Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. Christina Christopher Mnzava
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA K.n.y. MHE. KABULA E. SHITOBELA aliuliza: - Je, kuna mkakati gani wa kudhibiti matukio ya ubakaji na ulawiti katika shule za bweni?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu lakini vitendo vya ubakaji na ulawiti wa watoto wadogo ni vitendo ambavyo vimekithiri katika nchi yetu na moja ya sheria ni kufungwa kifungo cha miaka 30 jela. Je, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka kwa sababu ubakaji ni uuaji, kuleta mabadiliko ya sheria ili wabakaji na walawiti wa watoto waweze kuhukumiwa kifungo cha kifo?
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Mnzava kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli anayozungumza Mheshimiwa Mbunge kwamba imekuwepo sheria ya miaka
30 lakini inaonekanika kama ni sheria legevu kidogo naye Mheshimiwa Mbunge anatoa mawazo, anatoa mapendekezo kwa nini isiwepo adhabu hiyo?
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba tubebe mawazo yake hayo twende tukayafanyie tathmini tuweze kuangalia namna gani sheria hiyo inaweza kubadilishwa.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved