Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Dr. Immaculate Sware Semesi (4 total)

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa hii ya kutoa mchango wangu kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais na hoja yangu itakuwa upande wa Mazingira.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaanza kwa kutoa masikitiko yangu kuwa sekta hii ya mazingira imepewa kipaumbele cha chini sana, ukizingatia muda kwanza uliotengwa kujadili na hata sekta ya mazingira ilivyowekwa na Kamati ya Bunge imechanganywa na Viwanda na Biashara. Nataka tu nisisitizie umuhimu wa sekta hii ukiangalia hali ya nchi yetu ya Tanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania bado ni nchi maskini na tunategemea rasilimali tulizonazo ambazo ni mazingira katika sekta mbalimbali. Uvuvi huko kwenye maji, ukulima mashambani, ufugaji, yote haya ni mazingira. Ukiangalia Serikali kwa sasa mazingira imeipa priority ndogo sana, mfano tu mdogo, sasa hivi kuna harakati tukiongelea mazingira tunachokiona kwenye Vyombo vya Habari au harakati zinazoendelea ni kutoa warning kwenye viwanda au kufunga viwanda kwamba vinachafua mazingira ama tunasema kwamba tufanye usafi kwa kufagia au kupiga deki maeneo fulani. Kwa hiyo, hii concept nzima ya mazingira inakuwa sivyo inavyotakiwa iwe.
Mfano wa pili, kwenye mazingira ambavyo tumeipa priority ndogo sana na inashangaza, asilimia kubwa yetu, takribani asilimia 65 ya wananchi wa Tanzania ni wakulima. Ukulima uko wa aina gani? Ukulima huu uko katika kuvuna rasilimali au kupanda mazao kwenye haya maeneo, je, haya maeneo yanayolimwa yanafanya kazi vile inavyotakiwa kwenye kutunza mazingira ili huu ukulima wetu uwe endelevu?
Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia sekta ya mazingira pia katika shughuli za uvuvi, je hizi rasilimali tunazozichukua katika nchi yetu tunavuna vile inavyotakiwa? Sasa hivi kuna kesi kubwa sana mifano ya uvuvi haramu ambayo inaharibu hayo mazingira ya samaki. Hiyo ni mifano tu michache.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali yetu inaongelea kwamba, tunataka uchumi wa viwanda, lakini uchumi huu wa viwanda rasilimali zinatoka wapi? Ni kwenye haya haya mazingira. Hii ni sekta ambayo imeibeba nchi, lakini cha kushangaza ni sekta ambayo imepewa priority ndogo sana. Rasilimali zetu tunazitoa katika mazingira kwa nini hatuipi mazingira priority inayotakiwa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano mzuri ni katika hata hii Taasisi inayoshughulikia mazingira, National Environment Management Council (NEMC), imepewa bajeti kiasi gani ili kutekeleza majukumu ya kusimamia sera ya mazingira nchini, sifuri si ndiyo kwa mwaka huu wa bajeti? Je tutapitisha? Hilo ni suala la kuzingatia. Hapo nilikuwa naonesha tu umuhimu wa mazingira na jinsi ambavyo bahati mbaya hatujaipa sekta umuhimu katika nchi yetu vile inavyotakiwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikianza tu mifano michache kwa Wajumbe wengi ambao tupo humu ndani, tumepita njia ya Morogoro kufika hapa Dodoma. Katikati ya Morogoro na Dodoma nafikiri Wajumbe wengi wameona athari za mafuriko zilizotokea. Mfano mzuri ni Mto Mkondoa unao-flow kutoka Singida mpaka huko chini Morogoro, hapo katikati tunaona maeneo ya Kibaigwa wakazi wamepata madhara. Kuna reli ya kati eneo la Godegode, kila mwaka reli hii ya kati inatumia mamilioni ya pesa kurekebisaha na madhara ni nini? Ni kutokana na yale mafuriko yanayotokea katika Mto Mkondoa ambayo uharibu rasilimali hii muhimu ya nchi. Kwa hiyo, hela nyingi inatumika kugharamia hivyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano mwingine mzuri ni wale wananchi wanaoishi maeneo hayo, wanapata madhara makubwa. Wanapoteza mashamba yao, rasilimali zao nyingine zinaharibika, livelihoods zinakwisha, vyanzo vyao vya mapato pia vinaathirika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaanza lini kuchukulia umakini kwamba haya mafuriko tunayoyaona ni consequence ya kutokutunza mazingira kwa hali ya juu kwenye shughuli za kilimo au shughuli za mining, michanga inaingia kwenye mito, mito inakosa zile channel zake za asili, yanatapakaa maji all over the place. Mifano iko mingi hata kule Dar es Salaam, barabara ya Bagamoyo, maeneo ya Mbezi ni mafuriko maeneo ya Massana kila siku, kwa sababu ya miundombinu mibovu na mipango au mikakati ya kutunza hii mito haiko sawa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano wa tatu ni Uvuvi. Uvuvi ni sekta muhimu sana ambayo bahati mbaya haitiliwi mkazo. Unapofanya uvuvi haramu, mfano wa kutumia mabomu, unaharibu rasilimali ya ile bahari, mazalia ya samaki. Hata hivyo, tukumbuke kwanza kule baharini, bahari siyo tu kwa ajili ya shughuli za uvuvi, bahari yenyewe ndiyo kiini ambacho kina-influence hali ya hewa. Sasa hivi tunaimba climate change, climate change. Climate change vyanzo ni vingi, mojawapo pia ni uharibifu wa sehemu kama za bahari. Namba mbili, hii climate change tunayolia na mafuriko tunayoyaona impact yake inazidishwa na kutotunza hayo mazingira. Mfano halisi ni hizi floods tunazoziona na kadhalika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nikibaki hapo kwenye mabadiliko ya tabianchi, mazingira yanagusa karibu sekta nyingi, kwenye mifugo, kwenye kilimo, kwenye uvuvi, kwenye mining na kadhalika, ukiangalia hata work plans za Wizara mbalimbali au Bajeti hamna kipengele kinachoonyesha kwamba hizi sekta mabalimbali zitakabiliana vipi na mabadiliko ya tabianchi, hamna bajeti, hatuna sera ya climate change, tuna strategy tu. Kwa mfano, ukiangalia huu Mkutano uliokwisha wa Climate Change Forum wa Paris, walichokubaliana, mbona hatujakiwekeza sisi katika nchi yetu?
Kwa hiyo, nafikiri ni muhimu sana kuangalia issue za mazingira kwa upana wake na umuhimu wake katika nchi yetu na katika uchumi wa nchi yetu. Tusiangalie tu kwa narrow set kwamba ni usafi, mazingira si usafi bali mazingira yamebeba kila kitu katika kila sekta ya nchi hii. Tunasema viwanda, rasilimali mnazozitumia viwandani zinatoka kwenye hayo mazingira au hata ukiangalia afya ya jamii inayohusika ambayo watafanya kazi kwenye hivyo viwanda au shughuli mbalimbali za uchumi, wasipokuwa na afya ya mwili na akili ambayo inakuwa influenced na mazingira, huwezi kuwa na Taifa imara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, issues za mazingira zinagusa kila Mtanzania, zinagusa issue za economy, zinagusa issue za afya, zinagusa issue za elimu, zinagusa sekta mbalimbali na hata nchi imeiona hii, lakini katika karatasi. Policies au sera katika environment zipo tu kwenye paper work lakini hatuoni katika utekelezaji. Naishauri Serikali iangalie tena kwa upya, iende ikaji-analyse kwa sababu tunatakiwa tu-report back kwa nchi nyingine ambazo zimekubaliana nazo nini tunakifanya kwenye kutunza mazingira na pia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni hayo tu kwa sasa. Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nataka kuanza kutoa inputs zangu katika Wizara hii kwa kujiuliza: Je, ni mafaniko yapi tunayo katika Sekta ya Elimu, ukiangalia… okay, samahani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni inputs gani tunaziona katika Sekta ya Elimu? Matokeo gani tunayaona katika Sekta ya Elimu kwa kuangalia shughuli za kiuchumi au shughuli za huduma za maendeleo ya jamii? Je, uchumi wetu una-reflect elimu tuliyonayo? Au huduma za kijamii kama ni afya, Madaktari wanatuhudumia vile tunavyotakiwa kupata? Sekta nyingine kama za Utalii, Service Provisions, zikoje? Je, zina-reflect kiwango cha elimu tulichonacho?
Mheshimiwa Mwenyekiti, malalamiko ambayo yametolewa na Wajumbe ni mengi hata kwa Wizara nyingine zilizopita na hii yote ina-reflect level yetu ya elimu ikoje. Kwa hiyo, sitajikita sana katika kusema changamoto ni zipi za miundombinu, lakini changamoto ni zipi ukiziangalia katika outcome na jinsi ambavyo ina-affect elimu yetu kwa ujumla na uchumi wetu kwa ujumla? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia katika Sera ya Elimu yenyewe, katika kipengele cha muda wanafunzi wanaoanza shule, hii pia inaweza ikawa na outcome au ikaleta impact ambayo siyo sahihi. Watoto wadogo, miaka minne, mitano, mitatu, wanaamshwa saa 10.00 au 11.00 alfajiri, wamepumzika saa ngapi? Akili zikoje? Ukiangalia hata watoto wadogo wa Shule za Msingi Dar es Salaam, miundombinu hairuhusu wale watoto. Wanafika shuleni wamedumaa au hawana hizo akili, hawako creative. Kwa hiyo, chochote unachomfundisha yule mtoto hakiwezi kukaa, hiyo tayari ina impact katika siku za usoni. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia mitaala au curriculum zetu, ni masomo gani yanafundishwa? Kwa elimu ya sasa hivi, je, curriculum ipo sawa? Watoto wadogo wa primary school au nursery, content wanayofundishwa ni sawa? Watoto wanafundishwa mambo makubwa ambayo ni repetitive, ya kazi gani? Hii inaleta udumaivu au udumavu. Samahani sijui Kiswahili, hakiko vizuri sana, nayo ni reflection ya elimu yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia issue za mitihani ya primary au „O‟ Level, mwanafunzi au mtoto huyu anapewa one time chance, ambayo si sawa. Mtihani unafanya kwa siku moja mtoto wa Darasa la Saba, miaka yote saba inakuwa judged na siku moja. Hii lazima iwe reflected, haiko sawa. Au mtoto wa Form Four au Form Six, miaka yote hiyo minne au miwili aliyosoma inakuwa judged one time na chochote kinaweza kikatokea. Kwa hiyo, tunamnyima huyu mtoto nafasi au fursa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niguse kwenye issue ya Vyuo Vikuu na specialization. Tuna vyuo vya Serikali, naona hapa list inaonyesha vyuo 31. Ni chuo gani au vyuo hivi vikuu vime-specialize kwenye nini? Chuo Kikuu hakiwezi kuwa na faculties saba au nane. Hao wanaofundisha, wanaotoa huduma, hao Walimu wana qualities zinazotakiwa?
Kwa hiyo, lazima na hiyo nayo namshauri Mheshimiwa Waziri mhusika mwangalie specialization katika vyuo lazima iwe reflected inavyotakiwa na wataalamu wanaotakiwa wawepo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, issue nyingine ni miundombinu lakini kwenye njia ya ku-deliver elimu au kutoa mafunzo. Ni mbinu gani zinatumika kufundishia? Style tuliyonayo sasa hivi shuleni, hasa Shule za Serikali na hasa vijijini ni Mwalimu anaandika notes ubaoni na wanafunzi wanafanya kazi ya ku-copy. Kinachofuata ni ku-cram kile Mwalimu alichofundisha.
Sasa mtoto huyu anayefaulu, asilimia kubwa ni yule mwenye uwezo wa ku-cram halafu anakuja kutema baadaye kwenye exam. Hii nayo inakuwa reflected kwenye Vyuo Vikuu. Wanafunzi wanaokuja hawako creative, lakini tunaendelea kuwa na system za kukremisha. Sasa kama umejaliwa kukremisha ndiyo you have a better chance ya kufaulu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ni vizuri kujiuliza au kujitathmini, tutaendelea hivi mpaka lini? Tutaendelea kusema madarasa hayatoshi, Walimu hawatoshi, miundombinu hafifu lakini tunataka nini? Serikali kama Serikali tuna strategy gani ya kusema kwamba elimu yetu i-focus kwenye nini ili izae kitu gani? Kwa hiyo, ni lazima tujiulize: Je, ni vipaumbele vipi tulivyonavyo, kama hivyo vipaumbele vipo na tunajiwekea nini katika elimu? Au imekaaje kimkakati ku-reflect uchumi wetu na nini tunataka kukijenga katika nchi yetu? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, basi katika muktadha huo, naomba tujikite na tu-concentrate kuangalia kwamba elimu yetu ipo katika standard gani na tunataka ku-achieve nini na matokeo hayo ya elimu tunataka yaweje? Tu-focus kwenye impact au outcome ya mfumo mzima wa elimu tunataka uwaje. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni hayo tu kwa sasa. Ahsante.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Naibu Spika, malengo makuu (objectives) ni matatu badala ya manne. Lengo la nne lililotajwa kama ufuatiliaji si sawa, hii ni 4001 ya kufuatilia utendaji kazi ili kufuatilia malengo tajwa, page one.
Mheshimiwa Naibu Spika, maeneo ya kipaumbele kwa mwaka 2017/2018 kunakosekana the main priorities, page 18-22 ya hotuba ya Waziri. Maeneo tajwa ni 39, ni mengi mno kuweza kufanikisha.
Mheshimiwa Naibu Spika, the concept (dhima) ni kujenga uchumi wa viwanda ili kuchochea mageuzi ya uchumi na maendeleo ya watu. Hali halisi ya kiuchumi, je, tumefanikisha kwa kiasi gani dhana ya kilimo ni uti wa mgongo? Focus ya uchumi wa viwanda ni ipi? Ni rasilimali gani zinalengwa kwa aina gani ya viwanda? Kuna rasilimali watu inayolengwa maalum kwa aina gani za viwanda? Je, ni masoko gani yanayolengwa?
Mheshimiwa Naibu Spika, mpango unatakiwa kuainisha main strategies zitakazowezesha kukuza na kuimarisha uchumi wa nchi. Mfano, ni maeneo gani makuu matatu Serikali inatakiwa ku-focus into ili kusukuma maendeleo katika sekta nyingine?
Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru nitatoa maoni yangu na mapendekezo katika Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge. Kabla ya kutoa mapendekezo yangu nataka turejee katika Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara 63(2) kujikumbushia tu Waheshimiwa Wabunge. Sehemu hii inasema kwamba:- “Bunge litakuwa chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii”. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nimeamua kusema haya au kujikumbushia nini kinatuongoza katika nchi yetu kama Wabunge? Nina muda wa mwaka mmoja na zaidi hapa Bungeni, nikizingatia haya tuliyoambiwa, lakini ukiangalia mwenendo wetu nimeona kuna upungufu kwa jinsi ambavyo tunaishauri na kuifuatilia Serikali. Mheshimiwa Mwenyekiti, tunasimama hapa Mbunge mmoja mmoja tunatoa mapendekezo yetu kwa Wizara husika, tunatoa mapendekezo yetu kama Kamati husika lakini sisi tunaotoa hayo mapendekezo hatufuatilii utendaji, hakuna accountability upande wa pili. Waziri atakuja kujibu atasema sawa nimepokea au sawa hili sikubaliani nalo au hili nitalifanyia kazi lakini ukija mwaka unaofuata au Bunge linalofuata hatujui nini kimetekeleza au kama kweli kimetekelezeka. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano dhahiri, mwaka 2013 au 2014, kuliundwa Kamati Maalum ambayo ilikuwa inachunguza na kuleta mapendekezo juu ya hii migongano baina ya wakulima, wafugaji, wawekezaji na mambo ya ardhi. Kamati ile ilitoa mapendekezo mazuri sana kwa Serikali lakini huu ni mwaka 2016 bado tunaongelea lugha hiyo hiyo. Kamati zinatoa mapendekezo hayo hayo hatuoni accountability kutoka upande wa pili. Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano mwingine pia sisi ambao tulikuwa mtaani by then tulikuwa tunasikia kuhusu ESCROW, RICHMOND, Kamati zilitoa mapendekezo yake lakini sisi tuliotoka mtaani na sasa tumeingia Bungeni hatujui haya mapendekezo yaliishia wapi. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninachotaka kushauri, Kamati kama itaona inafaa waongeze katika mapendekezo yao kwamba Bunge linatakiwa liwe na special monitary and evaluation plan, mikakati ya kutathmini tunachokipendekeza kwa Serikali au tunachokishauri kwa Serikali je kinatekelezeka na kinatekelezeka kwa wakati gani. Hii itatusaidia kama Serikali yetu kuzipambanua hizi changamoto na ku-move forward.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niliuliza hapa na pale nikaambiwa wakati uliopita Bunge lilikuwa na kitengo cha kufuatilia ahadi za Serikali Bungeni, the government assurance unit. Sasa nataka kujua hiki kitengo kilikufa au kwa nini hakifanyi kazi kikatuambia ili tusiwe tunajirudiarudia kama Kamati au kwa Mbunge mmoja mmoja kushauri au kupendekeza mambo yale yale kila wakati. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, upande wa pili napenda kugusia kwenye mambo ya maadili kwa Kamati hii husika. Nimesoma booklet nikaona muundo wa Kamati, ina wajumbe 10 kutoka Chama Tawala na wajumbe sita (6) kutoka upande wa Upinzani. Sasa maadam hii Kamati ni special siyo kama Kamati nyingine inayoshughulikia maadili ya Wabunge, napendekeza ingekuwa ina 50-50 chance ili kuwe na uwazi au kusiwe na upendeleo wa aina yoyote hata na hao wajumbe wahusika wawe na mawazo mbadala. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine nilichokiona kwa Wabunge wenzetu waliopewa adhabu mbalimbali, evidence gani zilitumika? Hata vyombo vya habari, waandishi wetu wa habari wako hapa ndani, kukitokea tafrani humu ndani utaona upande wa Upinzani ndiyo unaoshutiwa kwamba wamefanya fujo. Hata hivyo, in every action there is a reaction yaani kwenye kila tukio lazima kuna sababu nyuma yake, lazima kuna mmoja…
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.