Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions from Hon. Susan Limbweni Kiwanga (38 total)

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini Wilaya ya Morogoro Kusini mpaka hivi sasa, hata hivyo vikundi alivyovizungumzia hapa; na kwa kuwa, Wilaya hiyo haina Makao Makuu ya Wilaya, wanaripoti Morogoro Mjini, kwa hiyo, inakuwa ngumu vijana hawa kufuatilia hizo fedha anazosema; na kutokana na idadi na umasikini wa wananchi wa Morogoro Vijijini, kwa kweli, kasi ya Serikali katika kuwawezesha vijana imekuwa ndogo sana kutokana na ukubwa wa Wilaya hiyo ambapo haina Ofisi ya Wilaya.
Je, Serikali ni lini sasa itaweka Ofisi ya Halmashauri ndani ya Wilaya ya Morogoro Vijijini ili vijana hao waache kuhangaika na kufuatilia masuala yao ndani ya Wilaya yao badala ya kukimbilia Morogoro Mjini ambako ni mbali na Wilaya yao? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Kwa kuwa matatizo ya vijana Wilaya ya Morogoro Mjini na Wilaya ya kilombero, hususan Jimbo la Mlimba yanalingana; mara nyingi katika hii Mifuko ya Vijana ukitaka kuangalia ufuatiliaji wake, kwanza Halmashauri hazipeleki hizo hela. Mara nyingi Wabunge wengi ndani ya Bunge hili wamelalamika kwamba pesa hizo haziwafikii vijana.
Je, Serikali ina mpango gani sasa kwa kusudio la kuhakikisha hela zinazotengwa kwa ajili ya vijana ambapo hazitengwi na Wakurugenzi kuweka kipindi maalum kulipa madeni ya nyuma na kuendelea kutoa zile asilimia ili vijana wengi wapate kujiajiri wenyewe katika awamu hii?
NAIBU WAZIRI (TAMISEMI, UTUMISHI NA UTAWALA BORA): Mheshimiwa Naibu Spika, agenda ya kwamba Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro haina Ofisi ni kweli. Swali hili nadhani nimelijibu wiki iliyopita hapa na nimetoa ufafanuzi wa kina kuhusu swali hili; na tumesema mchakato hivi sasa unaendelea wa ujenzi kule. Lengo kubwa, ni kweli watu wanaotoka maeneo ya mbali kabisa; kwa mfano mimi mwenyewe nilienda Morogoro Vijijini yapata karibuni mwezi uliopita, ukitoka maeneo ya Mvuha mpaka kufika mjini changamoto kubwa sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, tumeshatoa maelekezo kwamba mchakato ufanyike kwa haraka ilimradi wananchi wale wa Morogoro Vijijini kama Swali la Msingi alilouliza Mheshimiwa Tebweta, wiki iliyopita nilivyokuwa nikilifafanua.
Mheshimiwa Naibu Spika, suala zima la uwezeshaji wa vijana, ni kweli, nanyi mnakumbuka hapa mwaka 2015 katika mchakato wetu tulipitisha mpaka Baraza la Vijana. Lengo kubwa ni kuona jinsi gani vijana waweze kufanyiwa kazi. Katika Bajeti ya mwaka huu wa fedha, ninyi Waheshimiwa Wabunge mnakumbuka, katika kikao chetu kilichopita cha Bajeti, tulitenga mafungu katika maeneo matatu tofauti.
Katika Wizara ya Habari na Vijana, kipindi kile tulitenga karibu shilingi bilioni moja katika bajeti, halikadhalika Waziri wa Utumishi alipokuja hapa eneo kubwa la concentration jinsi gani vijana wanaomaliza vyuo wanakosa ajira, Serikali ilitenga takribani bilioni 233, lengo likiwa ni kuajiri waajiriwa wapya wapatao 71,408.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika hili nini kimefanyika hivi sasa? Siku mbili zilizopita hapa, Mheshimiwa Angellah Kairuki alizungumzia kwamba sekta ya afya peke yake itaajiri takriban wafanyakazi wapatao 10,870. Katika changamoto ya kuajiri walimu wapya, tunatarajia kuajiri walimu wapatao 40,000 ambao idadi katika bajeti ile ya shilingi bilioni 233, lengo kuwa ni kuwaajiri wafanyakazi wapya ambao ni vijana wapatao 71,408. Hii ni ajenda kubwa sana ya Serikali.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niwaambie ndugu zangu, tatizo hasa la kukosa 5% kwa vijana na akinamama, changamoto hii inatukabili sisi Wabunge. Kwa sababu own source inajadiliwa katika vikao vya Mabaraza ya Madiwani na sisi ni miongoni mwa Wajumbe katika Mabaraza ya Madiwani. Own source haiji TAMISEMI wala haiji Wizara ya Fedha.
Mheshimiwa Naibu Spika, kinachofanyika nini? Collection imefanyika ndani ya Halmashauri; Kamati ya Huduma za Jamii na Kamati ya Uchumi inakaa, baadaye Kamati ya Fedha; ninyi mnajua mwezi huu tumekusanya shilingi milioni 100 na wewe Mbunge upo na unafanya decision. Naomba niwaambie ndugu zangu, Taarifa ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, katika report yake aliyo-submit mwezi wa nne imeonesha kwamba takriban shilingi bilioni 38.7 ambazo zinawagusa akina mama na vijana hazijapelekwa katika makundi hayo, lakini sisi ndio wa kufanya maamuzi hayo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niwape changamoto ndugu zangu, hili jukumu ni la kwetu sisi sote. Kila Mbunge katika Kamati ya Fedha aende akasimame, own source zinazokusanywa ahakikishe 5% kwa vijana na akina mama inakwenda kwa ajili ya kuokoa uchumi wa vijana wetu. Katika hili tutawekeza ajira pana sana ya vijana wetu kwa sababu. Kwa sababu shilingi bilioni 38; sasa hivi tuna Halmashauri 181, takriban kila Halmashauri ikitoa shilingi milioni 100 ambayo collection ikiwasilishwa shilingi bilioni moja kwa mwaka, maana yake nini? Kwa Halmashauri 181 maana yake kuna shilingi bilioni 181 ilibidi ziende kwa vijana na akinamama.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niwasihi Wabunge wenzangu, sasa tufanye mabadiliko ya kweli kuwakomboa Watanzania. Mabadiliko haya yataanza na sisi na Wenyeviti wetu wa Halmashauri na Madiwani wetu kuhakikisha own source ya 5% kwa vijana na akina mama inakwenda kwa ajili ya mustakabali wa nchi yetu. (Makofi)
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, nauliza kwa kifupi ili na wengine wapate nafasi.
Mheshimiwa Naibu Spika, amesema upembuzi yakinifu unakamilishwa Juni, 2016 lakini kwa uhakika niliokuwa nao kwa sababu ni miaka sita niko Bungeni na hili swali nimekuwa nikiuliuliza na wamekuwa wakisema liko kwenye upembuzi yakinifu. Kama upembuzi yakinifu unachukua miaka sita, je, lini sasa mkandarasi atapatikana na ujenzi wa barabara hii utaanza lini? Maana ni muda mrefu mno nimezungumzia barabara hii na watu wanateseka sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, wananchi wa Mlimba wanasikia maana nimewaambia, kwa kuwa Jimbo la Mlimba linaunganika na Mkoa wa Njombe, lakini amezungumzia barabara ya kwenda mpaka Mlimba hukuzungumzia barabara ya kutoka Mlimba - Madeke Njombe. Ni nini mpango wa Serikali wa kujenga barabara hiyo ili wananchi wa Mlimba waunganike na wa Mkoa wa Njombe ili waweze kupata fursa za kimaisha na za kiuchumi?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza la Mheshimiwa Susan Limbweni Kiwanga anahoji dhamira ya Serikali na mimi naomba kumthibitishia kwamba Serikali hii ya Awamu ya Tano ina dhamira ya dhati na itatekeleza ahadi zake zote zilizoko katika Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015 -2020. Tumepewa dhamana ya kusimamia ahadi zote ikiwa ni pamoja na kuzikamilisha shughuli zote ambazo zilikuwa zimeanza kutoka Serikali ya Awamu ya Nne. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili linahusu kuunganisha Mlimba pamoja na Mkoa wa Njombe kupitia Madeke. Naomba kumhakikishia Mheshimiwa Susan Limbweni Kiwanga kwamba hoja yake tutaishughulikia. Barabara hii pia imeombwa na watu wa Njombe upande ule mwingine na ipo katika mpango wa TANROADS Mkoa wa Njombe na tutahakikisha wanashirikiana na TANROADS Morogoro ili barabara hii tuikamilishe yote kwa pamoja.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kuniona. Kwa kuwa Naibu Waziri amejibu kwamba kuna uwezekano mkubwa kabisa wa kupata halmashauri ndani ya Wilaya moja na kwa kuwa mchakato wa wilaya ni mrefu kidogo na mchakato wa kupata halmashauri uko ndani ya uwezo wake na kwa kuwa Jimbo la Mlimba lina kata 16 na urefu wa kilometa 265 kutoka Jimboni mpaka Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, ni lini Wizara italipa hadhi ya kiwango cha halmashauri Jimbo la Mlimba ili angalau tuanze sasa kujitegemea wenyewe kwa sababu vigezo vyote tunavyo?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, amezungumzia Jimbo la Mlimba nadhani akiwa na maana pamoja na Ifakara kwamba eneo lake ni kubwa. Kuanzisha halmashauri kwa mujibu wa vigezo vyetu lazima iwe na kata 15, hicho ndiyo kigezo cha kwanza. Kwa hiyo, kama mna kata 16 maana yake tulitarajia kwamba angalau kata ziongezeke. Tukiachia vigezo hivyo, kuna vigezo vingine vya jiografia maana kuna maeneo mengine kata zinaweza kuwa chache lakini mtawanyiko wa jiografia yake unakuwa ni mkubwa zaidi kama kwa akina Mheshimiwa Keissy kule ndiyo malalamiko ambayo kila siku wanayazungumza hapa.
Mheshimiwa Naibu Spika, imani yangu ni kwamba, kama mtakuwa mmekidhi vigezo tutafanya mchakato, lakini mwisho wa siku, wataalam wetu lazima watakuja field ku-assess uhalisia wa maeneo hayo yakoje. Lengo letu ni nini kama Serikali? Lengo letu ni kwamba katika maeneo ambayo wananchi wanatakiwa wapate huduma waweze kupata huduma. Kwa hiyo, thibitisho langu kwako ni kwamba, kama mtakuwa mmekidhi vigezo na wataalam wakija ku-verify wakiona kwamba vigezo hivi vimetimizwa na matakwa ya kisheria na taratibu zote zikishakamilika, basi Ofisi ya Rais, TAMISEMI haitosita kufanya maamuzi sahihi kwa ajili ya wananchi wa Mlimba.
Mheshimiwa Naibu Spika, siyo hapo tu, kutokana na jiografia ya Mkoa wa Morogoro hata watu wa Morogoro Kaskazini wana-issue kama hiyo hiyo. Kwa hiyo, naamini kwamba maeneo yote ambayo yataonekana kwamba yana kila haja ya kugawanywa, basi Serikali itaangalia, lakini wakati huo huo tutaangalia suala zima la kibajeti jinsi gani Serikali itaweza kuzihudumia hizi mamlaka mpya ambazo tutakwenda kuzianzisha.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante nimepokea majibu bahati nzuri naifahamu sana hii yote.
Kwa kuwa kwenye kikao cha RCC Mkoa tulipewa taarifa hiyo kwamba fedha hizo kweli za barabara ya Kidatu - Ifakara ina ufadhili wa USAID; nilitaka kujua sasa, mkandarasi huyu inachukua muda gani kwa sababu hela ipo tayari. Kwa hiyo, ili kumpata mkandarasi wa kuanza ujenzi barabara hiyo ningependa kupata majibu ya Serikali inachukua muda gani ili wananchi wa Kilombero wajue hii barabara inaanza kujengwa lini kwa kuwa hela ipo na upembuzi umeshafanyika? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mbili; kwa kuwa ujenzi wa daraja la Kilombero ulianza tarehe 21 Januari, 2013 na mimi nilienda kwenye uzinduzi wa ujenzi wa daraja hilo na ahadi ya Waziri wakati huo kwa wananchi waliambiwa ujenzi wa daraja utamalizika mwaka 2015. Leo mnasema Disemba, 2016. Kwa kuwa wafanyakazi wanaofanya kazi katika lile daraja walitoa taarifa kwangu na kwa Peter Lijualikali kwamba kule chini kuna crack jamani, je, kwa taarifa hizi ambazo wafanyakazi wapo na unasema daraja linaendelea vizuri ingawa si kweli sio asilimia 50, je, Serikali iko tayari sasa kwenda kufanya utafiti lile daraja kabla halijaenda mbali zaidi tuangalie...
SPIKA: Mheshimiwa Susan Kiwanga swali!
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Madhara yanayoweza kujitokeza katika daraja hilo kabla ya kuendelea?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Spika, tulieleza tarehe 27 Januari, wakati Mheshimiwa Peter Lijualikali alipouliza swali la nyongeza kuhusiana na hilo hilo kwamba tulilazimika kubadilisha muda kutokana na upatikanaji wa fedha. Hatuna namna, fedha hazikupatikana, kwa hiyo, hilo suala tunalikamilisha kadri fedha zitakapokuwa zinapatikana. Kwa hiyo, kwa upande wa USAID ni kweli fedha zipo utaratibu wa kumpata mkandarasi ni lazima tuufuate kwa sababu tukiwaharakisha hata USAID wenyewe hawatatoa hizo fedha. Kwa hiyo, naomba tuvumiliane taratibu za ki-procurement zikamilike kwa mujibu wa sheria.
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa suala la pili mimi naomba tu nimjulishe kwamba katika Wizara ambayo ina wataalam ni pamoja na sekta ya ujenzi. Naomba aamini suala hilo analoliongelea la crack ni la kitaalam, naomba tuwaachie wataalam na kwa mujibu wa wataalam wanaosimamia pale kazi ya ujenzi wa daraja hili itakamilika mwezi Disemba, 2016.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, ingawaje dah, Waziri kajibu kwa pozi kweli kweli mistari michache tu. (Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, anasema kwamba wanaendelea kujenga, hivi miaka 51 ya Uhuru upungufu nyumba 10,000 wapewe miaka mingapi ili wamalize hili tatizo katika nchi yetu? Magereza nimeshuhudia mwenyewe kwa mfano katika Wilaya yetu ya Kilombero kuna magereza mawili ya Idete na Kiberege wafungwa wanaenda kujenga nyumba za watu binafsi kwa nini msitumie nguvu kazi ya wafungwa hawa ili kwenda kujenga nyumba na Serikali muongeze hela kule juu kumalizia majengo haya? Hiyo nguvu kazi ya hawa wafungwa walioko magerezani mtafanya lini huo mpango? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika suala la Polisi yaani kama kuna tatizo kubwa ndani ya Mkoa wa Morogoro ni suala la nyumba za Polisi hasa Wilaya ya Kilombero likiwemo na Jimbo la Mlimba. Kwanza Wilaya ya Kilombero pale Ifakara kulikuwa na majengo ya Kituo cha Polisi, Mlimba hakuna kabisa wanategemea TAZARA…
MWENYEKITI: Mheshimiwa naomba uulize swali tafadhali.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Na zile nyumba zimeuzwa ule mwaka zilizouzwa nyumba za Serikali.
MWENYEKITI: Mheshimiwa naomba uulize swali kwa ufupi.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Sasa hivi hawana nyumba kabisa. Je, Serikali katika huo mpango wao wana mpango gani wa kujenga nyumba na Vituo vya Polisi ndani ya Wilaya ya Kilombero, Ifakara na Jimbo la Mlimba ambapo wanakaa kwenye vituo vya TAZARA?
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, huyu ni rafiki yangu sana. Ananiuliza tupewe miaka mingapi, yeye ana miaka mingapi? (Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeeleza na nirudie tena tunafanya kila linalowezekana tuhakikishe askari wetu wanakuwa na mahali pazuri pa kukaa. Ndiyo jibu sahihi, tunafanya kila linalowezekana askari wetu wawe na mahali pazuri pa kukaa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili nalo ni kwa sababu yeye ni rafiki yangu namjibu, mpango gani? Mpango nimeueleza kwenye jibu langu la msingi na nimhakikishie tu kwamba tutafanya kwa jinsi tulivyoeleza katika mpango wetu kuhakikisha kwamba askari wote wanapata nyumba nzuri na mahali pazuri pa kukaa.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti ahsante. Mimi nilifuata utaratibu nimeuliza swali fupi sana, lakini ukiona majibu marefu ujue hapa kuna udanganyifu. Sasa nina maswali mawili ya nyongeza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeuliza hili swali tangu nikiwa Mbunge wa Viti Maalum na Ofisi ya Wanyamapori wakati huo alikuwa Ndugu Sarakikya alinijibu kwamba walienda kupima na nikaenda Ofisi ya Ardhi Kilombero wakasema wananchi hawajashirikishwa. Baada ya kuwabana sana mkasema kwamba mnasubiri hela kutoka Ubelgiji na mmeshapata shilingi milioni 100 na sasa mnaaenda kushirikisha na mpaka kwenye Halmashauri yetu tunazo hizi taarifa, mnaenda mkashirikishe vijiji mkapime upya leo unaniletea majibu marefu. Nakuambia mradi wa ardhi hauendi kutatua migogoro unaenda kupima vipande vya ardhi ambavyo havina migogoro, Mheshimiwa Lukuvi huyu hapa. Sasa haya majibu yako mimi siyakubali, hiyo moja. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini sasa kuna barua ninayo hapa, Meneja wa Ramsar ametoa barua iko Kilombero anasema wataenda kutatua hiyo migogoro…
MWENYEKITI: Mheshimiwa Susan nenda kwenye swali.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Sasa ni lini mtaenda kutatua ile migogoro na mmeruhusu wafugaji waende kule kwa wakulima, magomvi karibu yatatokea, ardhi mmeitwaa, mmeenda kufanya nini? Lini mtaenda kurekebisha ile mipaka? Ninachotaka ni safari ya kwenda Kilombero. Mimi nasemea Kilombero lakini kuna Wilaya tatu, Ulanga na Malinyi, kuna vijiji 126 mmechukua bila idhini yao. Nendeni mkafanye kazi, hilo ndilo swali langu, ndiyo, lini mtaenda Kilombero na barua mnayo?
WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi tunaomjua Mheshimiwa Susan ndiyo lugha yake, hatumshangai.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na maelezo marefu ya Mheshimiwa Susan ni kweli kwamba tunayo migogoro mingi sana na Serikali tunajua kwamba tunayo migogoro mingi. Iko migogoro inayoweza kutatuliwa na Wizara moja moja, lakini iko migogoro ambayo haiwezi kutatuliwa na Wizara moja moja. Juzi nimetoka Kilombero yale yanayonihusu mimi nimejaribu kuyatatua, lakini hayo mengine anayoyasema sisi Serikali tumeunda timu. Hivi sasa tumekutana mimi na mwenzangu Waziri wa Mifugo, Waziri wa Maliasili na TAMISEMI tumeunda timu ziko mtaani huko mikoani na huko Kilombero watafika na nimewaambia hata juzi kwamba haya anayoyasema hayo siyo yangu, kuna Madiwani wameniambia kama alivyoniambia Mheshimiwa Susan.
Kwa hiyo, nimewaambia hili si letu kwa sababu haiwezekani Lukuvi anayekwenda siku moja akatatua mgogoro. Kwa hiyo, tumeunda timu ya wataalam wa Wizara nne wanapitia kuangalia namna bora ya kutushauri sisi Mawaziri tuamue juu ya migogoro hiyo mikubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge wanakumbuka wakati uliopita tuliwapa fomu fulani mkatupa ile migogoro iko, Mheshimiwa Susan ameandika kwenye kile kitabu. Kwa hiyo, kutokana na kile kitabu sasa tumeunda timu, nataka kukuhakikishia hata sisi kama Serikali tumejiwekea lengo katika miaka hii mitano lazima tuwe tumemaliza migogoro yote. Kwa hiyo, nataka tu kumueleza Mheshimiwa Susan kwamba migogoro ilikuwepo na itaendelea kuwepo lakini tumeamua kuikabili kisayansi.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa majibu ya kunakili kila swali anapoulizwa majibu yake ndiyo haya haya kwa hiyo ana-copy na ku-paste. Sasa kwa taarifa yako Waziri wa Mambo ya Ndani tarehe 5 Februari, 2017 alifanya ziara katika Jimbo la Mlimba na kuona hali halisi tete ilivyokuwa kule vituo vya polisi vimebandikwa pale TAZARA kwa hiyo hali ni mbaya zaidi ya kiusalama na akatoa ahadi kwenye mkutano wa hadhara baada ya kuona hali ni tete kwamba mwaka huu sisi tutafute kiwanja na kiwanja kimeshatafutwa karibuni ekari 80 kwa matumizi ya umma na sasa tulete ili iingie kwenye bajeti, nakushangaa unajibu swali huwasiliani na Waziri wako.
Sasa je, kwa ahadi aliyotoa Waziri wako tarehe 05 Februari, 2017 Serikali sasa iko tayari kuingiza kwenye mpango wa bajeti ya mwaka 2017/2018 ili Wananchi wa Mlimba wapate kituo cha polisi?
Kwa kuwa ndani ya Jimbo la Mlimba inafanana kabisa na Jimbo ya Kilombero, katika Makao Makuu ya Wilaya Ifakara, kituo cha polisi cha Wilaya kiko kwenye kituo cha maliasili na wakati wa mvua maji yanajaa askari wanaogelea kama bata. Ni lini sasa Serikali itapeleka pesa katika Mpango wa Bajeti wa mwaka 2017/2018 kuhakikisha wanajenga kituo cha Wilaya ya Polisi Ifakara maeneo ya Kibaoni ambapo kiwanja kimeshapatikana?
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nataka nimhakikishie Mheshimiwa Susan kwamba hakuna kupingana wala kugongana kokote kati ya mimi na Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, alichokifanya ndiyo tunakifanya ndiyo msimamo wetu. Alifanya ziara Mlimba na hivi juzi tu nimerudi kufanya ziara katika mikoa minne na nataka nikupe mfano ambao nimeuona katika Mkoa wa Mbeya kwenye Jimbo la Mbeya Vijijini ambapo Mbunge wake Mheshimiwa Oran amehamasisha wananchi kuweza kutafuta kiwanja, kuchangia fedha za awali za ujenzi na tukaahidi kama ambavyo Mheshimiwa Waziri alivyokuahidi wewe kwamba tutaangalia kama ambavyo jibu langu la msingi nimejibu pale ambapo fedha zitapatikana tuweze kuingiza katika bajeti kwa ajili ya kumalizia nguvu hizo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo mimi niseme tu kwamba Mheshimiwa Waziri alikuja na aliunga mkono jitihada hizo na naendelea kutoa wito tu kwa Waheshimiwa Wabunge wengine wote, wale ambao wataonakuna haja ya kufanya hivyo, kuongeza jitihada za Serikali kama ulivyotambua tuna upungufu mkubwa sana wa vituo katika nchi nzima. Wilaya, Tarafa na Kata tuna upungufu wa vituo 65 katika wilaya 65 nchi nzima. Kwa hiyo tatizo ni kubwa katika maeneo mengi nchini.
Kwa hiyo, tunaomba Mheshimiwa Susan usivunjike moyo, wewe endelea hivyo hivyo kuhamasisha wananchi, wachangishe na Mheshimiwa Waziri ahadi yake iko pale pale kwamba fedha zitakapopatikana tutachangia nguvu hizo.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Mimi swali langu dogo tu, nilikuwa naomba, maana uzoefu inaonekana kama Waziri Mkuu ama Waziri wa TAMISEMI anafika katika eneo kuangalia hali halisi ya matatizo ndiyo pale inapomuuma katika moyo na kutoa kipaumbele katika haya maeneo.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu ni kwamba ni lini sasa Waziri wa TAMISEMI ama Waziri Mkuu atafika kwenye Jimbo la Mlimba ili aangalie matatizo alie na machozi halafu aone sympathy ya kuwasaidia wananchi wa Mlimba katika masuala ya magari, afya na mambo mengine? Ni hapa tu.(Makofi/Kicheko)
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Kiwanga kwamba tulifanya ziara ofisi yetu, tumetembelea Halmashauri zote kati ya Halmashauri 185 tumebakisha chini ya Halmashauri kumi hivi sasa na moja ikiwa yako ya Mlimba. Ndiyo maana tumekubaliana hapa na nimezungumza katika kipindi mbalimbali kwamba baada ya Bunge nitakuwa na session maalum katika Mkoa wa Morogoro kumalizia Halmashauri zilizobaki na Mkoa wa Songwe, vilevile nitaenda kule Ukerewe pamoja na Mara ambako kuna Rorya, Tarime na Serengeti.
Mheshimiwa Naibu Spika, hayo tunaenda kuyafanya lengo kubwa ni kufikia maeneo mbalimbali tubadilishane mawazo tikiwa site kule tukubaliane, tubaini changamoto halafu tujadiliane, nini tutafanya ili kuwahudumia wananchi. Kwa hiyo, naomba nikutoe hofu katika hilo tutaenda kulifanya katika kipindi cha sasa.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Najua Naibu Waziri haya majibu amepata kwa wataalam, lakini ukweli ni kwamba katika Jimbo la Mlimba hakuna Kijiji kinachoitwa Ipela Asilia. Ipela Asilia ipo Wilaya ya Malinyi, Halmashauri mpya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilivyofuatilia Malinyi, Madiwani hawana taarifa yoyote, hata Baraza la Madiwani halina taarifa yoyote kuhusu hizi taarifa, wanaona tu watu wanaingia na kutoka. Ni kweli kabisa pale uwezekano wa mafuta upo mkubwa sana, wameshachimba kisima kimoja cha mfano.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa swali langu; kwa kuwa eneo hilo ni eneo nyeti, wanapatikana wale wanyama wasiopatikana duniani (puku), lakini Serikali inakwenda kutoa kibali cha kuchimba hayo mafuta na wananchi wanaozunguka hili eneo wamekatazwa kabisa kufanya shughuli za kibinadamu katika eneo hili.
MHeshimiwa Mwenyekiti, nataka majibu ya Serikali,
ni lini sasa watakwenda kuwaelimisha hawa wananchi na kuwapa wao maeneo ambayo wanaweza wakaendeleza shughuli zao za kilimo wakati mradi huu unaendelea na elimu haijatolewa katika kijiji hicho ambapo ni Kata ya Njiwa na Kata ya Itete; nimezungumza na Madiwani usiku.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la msingi; kwa kuwa amesema Mlimba; Mlimba katika Kata ya Mofu, Bwawa la Kibasila kuna utafiti ulifanyika na Mzee Magoma alikuwa Mkalimani wa wale Wazungu na ukweli ni kwamba Bwawa la Kibasila Kata ya Mofu, Kijiji cha Ikwambi kuna uwezekano mkubwa wa kupata mafuta kwa sababu kuna mikondo miwili inayotoka Ihenga na Mofu na Ikwambi na mkondo mwingine unatokea Mngeta, inakutana pale, kwa hiyo, wakasema kuna uwezekano mkubwa wa kupata mafuta.
Sasa nauliza swali hili kuhusu Jimbo la Mlimba; ni lini
sasa Serikali itakwenda katika Jimbo la Mlimba ikibidi waonane na huyu Mzee Magoma awaambie hali halisi, kwa sababu kuna uwezekano mkubwa wa kupata mafuta, lakini leo wamenijibu swali la Malinyi. Kwa hiyo, swali langu bado halijakidhi vigezo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi)
WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nipande kusema tu kwamba hatutakwenda kwa mzee yeyote kumuuliza uwezekano wa mafuta kupatikana, kwa sababu hili ni suala la kitaaluma, tutachukua utafiti uliofanywa Seismic Surveys ambayo kuna 2D na 3D, hizo ndizo zitakazotupeleka kule. Kwa hiyo, hatutakwenda kwa mzee.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine tena, mbali ya mchanganyiko wa majina, tunaomba radhi kama tumechanganya majina, lakini utafutaji wa mafuta, nataka kumweleza Mheshimiwa Mbunge kwamba, sehemu nyingine duniani watu wametafuta mafuta wameyakosa, lakini baada ya kubadilisha mbinu na namna ya kutafuta mafuta, wengine wakaja wakayapata. Kwa hiyo, hili ni jambo la kitaaluma na kitaalam, halina mjadala wa mambo ya kisiasa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Ni kweli kwamba kuna mpango wa kujenga Mahakama pale Mlimba, lakini sijui itachukua muda gani; ingawa hapo anaposema kwamba ni Mahakama, ni kibanda tu cha TAZARA wameazima na mara nyingi Mahakimu huwa hawapo muda mrefu sana. Labda kwa sababu hakuna Mahakama ambayo inatambulika rasmi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna Mahakama eneo la Utengule, kule alikotoka Chief Kiwanga, kwenyewe hakuna kabisa Hakimu. Kwa hiyo, watu wanapata shida sana katika kupata huduma. Je, pamoja na kuwa na mpango wa Serikali kujenga hiyo Mahakama hapo Mlimba ambapo ni Makao Makuu ya Jimbo, Serikali iko tayari sasa kupeleka Mahakimu kwenye maeneo ambayo kuna Mahakama lakini hakuna Mahakimu? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu Waziri huyu ameteuliwa hivi karibuni, je, yuko tayari sasa kufanya ziara kwenye Jimbo la Mlimba kuangalia hali halisi na miundombinu ili anapokwenda kwenye bajeti tuone kwamba anaikumbuka Mlimba na kuiwekea mafungu ambayo yanastahili ili wananchi wapate haki zao? (Makofi)
WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakubaliana na ombi lake la kuhakikisha kuwa Mahakama za Mwanzo katika Wilaya ya Kilombero, yaani Jimbo la Mlimba na Kilombero zinapata Mahakimu ili kusogeza huduma ya utoaji haki katika eneo hilo; hasa tukizingatia kuwa Wilaya ya Kilombero kama ilivyo Wilaya ya Loliondo, Kiteto, Manyoni ni Wilaya ambazo kijiografia maeneo yake ni makubwa sana na umbali ni mkubwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, naamini kabisa Wizara pamoja na Mahakama tutahakikisha Wilaya za aina hiyo, yaani Kilombero, Kiteto Loliondo na Manyoni, zinapata aina ya msisitizo katika kuhakikisha kwamba Mahakama zake za mwanzo zina Mahakimu wengi ili kupunguza umbali.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni dhahiri kabisa unapotoka Mlimba mpaka kwenda Kilombero kilometa 260 ni mikoa kwa sehemu nyingine. Kwa hiyo, tutalizingatia kabisa katika kuhakikisha kwamba Mahakama hizo kutegemea na Ikama iliyotolewa na Serikali, zinapata Mahakimu wa mwanzo wengi ikiwa ni pamoja na Utengule alipotoka Chifu Kiwanga.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu suala la ziara ya kwenda Mlimba, naipokea kwa mikono miwili; huu ni wakati wa mavuno; kwa hiyo, nitapata mchele na pepeta; siyo kama takrima, lakini kama ukarimu wa watu wa Mlimba.(Makofi)
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Mheshimiwa Spika, majibu ya Mheshimiwa Waziri kwa upande mmoja nakubali kwamba imeshafanyiwa upembuzi yakinifu na inasubiriwa sasa watafute hela ili ijengwe kwa kiwango cha lami. Msisitizo wangu, yeye amesema inapitika kipindicha mwaka mzima isipokuwa miezi michache, sasa mimi ndiye ninayetoka Mlimba na juzi tu mwezi Agosti nimetoka Mlimba, hii barabara imewekwa kwa kiwango cha inapitika angalau kwa miezi minne sikatai, kuanzia mwezi wa Septemba mpaka Desemba inapitika lakini kuanzia Januari mpaka Agosti hii barabara haipitiki. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kuna adha kubwa na hii barabara ina umuhimu wake siyo kwamba tu kusafirisha mazao lakini Hospitali ya Wilaya ya Rufaa, Mahakama na Kituo cha Polisi vipo Ifakara kilometa 231. Kwa hiyo, kipindi hicho akina mama, watoto na wazee adha inakuwa kubwa sana. Kwa hiyo, hii barabara licha ya suala la kiuchumi lakini watu wanakufa kwenye hiyo barabara na hakuna Hospitali ya Wilaya kule. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa barabara hii inapitika kwa miezi nne na inatengenezwa kwa kiwango cha vumbi na hii hela iliyotengwa hapa ni ndogo na kuna madaraja mengi, je, Serikali haioni umuhimu sasa wa kuitengea barabara hii pesa za kutosha ili ijengwe kwa kiwago cha changarawe wakati tunasubiri lami? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kila siku naongea na Mheshimiwa Waziri Mbarawa, je, yupo tayari sasa kuongozana na mimi kwenda kuikagua hiyo barabara na kuonana na wananchi wamwambie adha halisi wanayoipata kwenye barabara hiyo ili awe na huruma ya kuweka hela ya kutosha? Je, yuko tayari twende tukatembee mpaka Madeke kule Njombe?
Mheshimiwa Spika, naomba maswali yangu haya yajibiwe. (Makofi/Kicheko)
WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO:
Mheshimiwa Spika, ni kweli barabara hii kuna changamoto hasa wakati wa kipindi cha mvua na sababu kubwa ambayo imesababisha hivi, kwenye maeneo yale hakuna changarawe za kutosha na tunatumia mawe laini (soft rock). Sasa ukiweka mawe laini wakati wa mvua unakuwa na changamoto.
Mheshimiwa Spika, tumeamua tubadilishe mpango ule, tuweke soft rocks pamoja na cement tuichanganye pamoja ili kuhakikisha sasa barabara hiyo inaweza kupitika wakati wowote. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kuhusu kwenda kutembea na Mheshimiwa Susan, Mheshimiwa Susan ana speed kubwa kuliko mimi lakini tutakwenda pamoja tu. (Makofi/Kicheko)
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa hii nafasi.
Swali (a) kwa kuwa hapa ukiangalia tu haraka haraka kwenye jibu (a) unakuta kwamba kuna kazi kubwa inaendelea, lakini naomba hii kazi ukaone kwa macho.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini hii Mlimba aliyosema Mheshimiwa Naibu Waziri, kwa sasa inatumia maji ya kisima, kweli kuna kisima kimoja na hicho kisima kwa vile Mji wa Mlimba unakua kwa kasi na ni Makao Makuu ya Wilaya ya Tazara, yaani kwa wiki mara hii, moja, ndiyo maji tunapata. Kwa hiyo, naomba ukaone.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu sasa, kwa kuwa anasema kuna huu mradi ambao utakuja kufanyiwa upembuzi yakinifu kupata maji Mto wa Mgugwe na Mpanga, na kwa kuwa eneo la Mlimba lina vyanzo vingi vya mito, je, Serikali iko tayari kwenye huu mradi wa Mlimba kutumia maji ya Mpanga na Mgugwe kuingiza katika bajeti ya Serikali mwaka huu wa fedha ili wananchi wa Mlimba wapate maji safi na salama? (Makofi)
Pili, kwa kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri amezungumzia masuala ya Masagati, ni Kata ya Masagati; na hapa sitapoteza muda kusema mambo mengi, ninaomba sasa uje Mlimba maana umetoa ahadi nyingi sana hapa na Waheshimiwa Mawaziri wengi wakija wanaishia Ifakara badala kwenda Jimbo la Mlimba...
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi hiki tukimaliza Bunge naomba Mheshimiwa Naibu Waziri twende Mlimba akaone hali halisi maana sasa hivi muda hautoshi kusimulia, ili akija hapa anapojibu maswali aone kama anajibu hali halisi kutokana na hilo Jimbo la Mlimba. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Ukimwona mzee wa matobozano analia, ujue kuna jambo Mlimba. Kwa hiyo, mimi kama Naibu Waziri nipo tayari kwenda Mlimba.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine kwa kuwa kuna changamoto kubwa sana Mlimba kwa ruhusa yako, namwomba Mheshimiwa Susan tuweze kukutana baada ya Bunge ili tuweze kuangalia namna pekee ya kuweza kuwasaidia wananchi wake. Ahsante sana. (Makofi)
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Ni kweli kwamba kuna mpango wa kujenga Mahakama pale Mlimba, lakini sijui itachukua muda gani; ingawa hapo anaposema kwamba ni Mahakama, ni kibanda tu cha TAZARA wameazima na mara nyingi Mahakimu huwa hawapo muda mrefu sana. Labda kwa sababu hakuna Mahakama ambayo inatambulika rasmi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna Mahakama eneo la Utengule, kule alikotoka Chief Kiwanga, kwenyewe hakuna kabisa Hakimu. Kwa hiyo, watu wanapata shida sana katika kupata huduma. Je, pamoja na kuwa na mpango wa Serikali kujenga hiyo Mahakama hapo Mlimba ambapo ni Makao Makuu ya Jimbo, Serikali iko tayari sasa kupeleka Mahakimu kwenye maeneo ambayo kuna Mahakama lakini hakuna Mahakimu? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu Waziri huyu ameteuliwa hivi karibuni, je, yuko tayari sasa kufanya ziara kwenye Jimbo la Mlimba kuangalia hali halisi na miundombinu ili anapokwenda kwenye bajeti tuone kwamba anaikumbuka Mlimba na kuiwekea mafungu ambayo yanastahili ili wananchi wapate haki zao? (Makofi)
WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakubaliana na ombi lake la kuhakikisha kuwa Mahakama za Mwanzo katika Wilaya ya Kilombero, yaani Jimbo la Mlimba na Kilombero zinapata Mahakimu ili kusogeza huduma ya utoaji haki katika eneo hilo; hasa tukizingatia kuwa Wilaya ya Kilombero kama ilivyo Wilaya ya Loliondo, Kiteto, Manyoni ni Wilaya ambazo kijiografia maeneo yake ni makubwa sana na umbali ni mkubwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, naamini kabisa Wizara pamoja na Mahakama tutahakikisha Wilaya za aina hiyo, yaani Kilombero, Kiteto Loliondo na Manyoni, zinapata aina ya msisitizo katika kuhakikisha kwamba Mahakama zake za mwanzo zina Mahakimu wengi ili kupunguza umbali.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni dhahiri kabisa unapotoka Mlimba mpaka kwenda Kilombero kilometa 260 ni mikoa kwa sehemu nyingine. Kwa hiyo, tutalizingatia kabisa katika kuhakikisha kwamba Mahakama hizo kutegemea na Ikama iliyotolewa na Serikali, zinapata Mahakimu wa mwanzo wengi ikiwa ni pamoja na Utengule alipotoka Chifu Kiwanga.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu suala la ziara ya kwenda Mlimba, naipokea kwa mikono miwili; huu ni wakati wa mavuno; kwa hiyo, nitapata mchele na pepeta; siyo kama takrima, lakini kama ukarimu wa watu wa Mlimba. (Makofi)
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuuliza swali moja la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka huu nilipata ahadi kutoka Wizara hii kwamba kutapelekwa hela za ujenzi kituo kile cha Mchombe katika Jimbo la Mlimba kiliwekwa katika mpango wa Serikali na kilipata zile grade ambazo zinafaa kupewa pesa ili kuboresha Kituo cha Afya cha Mchombe ambapo kinahutubia kata zisizopungua 10. Je, na katika mpango uliopita hakuna hela iliyopelekwa, mimi tu mfuko wa jimbo nilipeleka hela kidogo kwa ajili ya kusaidia…
Je, ni lini sasa Wizara ya afya itapeleka pesa za kuimarisha Kituo cha Afya cha Mchombe ndani ya Jimbo la Mlimba?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Susan Kiwanga swali lake la nyongeza juu ya ahadi ambayo anasema ilitolewa, sina uhakika juu ya ahadi hiyo, lakini kama ahadi hiyo imetolewa kutoka Ofisi ya Rais, TAMISEMI naomba nimuhakikishie hivi karibuni ni kama nilivyojibu swali la nyongeza jana la Mheshimiwa Mipata kuhusiana na kituo chake cha afya Kasu kuna matarajio ndani ya mwezi huu kuna pesa ambazo zitapatikana kwa ajili ya vituo vya afya visivyopungua 25.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa sina uhakika kama katika hivyo 25 na yeye ni miongoni mwa hivyo ambavyo vinaenda kupelekewa pesa.
MHE. SUZAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa kuwa Naibu Waziri wa Fedha amesema kwamba wana mpango wa kufungua Benki ya Kilimo kwenye ngazi ya kanda na kwa kuwa Mkoa wa Morogoro hususan Wilaya ya Kilombero hasa Jimbo la Mlimba sasa hivi tupo kwenye ujenzi kwa kutumia mkopo katika Halmashauri yetu tunajenga Benki ya NMB Mlimba. Je, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka wa kupeleka dirisha katika mabenki haya ya NMB na CRDB kwa ajili ya kusogeza huduma kwa wananchi wakulima ambao wanateseka sana katika kupata pesa za kuendeleza kilimo chao badala ya kusubiri mpaka Benki ya Kilimo ikawa Kanda ya Kati?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, kufungua matawi haya kikanda ni kuwasogezea wakulima huduma kule walipo na hiyo kama nilivyosema iko kwenye mpango mkakati wa Benki ya Kilimo. Nimwombe Mheshimiwa Mbunge na Waheshimiwa Wabunge wote kwamba tuu-support mpango huu ili benki yetu iweze kuwasogelea wakulima wetu kule walipo katika kanda zao.
Mheshimiwa Naibu Spika, hili la kufungua dirisha katika mabenki mengine ya kibiashara ni wazo jipya, kama Serikali tunalichukua tuone kama linaweza kufanyiwa kazi na tuweze kuli-implement.
Mheshimiwa Naibu Spika, nipende kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba katika benki ambazo huwafuata wakulima kule walipo ni Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania. Kwa hiyo, popote pale wakulima walipo wanapokuwa wametuma maombi kwa ajili ya mkopo, Benki ya Kilimo huwatembelea wakulima hawa kule walipo. Kwa hiyo, tuendelee kuipa support Benki ya Maendeleo ya Kilimo iweze kuendelea kuwafikia wakulima wetu kwa ajili ya kuwahudumia. (Makofi)
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Nimepokea majibu ya Naibu Waziri. Kwa kuwa ametoa ahadi na bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi inakuja tarehe 17 Mei,2018 na tarehe 18 Mei, 2018, nitajiridhisha kwenye vitabu vyao kama kweli wametenga na wameingiza kuhusu ujenzi wa malambo ndani ya Jimbo la Mlimba.
Mheshimiwa Spika, hata hivyo, nampongeza Mkurugenzi na Halmashauri ya Kilombelo angalau tumetenga sisi kwa mapato ya ndani shilingi milioni 103 kwa ajili ya kuboresha na kujenga malambo ndani ya Halmashauri na Jimbo la Mlimba. Hizo ni jitihada tunafanya. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali langu linakuja, kwa kuwa, Jimbo la Mlimba lina takribani vijjiji 18 na kuna kilometa 606 eneo ambalo wafugaji wamekaa huko kwa wingi na vinaenda kufutwa, je, Wizara hii au Naibu Waziri yupo tayari sasa kwenda Jimbo la Mlimba kuangalia taharuki hii inayotokea kwa wafugaji hao na kuona umuhimu wa kuweka malambo ili wananchi hao na wafugaji wasiende kuingia kwenye haya maeneo ambayo yanachukuliwa na Serikali kwa ajili ya kupeleka maji kwenye Stiegler’s Gorge? Kuna taharuki kubwa sana ndani ya Jimbo la Mlimba. Je, yupo tayari sasa kwenda kuangalia na kupanga mipango sahihi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kunipa fursa ya kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Susan Kiwanga. Kwa ruhusa yako, naomba nimpongeze sana Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mlimba kwa kutenga pesa hizo kwa ajili ya kuhakikisha kwamba mifugo yetu inapata maji.
Mheshimiwa Spika, swali lake ni kutaka kujua kama niko tayari kwenda naye Mlimba kuangalia juu ya adha wanayopata wafugaji. Nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba sisi tunafahamu ufugaji ni maisha yetu na maisha yetu ni ufugaji. Hivyo, nipo tayari kwenda Mlimba kuungana naye kwa ajili ya kwenda kuwaona wafugaji hawa.
MHE.SUZAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa majibu ya Naibu Waziri. Mheshimiwa Waziri, amezungumzia suala la Malinyi na Ulanga, swali langu lilijikita zaidi Jimbo la Mlimba lenye kata 16 na kuna kata zisizopungua 14 ambazo zinatakiwa ziende zikafanyiwe marekebisho; na jibu lake limejikita kwenye kata tatu tu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa pamoja na mpango huo wa Serikali kutaka kuhifadhi hilo eneo, wananchi hatukatai, lakini kuna barua zimeshasambazwa kwamba, wananchi wanatakiwa waondoke, wafugaji na wakulima mwisho tarehe 30 mwezi Agosti. Zoezi la uelimishaji kweli limefanyika katika vijiji hivyo saba na imeundwa timu ya watu 15, lakini kiangazi ndiyo hiki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, waliahidi tangu mwezi Agosti watamaliza hilo zoezi kwenye hizo kata 14, ona, wamefikia kata tatu hata kata tatu wameunda tu timu lakini hawaenda kuweka vigingi. Je, lini sasa Serikali itaenda kuweka vigingi kwa kisababisho kwamba hamna hela? Kwa nini wanatufanyia hivi jamani? Lini watakwenda, hilo swali la kwanza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa wananchi hawana uhakika wa maeneo haya kama yataenda kwenye hifadhi ama watabaki nayo, katika kata zote 14 wananchi wanagoma kuchangia maendeleo ya kujenga shule na zahanati kwa sababu hawajui hatima yao katika maeneo hayo. Sasa Serikali kwa nini wanaleta kigugumizi hawapeleki hela? Wanatunyang’anya maeneo lakini wanasema hawana hela za kwenda kuweka mipaka na kiangazi ndio hiki je, ikifika wakati wa mvua watakwenda huko?
Mheshimiwa Mwenyekiti, wako tayari kwenda lini waniahidi hapa jamani? Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru.
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza napenda kumpongeza kwa kuamua kushirikiana vizuri kabisa na Serikali kwamba kuna haja ya kuweka hivyo vigingi ili mipaka ieleweke kwa wananchi kusudi waendelee kushughulika na shughuli zao na maeneo ambayo yamehifadhiwa yaendelee kuhifadhiwa, nampongeza sana kwa msimamo huo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kuweka vigingi ni kweli kabisa kwamba tulisimamisha kwa sababu ya mgogoro uliokuwepo, lakini kuna hatua kadhaa ambazo tulikuwa tumezichukua. Hatua ya kwanza tuliunda Kamati ya watu 22 wa kupitia wilaya zote tatu ili waweze kutoa ushauri kwa Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii, namna bora ya kuhakikisha kwamba vile vingingi vinawekwa na kupunguza migogoro ambayo ilikuwepo. Kamati hiyo tunatarajia kwamba itamaliza kazi yake na italeta ripoti wiki mbili zijazo kuanzia leo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kwenda kutenga fedha naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba fedha zimetengwa, fedha zipo; na nitumie nafasi hii kweli kuungana naye kwamba ni kipindi muafaka kwa sababu mvua zikianza itakuwa ni vigumu sana kwenda kuweka mipaka katika lile eneo hasa kipindi cha mvua, lakini kipindi hiki ndio kipindi muafaka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tutahakikisha kwamba ndani ya mwezi huu wa 10 mipaka hiyo inawekwa na nitaagiza taasisi zinazohusika zihakikishe kwamba hili zoezi linakamilika na wananchi wanashirikishwa na yeye mwenyewe Mbunge anashiriki kikamilifu katika hilo zoezi ili kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawasawa.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kuniona.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu linakuja kwenye haya mashamba. Katika Jimbo la Mlimba, Kata ya Namwawala, Vijiji vya Idandu, Miomboni na Namwawala sasa hivi kuna hekaheka kubwa kuzuia wananchi kwenda kulima mashamba yaliyokuwa eneo la Ramsar na matokeo yake na huku kijijini kwenyewe wanasema kuna uwekezaji wa sukari, lakini mpaka sasa Serikali hawasemi chochote kuhusu wananchi hao na Waziri Mkuu anajua, aliniahidi atakuja kutatua hiyo migogoro ili wananchi wawe kama outgrowers.
Je, lini sasa Waziri atakwenda Jimbo la Mlimba katika maeneo haya kuhakikisha kwamba wananchi hawa wanapata mahali salama pa kulima na pa kuishi katika Kata ya Namwawala na Mofu?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Mwenyekiti, kama alivyosema yeye mwenyewe, maeneo ambayo ni mashamba halafu hapohapo akataja jambo kubwa kabisa katika mazingira duniani linaitwa Ramsar, maeneo ambayo yametengwa kama Ramsar Sites ni maeneo ambayo hayastahili kuvamiwa au kutumiwa kwa maendeleo ya aina yoyote, yanatakiwa kulindwa, kuhifadhiwa kwa ajili ya mazingira. Mimi nadhani suala hili tutaendelea kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira kuhakikisha kwamba maeneo hayo yanatunzwa vizuri. Ahsante sana. (Makofi)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, (MUUNGANO NA MAZINGIRA): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuongeza katika majibu mazuri kabisa yaliyotolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI. Ni sahihi kabisa kwamba uhai wa ikolojia ya Mto Rufiji unategemea sana afya ya maeneo haya yaliyohifadhiwa kwa mujibu wa Mkataba wa Kimataifa wa Ramsar. Kwa hiyo matumizi ya maeneo yale lazima yawe uangalifu na Serikali kabla ya kuruhusu kazi za kilimo, ufugaji na matumizi ya kibinadamu, lazima ifanye utafiti wa kutosha na wa kujiridhisha ili tusije tukaharibu mifumo ya ki-ikolojia ya nchi yetu kwa kuruhusu shughuli za kibinadamu kwenye maeneo ambayo hayastahili kabisa kufanyika shughuli hizo.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante mimi siko mbali…
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Waziri Kangi Lugola ni awamu yake ya kwanza ya kuwa katika nafasi hii, na kwa kuwa mara nyingi nikimsikia na hata ndani ya Bunge amethibitisha ya kwamba atakomesha hiyo hali ya wananchi kuonewa, kuwekwa mahabusu muda mrefu bila utaratibu wowote.
Mheshimiwa Spika, je, Mheshimiwa Waziri yuko tayari sasa kwenda kwenye mahabusu ya Wilaya ya Ifakara na Mlimba kwenda kuangalia hali halisi, mahabusu wanavyowekwa ndani muda mrefu lakini hata chakula hawapewi, mara nyingi nimeenda kuwanunulia chakula na kuwapa mahabusu haki zao zinavunjwa kabisa za kibinadamu, hilo wa kutowapa mahabusu chakula unalizungumziaje?
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, kwanza wananchi wa Tanzania nataka niwahakikishie kwamba siyo nia wala lengo la Jeshi la Polisi kuwatesa mahabusu wanapokuwa wamekamatwa na wako ndani. Mahabusu wote wanapata chakula na wapo watu ambao wanapewa tender hizi za kuleta vyakula kwa mahabusu, hilo la kwanza.
Mheshimiwa Spika, pili kumekuwa na wananchi pia ambao wana vyakula wanavyohitaji kuwaletea wananchi mahabusu wao. Vyakula hivyo pia tumekuwa tukiwaruhusu kuwapatia mahabusu na kwa kuwa amelenga Mlimba, kwamba kuna matatizo nimeishasema kwamba kutokana na tatizo la baadhi ya askari wachache ama kuwabambikiza kesi wananchi ama kuwatesa nimesema jambo hilo halitakuwa na nafasi na litakomeshwa. Nimesema nitaanza ziara mikoa yote hivi karibuni na hizo kero nitazishughulikia. (Makofi)
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, kwa kuwa Jimbo la Mlimba kuna vijiji 18 ambavyo vyote vinaingia kwenye ardhi oevu na ile eneo ni eneo la wakulima.
Je, Waziri yuko tayari sasa kutembelea wakulima hawa walioko pembeni pembeni ili waone kwenye hiyo mito mikubwa iliyopo ndani ya Jimbo la Mlimba kuweka mabwawa ili wananchi wapate kilimo cha umwagiliaji kwa sababu watakuwa hawana tena mahali pa kulima?
WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, niko tayari kutembelea hilo eneo, lakini hatuwezi kuwaondoa wakulima kwenye maeneo ya oevu wanayolima mpaka tuwe tumshawawekea scheme maalum za umwagiliaji, tunamuondoa anaendelea na shughuli yake.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Spika, kama unavyoona hilo jibu la Serikali, nadhani hili linawagusa Wabunge wote. Ni hivi wameweka vituo vya ufundi, wanafunzi wanakwenda kule wanafundishwa lakini wakimaliza hawapewi cheti hata kimoja. Hivi hii ni halali kweli? Hii ni Tanzania nzima. Je, kwa nini Serikali mnawafanyia hivi watoto wa maskini wa nchi hii? Lini mtaanza kuwapa vyeti? Darasa la saba wanapewa vyeti, kwa nini wanaoenda ufundi hamuwapi vyeti ili waweze kujiendeleza? Kama si dhuluma ni nini kwa watu maskini? Hilo ni swali kwanza, Waheshimiwa Wabunge wote linawahusu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili, sawa wamesema hiyo inatiwa LGCD kwa maana ya grants. Bunge zima linajua mwaka huu hamna hata shilingi iliyokwenda na Waziri wa Fedha ameshindwa kujibu. Je, hiyo milioni shilingi 10, shilingi 15 mna uhakika gani itakwenda wakati shilingi bilioni 1.5 Wilaya ya Kilombero mpaka sasa mwaka unakaribia kwisha hawajapeleka hata senti 5. Kwa nini Serikali isiwe na mpango maalum na hii ni nchi ya viwanda kupeleka hizo pesa ili vituo hivi vya Mpanga na Mchombe viendelee kuliko kutegemea hiyo grants? Hakuna kitu hapa, hapa tunadanganyana tu, mimi nataka kujua lini mnapeleka hizo hela?
NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA):
Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa napenda kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge wa Mlimba kwamba tuko makini na wasikivu na ndiyo maana katika majibu yangu kwenye swali la msingi nimemwambia tumeupokea ushauri wake kikamilifu kwa ajili ya kuufanyia kazi.
Mheshimiwa Spika, kwanza, kwa sababu mafunzo haya katika vituo hivi ni mapya. Kweli mtalaa ni wa muda mrefu lakini tulikuwa hatuutumii, tumeanza kuutumia mwaka 2015 kwenye vituo hivi 208, tumepata mafunzo mazuri sana ya kutosha na tutakapoanza kutoa vyeti tutatoa vyeti vyote mpaka kwa wale ambao walisoma kuanzia mwaka 2015. Mwakani tutaanza kutoa vyeti, ndiyo maana nimesema tumechukua ushauri wake kwa ujumla kwa ajili ya kuufanyia kazi.
Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la pili, mimi sipendi sana kuwa mtabiri kutabiri mwaka 2018/2019 utakuwaje. Nimhakikishie kwamba hizi fedha ambazo tumezitaja katika jibu letu la msingi zitaenda wala asiwe na wasiwasi wowote.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwa kuwa, matatizo yanayotokea Masasi ni sawa kabisa na matatizo ya ndani ya Jimbo la Mlimba lenye kata 16, halina Kituo cha Polisi wala halina gari la Askari, hivyo kusababisha mahabusu kukaa muda mrefu kwenye kituo kidogo cha Polisi kilichopo pale TAZARA. Je, ni lini sasa na Waziri Mwigulu alishatembelea, Halmashauri tumeshatenga kiwanja na tuna baadhi ya matofali. Je, ni lini sasa Serikali itafikiria kuweka kituo cha Polisi Mlimba na kupata Askari wa kutosha ili kuwatawanya kwenye vituo ambavyo wananchi wamejitolea na tunakosa Askari kwa sababu hatuna mahali pa kuwaweka Askari kwa wingi pale Jimbo la Mlimba na hatuna kabisa usafiri na anajua? Mheshimiwa Spika, ahsante.
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, ni kweli mazingira yale aliyoyasema Mheshimiwa Mbunge nimeyashuhudia. Nilifika mazingira yale yanafanana kabisa na mazingira ya Jimbo la Mheshimiwa Joram Ismail Hongoli.
Mheshimiwa Spika, niseme tu Serikali inatoa uzito mkubwa kwenye maeneo kama hayo ambayo jiografia yake inalazimisha tuwe na usafiri wa kujitegemea ili kuweza kuwatengenezea mazingira mazuri Askari wetu ya kufanya kazi. Kwa hiyo, tunaweka uzito kwenye jambo hilo la usafiri pamoja na kituo hicho kikubwa anachokisemea. Punde tutakapoanza kutekeleza bajeti yetu na balance itakapokuwa imeruhusu tutatengeneza hili la kituo, lakini na hilo la gari tutakapokuwa tumeanza kugawa magari tutaweka uzito mkubwa katika Jimbo hilo.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Maliasili ndani ya Jimbo la Mlimba wamepeleka barua kwamba wananchi wakulima na wafugaji mwezi Julai waondoke wakati wa mipaka ya bonde hilo haijafanyiwa kazi na Waziri aliunda timu, kwenda kurekebisha mipaka ya Ramsar. Nini kauli ya Serikali kuhusu vitisho kwa wananchi hawa ambao hata mazao yao hawajavuna?
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Susan Kiwanga, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa mnamo mwaka jana tulitembelea bonde lote na tukazungumza na wananchi. Wananchi waliomba badala ya kuhama katika kipindi kile wapatiwe muda wa kutosha wa kujiandaa na waweze kuvuna mazao yao ndipo wahame. Ndipo Serikali ikatoa agizo kwamba ifikapo mwisho wa mwezi Agosti, 2018 wananchi hao wote wawe wamehama na wamevuna mazao yao yote. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi kama unaniambia kwamba wameambiwa wahame mwezi wa Julai, ni kinyume na agizo tulilokuwa tumelitoa awali. Agizo la Serikali tulisema wananchi wale waachwe, wavune mazao yao lakini ikifika tarehe 31 Agosti, 2018, wananchi wote wawe wameshahama katika eneo hilo. Kwa hiyo, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Susan na wananchi wake waendelee kutulia, wavune kwa utaratibu ili kusudi wahamie katika yale maeneo ambayo watakuwa wameelekezwa na Serikali.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Maliasili ndani ya Jimbo la Mlimba wamepeleka barua kwamba wananchi wakulima na wafugaji mwezi Julai waondoke wakati wa mipaka ya bonde hilo haijafanyiwa kazi na Waziri aliunda timu, kwenda kurekebisha mipaka ya Ramsar. Nini kauli ya Serikali kuhusu vitisho kwa wananchi hawa ambao hata mazao yao hawajavuna?
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Susan Kiwanga, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa mnamo mwaka jana tulitembelea bonde lote na tukazungumza na wananchi. Wananchi waliomba badala ya kuhama katika kipindi kile wapatiwe muda wa kutosha wa kujiandaa na waweze kuvuna mazao yao ndipo wahame. Ndipo Serikali ikatoa agizo kwamba ifikapo mwisho wa mwezi Agosti, 2018 wananchi hao wote wawe wamehama na wamevuna mazao yao yote. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi kama unaniambia kwamba wameambiwa wahame mwezi wa Julai, ni kinyume na agizo tulilokuwa tumelitoa awali. Agizo la Serikali tulisema wananchi wale waachwe, wavune mazao yao lakini ikifika tarehe 31 Agosti, 2018, wananchi wote wawe wameshahama katika eneo hilo. Kwa hiyo, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Susan na wananchi wake waendelee kutulia, wavune kwa utaratibu ili kusudi wahamie katika yale maeneo ambayo watakuwa wameelekezwa na Serikali.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Matatizo yaliyopo Ngara ni sawa kabisa tena yanapita ya Jimbo la Mlimba. Jimbo lenye kata 16 halina kituo cha polisi wala gari la polisi na kupelekea Mahabusu kukaa muda mrefu sana ili kuwapeleka katika Mahakama au Magereza yaliyoko kilometa 265. Je, ni lini sasa Serikali itaboresha miundombinu ya Jeshi la Polisi ndani ya Jimbo la Mlimba angalau uwapatie gari basi?
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:
Mheshimiwa Spika, ni sahihi katika Jimbo la Mlimba kuna upungufu ama ukosefu wa Kituo cha Polisi, lakini kama sehemu ya mkakati wa Serikali wa kujenga vituo 65 vya polisi nchi nzima tunaamini Mlimba ni moja ya katika maeneo hayo. Kwa hiyo, tu nimuombe Mheshimiwa Mbunge avute subira pale ambapo mpango huo utakapokuwa umekamilika kituo cha polisi kitapatikana Mlimba.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Swali langu linafafana na yaliyopita, kwa kuwa waliokuwa wafanyakazi wa TAZARA mwaka 2005 na mwaka 2009 wa miaka 55 walistaafishwa kwa lazima idadi yao ni 11,075. Ni lini wastaafu hao wa TAZARA watapewa mafao yao kwani mpaka sasa bado wanahangaika hapa Tanzania?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali moja la Mheshimiwa Susan Kiwanga, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze nimeongea naye kuhusiana na jambo hili siku mbili zilizopita na baada ya kuongea naye nimelifuatilia jambo hili na naomba kuweka takwimu sahihi. Kwa takwimu tulizonazo ndani ya Ofisi ya
Msajili wa Hazina, wastaafu waliostaafishwa kwa lazima miaka 55 ni 271 na wala siyo 11,075 kama Mheshimiwa alivyosema. Hao ndiyo wastaafu tunaowajua ndani ya Wizara ya Fedha na Mipango na sasa hivi faili lao liko mezani kwangu Mheshimiwa Mbunge tangu nimeongea nawe tumeanza kufuatilia ili malipo yao yaweze kulipwa kwa wakati.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante, nimepokea majibu ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, kwa kuwa upembuzi yakinifu umeshafanyika kuanzia Ifakara mpaka Kihansi; na kwa kuwa barabara hiyo hakuna kabisa sehemu ambayo unaweza ukapata changarawe kwa sababu upande wa kulia ni bonde oevu na upande wa kushoto ni Udzungwa. Je, Waziri husika yupo tayari kuongea na Waziri mwenzake wa Maliasili ili wakandarasi hao wanaotengeneza hiyo barabara ingawaje kwa kiwango cha changarawe waweze kupata kifusi au moramu katika eneo ambalo watalitenga kwenye eneo la Udzungwa? Nasema hivyo kwa sababu ni udongo tupu na hii barabara inabomoka kwa muda mfupi sana na wananchi wanapata tabu.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa pale Mlimba Mjini, TARURA kwa bajeti zao wanasema wataweka angalau kilometa 1 kiwango cha lami lakini kuna mita 500 za TANROADS zinazopita kwenda pale mjini. Je, TANROADS sasa wako tayari kwenye ile barabara yao pale Mlimba Mjini hizo mita 500 kuunganisha na ile lami ya Kihansi, Mlimba Mjini ili TARURA wanapofanya kazi yao kusiwepo na kipande kingine cha vumbi pale Mlimba Mjini, kwenye mji wa Mlimba?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Susan Kiwanga, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbunge anafahamu tulipata nafasi ya kutembelea barabara hii na changamoto ya kupata changarawe ili kuifanya barabara iwe bora zaidi tuliizungumza na tulikuwa tumefanya mazungumzo na wenzetu upande wa Maliasili. Hata hivyo, kwa vile amelisema tena hapa nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba tutafanya mazungumzo ili tuweze kupata kibali cha kifusi ambacho kitafanya barabara hii matengenezo yake yawe imara.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili la kipande cha mita 500, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba nalichukua ili niweze kulielekeza upande wa wenzetu wa TANROADS, Mkoa wa Morogoro ili kilometa 1 itakayotengenezwa na TARURA iwe na muunganiko mzuri na hizi mita 500, hii nimelichukuwa.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kuniona swali hili la Mheshimiwa Koka, tena hili la juzi, lakini katika Jimbo la Mlimba kuna mradi mkubwa wa umeme mkubwa ulikuwa unapelekwa kutoka Kihansi Jimboni Mlimba kwenda Wilaya ya Malinyi, katika mwaka 2014 na mpaka 2016 TANESCO ikakubali kwamba wale watu wanatakiwa walipwe, lakini mpaka leo unavyozungumza wengine wameshakufa, wengine wameshazeeka hawajalipwa hata senti tano. Je, ni lini sasa Serikali itawalipa hawa wananchi au kwa vile wako mbali sanahakuna barabara jamani kosa, letu nini wananchi wa Mlimba?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Susan, Mbunge wa Jimbo la Mlimba kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli nipokee hii changamoto ambayo ameielezeaMheshimiwa Suzana na nikitambua kwamba kwa kipindi cha Bunge hili la Kumi na Moja, awamu ya kwanza alihudumu Kamati ya Nishati na Madini na nimwahidi kwamba tutaenda kufuatilia kwa sababu maeneo haya anayoyataja na kwa kuwa mradi mkubwa wa Kihansi unaozalisha umeme zaidi ya megawati 180 ni ya wananchi wa maeneo hayo, hivyo tunawategemea sana na wamekuwa watunzaji wazuri wa mazingira na mpaka sasa hivi hatujawahi kupata changamoto yoyote ya kusema labda maji yamepungua katika uzalishaji wa umeme. Kwa hiyo nimwahidi Mheshimiwa Mbunge baada tu ya hapa naomba tufuatilie, kwa sababu hata jana aliniambiakuhusu hili suala ili kuona fidia imefikia wapi, lakini nihakikishe kwamba kama haki hiyo ipo na tahmini ilifanyika Serikali ya Awamu ya Tano inalipa fidia. Ahsante sana.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Nasema tu kwamba Wilaya ya Kilombero na hasa kutokana na miundombinu yake ina upungufu wa Walimu 1,018 na sio wa sayansi tu, wa kada zote. Kwa mfano, Jimbo la Mrimba unakuta shule ina Walimu watatu lakini ina wanafunzi 800 au 1,000. Je ni lini sasa Serikali katika hawa Walimu wanaosema wanawaajiri sasa hivi watatupelekea Walimu kwenye Wilaya ya Kilombero, ikiwemo na wanawake kwa sababu kuna shule haina Mwalimu mwanamke hata mmoja. Sasa wale watoto wanaokuwa wakamuone nani? Kwa hiyo, ni lini sasa mtapeleka walimu hususan Jimbo la Mrimba ili watoto wale waendelee kukua wakiwa na chakula cha akili? Ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Naomba nijibu swali la Mheshimiwa Suzan Kiwanga, Mbunge wa Mrimba kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, tumeshatoa maelekezo zile shule ambazo zina Walimu wa kike peke yake au wa kiume peke yake ni lazima wachanganywe. Hii kwa kweli ni kazi ambayo inafanywa ndani ya Wilaya na Mkurugenzi mwenyewe kwani ana uwezo kupata taarifa na Mheshimiwa Mbunge anawasiliana naye halafu wanawabadilisha ndani, kama ni Mwalimu kutoka nje ya mkoa mwingine hilo ndio unakuja ngazi ya TAMISEMI. Kwa hiyo, nadhani hilo lifanyike na ningepeda kueleza kwa kweli itakuwa sio sawasawa kama kuna shule ina Walimu wa kiume tu na shule ile ni mchanganyiko. Kwa hiyo, naomba nitoe maelekezo kwa Wakurugenzi wote na Maafisa Elimu wa Mikoa na Makatibu Tawala, hili jambo walifanyie kazi sio zaidi wiki mbili kwa sababu inawezekana na ndani ya mazingira yao.

Mheshimiwa Spika, kama nilivyozungumza, ajira hizi ambazo tumetangaza tutazingatia maeneo ambayo yana upungufu mkubwa na tuliomba Mheshimiwa Mbunge anajua kuna shule ambayo, shule za msingi inawezekana kwamba unaweza ukawa na Walimu wachache kwa sababu wanafundisha masomo mengi kwa wakati mmoja, lakini sekondari lazima kila mtu ana somo lake au masomo mawili ambayo anafundisha, haya maeneo ambayo yana changamoto kubwa na tutahakikisha kwamba tunapeleka Walimu katika maeneo haya. Ndiyo maana tumezuia pia na uhamisho, labda niliseme hili, kwa maana kwamba kuna maeneo ya halmashauri kwa sababu yana mazingira magumu, watu wamekuwa na sababu nyingi sana za kuwahamisha na kuomba uhamisho.

Mheshimiwa Spika, maelekezo yametoka kwa Serikali kwamba tusimamishe uhamisho kwanza wa Walimu nchi nzima ili tutengeneze mifumo ambayo, anapoomba uhamisho kwa sababu yoyote ile hata kama ni mgonjwa, kumfuata mume wake au mke wake au vyovyote itakavyokuwa tujue je, anapotoka kule Kaliua, Mrimba, Kilosa anapooenda kule balance ikoje kule ya Walimu, kwa maana ya kuangalia ikama hiyo. Kwa hiyo, tumelichukua hatua hiyo baada ya kugundua kwamba kuna maeneo wanakimbia mazingira magumu ya kazi, wanaenda sehemu ambayo kuna unafuu, anapaswa kufundisha mahali popote kulingana na mkataba wake wa kazi. Ahsante.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante, kama ilivyo kwa Mheshimiwa Maghembe Mwanga, Wilaya ya Kilombero yenye majimbo mawili ilikuwa na upungufu wa walimu 1,118 na hivi juzi tu tumeletewa walimu 34, wanne wa sayansi sekondari na 30 wa msingi na kufanya nakisi upungufu huo ubaki 1,084.

Je, Serikali ni lini sasa itapeleka walimu ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, ili watoto wale wapate chakula cha akili, ukizingatia na miundombinu yetu si rafiki?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, ni kweli, kama nilivyosema, tumeajiri walimu 4,549, tuna shule za msingi 16,000 za Serikali na tuna shule zaidi ya 4000 za sekondari. Katika hali ya kawaida upungufu huo naupokea kama Serikali ni kweli, kuna upungufu mkubwa na tusingeweza kupeleka kila mahali. Lakini tuliangalia kwa mfano kuna shule ambazo pale kulikuwa na wakumu ambao wanapelekwa shule za msingi, wameenda mahitaji maalumu, wameenda na masomo ya sayansi na hisabati.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, angalau tukaangalia shule ambazo zina upungufu mkubwa zaidi tukapeleka pale, kwingine tumepeleka walimu mpaka watano, wengine wanne.

Mheshimiwa Spika, lakini, Mheshimiwa Susan Kiwanga wiki iliyopita aliuliza swali hap ana walimu hao. Tumeshatoa maelekezo, kwanza kuna walimu wapo kwenye halmashauri, makao makuu ya wilaya au ya mji, lakini unakuita pembezoni kule unakuta walimu ni wachache, lakini walimu wapo. Tumeshapeleka fedha katika halmashauri zote nchini za kuweza ku-balance ikama.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tunatarajia kwamba kazi hii itafanyika kwa kusimamiwa na Makatibu Tawala Mikoa na Wakurugenzi, ndani ya wiki mbili mpaka tatu, tupate taarifa rasmi.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu ilikuwa kuhamisha walimu kupeleka pembezoni ilikuwa ni ngumu kwa sababu fedha hazipo, sasa fedha wameshapelekewa Halmashauri zote, zinatakiwa kazi ifanyike, halafu ajira inayofuata tutazingatia maeneo yote ambayo yana upungufu mkubwa. Shule za msingi, hisabati na masomo ya sayansi.

Mheshimiwa Spika, ahsante, likiwemo na eneo la Kongwa.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kuniona. Nimeongea na Waziri mara nyingi na akaniahidi kwamba kwenye mradi wa REA ambao sasa hivi upo field kwenye Kata ya Idete, Shule ya Sekondari Matundu Hill na Shule ya Sekondari Kamwene ambapo mradi unapita pembeni kidogo anasema maeneo haya ni muhimu kupeleka, lakini mpaka leo hakuna jitihada za Serikali.

Je, ni lini sasa Shule ya Sekondari Matundu Hill Idete na Shule ya Sekondari Kamwene watapatiwa umeme ili wanafunzi wa sekondari waweze kujisomea na kupata ufaulu mzuri?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda nijibu swali la Mheshimiwa Kiwanga Susan kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimshukuru kwa swali lake zuri, nami nimewahi kufika Idete; katika Idete pale ikiwemo Gereza la Idete limeunganishiwa umeme kwa kutumia ile umeme wa low cost design. Kwa hiyo nataka nimtaarifu Mheshimiwa Mbunge ahadi ya Mheshimiwa Waziri na hapa nitoe malekezo kwa Shule za Sekondari Kamwene na Matundu Hill Idete nimwagize mkandarasi State Grid wa Mkoa wa Morogoro atekeleze maagizo ya Mheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Naibu Spika, agizo hili sio kwa mkandarasi wa Morogoro peke yake na wakandarasi wote nchi nzima, watekeleze agizo la Serikali la kuhakikisha wanapofikisha umeme katika maeneo mbalimbali kama pana taasisi za umma iwe kituo cha afya, iwe mradi wa maji, iwe sekondari waunganishe. Tuliwaeleza variation ya namna hiyo inakubalika na Serikali hii ya Awamu ya Tano haiwezi kushindwa kulipa gharama kama inagharimu mradi mzima wa REA awamu ya tatu zaidi ya takribani trioni moja na bilioni mia moja. Kwa hiyo, nawaomba wakandarasi watii maelekezo ya Serikali. Ahsante sana.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi nipate kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Kwa kuwa suala la ultrasound katika vituo vya afya au Hospitali za Wilaya na Halmashauri, ni suala kubwa sana na halipatikani maeneo mengi nchini Tanzania na hii inaathiri kina mama na wanaokwenda katika Hospitali hizo kuangalia hali zao za kiafya hasa katika suala la tumbo.

Je, ni lini sasa Serikali itaweka mkakati kupeleka ultrasound kwenye vituo vyote vya afya nchini Tanzania na Hospitali za Wilaya ili wanawake wapate huduma hizo katika hospitali nchini?

Mheshimiwa Spika, katika Jimbo la Mlimba, Kituo cha Afya cha Mlimba kina ultrasound na mfuko wa Jimbo nilichukua nafasi mimi kumpeleka kwa kuomba na DMO kwenda kumsomesha mtaalam ambaye amesharudi na huduma hii inapatikana Kituo cha Afya cha Mlimba, lakini kuna Kituo cha Afya cha Mchombe, hakina ultrasound.

Je, nini kauli ya Serikali kupeleka ultrasound katika Kituo cha Afya cha Mchombe, ndani ya Jimbo la Mlimba?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Spika, nakubaliana kabisa na Serikali inatambua umuhimu wa uwepo wa kifaa cha ultrasound na ndiyo maana katika vituo vyote vya afya ambavyo tunavijenga, tayari fedha tulishapeleka MSD kwa ajili ya kuhakikisha kwamba kituo cha afya vinavyokamilika vinakuwa na vifaa ikiwa pamoja na ultrasound.

Mheshimiwa Spika, na kwa mfano, katika swali la msingi la Kituo cha Afya cha Ujiji, tayari fedha imepelekwa na fedha hiyo imepelekwa tarehe 29 Aprili uliopita na baada ya wiki tatu, katikati ya mwezi Juni, tayari ultrasound itakuwa imefika.

Mheshimiwa Spika, lakini katika swali lake la pili, hicho kituo cha afya ambacho anakisema cha Mchome, naamini ni miongoni mwa vituo vya afya ambavyo tayari tumeshapeleka fedha MSD, kwa hiyo, tukishamaliza kipindi cha maswali na majibu, ni vizuri tukakutana na Mheshimiwa Mbunge ili tutazame wao lini wanatarajia kupata ultrasound.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante majibu ya Waziri ni kama vile ya kukopi na ku-paste sasa nimeuliza swali kama Mbunge wa Halmashauri ya Mlimba pamoja na kuwa kuna halmashauri nyingine zimeshaanza kupata hizo hela na zinajengwa lakini kila mtu analia na pale panapo mbana. Sasa Halmashauri ya Mlimba yaani kwa miaka mitatu mfululizo wanafunzi waliomaliza Kidato cha Nne takribani milioni nne laki nane na themanini na saba wako mtaani ukiachilia mbali wa darasa la saba. Sasa na pale Mlimba katika Kituo cha Mpanga Utengule kuna majengo kabisa yapo kwa hiyo Serikali haiwezi kuwa na gharama kubwa kwenda kujenga majengo mengi.

Je, kwa nini Serikali isiende kwenye Kituo hiko cha Mpanga kwenda kukiboresha ili wanafunzi hao wanaozagaa mtaani waanze pale baada ya kujenga majengo makubwa hayo tunayosubiri kwa miaka mingi na watoto wanazidi kupotelea mtaani? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, je, Serikali ina mpango gani sasa wa kuboresha hizo Shule za Sekondari au za Msingi kuwepo na Kitengo cha Ufundi ili hawa wanafunzi hata kama wakifeli kuingia darasa la juu wawe tayari wamepata miundombinu ya kiufundi katika maeneo haya katika Shule zote Tanzania? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kuhusu kama jibu langu ni la kukata na kupaka yaani cut and paste naomba nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba hata swali ambalo ameniuliza nalo siyo jipya sana linaulizwa mara nyingi kwa hiyo majibu yanakuwa ni yale yale siyo kwamba lenyewe ndiyo limeanza kuulizwa leo.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo kuhusiana kama inawezekana Serikali kutoa fedha ili kuendeleza Kituo ambacho tayari kipo ili kiwe Chuo cha VETA naomba tu nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kama kuna Taasisi ambayo tayari inatumika na inaonekana inafaa kuwa VETA bila kuvunja matumizi au kuondoa matumizi ya sasa Serikali iko tayari kufikiria lakini ni baada vilevile ya kufanya tathmini ya kuhakikisha kuwa inafaa kwa ajili ya kuachwa Chuo cha VETA.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake kuhusu Serikali kuboresha au kuanzisha mafunzo ya Ufundi katika Shule zote naomba nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari kuna Mpango madhubuti wa kuboresha baadhi ya Shule zetu za Ufundi lakini kwa sasa jitihada kubwa tunaweka katika kuanzisha Vyuo vya VETA kila Wilaya kuliko kila Shule ya Sekondari kuwa Shule ya Ufundi kwa sababu vilevile ina mahitaji makubwa hasa ikichukuliwa kwamba tunahitaji kuwa na Walimu wa kutosha.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa majibu haya ingawa wamekosea sana majina ya vijiji vyangu na kata zangu na pale napenda kutoa marekebisho kwamba pale Taweta ni Kijiji cha Tanganyika siyo Tanga, sisi kwetu hatuna Tanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na jitihada za Serikali lakini jimbo la Mrimba lina changamoto kubwa sana ukizingatia sisi ni wakulima kama asilimia 99 kwa hiyo madaraja haya yasipojengwa kwa wakati kwa hiyo mazao mengi yanashindwa kufika sokoni na wakulima kuwa maskini miaka yote.

Je, pamoja na bajeti hii imetengwa, Serikali haioni kwamba iliangalie Jimbo la Mlimba kwa akina ya pekee kuhakikisha kwamba wananchi hawa wanapata miundombinu hii ukizingatia mito mingi mikubwa kwa mfano hii Tanganyika kuna huo Mto Kilombero ndiyo unapita huko, chini kuna mamba wengi lini mtafanya na kunatakiwa daraja kubwa.

Je, Waziri mara nyingi naongea na wewe upo tayari sasa kutembelea hilo Jimbo la Mlimba hivi uone hali halisi na uone kwamba kunajitihada za kujenga haya madaraja uone wananchi wanavyoteseka na mara nyingi nakuomba lakini hutaki kwenda? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kwanza atuwie radhi kwa kukosea majina ya vijiji vyake hatukukusudia hilo, lakini na yeye mwenyewe amekiri kwamba tumetenga kiasi cha shilingi milioni 300 kwa ajili ya kuanza kujenga hilo daraja ambalo ni kubwa lakini kiasi cha shilingi 127; naomba Mheshimiwa Mbunge aridhike na jitihada ambazo zinafanywa na Serikali kwamba ni azma yetu kuhakikisha kwamba wananchi wa Mlimba wanapata madaraja na barabara za uhakika katika kipindi chote na mimi nashukuru, leo ameongea hajalia na sisi tunamhakikishia haitatokea kulia tena.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini Mheshimiwa Susan amesema amekuwa akiniomba twende Mlimba naomba nimhakikishie nipo tayara ilikuwa ni swala tu la muda tupange na yeye mwenyewe tumewasiliana kunapindi fulani akasema kipindi hiki mvua zinanyesha sana hatuwezi kwenda, niko tayari.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Tatizo la huu ugonjwa wa mnyauko katika migomba, linafanana kabisa kwa miaka mingi na mnyauko au ugonjwa wa manjano kwa kilimo cha mpunga ndani ya Wilaya ya Kilombero na mwaka huu athari hii imekuwa kubwa mno. Kila mara nilikuwa nafuatilia hapa kuuliza maswali Bungeni lakini hatujapata jibu kwamba tunafanyaje sisi wakulima wa mpunga kwani tunapata hasara kubwa?

Je, Serikali ina mpango gani wa kutupa majibu wakulima wa mpunga hususan wa Wilaya ya Kilombero, Ulanga, na Malinyi ambapo ndio walimaji wakubwa wa mpunga ili tuepukane na hizi harasa tunazopata kila mwaka? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA): Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema kwenye swali langu la msingi, Serikali inatambua kwamba kuna changamoto ya mabadiliko ya tabianchi na moja ya changamoto hizi ni magonjwa ambayo yanashambulia mazao yetu likiwemo zao la mpunga kama Mheshimiwa Susan alivyosema.

Mheshimiwa Spika, Serikali tunatambua mazao haya, ni lazima tuweke jitihada ya kuhakikisha tunaongeza uzalishaji wa wakulima wetu kwa sababu nchi zinazunguka Tanzania zina uhitaji mkubwa wa mchele na mazao mengine. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Susan kwamba Serikali inatambua changamoto zilizopo kwenye mabadiliko ya tabianchi. Kwa kupitia Taasisi zetu za TARI na ASA, tutaenda hata Jimboni kwake kuangalia changamoto alizozitaja ili tuweze kuzifanyia kazi.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, matatizo ya walimu wa sayansi yameikumba sana Wilaya Kilombelo hususani jimbo la Mlimba karibuni ina shule 26 za sekondari. Lakini hivi karibu tumepata walimu wa sayansi wanne tu na kupelekea shule nyingi za sekondari kukosa walimu wa sayansi.

Je, Serikali ina mpango gani kutupelekea walimu wa sayansi Wilaya ya Kilombero husani jimbo la Mlimba ukizingatia tunakula samaki, kwa hiyo, watoto wana akili sana ya mahesabu na sayansi kwa mfano bora angalia tumemtoa Mheshimiwa Likwelile alikuwa kule Wizarani tumemtoa Benno Ndulu kwa hiyo sasa hivi tunakosa wasomi kwa sababu hatuna walimu wa sayansi. Ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA W. WAITARA): Mheshimiwa Spika, ni kweli Mheshimiwa Mbunge ameuliza mara kadhaa swali hili tunamshukuru, lakini tumepeleka walimu wachache kulingana na mahitaji yaliyopo, lakini tumeomba kibali cha kuajiri walimu wa kutosha mwezi huu wa sita au mwaka wa fedha mpya ukianza. Kwa hiyo, pindi tutakapopata hicho kibali Mheshimiwa Mbunge ndio maana nakuhakikisha kwamba suala Mlimba na maeneo mengine yenye upungufu mkubwa kama kwako kule tunazingatia maombi yako muhimu. Ahsante.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, kwa kweli ukizungumza suala la barabara, ukiangalia Mheshimiwa Mgimwa, Mheshimiwa Mwamoto na Mheshimiwa Hongoli wote hawa wanatobozana kwenye Jimbo langu. Hiyo inakuza uchumi ndani ya Mkoa wa Morogoro Wilaya ya Kilombero hususan Jimbo la Mlimba. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kama ulivyosema siku ile nipewe maji hivi sasa hali ya barabara ya Ifakara – Mlimba inapitika kwa magari tu ya mizigo midogo midogo, magari ya abiria hayapiti kwa hiyo kupata taabu sana kina mama ambapo wanakwenda kufuata huduma ndani ya Wilaya ya Kilombero - Ifakara.

Je, Serikali ina mpango gani wa dharura kurekebisha ile barabara ya kutoka Mlimba hadi Ifakara ili kina mama na watoto na abiria wengine na mizigo sasa hivi tunavuna ili ipate kupita kwenda sokoni na kupata huduma za jamii? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli Mlimba pamekuwa special kidogo kwa sababu yako mahitaji ya kuunganika na Njombe kwa maana ya kutoka kule Lupembe, Madeke kuja Mlimba, lakini iko kiu ya kuunganishwa na Mufindi kama Mheshimiwa Mgimwa alivyozungumza, lakini pia kutoka Kilolo kuja Mlimba. Kwa hiyo, utaona wananchi wa maeneo haya na kihistoria walikuwa sehemu moja na bado shughuli zao za kiuchumi zinafuatana. Niseme tu kuhusu mpango wa dharura wa kutengeneza maeneo haya na Mheshimiwa Susan amerusha picha nyingi sana kuonesha wananchi walivyopata adha nyingi sana wakati wa mvua zikiwa nyingi.

Mheshimiwa Naibu Spika, atakubaliana na mimi kwamba wakati wa mvua zikiwa nyingi na maji yakiwa mengi kufanya matengenezo kwenye barabara zetu inakuwa ni ngumu, lakini kwa vile mvua zimepungua na tunazo fedha za emergency kwa ajili ya matengenezo. Tumetoa maelekezo kwamba mvua zikipungua mara moja cha kwanza ni kuhakikisha kwamba maeneo ambayo yameharibiwa na mvua yanarekebishwa ili wananchi waendelee kupata huduma hii ya barabara, huduma muhimu.

Kwa hiyo, Mheshimiwa Susan vuta subira tumea maelekezo na ninarudia kuelekeza wenzetu TANROADS Mkoa wa Morogoro baada ya mvua kupungua sasa nguvu kubwa ielekezwe kwenye maeneo ambayo wananchi wamepata shida wakati wa mvua kubwa zilizonyesha hivi karibuni. Ahsante sana.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Katika Jimbo la Mlimba, Mkandarasi Ben Investment Company Limited anayejenga Mradi wa Maji Chita amesimama kujenga kwa sababu hajalipwa fedha zake kiasi cha shilingi 192,000,000 yapata kama miezi nane sasa. Je, ni lini Serikali itamlipa huyu mkandarasi ili aendelee kujenga huo mradi wa Chita?
NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda nijibu swali la Mheshimiwa Mbunge mama yangu Susan Kiwanga, lakini kikubwa ambacho nataka kusema utekelezaji wa miradi ya maji inategemeana na fedha na tunashukuru Serikai kila mwisho wa mwezi huwa wanatoa fedha zile za Mfuko wa Maji zaidi ya shilingi bilioni 12. Nataka nimhakikishie dada mwezi huu tutakapopata ile fedha ya mfuko tutahakikisha kwamba tunakupa kipaumbele ili Mradi wa Chita uweze kuendelea.