Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Regina Ndege Qwaray

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. REGINA N. QWARAY K.n.y. MHE. ZACHARIA P. ISSAAY aliuliza: - Je, ni lini ujenzi wa maabara za sayansi katika shule za sekondari utakamilika kama ilivyokusudiwa katika bajeti ya 2022/2023?

Supplementary Question 1

MHE. REGINA N. QWARAY: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kuniona. Swali la kwanza; je, kwa shule ambazo zimekwishakukamilisha maabara, Serikali ina mkakati gani wa kupeleka wataalam wale lab technician ili waweze kutoa huduma katika maabara hizo? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, je, Serikali ina mkakati gani kwa maabara ambazo zimekwishakukamilika kupeleka vifaa ili wanafunzi waanze kujifunza kwa vitendo zaidi? (Makofi)

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI): Mheshimiwa Spika, kwenye swali lake la kwanza la nyongeza lini shule hizi ambazo maabara zimekamilika zitapelekewa wataalam. Serikali imetangaza ajira 21,000 kwa sekta ya elimu na afya na katika walimu tutaajiri jumla ya walimu karibia 13,390 ambapo wengi watakuwa ni walimu wa sayansi ili kwenda kukidhi hitaji hili la maabara katika shule hizi ambazo Serikali ilipeleka fedha kumalizia maabara.

Mheshimiwa Spika, nikienda kwenye swali lake la pili la vifaa. Serikali itapeleka vifaa hivi kadri ya upatikanaji wa fedha lakini ni priority ya Serikali kuhakikisha wataalam wanapofika katika maabara hizi vilevile na vifaa vinakuwepo vya kufundishia.