Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Furaha Ntengo Matondo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FURAHA N. MATONDO K.n.y. MHE. KABULA E. SHITOBELO aliuliza: - Je, lini Serikali itaongeza wauguzi katika Hospitali ya Bugando kwani kwa sasa ina upungufu wa wauguzi 1,200?

Supplementary Question 1

MHE. FURAHA N. MATONDO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Bugando ni Hospitali ya Kanda, kutokuwa na watumishi wa kutosha kunaathiri utendaji kazi na hivyo kusababisha vifo vingi sana; na kwa kuwa Bugando inahudumia mikoa ya Kanda ya Kati, mikoa ya Kanda ya Magharibi na mikoa ya Kanda ya Ziwa: Je, Serikali haioni sasa kuna haja ya kulipa umuhimu suala hili ili kuweza kupata watumishi wa kutosha na kuweza kuondokana na tatizo lililopo la vifo vingi vya wananchi wetu?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza tunapokea maombi yake, na tutaenda kuyachakata kwa sababu Hospitali ya Bugando kwa siku inapata wagonjwa 1,200 mpaka 1,500 na unaona idadi ya watumishi hapa ni 1,930. Sasa tutaenda kuchakata tuone tutakachoweza kufanya, lakini mwaka 2022 walipewa watumishi 367. Kwa hiyo, tutaendelea. Kwa kuimarisha Hospitali ya Kanda ya Chato na kuimarisha hospitali yetu ya mkoa iliyopo pale na hospitali za wilaya, foleni itapungua kwenye eneo la Bugando na itawezekana sasa kumaliza hili tatizo la watumishi na msongamano uliopo pale.