Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Mariamu Nassoro Kisangi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MARIAM N. KISANGI K.n.y. MHE ASKOFU JOSEPHAT M. GWAJIMA aliuliza: - Je, lini Serikali itamaliza migogoro ya ardhi maeneo ya Chasimba, Chatembo, Chachui, Nkasangwe na Mabwepande – Kawe?
Supplementary Question 1
MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi niweze kuuliza maswali ya nyongeza. Pamoja na majibu mazuri, kwanza naipongeza Serikali kwa niaba ya Mheshimiwa Askofu Gwajima, kwa kweli alikuwa huko na amelishughulikia suala hili na Serikali imelipokea na imelifanyia kazi. Pongezi sana kwa Serikali. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, je, Serikali imejipanga vipi sasa kuhakikisha inadhibiti migogoro yote iliyopo katika jimbo hilo ili isijirudie tena? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili. Je, Serikali imejipanga vipi kuhakikisha Mgogoro wa Shamba la Malolo upande wa Jimbo la Kibamba Halmashauri ya Ubungo nao unaumaliza kama vile walivyomaliza kwenye Wilaya ya Kinondoni? (Makofi)
Name
Geophrey Mizengo Pinda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kavuu
Answer
NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Napenda kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kwanza udhibiti wa migogoro isiweze kujitokeza, ni juhudi za Serikali na tumekuwa tukishirikiana na taasisi mbalimbali katika kuhamasisha migogoro hii isiendelee kujitokeza. Hata hivyo, suala la Malolo, Kibaha nimwahidi tu Mheshimiwa Mbunge kwamba kwamba baada ya Bunge lako Tukufu kumalizika, tutaanza ziara za kutembelea maeneo haya na kukutana na wananchi na taasisi zile ambazo zinagongana kwenye migongano hii ili kuitafutia suluhisho la kudumu, ahsante. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved