Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Daniel Edward Mtuka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Manyoni Mashariki
Primary Question
MHE. DANIEL E. MTUKA aliuliza:- Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni imepata USD 17 milioni katika mgao wa USD 500 milioni zilizotolewa na Serikali ya India kusaidia miradi ya maji kwa bajeti ya 2016/2017. Je, ni lini fedha hizo zitaanza kupelekwa katika Halmashauri husika ikizingatiwa kuwa shida ya maji imezidi kuwatesa wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni na kwingineko katika nchi yetu kwa ujumla?
Supplementary Question 1
MHE. DANIEL E. MTUKA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa muda niulize swali la nyongeza.
Kwa kuwa hali ya maji Manyoni ni tete kwa watu na kwa mifugo. Tunajua bado taratibu za mkopo zinaendelea. Wakati wa Mkutano wa Tatu, aliyekuwa Mheshimiwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Mwigulu Nchemba wakati anawasilisha hotuba yake ya bajeti alisema analitambua suala la ukame na hasa kwenye maeneo yale kame na kuna utaratibu Wizara ya Kilimo itawasiliana na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa waweze kupata kibaliā¦
MHE. DANIEL E. MTUKA: Nakuja kwenye swali. Barua ile ilikuwa imeshaandikwa kwa maana ya mawasiliano ya Wizara mbili ya Kilimo na Wizara ya Ulinzi. Sasa swali, Wizara ya Ulinzi au Serikali inatoa majibu gani kuhusiana na mawasiliano ya Wizara ya Kilimo ili kuweza kuruhusu yale magreda kwenda kutuchimbia mabwawa kwa ajili ya watu na mifugo kwa ajili ya umwagiliaji? Ahsante.
Name
Jenista Joackim Mhagama
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Peramiho
Answer
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Spika, naona Mheshimiwa Mbunge pamoja na kuuliza swali la nyongeza anajaribu kutushauri Serikali kutumia Wizara na taasisi zilizopo ndani ya Serikali kushughulika tatizo hilo. Ningeshauri tu tuwasiliane naye halafu tuweze kujua tunaweza kuunganishaje hizo taasisi katika kutatua tatizo lake. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved