Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Issa Ally Mchungahela
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lulindi
Primary Question
MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA aliuliza: - Je, lini Serikali itamaliza tatizo la umeme Mkoani Mtwara hususani Wilaya ya Masasi na Jimbo la Lulindi?
Supplementary Question 1
MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nisikitike sana kutokana na majibu ya Naibu Waziri, haya majibu sidhani kama wanafanya research. Manati, watoto wanapiga vikombe kweli? Ni kitu cha kushangaza sana, lakini sasa kinachonishangaza zaidi kwenye chanzo cha umeme ndiko kwenye shida kubwa ya umeme. Je, ni lini Serikali itatuhakikishia kwamba huku tunapata umeme wa uhakika? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimekuwa nikilalamika hapa kila siku kuhusiana na Jimboni kwangu Lulindi. Mkandarasi alipewa vijiji takribani 30 kushughulika na umeme kwa maana ya viunganishi, hakushughulikia hata kijiji kimoja, nimekuwa nikiimba kama wimbo. Je, ni lini nitaacha kuja hapa kulalamika kuhusiana na suala la umeme jimboni kwangu? (Makofi)
Name
Stephen Lujwahuka Byabato
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bukoba Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyomalizia paragraph ya mwisho; upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa Mkoa wa Mtwara utatokana na kukamilisha hizi njia mbili ambazo zinaleta umeme wa gridi ya Taifa kutoka katika maeneo mengine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kuna tatizo kwenye njia ya umeme, hata kama ni kwenye eneo la chanzo umeme utakatika. Kwa hiyo, azma ya Serikali ya Awamu ya Sita ni kuhakikisha kwamba, miundombinu yote hii inarekebishwa na kuimarishwa, ili iweze kusafirisha umeme kwa wakati wote na kuwafikia wale walengwa ambao wanatakiwa kuutumia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye eneo la pili; mkandarasi anayetekeleza miradi ya REA katika eneo la Lulindi ambalo ni Masasi, ana Wilaya ya Masasi na Nanyumbu, anaitwa Namis, alikuwa katika wale wakandarasi wenye lot zile saba ambazo zilikuwa zinasuasua, lakini tumesukumana naye na kuwekeana masharti na tunaamini kufikia Disemba na yeye atakuwa amekamilisha kazi yake. Kwa Lulindi alishawasha vijiji kama sita au saba kutoka kwenye vile alivyokuwanavyo na tunaamini kabla mkataba haujaisha atakamilisha kazi kwa sababu, tunasimamiana naye kwa karibu sana.
Name
Festo Richard Sanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Makete
Primary Question
MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA aliuliza: - Je, lini Serikali itamaliza tatizo la umeme Mkoani Mtwara hususani Wilaya ya Masasi na Jimbo la Lulindi?
Supplementary Question 2
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kuuliza swali la nyongeza. Kupitia Bunge hili tuliahidiwa kwamba, umeme wa Makete watabadilisha line kutoka Mbeya kuja Makete ni line ambayo inasumbua na imechoka kwa muda mrefu na inasababisha umeme Makete kukatika mara kwa mara. Wakatuahidi kwamba, watajenga substation Wanging’ombe ili wananchi wa Makete tuchukue umeme kutoka Njombe. Je, hatua hiyo imefikia wapi ili wananchi wa Makete wanaosikiliza sasa hivi wapate uhakika wa majibu ya Serikali? Ahsante.
Name
Stephen Lujwahuka Byabato
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bukoba Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, mojawapo ya changamoto ambayo tumekuwa nayo ni umeme kusafirishwa umbali mrefu kutoka kwenye chanzo. Tulifanya tathmini kupitia TANESCO na tukabaini makundi matatu, kuna wale ambao wana shida zaidi, kuna wenye shida za kati na kuna wale ambao maisha yanaweza yakaendelea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwenye maeneo yenye shida zaidi tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita imetupatia pesa bilioni 500 kwa ajili ya kutekeleza Mradi unaitwa Gridi Imara na utajenga vituo vya kupoza umeme 14 katika awamu hii ya kwanza. Sasa nimhakikishie Mheshimiwa Festo kwamba, eneo lake nitaenda kuliangalia limewekwa kwenye category ipi katika yale maeneo matatu yenye matatizo makubwa, matatizo ya kati na matatizo ya juu na nitamfahamisha endapo kitajengwa kituo cha kupoza umeme kipindi hiki au kitajengwa katika awamu inayofuata, lakini kabla ya miaka sita ijayo kwisha tunatarajia kuwa na kituo cha kupooza umeme kwa kila wilaya ili kuondoa matatizo ya umeme kusafirishwa kwa muda mrefu.
Name
Catherine Valentine Magige
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA aliuliza: - Je, lini Serikali itamaliza tatizo la umeme Mkoani Mtwara hususani Wilaya ya Masasi na Jimbo la Lulindi?
Supplementary Question 3
MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Wilaya ya Ngorongoro tangu iunganishwe na Gridi ya Taifa mwaka jana tatizo la umeme limezidi kuongezeka. Gridi ile iliunganishwa kutoka Wilaya ya Longido, ikitokea hitilafu ya umeme katika Wilaya ya Longido, Ngorongoro wanakosa umeme, ikitokea hitilafu Ngaramtoni, Ngorongoro wanakosa umeme na ikitokea hitilafu wilayani kwao wanakosa umeme. Imekuwa changamoto kubwa sana kwa wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro. Je, ni lini wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro watapata umeme wa uhakika?
Name
Stephen Lujwahuka Byabato
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bukoba Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyotangulia kujibu swali la Mheshimiwa Festo, maeneo yote ambayo yana changamoto ya umeme kufika katika maeneo yale kwa sababu ya kusafirishwa kwa umbali mrefu yamechukuliwa katika Mradi wetu wa Gridi Imara. Nimhakikishie Mheshimiwa Catherine Magige nitawasiliana naye kumwonesha plan ya Serikali ya kuhakikisha Wilaya yetu ya Ngorongoro inapata umeme wa uhakika na unaotoka katika maeneo yake kwa sababu, kuna wananchi ambao wanatakiwa pia wapate huduma hiyo kwa usahihi kabisa.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved