Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Iddi Kassim Iddi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Msalala

Primary Question

MHE. IDDI K. IDDI K.n.y. MHE. HUSSEIN N. AMAR aliuliza: - Je, ni lini Serikali itajenga chujio la kuchuja na kutibu maji toka chanzo cha maji Nyamtukuza kabla ya kuyapeleka kwa wananchi?

Supplementary Question 1

MHE. IDD K. IDD: Mheshimiwa Mwenyekiti ahsante sana. Kwanza kabisa tunaipongeza Serikali kwa majibu mazuri haya na kwa kuwa mradi huu tayari umekamilika, sasa ni lini Wizara itatenga fedha ili kupeleka maji katika Kata ya Shabaka, Kata ya Kaboha, Kata ya Busolwa na Kata ya Mwingiro?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili la nyongeza; kwa kuwa Mradi huu wa Mangu – Ilogi umeshakamilika, je, ni lini sasa Serikali itatenga fedha kwa ajili ya kupeleka maji katika Kata ya Runguya na Kata ya Segese? Ahsante sana.

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Idd kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge, kwa kuwa tunaendelea na mpango na bajeti wa mwaka huu unaokuja wa 2023/2024, maombi yake tutayaingiza katika bajeti hiyo ili wananchi wa maeneo husika waweze kufaidika na huduma bora ya maji. (Makofi)

Name

Catherine Valentine Magige

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. IDDI K. IDDI K.n.y. MHE. HUSSEIN N. AMAR aliuliza: - Je, ni lini Serikali itajenga chujio la kuchuja na kutibu maji toka chanzo cha maji Nyamtukuza kabla ya kuyapeleka kwa wananchi?

Supplementary Question 2

MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwa muda mrefu sana Jimbo la Monduli hasa katika Kata ya Sepeko, Mswakini, Lepulko, Narami na Lemoti kumekuwa na changamoto kubwa ya maji. Je, ni lini Serikali itatimiza ahadi zake katika maeneo haya? (Makofi)

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Catherine Magige, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, niendelee tu kuwakumbusha wananchi kwamba miradi ya maji imeweza kutekelezwa katika miaka hii iliyopita, lakini kuna baadhi ya maeneo ambayo bado hatujawafikia. Tuwaahidi tu kwamba kwa kuwa tunaenda kwenye bajeti husika tutawaingiza katika bajeti hii inayokuja ili waweze kupata huduma bora ya maji safi.