Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Tunza Issa Malapo

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TUNZA I. MALAPO aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kukuza utalii wa fukwe za bahari nchini?

Supplementary Question 1

MHE. TUNZA I. MALAPO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri nataka tu kujua wanasema kubaini maeneo mapya ya uwekezaji kwani yale ya zamani Mheshimiwa Waziri mmeyaendeleza? Hilo swali langu la kwanza?

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi kule kwetu Mtwara hususan wilaya ya Mtwara ambayo inahusisha Jimbo la Mtwara mjini na Mtwara Vijijini kuna fukwe nzuri sana ambayo ikiendelezwa itavutia utalii na hivyo kusababisha shughuli za maendeleo pale Mtwara zipatikane sasa swali langu. Serikali imejipanga vipi kuhakikisha wanatangaza fukwe zile zinaendelezwa ili watalii waje? Nakushukuru.

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Tunza Issa Malapo Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo. Kwanza nimpongeze Mheshimiwa Tunza kwa kuliona hili na mimi niseme tu kwamba haya maeneo ambayo ni maeneo ya fukwe kwa asilimia kubwa yanamilikiwa na Serikali za Mitaa lakini pia na wananchi binafsi. Kwa hiyo sisi tumekuwa tukitafuta wawekezaji lakini baada ya kutafuta wawekezaji tunawapeleka katika wamiliki ambao wanamiliki haya maeneo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo baada ya Royal Tour ambayo Mheshimiwa Rais, tunamshukuru sana, ameizindua na pia kutafuta wawekezaji tumetengeneza namna na mbinu bora ya kuwakutanisha sasa hawa wamiliki wa maeneo haya na kuyaweka wazi na kuyasajili ili sasa kuwepo na uwezekano ukipata mwekezaji basi unamuonyesha tu kwamba nenda hapa.

Kwa hiyo nimuondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge kwamba sasa hivi Serikali inayashughulikia kwa ukaribu na hivi punde tutaanza kuwaona wawekezaji wengi wanaenda kwenye maeneo haya na tutahakikisha wanayapata kwa sababu tayari tumeshaanza kuyasajili na wamilki wameshakuwa wazi na wameshaanza kuiona Serikali na tayari tuna mpango mzuri ahsante.

Name

Asya Mwadini Mohammed

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TUNZA I. MALAPO aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kukuza utalii wa fukwe za bahari nchini?

Supplementary Question 2

MHE. ASYA MWADINI MOHAMMED: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Kwa kuwa nchini kuna maeneo ya fukwe ambayo yameendelezwa kiutalii, lakini maeneo haya yanakabiliwa na changamoto kubwa ya uchafuzi wa mazingira.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuyahifadhi maeneo haya ili kuweza kuwavutia watalii nchini?

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Asya Mohammed, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni jukumu la Serikali kuhakikisha kwamba maeneo yote ambayo tunapeleka watalii lazima yawe ni masafi yenye kuvutia ili tuendelee kupata watalii. Kwa hiyo nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kwenye yale maeneo ambayo yanaonekana yana changamoto hizo Serikali itaendelea kuchukua hatua ili kuhakikisha kwamba maeneo haya yanavutia na wawekezaji na watalii waendelee kuja.

Name

Neema William Mgaya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TUNZA I. MALAPO aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kukuza utalii wa fukwe za bahari nchini?

Supplementary Question 3

MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Kwa kuwa ni muda mrefu Nyanda za Juu Kusini tumekuwa tukiainisha vivutio vipya mbalimbali vya utalii, lakini vile vile Nyanda za Juu Kusini tumebarikiwa kuwa na hifadhi ya kipekee ya Kituro ambayo hifadhi hii ulimwenguni ni aina ya kipekee, hakuna ambayo inafanana nayo.

Je, Serikali mmejipanga vipi kuhakikisha kwamba mnakuza utalii wa nyanda za juu kusini?

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Neema Mgaya Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote nimpongeze sana Mheshimiwa Neema kwa kuendelea kuhamasisha utalii na hili ninalisema kwa dhati kabisa kwa sababu sasa hivi focus yetu ni kuelekea kwenye Nyanda za Juu Kusini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna mradi wa REGROW ambao ulishaanza tayari na tayari ni mradi ambao una madhumuni ya kuboresha maeneo ya Nyanda za Juu Kusini hususan miundombinu. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, kwa kuwa Kaskazini sasa hivi tunaelemewa watalii nikimaanisha kwamba ukipeleka watalii 1000 tayari kule kuna jam; focus ya Serikali ni kuelekeza hawa watalii sasa warudi nyanda za juu kusini na maeneo mengine na ndiyo mkakati wa Serikali. Nimhakikishie kwamba uhamasishaji unaoendelea sasa hivi ni kuwekeza lakini pia na kuhamasisha utalii katika maeneo ya Nyanda za Juu Kusini.

Kwa hiyo hili tumeliona na tunaendelea kulitengenezea mkakati madhubuti. Ahsante sana.