Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Conchesta Leonce Rwamlaza

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itapeleka maji katika Kata za Maruku, Karabagaine, Nyakato, Kunazi, Katoma, Kemondo na Bujugo Jirani na Bukoba Manispaa?

Supplementary Question 1

MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Pamoja na majibu ya Serikali ninayo maswali mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza, napenda kujua sasa kwa miradi ambayo inaendelea itakamilikalini?

Swali langu la pili, Bukoba Manispaa mradi wake una chanzo cha uhakika ambacho ni Ziwa Victoria. Je, Serikali haioni kwamba kwa kushirikiana na BUWASA wanaweza kutazama uwezekano wa kutumia mradi huu ambao una maji mengi, ambao unaweza kupeleka maji katika Kata za Bujugo na Maruku? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI K.n.y. WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali madogo mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Conchesta Leonce Rwamlaza, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, miradi ambayo imeanza kama ambavyo tumeainisha hapa, mingine ipo asilimia 88 maana yake iko katika hatua za mwisho za utekelezaji wake, kwa hiyo kikubwa tu nimhakikishie kwa niaba ya Waziri wa Maji kwamba Wizara itaendelea kufuatilia kwa karibu ili miradi yote itekelezeka kama ambavyo tumesainiana katika mikataba kati ya Wizara na Mkandarasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu chanzo cha uhakika cha Ziwa Victoria na maoni ambayo umeyatoa Wizara imeyapokea na itayafanyia kazi ili kuhakikisha tutumie hicho chanzo kuwaletea huduma wananchi wa Bukoba Manispaa. Ahsante sana. (Makofi)