Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Joseph George Kakunda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Sikonge
Primary Question
MHE. JOSEPH G. KAKUNDA aliuliza: - Je, ni lini Wananchi wa Sikonge watapatiwa eneo la hekta 33,000 kwenye Mbuga ya Ipembampazi litumike kwa kilimo na ufugaji?
Supplementary Question 1
MHE. JOSEPH G. KAKUNDA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali, hata hivyo nina maswali mawili madogo ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; kwa kuwa Bwawa la Olua ambalo lilizinduliwa na Mwalimu Nyerere tarehe 15 Julai, 1977, yeye mwenyewe aliahidi kwamba atatoa eneo kwa ajili ya scheme ya umwagiliaji kwa kutumia maji ya bwawa hilo.
Je, ahadi ya Rais tangu lini ilifutwa?
Swali la Pili; kwa kuwa Mawaziri sita wa Maliasili wameshalitembelea eneo hilo tangu mwaka 2010 na Waziri wa mwisho alikuwa Mheshimiwa Dkt. Hamis Kigwangalla mwaka 2019: -
Je, ni lini ahadi ile ya Mheshimiwa Rais na ahadi ya Waziri wa Maliasili itatekelezwa?
Name
Mary Francis Masanja
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Joseph George Kakunda, Mbunge wa Sikonge kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kwanza nirejee tu kwenye jibu langu la msingi kwamba maeneo haya yanapokuwa yameombwa mara nyingi wataalam wanaenda kuhakiki na wanaangalia kama kuna maeneo ambayo ndani yake kuna wanyama wakali na waharibifu hususani tembo, pia tunaangalia vitu mbalimbali ikiwemo masuala ya ikolojia wataalam walipoenda kuangalia walikuta umuhimu wa maeneo haya kuendelea kuhifadhiwa, na hii ahadi iliyotolewa ilikuwa ya mwaka 1977, tunatambua kabisa hifadhi hizi zinasimamiwa na Halmashauri lakini pale ambapo kunakuwa na umuhimu wa kuwaachia wananchi basi Serikali inafanya tathmini na inarejea na kuwarudishia wananchi waendelee kuyatumia kwa ajili ya shughuli nyingine.
Mheshimiwa Spika, naendelea kumuomba tu Mheshimiwa Mbunge kwamba ahadi bado ipo, tathmini itaendelea kufanyika na pale ambapo tutaona kuna umuhimu wa kuyarejesha haya maeneo basi tutafanya hivyo.
Name
Robert Chacha Maboto
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bunda Mjini
Primary Question
MHE. JOSEPH G. KAKUNDA aliuliza: - Je, ni lini Wananchi wa Sikonge watapatiwa eneo la hekta 33,000 kwenye Mbuga ya Ipembampazi litumike kwa kilimo na ufugaji?
Supplementary Question 2
MHE. ROBERT C. MABOTO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Wananchi wa Jimbo la Bunda Mjini mwaka 2021/2022 ambao mashamba yao yaliliwa mashamba yao hawajalipwa fidia yao. Je, Serikali itawalipa lini? Ahsante.
Name
Mary Francis Masanja
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Maboto Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, tumejitahidi sana kupunguza madai ya kifuta machozi na kifuta jasho, kwa upande wa Mkoa wa Mara ninaahidi tu kupitia Bunge lako hili ndani ya kipindi hiki tunachoendelea na bajeti tutaenda kumalizia madai haya. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved