakina umeme na kuna wakazi wengi ambao wameshafanya wiring? Ahsante.
Name
January Yusuf Makamba
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bumbuli
Answer
WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu maswali mawili madogo ya Mheshimiwa Cecili David Mwambe Mbunge wa Ndanda kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, nakubaliana kwamba kuna haja ya kuharakisha ili Mkandarasi huyu afanye kazi kwa pamoja katika vijiji vyote kwa mpigo na nimepokea pia ushauri na maombi ya Mheshimiwa Mbunge kwamba Mkandarasi huyu pia apeleke umeme katika kitongoji hicho na jambo hilo linawezekana.
Name
Maimuna Salum Mtanda
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Newala Vijijini
Primary Question
MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza: - Je, ni lini Serikali itafikisha umeme katika Kata mbili ambazo hazijawahi kupata umeme kabisa katika Jimbo la Ndanda?
Supplementary Question 2
MHE. MAIMUNA S. MTANDA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwakunipatia nafasi hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuiomba Serikali je, haioni haja ya kufanya review ya Wakandarasi waliopewa kazi ya REA III, Round II kwa sababu wengi wanasuasua akiwemo yule aliyepewa kazi katika Jimbo la Newala Vijijini?
Name
January Yusuf Makamba
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bumbuli
Answer
WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Maimuna kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli ipo changamoto kubwa sana ya kuchelewa kwa miradi ya REA na sababu iliyopo ni kwamba mikataba ambayo REA imeingia na Wakandarasi ni mikataba ambayo inaweka bei fixed. Bahati mbaya katika kipindi cha mwaka mzima uliopita, gharama ya vifaa hasa alluminium na copper duniani imepanda kwa asilimia zaidi ya 137. Kwa hiyo, jambo ambalo Serikali imefanya ni kutafuta bajeti ya ziada kufidia ongezeko la bei za vifaa hivyo na hadi sasa tumeongea na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ili kufungua mikataba na kuirekebisha kwa kuzingatia mabadiliko ya bei hizo na tunaamini kabisa kwamba hivi karibuni tutafanikiwa na miradi ile ambayo inakwamakwama kutokana na kutopatikana kwa vifaa itaendelea na hili ni kwa nchi nzima.
Name
Deodatus Philip Mwanyika
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Njombe Mjini
Primary Question
MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza: - Je, ni lini Serikali itafikisha umeme katika Kata mbili ambazo hazijawahi kupata umeme kabisa katika Jimbo la Ndanda?
Supplementary Question 3
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi na mimi kuuliza swali dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, Jimbo la Njombe Mjini, Kata ya Lugenge, Kata kubwa watu wengi iko karibu kabisa na Mjini mpaka leo hakuna umeme hata Kijiji kimoja.
Ni lini sasa Serikali itapeleka umeme kwenye Kata hiyo ya Lugenge?
Name
January Yusuf Makamba
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bumbuli
Answer
WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Deodatus Mwanyika, Mbunge wa Njombe Mjini kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, tumeingiza vijiji vyote vilivyobakia katika nchi hii katika mradi wa REA awamu ya tatu na mzunguko wa pili ulioanza kutekelezwa mwezi Aprili mwaka jana. Kata hii ipo katika mpango huo na itapata umeme na mradi huo kukamilika kabla ya Desemba 2022.
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Primary Question
MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza: - Je, ni lini Serikali itafikisha umeme katika Kata mbili ambazo hazijawahi kupata umeme kabisa katika Jimbo la Ndanda?
Supplementary Question 4
MHE. DANIEL B. SILLO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali moja dogo la nyongeza.
Mpango wa Serikali ni kuhakikisha kwamba ifikapo Desemba mwaka huu Vijiji vyote vya nchi hii ikiwepo Babati Vijijini vinapata umeme. Lakini kwa kasi hii ndogo ya kusuasua ya Wakandarasi je, mpango huu bado upo au umebadilika? (Makofi)
Name
January Yusuf Makamba
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bumbuli
Answer
WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Sillo Mbunge wa Babati Vijijini kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba kumekuwa na changamoto hiyo niliyoieleza awali ya bei na upatikanaji wa vifaa vya umeme. Katika makubaliano mapya ambayo tutaingia na Wakandarasi wa REA kutakuwa na program mpya ya kazi ambayo itakuwa na maelekezo ya kuharakisha utekelezaji wa kazi hizi, kwa sababu pale ambapo mikataba itarekebishwa, itarekebishwa kwenye bei lakini tunaamini kwamba ratiba ya kazi itakuwa pale pale, bado nia yetu ni kukamilisha miradi hii kabla ya Desemba, 2022.
Name
Vita Rashid Kawawa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Namtumbo
Primary Question
MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza: - Je, ni lini Serikali itafikisha umeme katika Kata mbili ambazo hazijawahi kupata umeme kabisa katika Jimbo la Ndanda?
Supplementary Question 5
MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa fursa hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwetu kuna Kata ya Lusewa ambayo kuna Kijiji cha Ligunga, kuna shule mbili za Serikali, kuna taasisi ya dini, pia kuna mradi wa maji ambao inatumia generator kusambaza maji hayo. Lakini Kijiji hicho kimerukwa kwenye scope hii ya mzunguko wa tatu wa REA na umeme umepita pale pale.
Je, Serikali iko tayari kushusha umeme pale ili uweze kusambazwa katika Kijiji hicho?
Name
January Yusuf Makamba
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bumbuli
Answer
WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Vita Kawawa Mbunge wa Namtumbo, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu maelezo hay ani mahususi basi tutatoa maelekezo kwa REA waende wakatembelee katika eneo lile na kwa sababu kupeleka umeme katika taasisi za kijamii na taasisi za umma ni vipaumbele vya REA basi bila shaka yoyote tutahakikisha kwamba umeme unafika huko.
Name
Tecla Mohamedi Ungele
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza: - Je, ni lini Serikali itafikisha umeme katika Kata mbili ambazo hazijawahi kupata umeme kabisa katika Jimbo la Ndanda?
Supplementary Question 6
MHE. TECLA M. UNGELE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.
Mheshimiwa Naibu Spika, maeneo mengi ya Mkoa wa Lindi Vijiji vyake havijapata umeme. Wakandarasi wale kasi yao siyo nzuri hasa maeneo ya Vijji vya Nachingwea na Kilwa Kisiwani.
Je, ni lini Serikali itakamilisha usambazaji wa umeme Vijiji vya Mkoa wa Lindi? (Makofi)
Name
January Yusuf Makamba
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bumbuli
Answer
WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Tecla Mbunge kutoka Lindi, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, vijiji takribani vijiji vyote vilivyobakia ambavyo havijapata umeme vimeingizwa katika program ya kupata umeme ya round hii ya awamu ya tatu mzunguko wa pili. Kama nilivyoeleza na changamoto zile zilizojitokeza za kupanda kwa bei ya vifaa vya umeme inashughulikiwa na imani yetu ni kwamba lengo la Serikalii la kukamilisha upelekaji wa umeme katika vijiji vyote vilivyobakia litatimia Desemba, 2022.
Name
Boniphace Mwita Getere
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bunda
Primary Question
MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza: - Je, ni lini Serikali itafikisha umeme katika Kata mbili ambazo hazijawahi kupata umeme kabisa katika Jimbo la Ndanda?
Supplementary Question 7
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kuna mradi wa densification na huu mradi ulikuwa unapeleka umeme kwenye Kitongoji cha Guta A, Gogea Mgeta, Bukoba Mgeta, Chamrio Mgeta, Tariamang’ari Kumsanga. Huu mradi wa densification ambao umekuwepo kwa muda mrefu, kasi yake ya kufanya kazi kwenye maeneo hayo imekuwa ni kidogo sana. Ni lini sana hivi vitongoji maalum ambavyo vina miradi mingi vitapata umeme wa densification?
Name
January Yusuf Makamba
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bumbuli
Answer
WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Getere Mbunge wa Bunda kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu maneno aliyoyataja ni mahsusi kwa mradi mahsusi basi ningependa baada ya hapa tuzungumze naye na wataalam wangu ili kuona changamoto mahususi katika eneo hilo ni zipi na tuweze kusaidia kuzitatua. (Makofi)
Name
Dr. Joseph Kizito Mhagama
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Madaba
Primary Question
MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza: - Je, ni lini Serikali itafikisha umeme katika Kata mbili ambazo hazijawahi kupata umeme kabisa katika Jimbo la Ndanda?
Supplementary Question 8
MHE. DKT. JOSEPH K. MHAGAMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, Kijiji cha Ifinga kipo kilometa 48 kutoka Kijiji cha Wino ndani ya Halmashauri ya Madaba. Kijiji hiki kiliahidiwa umeme tangu miaka Mitatu iliyopita na mpaka sasa hakuna utekelezaji.
Je, ni lini wananchi wa Ifinga watanufaika na kodi za Watanzania kwa kupata umeme wa uhakika?
Name
January Yusuf Makamba
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bumbuli
Answer
WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Joseph Mhagama Mbunge wa Madaba kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, ningependa Mheshimiwa Mbunge baada ya kipindi hiki basi tuonane pamoja na wataalam wetu wa REA tuone iwapo kuna changamoto mahsusi ambazo zimepelekea hata Wakandarasi kutokuwepo site katika vijiji ambavyo imani yetu ni kwamba vijiji vyote nchini vimejumuishwa katika REA awamu ya tatu mzunguko wa pili.
Name
Innocent Sebba Bilakwate
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kyerwa
Primary Question
MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza: - Je, ni lini Serikali itafikisha umeme katika Kata mbili ambazo hazijawahi kupata umeme kabisa katika Jimbo la Ndanda?
Supplementary Question 9
MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
REA awamu ya kwanza Wilayani Kyerwa ilipita laini kuu na wakapeleka umeme kwenye maeneo ya center. Kwa hiyo vijiji vingi pamoja na vitongoji havijafikiwa na umeme.
Ni lini Serikali itapeleka umeme kwa wale wananchi ambao walipitiwa na laini kuu?
Name
January Yusuf Makamba
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bumbuli
Answer
WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Innocent Bilakwate Mbunge wa Kyerwa, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyoeleza awali kwamba vijiji vyote vimeingizwa katika mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa pili na iwapo kuna maeneo ya vijiji ambayo hayajaingizwa basi tutawasiliana na Mheshimiwa Mbunge kuhakikisha kwamba yanaingizwa na kuhakikisha kwamba vijiji hivyo vinapata Mkandarasi ambaye atafanya na kumaliza kazi hiyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu vitongoji ipo program mpya ambayo inaandaliwa ya kupeleka umeme katika vitongoji vyote. Ningependa pia kuongeza kwamba wiki moja kabla ya bajeti yetu ya Wizara ya Nishati hapa katika viwanja vya Bunge kwa ridhaa ya Mheshimiwa Spika, tutawaleta Wakandarasi wote nchi nzima na mameneja wote wa TANESCO nchi nzima na waratibu wote wa REA nchi nzima, watakuwepo hapa kwa muda wa siku nne katika viwanja vya Bunge, ambapo Waheshimiwa Wabunge watapata fursa ya kupata majibu ya moja kwa moja kwa Wakandarasi hao. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho ni kwamba Serikali imeamua kuajiri waratibu wa miradi ya REA kwa kila Jimbo. Kama inafahamika REA haina watumishi kwenye wilaya kutokana na changamoto za maswali mengi kuhusu maendeleo ya miradi ya REA tumeamua kwamba kila Jimbo kutakuwa na mtu mahsusi wa REA ambaye atakuwa ni kiungo kati ya Wabunge, Wizara, TANESCO na Mkandarasi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, maombi ya ajira hiyo yapo Ofisi ya Rais Utumishi, imani yetu ni kwamba kibali kikitoka mapema kabla ya bajeti yetu basi hao watu watakuwepo wakati wa bajeti yetu ili tuwaunganishe na Wabunge, kila Mbunge awe na mtu wake anayemjua ambaye atakuwa anamtuma wakati wowote au anampa taarifa Mheshimiwa Mbunge kuhusu maendeleo ya miradi ya REA na pale panapokwama basi huyo awe kiungo kati ya Wabunge, Halmashauri, REA, TANESCO na Wizara. (Makofi)
Name
Eng. Stella Martin Manyanya
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Nyasa
Primary Question
MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza: - Je, ni lini Serikali itafikisha umeme katika Kata mbili ambazo hazijawahi kupata umeme kabisa katika Jimbo la Ndanda?
Supplementary Question 10
MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.
Kwa kuwa, Serikali inawekeza fedha nyingi sana katika kusambaza umeme hasa kwa njia ya nguzo katika maeneo yetu. Lakini unakuta kwamba hizo nguzi sasa badala ya kuishi miaka 15 angalau ndio iwe life span yake inaishi wakati mwingine ni miaka 4 nguzo inadondoka. Je, Serikali ina mpango gani wa kuwachukulia hatua kali au kuwafukuza kabisa hawa watengenezaji wa nguzo hizo hafifu ili kupunguza gharama ambazo zitajitokeza katika ku-maintain mfumo wa TANESCO?
Name
January Yusuf Makamba
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bumbuli
Answer
WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Stella Manyanya kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kama unafahamu wiki kadhaa zilizopita nilikuwa Mafinga kuzungumza na wadau wa nguzo nchini ambapo moja ya masuala tuliyozungumza kwa kina ni uhakika wa upatikanaji wa nguzo zenye ubora wa kutosha kwa ajili ya miradi ya TANESCO na REA.
Ni kweli ipo changamoto kwamba katika maeneo mengi nguzo zilizowekwa hazikidhi viwango na ubora. Changamoto hiyo siyo tu kwa wauzaji wa nguzo bali hata kwetu sisi TANESCO na REA kwa sababu mpaka nguzo inasimikwa maana yake tumeipokea na kuikubali.
Kwa hiyo, tumeweka utaratibu mpya wa kuhakikisha pamoja na kwamba nguzo tutazipata ndani ya nchi lakini mfumo wa udhiti wa ubora unaanzia kiwandani, unaanzia kwetu sisi, mnunuzi pia na taasisi zinazohusika na ubora ikiwemo TBS. Kwa hiyo upo mfumo mpya ambao umewekwa sasa hivi wa kudhibiti viwango na ubora kwa nguzo zinazohitajika.
Name
Bupe Nelson Mwakang'ata
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza: - Je, ni lini Serikali itafikisha umeme katika Kata mbili ambazo hazijawahi kupata umeme kabisa katika Jimbo la Ndanda?
Supplementary Question 11
MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza.
Ni lini Serikali itapeleka umeme katika Kijiji cha Malangali kilichopo Wilaya ya Sumbawanga Mjini, ambacho waliambiwa wananchi wanaokaa pale watalipwa fidia halafu watapelekewa umeme. Sasa ni lini Serikali itapeleka umeme katika Kijiji hicho? Ahsante.
Name
January Yusuf Makamba
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bumbuli
Answer
WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Bupe kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya Bunge la Bajeti nitatembelea Mkoa wa Rukwa na nitafika eneo hilo ili kupata taarifa ya kina lakini na kutoa uhakika kwa wananchi kuhusu lini mradi wa umeme katika Kijiji hicho utakamilika.