Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Faida Mohammed Bakar
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. FAIDA MOHAMED BAKAR (K.n.y. MHE. BAHATI ALI ABEID) aliuliza:- Simu fake zimezimwa kwa sababu ya madhara ya kiafya kwa Watanzania. (a) Je, wananchi wanaoendelea kuzitumia kwa matumizi mengine hazitawaletea madhara ya kiafya? (a) Kama zina madhara, je, Serikali haioni kuwa sasa ni wakati muafaka wa kutoa elimu kwa umma?
Supplementary Question 1
MHE. FAIDA MOHAMED BAKAR: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi ya kuuliza swali moja la nyongeza.
Kwa kuwa simu fake mpaka sasa hivi zinaingizwa hapa nchini na wananchi wengi huwa wanazinunua kwa kuona kana kwamba sio simu fake, maana hazina utambulisho rasmi kuonekana hii ni fake ama hii si fake, unaweza ukaiona simu kubwa, ukaipenda kumbe hiyo ndiyo fake yenyewe. Sasa baada ya wananchi kuzinunua simu hizo hapo, TCRA wanazifungia kwa kuona kwamba ndiyo simu fake, mimi naomba kuuliza hivi; kwa nini Serikali haioni umuhimu wa kuwafungia wale wanaozileta badala ya kuwanyanyasa wananchi? Ahsante sana.
Name
Prof. Makame Mnyaa Mbarawa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkoani
Answer
WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Spika, ni kweli bado zinaingia simu fake lakini mara ukienda kununua simu, ukiiwasha pale kama simu fake haiwezi kuwaka. Sasa kabla ya kulipia simu unaponunua hakikisha kwamba unamwambia yule muuzaji akutilie line pale na ujaribu, kama ni simu fake simu hiyo haiwezi kuwaka kwa sababu simu zote fake sasa hivi zinazoingia nchini haziwezi kufanya kazi.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved