Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ndaisaba George Ruhoro

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngara

Primary Question

MHE. NDAISABA G. RUHORO aliuliza: - Je, lini Mradi wa Bwawa la kufua umeme wa RUSUMO utazinduliwa ili kuondoa tatizo la kukatika kwa umeme Ngara?

Supplementary Question 1

MHE. NDAISABA G. RUHORO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Nimefurahishwa na majibu ya Serikali nina swali moja la nyongeza. Kwa kuwa eneo lile la Rusumo limewahi kukumbwa na majanga ya moto hasa eneo lile ambalo bwawa lenyewe limejengwa. Na kwa kuwa ulipotokea moto tulilazima kuomba ndege ya kuzima moto kutoka Taifa Jirani. Ni upi mkakati wa Wizara wa kuhakikisha tunakuwa na gari la zimamoto ili kulinda miundombinu yetu tuliyowekeza pale, pale itakapotea majanga ya moto kama ilivyotea huko nyuma? Ahsante sana. (Makofi)

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nishukuru kwa niaba ya Serikali kwa kufurahishwa na majibu haya na ukamilikaji wa mradi. Nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa kufatilia mradi wote lakini hasa suala la kuzima moto. Nimuahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inalichukua tunaamini mradi utakapo kamilika kuna serving ambayo itatafanyika. Tutahakikisha basi tunawashawishi ili waombe katika mahitaji yao muhimu ya matumizi ya ile pesa itakayobaki.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia katika Miradi ya CSR ambayo itaanza kufanyika baada ya mradi kukamilika tutawashauri pia walilete kama moja wapo ya hitaji lao ili tuweze kulifanyia kazi na Serikali itahakikisha kwamba linafanyika kwa ajili ya ku–safe guard maisha ya watu wanayo tumia maeneo hayo.

Name

Boniphace Mwita Getere

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda

Primary Question

MHE. NDAISABA G. RUHORO aliuliza: - Je, lini Mradi wa Bwawa la kufua umeme wa RUSUMO utazinduliwa ili kuondoa tatizo la kukatika kwa umeme Ngara?

Supplementary Question 2

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Mheshimiwa Waziri nawashukuru sana Wizara ya Nishati, mmeleta pale vijiji 33 kutengeneza umeme kilometa mbili mpaka kilomita tatu na sasa Mkamburo Mkandarasi atengeneze kilometa moja tu na ameleta mzozo mkubwa kwa wananchi wale waliyopimiwa mara ya kwanza kuwaonyesha kwamba ni kilomita mbili. Ni lini sasa mtaongeza hizo kilomita mbili au tatu zilizokuwa zimepungua kutoka kilometa tatu mlizokuwa mmeongeza zamani? (Makofi)

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, tayari tunaendelea kukamilisha mikataba ya kuongeza kilomita mbili kwa kila kijiji kutoka kwenye ile kilomita moja ambayo ilikuwa inafanyika katika ya awamu ya tatu mzunguko wa pili wa REA.

Mheshimiwa Naibu Spika, siku siyo nyingi wakandarasi wale ambao wameonekana wakikidhi kufanya vizuri miradi hii ya REA three round two watakuja site kuonyeshwa hizo kazi za nyongeza. Wale ambao wameonekana wakilegalega tutahakikisha tunapata wengine ili waje wafanye hiyo kazi na kuikamilisha yote kwa pamoja.

Name

Salome Wycliffe Makamba

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NDAISABA G. RUHORO aliuliza: - Je, lini Mradi wa Bwawa la kufua umeme wa RUSUMO utazinduliwa ili kuondoa tatizo la kukatika kwa umeme Ngara?

Supplementary Question 3

MHE. SALOME W. MAKAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi Kata ya Mamboya katika Jimbo la Kilosa maeneo mengi hakuna umeme. Nini mpango wa Serikali kuweka umeme katika maeneo hayo?

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo tumeeleza mara kwa mara hapa Bungeni ni azima ya Serikali wa Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha kwamba kabla kabla ya Desemba, 2023 vijiji vyote vimepata umeme. Naamini katika kata hiyo waliyoitaja vijiji vilivyomo ambavyo havijapata umeme vinakuwa vimepata umeme kabla ya mwezi Desemba kuisha mwaka huu.

Name

Festo Richard Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makete

Primary Question

MHE. NDAISABA G. RUHORO aliuliza: - Je, lini Mradi wa Bwawa la kufua umeme wa RUSUMO utazinduliwa ili kuondoa tatizo la kukatika kwa umeme Ngara?

Supplementary Question 4

MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante Wilaya ya Makete mmetupatia mradi wa ujenzi wa Bwawa la Umeme la Rumakali mmeishafanya demarcation, mmeifanya tathimini ni takribani miezi mitano toka mmefanya hivyo amjaanza kulipa kwa maana kuwalipa wafanyakazi wale. Muda huu wananchi wa Makete wanawasikiliza ni lini Serikali itawalipa wananchi wanaozunguka bwawa hilo ili waachane na shughuli za kilimo na za kiuchumi zilizoko pale waanze kufanya shughuli zingine? Ahsante. (Makofi)

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, nikweli Serikali ya Awamu ya Sita inayo dhamira ya kujenga Mradi wa Rumakali wa kuzalisha megawati 222 kwa kutumia nguvu ya maji. Kama alivyosema Mheshimiwa Festo tayari tumeishafanya upembuzi yakinifu na tathimini ya site imeishafanyika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kinachotarajiwa sasa ni mwezi unaofuata wa sita wananchi wataenda kuonyweshwa nani atalipwa shilingi ngapi, ili kwenye mwaka wa fedha unaokuja kuanzia Julai fidia hiyo iweze kufanyika. Kwa hiyo, wananchi wawe na subiri kidogo ndani ya miezi miwili, mitatu fidia yao itaanza kulipwa kwa ajili ya kupisha maeneo ya mradi.