Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions from Hon. Hamidu Hassan Bobali (32 total)

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa fursa hii ya kumwuliza Mheshimiwa Waziri maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri hakujibu swali langu. Nimeuliza, Serikali haioni umuhimu wa kujenga Chuo cha Uvuvi Lindi, nikimaanisha Mkoa wa Lindi, siyo Mikindani Mtwara.
Mheshimiwa Spika, pia kwa mujibu wa hotuba ya Mheshimiwa Rais aliyoitoa humu Bungeni tarehe 20 Novemba…
MBUNGE FULANI: Hukuwepo!
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Aidha, nilikuwepo au sikuwepo lakini kuna Kitabu. (Makofi)
Mheshimiwa Rais anasema, katika kutatua tatizo la ajira nchini, ataweka mkazo katika sekta tatu; viwanda, kilimo na uvuvi. Mimi nilitegemea, Serikali ingekuja na mkakati wa kuanzisha hivi vyuo katika kila mkoa ambapo tumepakana na bahari ama kuna maziwa. Waziri anajibu, watatoa mafunzo ya muda mafupi kwa watu arobaini arobaini.
Mheshimiwa Spika, watu 40 sidhani kama ni mkakati huu anaozungumzia Rais. Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Waziri atueleze kwamba huu msisitizo alioutoa Mheshimiwa Rais ndiyo huu wa kuchukua watu arobaini arobaini?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba kwa sasa hamna chuo kinachojengwa Mkoani Lindi, lakini tulichokuwa tunaelezea ni kwamba tayari kuna jitihada ya kujenga vyuo kama hivyo katika maeneo mbalimbali nchini na tayari kuna chuo ambacho kipo karibu na Mchinga. Ni kweli kwamba Mheshimiwa Rais alielezea kuhusu umuhimu wa kujenga vyuo hivyo, lakini tayari tumeanza kwenye baadhi ya maeneo.
Mheshimiwa Spika, tayari kuna vyuo vinafanya kazi, kwa mfano tayari kuna Chuo cha Mbegani ambacho kinatoa mafunzo chenye uwezo wa wanafunzi 120; tayari kuna Chuo Kibirizi, Kigoma na Chuo cha Nyegezi Mwanza nacho kinatoa mafunzo.
Kwa hiyo, kadri tunavyozidi kuendelea, tunazidi kuanzisha vyuo katika maeneo mbalimbali na hatimaye ikiwezekana maeneo yote au Mikoa yote ambayo imezungukwa na maji, yatakuwa na vyuo hivyo. Vilevile tunatambua kwamba hatuanzishi tu vyuo kwenye maeneo ambayo yapo karibu na bahari kwa sababu tunachosisitiza siyo vyuo tu vya uvuvi katika maeneo ya bahari na maziwa, lakini hata siku hizi tunakazania sana kuhusu suala la ufugaji wa samaki (aquaculture). (Makofi)
Kwa hiyo, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba mpango upo lakini tumeanza taratibu kwasababu hatuwezi tukaanza katika maeneo yote. Nashukuru sana.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimuulize swali moja la nyongeza Mheshimiwa Waziri.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa, tatizo la pembejeo lililopo kwenye zao la ufuta lipo pia kwenye zao la korosho ambalo ni zao la pili la biashara Mkoa wa Lindi. Changamoto ya pembejeo Mkoa wa Lindi inatokana na utofauti wa maeneo na hali ya hewa. Pembejeo inayoletwa Lindi, Sulpha inaletwa mwezi wa 5 mwezi wa 6 ambao kwa Mchinga wakati huo inakuwa tayari korosho zimeishaanza kuzaa, lakini maeneo mengine ya Tandahimba na Masasi yanakuwa bado.
Je, Serikali ipo tayari sasa, kusambaza pembejeo ya zao la korosho ifikapo mwezi wa tatu ili korosho zinazowahi katika Jimbo la Mchinga ziwahi kupuliziwa na hizo pembejeo.
WAZIRI WA KILIMO MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nishukuru sana kwa swali lake la nyongeza ni swali zuri ambalo linahusisha pia pembejeo zinazotolewa kwa mazao mengine.
Mheshimiwa Naibu Spika, niseme tu kwamba Wizara yangu, inapanga kuangalia, utaratibu mzima wa utoaji ruzuku, kama nilivyosema jana. Lakini katika kuangalia kwake, nimewaagiza wataamu wangu kila mtaalamu anayesimamia ugawaji wa pembejeo ama mbegu katika eneo husika awe na bango kitita linaloonesha msimu unaanza lini katika eneo gani, na kuhakikisha kwamba Serikali tunasimamia upatikanaji wa ruzuku ama pembejeo husika, kama ni mbegu angalau mwezi mmoja kabla ya msimu kuanza ili kuweza kuwapa fursa wakulima kupata pembejeo hizo kwa wakati.
Mheshimiwa Naibu Spika, niliongea na wataalam wangu ni aibu kwa watu waliosoma wakaaminiwa na Serikali, wakaaminiwa na wananchi wakapewa dhamana kupeleka mbegu ama mbolea ya kupandia, wakati eneo husika watu wako kwenye kupalilia na walishapanda mbegu zao na walishatumia mbolea yao. Kwa hiyo, nimeagiza watu wawe na bango kitita ambalo itasaidia kuwa na uelewa na kuwa na kitu cha kuangalia tunapopeleka pembejeo, tupeleke kwa wakati angalau mwezi mmoja kabla ya msimu kuanza.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninawaombe Wabunge, katika maeneo yenu nifikishieni kila mmoja kutoka kwake na mimi nitakuwa na bango kitita langu, anapendekeza mbegu ama pembejeo iwe imeishafika katika eneo lake ifikapo muda gani, na hiyo ndiyo nitakayotumia kusimamia Wizarani kwangu. (Makofi)
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru naitwa Bobali, Mbunge wa Mchinga.
Kwa kuwa matatizo yaliyopo katika Mkoa wa Katavi yanafanana kabisa na matatizo ya kituo cha afya ya Chalutamba katika Jimbo la Mchinga kumekuwa na kuharibika mara kwa mara kwa gari ya kituo kile.
Je, Wizara haioni kwamba kuna haja sasa ya yale magari yaliyochakaa kuya-compensate katika vituo vyote ambavyo vina magari yaliyochakaa wakapewa magari mapya?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, tumelisikia suala la Mheshimiwa Bobali, lakini mimi nikijua kwamba hapa tulivyokuwa tunapitisha bajeti tuliona vipaumbele vya kila Halmashauri, wengine walitenga gari, wengine wakatenga vituo vya afya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwa sababu yale magari yamechakaa lakini nadhani tutaangalia jambo kubwa ni kwamba kama Halmashauri tunapokaa katika priority zake katika mpango wa bajeti ni vema zaidi kuona kwamba kama gari limechaka basi tutenge bajeti maalum kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tunapata gari jipya ili kuondoa gharama za matengenezo ya kila siku.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi kama Serikali tumelisikia hilo, niwahamasishe sasa katika maeneo ya vipaumbele tuangalie lipi hasa ni kipaumbele cha wananchi katika eneo letu husika ili wananchi wapate huduma bora.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kumekuwa na tabia ya walimu kuto-report kwenye mikoa ambayo inaitwa mikoa ya pembezoni kama Mkoa wetu wa Lindi. Je, kuna mkakati gani mwaka huu wa kuhakikisha kwamba walimu watakaopangwa watakwenda Lindi kutatua tatizo kubwa la walimu lililopo kwenye shule zetu?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli, wiki iliyopita nilisema kwamba kuna tatizo, si mkoa wa Lindi peke yake, ukienda Katavi, Kigoma, Mara, Sumbawanga na maeneo mengine. Tumesema mwaka huu tu tunaajiri walimu wapatao 35,000, lakini walimu wengine wakipelekwa kule hawaendi; na kwa bahati mbaya wengine wakienda wanataka kuishia pale pale mjini. Na ndiyo maana tumetoa maelekezo mwaka huu kwamba walimu wote watakaokwenda ku-report wahakikishe wanafika vituoni.
Naomba kutoa rai, mwaka huu tumepeta maombi mengi sana ya walimu ambao ndani ya miaka mitatu, minne walishindwa ku-report wakaenda private schools, sasa hivi private schools hali imekuwa mbaya, wanakuja kuomba tena ajira Serikalini.
Tuombe kutoa maelekezo; kwamba walimu watakaoshindwa kufika katika vituo vyao wasitarajie kuja kuomba mwakani baada ya kuona kwamba wamekosa nafasi katika private schools. Hili ni agizo letu na tutaenda kulisimamia kwa nguvu zote.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimwulize swali moja la nyongeza Mheshimiwa Waziri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vita dhidi ya ukoloni ilikuwa imegawanyika katika maeneo mawili; kulikuwa na vita ambayo ilipiganwa na viongozi wetu wa jadi kabla ya kuingia kwa ukoloni ambapo walikuwa wana-resist ukoloni usiingie, lakini kulikuwa na Vita ya Maji Maji ambayo ni vita pekee iliyopiganwa wakati tayari Wakoloni wanatawala Tanganyika na sehemu ya nchi yetu. Kwa hiyo, Vita ya Majimaji ni tofauti na hivyo vingine alivyovitaja Mheshimiwa Waziri kwenye majibu yake ya msingi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile ukienda kwenye Hospitali ya Wilaya pale Kilwa, kuna orodha ndefu ya wazee wetu waliopoteza maisha tena kwa kunyongwa kutokana na Vita hivi vya Majimaji. Kwa hiyo, nataka kujua orodha ile ya wazee ambayo imewekwa pale kwenye Hospitali ya Kilwa, inatunufaishaje sisi wakazi wa Kilwa na Lindi kwa kujua tu kwamba hawa walinyongwa kwenye vita dhidi ya Ukoloni?
WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ilivyo kwa vita vingine vyote, kumbukumbu huwa zinawekwa na siyo ya Majimaji tu, ukienda katika nchi yoyote iliyopigana vita, utakuta kuna makaburi ya mashujaa na kuna majina yao kama kumbukumbu za kivita. Hoja yangu katika jibu langu la msingi ni kwamba hatupaswi kama Wazalendo kuomba fidia kwa kuitetea nchi yetu. Hii siyo kwa Maji Maji tu, hata kwa Vita vya Kagera watu walipigana; watu wamepoteza maisha; tumeweka makaburi ya mashujaa kwa wale waliokwenda kukomboa Afrika nje ya nchi. Kwa hiyo, tunachosema ni kwamba tutawakumbuka kama mashujaa na tutaendelea kuwaenzi na kuweka kumbukumbu ya kivita, lakini siyo rahisi kuwalipa fidia kwa sababu walikuwa wanajitolea kwa ajili ya nchi yao; na hii imefanywa na wengi ikiwemo Vita vya Kagera. Hakuna aliyelipwa fidia, bali tunawaenzi kwa kazi nzuri waliyoifanya kuilinda nchi yetu.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwa kuwa wananchi wa Jimbo la Mchinga wameamua kuitikia wito wa kupambana na uvuvi haramu especially uvuvi wa mabomu na wameanzisha BMU katika maeneo ya Mchinga, Mvuleni, Kijiweni na Ruvu. Je, nini kauli ya Serikali kwenye kuzisaidia na kuzijengea uwezo hizi BMU ili ziweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza niwapongeze sana wananchi wa Mkinga na ukanda huo wa Pwani kwa sababu ni kweli kwamba wameitikia ombi au mkakati wa Serikali wa kuhakikisha kwamba tunatokomeza uvuvi haramu.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba, nipo tayari kuongea naye ili tuone namna gani ya kusaidia Halmashauri yake ili waweze kutoa msaada na elimu kwa wananchi ambao wako kwenye Beach Management Units. Kwa hiyo, naomba kwa kuwa yuko kwenye Kamati yangu, tukitoka hapa, tuongee, tuangalie namna ya kusaidia.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti swali la msingi, Mheshimiwa Mbunge aliyeuliza alizungumzia fedha iliyotengwa mwaka 2013/2014 na kiwango ambacho Serikali walikuwa wamekitoa. Nataka kujua ni kiasi gani cha pesa kilitengwa na kimepelekwa katika mwaka huu wa fedha tulionao wa 2016/2017?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA NA VIJANA: Mheshimiwa Mwenyekiti, labda kabla sijaenda katika kujibu swali lake nisaidie kutoa ufafanuzi kidogo ili jambo hili lieleweke vyema.
Katika utaratibu wa kuwasaidia vijana nchini iko mifuko mingi ambayo inashughulika na shughuli hii ya kuwasaidia vijana, lakini ndani ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira tunao Mfuko wa Maendeleo wa Vijana ambao pamoja na mfuko huu tunao pia utaratibu wa utengaji wa asilimia tano za mapato ya ndani ya kila Halmashauri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi ndani ya mfuko wetu mpaka hivi sasa ninavyosema tayari tumeshakopesha vikundi vya vijana takribani 309 na wamepatiwa takribani shilingi 1,700,000,000 kwa hiyo, katika utaratibu ulioko hivi sasa, mwaka huu wa fedha tumetengewa shilingi bilioni moja ambako hizo nazo tutazisambaza kwa ajili ya vikundi vya vijana ili waweze kunufaika Nchi nzima.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Naibu Waziri naomba kuongeza tu hapo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika suala zima la Halmashauri mwaka huu katika Bajeti ya Halmashauri kwanza tulitoa maelekezo katika utengenezaji wa Bajeti ya mwaka 2016/2017 ni lazima kila Halmashauri itenge 10% ya tano kwa vijana na tano kwa akina mama ambapo jumla ya fedha zote shilingi bilioni 64.5. Katika fedha hizo sasa kwa hivi sasa katika upande wa Halmashauri tumeenda sasa hivi karibuni shilingi bilioni tano Halmashauri mbalimbali zimeshaanza kutoa hivi sasa niwaelekeze Halmashauri mbalimbali sasa suala lile siyo suala la hiari, ni suala la lazima kila Halmashauri lazima itoe asilimia tano kwa vijana na asilimia tano kwa akina mama na hata hivyo mchakato wa bajeti tunaoondoka nao hivi sasa Halmashauri yoyote tutaizuia bajeti yake mchakato wake mpaka ile commitment tuloiwekea iwe imetekelezeka katika mwaka huu wa fedha.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nishukuru kwamba uwanja wa ndege wa Lindi upo kwenye mapendekezo ya Serikali ya kutaka kuufanyia
ukarabati lakini kwa sasa wananchi wa Lindi tunakosa huduma ya ndege mpaka twende Mtwara kwa kuwa uwanja ule sasa hivi umekuwa ni chakavu sana. Nataka commitment ya Serikali, ni lini itakamilisha ukarabati wa uwanja wa ndege
wa Lindi ili ndege zianze kutua kama kawaida?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA
MAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli uwanja wa Lindi ni kati ya viwanja 11 vinavyofanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa kutumia fedha za mkopo kutoka Benki ya Dunia. Kimsingi kazi hii itakapokamilika ndipo
tutapata ratiba kamili ya tuanze wapi na tumalizie wapi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, labda tu nimkakishie
Mheshimiwa Bobali, kwamba kutokana na umuhimu wa kuhakikisha wananchi wa Lindi nao wanakuwa na kiwanja cha ndege, tutahakikisha katika kuangalia priority, na lindi tutaiangalia kwa macho matatu.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza pamoja na majibu ya Mheshimiwa Waziri, lakini majibu aliyonijibu ni too general. Mimi niliulizia suala la Kingulungundwa lakini ametoa takwimu nyingi za Magereza ya Ukonga na maeneo mengine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la kwanza la nyongeza; nahitaji kufahamu hizi nyumba 320 ambazo Mheshimiwa Waziri amezisema zinajengwa huko Ukonga na maeneo mengine; je, kati ya hizo, Kingulungundwa zinapelekwa nyumba ngapi? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, katika Gereza lile, kuna shida kubwa ya maji ambayo inasababisha wakati mwingine wafungwa na Askari watumie muda mwingi kabisa kutafuta maji. Kama inavyofahamika, hili ni Gereza maalum kwa Mkoa wa Lindi, limewekwa mbali kidogo na makazi ya wananchi kwa kazi maalum ambayo nadhani Mheshimiwa Waziri anaijua.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba kupata commitment ya Mheshimiwa Waziri ni lini Serikali itawapatia maji Gereza la Kingulungundwa na jirani zao wa Mjimwema ili kuondoa adha ambayo wanaipata wafungwa na Maafisa wa Gereza lile? (Makofi)
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Bobali, Goal Keeper wa Timu ya Bunge ya Wabunge wa Yanga, kama ifuatavyo:- (Makofi)
Moja, suala la nyumba za Ukonga; tulikuwa tunaelezea tu commitment ya Serikali kuhusu nyumba za Askari Magereza kwa maana ya kwamba zinajengwa kule, tunaendeleza ili kutatua tatizo hilo na tunakamilisha nyumba nyingine ambazo ziko katika hatua za mwisho ili Askari waweze kuhamia, hatuzihamishi zile za Ukonga kwenda Gereza lile.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu upande wa maji,
hata wakati napitisha bajeti, Mheshimiwa Salma Kikwete aliniambia hatashika shilingi, lakini anaomba siku nikipita Lindi niende kwenye Gereza hilo kujionea tatizo hilo la maji. Mheshimiwa Mbunge amelitaja jambo hili, naweka uzito, nitakapozungukia kule, nitahakikisha napita kujionea lakini hoja hiyo tumeshaipokea kama Serikali kuhakikisha kwamba tunaweka kipaumbele kuweza kuhakikisha kwamba suala la maji linaenda sambamba na hilo la barabara ambalo lilikuwepo kwenye swali la msingi. (Makofi)
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003 miongoni mwa privilege ambayo inawapa wazee ni kutibiwa bure lakini hivi sasa imekuwa kama ni uamuzi wa Daktari wa Kituo cha Afya husika ambaye anakuwepo pale. Kwa hiyo, mara nyingi wazee wamekuwa wakinyanyaswa kutokana na kukosekana kwa sheria. Mheshimiwa Waziri anatuthibitishia kwamba ni lini atatuletea Sheria ya Wazee ili kwenda sambamba na Sera ya Wazee ili wazee wetu waweze kutibiwa isiwe sasa ni privilege au maamuzi ya Daktari katika kituo husika?
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Spika, ni lini tutaleta mapendekezo ya kutungwa kwa Sheria ya Wazee kwenye Bunge lako Tukufu, hatuna uhakika ni lini exactly, lakini tutaleta sheria hiyo. Hata hivyo, mpaka sasa kuna mchakato unaendelea ndani ya Serikali na pindi tutakapopata idhini ya Baraza la Mawaziri ya kuleta sheria hiyo hapa Bungeni basi itafika. Kwa sasa tuna mchakato ndani ya Serikali, sheria hii ni muhimu.
Mheshimiwa Spika, pamoja na kutokuwa na sheria hii, tayari tumeshaanza kutekeleza afua mbalimbali ambazo zinawahusu wazee hususan kwenye sekta ya afya. Kwa mfano, tuna mkakati niliusema hapa wiki iliyopita wakati nikijibu maswali wa ‘Mzee Kwanza, Mpishe Mzee Apite’ ambao tumeu--roll out nchi nzima na mkakati huu wazee wameupenda na wameufurahia sana.
Mheshimiwa Spika, pia tumetoa mwongozo kwa kila Halmashauri nchini kuhakikisha zinawakatia kadi za CHF wazee wote ili waweze kupata huduma za afya kwenye vituo vyao. Tunachokifanya sisi ni kufanya maboresho ya huu Mfuko wa Afya ya Jamii yaani CHF ili uwe na value zaidi, uweze kumsaidia mtu kupata huduma palepale kwenye zahanati yake kijijini ama kwenye kituo cha afya na kuzunguka mkoa mzima yaani awe anapata referral kwa kutumia kadi ya CHF.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kama Halmashauri zita-comply kutekeleza mapendekezo yetu ya kuwa na kadi ya CHF kwa wazee wote ambao wanastahili kupewa kadi hizo za msamaha kwenye Halmashauri zao maana yake katika miaka hii miwili huduma za afya kwa wazee zitaboreka sana.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwa na tabia kwenye Halmashauri wanapokwenda masomoni baadhi ya watumishi kwenye Halmashauri, Halmashauri zinakuwa zinagharamia hususan wale walioko kwenye ngazi ya pale Halmashauri. Lakini si kwa kada za ualimu na kada zingine.
Je, nini kauli ya Serikali kwamba Halmashauri zinagharamia masomo kwa wale watumishi waliopo ndani ya Halmashauri pale pale au kwa watumishi wa Halmashauri nzima? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, utaratibu ni kwamba kuna utaratibu wa mapendekezo ya watu kuonyesha preference yao kwamba watu wanataka kwenda kusoma, hili mara nyingi sana huwa inawekwa katika mchanganuo wa kibajeti katika kila Idara, kwamba kila Idara ina utaratibu na mipango yake kwamba mwaka huu kuna watu wangapi wataenda kusoma. Kwa hiyo, jambo hili sio wale wa Makao Makuu peke yake hapana, jambo hili maana yake ni kwa Halmashauri nzima, kama kuna Halmashauri ambayo inafanya kuwapa upendeleo maalum wale waliopo Makao Makuu peke yake, hilo ni kosa na halikubaliki.
Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo, utaratibu ni kwamba mpango wa bajeti wanapopanga bajeti wanapanga mwaka huu Idara fulani tutapeleka watu fulani kusoma katika level fulani ambayo inaingizwa katika bajeti, then unaweka hilo open door policy katika hiyo Idara, kila mtu aweze ku-apply kuangalia nani ata-qualify katika kipindi hicho kuweza kupata fursa ya masomo, kwa sababu mkate huo ni mkate wa Halmashauri nzima siyo watu maalum katika Makao Makuu ya Halmashauri.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Hoja ya kulipa fidia watu wanaopisha mradi wa TANESCO inafanana na watu ambao walichomewa moto mashamba yao wakati wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam katika Kijiji cha Kilangala. Bahati TPDC kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Lindi waliunda Tume ya kwenda kuhakiki yale madai ya kuunguziwa moto mashamba yao mwaka 2013.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tayari tathmini imeshafanyika na kinachosubiriwa ni kulipwa tu lakini tuliahidiwa wananchi wale wangelipwa mwezi wa Julai. Naomba commitment ya Serikali, ni lini wananchi wa Kilangala watalipwa hizi fedha zao ambazo zilitokana na wao kuchomewa moto mashamba yao? Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru.
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Ni kweli tathmini ilifanyika na naomba nimtaarifu kwamba wananchi wa Kijiji cha Kilangali watalipwa kwa mujibu wa sheria na taratibu. Ahsante.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa fursa hii naomba niulize maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, uvuvi wa bahari Kuu unahitaji uwekezaji wa fedha na mitaji na wavuvi wengi katika maeneo ya Ukanda wa Pwani walikuwa wanatumia uvuvi wa kupiga mabomu ili kupata samaki na Jimboni kwangu katika maeneo ya Mchinga, Ruvu, Mvuleni, Maloo na maeneo mengine wale watu wameacha sasa upigaji wa mabomu kwa kufuata na kutii sheria za nchi sasa.
Je, nauliza Serikali ina mpango gani ya kuwasaidia hawa wavuvi ambao walikuwa wanavua kwenye eneo la bahari kuu kwa kutumia mabomu na sasa wameacha kwa kutii sheria wana mpango gani wa ziada wa kuwasaidia ili waendelee kuvua?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, ukanda wetu wa bahari una takribani urefu wa kilometa 1,424 kutoka Tanga mpaka Mtwara, lakini ukiacha maeneo ya Miji Mikuu kama Dar es Salaam, Tanga na Mtwara, maeneo yote yaliyopo kwenye ukanda wa bahari watu wake ni maskini sana. Nataka kujua, Serikali inajifunza nini kwa watu wa Ukanda wa Pwani kuwa maskini kwa kiwango kile wakati wana rasilimali hii nzuri ya bahari? Nakushukuru. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UVUVI NA MIFUGO: Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza ametaka kujua mikakati zaidi ya namna ambavyo Serikali imejipanga kuwasaidia wavuvi ili waweze kuvua katika eneo la bahari kuu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema katika jibu la msingi ya kwamba Serikali ina mipango kadha wa kadha na tayari tumekwisha anza nayo. La kwanza ni hili la kuwawezesha kupata ruzuku kupitia vikundi vyao ambapo wavuvi mbalimbali katika nchi yetu wamepata ruzuku hii ya mashine. Hata yeye Mheshimiwa Bobali wavuvi wake wa jimbo la Mchinga tuko tayari kuhakikisha kwamba wanapata mashine hizo za kuweza kwenda kuwasaidia kwenda kufika bahari kuu.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kama haitoshi, Serikali kupitia Taasisi mbalimbali na mifumo ya ushirikiano tunao mradi mkubwa wa SEOFISH ambao utakwenda kuhakikisha kwamba kama tulivyofanikiwa katika Mradi wa MACEMP hapo nyuma utakwenda kuwasaidia wavuvi hawa wa Ukanda wa Pwani kuweza kupata elimu za ujasiriamali, kuweza kuwasaidia kivyombo na kimifumo ili waweze kuwaondoa katika umaskini.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili linahusu kwa nini na Serikali ina mpango gani. Ni kweli jamii nyingi za wavuvi wakiwemo wavuvi wa Jimbo la Mkuranga katika eneo la Kisiju ni kweli wapo katika hali ya umaskini na wavuvi wengine wote nchini. Ndiyo maana Serikali ya Awamu ya Tano ya Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kujua hilo tukadhamiria kuona kwamba tuondoe tozo mbalimbali ambazo zinawagusa wavuvi na kuwarudisha nyuma na kupata unafuu wa maisha yao. Tutaendelea na jitihada hizo ili kuhakikisha wavuvi wetu wanapiga hatua ya maendeleo. (Makofi)
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Naibu Spika nakushukuru.
Kumekuwa na tabia ya umeme kukatika katika Mkoa wa Lindi hususan maeneo ya Mchinga, Mvuleni na Kilolambwani kadri mvua inaponyesha, lakini siku mvua haikunyesha umeme huwa haukatiki.
Nataka kujua, kuna changamoto gani kwamba siku za mvua lazima umeme ukatike hata kama hatuoni nguzo iliyodondoka?
WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali moja zuri sana la Mheshimiwa Mbunge wa Lindi. Ni kweli, kwanza kabisa nitumie nafasi hii kuipongeza sana Serikali yetu, kulikuwa na matatizo makubwa sana ya umeme katika Mkoa wa Mtwara na Lindi miaka na miezi michache iliyopita. Lakini tangu mwezi Desemba, Serikali yetu imetenga fedha na imelipa fedha na tumekarabati mitambo yote iliyokuwa haifanyi kazi katika Jimbo la Mheshimiwa Mbunge na Mikoa ya Mtwara na Lindi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kadhalika ni kweli mvua na umeme ni vitu viwili tofauti sana, mara zote kunapokuwa na mvua hasa ya muungurumo wa radi huwa inaingilia sana miundombinu ya umeme, hata inapokuwa mvua ya upepo mara nyingi nguzo zetu zinaanguka.
Mheshimiwa Naibu Spika, ingawa amesema mara zote kunapokuwa hakuna mvua umeme hauna shida, ili kuondokana na tatizo hilo sasa hivi tunaanza utaratibu wa kuleta nguzo za zege ambazo zitakuwa imara, wakati wa mvua zitakuwa hazidondoki. Kwa hiyo, tatizo hilo litakwisha mara moja, siyo kwa Lindi tu ni kwa nchi nzima.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Jimbo la Mchinga, katika vijiji vya Lihimilo na Kitowavi katika mwaka wa fedha 2016/2017 vilichimbwa visima ambavyo vinahitaji umaliziaji wa takribani kama shilingi milioni 142 kwa kisima kimoja na kingine shilingi milioni 132. Sasa kwa kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri amesema kwamba tayari wanazo pesa shilingi bilioni saba na anajua nimeshamsumbua sana juu ya suala hili, nihakikishie sasa ni lini hizi fedha, shilingi milioni 142 kwa Lihimilo na shilingi milioni 132 kwa Kitowavi mtazipeleka ili mkakamilishe vile visima?
NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa bahati nzuri yeye mwenyewe ni Mjumbe, kwenye hii Kamati ya Maji na Umwagiliaji. Tumeweka utaratibu Mheshimiwa Mbunge, visima tumechimba, maji yamepatikana kilichobaki ni miundombinu. Utaratibu wetu tuliouweka, mwambie Mkurugenzi wako, wewe ni Diwani kwenye Halmashauri Mkurugenzi aingie mikataba na wakandarasi kwa ajili ya miradi ya kusambaza hayo maji kupeleka kwa wananchi, wakishasaini, wakitekeleza, certificate ikapatikana, Mheshimiwa Mbunge nakuomba uiwasilishe hata kesho.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge, ni kwamba hatupeleki hela bila kuwa na hati ya madai, tulifanya hivyo huko nyuma tukapata shida sasa hivi tumeboresha na niwaambie tu kwamba tumekwenda vizuri sana, hadi mwezi wa nne tarehe 30.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naishukuru sana na Hazina wanaendelea kuleta fedha, Wizara ya Maji kupitia Mfuko wa Maji tumeshapokea shilingi bilioni 118. Kwa hiyo, fedha tunayo, wakamilishe huo mradi walete tutalipa hiyo hela.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Mfumo wa ulipaji wa fedha sasa hivi kwa wakulima wa korosho, kuanzia mwaka jana unatumika katika kulipa kwenye akaunti zao. Wakulima wameamrishwa wafungue akaunti benki ili waweze kulipwa kupitia benki. Sambamba na hilo alilouliza Mheshimiwa Mponda, Serikali haioni kwamba sasa kuna umuhimu wa hizi benki wakati wa kulipa wakulima wa korosho, wakawa wanakwenda kufanya huduma kule vijijini kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, badala ya wananchi kuwa wanasafiri kwenda umbali mrefu. Kwa mfano pale Mchinga kwenda Lindi kwenda kuchukua fedha, wakati unajulikana kabisa leo fulani anaenda kuchukua pesa kutoka benki. Hilo ndiyo swali langu.
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Bobali ametoa ushauri na sisi kama Serikali tunauchukua kuona unatekelezwa vipi ili kuhakikisha kwamba wananchi wetu wako salama, wanapokwenda kuchukua na kupokea fedha zao kutoka kwenye malipo hayo. (Makofi)
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba nimuulize maswali mawili ya nyongeza Mheshimiwa Naibu Waziri:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa lugha yoyote ambayo tunaweza tukazungumza haiondoi ukweli kwamba dinosaurian huyu ni mali yetu sisi Watanzania, kwa hiyo, manufaa yoyote yanapaswa sisi tuanze kunufaika. Sasa kwa kuwa, Serikali imesema kwamba, Serikali ya Ujerumani imeji- commit katika masuala matatu aliyoyasema Mheshimiwa Waziri katika jibu lake la msingi, naomba jibu kwamba, ni lini utekelezaji wa haya utafanyika, ili tuweze kujua kwa sababu, wakati anajibu amesema kwamba, majibu yalikuwa yanatolewa wakati huo kwa wakati huo. Sasa sasa hivi nataka katika hizi commitment tatu ambazo Serikali ya Ujerumani wamezitoa, ni lini sasa utekelezaji utafanyika?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, hivi sasa tunapozungumza kumekuwa na tendency ya watalii kuwa wanakwenda, mwaka huu tumepokea watalii zaidi ya watano ama sita wamekwenda, lakini walikuwa wanapata kikwazo kikubwa cha barabara. Sasa Mheshimiwa Waziri haoni kwamba, kuna haja ya kujenga barabara hata kwa dharura ya kwenda kule, ili njia ikawa inapitika wakati tunasubiri hayo makubwa ambayo Serikali ya Ujerumani imeji- commit? Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru.
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Bobali kwa kuungana na Wabunge waliotangulia kabla yake, lakini pia na mawazo ya Wabunge wengine wote humu ndani ambao wana nia njema ya kuhakikisha kwamba, rasilimali na maliasili za nchi hii zinanufaisha Taifa hili. Hongera sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kuhusu swali lake kwamba, ni lini hatua hizi zinazozungumziwa zitachukuliwa. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba hatua hizi ni za majadiliano ya pande mbili. Hivi ninavyozungumza Naibu Waziri wa Mambo ya Nje alikuwa asafiri wiki hii, kutokana na changamoto nyingine za Kiserikali safari hiyo imesogezwa mbele kwa wiki moja. Atakapokwenda, matokeo ya mazungumzo hayo pengine yatakuja sasa na mpango kazi na ratiba.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni vigumu kusema sasa hivi kwa upande mmoja bila kujua sasa kwa pamoja sisi sasa, Serikali ya Tanzania na Ujerumani, ratiba yetu ya utekelezaji wa haya ambayo yanaonekana kwamba tunakubaliana inaanza lini. Wakati huo utakapofika basi, utapata jawabu kwamba lini tunaanza na tunategemea kukamilisha lini programu tunayoizungumzia.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini katika swali lake la pili, anataka mpango wa muda mfupi, kwamba, kwa sasa hivi hatuwezi kufanya utaratibu pale, hivyo hivyo palivyo kwa sababu tu za kihistoria watu wanajua kwamba alitoka mjusi mkubwa pale wa vipimo na viwango tunavyovizungumzia watu wanataka kwenda kuona kwa mazingira hayahaya yaliyopo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu hili nafikiri nipate nafasi sasa ya kufika kwa uhalisia kabisa kwenye eneo hilo na kuona barabara hiyo inayozungumziwa, kwanza ni barabara ya aina gani. Barabara ya Mkoa, ni barabara ya Halmashauri au ni barabara ambayo jukumu lake linatakiwa kutekelezwa na nani Serikalini. Baada ya hatua hiyo tutaweza kujipanga vizuri zaidi kutekeleza, ili hayo mambo mazuri tunayokusudia yaweze kutekelezwa. (Makofi)
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba sasa niulize maswali mawili madogo ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, shule za kata tangu zimeanzishwa sasa takribani ni muongo mmoja; na kwa bahati mimi nilikuwa ni miongoni mwa walimu walioanzisha shule za kata. Matatizo na changamoto yaliyokuwepo mwaka 2006/2007 wakati shule za kata zinaanzishwa kama vile madarasa, ukosefu wa maabara, ukosefu wa walimu wa sayansi na hisabati, bado mpaka leo changamoto zile zipo.
Naomba sasa kujua ni lini Serikali itatuhakikishia kwamba changamoto za walimu wa sayansi, hisabati na madarasa katika shule zetu zitakwisha? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, hivi karibuni Mheshimiwa Waziri Mkuu wakati anazindua Mbio za Mwenge kule Geita, aliorodhesha mikoa inayoongoza kwa utoro na Mkoa wa Lindi siyo miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa utoro; bahati mbaya ni miongoni mwa mikoa inayofanya vibaya sana katika matokeo ya kidato cha nne na matokeo ya darasa la saba. Moja ya mkakati wa Mkoa ni kuhakikisha tunatoa chakula mashuleni.
Naomba sasa leo Serikali iji-commit hapa; je, iko tayari sasa kutuhakikishia kwamba sisi wa Mkoa wa Lindi tuendelee na programu ya kuwashirikisha wazazi ili waendelee kuchangia chakula ili matokeo yaweze kuboreka katika shule zetu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Naibu Spika, hadi sasa kuanzia mwezi Oktoba, 2017 hadi sasa tumeajiri walimu 200 wa masomo ya sayansi na hisabati. Mpango uliopo hadi tarehe 30 Juni tutaajiri walimu 6,000 na lengo tunataka kuondoa kabisa tatizo la walimu wa sayansi na hisabati katika shule za sekondari ifikapo mwaka 2020, maana yake inakwenda polepole.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu suala la miundombinu pamoja na chakula, nimhakikishie Mheshimiwa Hamidu Bobali na Waheshimiwa Wabunge wote kwamba Serikali haijakataza michango ya wananchi kuchangia miundombinu ya shule zikiwemo maabara. Kilichokatazwa ni kumpa adhabu mwanafunzi ya kukosa masomo kwa sababu tu mzazi wake hajatoa mchango. Kwa hiyo, hiyo ndiyo iliyokatazwa, lakini kupitia Serikali za Vijiji, mnaruhusiwa kuendelea kuhamasisha wananchi ili wachangie maendeleo ya shule zao ikiwemo miundombinu pamoja na chakula. (Makofi)
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa fursa hii. Mheshimiwa Waziri amekuwa akija Mkoani Lindi mara kwa mara, zaidi ya mara mbili au tatu nimekutana naye kwa ajili ya mradi ule wa maji pale Napa. Lakini tuna Skimu ya Umwagiliaji iliyopo kwenye Jimbo la Mchinga, ya Kinyope na skimu nyingine iko Jimbo la Mtama kwa Mheshimiwa Nape, ya Kiwalala. Skimu hizi zilijengwa chini ya kiwango na hivi sasa hazifanyi kazi vizuri ingawa zilitumie pesa nyingi ya Serikali. Je, Waziri uko tayari kutuma wawakilishi wako au wewe mwenyewe kwenda kujionea kinachoendelea katika skimu hizo?
WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli skimu hizo zilitekelezwa, zilikumbwa na matatizo ya mafuriko lakini kwa sasa tayari tunazifanyia kazi ili ziweze kujengwa na kutimiza matakwa ambayo yalikuwa yanatakiwa kwa ajili ya kuwapatia wananchi huduma nzuri ya maji ili waweze kufanya kilimo cha umwagiliaji. Niko tayari kwenda kutembelea eneo hilo.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa fursa hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka jana tulikubaliana na Mheshimiwa Waziri na Wabunge wote wa Mkoa wa Lindi kwamba zao la ufuta mwaka huu litanunuliwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani, lakini mpaka hivi sasa tunapozungumza hakuna mipango ama mikakati yoyote ambayo tayari Serikali wameshaiweka tuanze kununua kwa stakabadhi ghalani na ufuta upo tayari.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba commitment ya Mheshimiwa Waziri, kwamba tunakwenda na stakabadhi ghalani ama tunatumia mfumo wa kawaida ili wakulima sasa waache kuyumba kuona kwamba mfumo gani utatumika mwaka huu? (Makofi)
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli tuli-commit kwamba msimu huu tutajitahidi kadri iwezekanavyo tuweze kuanza kuuza au kununua ufuta kwa mfumo wa stakabadhi ghalani na maandalizi yanaendelea na hivi kesho tutakuwa na kikao cha Wakuu wa Mikoa yote inayozalisha ufuta ili tuone maandalizi yamefika kiasi gani na tuweze kutangaza rasmi lini tunaanzisha mfumo huu.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mtemi, nakushukuru kwa kunipa fursa hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, tuna mto ambao una-flow maji kipindi chote, Mto Lukuledi unaopatikana katika Jimbo la Mtama na kuna skimu za umwagiliaji ambazo zilianzishwa na Serikali lakini kwa bahati mbaya zimeishia katikati, zime-stuck sasa zaidi ya miaka mitano. Tunataka kujua ni lini Serikali itakwenda kufanya upembuzi ili kujua kitu gani kilikwamisha na kuweza kufanya mpango ili zile skimu ziweze kufanya kazi yake kama ilivyokuwa imekusudiwa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie nafasi hii kwanza kumpongeza Mheshimiwa Mbunge. La pili, tuna skimu zaidi ya 2,947. Sisi kama Wizara kwa muda huu tumeona tuna skimu nyingi lakini kwenye uzalishaji matokeo ni madogo sana. Waziri wangu akaona haja ya kuunda timu kuangalia changamoto zilizoko katika hizi skimu za umwagiliaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya changamoto tulizoziona, tuna skimu nyingi lakini bado hazijakamilika. Mkakati wetu ni kwamba tunataka tuwe na skimu chache lakini ziwe na tija kubwa ili tuweze kufikia uchumi wetu ule wa viwanda katika kuhakikisha tunakuwa na kilimo cha umwagiliaji kizuri. Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Wakati wananchi wa Mkwaya hawajajua mmiliki halali wa eneo hili ni nani kwa kuwa kulikuwa na mgogoro baina ya Serikali na mwekezaji, wakati fulani Machi, 2017 wananchi waliamua…
Ahsante. Kuna watu wameshtakiwa wakati wanaomba hili eneo liweze kuchukuliwa na bado kesi ziko mahakamani lakini Serikali imeshinda kesi. Sasa Mheshimiwa Waziri, anasemaje kuhusu hawa watu walioshtakiwa wakati wanalipigania eneo hili? Ni hatua gani Serikali itachukua ili kuwasaidia wale watu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE):
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Bobali, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mbunge anajua historia ya mgogoro huu kwamba inaanzia miaka ya 1995 na kwamba kuna wakati ambapo wananchi walivamia maeneo yale ya mwekezaji wakachukua ndizi na wengine wakaenda kutikisa mikorosho. Kwa hiyo, haiwezekani tukasema kwamba sasa hao ambao walivunja sheria Serikali iwatetee, ni vizuri sheria ikafuata mkondo wake.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimshukuru Meneja wa TARURA wa Lindi DC, hii barabara sasa hivi iko kwenye matengenezo, kipande cha kutoka Nangalu kwenda mpaka Moka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara hii inahusisha Halmashauri mbili, Manispaa ya Lindi kwa eneo la Mtange, Chikonji na maeneo ya Kineng’ene pamoja na Lindi DC. Sasa nilitaka kujua, ili barabara hii yote ikamilike ni Meneja gani wa TARURA anahusika kwa sababu barabara hii ni zaidi ya kilometa 50 na inahusisha Manispaa pamoja na Lindi DC?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, kama nilivyosema kwenye swali la msingi kwamba Mheshimiwa Rais alikwenda Nangalu wakati wa kampeni, akaahidi barabara hii ataipandisha hadhi na kuna vitu aliviangalia ndiyo maana akaahidi hivi. Sasa Mheshimiwa Waziri naomba mtufikishie salamu hizi kwamba ile ahadi ya Mheshimiwa Rais kuna haja ikatekelezwa kwa sababu ya umuhimu na urefu wa barabara hii. Nakushukuru.
NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Bobali, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza zile pongezi ambazo amezielekeza TARURA nazipokea na tutazifikisha TARURA. Niseme tu ni azma ya Serikali kwa kweli kuja na TARURA ili kuhakikisha kwamba barabara zetu sasa tunazisimamia na tunazitengeneza kwa kufuata weledi (Professionalism).
Mheshimiwa Mwenyekiti, TARURA ni mwaka tu toka waanze na wameanza kwa kupokea bajeti iliyokuwa kwenye Halmashauri na wameanza vizuri na uratibu. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge wameratibu barabara zote, kwa maana kwamba sasa hata allocation ya mafungu itakwenda kwa kulingana na kuwiana na mahitaji ya barabara zetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la barabara hii aliyoitaja kuhusisha Lindi Manispaa na Lindi DC, uko utaratibu wa usimamizi wa barabara. Kama hii barabara aliyoitaja imetajwa kwa maana ya kwamba ina jina moja project namba fulani, kama itaunganisha barabara zote utaratibu wetu kama Serikali ni kwamba mafungu yanaweza kutengwa kupitia TARURA upande mmoja lakini upo utaratibu wa hawa Mameneja kuwasiliana kuhakikisha kwamba barabara inakwenda kwa standard zilezile. Kwa hiyo, asiwe na wasiwasi lengo ni kuhakikisha barabara aliyoitaja itapata huduma bila kujali Meneja yupi amesimamia. Cha msingi ni kupeana mrejesho kama kuna sehemu ambayo tunatakiwa kuitazama kwa umakini zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ahadi za Mheshimiwa Rais kama alivyosema, hizo salamu kwa kweli Mheshimiwa Rais amezisikia, tunakushukuru sana kwa pongezi zako. Kwa kweli ni hulka nzuri kutoa kutoa shukrani pale ambapo jambo jema limetokea. Kwa hiyo, nasi tukupongeze sana Mheshimiwa Mbunge na tutaendelea kushirikiana, ahsante sana. (Makofi)
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushuru, Jimbo la Mchinga halina Mamlaka ya Mji Mdogo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kujua tu kwa Mheshimiwa Waziri, ni kigezo gani kinachotumiwa na TANESCO Lindi kuwalipisha watu wa Mchinga fedha nyingi ya kuunganisha umeme tofauti na vijiji vingine wakati Mchinga yenyewe ni kijiji kama maeneo mengine?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, uunganishwaji wa umeme katika maeneo ya vijijini bei yake ni shilingi 177,000, umeme ambao unaunganishwa kupitia TANESCO na ile shilingi 27,000 ni kwa umeme vijijini. Kwa hiyo, naomba nimthibitishie Mbunge kwamba hakuna tofauti, ila mijini ni shilingi 377,000 na vijijini ni shilingi 177,000. Kama wanakuwa-charged zaidi ya hizo, naomba tuonane ili niweze kulishughulikia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba radhi kwa Waheshimiwa Wabunge kwa tatizo lililojitokeza sasa hivi. Ahsante. (Kicheko/Makofi)
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kumekuwa na changamoto ya wazazi wanaopata watoto ambao ni pre-mature babies, hawa watoto njiti, kupata leave inayofanana na wazazi waliojifungua kawaida. Serikali haioni kuna haja sasa akina mama watumishi wanaojifungua watoto ambao hawajatimiza muda wao wakaongezewa ile leave ili waweze kuwalea vizuri wakiwa bado ni wadogo? (Makofi)
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya kusimamia haki na maslahi ya wafanyakazi kwenye maeneo tofauti ikiwemo eneo hili la afya pamoja na hili la afya ya uzazi tumekuwa na sheria mbalimbali zinazotuongoza. Sheria hizo zimekuwa zikifanyiwa mabadiliko kwa kuzingatia hali halisi ya namna nzuri ya kuweza kuwahudumia wafanyakazi. Tumeshapokea maombi ya kuangalia ni namna gani wafanyakazi wanaokumbana na hasa wanawake wanaopata matatizo ya namna moja ama nyingine kwenye kujifungua wasaidiwe.
Mheshimiwa Spika, naomba kulihakikishia Bunge lako Tukufu pamoja na Mheshimiwa Mbunge hayo ni mambo ambayo yanaendelea kujadiliwa na kufanyiwa kazi ili kuweza kuwasaidia wanawake. Hii pia ni hata kwa wanaume ambao wake zao wamejifungua watoto ambao wamezaliwa kabla ya umri wao ili waweze kupewa haki na kusaidia malezi ya watoto na malezi ya familia kwa ujumla. (Makofi)
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kumekuwa na wimbi sasa limeibuka la wizi wa kutumia mitandao ya simu, wakiwa wanatuma message kwamba umeshinda Tatu Mzuka, umeshinda Tigo, tuma pesa kwenye namba hii; kumekuwa na desturi hiyo sasa hivi. Nilitaka kupata majibu kutoka kwa Waziri, TCRA imechukua juhudi gani kuhakikisha kwamba wizi wa mitandao kwa kutumia simu unakomeshwa na wahusika wanakamatwa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE):
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Bobali, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba kumekuwa na matukio ya Watanzania mbalimbali kutumiwa message ambazo zinaonyesha na kuashiria kwamba kuna utapeli unaoendelea katika huduma za mawasiliano. Kwa kutumia Sheria ya Mitandao ya 2015, TCRA kwa kushirikiana na Polisi wameendelea kufanya kazi kwa karibu kuhakikisha kwamba wote wanaosambaza ujumbe huo, wanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Swali kama hili ambalo Mheshimiwa Ngombale leo ameuliza, nililiuliza mimi 2016 na majibu yalikuwa haya haya. Sasa Mheshimiwa Naibu Waziri Mkoa wa Lindi usikivu wa TBC ni tatizo sana, naomba commitment ya Mheshimiwa Naibu Waziri kama alivyotoa wakati anajibu kwa Mheshimiwa Ngombale; kwamba katika mwaka huu wa fedha huo mnara aliosema utajengwa ili Watanzania wanaomsikia wajue kwamba Serikali imeji-commit ndani ya Bunge.
WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO:
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze sana Naibu Waziri kwa majibu mazuri aliyoyatoa ambayo ameyatoa kwa maswali aliyoulizwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, ningependa kumjibu Mheshimiwa Bobali kwamba, kwanza si sahihi kusema kwamba eti majibu tuliyotoa sasa ndio majibu tuliyotoa kipindi kilichopita miaka miwili iliyopita wakati kuna miradi tayari tumeitekeleza mwaka huu na mwaka jana. Ni kichekesho, sasa sisi tumekuwa waganga wa kienyeji kwamba tumetekeleza hayo mambo mwaka huu..
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba tu nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge awe na imani na Serikali yetu, kwamba tumehakikisha kwamba katika mwaka 2018/2019 mradi wa kujenga mtambo wa FM kurusha matangazo eneo la Nangurukuru utatekelezwa.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, magari ambayo ameyazungumzia Mheshimiwa Sannda kwetu Mchinga tunayahitaji sana. Kituo cha Afya Kitomanga kinahitaji gari la wagonjwa lakini hakuna, nataka kujua tu, ni sifa gani ambazo haya magari yanapatikana ili tufuate hizo procedure kwa sababu taarifa tulizonazo humu ndani kuna Wabunge wamepewa mpaka magari mawili, wengine matatu, wakati wengine hatuna hata moja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu ni hilo kwamba tutumie vigezo gani tupate haya magari?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwamba kuna sifa specific ambayo inabidi itumike ili kupata gari, hilo sina. Kinachozingatiwa ni uhitaji mkubwa wa maeneo ambayo yanahitaji magari na kwa uwiano kwamba zimepatikana gari ngapi ndipo zinagawiwa. Kwa hiyo, hakuna specific procedure kwamba sasa Mheshimiwa Bobali sasa hiyo sifa uwe nayo ili uweze kupata gari hiyo. Pale ambapo kuna uhitaji mkubwa na kwa kuzingatia jiografia ya maeneo husika na umbali wa wananchi kuweza kwenda kupata huduma hizo ndiyo sifa ambazo zinatakiwa.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Mheshimiwa Naibu Waziri anajua kwamba kijiji cha Ruhoma, Jimbo la Mchinga kimevamiwa na tembo na wanakula mashamba ya wakulima. Nataka kujua hawa watu mnafanyaje kuwa-compensate gharama zile za mashamba yao kuliwa na tembo?
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba nikiri kwamba, tatizo la wanyama kuvamia mashamba na makazi ya watu limeongezeka. Limeongezeka baada ya usimamizi wa maeneo haya yenye wanyamapori pia, kuimarika na watu waliokuwa wanafanya mauwaji ya wanyama kwenye hifadhi zetu kupungua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili limesababisha pia, uharibifu mkubwa wa mazao kwenye maeneo mbalimbali. Lakini utaratibu upo kwamba, pale ambapo wanyama hawa wanapovamia eneo na kuharibu mashamba ya wananchi utaratibu umewekwa kwamba, afisa wetu wa wanyamapori apewe taarifa. Tunamuelekeza anakwenda pale anafanya tathmini na tathmnini ile inapofika katika Wizara yetu tunaelekeza kulipa mara moja.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa fursa kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwa bahati wakati mifugo inahama inakwenda Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Naibu Waziri aliyekuwa anajibu alikuwa Mkuu wa Wilaya kule Kilwa na wakati mwingine akikaimu nafasi ya Mkuu wa Mkoa, kwa hiyo, jambo hili analifahamu vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tatizo lililopo ni kwamba, mifugo iliyokuja wakati ule na leo imekuwa mingi kama ime-double kwa hiyo, Mkoa kama wa Lindi umezidiwa na idadi ya mifugo. Swali la msingi Mheshimiwa Mbunge ameuliza kwamba, je, Serikali ipo tayari kuandaa mpango mwingine wa kuhakikisha mifugo ile inapungua kwa sababu, sasa hivi ukataji wa misitu umekuwa mkubwa kulingana na idadi ya mifugo ambayo tunayo? Kwa hiyo, hilo swali la kwanza?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kuna malambo Serikali walijenga katika maeneo haya ya wafugaji, mfano hata pale Jimboni kwangu Mchinga katika eneo la Ktomanga limejengwa lambo kubwa la zaidi ya milioni 300, lakini kwa mwaka wa tatu sasa lambo lile halitumiki kwa sababu tu linahitaji ukarabati wa fedha wa shilingi milioni 22 na kwenye bajeti ya Halmashauri ya mwaka huu ya 19 na 20 tumeomba tupatiwe milioni 22 ili lambo lile lifanyiwe ukarabati na wale wafugaji waweze kupata huduma zao. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri yuko tayari sasa kututhibitishia kwamba, hii milioni 22 wataitoa kwa kuwa ipo kwenye bajeti ili tuweze kutoa huduma kwa wafugaji waliopo maeneo yale? Nashukuru.
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Bobali, Mbunge wa Mchinga, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la kwanza Mkoa wa Lindi umezidiwa na je, Serikali ina mipango gani ya kuhakikisha kuwa inapunguza mifugo ile iliyozidi pale katika Mkoa wa Lindi. Serikali imefanya jitihada kadhaa, moja ya jitihada ni katika kuhakikisha kwamba, wafugaji wanavuna mifugo yao. Katika kuvuna mifugo hii ni pamoja na ile jitihada ya makusudi ya kuanzisha machinjio za kisasa.

Kwa upande wa Mkoa wa Lindi, Lindi Manispaa imejengwa na inaendelea kujengwa machinjio ya kisasa itakayorahisisha na kuwapa fursa wafugaji wetu waweze kuvuna mifugo yao na kwenda kuiuza katika machinjio ile na hatimaye kuweza kupata faida kwa upande wa wafugaji wenyewe, lakini kwa upande wa nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile Serikali inao mpango madhubuti wa kuhakikisha kuwa inaboresha ufugaji huu, ili kusudi kuweza kufanya ufugaji wenye tija. Ufugaji ambao utamfanya mfugaji awe na mifugo michache, lakini yenye kumpa faida kubwa zaidi kuliko kuwa na makundi makubwa ya mifugo ambayo tija yake wakati mwingine inakuwa ni ndogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili Mheshimiwa Bobali ameeleza kuwa liko lambo katika Mji wa Mchinga ambalo lambo lile halitumiki na tayari wameshaliweka katika bajeti. Naomba nimhakikishie kuwa, Mheshimiwa Bobali pindi pesa hizi zitakapopatikana sisi kama Serikali tuko tayari kuboresha huduma za mifugo, hivyo, tutalichukua jambo hili na kulitekeleza.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Swali la msingi lilikuwa linaulizia mradi wa LNG wa Lindi. Napenda kufahamu kutoka Serikalini, ni lini Serikali italipa fidia wakazi wa Likong’o, Mto Mkavu na Mchinga ambao wapo tayari kupisha mradi huu?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Bobali, Mbunge wa Mchinga, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ameuliza lini fidia italipwa kwa wakazi wa maeneo ya Likong’o, Mchinga na Mitwelo Mkoani Lindi ambao wamepisha eneo kwa ajili ya Mradi huu mkubwa wa LNG. Napenda nimtaarifu Mheshimiwa Mbunge kwamba mwezi uliopita wataalamu wa TPDC na Wizara ya Fedha na Mipango walikuwa ziara katika Mkoa wa Lindi kuhitimisha zoezi zima la tathmini. Matarajio yetu ifikapo Disemba 2019 zoezi la kuanza kulipa fidia kwa wakazi wa maeneo hayo litaanza na litaendelea na hatimaye kukamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niwathibitishie wakazi wa Mkoa wa Lindi ambao kwa kweli kwa muda mrefu wamekuwa wakiulizia fidia hiyo, Serikali ya Awamu ya Tano sasa iko tayari kuwalipa. Fidia iliyotengwa ni kiasi cha shilingi bilioni 56 na mambo yote yamekamilika na itaanza kulipwa na wakati huo sisi Serikali na wawekezaji tunaendelea na mazungumzo. Ahsante.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Nataka nipate tu maelezo ya Serikali ni lini mtapeleka umeme katika vile vijiji ambavyo vilishapitishwa kwenye mradi wa REA II vijiji vya Ruvu na Dimba katika Jimbo la Mchinga?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbunge ameulizia vijiji vyake viwili ambavyo viko kwenye mpango wa kupelekewa umeme katika REA III mzungunguko wa kwanza, nataka nimthibitishie Mheshimiwa Mbunge na tulikutana Lindi nikamuahidi baada ya Bunge hili la Bajeti tutatembelea Jimbo lake na Mkandarasi State Grid kupitia ziara ambayo alifanya Mheshimiwa Waziri katika Wilaya ya Luwangwa, Wilaya ya Nachingwea na Jimbo la Mtama Lindi vijijini ameonesha kupata kasi zaidi.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nilitaka nimtaarifu tu kwamba kazi inaendelea katika vijiji alivyovitaja na baada ya Bunge hili kwa ruksa ya Mheshimiwa Waziri tutaambatana naye tukague na tuwashe umeme katika vijiji vyake asiwe na wasiwasi ahsante sana. (Makofi)