Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Festo Richard Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makete

Primary Question

MHE. FESTO R. SANGA: Aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kuitangaza Hifadhi ya Taifa ya Kitulo?

Supplementary Question 1

MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante, licha ya majibu mazuri ya Serikali ya kuitangaza Hifadhi ya Kitulo lakini Serikali ina mradi wa regrow mradi ambao umejikita kwenye kutangaza utalii Kusini mwa Tanzania na hifadhi hii ni hifadhi ya kipekee Barani Afrika na Tanzania, kwa nini mradi regrow haujaenda kwenye Hifadhi ya Kitulo ili uweze kuisaidia hifadhi hii kutangazwa kwa ukubwa zaidi?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwenye Hifadhi ya Kitulo kumekuwa na changamoto ya kimahusiano kati ya wananchi na hifadhi kwa maana ya migogoro ya mipaka. Sasa katika jitihada za kutangaza utalii ni upi mkakati wa Serikali kutatua migogoro iliyopo kwenye vijiji vya Misiwa, Ujuni, Nkondo, Makwalanga, Lugoda na Igenge. Vijiji hivi kwa muda mrefu vimekuwa na mgogoro na hifadhi, upi mkakati wa Serikali kutatua mgogoro huu ili mahusiano yaweze kuimarika kati ya hifadhi na Wananchi wa Wilaya ya Makete?

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Festo Richard Sanga kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwenye upande wa miradi ya regrow, mradi wa regrow phase one ulikuwa unawezesha kufanya maboresho katika hifadhi nne ambazo ilikuwa ni Mikumi, Nyerere, Udzungwa na Ruaha, lakini Serikali inatarajia kuingia mkataba tena kwenye REGROW Phase Two ambayo Hifadhi ya Kitulo pia itaingizwa katika mradi huo. Kwa hiyo, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba Kitulo itaingizwa kwenye phase two na maboresho yatafanyika.

Mheshimiwa Spika, kwenye upande wa migogoro tulishapeleka tathmini tayari ilishafanyika na sasa hivi ni utekelezaji tu wakuainisha mipaka mipya. Kwa hiyo, nimuahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba hivi sasa naomba nielekeze tu TANAPA waende kuweka vigingi katika maeneo ambayo yameainishwa baada ya tathmini kuwa imefanyika lakini na sisi pia tutaenda kujihakikishia.