Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Ignas Aloyce Malocha (38 total)

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nikushukuru kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuungana na wenzangu katika kuchangia Wizara hii. Kabla ya yote niungane na wenzangu kumpongeza Mheshimiwa Waziri wa Nishati, ndugu yangu Profesa Muhongo, Naibu Waziri na Katibu wake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pongezi hizi siyo za unafiki, zinadhihirisha uwezo alionao, hasa kwa sisi ambao tulikuwamo katika awamu ile ya kwanza na awamu hii, tulikuwa tunamlilia arudi aokoe jahazi juu ya Wizara hii. Mwenyezi Mungu ameturudishia, ni haki yake kuwepo hapo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi sote tunatambua umuhimu wa nyenzo muhimu hii ya umeme kwamba, umeme ni nyenzo muhimu katika maendeleo. Umeme unaongeza uchumi, unaongeza ajira, unaboresha huduma mbalimbali, ni chanzo muhimu cha uchumi katika njia zote za uchumi; bila umeme hakuna viwanda, hakuna maendeleo, hakuna ustaarabu! Hivyo ni wajibu wa Serikali kuhakikisha umeme huo unamfikia kila Mtanzania mahali popote alipo, ili aweze kufaidika na kupata huduma zinazostahili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa masikitiko yangu makubwa kwa upande wa umeme wa REA. Tumekuwa na REA I, REA II na sasa hivi tunakwenda REA III, lakini ni jambo la ajabu sana Wilaya yangu ya Sumbawanga pamoja na ukubwa wote vijiji karibu 150, watu zaidi ya laki nne na nusu, hakuna hata kijiji kimoja chenye umeme! Sasa Mheshimiwa Waziri, kama wewe ndiy ungekuwa Mbunge, sijui ungejisikiaje na wananchi wako wangekuelewaje? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nataka kwanza mwelewe kwamba, wilaya yangu ina kanda mbili, kanda ya kwanza iko Ufipa Juu, unaanzia Sumbawanga kwenda Tunduma na ukanda wa pili unaanzia Stalike, kule tunapakana na Mheshimiwa Lupembe, mpaka huku tunapakana na ndugu yangu, Mheshimiwa Silinde. Sasa nianze na ukanda wa juu. Ukanda wa juu zipo kata 13 ambazo zinatakiwa kupitisha umeme, nimeona nitaje kata maana nikitaja vijiji ni vingi mno.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna Kata ya Msandamungano, Sandulula, Jangwani, Mpwapwa, Kaengesa, Kanda, Lyangalile, Mpui, Ikozi, Kalambanzite, Lusaka, Laela, Kasanzama, Myakula, Mlangalua; hizi ni kata za Ukanda wa Ufipa juu, lakini zipo Kata za Ukanda wa Ziwa Rukwa, maana kata yangu ina maeneo mawili tofauti, ndiyo maana mara nyingi nimekuwa nikilalamika jiografia ya hii Kata! Ukanda wa Ziwa Rukwa tunazo Kata 13 ambazo zina vijiji vingi; hakuna hata kata moja iliyopata umeme, ambayo ni Muze, Mto Wiza, Milepa, Ilemba, Kapenta, Kaoze, Kilya, Jamatundu, Kilangawana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, haya maeneo ni makubwa. Ninapotaja hizi kata, nataja kwa sababu ni kata, lakini maeneo mengine kata moja inaweza ikagawanyika kuwa kata tatu kwa ukubwa wa kata jinsi ulivyo, lakini unashangaa ni vigezo gani vinatumika kutopeleka umeme katika maeneo haya! Sijajua kwa nini Serikali, mara nyingi, imekuwa ikifanya Wilaya ya Sumbawanga Vijijini kuwa ni ya mwisho katika kupeleka huduma mbalimbali! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata suala la barabara tumekuwa karibu wa mwisho kuletewa barabara, sijui mlishatazama namna gani; kwa maana hiyo, lazima Waziri anieleze sababu za msingi za kutofikisha umeme katika maeneo hayo. Tena eneo hilo la ukanda wa chini ni eneo lenye uchumi mkubwa, jamani umeme unahitajika! Watu wa kule wana uchumi mkubwa, yapo maeneo mnapeleka umeme, nguzo zimesimama, watu hawataki kuingiza ndani ya nyumba kwa sababu hawana fedha! Sasa mnapeleka tu kama formality wakati umeme unatakiwa kujizungusha urudishe pesa! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa maeneo ninayosema haya ni maeneo ya watu wenye uchumi mzuri, ukipeleka umeme wataingiza umeme kwenye nyumba zao, wataufanyia shughuli za maendeleo, wataongeza uchumi wao, wataongeza uchumi wa Taifa; kwa nini hamtaki kufanya hivyo? Nataka unapokuja hapa unipe vigezo vinavyokufanya usipeleke umeme katika maeneo haya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie umeme tunaoutumia Mkoa wa Rukwa. Mkoa wa Rukwa wote tunatumia karibu megawatts tano kwa mkoa mzima na umeme huo mwingine tunaupata kutoka Zambia na mwingine unakuwa ni umeme wa generator. Ninachotaka kusema, tunavyo vyanzo vingi vya kuweza kuongeza umeme katika Mkoa wetu wa Rukwa. Kwa mfano, nikitaja umeme unaotokana na maji, Mto Nzovwe una maporomoko makubwa na ulishafanyiwa utafiti kwamba, unaweza kutoa megawatts nane ambazo zikiongezeka katika Mkoa wa Rukwa unaweza ukawa na megawatts nyingi zinazoweza kusambazwa na viwanda vikaweza kutekelezeka vizuri zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashangaa ni kwa nini hawataki kuutumia mto huo ambao ulishafanyiwa utafiti na haukauki na bahati nzuri Mkoa wetu wa Rukwa ni karibu kila mwaka una mvua. Kwa nini wasitumie maporomoko hayo ambayo yameshafanyiwa utafiti wa kutoa megawatts nane! Kwa hiyo, nataka Mheshimiwa Waziri aje anieleze, ni kwa nini hawataki kutumia njia nyingine ya kupata umeme katika Mkoa wetu wa Rukwa ambao gharama yake inakuwa ni ndogo kuliko hata umeme wa generator? Sijui wataalam wetu, nashindwa hata kuwaelewa! Tatizo hili ni kutozunguka, kutotembea! Yapo maeneo mlishayatenga, mnarudia rudia, maeneo mengine hamtaki kwenda! Mnazunguka, mnarudia maeneo yale yale! Sijui ni kwanini? Sisi sote ni Watanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ninalotaka kuzungumzia ni juu ya utafiti. Lazima nchi yetu ijielekeze kwenye utafiti katika mambo mbalimbali kwa sababu, yapo maeneo mengi yana rasirimali, lakini nchi hii haijagundua! Ndiyo maana hata juzi nimekuja kugundua Mtwara mmegundua gesi, mmegundua mafuta, lakini rasilimali hizo zipo maeneo mengi ila hamjaweka upendeleo wa kufanya utafiti.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka pia kuzungumzia juu ya Ziwa Rukwa. Ziwa Rukwa halina tofauti na Ziwa Albert la Uganda, jiografia ni ile ile na bahati nzuri nimeshafika, lakini nataka anieleze ni utafiti gani umeshafanyika wa Ziwa Rukwa ili kuangalia kuna kitu gani na mkishajua maana yake mtaweza kulitunza. Ndiyo maana mmelitelekeza, hamna habari nalo, suala la mazingira hamna habari, lakini naamini upo uchumi mkubwa katika eneo lile. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kuzungumzia suala lingine la utafiti, kuna shamba ambalo nimekuwa nikizungumzia mara kwa mara, Shamba la Malonje. Yule Mtaalam wa Kenya alilizungukia lile shamba akasema, lile shamba, 1/8 ya lile shamba lina madini ya kopa, lakini watafiti wetu hawajakwenda kuangalia ni kitu gani kinafanyika! Matokeo yake mwekezaji akija anang‟ang‟ania kwa sababu, anajua pale kuna faida kwa baadaye. Kwa nini, watafiti hamtaki kufanya kazi inayostahili, ili kuweza kuboresha nchi yetu? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine nataka tu kusisitiza kwamba, Mheshimiwa Waziri sisi sote tunafahamu uwezo wake na msukumo wake. Siwezi kuunga mkono kwa sababu, wananchi watanishangaa! Huna umeme hata kijiji kimoja, vijiji 150, halafu leo hii unasema unaunga mkono, watakushangaa! Mpaka nipate maelezo ya Mheshimiwa ndipo naweza kuunga mkono hoja, lakini kwa sasa siwezi kuunga mkono hoja wananchi watanishangaa, kwanza ni aibu kubwa, ni aibu kubwa!
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nasisitiza Mheshimiwa Waziri anieleze ni kwa namna gani atapeleka umeme katika Wilaya ya Sumbawanga Vijijini? Mkija Sumbawanga Mjini mnadhani ndio Sumbawanga Vijijini, hata Kijiji kimoja! Ni aibu kubwa sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza napenda kuchangia kuhusu shamba la Malonje. Ni lini Serikali itamaliza mgogoro wa shamba la Malonje kati ya wananchi na mwekezaji? Mgogoro huu umekuwa ni wa muda mrefu, wananchi wameteseka kwa kukosa ardhi ya kulima. Naomba Mheshimiwa Waziri atoe maelezo kuna maeneo kadhaa yenye migogoro Waziri huyu ameimaliza huu unamshindaje au kuna mikono ya wakubwa? Naomba maelezo kwani wananchi wamechoka na ahadi ambazo zimekuwa zikitolewa na Serikali. Naomba Serikali imalize haraka mgogoro huu kuepusha shari inayoweza kutokea. Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuchangia hotuba hii kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na mgogoro katika Hifadhi ya Akiba ya Uwanda kutokana na ongezeko kubwa la watu waliopo katika vijiji vinavyozunguka hifadhi hiyo kwa sababu zifuatazo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, hifadhi hiyo mipaka yake kutoeleweka, askari wanyama pori kutoza wafugaji fedha ili walishe mifugo yao ndani ya hifadhi; kukodisha ardhi iliyomo ndani ya hifadhi ili wakulima waweze kulima; askari wa wanyama pori kuruhusu wananchi wasio na uwezo wa fedha walime mazao yao na mazao yakishakomaa hutumia ujeuri wa kupora mazao yao wanayauza na kuingiza fedha hizo mifukoni mwao; kuwanyang‟anya pikipiki, baiskeli, majembe ya plau na majembe ya mkono, fyekeo, panga na kadhalika, jambo ambalo linahatarisha amani. Kama Serikali haitachukua hatua haraka ipo siku yatatokea mapigano kati ya askari hao na wananchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hifadhi hiyo kwa sasa haina sifa, ni hasara tu kwa Serikali, inawanufaisha Askari tu. Hivyo kutokana na uhaba wa ardhi, nashauri, hifadhi hiyo ipunguzwe au kufutwa kabisa, wananchi wagawiwe ardhi hiyo waendeleze uchumi wao kwa kulima.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Waziri anieleze nini faida ya hifadhi hiyo kwa Serikali na kwa wananchi hadi sasa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri hifadhi ipunguzwe kama siyo kufutwa kabisa. Mipaka ijulikane, Serikali itoe misaada ya kuwajengea shule, zahanati na kuwapatia madawati ili kuwatia moyo wananchi. Pia nashauri Mheshimiwa Waziri atembelee eneo hili la hifadhi ili ajifunze na baadaye aweze kutoa uamuzi sahihi kuliko kusikiliza kwa mbali. Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa utendaji wake wa kazi. Mwenyezi Mungu aendelee, kumpatia afya njema, aendelea kuimarisha Tanzania yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza Mheshimwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu Ndugu Nyamhanga na Watendaji wote wanaofanya kazi katika Wizara hii, hongereni sana na endeleeni kuchapa kazi tupo pamoja nanyi na kazi yenu Watanzania wanatambua uwezo wenu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru Mheshimiwa Waziri na Katibu wa Wizara hii Ndugu, Nyamhanga, kwa kusikiliza kilio cha wananchi wa Jimbo langu la Kwela, kilio cha muda mrefu, juu ya barabara sugu na yenye gharama kubwa ambayo Halmashauri haina uwezo nayo kwa maombi yangu. Kwanza ulitupatia milioni 431 na bado barabara hiyo ichukuliwe na TANROAD. Nashukuru barabara hiyo leo imekwishachukuliwa na TANROAD. Ahsante sana na Mwenyezi Mungu awabariki katika kazi zenu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru vilevile kwa kuanza utaratibu wa ujenzi wa daraja la Mto Momba. Daraja ambalo ni kiungo kikubwa kwa barabara ya Kibaoni - Kulyamatundu, Kamsamba, Mlowo, tunaomba kasi iendelee katika kuanza kulijenga Daraja hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba Serikali iharakishe kufanya usanifu katika barabara ya Kibaoni, Kilyamatundu, Kamsamba, Mlowo. Barabara hii ni muhimu sana kiuchumi kutokana uzalishaji wa mazao ya mpunga, mbaazi, matunda mbalimbali, samaki na mifugo. Tunaomba barabara hii itengenezwe haraka kwa kiwango cha lami ili kusaidia wananchi katika ukanda huo wa bonde la Ziwa Rukwa.

Maombi ya fedha kwa barabara ambazo Halmashauri haina uwezo nazo ambazo ni barabara ya Miangalua - Chombe - Kipeta, barabara ya Mawenzusi - Msia, barabara ya Mlimani inayounganisha Bonde la Rukwa na Sumbawanga kilomita 47. Pia maombi ya fedha ili kutengeneza daraja la Kaengesa, daraja la Laela kwenda Kituo cha Afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuchangia Wizara hii, kwanza kwa kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri na watendaji wote wa Wizara hii kwa uwajibikaji wao mzuri, hongereni sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja yangu ni ukosefu wa magari ya wagonjwa katika Jimbo langu la Kwela na hasa kituo cha afya Milepa, kituo ambacho kiko mbali na huduma na kiko katika mazingira magumu na kinaongoza kwa vifo vya akina mama wajawazito na watoto. Naomba kujua kwa nini Serikali haitaki kupeleka gari, kuna nini? Tunajua wazi yapo maeneo yanagawiwa magari karibu vituo vyote vya afya walivyonavyo. Mheshimiwa Waziri mnatumia vigezo gani? Nimesema tatizo la gari katika kituo hiki toka mwaka 2012 bado sijafanikiwa.

Naomba nijibiwe hii siyo haki, baadae natarajia, kutoa idadi ya vifo vya akina mama na watoto waliopoteza maisha yao kwa kungojelea gari la wagonjwa hadi kufa kwa kukosa msaada wa gari la wagonjwa.
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Kwanza kabisa namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa uhai na uzima kwa siku ya leo. Pia nampongeza Rais wetu, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa utendaji wake wa kazi. Naomba ndoto yake ifike mahali ifikie mwisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile nawashukuru na kuwapongeza Mawaziri wote; ndugu yangu Mheshimiwa Jafo; Naibu Mawaziri, ndugu yangu Mheshimiwa Kandege, Mheshimiwa Kakunda na Mheshimiwa Mkuchika. Nawapongeza kwa sababu kubwa, kwanza kwa hekima zao, busara, uwajibikaji, unyenyekevu, uzalendo na usikivu. Tunachoweza kuomba kwa Mwenyezi Mungu, aendelee kuwapa afya njema ili waendelee kulitumikia Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naanza na utawala bora. Utawala bora ni pamoja na kusogeza huduma karibu na wananchi. Ili wananchi waweze kupata huduma bora, ni lazima wawe karibu na huduma. Nazungumza jambo hili kutokana na mazingira ya Jimbo langu. Jimbo langu lina jiografia mbaya na ni kubwa na limekaa vibaya na linawatesa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukimchukua mwananchi aliyepo kule Ilambo ili afike Makao Makuu apate huduma, anatumia karibu nauli ya Sh.50,000/=; kwenda na kurudi Sh.100,000/=, nauli ya kutoka Sumbawanga mpaka hapa Dodoma. Sasa akiwa na mgonjwa, kukodi gari, lazima awe na shilingi milioni moja; au akiwa na kesi, anahitaji mashahidi watano, lazima awe na Sh.500,000. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili linawatesa wananchi na sijajua ni kwa nini? Kwa sababau tumepeleka maombi mara kadhaa. Bahati nzuri wapo mashuhuda mbalimbali ambao wameshuhudia jambo hili na ukubwa wake, ambao nataka niwataje leo hii. Shuhuda wa kwanza ni yeye mwenyewe Mheshimiwa Mkuchika, alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, anayafahamu mazingira vizuri mno. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, shuhuda wa pili ni Mheshimiwa Ole Njoolay, alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. Shuhuda wa tatu ni ndugu yangu Mheshimiwa Stella Manyanya, alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na jitihada alizianza yeye mwenyewe japokuwa hazijafanikiwa. Shuhuda wa nne alikuwa Zolote Stephen Zolote. Shuhuda wa tano ni Waziri Mkuu, ndugu yangu Mheshimiwa Majaliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nampongeza sana, juzi alifika mpaka Mto Wisa mahali ambapo kuna changamoto kubwa sana. Shuhuda wa sita ni Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana; yeye tena alitamka kabisa kwamba Jimbo hili lazima ligawanyike, Wilaya lazima ipatikane na Halmashauri lazima zipatikane. Huyo ni shuhuda wa sita. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, shuhuda wa saba ni Waziri wa Uchukuzi, ndugu yangu Mbalawa, juzi amepita kule ameliona Jimbo jinsi lilivyo. Shuhuda wa nane ni Makamu wa Rais, Mheshimiwa Samia Suluhu, alifika kule wakati wa kampeni, akashangaa kwamba hivi kweli eneo kama hili linakuwa na changamoto namna hii, linatengwa kiasi hiki?

Mheshimiwa Mwenyekiti, shuhuda wa tisa ni Waziri wa Mambo ya Ndani, ndugu yangu Mheshimiwa Mwigulu, wakati wa kampeni alikuja kule akashangaa eneo jinsi lilivyo. Shuhuda wa kumi ni Waziri wa TAMISEMI ndugu yangu Mheshimiwa Jafo. Alikuja akakaa na Mkuu wa Mkoa mpaka akaanza kumpa jiografia, bahati mbaya hakuzunguka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, shuhuda wa 11 ni Naibu Waziri, ndugu yangu Mheshimiwa Kandege, anajua hali halisi jinsi ilivyo. Shuhuda wa 12 ni Wabunge wote wa Mkoa wa Rukwa na Wabunge majirani wa Mkoa wa Songwe na Mkoa wa Mbeya na baadhi ya Madiwani ambao wamefika katika maeneo yale. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, shuhuda mwingine wa 13 ni Naibu Katibu Mkuu wa Elimu, ndugu yangu Zunda, alikuwa Afisa Tawala juzi juzi kwetu. Shuhuda wa 14 ni ndugu yangu Katibu Mkuu Iyombe, alikuwa Meneja wa TANROAD Mkoa wa Rukwa. Anayafahamu mazingira vizuri mno. Shuhuda wa 15 ni Waziri Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa Warioba, alishawahi kufika maeneo yale. Alishangaa sana maeneo yale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, shuhuda wa 16 ni Waziri Mstaafu, ndugu yangu Pinda na alitamka hata hapa Bungeni kwamba kwa kweli Jimbo lile ni kubwa na jiografia ni mbaya. Shuhuda wa 17 ni wengine wengi Watendaji wa Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa jamani, hata kama Serikali imesimamisha matumizi, wakati mwingine Rais wetu hamumwelezi hali halisi. Mheshimiwa Rais huyu ana huruma kubwa mno. Tunaona maeneo mengi anavyofika anatetea wanyonge. Angepata hali halisi, nami naomba Mwenyezi Mungu, huyu mtu siku moja afike kwenye Jimbo langu, atatamka pale pale kwa jinsi ninavyomfahamu Mheshimiwa Rais huyu kwa huruma yake, atatamka siku ile ile. Ila wana- by pass hawampii information hali halisi ya mateso ya wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli jambo hili linaumiza wananchi na bahati nzuri walio wengi najua wengi wanalijua Jimbo langu. Inaumiza sana hasa wananchi wangu wanashindwa kupata huduma sahihi. Hii maana yake nini? Naomba Mheshimiwa Jafo jambo hili alitolee ufafanuzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo nataka kuzungumza ni suala la afya. Kwanza naishukuru Serikali, juzi juzi wametuambia wametutengea Sh.1,500,000,000/= kwa ajili ya kujenga Hospitali ya Wilaya, tunashukuru sana, lakini vilevile walitupa Sh.400,000,000/= kwa ajili ya kupanua Kituo cha Afya cha Milepa, tunashukuru na kinaenda vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba upanuzi wa vituo vingine vya afya kama Kituo cha pale Nkuhi; Naibu Waziri, ndugu yangu Mheshimiwa Kandege alienda pale akakutana na Watendaji na wananchi wa pale Nkuhi na akasema atalishughulikia. Naomba sasa jambo hili ndugu yangu Mheshimiwa Kandege, wananchi wa Nkuhi wanasubiri awasaidie, kile kituo kiingie kwenye upanuzi na vilevile Kituo cha Ilemba. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vituo vingine ambavyo vinaendelea katika kumalizika katika hatua mbalimbali ni Muze, Kahoze, Kipeta na Kalambazito. Vilevile tunazo zahanati ambazo zilishafika katika hatua mbalimbali. Zahanati 21 zinahitaji tu kupewa fedha ili ziweze kumalizika na zianze kutoa huduma kwa wananchi. (Kicheko/ Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ninalotaka kuzungumzia ni utaratibu wa upatikanaji watumishi katika Vituo vya Afya wa kada ya ulinzi, dobi na wapishi. Bado na lenyewe hili ni changamoto, halijulikani vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine nizungumzie kuhusu suala la elimu. Kwanza tunashukuru Serikali yetu kwa elimu bure, lakini vilevile zipo changamoto ukiacha Walimu wa Sayansi; na juzi nimepita Lahela pale wananchi wamelalamikia shule yao ile ya Uchile, hawana Walimu wa masomo ya sayansi, lakini vile vile zipo shule kadhaa ambazo zimeanzishwa na wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hilo nataka nilizungumze, hizi shule mpya ambazo zinaanzishwa na wananchi, wanazianzisha kwa mahitaji ya watoto wao ambao wakati mwingine shule nyingine ziko mbali au kuna changamoto ya daraja wanaogopa watoto wao wasije wakapata madhara? Wanaamua wao wenyewe kujichangisha nguvu kazi kujenga shule mpaka wanafikia kujenga madarasa manne, ofisi, madawati, lakini changamoto ni namna ya kujisajili. Sijajua hapa kuna jambo gani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi hawa wamejitolea wenyewe na sheria inasema shule mpya ya wananchi waliojitolea wenyewe; japokuwa tunapasha kuliangalia upya. Wananchi hawa wengi watoto wao watakosa elimu kwa sababu ni wachache wanaoweza kujitoa. Lenyewe hili nilitaka mliangalie vizuri. Pia shule yangu ya pale Kirando ambayo wananchi walishajitolea wakajenga, iko vizuri; na Shule ya kule Nhungwe, shule ya kule Nkuhi na Shule ya Mahenje kule Milepa Kinamo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine naiomba Serikali ijaribu kuangalia fedha za ujenzi wa madaraja, nyumba za Walimu na Vyuo ambavyo zinasimamiwa na elimu. Nashauri fedha hizi ziende TAMISEMI. Wale wabaki na shughuli ya kusimamia taaluma. Ziende TAMISEMI waweze kusimamia fedha hizi. Kwa hiyo, naishauri Serikali iweze kuliangalia jambo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni la barabara. Kwanza naishukuru Serikali ya Chama cha Mapinduzi, namshukuru Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Magufuli, alipokuwa Waziri ni mara kadhaa nilikuwa nikimwomba juu ya fedha za kujenga daraja la Mto Momba na alikuwa akiniahidi. Nashukuru kwamba baada ya kuwa Rais, katika jambo ambalo alikuwa na kumbukumbu nalo ni kutoa fedha za ujenzi wa daraja la Mto Momba, ametupa shilingi bilioni 17.8 na daraja limeshaanza kujengwa, tunatarajia mwezi wa Saba litamalizika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba baada ya kumalizika daraja hilo, Serikali ianze sasa hatua nyingine za upembuzi yakinifu ya kuunganisha barabara kwa ajili ya lami kwa maana ya kutoka Kibaoni kuja Kilyamatundu kuungana na wenzetu wa Songwe kwa maana ya kutokea Mloo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ile bado ina changamoto kubwa, ina madaraja mengi na ni eneo ambalo lina uzalishaji wa hali ya juu; mpunga, mahindi, karanga, mtama na kadhalika. Ile barabara ikikamilika, ndilo eneo ambalo tumetarajia hata viwanda vyenyewe vinaweza vikapatikana katika eneo lile kwa sababu mpunga unalimwa kwa wingi. Tunakosa kutangaza…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Kwanza kabisa namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa uhai na uzima kwa siku ya leo. Pia nampongeza Rais wetu, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa utendaji wake wa kazi. Naomba ndoto yake ifike mahali ifikie mwisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile nawashukuru na kuwapongeza Mawaziri wote; ndugu yangu Mheshimiwa Jafo; Naibu Mawaziri, ndugu yangu Mheshimiwa Kandege, Mheshimiwa Kakunda na Mheshimiwa Mkuchika. Nawapongeza kwa sababu kubwa, kwanza kwa hekima zao, busara, uwajibikaji, unyenyekevu, uzalendo na usikivu. Tunachoweza kuomba kwa Mwenyezi Mungu, aendelee kuwapa afya njema ili waendelee kulitumikia Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naanza na utawala bora. Utawala bora ni pamoja na kusogeza huduma karibu na wananchi. Ili wananchi waweze kupata huduma bora, ni lazima wawe karibu na huduma. Nazungumza jambo hili kutokana na mazingira ya Jimbo langu. Jimbo langu lina jiografia mbaya na ni kubwa na limekaa vibaya na linawatesa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukimchukua mwananchi aliyepo kule Ilambo ili afike Makao Makuu apate huduma, anatumia karibu nauli ya Sh.50,000/=; kwenda na kurudi Sh.100,000/=, nauli ya kutoka Sumbawanga mpaka hapa Dodoma. Sasa akiwa na mgonjwa, kukodi gari, lazima awe na shilingi milioni moja; au akiwa na kesi, anahitaji mashahidi watano, lazima awe na Sh.500,000. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili linawatesa wananchi na sijajua ni kwa nini? Kwa sababau tumepeleka maombi mara kadhaa. Bahati nzuri wapo mashuhuda mbalimbali ambao wameshuhudia jambo hili na ukubwa wake, ambao nataka niwataje leo hii. Shuhuda wa kwanza ni yeye mwenyewe Mheshimiwa Mkuchika, alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, anayafahamu mazingira vizuri mno. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, shuhuda wa pili ni Mheshimiwa Ole Njoolay, alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. Shuhuda wa tatu ni ndugu yangu Mheshimiwa Stella Manyanya, alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na jitihada alizianza yeye mwenyewe japokuwa hazijafanikiwa. Shuhuda wa nne alikuwa Zolote Stephen Zolote. Shuhuda wa tano ni Waziri Mkuu, ndugu yangu Mheshimiwa Majaliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nampongeza sana, juzi alifika mpaka Mto Wisa mahali ambapo kuna changamoto kubwa sana. Shuhuda wa sita ni Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana; yeye tena alitamka kabisa kwamba Jimbo hili lazima ligawanyike, Wilaya lazima ipatikane na Halmashauri lazima zipatikane. Huyo ni shuhuda wa sita. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, shuhuda wa saba ni Waziri wa Uchukuzi, ndugu yangu Mbalawa, juzi amepita kule ameliona Jimbo jinsi lilivyo. Shuhuda wa nane ni Makamu wa Rais, Mheshimiwa Samia Suluhu, alifika kule wakati wa kampeni, akashangaa kwamba hivi kweli eneo kama hili linakuwa na changamoto namna hii, linatengwa kiasi hiki?

Mheshimiwa Mwenyekiti, shuhuda wa tisa ni Waziri wa Mambo ya Ndani, ndugu yangu Mheshimiwa Mwigulu, wakati wa kampeni alikuja kule akashangaa eneo jinsi lilivyo. Shuhuda wa kumi ni Waziri wa TAMISEMI ndugu yangu Mheshimiwa Jafo. Alikuja akakaa na Mkuu wa Mkoa mpaka akaanza kumpa jiografia, bahati mbaya hakuzunguka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, shuhuda wa 11 ni Naibu Waziri, ndugu yangu Mheshimiwa Kandege, anajua hali halisi jinsi ilivyo. Shuhuda wa 12 ni Wabunge wote wa Mkoa wa Rukwa na Wabunge majirani wa Mkoa wa Songwe na Mkoa wa Mbeya na baadhi ya Madiwani ambao wamefika katika maeneo yale. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, shuhuda mwingine wa 13 ni Naibu Katibu Mkuu wa Elimu, ndugu yangu Zunda, alikuwa Afisa Tawala juzi juzi kwetu. Shuhuda wa 14 ni ndugu yangu Katibu Mkuu Iyombe, alikuwa Meneja wa TANROAD Mkoa wa Rukwa. Anayafahamu mazingira vizuri mno. Shuhuda wa 15 ni Waziri Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa Warioba, alishawahi kufika maeneo yale. Alishangaa sana maeneo yale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, shuhuda wa 16 ni Waziri Mstaafu, ndugu yangu Pinda na alitamka hata hapa Bungeni kwamba kwa kweli Jimbo lile ni kubwa na jiografia ni mbaya. Shuhuda wa 17 ni wengine wengi Watendaji wa Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa jamani, hata kama Serikali imesimamisha matumizi, wakati mwingine Rais wetu hamumwelezi hali halisi. Mheshimiwa Rais huyu ana huruma kubwa mno. Tunaona maeneo mengi anavyofika anatetea wanyonge. Angepata hali halisi, nami naomba Mwenyezi Mungu, huyu mtu siku moja afike kwenye Jimbo langu, atatamka pale pale kwa jinsi ninavyomfahamu Mheshimiwa Rais huyu kwa huruma yake, atatamka siku ile ile. Ila wana- by pass hawampii information hali halisi ya mateso ya wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli jambo hili linaumiza wananchi na bahati nzuri walio wengi najua wengi wanalijua Jimbo langu. Inaumiza sana hasa wananchi wangu wanashindwa kupata huduma sahihi. Hii maana yake nini? Naomba Mheshimiwa Jafo jambo hili alitolee ufafanuzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo nataka kuzungumza ni suala la afya. Kwanza naishukuru Serikali, juzi juzi wametuambia wametutengea Sh.1,500,000,000/= kwa ajili ya kujenga Hospitali ya Wilaya, tunashukuru sana, lakini vilevile walitupa Sh.400,000,000/= kwa ajili ya kupanua Kituo cha Afya cha Milepa, tunashukuru na kinaenda vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba upanuzi wa vituo vingine vya afya kama Kituo cha pale Nkuhi; Naibu Waziri, ndugu yangu Mheshimiwa Kandege alienda pale akakutana na Watendaji na wananchi wa pale Nkuhi na akasema atalishughulikia. Naomba sasa jambo hili ndugu yangu Mheshimiwa Kandege, wananchi wa Nkuhi wanasubiri awasaidie, kile kituo kiingie kwenye upanuzi na vilevile Kituo cha Ilemba. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vituo vingine ambavyo vinaendelea katika kumalizika katika hatua mbalimbali ni Muze, Kahoze, Kipeta na Kalambazito. Vilevile tunazo zahanati ambazo zilishafika katika hatua mbalimbali. Zahanati 21 zinahitaji tu kupewa fedha ili ziweze kumalizika na zianze kutoa huduma kwa wananchi. (Kicheko/ Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ninalotaka kuzungumzia ni utaratibu wa upatikanaji watumishi katika Vituo vya Afya wa kada ya ulinzi, dobi na wapishi. Bado na lenyewe hili ni changamoto, halijulikani vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine nizungumzie kuhusu suala la elimu. Kwanza tunashukuru Serikali yetu kwa elimu bure, lakini vilevile zipo changamoto ukiacha Walimu wa Sayansi; na juzi nimepita Lahela pale wananchi wamelalamikia shule yao ile ya Uchile, hawana Walimu wa masomo ya sayansi, lakini vile vile zipo shule kadhaa ambazo zimeanzishwa na wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hilo nataka nilizungumze, hizi shule mpya ambazo zinaanzishwa na wananchi, wanazianzisha kwa mahitaji ya watoto wao ambao wakati mwingine shule nyingine ziko mbali au kuna changamoto ya daraja wanaogopa watoto wao wasije wakapata madhara? Wanaamua wao wenyewe kujichangisha nguvu kazi kujenga shule mpaka wanafikia kujenga madarasa manne, ofisi, madawati, lakini changamoto ni namna ya kujisajili. Sijajua hapa kuna jambo gani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi hawa wamejitolea wenyewe na sheria inasema shule mpya ya wananchi waliojitolea wenyewe; japokuwa tunapasha kuliangalia upya. Wananchi hawa wengi watoto wao watakosa elimu kwa sababu ni wachache wanaoweza kujitoa. Lenyewe hili nilitaka mliangalie vizuri. Pia shule yangu ya pale Kirando ambayo wananchi walishajitolea wakajenga, iko vizuri; na Shule ya kule Nhungwe, shule ya kule Nkuhi na Shule ya Mahenje kule Milepa Kinamo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine naiomba Serikali ijaribu kuangalia fedha za ujenzi wa madaraja, nyumba za Walimu na Vyuo ambavyo zinasimamiwa na elimu. Nashauri fedha hizi ziende TAMISEMI. Wale wabaki na shughuli ya kusimamia taaluma. Ziende TAMISEMI waweze kusimamia fedha hizi. Kwa hiyo, naishauri Serikali iweze kuliangalia jambo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni la barabara. Kwanza naishukuru Serikali ya Chama cha Mapinduzi, namshukuru Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Magufuli, alipokuwa Waziri ni mara kadhaa nilikuwa nikimwomba juu ya fedha za kujenga daraja la Mto Momba na alikuwa akiniahidi. Nashukuru kwamba baada ya kuwa Rais, katika jambo ambalo alikuwa na kumbukumbu nalo ni kutoa fedha za ujenzi wa daraja la Mto Momba, ametupa shilingi bilioni 17.8 na daraja limeshaanza kujengwa, tunatarajia mwezi wa Saba litamalizika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba baada ya kumalizika daraja hilo, Serikali ianze sasa hatua nyingine za upembuzi yakinifu ya kuunganisha barabara kwa ajili ya lami kwa maana ya kutoka Kibaoni kuja Kilyamatundu kuungana na wenzetu wa Songwe kwa maana ya kutokea Mloo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ile bado ina changamoto kubwa, ina madaraja mengi na ni eneo ambalo lina uzalishaji wa hali ya juu; mpunga, mahindi, karanga, mtama na kadhalika. Ile barabara ikikamilika, ndilo eneo ambalo tumetarajia hata viwanda vyenyewe vinaweza vikapatikana katika eneo lile kwa sababu mpunga unalimwa kwa wingi. Tunakosa kutangaza…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Madini
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuchangia Wizara hii, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujua ni lini gesi ya helium iliyogunduliwa katika Ziwa Rukwa itaanza kuchimbwa. Tunaambiwa gesi hiyo ni adimu sana duniani na ina thamani kubwa. Ni sababu zipi zinatufanya tuchelewe kuanza kuichimba?

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja, ahsante.
Mapendekezo ya Mpango wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali katika Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue fursa hii kukushukuru kwa kunipa nafasi, lakini pia nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuingia tena kwa mara ya pili katika mjengo huu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nawashukuru sana Wananchi wa Jimbo la Kwela kwa kuniwezesha, kwa kuniamini kunirudisha tena ili niweze kuwatumikia na wananchi hao walisimama kidete sana japo kuwa kulikuwa na mizengwe mingi sana lakini wananchi waliweza kusimama na hatimaye kuniwezesha kurudi katika ukumbi huu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Magufuli, kwa kasi hii aliyoianza ya kusimamia wananchi. Ni kasi ya hali ya juu na mimi nawapongeza wale ambao wanatambua kwamba kasi ile ndiyo iliyokuwa inahitajika katika nchi hii kwa sasa. Nawapongeza na Mawaziri wote ambao wametambua hivyo na wameanza na kasi hiyo, ninachowaomba Mawaziri wote mtambue kwamba mna watu wenu mpaka huko chini waimarisheni, wabadilisheni kifikra ili waendane na kasi hii ya Mheshimiwa Magufuli. (Makofi)
Kwa sababu Mheshimiwa Magufuli hawezi kufanya kazi peke yake bila sisi wote kujibadili kufanana na yeye, atachoka lazima tumsaidie na kumsaidia ni kuweka mtandao wa kasi kuanzia ngazi ya juu mpaka kule chini. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niungane na wenzangu katika kuchangia Mpango wa Maendeleo 2015/2016. Sisi tunatambua kwamba mpango huu wa maendeleo umelenga katika kukuza uchumi, katika kuhakikisha wananchi wanaondokana na umaskini, katika kukuza pato la Taifa. Hata hivyo, nataka nichangie kwa upande wa kilimo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatambua sisi wote kwamba nchi yetu sehemu kubwa ya wananchi wanategemea kilimo na katika kilimo, nataka nizungumzie jambo moja, lazima tujiridhishe hivi Watanzania wote waliopo mijini na vijijini wote wana ardhi ya kutosha kuwaendeleza? Hilo ni la kwanza kujiuliza, na mimi nasema baadhi ya maeneo yanawezekana yanatosha lakini maeneo mengi bado ni tatizo. Ni tatizo kwa sababu tumeachia watu wachache wameatamia maeneo makubwa, Serikali inazungumza kila siku haichukui hatua. Sijaona ni kwa sababu gani Serikali inachelea kuchukua uamuzi wa haraka, hii haitaji hata kusubiri. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni mara nyingi nimekuwa nikisimama hapa nikitetea wananchi wa Jimbo la Kwela kuhusu shamba la Malonje nimelizungumza kadha wa kadha hatimaye hata kwenye uchaguzi imeniletea mpambano mkubwa sana lakini Mwenyezi Mungu akisimama hakuna ubishi ndiyo maana niko leo hapa. Wananchi wa Jimbo la Kwela nitaendelea kuwatetea lazima shamba hilo lirudishwe mikononi mwa wananchi. Namwomba Mheshimiwa Waziri kwa sababu wewe Mwenyewe umefika mara ya mwisho ukasema mimi nitakuwa mtu wa mwisho kuzungumzia suala la ardhi hii ya shamba hili la Malonje naomba utimize ahadi yako wananchi wale warejeshewe lile shamba. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo lingine katika upande wa ardhi na mimi nataka niishauri Serikali. Serikali ni kweli ilitenga Mapori ya Akiba. Unaposema mapori ya akiba lazima uende na pande zote mbili, mapori ya akiba aidha kwa wanyama lakini mapori ya akiba kwa binadamu, tusiende upande mmoja. Wakati mapori yale yametengwa baadhi ya wananchi walikuwa hawajaongezeka lakini sasa hivi watu wameongezeka. Unaita pori la akiba lakini wananchi wananyanyasika hawana kwa kulima, pori hilo halina mnyama hata mmoja hata ndege mmoja, Jamani huu ni ubinadamu? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nazungumzia Pori la Uwanda Game Reserve. Linatesa wananchi isivyo kawaida na halina faida yoyote kwa Serikali na nashukuru Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii nimeongea na wewe, nimekusimulia kwa kirefu sana na nikakuomba ufike, inawezekana maneno haya ninayozungumza usiyaamini, basi ufike ukaone.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wanakatiza mle kwenye lile pori la akiba, wananyang‟anywa majembe, wananyang‟anywa panga zao, wananyang‟anywa fyekeo, pikipiki, wanapigwa wana nyanyasika, wakati pori lenyewe halina mnyama hata mmoja. Jamani tumefika wapi hapo? Haya mambo mengine ni ya kuchukua hatua za haraka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ili uamini, maana mara nyingine mnachukulia sisi kama ni wanasiasa uende, namwomba Waziri wa Maliasili afike eneo lile. Hata hivyo, nikupongeze kwa sababu nilipokueleza ulitoa amri ya wananchi kurejeshewa vifaa vile walivyokuwa wamenyang‟anywa, nakupongeza katika hilo na naomba uendelee katika kutatua tatizo hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni umeme, tunatambua kabisa maendeleo hayawezi kuja bila umeme, lakini nitoe masikitiko kidogo katika Jimbo langu au Wilaya yangu ya Sumbawanga Vijinini, pamoja na Wilaya hii kuwa ya siku nyingi, pamoja na jitihada zote za Serikali, Jimbo langu halina umeme hata kijiji kimoja. Vijiji 114, Kata 27, watu zaidi ya 450,000, halina hata kijiji kimoja chenye umeme.
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Wakati mwingine Serikali inaweza ikatutambua sisi viongozi, tunaotokana na Chama cha Mapinduzi kama vile tunaipinga Serikali hapana, ni masikitiko ya kuona wananchi wanahangaika, hivi Serikali hii inaendeshwa kwa upendeleo?
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, natambua Muhongo ni mchapakazi na nimeongea na wewe ninataka kwa kweli wananchi hawa wapate umeme, awamu ya kwanza ulisema utatoka Sumbawanga- Laela, ni nguzo tu zimelala, awamu ya pili ni Ukanda wa Ziwa Rukwa, kwa hiyo naishauri Serikali iweze kuhimiza kwa haraka ili wananchi hawa waweze kupata umeme. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ninalotaka kulizungumzia ni kupunguza ukubwa wa maeneo ya Utawala, nazungumzia Jimbo langu la Kwela ni Jimbo kubwa na lina watu zaidi ya 450,000 lina sifa zote za kugawanya na nilipozungumza hapa kwa mara ya mwisho na Waziri Mkuu Mstaafu ali-support, kwa sababu anafahamu. Hata Mheshimiwa Keissy juzi amezungumza, hata baadhi ya Wabunge ambao wamekwenda kule akina Paresso wanafahamu, Mheshimiwa Mbatia, Mheshimiwa Aeshi wanafahamu, ni Jimbo kubwa kuliko, wakati mwingine unasema nitafanyaje kazi katika Jimbo hili, ni kubwa ukienda upande huu wengine wanakusahau.
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Naishauri Serikali na bahati nzuri uliyekuwa Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa Manyanya uko hapa, naomba jambo hili tulivae wote, tuihabarishe Serikali inatuletea matatizo makubwa sana, Jimbo hili linatakiwa kugawanyika, kama tunatenda haki kwa sababu lina sifa zote. Yapo Majimbo yamegawanywa zaidi ya mara 3, hayana sifa zote. Lakini Jimbo langu limebaki pale pale.
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mapendekezo tumeleta yote ya kuomba Jimbo, kuomba Wilaya, kuomba Halmashauri, hakuna hatua hata moja ambayo imechukuliwa, sasa jamani na hawa wananchi mnawaweka katika upande gani? Naishauri Serikali ijaribu kutenda haki kwa maeneo yote yenye matatizo kama haya, nimeona nilizungumzie.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni miundombinu ya barabara, ninapozungumzia barabara nizungumzie barabara ya kutoka Kibaoni, kuja Kiliamatundu na kwa maana hiyo ukifika Kiliamatundu unatakiwa ukatishe uende Kamsamba, ukatokee Mloo. Ile barabara ina zaidi ya kilometa 200.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru Serikali kwa sababu katika ilani mmeiweka katika kipaumbele cha kuifanyia usanifu. Hata hivyo, naomba isiwe usanifu ile barabara inatakiwa kutengenezwa kwa kiwango cha lami kwa sababu ina uchumi mkubwa sana. Hizi kilometa 200 ninazosema karibuni kila baada ya kilometa tano kuna kijiji cha wananchi wenye uzalishaji, ukitengeneza barabara hii utakuwa umeufungua ukanda ule kiuchumi, utaongeza pato kwa wananchi, utaongeza pato kwa Serikali. Kwa hiyo, naomba Serikali iweze kushughulikia barabara ile kwa kiwango cha lami, ikiwa ni pamoja na kutengeneza daraja la mto Momba.
Mheshimiwa Mwenyekiti, imekuwa miaka mitatu tunaambiwa upembuzi yakinifu tumechoka na maneno hayo, tunataka waanze kujenga. Ukijenga daraja hilo umeshawaunganisha wananchi na Wilaya ya Momba wanaotokea Mloo, uchumi utaenda kwa kasi kubwa sana. Kwa hiyo, naiomba Serikali iweze kuchukua jambo hili katika masuala ya utekelezaji, kwa sababu linaumiza sana na ni ukanda wenye uchumi mkubwa sana, uzalishaji wa mpunga, ufuta, uvuvi. Sasa tunapozungumzia kutengeneza barabara si tuangalie na vigezo, vigezo ni kuongeza uchumi wa wananchi na Taifa zima kwa ujumla siyo unapeleka barabara huna hata matumaini ya kurejesha uchumi wenyewe.
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. Ahsante.(Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi nishukuru kupata fursa hii ili niweze kuchangia hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa niseme ninaunga Mkono hoja hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa asilimia 100. Sababu ziko wazi, imesheheni karibu pande zote, mikakati yote, kutokana na utendaji wa kazi tunaouona kwa sasa wa Mheshimiwa Rais na Mawaziri wake hatuna mashaka, tusonge mbele. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nichangie upande wa hotuba ya Waziri Mkuu ukurasa wa nane mpaka wa 10 katika eneo la siasa. Mheshimiwa Waziri Mkuu alitoa maagizo kwenye Tume ya Uchaguzi kubaini sababu zilizopelekea wapiga kura milioni saba kutokupiga kura. Idadi hiyo ni kubwa sana, lazima na sisi tuweze kueleza baadhi ya sababu ambazo zinaweza kuwa kwa namna moja au nyingine zimechangia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya sababu ni umbali wa vituo vya kupigia kura. Watu walikuwa wanatembea kilometa 20 mpaka 10 kufuata kituo cha kupigia kura, sasa ni watu wachache ambao wanaweza wakamudu hali hiyo, lakini zipo sababu zingine za baadhi ya wananchi kukata tamaa zikiwemo sababu zifuatazo:-
Kwanza, wananchi kukata tamaa kutokana na baadhi ya Viongozi kutotenda haki, kuwa na upendeleo na ubinafsi uliokithiri. Hiyo ni sababu mojawapo inayowafanya wananchi wakate tamaa na ninaomba nieleze sababu hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla hatujaenda kwenye uchaguzi wa mwaka 2015, Tume ya Uchaguzi ilitoa vigezo vinavyoweza kuwezesha Jimbo likagawanyika. Sisi wote tunajua, vigezo tunavijua lakini cha ajabu unakuja kuona majimbo ambayo hayakufikia vigezo hivyo yaliweza kugawanywa na kuacha majimbo ambayo vigezo vimezidi hata vigezo vilivyowekwa. Unashindwa kupata majibu, wananchi wanakata tamaa, wananchi wanaelewa, wananchi wanafuatilia sana vyombo vya habari na wanachanganua na wanaona wakati mwingine kama Serikali ina upendeleo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu wanakuwa wameomba mara kadhaa, wameomba Wilaya, wameomba Halmashauri, wameomba Jimbo hawajapata na ninao ushahidi wa kutosha, katika Wilaya yangu Jimbo la Kwela Halmashauri ya Wilaya imeomba Wilaya, imeomba Jimbo, imeomba Halmshauri haijapata wakati ina vigezo vilivyopitiliza. Hii inatokana na viongozi kutokutembelea maeneo yote, hii ni moja ya sababu muhimu sana ambayo inakatisha wananchi tamaa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sababu nyingine ni kuchelewa kwa utatuzi wa Migogoro ya ardhi. Kwanza napaswa nimpongeze Mheshimiwa Waziri wa Ardhi aliyepo sasa hivi, kwa kweli lazima tumpongeze anafanya kazi kubwa sana, tena yenye moyo na kujitoa muhanga, mimi nampongeza sana. Lakini ningeomba ajielekeze katika maeneo sugu ambayo yamelalamikiwa kwa muda mrefu kutoa ufumbuzi na utatuzi wa mara moja ili kutokukatisha wananchi tamaa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapozungumza hivi ninaongelea suala la shamba la Malonje ambalo limekuwa ni sugu sana na kwenye uchaguzi limetupa shida sana, hasa mimi Mbunge ndiye nimepata kazi kubwa kana kwamba mimi ndiye niliyebeba mzigo huo. Kwa hiyo, ninaomba Mheshimiwa Waziri uliangalie hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni baadhi ya maeneo kutofikiwa na viongozi wa Kitaifa. Tangu tumepata Uhuru sasa hivi tuna Rais wa Awamu ya Tano, lakini yapo maeneo hawajawahi kumuona Rais hata wa Awamu ya Kwanza, ya Pili na Awamu ya Tatu, wanamuona tu kwenye luninga, sababu za msingi hazipo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati mwingine kiongozi anaenda wanasema hakupitiki barabara ni mbaya nani atengeneze? Huko ni kutenga wananchi!
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba viongozi mnaotumbua majipu muangalie hayo ni majipu, kama Kiongozi anakuelekeza mahali pa kwenda kuzuri huko anaficha nini? Ni majipu nayo vilevile tunaomba tabia hiyo isiwepo tena, tunaimani na Serikali hii tabia hiyo itajifuta yenyewe. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni kubaki nyuma kimaendeleo, kukosa huduma muhimu. Kwa mfano, nitoe mfano kwa mambo mawili, barabara na umeme. Wilaya ya Sumbawanga Vijijini pamoja na kuwa kubwa mno, ina kata zaidi ya 28, vijiji 115 hakuna hata kijiji kimoja ambacho kina umeme, na wananchi wanasikia maeneo mengine kata mbili zina umeme na hata Kata jirani zina umeme, unadhani wananchi wanatafsiri kitu gani?
Mheshimiwa Mwenyekiti, tafsiri nyepesi ya wananchi wanadhani labda Mbunge wao hana uwezo, hasemi! kitu ambacho kila wakati tunazungumza. Kwa hiyo, ningeomba Serikali ijaribu kuweka uwiano isiwe na upendeleo, iweke uwiano kwa sababu nchi hii ni yetu sote. Iweke uwiano siyo kukimbilia upande mmoja, huko ni kuumiza wananchi bila sababu, niliona na lenyewe hilo nilizungumzie. (Makofi)
Suala lingine ni miundombinu ya barabara. Katika Jimbo langu ni mibovu mno, kwanza jiografia yenyewe ya Jimbo imekaa hovyo, miundombinu ni mibaya, hata viongozi wanaokuja, mfano Dada yangu Paresso alikuja wakati wa uchaguzi, Katika vitu alivyovitumia ni uchakavu wa miundombinu katika Jimbo langu, aliuliza hii ni Tanzania au ni Tanganyika? Nikamwambia Tanzania. Tulipata taabu kweli, hebu jamani jaribuni kuangalia maeneo haya, zipo barabara zaidi ya 10 hazipitiki. Sina sababu za kuzitaja kwa sababu naona muda hautoshi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ambalo ninapenda kulizungumzia ni kuhusu kilimo. Katika Hotuba ya Waziri Mkuu upande wa akiba ya chakula, inaonesha kwamba wametenga kununua tani 100,000 hicho kiwango ni kidogo mno, na sijui vigezo gani mnavitumia? Sijajua vigezo gani mnavitumia hivi tani 100,000 mnapanga zinaweza kuwasaidia Watanzania kama mvua hazitapatinaka miaka miwili, mitatu? Hizo tani 100,000 zinaweza zikasaidia? Na bado miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji bado hatujafikia kiwango kizuri.
Kwa hiyo, mazoea ambayo tumekuwa nayo ya neema ambayo tunayo Tanzania tunadhani miaka yote tutakuwa tunapata mvua mfululizo ndiyo sababu ya kutenga kiwango kidogo ,tani 100,000 ni kiwango kidogo mno kwa Nchi ya Tanzania. Kwa hiyo, ningeshauri kiwango hiki kiongezwe ni kidogo sana.
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Hiyo ni Rukwa peke yake kama anavyozungumza Mheshimiwa aliyepo nyuma yangu, naomba kiwango hicho kiongezwe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni upande wa afya, tunalo tatizo la upungufu wa wataalamu, waganga, tunalo tatizo la ukosefu wa kumalizia zahanati ambazo zimeanza kujengwa na wananchi na vituo vya afya, madaktari hakuna, ukosefu wa magari ya kubeba wagonjwa.
Mfano, tatizo la Kituo cha Afya cha Milepa, maombi yamekuja huu ni mwaka wa tatu na kutokana na kuchelewa tumepoteza karibu akina mama wajawazito 10 kwa mwaka jana tu, nimetoa taarifa mara kadhaa, nimerudia kuomba mara kadhaa. Naomba Mheshimiwa Waziri Mkuu mambo mengine kama haya uyachukulie ni mambo muhimu, yanatutia doa kwa Serikali yetu nzuri hii ya sasa. Naomba uyabebe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni upande wa elimu. Tunalo tatizo la upungufu wa walimu wa sayansi upande wa shule za msingi hata upande wa shule za sekondari.
Tumejenga shule nyingi za sekondari za kata, tunaomba tupate Walimu wa Sayansi na wapo walimu ambao wamepata mafunzo wamemaliza wanazagaa mitaani hatujui wataajiriwa lini? Tunaomba wakati Mheshimiwa Waziri Mkuu anakuja kutoa ufafanuzi atueleze wataajiriwa lini walimu wapya wa sayansi na kwa kiwango gani kinachoweza kukidhi hali tuliyonayo kwa sasa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni ukosefu wa hosteli hasa hosteli za wasichana. Shule za Kata zina tatizo kubwa la kukosa hosteli za wasichana, jambo ambalo linarudisha maendeleo nyuma la vijana wetu wa kike, sote tunafahamu watoto wa kike wana vikwazo vingi, kutembea kilometa 5 anapambana na vikwazo vingi, wakati mwingine tunaweza tukalaumu kumbe waharibifu ni sisi wenyewe tusioangalia matatizo kama haya. Kwa hiyo, ni vizuri Serikali ikatilia umuhimu wa kujenga hizi hosteli kwa shule zetu za kata.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuchukua fursa hii kuishukuru Serikali kwa haya ambayo wameandika humu, tunasubiri utekelezaji na vilevile kwa haya niliyoyasema ningeomba ufafanuzi hasa kuitenga Wilaya ya Sumbawanga kutoipa Jimbo au Wilaya au Halmashauri wakati inavigezo lukuki.
Mheshimiwa Mwenyekiti naunga mkono hoja
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Naibu Spika, unapozungumzia kilimo huwezi kukosa kuzungumzia ukosefu wa ardhi ya kilimo kwa baadhi ya maeneo ikiwa ni pamoja na migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji, wafugaji na hifadhi za Serikali, wakulima na hifadhi. Mfano mzuri upo mgogoro kati ya wakulima na Hifadhi ya Akiba ya Uwanda katika Jimbo langu la Kwela. Mwingine ni mgogoro wa wananchi na mwekezaji wa shamba la Malonje. Serikali imalize haraka migogoro hii bila kufanya hivyo inaweza kusababisha mapigano na kuleta maafa makubwa sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna changamoto kwenye pembejeo. Pembejeo nyingi hazifiki kwa wakati, hazitoshelezi, wanaofaidika ni wachache na bei kuwa kubwa isiyolingana na bei ya mazao. Naomba Serikali iangalie suala hili.
Mheshimiwa Naibu Spika, bila kuimarisha kilimo cha umwagiliaji nchi yetu haiwezi kuwa na uchumi imara. Tunayo mito mingi inayotiririsha maji msimu wote, lakini bado hatujaitumia vizuri. Nichukulie mfano katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, miaka minne mfululizo tuliomba miradi ya umwagiliaji lakini hatujapata fedha za kujenga miradi hiyo. Miradi hiyo ni wa Msia, Uzia, Maleza, Nkwilo, Nankanga na Mbulu. Naomba Serikali itupatie fedha kwa ajili ya miradi hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, bado tunalo tatizo kubwa la wakulima wetu kukosa soko la mazao na kuwafanya kukata tamaa na vijana wengi kukimbilia mijini baada ya kuona kilimo hakiwalipi. Hivyo, Serikali itafute masoko ya bei nzuri ya mazao.
Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa maghala. Mkoa wa Rukwa ni miongoni mwa Mikoa inayozalisha chakula kwa wingi lakini hakuna maghala ya kutosheleza kuhifadhi mazao. Matokeo yake ikifika wakati wa mvua mazao hunyeshewa na kuoza. Naomba Serikali itueleze ni lini Mkoa wa Rukwa utajengewa maghala.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imetelekeza Ziwa Rukwa pamoja na ziwa hilo kutoa ajira kubwa kwa wananchi na hasa vijana. Serikali haijawahi kutoa mikopo ya vikundi vya wavuvi, kwa nini mmelitelekeza Ziwa Rukwa?
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuchangia katika Wizara hii kama ifuatavyo:-
Mhshimiwa Mwenyekiti, Elimu ya Awali ni muhimu sana katika kumwandaa mtoto kuanza Darasa la Kwanza kwa mwaka unaofuata, hivyo ni vyema Walimu wa kufundisha watoto hawa wakawa rasmi na kupewa cheti cha kufuzu masomo hayo kwa kufaulu badala ya kuchukua Walimu waliochoka, wasio na taaluma hiyo kama ilivyo sasa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Elimu ya Ufundi ni nyenzo muhimu sana kwa vijana wetu ambao hawakubahatika kuendelea na masomo ya elimu ya juu, hivyo ni jambo la muhimu vijana hao wakapata mafunzo ya ufundi ili elimu hiyo iwasaidie katika kumudu maisha yao, pia kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa Taifa lao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tutambue kwamba sera ya Serikali ni kwamba kila Wilaya kuwa na Chuo cha Ufundi (VETA) angalau kimoja. Je, sasa nataka Mheshimiwa Waziri anieleze ni lini sasa Wilaya ya Sumbawanga vijijini itajengewa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi (VETA)? Ni lini Mkoa wa Rukwa utajengewa Chuo cha Ufundi VETA? Naomba majibu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Serikali ianzishe haraka Kidato cha Tano na Sita ili kwenda sambamba na uanzishaji wa sekondari kila Kata ili wanafunzi wanaomaliza Kidato cha Nne wapate nafasi ya kuendelea na Kidato cha Tano na cha Sita.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hii itasaidia sana na hasa kwa familia masikini ambao wazazi wao hawana uwezo wa kuwapeleka mbali. Nitolee mfano wa Wilaya ya Sumbawanga vijijini, inazo Shule za Kata zinazofika Kidato cha Nne 19, ikiwa tunayo shule moja tu ambayo imepandishwa kufikia Kidato cha Sita.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa Mheshimiwa Waziri atukubalie kupandisha shule zifuatazo kufikia Kidato cha Sita; Vuna Secondary School, Mazoka Secondary School, Mzindakaya Secondary School, Milenia Secondary School. Naomba majibu ya Mheshimiwa Waziri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naendelea kuchangia kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kitengo cha Ukaguzi kimezorota sana ukilinganisha na ilivyokuwa hapo awali, hivyo kitengo hiki kiimarishwe kwa kupewa vitendea kazi kama vile, magari pikipiki, vifaa vya Ofisi na Ofisi zao zijitegemee bila kuingiliwa, kuwe na mafunzo ya mara kwa mara, fungu la kutosha kwa maana ya OC ili kuwezesha kitengo hiki kufanya kazi vizuri na kwa uhuru bila mashindikizo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inapaswa kujipanga juu ya ujenzi wa hosteli ili kunusuru vijana wetu na hasa watoto wa kike ili kuwapa fursa nzuri ya kusoma na kuwaepusha na vishawishi wanavyovipata wanapokuwa huru katika mazingira ya uraiani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wamejitahidi sana katika ujenzi wa maabara, hivyo tunaomba Serikali itoe vifaa vya maabara ili kuboresha na kuiimarisha, vijana wetu waweze kupata elimu bora katika masomo ya sayansi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naishauri Serikali itoe posho kwa Walimu wanaokwenda kukaa katika umbali na ukosefu wa huduma muhimu kama vile umeme, mabenki, mawasiliano na usafiri. Naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake pamoja na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018.
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuwa miongoni mwa wachangiaji katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu.
Mheshimiwa Naibu Spika, niungane na wachangaiaji waliotangulia kumpongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu, Waheshimiwa Mawaziri, Manaibu Waziri na Makatibu Wakuu kwa speed tunayokwenda nayo sasa hivi. Niwatie moyo kwamba endeleeni kukaza uzi mambo yanakwenda barabara. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kuchangia upande wa kilimo. Sisi wote tunatambua kwamba asilimia kubwa ya Watanzania wanategemea kilimo kwa zaidi ya asilimia 85. Hata hivyo, ukiangalia hali halisi ya Serikali kutilia maanani suala hili sijaona. Serikali haijazama kwa undani zaidi kuona kwamba kilimo ndiyo kinachoweza kuwasadia Watanzania hawa wengi na mtiririko wa vijana wengi wanaomaliza vyuo vikuu hatutaweza kuwaajiri wote wangeweza kukimbilia kwenye kilimo kama tungeweka mipango yetu vizuri. Kilimo kinalipa kwa mtu ambaye atakuwa amejipanga vizuri na Serikali imeweka mazingira mazuri. Kwa hiyo, naiomba Serikali itilie maanani sana upande wa kilimo ambacho ndiyo kinaweza kuokoa Watanzania walio wengi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie kuhusu mbolea na pembejeo. Toka nimeingia katika Bunge hili sijawahi kuona mwaka ambao pembejeo kwa maana ya mbolea na mbegu imewahi msimu wa kilimo hata siku moja. Ni miaka yote imekuwa ikichelewa na sijajua ni kwa sababu gani. Kama tuna dhamira thabiti ya kuwasaidia wananchi tupeleke pembejeo kabla ya msimu kuanza. Ningefurahi mwaka huu jambo hili iwe ni mara ya kwanza Serikali kuwahisha pembejeo kwa wakulima kabla ya msimu kuanza. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lipo tatizo lingine la kupeleka mbegu fake na dawa fake za palizi. Yapo maeneo ambayo yanatengeneza mbegu fake na dawa fake za palizi wakulima wetu wananunua na kwenda kuyatumia yanatia hasara kubwa sana. Naomba vyombo vinavyohusika vijaribu kufuatilia makampuni haya ambayo yanapeleka mbegu fake na dawa fake za palizi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, bado lipo tatizo kubwa la upungufu wa ardhi katika maeneo mbalimbali. Vijana wengi wanapenda kulima, lakini lazima tukubali baadhi ya maeneo ardhi haitoshi. Hii ni kutokana na watu wachache kukumbatia ardhi. Vilevile Serikali ijaribu kuangalia yale maeneo ambayo tulitenga kwa kazi nyingine iyatoe kwa vijana hawa waweze kujiendeleza kwa kilimo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni umwagiliaji. Sisi wote lazima tukubali kwamba kilimo ni sahihi kisicho na risk ni kilimo cha umwagiliaji. Huwezi ukalinganisha kilimo cha umwagiliaji na kilimo cha mvua. Kilimo cha mvua kina risk nyingi sana, unaweza ukapata mafuriko, upepo
mvua au kukosekana kwa mvua. Ndiyo maana hata benki ukienda kuomba mradi wa kilimo kwa kutegemea kilimo cha mvua hupati mkopo. Ukienda na kilimo cha umwagiliaji utapata mkopo kwa sababu wanajua kwamba ni kilimo cha uhakika. Naomba Serikali izame kwa undani zaidi kuhakikisha inainua kilimo cha umwagiliaji. Tunayo mito mingi, mabonde mengi, maziwa mengi, kuna tatizo gani la Serikali kutozama katika kilimo cha umwagiliaji ambacho tunajua kwamba ni kilimo cha uhakika? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, halmashauri yangu iliweza kuomba miradi ya umwagiliaji katika vijiji kadhaa vya Uzia, Ilemba, Msia, Milepa hatujawahi kupewa hata mwaka mmoja. Naomba safari hii tuweze kupewa angalau hata kwa mradi mmoja hasa ule mradi wa Mareza ambao una hekta 7,000 ambazo zinaweza kutumika kwa kilimo cha umwagiliaji. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tunao upungufu wa maghala kwa baadhi ya mikoa inayozalisha sana kwa mfano Mkoa wa Rukwa. Ukienda pale kwenye maghala ya Serikali utakuta mahindi yamepangwa nje jambo ambalo ni risk mvua zitakapokuwa nyingi. Tungeomba Serikali iweze
kujenga maghala ya kutosha katika maeneo hayo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, niende Wizara ya Afya, katika ukurasa wa 40, Mheshimiwa Waziri Mkuu ameelezea vizuri sana kwamba kumekuwa na ongezeko la fedha za kununua dawa kutoka shilingi bilioni 31 mwaka 2015/2016 kwenda shilingi bilioni 251 mwaka 2016/2017. Tunapongeza kitendo hicho na tunaomba Serikali iendelee kuongeza fedha mwaka hadi mwaka kwa suala la ununuzi wa dawa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini lazima tukubali, sera yetu ya Serikali kupitia Chama cha Mapinduzi iliji-commit kwamba lazima kuwe na zahanati kila kijiji, kituo cha afya kila kijiji na Wilaya kuwa na Hospitali ya Wilaya. Sera hiyo ilieleweka vizuri sana kwa wananchi na ndiyo maana wamejitoa kujenga maboma mengi sana katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu kwa sababu wanajua ingeweza kuwasaidia. Cha ajabu maboma hayo hayajamalizika kutokana na Serikali kutopeleka fedha kwenye halmashauri. Ni nguvu za wananchi na wakati mwingine unakuta Mbunge anajitolea kupitia Mfuko wake wa Jimbo lakini Serikali kama Serikali tungeomba ipeleke fedha ili miradi hiyo iweze kumalizika mapema iwezekanavyo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano, kwenye Jimbo langu kuna maboma karibu 13 ambayo wananchi wamejenga, mengine yamefikia hatua nzuri mengine bado katika vijiji vya Ilambo, Maleza, Kirando, Kiryamatundu, Mtapenda, Kasekela, Lyapoo, Nakazi, Mumba, Jangwani,
Kizumbi, Kawila na kasekela. Wananchi wamejitoa kujenga majengo haya, naomba Serikali iweze kupeleka pesa kwenye halmashauri zetu ili iweze kukamilisha majengo haya. Kadhalika, vituo vya afya wananchi wamejitoa michango yao, nguvu zao, wamejenga majengo kwenye Kata za Mfinga, Muza, Ilemba, Kaoze, Kipeta na kalambazite. Tunaomba Serikali ipeleke fedha ili iweze kumalizia majengo hayo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ni ukosefu wa magari ya kubeba wagonjwa katika vituo vya afya. Ninavyo vituo vya afya vinne ambavyo havina magari vya Milepa, Lahela, Mpui na Msandamugano lakini sanasana nizungumzie Kituo cha Afya Milepa ambacho kimejengwa
kwenye mazingira magumu kulingana na jiografia ilivyo. Kile kituo kimepoteza akina mama wengi na watoto. Mheshimiwa Waziri Ummy nimekueleza mara kadhaa hata Naibu Waziri nimewaeleza athari kubwa inayotokea ya vifo vya akina mama kutokana na kituo hiki kukosa usafiri. Nina imani kwa maelezo ya leo kwa huruma yako tungeomba uwapatie gari la wagonjwa katika kituo hiki cha afya cha Milepa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tunao upungufu mkubwa sana wa watumishi kwenye zahanati zetu hasa mikoa ya pembezoni. Unakuta zahanati inaongozwa na Mhudumu Muuguzi sasa unategemea nini katika mazingira ya namna hiyo? Tunaomba Serikali iweze kuliangalia hilo na ikiwezekana kutoa ajira kwa watumishi wenye sifa wa kuweza kuongoza hizo zahanati. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba vilevile nikumbushie maombi ya Halmashauri ya kuomba
halmashauri, wilaya na jimbo. Jambo hili wengine wamekuwa wakiona kwamba labda tunafanya mzaha. Mimi nataka nieleze ukweli, kama Watanzania tuna huduma, Mheshimiwa
Waziri Mkuu umefika katika maeneo yale, tena nikushukuru sana, hukupangiwa kwenda, mimi ndiye niliyekuomba na ukafika. Hata hivyo, nakuambia, sehemu uliyofika ni moja ya nane ya eneo langu. Ulijionea hali halisi ilivyo, jiografia ilivyo na ukubwa wa jimbo ulivyo. Pamoja na Serikali kuweka msimamo wa kutoongeza maeneo, myaangalie maeneo nyeti kama haya. Mimi nazungumza kwa niaba ya wananchi. Wananchi ndiyo wamenituma nizungumze jambo hili
isionekane mimi ndiye ninayezungumza. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna wananchi wapiga kura zaidi ya 200,000 na idadi ya wananchi karibu 400,000…waaminifu kwa Chama cha Mapinduzi inakuwaje hawa watu msiwaangalie? Kama tulifanya makosa ya kutoa halmashauri kwenye maeneo ambayo hayana sifa basi yavunjeni hayo mtoe haki kwa wale ambao wanastahili kupewa haki kuliko kuweka kizuizi watu
wengine wasiweze kuomba. Mimi nadhani hili ni tatizo kubwa sana katika eneo langu. Nakuomba Mheshimiwa Waziri Mkuu uweze kulibeba kama ulivyokuwa umelibeba toka siku ile
wala siyo jambo la kupuuza. Wananchi ndiyo kilio chao kikubwa kutokana na mazingira na huduma mbovu wanayoipata kutokana na mazingira yaliyopo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine nililotaka kuzungumzia ni upande wa elimu. Tuna upungufu mkubwa sana wa walimu wa sayansi kwa shule zetu za sekondari hata shule za msingi. Vilevile umaliziaji wa maabara ambazo wananchi wameshajenga, tungeomba Serikali iweze kumalizia hizo maabara.
Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ni uanzishwaji wa shule mpya... (Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuchangia hotuba hii ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikaki za Mitaa). Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniweka hai na mwenye afya njema katika siku ya leo niweze kushiriki kuchangia katika hotuba hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa, nami naungana na Watanzania kumpongeza Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi anazozifanya, Watanzania wanaziona. Vilevile nampongeza Mheshimiwa Jafo kwa kazi kubwa anayofanya, kijana huyu ni hodari, lazima tuseme ukweli, anafanya kazi vizuri sana. Niwapongeze Naibu wake; Mheshimiwa Kandege na Mheshimiwa Waitara, wanafanya kazi vizuri. Nimpongeze Katibu Mkuu, Eng. Nyamhanga na watumishi wote wa Wizara hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti kwa kuanza, naomba nizungumzie barabara za vijijini. Barabara za vijijini ndiyo msingi wa maendeleo katika nchi yetu, kwa sababu huko ndiko kunatoka chakula, kuna wananchi wanyonge na huko ndiko wananchi wanauza mazao kwa bei mbaya kutokana na hali ya barabara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuliunda hapa chombo cha TARURA kwa matumaini mema tu kwamba kitaweza kutusaidia. Mimi nikiri kabisa kwamba chombo hiki ni kizuri na Watendaji wana uwezo wa kusimamia fedha vizuri kwa ajili ya kujenga barabara, shida iliyopo wanapewa pesa kidogo mno. Sasa matumaini ya Watanzania na sisi Wabunge tunashindwa kuelewa ni kwa namna gani hizi barabara zitajengwa kama tulivyokusudia. Tunaomba kwa kweli chombo hiki kiongezewe pesa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, mimi katika Jimbo langu nina barabara sugu sana, lakini ninachokiona hata mgawanyo wa pesa hizo ndogo hauendi sawa, ni kama kuna upendeleo wa namna fulani. Nakuomba kabisa uagalie ukurasa wa 196, angalia mgao wa fedha katika Halmashauri ya Sumbawanga DC vilevile uende ukurasa wa 200 - 201 uone jinsi Halmashauri ya Sumbawanga DC ilivyopata pesa kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiacha hapo twende kwa Mkoa mzima wa Rukwa, umepewa shilingi bilioni nne, mkoa wenye uzalishaji mkubwa na wenye barabara sugu na mvua nyingi ambazo zinaharibu barabara kila siku kupewa kiasi hiki siyo sawa. Kwa kweli naona jambo hili sio jema, mtafakari upya na maeneo niliyokwambia yafuatilie utaona kama ni sawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie barabara sugu ambazo ziko katika maeneo yetu ambazo tulizipitisha kwamba walau zikitengenezwa hizi, zinaweza zikasaidia kiasi fulani. Barabara ya Kahengesa - Kitete pamoja daraja; barabara ya Kahengesa – Itela – Ntumbi – Ilembo; na barabara ya Mawenzuzi – Msia. Barabara hii Serikali iliwahi kutupa pesa shilingi milioni 400 lakini imeitelekeza maana yake zile pesa thamani yake itapotea kwa sababu hakuna nyongeza iliyoongezeka ili barabara iweze kutengenezwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nyingine ni barabara ya Mtowisa - Ng’ongo. Barabara hii ni ahadi ya Makamu wa Rais, hebu tumheshimu Makamu wa Rais, kwa huruma ya akina mama akasema hii barabara lazima itengenezwe kwa changarawe. Nashangaa mpaka sasa hivi sioni ahadi ile kama inatekelezeka na miaka inaendelea kuisha. Ni lazima tumheshimu mama huyu kwa kazi anazozifanya, walau tumpe upendeleo wa barabara hii iweze kutengenezwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ipo barabara Mihangalua - Chombe na Chombe – Kahoze. Hizi barabara nazozungumzia ni barabara sugu. Barabara zipo nyingi lakini hizi tulizitenga kwamba ni sugu, zikitengenezwa zinaweza zikapunguza kiasi fulani maumivu kwa wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo nataka kuzungumzia ni katika ukurasa wa 5 ambapo Mheshimiwa Waziri umeelezea namna Serikali ilivyojipanga katika kujenga majengo ya utawala. Nimeangalia nikaona Sumbawanga DC ambayo ina jengo la utawala ilianza kujenga mwaka 2011 mpaka sasa hivi halijaisha, Serikali ilitupa shilingi bilioni 1.6 na mkataba wa jengo hili ni shilingi bilioni 2 na mwaka huu tuliomba shilingi milioni 700 lakini hatujapangiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jengo limechukuwa miaka mwishowe litachakaa, watumishi watakosa pa kufanyia kazi, kumbukumbu zitahifadhiwa wapi? Naomba Mheshimiwa Jafo ulione hili, jengo ni la muda mrefu, ni ghorofa moja, miaka imekuwa mingi na linachakaa na tuliomba pesa tunashangaa hamjatupangia. Tunaomba Mheshimiwa Jafo uliangalie jambo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni suala la wakandarasi upande wa maji hawalipwi kwa wakati. Kama tatizo ni pesa kwa sababu tatizo la maji ni kwa nchi nzima, tulijadili kwa pamoja tutafute ufumbuzi kuliko wakandarasi wanafanya kazi muda mrefu wanadai pesa hawapati sasa tunaanza kushangaa tatizo ni nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata ahadi ya Serikali inavyosema miradi ya maji itajengeka, sijaona itajengeka kwa namna gani, kwangu mpaka sasa hivi nina wakandarasi zaidi ya wanne wanadai pesa hawajalipwa. Kwa mfano, mkandarasi wa mradi wa pale Ikosyi, alipeleka vifaa ameanza kujenga, mwishowe ameamua kuviondoa kwa sababu hajalipwa na amedai kwa muda mrefu na nimefuatilia mara kadhaa nashangaa Serikali haijamlipa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine napenda kuzungumzia upande wa afya. Kwanza kabisa, niishukuru Serikali mmetupa shilingi 1,500,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya, hongereni sana. Halafu mmetupa shilingi 400,000,000 kwa ajili ya upanuzi wa kituo cha afya na kwenye bajeti hii mmetupa shilingi 200,000,000 kwa ajili ya kupanua Kituo cha Afya pale Mpuli, tunawashukuru sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini naomba kuongezea Mheshimiwa Waziri uliangalie Jimbo lilivyo na jiografia yake. Nashukuru kwa hiki mlichotupatia lakini hebu jaribuni kutanuka zaidi. Mimi Jimbo langu ni kubwa na jiografia ni mbaya, majimbo mengine yamepata vituo vya afya vinne, vitatu sasa najiuliza, jimbo langu ambalo ni kubwa na Mheshimiwa Jafo umefika umeliona mpaka ukatuonea huruma, hebu jaribu huruma hiyo upeleke kwenye vitendo. Tunaamini kwa sababu utakuwa umesikia na ni kijana msikivu endelea kulingalia uweze kutuongezea kituo kingine cha afya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile nizungumzie tatizo la gari. Jimbo langu halina gari la wagonjwa na mazingira unayajua, nimeomba gari hili karibu miaka mitatu, unaenda mwaka wa nne, naahidiwa sijapewa. Naomba na lenyewe hilo Mheshimiwa Jafo uweze kuliangalia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni maombi ya fedha za kumalizia maboma yetu. Tuna zahanati 20 ambazo zimejengwa na wananchi kutoka usawa wa lenta na wengine wameweka na mabati, tunaomba tupewe fedha za kumalizia hizo zahanati vinginevyo wananchi watakata tamaa. Tunavyo vituo vya afya kama vitano ambavyo wananchi wameshajenga majengo ya utawala wakaezeka tunasubiri kupewa fedha tuweze kumalizia ili yaweze kufanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile upande wa watumishi, tuna upungufu mkubwa sana wa watumishi. Halmashauri ya Sumbawanga DC ina upungufu wa watumishi 667. Ukiangalia mgao unaotolewa unakuta sisi tumepata kidogo hata wale ambao wana nafuu wanapata watumishi zaidi. Sijajua ni vigezo gani vinatumika katika kugawa watumishi hawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba jamani mtuangalie maana Sumbawanga DC tuko vijijini, mara nyingi tukisema Sumbawanga DC mkija mnafikiri ni pale mjini, hapana, kuna mazingira magumu sana, Mheshimiwa Jafo umetembea umeyaona, hata Waziri Mkuu alipita akashangaa kwamba katika nchi hii kuna mazingira ya namna hii. Sasa kama hata viongozi mmeyaona si mtupendelee basi hata wa kutupa wa fedha. Kama mmekataa kugawa Halmashauri na Jimbo basi tupeni fedha za kukidhi mahitaji na shida za wananchi. Sasa kama kotekote mnatunyima wananchi watatufikiriaje? Tunaomba sana jambo hili muweze kuliangalia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, upande wa elimu, tuna maboma mengi. Kwenye Halmashauri yangu tuna maboma 259 ya madarasa na nyumba za Walimu tunaomba na hilo mfikirie. Tunashukuru mmetupa shilingi milioni 75, lakini ukilinganisha na maboma yale, kwa kweli hakuna uwiano, hazitoshi. Tunaomba na lenyewe hilo muweze kuliangalia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni upande wa posho za Wenyeviti wa Vitongoji, Vijiji na Madiwani. Lazima tufike mahali tulitazame jambo hili. Hata miradi mikubwa tunayopeleka, ni wale ndio wanaosimamia, wanashinda kutoka asubuhi mpaka jioni bila posho. Hebu fikiria kama ungekuwa ni wewe, ungeweza kufanya kazi hiyo. Tujaribu jamani kutafuta namna yoyote ya kuwafuta jasho hawa watu, angalau kama hatuwezi kuwapa mishahara, basi tuweke hata posho, baada ya uongozi wake apate hata kiasi fulani cha kumfuta jasho, hata kama hapati mshahara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hawa watu wanafanya kazi kubwa sana. Kama hatuwapi posho ya kutosha hawa Madiwani basi tuwatengee posho hata mara moja baada ya miaka mitano mtu aweze kupata posho ya kufuta jasho lake kuliko kuacha kama jinsi ilivyo. Hawa watu wanafanya kazi kubwa mno. Nasi tunashuhudia tukienda tunashinda nao, unaweza ukachoka, wenyewe wanaendelea. Hebu jamani mjaribu kuangalia jambo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine napenda kuishukuru Serikali, tulikuwa na kilio cha muda mrefu cha daraja la mto Momba. Nashukuru daraja hili linaelekea kukamilika, Serikali imetupa shilingi bilioni 17,700,000,000/=, daraja hili linaelekea mwisho, tunashukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba tusiishie hapo, lengo la daraja ile ni kuunganisha mikoa mitatu. Kwa hiyo, tunaomba sasa Serikali ifikirie namna ya kuanza kujenga barabara ile kwa kiwango cha lami. Mkifanya hivyo, mtakuwa mmetutendea haki wananchi wa maeneo yale na ni maeneo kwa kweli yenye uzalishaji, hakuna zao linalokataa katika maeneo yale, lina rutuba nyingi sana. Mazao mengi mnayoyaona hata kule Mpanda, yanatoka Sumbawanga Vijijini; hata huko Mbeya Tunduma yanatoka Sumbawanga Vijijini. Kwa hiyo, ndiyo maeneo yenye uzalishaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba sana Serikali iweze kuangalia jambo hilo.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana.

MHE. IGNAS A. MALOCHA Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2015, Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue fursa hii kushukuru kwa kupata nafasi hii ili niweze kuungana na wenzangu katika kuchangia bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango. Lakini kabla ya yote nikupongeze wewe kwa umahiri wako na msimamo, umeonesha umahiri wa hali ya juu na kiti kimeku-fit, hongera sana mama, hongera sana jembe. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile nichukue fursa hii kumpongeza Waziri wa Fedha, Naibu wake na watendaji wote walioko ndani ya ofisi yake, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu. Mheshimiwa Waziri tunamfahamu umahiri wake hata kabla hajaingia ndani ya Bunge, uwezo wake tunaujua, isipokuwa michango yetu ni ya kumsaidia tu ili aweze kufunga goli vizuri kama ataitumia vizuri. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuchangia nianze kwa kusema kwamba mapato yote, uchumi wote ili kuboresha uchumi, kuongeza mapato huwezi ukatenga vitu viifuatavyo katika kuviboresha, ikiwemo barabara, reli, umeme, maji, afya, elimu, kilimo, tena kilimo cha umwagiliaji. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru Mheshimiwa Waziri katika kitabu chake ameeleza mikakati ya ujenzi wa reli ya kati na mambo mengine, lakini katika hili nataka nitoe ushauri kwa upande wa barabara. Yapo maeneo katika nchi hii ambayo hayawezi kupitiwa na reli, ama kwa sababu ya jiografia au ukanda wenyewe kwa jinsi ulivyokaa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo ni vyema kabisa maeneo haya na yenyewe yakatazamwa kwa upekee kwa maana ya kuwajengea barabara za lami. Kama unapitisha reli upande huu, upande huu hawana reli ni vizuri basi tukatenda haki na upande wa pili ukapeleka nguvu ya barabara za lami, kwa sababu reli haiwezi ikapita pande zote katika nchi hii. Kwa hiyo, mgawanyo mzuri ni kuweza na wenyewe kuwapelekea barabara ya lami. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ninapozungumzia suala hili nizungumzie upande wa jimbo langu, Ukanda wa Ziwa Rukwa kutoka Kibaoni, unakuja Kilyamatundu unakwenda Kamsamba hadi Mlowo, ukanda ule huwezi ukapitisha reli lakini ni ukanda mkubwa tena wa uchumi wa hali ya juu. Nasikitika sana Serikali haijaangalia ukanda ule, una uchumi mkubwa, barabara yake ni kilometa zaidi ya mia mbili na kitu.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kwa sababu Serikali imeazimia kujenga Daraja la Mto Mumba ambalo wameshatangaza tenda yake, ili kuimarisha barabara hii ni vyema wakajenga sasa lami ili iweze kutoka Kibaoni mpaka Kamsamba ikatokee Mlowo ili kuunganisha watu wa ukanda ule na mikoa mingine. Bila kufanya hivyo wale watu utakuwa umewaacha kisiwani, ile barabara ya lami unayoona Sumbawanga kwa wale watu haiwafai wala hawana matumizi nayo kabisa kwa sababu ni ukanda ambao umejitenga, kwa hiyo, nailitaka nisisitize hivyo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ni suala la CAG, wenzangu wamelizungumza kwa utaalam mkubwa sana, na kwa utafiti wangu karibu asilimia 90 ya Waheshimiwa Wabunge wamegusa jambo hili. Nina imani amesikiliza na mimi nimeona nigusie kwa sababu CAG ndiyo jicho, ndiyo dira ambayo inatuonesha kitu gani kimefanyika. Unapomtenga mtu huyu ni kama unataka kuficha uovu wako na sipendi Serikali hii ambayo Rais wetu amedhamiria kuondoa mafisadi halafu na mtu ambaye anaweza akawa jicho lake akapata kifungu kidogo. Kwa hiyo, nashauri kama wenzangu walivyoshauri, ofisi hii iweze kuangaliwa kwa kipaumbele cha hali ya juu.
Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie suala la migogoro ya ardhi, Serikali imetenga bilioni tano kwa ajili ya fidia ya migogoro ya ardhi, lakini kiwango hiki ni kidogo sana, karibu nchi yote imetapakaa migogoro ya ardhi. Bilioni tano haitoshi kuweza kufidia maeneo mbalimbali katika nchi nzima ya Tanzania, ni kitu ambacho hakiwezekani. Kama tuna azma kabisa ya kuondokana na migogoro hii ningeomba Serikali iweze kuangalia ni namna gani inaweza kufanya katika suala zima la kuongeza. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ni suala la mapato kutokana na wananchi kudai risiti wakishapata huduma na namshukuru Mheshimiwa Rais amepiga kauli mbiu sana kwenye TV tunamsikiliza. Sasa kauli mbiu hii ya Mheshimiwa Rais isiishie kwenye TV maana yake ni indicator kutuambia sisi viongozi wote, Waheshimiwa Wabunge, Wenyeviti na raia wote wenye nia njema, huko tunakofanya mikutano kipaumbele iwe ni kuwaelimisha wananchi wetu kudai risiti anapopata huduma na hasa huko vijijini. Tumuunge Mheshimiwa Rais, anazungumza kwenye TV, sisi twende nayo kwenye mikutano ya hadhara kutoa elimu kwa wananchi wetu ili waweze kudai risiti pindi wanapopata huduma. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie mashine za kutoa risiti. Ili tuweze kuleta ufanisi vizuri ni vyema kabisa mashine hizi zikatolewa bure na si bure, kwa sababu mtu akitoa mashine atakapokuwa anazitumia ndiyo nia njema ya kuleta mapato kwenye Serikali. Kwa hiyo, nashauri, ni vyema kabisa mashine hizi zikatolewa bure. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ambalo limezungumzwa na karibu Waheshimiwa Wabunge asilimia 90, ni kuondoa msamaha wa kiinua mgongo kwa Waheshimiwa Wabunge. Suala hili ukiliangalia, Mheshimiwa Waziri wa Fedha, ni kama limechomekwa, halijaja kwa muundo rasmi, limechomekwa. Sasa kama limechomekwa ni kazi rahisi, lichomoe tu, hakuna sababu ya kuhangaika nalo. Lichomoe, kwa sababu lingekuwa limekaa kwa mpangilio lingegusa viongozi wote wa kisheria ambao wanatakiwa kusamehewa na msamaha huo, lakini kwa sababu limepachikwa basi wewe usipate kazi ngumu, lichomoe, wala halina hata uzito wowote, lichomoe. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa maana hiyo, watu wengine wanaweza wakadhani sisi Waheshimiwa Wabunge tunajisemea, sisi siyo Wabunge wa maisha, tupo leo, kesho watakuja Wabunge wengine, kwa hiyo hatujizungumzii sisi, tunazungumzia hata watakaokuja. Maana mtu mwingine anaweza kusema hawa Waheshimiwa Wabunge wanajitetea, hapana, sisi siyo Wabunge wa milele, wangapi walikuwepo hapa hawapo, hata Mawaziri hawapo. Kwa hiyo, tunazungumza kwa niaba ya Watanzania na kwa nia njema. Kwa hiyo, tunaomba sana Mheshimiwa Waziri aweze kuliangalia jambo hili. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nadhani kwa haya machache yametosha. Naunga mkono hoja.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakuru sana kwa kunipa nafasi
niungane na wenzangu katika kuchangia taarifa hizi zote mbili, Kamati ya Miundombinu na
Kamati ya Nishati na Madini.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuanza naomba nianze na Kamati ya Miundombinu,
kwanza naipongeza Kamati kwa taarifa nzuri, nampongeza Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na
watendaji wote katika Wizara hii kwa utendaji mzuri. Kwa kweli kiuwajibikaji wanawajibika vizuri
na nadhani tatizo kubwa litakuwa ni pesa. Sasa labda nizungumzie suala moja ambalo naona
kwangu kama linanitesa, ni vipaumbele vya Serikali katika suala la barabara za lami,
tunafahamu kwamba sisi wote kwamba kuunganisha Mikoa na baadae itakuja Wilaya.
(Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nazungumzia Mkoa wa Rukwa unasemekana
tumeunganisha barabara ya lami ni sawa, ni katika ukanda wa upande wa juu. Mkoa wa
Rukwa umegawanyika katika pande mbili; ukija ukanda wa Bonde la Ziwa Rukwa barabara
kuanzia kibaoni unakuja, Kiliamatundu, unakuja Kamsamba, unakuja Mlowo; ni ukanda
mwingine tofauti kabisa ambao hauwezi kufaidika kabisa na barabara ya lami ya kutoka
Tunduma mpaka Sumbawanga. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu imekingwa na mlima ambao gari haiwezi kubeba
mzigo wa zaidi ya tani tatu, lazima iwe inabeba nusunusu na barabara hii bahati nzuri
inaunganisha Mikoa mitatu; Katavi, Rukwa na Songwe. Barabara hii ina kilometa karibu 200 na
ni barabara ya siku nyingi hata wakati wa ukoloni ilikuwepo ndio maana sababu ya kuwepo
wakati wa ukoloni ni umuhimu wake; potential zilizopo katika maeneo yale, kilimo ni bonde la
ufa linakubali mazao karibu mengi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa sijaua ni kwanini Serikali haijatilia umuhimu wa kuweka
lami katika barabara hii, na juzi wakati wamekuja watu wa MCC II waliuona umuhimu wa
kuweka lami barabara hiyo kulingana na vigezo vilivyokuwa vimewekwa, ni bahati mbaya tu
waliweza kujiondoa.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nataka kuiambia Serikali kwa nini haitaki kuona umuhimu
huo ambao hata watu wa MCC wamekuja kuiona na wakoloni waliona; kwa nini haitaki kuona
umuhimu wa kutenegeza barabara hii katika kiwango cha lami? Ni barabara ambayo ina eneo
la bonde la ufa na ina rutuba, inakubali mazao yote, inalima mpunga, matunda; ina mito
isiyokakuka karibu kipindi chote cha mwaka na mvua za kutosha. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nilikuwa naomba Waziri atakapokuwa anakuja
kutoa maelezo atueleze ni kwa nini Serikali haitaki kuangalia barabara hii na ninajua sababu
yake ni viongozi kutokupita katika maeneo yale na bahati mbaya sana Mawaziri karibu walio wote ni wageni. Nawaomba safari hii mjaribu kutembelea ile barabara mtaona umuhimu,
itawagusa mpaka kwenye mioyo yenu, naombeni sana mtusaidie katika eneo hilo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nishukuru kwa ujenzi ambao mnatarajia kuanza wa
daraja la Mto Momba, niwashukuru sana. Lakini faida ya ujenzi wa daraja lile ni kuunganisha
sasa ile barabara kwa lami; lakini kama mtalijenga mkaacha barabara ya vumbi itakuwa haina
maana yoyote. Kwa hiyo, na mimi nashauri kabisa jitihada za kujenga hilo daraja tunapongeza
lakini ziende sambamba na kufanya barabara ile iweze kujengwa kwa kiwango cha lami.
(Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nakuja kwa upande wa Kamati ya Nishati na Madini; kwanza
nampongeza Waziri, Naibu Waziri na watendaji wake wote na Kamati kwa taarifa yao nzuri.
Lakini nataka kusema ni muhanga wa REA katika Jimbo langu. Jimbo langu nimeeleza mara
kadhaa kwamba ni jimbo ambalo limeachwa kabisa halina miundombinu ya umeme; na kwa
jinsi lilivyokaa kijiografia sijajua ni kwa sababu gani linaendelea kuchelewa. Ninafahamu wazi
kwamba tumepangiwa kuletewa umeme katika REA III.(Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwa nini sisi tunakuwa nyuma kiasi hicho, kila jambo
tunakuwa nyuma na tunakaa gizani? Na bahati nzuri yapo maeneo mnapeleka umeme
mnapeleke watu hawataki kuutumia, umeme umeenda watu hawataki kuutumia, lakini lie eneo
ni eneo ambalo ukipeleka umeme watu watautumia kwa sababu vipo viashiria vya uchumi
vingi sana na ndio maana utakuta karibu eneo lote watu wamefunga solar; sasa watu
wanaojimudu kununua solar ukiwapelekea umeme utakuwa umewasaidia sana.
Ninamuomba Mheshimiwa Waziri ulione hili, nataka kipaumbele katika suala la umeme
katika maeneo yale yote; nikiungana na Mheshimiwa Kikwembe kule hatuna umeme kabisa.
(Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, halafu cha ajabu mmekuja kupitisha nguzo mkapitisha Muze,
mkapitisha kwenye Kata zangu mkapeleka Mpanda sijui mlipeleka wapi huko; kwa hiyo
wananchi wangu wanaziona nguzo tu. Juzi niliongea na Meneja wa TANESCO kwamba
naomba basi ulete hata umeme wa TANESCO potelea mbali wananchi watalipa; wamewasha
kijiji kimoja cha Muze wananchi wamelipa karibu shilingi laki moja na kitu; wanajitoa wamalipa.
Sasa wanalipa kwa gharama hiyo je, ukipeleka umeme wa REA si wananchi wengi watafaidika
na umeme huu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lipo jambo lingine ambalo nilikuwa naomba Mheshimiwa
Waziri unisaidie umeme ambao mnapeleka REA III kwangu upande wa Kusini Mashariki,
mmefikisha nguzo katika Wilaya ya Mbozi kwa kijiji cha Kamsamba; kijiji cha Kamsamba kinacho
tutenganisha ni mto. Mmeshapeleka nguzo mmefunga na transfoma kwa maana REA II
watapata umeme wale watu, nina vijiji zaidi ya nane ambavyo vimepangana vinauangalia
umeme utawashwa Kamsamba halafu huku hakuna umeme, zaidi ya vijiji nane na vyenye
uchumi.
Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa naomba Mheshimiwa Waziri uliangalie hilo, kuwasha
umeme Kamsamba halafu kinachotutenganisha ni mto haizidi hata mita 500; kwa nini umeme
usivuke ukaja kuvisaidia vijiji vyangu zaidi ya nane ambavyo vina uhitaji huo umeme na
kupunguza gharama?
Mheshimiwa Naibu Spika, halafu tukubaliane vile vile hata kisiasa mnakuwa mmeniweka
mahali pabaya; wananchi wanashangaa kijiji kimoja kimepata umeme ng‟ambo ile, vijiji zaidi
ya nane viko huku vinachelewa kwa Mheshimiwa Silinde ni mambo ya ajabu sana. Kwa hiyo, Mheshimiwa utakapokuwa unakuja ueleze ni kwa nini usitumie ule ule umeme kuvusha huku.
(Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ukanda ule una mito mingi sana isiyokauka na
nilishaeleza hapa kuna mto mmoja unaitwa Mto Nzovwe ulishafanyiwa utafiti kwamba unaweza
kutoa megawati kumi; nashangaa kwanini Serikali haitaki kutumia chanzo hiki kuongeza umeme
katika Mkoa wa Rukwa na umeme ambao una unafuu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nataka Waziri utakapokuja kama ukipata nafasi
unipe maelezo juu ya jambo hili. Nilikuwa na jirani yangu Mheshimiwa Mipata anasema kwake
umeme unakatika katika kwa hiyo, mliangalie na suala la kukatika katika umeme kwenye
baaadhi ya maeneo.
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo naunga mkono hoja lakini naomba
maelezo kutoka kwa Mheshimiwa Waziri.
Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kuweza kunipa nafasi hii ili na mimi niweze kuungana na wenzangu katika kuchangia taarifa za Kamati mbalimbali, Kamati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Kamati ya Maliasili. Kwanza naunga mkono taarifa za Kamati.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuanza nizungumzie mgogoro kati ya wakulima, wafugaji na hifadhi za akiba za ardhi. Tulishazungumza mara kadhaa hapa kwamba zipo baadhi ya akiba za hifadhi ambazo hazina faida zaidi ya miaka 50 na ukimuuliza Waziri hii akiba ya hifadhi hii imeleta faida gani kwa Taifa hili au kwa wananchi hawa zaidi ya askari wa wanyamapori au askari wa misitu kuitumia kwa manufaa yao, kukamata wananchi na kuwatoza rushwa halafu kuwaruhusu wengine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie hifadhi ya akiba ya Uwanda Game Reserve. Hifadhi hii ni zaidi ya miaka 50 na wakati hifadhi hii imetengwa idadi ya wananchi ilikuwa kidogo lakini sasa hivi hifadhi hii inazungukwa na vijiji zaidi ya 15, zaidi ya wananchi 26,000. Kwa hiyo, wananchi wanashindwa walime wapi, lakini hifadhi hii ukiiangalia faida yake haipo matokeo yake askari wanatumia hifadhi hii kwa manufaa yao binafsi. Mwananchi akisogelea hii hifadhi hata kwa kupita tu anakamatwa, anadaiwa pesa, asipokuwa na pesa anakamatwa anarundikwa ndani na wengine wamekuwa vilema, wengine wamepoteza maisha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe mfano, tarehe 2 Januari, 2017, mwananchi mmoja anaitwa Luanda Salanganda Malele amepigwa risasi kwenye goti na askari anayeitwa Limomo baada ya kumkuta nje ya hifadhi. Akaambiwa kuna mtoto wako tumemkamata, akawaambia mimi sina mtoto aliyekamatwa, wakamdadisi kumdai pesa akakataa wakamwambia wewe una mazoea ya kujidai mjuaji tukikuomba pesa hutupati, wakaanza kumtishia kwa risasi. Katika kumtishia akakimbia akaenda kwenye nyumba ya jirani wakamtandika risasi kwenye goti, goti limechanikachanika sasa hivi yuko Muhimbili anasubiri kukatwa mguu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sisi kama binadamu Mwenyezi Mungu kweli anaweza akapenda maonevu ya namna hii? Hizi hifadhi zimewekwa kwa ajili ya binadamu tena tunaita hifadhi ya akiba, tulishasema kwa nini Serikali isipite kufanya utafiti wa kina kuona hifadhi ambazo hazina faida, hata kama zina faida wanaangalia maslahi makubwa ya wananchi waweze aidha kurekebisha mipaka au kuziondoa kabisa. Kwa mfano, Uwanda Game Reserve haina manufaa kabisa kwa Taifa zaidi ya kusumbua wananchi kwa kuwakamata kila siku.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kuna Kamati inapita au Waziri aende kwenye hifadhi hii, akakutane na wananchi aweze kuzungumza nao wamueleze matatizo yao, vinginevyo yatatokea mapigano makubwa sana kwa hali iliyopo sasa hivi. Sisi tumebeba mzigo wa kila siku kutuliza hali hii ya hewa, kwa hiyo, tunaomba Serikali au Waziri afanye utaratibu wa kwenda kukutana na wananchi ili aweze kuwasikiliza na kutafuta muarobaini wa mgogoro huo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ninalotaka kuzungumzia ni uhaba wa ardhi. Lazima tukubali ipo baadhi ya Mikoa au Wilaya zina uhaba wa ardhi na zina uhaba wa ardhi kwa sababu…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuchangia Wizara hii kwa masikitiko makubwa juu ya kero ya wananchi wa Jimbo langu juu ya migogoro ya mipaka kati ya Hifadhi ya Akiba ya Uwanda na vijiji vya Kilangawana, Mpande, Maleza, Legeza, Kapenta, Ngomeni na Nankanga kwa kuweka mipaka hadi katika makazi ya wananchi pamoja na mashamba yao, jambo ambalo limeleta mgogoro mkubwa hadi kuhatarisha amani katika eneo hilo.

Naomba Mheshimwa Waziri afike kutafuta muafaka wa pande zote mbili. Nimemuomba Mheshimiwa Waziri mara kadhaa afike katika maeneo hayo, naomba majibu. Mheshimiwa Waziri kama huwezi kwenda wananchi wamejiandaa kuja ofisini kwake kwa maandamano na tayari wamechangishana fedha za safari hiyo.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Maji na Umwagiliaji
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Naibu Spika, nachangia Wizara hii kama ifuatavyo:-

Kwanza, bajeti iliyotengwa katika Wizara hii haitoshi, Serikali iongeze fedha katika Wizara hii; pili ni kuhusu maombi ya fedha kwa ajili ya Muze Group. Mheshimiwa Naibu Waziri maombi ya mradi huu ni maombi ya kupeleka maji ya mserereko toka chanzo cha Mto Kalumbaleza na mradi huu unatarajiwa kupeleka maji katika vijiji kumi na mbili, kwa nini mradi huu haujatengewa fedha?

Tatu, miradi ya umwagiliaji tumekuwa tukiiombea pesa mfululizo miaka mitano hatujawahi kupewa, tatizo ni nini? Mradi wa umwagiliaji wa Maleza, mradi wa umwagiliaji wa Uzia na mradi wa umwagiliaji wa Msia. Naomba maelezo kwa nini Serikali haitoi pesa katika miradi hiyo ya umwagiliaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii ili niweze kuungana na wachangiaji waliopita katika Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nachukua fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa ahadi zake za kuondoa tozo mbalimbali za mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi, nampongeza sana. Nampongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri na Makatibu wao kwa taarifa yao nzuri. Tunajua ameingia hivi karibuni, lakini taarifa hii inaonesha mtu huyu ana uwezo wa kuibeba hii Wizara. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naipongeza Kamati ya Kilimo, imechanganua vizuri sana. Naipongeza kwa kweli Kamati mmefanya kazi yenu vizuri sana, hongereni sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kilimo ni uhai, kilimo ni viwanda, kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wa Taifa letu. Nchi ikikosa chakula, haina utengamano wa kisiasa, kiusalama na hakuna atakayekusikiliza kwa jambo lolote lile. Ndiyo maana Waswahili wanasema adui mwombee njaa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na hali hiyo, bajeti ya kilimo kama wenzangu walivyotangulia kusema, ni ndogo sana. Hata tuseme maneno namna gani, tutamlaumu Mheshimiwa Waziri bure, bajeti ni ndogo. Sisi wote tuungane kusukuma jambo hili kwamba bajeti haitoshi. Kama kweli kilimo ni uti wa mgongo, ni wazi kwamba tukubaliane bajeti hii haitoshi. Tusiposhikamana, basi tusilaumiane, turidhike na kilichopo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuchukua fursa hii kuwapongeza wananchi wa Mkoa wa Rukwa kwa jitihada walizonazo za kilimo. Wananchi wa Mkoa wa Rukwa hawahimizwi kulima, hapana. Wananchi wa Mkoa wa Rukwa wanaweza kudhoofishwa na kilimo kwa kukosa soko, kwa kucheleweshewa pembejeo, mbegu na kupewa madawa feki. Ukiwatimizia mambo hayo wananchi hawa ni hodari kwa kilimo. Hata mwaka huu wamelima vizuri sana, wafanyabiashara njooni mnunue mahindi mkoa wa Rukwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ninalotaka kuzungumzia ni kilimo cha umwagiliaji. Lazima tukubali kwamba ili twende mbele bila mashaka, ni lazima tukubaliane kwenda kwenye kilimo cha umwagiliaji. Nchi yetu ina hekta za kilimo milioni 29.4 ambazo zina sifa ya umwagiliaji, lakini mpaka sasa tunatumia hekta 463,000 tu. Kwa hiyo, hatujafikia hata 2% ya eneo tulilonalo la umwagiliaji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunafanya nini ili hizi fursa ambazo tumepewa na Mwenyezi Mungu tuzitumie kikamilifu? Kilimo cha umwagiliaji ndiyo kinaweza kulivusha Taifa hili na kuliweka mahali pazuri. Kwa hiyo, tunaomba Wizara na Serikali itambue jambo hili kwamba ni la muhimu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hifadhi ya chakula ni muhimu sana kwa sababu hatuwezi kumpangia Mwenyezi Mungu kwamba mvua hii itanyesha mwaka huu, mwaka kesho; lazima tuweke chakula cha kutosha hata cha miaka mitano. Unapowapa NFRA shilingi bilioni tisa, maana yake unategemea kununua tani karibu 180,000 ambazo ni Mkoa wa Rukwa peke yake unaweza ukatosheleza. Lazima tutenge pesa za kutosha kwa ajili ya kununua chakula cha kuhifadhi kama akiba. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nije kwenye ujenzi wa maghala. Wananchi wetu wakati mwingine wanaharibu chakula kwa hofu ya kwamba mazao yao watayaweka wapi? Yanaweza yakanyeshewa na mvua, lakini tungekuwa na maghala ya kutosha, wananchi wangeweza kuhifadhi mazao yao pale anapokuwa na shida ya kuuza anakwenda anauza. Analazimika kuuza kwa lazima kwa sababu hawana mahali pa kuhifadhi; na uwezo wa kujenga maghala hawana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine nizungumzie migogoro ya wakulima na hifadhi za akiba. Jambo hili limezungumzwa mara kadhaa; lipo tatizo kubwa sana la mgogoro wa Hifadhi ya Uwanda Game Reserve na wananchi. Hili eneo ni dogo. Bahati nzuri nimemwambia Mheshimiwa Waziri mara kadhaa, rafiki yangu, Mheshimiwa Maghembe, ikiwezekana basi aende akaone suluhisho la kufanya juu ya mgogoro ule. Ataacha watu wauane! Aende ikiwezekana akarekebishe mipaka. Namwomba sana angalau uende, wananchi wakuone inaweza kusaidia sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni shamba la Malonje. Shamba hili nimelizungumzia miaka sita. Sijui kuna mwarobaini gani katika jambo hili? Kwa mara ya mwisho amekuja Waziri wa Ardhi, Mheshimiwa Lukuvi akasema mimi ndio nitakuwa wa mwisho kuzungumzia mgogoro wa shamba hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, nami nasema Mheshimiwa Lukuvi ni hodari, anafanya kazi vizuri sana na Naibu wake. Amefanya kazi katika maeneo mengi, tunamsifu, lakini kuna mfupa gani umemshinda katika shamba hili? Kuna tatizo gani? Shamba tumelizungumzia miaka sita na yeye alisema atakuwa mtu wa mwisho kuzungumzia mgogoro huu, kuna tatizo gani katika jambo hili? Huu mfupa hata fisi anang’ang’ania mpaka anaupasua, hata kama ni mkubwa kiasi gani!

Mheshimiwa Naibu Spika, tunamwomba akamalize mgogoro huu, wananchi wamenipigia simu Jumanne wamechangishana pesa wanakwenda ofisini kwake kupata mwarobaini wa jambo hili. Limechukua muda mrefu mno, wananchi hawana mahali pa kulima.

Mheshimiwa Naibu Spika, namwomba sana Mheshimiwa Waziri wa Ardhi, jambo hili walishike vizuri walimalize kwa usalama. Kwanza wanamtia hofu hata mwekezaji mwenyewe, wanamfanya asifanye kazi kwa uhuru kwa sababu ana mashaka na hata wananchi. Pande zote mbili zinahitaji suluhu ili jambo hili liishe na usalama uweze kuwepo.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba na nasisitiza sana, Mheshimiwa Waziri mgogoro huu waweze kwenda kuumaliza ili wananchi waweze kupata mahali pa kulima. Ila namjulisha kwamba wananchi wamechangishana pesa wanakwenda ofisini kwake, vijiji vyote vinavyozunguka shamba lile, Jumanne wanakwenda. Shamba hili limechukua muda mrefu mno.

Mheshimiwa Naibu Spika, nadhani kwa leo naishia hapo. Naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Fedha na Mipango
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuchangia kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja, kutokupeleka fedha kwenye Halmashauri kama zilivyopitishwa katika bajeti. Kama tunavyoambiwa Serikali inakusanya fedha wakati mwingine hadi kuvuka lengo, kwa nini sasa hazipelekwi katika Halmashauri zetu? Kutokutoa OC za Idara za Halmashauri zetu ni kuzidhoofisha na kusababisha makusanyo wanayokusanya kushindwa kufanya kazi iliyokusudiwa na badala yake fedha hizi za makusanyo ya Halmashauri kutumika kama OC.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokulipa madeni ya Wazabuni kwa wakati, wakiwemo Mawakala waliosambaza pembejeo. Hii ni kuendelea kufanya wananchi wafilisike na kufilisiwa na taasisi zinazotoa mikopo ya fedha na vile vile kufanya huduma zilizokusudiwa kutotolewa kwa wakati na kwa kiwango kinachotakiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kushindwa kurejesha asilima 30 ya makusanyo yanayotokana na makusanyo ya kodi ya majengo, hivyo kuyumbisha malengo na bajeti za Halmashauri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nashauri Serikali kuheshimu bajeti zinazopitishwa na Bunge. Matumizi ya fedha za Serikali yafuate bajeti iliyopitishwa na Bunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuzungumza juu ya mgogoro wa muda mrefu wa shamba la Malonje. Serikali inatakiwa kumaliza mgogoro huu ambao Serikali imekuwa ikipiga danadana kila siku. Hakuna jambo linaloweza kushinda Serikali kwani tunashuhudia jinsi Mheshimiwa Waziri Lukuvi anavyojitahidi kutatua migogoro mbalimbali katika nchi hii na mara ya mwisho aliwaahidi wananchi wa Vijiji vinavyozunguka shamba hilo kuwa atakuwa Waziri wa mwisho kuzungumzia mgogoro huo. Hivyo wananchi walishajenga imani kubwa sana kwake kwa kauli aliyoitoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunamwomba aumalize mgogoro huu. Kama kuna makosa yaliyofanywa na viongozi wa Wilaya, Mkoa ndiyo maana yote hayo yamefikishwa kwake hakuna sababu tena ya kukwepa jambo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa Tarafa ya Kipeta na hifadhi ya akiba ya Uwanda Game Reserve. Tunaomba mipaka ichunguzwe upya kwani uwekaji wa mipaka ya hifadhi hiyo imeingilia maeneo ya Vijiji jambo linalofanya wananchi wa maeneo hayo kukosa ardhi ya kilimo na mifugo, tunaomba Serikali ifuatilie jambo hili haraka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wa vijiji hivyo wapo hapa Dodoma kutaka kuonana na Mheshimiwa Waziri Lukuvi, pia ikishindikana kumwona Mheshimiwa Waziri, wamwone Mheshimiwa Rais. Tunaomba wasikilizwe (ni juu ya shamba la Malonje).

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017.
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, maliasili na utalii; naunga mkono taarifa zote mbili na mapendekezo yake yote. Migogoro ya hifadhi za akiba na wakulima itamalizika lini? Upo mgogoro mkubwa kati ya Hifadhi ya Uwanda na wananchi juu ya utata wa mipaka

Mheshimiwa Mwenyekiti, ipo ramani iliyokuwepo toka mwaka 1959 na ikafanyiwa marekebisho mwaka 1974. Cha ajabu ramani zote hizo zinapuuzwa na watumishi wa maliasili na kuingilia makazi ya wananchi. Naomba Wizara ifanye haraka kufanya makubaliano ya mipaka iliyowekwa Kisheria kwa kufuata ramani na siyo kukandamiza wananchi

Mheshimiwa Mwenyekiti, Maafisa wa Maliasili waliopo katika Hifadhi ya Akiba ya Uwanda hula rushwa na kuruhusu mifugo kukaa ndani ya hifadhi hiyo kwa kuwatoza wafugaji fedha kati ya milioni mbili na kuendelea bila kutoa risiti inakuwa ni fedha yao na haingii Serikalini. Majina ya Maafisa hao nilishayapeleka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi Maafisa wa Maliasili wamefyeka mazao ya mwananchi mmoja aitwae Langi Lusangija Nonga, kisa kukataa kutoa rushwa. Naomba Serikali ifuatilie suala hilo

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanyama wanaodhuru; tarehe 9 Januari, 2018 Mamba amekamata mwananchi aitwae Didas Chendelwa katika Mto Momba. Maafisa wa Maliasili wamejulishwa juu ya jambo hili hawajachukua hatua yoyote na mamba hao wanazidi kutishia maisha ya wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi; soko la mahindi linawatesa wakulima wa mahindi. Serikali imewatelekeza wakulima wa mahindi hawana kwa kuuza mahindi yao. Leo hii Sumbawanga debe moja la mahindi ni Sh.3,500 hii siyo sawa kabisa. Serikali itueleze, je, hali hii itaendelea hadi lini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuna tatizo la pembejeo kuletwa kwa kuchelewa, uchache wa mbolea, bei kuwa kubwa ya pembejeo.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, mahindi ni zao la chakula na uzalishaji wake umepanda kutokana na mwamko wa wakulima kutokana na hamasa kubwa iliyotolewa na Serikali. Pamoja na yote hayo ukulima wa mahindi leo hii ni kama adhabu kwani hakuna soko la mahindi, bei yake ni ya chini, gunia moja ni kati ya shilingi 25,000 mpaka shilingi 30,000. Je, kwa bei hiyo mkulima atamudu kununua pembejeo, mbolea, mbegu, dawa na gharama nyingine za kuendesha kilimo?

Mheshimimwa Mwenyekiti, mkulima ataendeshaje shughuli nyingine za maisha huku tukijua kuwa zao la mahindi kwa mkulima ndiyo zao la chakula na biashara. Akiugua anategemea auze mahindi, watoto kwenda shule auze mahindi, kujenga nyumba auze mahindi na kulipa michango auze mahindi. Hivyo, unapofungia mahindi yasipelekwe nje huoni kuwa ni kuwatesa wakulima wakati Serikali hainunui mahindi? Hivi Serikali inataka wakulima warudi kwenye jembe la mkono au kilimo kwa ajili ya familia tu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, bila kilimo hakuna viwanda. Wafanyakazi wa viwandani wanahitaji kula, viwanda vinahitaji malighafi inayotokana na kilimo. Hata bidhaa itakayozalishwa viwandani lazima soko la kwanza liwe wananchi wenyewe. Je, watanunuaje bidhaa kama hawana fedha kwa sababu Serikali imewafanya wawe maskini kwa kutonunua mazao yao?

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, itakuwa ni vizuri wananchi wote wanaolima wahamie kulima korosho? Wakulima waache kulima mzao ya chakula wote wahamie migodini kuchimba madini? Wananchi wa Tanzania wataweza kununua chakula nje?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri wa Kilimo akumbuke maneno yafuatayo ya Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli, alisema:-

1. Mkulima asinyanyaswe.

2. Mkulima asipangiwe bei ya mazao yake hukumsaidia kulima.

3. Hata kama utanunua debe moja la mahindi kwa ng’ombe watatu ni sawa tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais huyu anajua shida ya wakulima cha ajabu Waziri wake anakwenda kinyume na bosi wake. Kwa hali hiyo viongozi tumuelewe Mheshimiwa Rais wetu, tusimchonganishe na wananchi (wakulima).

Mheshimiwa Mwenyekiti, zuio la kuuza nje lina tafsiri kama ifuatavyo:-

(i) Unapomzuia mkulima asiuze mazao yake (mahindi) nje wakati na wewe hununui maana yake ni kumpangia bei wakati hukumsaidia kulima.

(ii) Unaposema wafanyabiashara wakanunue mahindi na kupeleka mikoa isiyo na chakula, je, huyo mfanyabiashara umempatia fedha za kwenda kununua hayo mahindi kiasi kwamba uwe na uhuru wa kumpangia bei ya kwenda kununua hayo mahindi? Je, hao wafanyabiashara utawatafutia soko zuri la kurudisha gharama zao ili wapate faida?

(iii) Unaposema kuuza chakula nje kwa maana ya mahindi/mchele mpaka wa-process wauze unga na mchele. Je, wakulima hao wameandaliwa kuwa na uwezo huo kwa sasa?

(iv) Unaposema wakulima hao kuuza nje wa-process wauze unga/mchele, je, wakulima wetu wamefikia kiwango hicho? Je, ni kila sehemu kwa sasa kumefikiwa na umeme?

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nimwambie Mheshimiwa Waziri wa Kilimo ni uungwana sana ukiaminiwa na Rais tenda haki kwa watu wake na ukiona ngoma ni nzito siyo vibaya kuachia ngazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu afya, nashauri kuwe na mpango wa kumalizia maboma ya majengo ya zahanati na vituo vya afya ambavyo tayari wananchi wametoa nguvu kujenga maboma hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mpango haujaonesha kununua magari ya wagonjwa kwa vituo vya afya ambavyo bado. Mfano, Kituo cha Afya Milepa na Laela katika Jimbo la Kwela - Sumbawanga Vijijini havina magari ya kubebea wagonjwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu umeme, Mpango ueleze juhudi za makusudi kuhakikisha kila kijiji/kitongoji kinapata umeme. Mfano, Jimbo la Kwela lipo nyuma halijapata umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa barabara, naishukuru Serikali kwa kuanza ujenzi wa Daraja la Mto Momba. Naomba baada ya daraja kukamilika ianze ujenzi wa barabara ya Kasansa - Kilyamatundu - Kamsamba - Mlowo kwa kiwango cha lami.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa naipongeza Serikali kwa kazi kubwa inayoifanya katika Wizara hii. Tumeona mambo mengi na makubwa yanayofanyika, ujenzi wa reli, barabara, viwanja vya ndege, ununuzi wa ndege, meli na kadhalika. Hongereni sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, yapo maeneo mbalimbali au Mikoa ambayo haijabahatika kupitiwa na reli, iwe ya zamani au reli iliyojengwa kwa standard gauge. Mikoa hiyo ambayo haipitiwi na reli ipewe kipaumbele kuhakikisha inatengeneza barabara za Mikoa kwa kupitika vizuri ili wananchi waweze kusafirisha mazao yao kwa urahisi (mfano Mkoa wa Rukwa). Barabara ya Kibaoni – Kilyamatundu – Kamsamba itengenezwe kwa kiwango cha lami kwani barabara hii ina umuhimu mkubwa sana kiuchumi kwa wananchi na kwa Taifa zima kwa ujumla.

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ya Kalamba – Nzite – Ilemba ipanuliwe eneo la Mlimani kupunguza miinuko ya milima na kuweka zege eneo lote la Mlimani. Barabara ya Ntendo – Muze ijengwe kwa kwa kiwango cha lami. Eneo la Mlimani lipanuliwe, liwekewe kingo eneo la mlimani na mlima wote ujengwe kwa zege.

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ya Miangalua– Chombe nayo ipanuliwe eneo la Mlimani iwekewe zege eneo lote. Tunaomba ujenzi wa Daraja la Kilyamatundu – Kamsamba lijengwe haraka kama mkataba unavyojieleza.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naunga mkono hoja.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017.
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nashukuru kupata nafasi hii ili niweze kuchangia hoja za Kamati hizi mbili; Kamati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Kamati ya Maliasili na Utalii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa naunga mkono taarifa ya Kamati zote mbili. Taarifa imechambuliwa vizuri; na kwa kweli kama Serikali inaweza ikasimamia utekelezaji wa maazimio ya Kamati, tunaweza tukapiga hatua kubwa sana. (Makofi)

MheshimI Mwenyekiti, nizungumzie suala la kilimo, naona kama Serikali imefika mahali inaenda tofauti na wakulima wa zao la mahindi, yaani wakulima wa zao la mahindi wakizalisha, wakianza kupata soko zuri, Serikali inazuia ili wapate hasara, na mimi sijajua ni kwa sababu gani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama wananchi wangekuwa na fursa ya kuja hapa Dodoma, lugha ambazo wangezisema, Serikali sijui ingesema nini! Sisi tunatumia lugha ya kiuongozi, lakini Serikali ilivyo kwa wananchi ni mbaya mno, wananchi wamepata hasara kubwa mno. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndugu yangu Mheshimiwa Waziri wa Kilimo, wananchi hawakuelewi kabisa! Ni kama Wizara hii haipo kabisa! Cha ajabu mwaka 2017 bei ya mazao ilianza kuwa nzuri, wananchi wakaanza kuuza shilingi 70,000 na shilingi 80,000 kwa gunia. Ghafla tu Serikali ikakata mrija, kwamba hamna kupeleka mazao nje. Sasa kilichotokea, wananchi sasa hivi debe moja la mahindi wanauza shilingi 3,500. Gunia shilingi 21,000. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiuliza Serikali, hivi ina vyombo inavyotizama hali hii? Ina wataalam wanaochunguza hali hii? Hivi Serikali inapata taarifa sahihi za jambo hili? Hali ni mbaya sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakulima wa mahindi wana hali mbaya kupita maelezo. Wamepata hasara kubwa sana. Sasa cha ajabu hata wale waliozalisha kwa sababu hawana maghala ya kuhifadhi mahindi, yamekaa yanaoza, yamepecha, hakuna kwa kupeleka. Sasa mnatarajia nini? Jambo hili linaumiza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile Serikali mwaka 2017 ilisema itapeleka mbolea mwezi Novemba, lakini mbolea ya kupandia inaenda palizi ya pili, halafu mbolea ya kukuzia inaenda wakati mazao yameshakua, ni kinyume kabisa na matamshi ya Serikali. Na mimi nashindwa kuelewa kama Wizara hii ina wataalamu sahihi kweli, lazima Serikali ifuatilie jambo hili, ni maumivu makubwa sana kwa wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine nizungumzie maliasili. Kamati imeeleza vizuri sana juu ya mgogoro wa hifadhi na wananchi. Mimi nizungumzie juu ya mgogoro wa Hifadhi ya Uwanda Game Reserve.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Uwanda Game Reserve ramani yake ya kwanza ilichorwa mwaka 1959 ikafanyiwa marekebisho mwaka 1974 kuonesha kwamba reserve inaishia humu. Cha ajabu kuna mgogoro mkubwa sana. Na mimi niseme kwa ujumla kwamba reserve ile imebaki kama ni ya watumishi wa Maliasili, kwa sababu hata ukienda sasa hivi, wamechukua rushwa, mifugo imejaa mle ndani. Sasa hata reserve yenyewe iko wapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri nimekueleza juzi kwamba ng’ombe wamejaa, lakini wafugaji wanalanguliwa, bila shilingi milioni mbili au tatu huingizi ng’ombe. Hata ukienda sasa hivi, utakuta mifugo imejaa, hakuna hata maana ya reserve.

Mheshimiwa Mwenyekiti, cha ajabu juzi wamemwendea mfugaji mmoja, tena yupo nje ya reserve, wakamwambia tupe hela, akawaambia siwapi hela. Wamefyeka mazao yake. Mimi nimekupa majina ya watumishi hao, lakini nashangaa kwa nini Serikali haichukui hatua? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mgogoro huu umeanza toka Waziri wa Maliasili akiwa Mheshimiwa Maige. Ametoka Mheshimiwa Maige, akaja Mheshimiwa Kagasheki, ametoka Mheshimiwa Kagasheki, akaja Mheshimiwa Nyalandu, ametoka Mheshimiwa Nyalandu akaja Mheshimiwa Maghembe juzi ameenda kujionea, akakuta kweli wananchi wanaonewa. Akatoa suluhu kwamba atatuma wataalam wake kwenda kumaliza jambo hili, lakini mpaka sasa jambo hili bado linaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri ajue, akitaka aondoke hata sasa hivi, atakuta reserve hii imejaa mifugo, wala haieleweki. Kwa hiyo, vitu vingine hivi vinafanya wananchi wapate hasira kubwa sana. Ipo siku moja mtashuhudia mauaji ya ajabu, jambo ambalo siyo zuri kwa nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, namuomba Waziri wa Maliasili, kama atapata nafasi, aondoke hata kesho aende akajionee hali hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni wanyama waharibifu. Juzi mamba amekamata mwananchi mmoja Mto Momba. Tumetoa taarifa Maliasili; Maliasili hawana habari, kwa sababu wanajua kwenda kumuua mamba hawapati rushwa, wamekaa tu wanaangalia. Mimi mwenyewe nimewajulisha, lakini hawana habari na mamba yule bado anavizia wananchi katika Kijiji cha Kipeta na Kinyamatundu. Kwa hiyo, naomba, kwa sababu Mheshimiwa Waziri umesikia, jaribu kuwapigia simu waende wakatatue tatizo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yalikuwa ni hayo tu. Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi. Kwanza kabisa niungane na wenzangu kushukuru Serikali kwa kauli ambayo imetoa asubuhi ya kuwarejesha Watendaji wetu wa Vijiji wa darasa la saba. Ilikuwa ni huzuni kubwa sasa imekuwa furaha, tunashukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichangie hotuba ya Waziri Mkuu katika kipengele kinachohusiana na kilimo. Ukiangalia ukurasa wa 27 katika hotuba ya Waziri Mkuu ameelezea kwa kifupi juu ya uzalishaji wa mazao ya kilimo na biashara. Katika maelezo yake ameelezea ufanisi mkubwa uliokuwa umetokea katika msimu wa 2016/2017 na 2017/2018 kwamba wananchi walizalisha chakula yapata tani milioni 15.9 na mahitaji ya chakula yalikuwa ni milioni 13.3, kwa maana ya ziada ilikuwa ni tani milioni 2.6 na ziada nyingine ambayo ilinunuliwa na NFRA ni tani 26. Ukifanya hesabu unakuta karibu tani milioni 5.5 haikununuliwa na kiwango hicho ndiyo kilibaki kwa wananchi wamehangaika nacho na hawakujua wauze wapi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili linahuzunisha sana katika nchi yetu. Wakulima wa mahindi wamepata shida sana katika jambo hili, wanazalisha kwa jitihada zao na kwa nguvu kubwa lakini wanakosa wapi wauze mazao hayo. Hadi sasa kilio hicho bado kinaendelea, wananchi wana hali mbaya sana hasa Mkoa wangu wa Rukwa ukienda karibu Wilaya zote, ukienda kwenye magulio yale utafikiri watu wana msiba kwa sababu mazao yao wamekosa kwa kuuza na maendeleo yamesimama. Kama mtu alianza nyumba 2015 imesimama vilevile haiendelei. Sasa tunajiuliza hii hali itaendelea mpaka lini? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika maelezo ya kitabu hiki cha Waziri Mkuu hakuna mahali ambapo wameeleza ni namna gani watatatua tatizo hili. Kwa hiyo, wameacha wakulima kwenye dilemma, sasa sijui wakulima wa mahindi waache kulima au ni kitu gani kinatokea. Hali hii ni mbaya sana, uchumi umesimama na wananchi wamefilisika, je, Serikali inakubali hali hii iendelee na hata huu uchumi wa viwanda tunaouzungumzia, vitakuwa na faida gani kama mwananchi hana uchumi wa kununua bidhaa ndani ya kiwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nataka nizungumzie jambo labda Waziri wa Kilimo atakuja kutuelezea ni namna gani mwaka huu amepanga mipango mizuri ya kuwezesha wananchi kuuza mahindi yao ikiwa ni pamoja na kufungua mipaka. Kwa sababu kuacha hali hii kuendelea sioni sababu ya wananchi kuendelea kulima mahindi, watasimama na ndiyo maana hata unaona hata mwaka huu uzalishaji umepungua wameshindwa kununua mbolea kwa sababu hawana pesa, wamelima kienyeji, wamepanda mbegu ambayo sio bora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukizunguka katika Wilaya zetu zote za Mkoa wa Rukwa mazao yapo chini sana hayajastawi, hii ni kutokana na wananchi kukosa fedha za kununulia pembejeo kwa sababu mahindi waliyozalisha hayajanunuliwa na mengine yameoza. Kwa hiyo, jambo hili ni la kuangaliwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine nataka nizungumzie suala la TARURA. Kwanza tunapoingeza Serikali, tuna imani chombo hiki kimeanza kufanya kazi nzuri. Tunachoomba chombo hiki kinapaswa kipewe fedha za kutosha, kisipopewa fedha za kutosha itakuwa ni sawa na Halmashauri zetu zilivyokuwa zinahangaika na barabara hizi zinashindwa kutengenezwa kwa sababu zilikuwa zilikuwa zinapewa fedha kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kutoa pesa hizi angalieni Halmashauri ambazo barabara zake zina changamoto. Kwa mfano ukichukulia Halmashauri yangu ya Wilaya ya Sumbawanga jiografia yake ni mbaya na barabara ni mbaya, hazipitiki muda mwingi kwa sababu jiografia yake imekaa utata, barabara zinaunganishwa na milima. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, ukiangalia barabara ya Mawezunzi – Msia, Miangalua - Chombe – Kipeta, ukija huku Miangalua kuelekea Laela ukizunguka kule Kwakifuti barabara ni mbaya, daraja la Kaengesa limeshabomoka ambalo lilijengwa na Wamishionari sasa hivi halipo, linahitaji pesa nyingi. Barabara ya Kaengesa – Myunga inahitaji pesa nyingi, kivuko cha pale Laela kwenda kwenye hospitali kinahitaji pesa nyingi. Kwa hiyo, tunaomba TARURA waweze kuwezeshwa kupata pesa nyingi ili waweze kumudu kutengeneza barabara hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tumeona Serikali inafanya jitihada ya kutengeneza standard gauge, tunashukuru…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kutumia nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na watendaji wote kwa kazi kubwa wanayofanya Wizara hii. Hongereni sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na pongezi hizo, naomba kuelezea shida na adha kubwa ya ukosefu wa maji safi na salama katika Jimbo la Kwela.

Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na adha hiyo, tunaomba Serikali itupatie fedha za kutekeleza miradi ya maji kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji Muze Group kwa vijiji vifuatavyo ambavyo vinaweza kupata maji katika chanzo cha maji cha Mto Kalumbaleza ni Kalumbeleza, Mnazi (MUA), Mnazi Mmoja (ASILIA), Ilanga, Mbwilo, Muze, Kalakala, Uzia, Isangwa na Kalumbale (B).

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile kuna Mradi wa Maji wa Kifinga kwa vijiji vya Kifinga na Mkamba; na Mradi wa Maji wa Mtowisa ambao unatakiwa kufanyiwa ukarabati na kupanuliwa kwa kuhudumia vijiji vya Mwela, Mtowisa A, Mtowisa B, Lwanji, Ng’ongo na Sontaukia.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia upo mradi wa maji wa kijiji cha Msia na Mradi wa Ilemba unaotakiwa kufanyiwa ukarabati kwa kupanuliwa na kufikia vijiji vyote vya Ilemba A, B, C na Kaswepa.

Mheshimiwa Naibu Spika, upo Mradi wa Maji wa Kaoze Group utakaosaidia vijiji vya Kaoze, Kianda Igonda, Mazinge na Kitongoji cha Kikwale.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kuna Mradi wa Kaesenga Group kwa vijiji vya Kaengesa A, Kaengesa B, Mkunda, Itela, Kitete, Kazi na Kazi Katonto. Vilevile tunao Mradi wa Kijiji cha Lyapona.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo Jimbo langu lina mabonde makubwa na mito mingi inayofaa kwa miradi ya umwagiliaji. Nashangaa kuona Wizara haijatenga fedha za umwagiliaji katika Jimbo langu kwa miradi ifuatayo:-

(1) Mradi wa Umwagiliaji wa Maleza hekta 7000;
(2) Mradi wa Maji wa Umwagiliaji wa Nkwilo;
(3) Mradi wa umwagiliaji wa Uzia;
(4) Mradi wa Umwagiliaji wa Msia;
(5) Mradi wa Umwagiliaji wa Milepa; na
(6) Mradi wa Umwagiliaji wa Ilemba.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia naomba kutoa ushauri kwa miradi ya maji inayojengwa nchini baada ya kumalizika, itengewe fedha za matengenezo (service) kuliko kutegemea michango kuliko kutegemea michango ya wananchi ya shilingi 50 kwa ndoo moja. Kiasi hicho ni kidogo sana, hakiwezi kutosha kutengeneza miradi mikubwa ya maji iliyotumia mabilioni ya fedha.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho naunga mkono hoja. Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa naunga mkono hoja, naomba nitoe mchango wangu kwa kuanza na suala la ukosefu wa gari la wagonjwa. Katika Halmashauri yangu ina vituo vya afya vya Serikali ambavyo ni Mtowisa, Laela, Miwepa, Mpui na Msanda Muungano. Vituo hivi havina gari la wagonjwa isipokuwa ni juzi tu Serikali ilitupatia gari la wagonjwa aina ya P-Suzuki gari ambalo kulingana na mazingira ya jimbo langu tuliamua kulipeleka Kituo cha Afya Laela. Hivyo tunaomba kwa kuanzia tena tupatiwe gari la Kituo cha Afya Milepa kituo ambacho kina msongamano wa wagonjwa na kina hudumia kata saba na kiko katika mazingira magumu kimiundombinu. Pili, ikiwezekana na Kituo cha Afya Mpui nacho kipatiwe gari la wagonjwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu upanuzi wa vituo vya afya, tunashukuru Serikali kutupatia shiligi milioni 400 kwa ajili ya upanuzi wa kituo na kazi inaendelea vizuri, tatizo litakalobaki katika kituo cha afya hicho cha Milepa ni gari la wagonjwa. Tunaomba kutokana na jiografia ilivyo katika jimbo langu, naomba sana tupatiwe fedha kwa ajili ya upanuzi wa kituo cha afya Mpui.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu upungufu wa watumishi wa Wizara ya Afya katika Halmashauri yangu yapata asilimia 67 kwa maana ya waganga, wahudumu, wauguzi, manesi na kadhalika. Tunaomba Serikali ipeleke watumishi wa kutosha. Kwa upande wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya, tunashukuru sana Serikali kututengea shilingi bilioni
1.5 kwa ajili ya kujenga Hospitali ya Wilaya katika Wilaya ya Sumbawanga ambapo Halmashauri tayari ilishahamasisha wananchi kupitia Mkuu wa Wilaya Dkt. Haule akilishirikiana na viongozi wengine Mheshimiwa Mbunge na Waheshimiwa Madiwani. Hadi sasa tumeshafyatua tofali 400,000; pia kutenga eneo hekari 30, tunasubiri fedha zije tuanze kazi ya ujenzi, tunashukuru sana na naunga mkono hoja.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika jimbo langu tunavyo vituo vya afya vinavyoendelea kujengwa kwa kushirikiana na wananchi kwa nguvu kazi na michango mbalimbali. Tunaomba Serikali itupatie fedha za kumaliza ujenzi wa vituo hivyo ambavyo ni Muze, Ilemba, Kaoze,Kipeta na Kalambanzite.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama sera ya Chama cha Mapinduzi inavyoelekeza kuwa na ujenzi wa zahanati kila kijiji wananchi waliitikia wito huo kwa dhati na kuanza kazi hiyo. Tunazo zahanati yapata nane ambazo zimefikia katika hatua ya mwishoni ili ziweze kusajiliwa na kuanza kutoa huduma, na ni kutokana na nguvu za wananchi, michango na kushirikiana na Mbunge wao kupitia Mfuko wa Jimbo ambazo ni zahanati ya Maleza, Mpona, Ilanga, Mumba, Jangwani, Kizumbi, Kazi na Mtapenda. Tunaomba Serikali kuunga mkono kwa kutoa fedha ili kumalizia zahanati hizo haraka ili ziweze kutoa huduma haraka kwa wananchi, ikiwa ni pamoja na kutowakatisha wananchi hao tamaa. Zipo pia zahanati za wananchi ambazo ni kama zifuatavyo; Ngingo, Kawila, Ilambo, Ndelema, Mshani, Sikaungu. Zipo pia zahanati ambazo zilisha anza kutoa huduma, tunaomba Serikali itoe fedha za kuboresha kwa kumalizia majengi zahanati hizo ni Kisa, Msia, Sakalilo, Kisa, Lyapona, Ilembo, Kinambo.
Makadilio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Spika, naomba kuchangia Wizara hii kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, maliasili na utalii kuweka mipaka ya hifadhi ya uwanda iliyowekwa toka mwaka 1959, eneo lililotolewa na wakulima, lakini kwa sasa ramani hiyo imekiukwa na kuingilia makazi ya wananchi katika mipaka ya Vijiji vya Kilangawana, Maleza, Kilyama, Tundu, Legeza, Kapenta, Mkusi Iwelya Mvua na Nankanga. Nataka Mheshimiwa Waziri anipatie majibu kwa hoja zifuatazo:-

(a) Hifadhi ya Uwanda, je, ni mali ya Maafisa Misitu wa Mkoa wa Rukwa?

(b) Kwa nini hifadhi hiyo imejaa mifugo mingi hata uthamani wa hifadhi haupo tena?

(c) Kwa nini wanaingiza mifugo (ng’ombe) kwa kuwatoza pesa kwa manufaa binafsi?

(d) Kwa nini wanaruhusu wakulima ndani ya hifadhi hiyo baada ya mpunga kukomaa wanavuna wao kwa kutumia ukatili wa kinyama kabisa? Naomba nipatiwe majibu katika hoja hizi vinginevyo sitaunga mkono hoja na nitashika shilingi ya Mheshimiwa Waziri wa Maliasili.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja kwanza kwa Jeshi la Polisi kwa kazi nzuri wanayofanya. Pili, nampongeza Waziri Mheshimiwa Mwigulu Nchemba kwa kazi yake nzuri anayofanya. Pia namshukuru sana kwa kutupatia gari la Kituo cha Polisi Mtowisa, ahsante sana. Hata hivyo, palipo na mazuri hapakosi changamoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Jimbo la Kwela yapo mauaji ya mara kwa mara. Kwa mfano mwezi wa Pili Ndugu Paul Kisiwa, Mwenyekiti wa Kamati wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Mtowisa ameuawa kinyama na watu wasiojulikana. Mwezi huu tarehe 2 Mei, 2018 Ndugu Benedict Chapewa, Mtendaji wa Kata ya Mwadui na aliyekuwa Katibu Mwenezi 2010 - 2015 ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaishauri Serikali kukomesha mauaji haya kwa kujenga Vituo vya Polisi kwa na kuvipatia bunduki. Jambo la kushauri ukanda ule wa bonde la Ziwa Rukwa kuwe na Wilaya ya Kipolisi hii ni kutokana na jiografia ilivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine tunaomba Serikali kusaidia vituo ambavyo vimeanzishwa kujengwa na wananchi. Vituo cha Polisi vya Ilemba, Milepa na Kipeta.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Kilimo
MHE. IGNAS A MALOCHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi ili na mimi niweze kuchangia katika Wizara hii ya Kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa, nitangulie kusema moja kwa moja siungi mkono hoja. Siungi mkono kwa sababu nitakazozieleza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkulima wa mahindi katika nchi hii amekuwa kama mfungwa au kuku ambaye mama yake amekufa. Toka mwaka jana Waheshimiwa Wabunge wengi wamekuwa wakizungumzia shida ya mkulima wa mahindi katika nchi hii na mpaka sasa hivi shida hiyo inaendelea. Nilitarajia kwenye bajeti hii kutakuwa labda na maelezo ya kuwakosha wakulima wa mahindi lakini ndiyo inazidi kuwaumiza zaidi. Kwa kweli hii si haki hata kidogo.
(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkulima wa mahindi anauza gunia Sh.15,000, huyu mtu nadhani yuko mbioni kujinyonga, hakika. Kwa kweli kitendo hiki hakiridhishi na hakifurahishi mtu yeyote. Wakulima wa mahindi katika nchi wanateseka sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mbaya zaidi Waziri katika hotuba yake anasema kuuza mahindi nje mpaka apewe kibali, apewe kibali ulimsaidia kulima? Amelima kwa jitihada zake mwenyewe, mkulima wa kijijini kule aanze kushughulika na kibali? Jamani, tufike mahali tuwaonee huruma wakulima yaani mkulima wa kijijini aanze kuangalia na kibali, amelima kwa shida aanze kutafuta kibali cha nini? Kama unaona kuna shida si ununue mazao hayo uyahifadhi mwenyewe kwenye ghala lako? Nunua uhifadhi kwenye ghala si kazi ya mkulima kutunza chakula cha nchi hii, mkulima analima kwa ajili ya kujikimu maisha yake yeye mwenyewe. Mimi nadhani tufike mahali tulione jambo hili, si sahihi hata kidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nazungumza hili kwa niaba ya wananchi. Mimi wananchi wangu wa Jimbo wako karibu 450,000, wamenituma nizungumze kwa nguvu zote jambo hili na linawauma kwelikweli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni kutotenga fedha za kutosha katika kilimo cha umwagiliaji, hii ni ajabu sana. Duniani kote kilimo cha umwagiliaji ndiyo chenye tija. Bahati nzuri katika takwimu zetu zinaonyesha karibu hekta milioni 29.4 tunazo fursa za kulima kilimo cha umwagiliaji lakini katika utekelezaji zilizoshughulikiwa ni hekta 461 sawa na asilimia 1.6. Hivi kweli tuko serious katika kilimo? Hatuko serious katika kilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nashangaa, maendeleo ya viwanda duniani kote yalianza na mapinduzi ya kilimo. Mapinduzi ya kilimo ndiyo yanaleta viwanda. Sasa ni ajabu sana kilimo kinakuwa pembeni. Hivi vipaumbele mnavyoweka mnamuuliza nani? Mtuulize sisi tunaotoka kwa wananchi, ndiyo, mtuulize sisi ambao tunatoka kwa wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais wakati wa uchaguzi alisema wazi kwamba hatambughudhi mkulima, mkulima awe uhuru kuuza kokote anakotaka, sasa haya maneno mnayatoa wapi? Mimi nashangaa Ndugu yangu Mheshimiwa Tizeba siwezi kukulaumu kwa sababu bajeti hii hupangi nyumbani kwako, hivi hawa wataalamu ambao wamesomeshwa na nchi hii wanafanya kazi gani kusaidia wananchi hawa? Kwa sababu hii bajeti Waziri hupangi nyumbani kwako, unakaa na wataalam mnashauriana sasa wanashauri kitu gani, hayo ma-degree waliyonayo ni ya kumuumiza mkulima? Mimi nashindwa kuelewa. Kwa kweli tufike mahali tuangalie jitihada anazofanya mkulima kwa kukimu maisha yake tusimtese kwa kiasi hiki. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni pembejeo. Kila mwaka pembejeo zinachelewa, sijawahi kuona mwaka pembejeo zikawahi au zikakidhi, ni stori isiyo na mwisho, hii stori itaisha lini? Kwa sababu ni mazoea, mimi tangia nimeingia Bunge hili hiki ni kipindi cha pili sijawahi kuona pembejeo zikatosheleza au zikawahi. Pembejeo za kupandia zinakuja wakati wa kupalilia mahindi na za kukuzia zinakuja karibu watu wavune mahindi, huu ni utaratibu wa wapi? Tunaomba Mheshimiwa Tizeba anapokuja kujibu afafanue mambo haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni suala la mawakala. Mawakala hawa ni binadamu kama binadamu wengine, ni wafanyabiashara kama wafanyabiashara wengine. Kama lilitokea tatizo la wizi si mmeshachambua basi tangazeni kwamba idadi ya watu fulani ni wezi hamlipwi. Hivi wote ni wezi kweli jamani, hivi mawakala wote ni wezi? Hii ni dhuluma na Mwenyezi Mungu hapendi dhuluma ya namna hii. Lazima mfike mahali mchambue wezi muwapeleke Mahakamani wenye haki wapate, siyo kwamba mawakala wote walikuwa wezi, hamna kitu cha namna hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu mawakala hawa ndiyo wanaoishi na wananchi na ndiyo wanaosaidia nchi hii katika kuleta maendeleo, sasa leo hii mnawatema kiasi hiki ndugu zangu? Hapana, hii si haki hata kidogo. Jaribuni kuchambua wale waliofanya kazi kwa uaminifu wapate kilicho chao. Kama wengine walivyochangia, wengine wamekufa, wengine nyumba zao zimeuzwa, hii siyo haki hata kidogo. Tunaomba Serikali mjaribu kuliangalia suala hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo nilitaka kuzungumzia ni suala la mbolea. Tunajua Serikali inataka kuleta mfumo wa mbolea inayotengezwa ndani ya nchi tunakubali na kwa jina mnasema Minjingu, hii Minjingu mmeifanyia utafiti wa kutosha? Kwa sababu kipindi kilichopita wananchi walilalamika sana na wengine walipata hasara, hatukatai kama imeboreshwa mtueleze imeboreshwa kwa kiasi gani lakini hata kama imeboreshwa uwezo wa kukidhi nchi hii kwa Minjingu sidhani kama itaweza. Kwa hiyo, lazima hilo nalo Serikali mliangalie, nia ni njema mnataka tuchukue mbolea ndani ya nchi lakini mtueleze Minjingu imeboreshwa kiasi gani na uzalishaji wake uko kiasi gani kama unaweza ukakidhi mahitaji ya wananchi. Kwa hiyo, jambo hili mnapaswa kuliangalia kwa macho mawili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni kushuka kwa bajeti ya kilimo. Bajeti ya kilimo inashuka mwaka hadi mwaka. Mimi nashindwa kuelewa, kwa mfano mwaka jana bajeti ya kilimo ilikuwa ni Sh.150,253,000,000 zilizotolewa ni Sh.27,231,305,232 sawa na asilimia 18, hapa ndipo unaweza ukaona hivi kuna u-serious katika kilimo? Yaani mmetenga bajeti halafu kiasi mnachotoa ni asilimia 18 na mbaya zaidi kwa mwaka huu imeshuka tena hata ile bajeti, kama bajeti imeshuka hivi asilimia itakayokuja ni asilimia 3, hakika. Kwa sababu unaangalia hata bajeti iliyotolewa imeshuka badala ya bajeti ya kile kiwango kilichopita. Jamani msaidie Rais huyu, tunaona kazi nyingi zinaleta ufanisi pale Rais au Waziri Mkuu wanapoingilia kati ninyi wasaidizi wake msaidieni Rais huyu wa wanyonge. Sasa wanyonge wenyewe hawa wakulima ndiyo wanaanza kuteseka, mnaenda kinyume na matamko ya Rais. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni Maafisa Ugani. Tunaomba Serikali iwasimamie hawa Maafisa Ugani. Maafisa Ugani wanafanya kazi wanavyotaka, hakuna anayewasimamia kuleta tija katika kilimo, wanafanya kazi kama wanavyotaka. Tunaomba hawa watu muwasimamie kila Afisa Ugani kwenye eneo lake aeleze ameleta tija kiasi gani na uzalishaji umeongezeka kiasi gani kwa eneo dogo. Wapimwe kwa vigezo vya uzalishaji katika eneo dogo, maana tunaona tu wanakaa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine wapeni mafunzo rejea, mmewapeleka tu hawana mafunzo rejea. Juzi tumeelezwa juu ya wadudu wanaoshambulia mazao mbalimbali sina hakika kama Maafisa Ugani wanapewa elimu hiyo, hawapewi. Tunafanya kazi kwa mikupuo, tungeomba Maafisa Ugani wasimamiwe kwanza lakini wapewe elimu rejea na vilevile wapewe malengo kwamba wewe umepewa eneo hili tunataka kiwango cha uzalishaji kiongezeke kutoka mahali hapa kwenda mahali hapa na anafuatiliwa kila siku.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile ongezeni idadi ya Maafisa Ugani kwa sababu utaalam unasema Afisa Ugani anatakiwa kuhudumia wakulima 1,600. Sasa unaweza ukakuta Afisa Ugani ni wa kata nzima yenye vijiji vitano ataweza kweli na hana usafiri? Kwa hiyo, hili nalo tungeomba Serikali iweze kuliona. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, siungi mkono hoja mpaka nitakapopata maelezo.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukua nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Watendaji wote katika Wizara hii, hongereni sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali imalize migogoro ya ardhi ya muda mrefu inayosababisha wananchi kunyanyasika na kuwa maskini. Migogoro hiyo ni kama ifuatavyo:-

(1) Migogoro kati ya Hifadhi ya Uwanda ya Akiba na Vijiji vya Ilambo, Kilangawana, Maleza, Legeza, Kapenta, Mkusi, Mpande, Kawila na Kipeta.

(2) Mgogoro mwingine ni kati ya Mwekezaji wa Shamba la Malonje na wanachi wa Kata ya Msanda Muungano; tunaomba mgogoro huo ufike mwisho.

(3) Mgogoro wa Gereza la Molo na wananchi wa Kata ya Msanda Muungano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 - Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa naunga mkono hotuba ya Waziri Mkuu. Natoa shukrani kwa Serikali kwa ujenzi wa daraja la Mto Momba linalounganisha Mikoa miwili y Songwe na Rukwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na shukrani hizo, tunaomba sasa barabara ya kutoka Kilyamatundu hadi Kasansa, barabara inayounganisha Mikoa mitatu ya Rukwa, Songwe na Katavi. Barabara hiyo sasa itengewe fedha kwa ajili ya usanifu ili hatimaye ijengwe kwa kiwango cha lami kama ilivyoainishwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutengewa pesa kwa ajili ya kumalizia maboma ya majengo ya madarasa na nyumba za walimu. Katika Jimbo la Kwela lililopo Sumbawanga DC upande wa elimu tunayo maboma 259. Zahanati tunayo maboma 32 ambayo yamejengwa na wananchi yanahitaji fedha za kumalizia. Vituo vya afya vilivyoanzishwa na wananchi saba (7) vinahitaji fedha ili vimaliziwe vianze kufanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tuna upungufu wa watumishi. Upande wa afya tuna upungufu wa watumishi 667 katika Halmashauri ya Sumbawanga DC.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nashauri Serikali itoe mgao wa miradi ya maendeleo na watumishi kwa uwiano ulio sawa bila kuwa na upendeleo. Baadhi ya Mawaziri wanapendelea maeneo yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Ntendo - Muze, tunaomba ijengwe kwa kiwango cha lami. Tunashukuru Serikali katika bajeti ya mwaka 2018/2019 ilitengewa fedha na kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami kilomita 2. Kutokana na umuhimu wa barabara hiyo, tunaomba kilomita ziongezeke walau ziwe kilomita 5 ili kuwatendea haki wananchi kwani barabara hii ina umuhimu mkubwa sana kwao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kukosekana kwa gari katika Kituo cha Afya Milepa. Kituo hiki ni kwa muda mrefu Serikali iliahidi kukipatia gari lakini hadi leo hakijapatiwa. Matokeo yake kimekuwa kikipoteza akina mama wajawazito wengi baada ya kukosa gari la kuwasafirisha kuwapeleka katika hospitali za rufaa kwa ujuzi ulio juu zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Makamu wa Rais, Mheshimiwa Samia Hassan Suluhu, wakati wa Kampeni za Uchaguzi za mwaka 2015 alitoa ahadi ya kujenga barabara ya Mtowisa – Ng’ongo - Kristu Mfalme kwa kiwango cha changarawe. Tunaomba ahadi hiyo itekelezwe ili kumpa heshima mama yetu na kuondoa shida wanayopata wananchi wa eneo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maji bado ni tatizo kubwa katika nchi yetu hususan Jimbo langu la Kwela, nikianzia na Serikali kutucheleweshea kibali cha kutangaza mradi wa maji wa Vijiji kumi unaoitwa MUZE GROUP. Tunaomba kibali hicho kitolewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kushindwa kulipa fedha kwa wakandarasi mfano Mradi wa Maji Ikozi. Naomba Serikali iwalipe wakandarasi hawa ili wasaidie upatikanaji wa maji kwa wananchi wangu.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ina upungufu mkubwa sana wa Walimu na uhaba wa Walimu hasa Walimu wa Sayansi. Vilevile Walimu wa kike, tunaomba Serikali ituongezee Walimu kwani kutokana na tatizo hili mara nyingi Halmashauri hii inakuwa chini sana katika ufaulu wa wanafunzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunazo shule shikizi zifuatazo ambazo zimeanzishwa na kujengwa kwa nguvu za wananchi, lakini Serikali inachelewa kuzifungua na kusababisha watoto wengi kutosoma. Shule hizo ni Kirando na Karanda. Tunaomba shule hizo zifunguliwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunashauri Serikali kupandisha madaraja ya walimu ambapo ni kwa muda mrefu hawajapandishwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni kulipa posho ya mazingira magumu kwa Walimu. Serikali itoe posho kwa Walimu wanaofundisha katika mazingira magumu ya Vijijini kusiko na barabara nzuri, kwani wanatembea umbali mrefu kufuata huduma. Pia wapandishiwe mishahara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baadhi ya shule za Sekondari za Kata bado hazijapelekewa vifaa licha ya kuwa na majengo ya maabara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lipo tatizo la kukosekana kwa mabweni hasa kwa watoto wa kike ambao wanatembea umbali mrefu unaowasababishia kukumbana na vishawishi vingi na hatimaye kushindwa kuhitimu masomo yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kupata muda kuchangia Wizara hii ya Ujenzi. Kwanza kabisa namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniweka hai mpaka siku ya leo. Napenda kabisa kumpongeza Mheshimiwa Waziri Engineer Kamwelwe, Naibu Mawaziri Mheshimiwa Engineer Nditiye na Mheshimiwa Kwandikwa, Katibu Mkuu TANROADS Engineer Mfugale na watendaji wote wa Wizara hii. Vilevile bila kumsahau Meneja wangu wa TANROADS Mkoa wa Rukwa na wasaidizi wake wanafanya kazi vizuri sana, nawapongeza sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuanza napenda kusema kwamba Mkoa wa Rukwa ni mkoa wenye mvua nyingi sana, kwa maana hiyo barabara zake za changarawe ni mara nyingi zinaharibika sana lakini fedha tunazopangiwa ni kidogo sana, hazikidhi mahitaji ya uharibifu wa barabara zile. Nishukuru Serikali kwa ujenzi wa daraja lile la Mto Momba kama wenzangu walivyoshukuru, sasa hivi tumeona urahisi hata malori yanayopita sasa hivi yaliyokuwa yanazunguka kule Kibaoni yamebeba nguzo, sasa hivi yanakatisha yanapita yanaingilia Songwe yanakuja kutokea Kamsamba na kuleta nguzo; tunashukuru sana kwa kweli Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile, tunaishukuru Serikali kwa kilio cha wananchi wa Mji Mdogo wa Laela walikuwa wana kilio cha kivuko lakini kupitia TAMISEMI tumepata milioni 163 kujenga kivuko kile, tunashukuru sana Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nizungumzie barabara ya Kiliamatundu, Muze, Ntendo na Kasansa. Waziri aliyepo sasa hivi ni Waziri ambaye huwezi ukamwambia chochote juu ya barabara hii. Anaifahamu vizuri umuhimu wake na jinsi inavyounganisha mikoa hii mitatu; tunashukuru mmejenga daraja lakini tunaomba sasa muweke nguvu kuiwekea lami. Na mmetenga kiasi cha milioni 180 kwa ajili ya usanifu lakini naona fedha hii sidhani kama inaweza ikatosha kwa urefu wa ile barabara, ile barabara ni muhimu sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Eng. Kamwelwe wewe ni mwenyeji wa maeneo yale, tunaomba kabisa katika awamu yako hii weka nguvu ile barabara iweze kutengewa fedha ili kupata lami; kama tutakosa katika kipindi chako sidhani kama tunaweza tukapata tena. Ni kipindi muhimu kabisa na muafaka kwa sababu unajua umuhimu wa barabara ile kiuchumi, tunakuomba sana utilie maanani katika barabara hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie kipande cha barabara cha Ntendo – Muze. Barabara hii ndiyo inayotumika katika kuingiza malighafi inayotoka ukanda wa Ziwa Rukwa, ni barabara ambayo ipo busy sana muda wote, malori ni muda wote. Nashukuru Serikali mwaka jana mlitupangia pesa tukaweza kutengeneza kilometa 2 za lami lakini nashangaa badala ya kuongeza, mwaka huu mmepunguza badala ya kutuongeza kilometa 5 mmetuwekea kilometa 0.8 badala ya kuongeza. Sasa nashindwa kuelewa ni kwa namna gani tena mnarudi nyuma badala ya kwenda mbele, tunaomba sana Mheshimiwa Engineer Kamwelwe utuongezee pesa hii barabara iweze kutanuliwa na kumalizika kwa haraka.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiacha hilo, barabara hiyo kilometa 8 za Mlima ambao wakati mwingine barabara ni finyu, kama lori lilikwama lingine haliwezi likapita. Nakumbuka mwaka juzi Waziri Mkuu alikwama, tukaanza sisi wote kutafuta namna gani Waziri Mkuu atapita lakini solution ilipatikana, alikuja Katibu Mkuu ambaye sasa hivi hayupo hapo akashauri tuipanue lakini nashangaa katika bajeti hii sijaona. Mheshimiwa Engineer Kamwelwe naomba hilo na lenyewe uweze kuliangalia, eneo la Mwilimani linahitaji kabisa kupanuliwa na kuwekwa zege sehemu zote.

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara nyingine ni ya Kalambanzite – Ilemba kilometa 24; kilometa 12 zipo mlimani. Hii barabara tunashukuru TANROADS ilishaichukua, tunaomba na yenyewe basi iweze kujengwa kwa kiwango kizuri cha changarawe na mlima wote uwekwe zege lakini nimeona kwenye bajeti mmetenga pesa kidogo kama milioni 30, milioni 30 utatengeneza kitu gani?

Mheshimiwa Naibu Spika, ningeomba sana Mheshimiwa Waziri uweze kuliona hili, tena ahadi ya Rais wa Awamu ya Tano aliahidi kuiwekea lami, sasa nashangaa sasa hivi suala badala ya lami hata changarawe, hata kuweka zege mlima wa kilometa 12 tunashindwa kuweka fedha.

Mheshimiwa Naibu Spika, nyingine ni barabara ya Miangalua – Chombe…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa kengele ya pili imegonga.

MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi nami niweze kuchangia Wizara hii muhimu ya Maliasili na Utalii. Kwanza kabisa nimpongeze Mheshimiwa Waziri Dkt. Kigwangalla, Naibu wake na watendaji wote wa ofisi yake. Kwa kweli wanafanya kazi nzuri sana, unaweza kusema sasa Wizara imepata viongozi na sio viongozi wamepata Wizara. Hongereni sana kwa kazi nzuri. Tumeona kuna mabadiliko mengi ongezeko la watalii na mambo mbalimbali. Kwa kweli hongereni sana tunawaombea kwa mwenyenzi Mungu aweze kuwazidishia afaya muweze kuitendae haki nchi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yapo ambayo yanaweza wakati mwingine yakafanywa na watu chini yake na si yeye ni vyema kabisa tukamweleza japo kuwa nimeeleza kwa njia moja au nyingine, nimeona leo hii nirudie. Upo mgogoro mkubwa sana kati ya wavuvi wa Ziwa Rukwa na watu wa Maliasili wa Uwanda wa Game Reserve. Hii uwanda wa Game Reserve miaka ya 60 ilikuwa na squire kilometre 5,000, lakini baada ziwa kupanuka limemeza uwanda mkubwa wa game reserve limemeza karibu kilomita 4,100. Kwa hiyo nchi kavu ya Uwanda Game Reserve ishabakia na kilomita 490, kwa hiyo, sehemu yote ni ziwa

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa wapo wavuvi kutoka maeneo mbalimbali au kutoka mikoa mbalimbali ambao wanaenda kutafuta riziki katika maeneo yale na wanapoingia wanakata leseni za biashara, wanakata leseni za mitumbwi, wanakata leseni za uvuvi, wanakata leseni za mazao ya samaki. Wanaingia kwa njia halali, lakini hawa watu wanasurubishwa, wanakamatwa, wanaharibiwa vyombo vyao utadhani sio Watanzania, utadhani hawalipi kodi. Mgogoro huu ninaozungumza ni mkubwa sana umefika mahali ambapo kama Wizara haitachukua hatua utaleta mgongano mkubwa sana kwa sababu, watu wanaohusika na uvuvi ni watu wa uvuvi. lakini maliasili wameingilia kati kuwa-harass wavuvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kule wanaenda akinamama wajane, vijana wanaotoka vyuoni wanakwenda kujipatia riziki, lakini wanakamatwa. Mpaka saa hivi kuna engine kama tisa zimenyang’anywa, boti 30, engine 17 zimepasuliwa, na engine mbili zimechomwa katika Forodha ya Nankanga na Ilanga. Kwa hiyo namwomba Mheshimiwa Waziri alifuatie jambo hili. Niliongea na Mheshimiwa Kanyasu, sikuongea na Mheshimiwa Waziri, akanimbia atakwenda kuongea na wavuvi aone kulikoni na vilevile katibu Mkuu nimeongea naye, nashangaa mpaka sasa hivi sijaona hatua zozote. Kwa hiyo naomba sana najua amekuja kwangu mara ya kwanza, alifanya kazi nzuri sana na alisharejesha nidhamu, lakini katika hili namwomba tena atafute namna ya kwenda kuumaliza mgogoro huu, wavuvi wanapata tabu sana. wananyanyaswa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikwambie wakati fulani wale watendaji wadogo wanachukua rushwa, kama huna hela unaonekana sio mtu, ukitoa hela wanakuachia tu, wanakuachia uendelee kufanya shughuli zako. Ndugu zangu wapo akinamama wajane wanaenda kujitafutia riziki, lazima ifikie mahali tuwe na ubinadamu. Kama Mheshimiwa Rais anaweza kuwa na huruma ya kusema tuangalie mapori yale ya akiba, tuwasaidie wafugaji na wakulima, sasa itakuwa eneo ambalo lipo ndani ya maji ambalo ni kwa ajili ya wavuvi. Tufike mahali wakati mwingine tuangalie mwelekeo na huruma ya Rais wetu na tumuunge mkono.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nataka hili nilisisitize sana sana hasa kule Ilanga, Ilanga ipo karibu na reserve ya Lukwati. Sasa watu wanaingia kuvua wanakamatwa, wananyang’anywa vifaa, wanapelekwa Mpanda, wanaambiwa kung’oka hapa ni mpaka milioni mbili. Kwa kweli wanawa-harras vibaya sana. Namwomba sana Mheshimiwa Waziri anisikilize vizuri na jambo hili alifuatilie, naona kama hanisikilizi vizuri anashika makaratasi. Jambo hili litaleta matatizo makubwa sana, naomba anisikilize na alifuatilie, wakati anatoa majumuisho alitolee uamuzi. Hizi engine ambazo zimekatwa wazirejeshe, wameziweka tu boti, engine za watu, wamerundika kwenye stoo zao zinafanya kazi gani? Tunaomba Waziri atoe tamko la kurejesha vifaa hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine, nataka nimkumbushe Mheshimiwa Waziri, alipokuja kule kwenye jimbo langu aliahidi kusaidia ile Zahanati ya Maleza ili iweze kumalizika na aliwaahidi kuwachimbia kisima cha maji. Pia wakati Mheshimiwa Profesa Maghembe akiwa Waziri, naye aliwaahidi Kijiji cha Kilangawana kuwapatia mabati 100. Hii ni ahadi ya Wizara, hata kama hayupo tunaamini kwamba Wizara ipo na Waziri yupo, tunaomba atusaidie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni wingi wa mamba katika Ziwa Rukwa. Ziwa hili lina mamba wengi sana hakuna mwaka ambao mambo hawajala watu zaidi wawili watatu. Wanakula watu na wengine wanajeruhiwa, wengine wanakatika miguu, wengine mikono, ni kigugumizi gani kinafanya wasipunguzwe mamba katika hili Ziwa Rukwa? Mamba wapunguzwe, si ni biashara, wanaweza wakafanyiwa biashara ya ngozi, kuliko waendelee kula binadamu, kuwapunguza binadamu na kupunguza nguvu kazi. Ningeomba sana katika suala hili Mheshimiwa Waziri aweze kutusaidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli nirudie kumpongeza Mheshimiwa Waziri, anafanya kazi vizuri na Manaibu wake isipokuwa hawa watu wa chini ndio wanaweka doa katika Wizara hii. Tunaomba sana sana ufuatilie wavuvi hawa warudishiwe haki zao na ikiwezekana Wizara ya Maliasili na Wizara ya Uvuvi wakutane wajadili namna ya watu, wanaoenda kuvua ziwani kwa nini wanakamatwa? Ile ni ajira, wasione vijana tu, hata wa chuo kikuu wanakimbilia ziwani na lile ziwa linachukua mikoa mingi. Ukienda watu wa Mbeya, Songwe wapo kule hata watu wake wa Tabora akija atawakuta, hata watu wa Katavi wapo kule wanajitafuta riziki, tuwasaidie vijana hawa na wananchi hawa waweze kupata riziki na bahati nzuri wanalipa kodi, hawana matatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, nashukuru sana na naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia Wizara hii. Kwanza kabisa nimpongeze Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na watendaji wote katika Wizara hii, lakini bila kumsahau Meneja wetu wa Mkoa wa Rukwa ndugu Chambua anafanya kazi vizuri sana anamwakilisha Mheshimiwa Waziri vizuri sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa lazima tutambue kwamba pamoja na kusudio la kupeleka umeme vijijini, ili kuchochea maendeleo lakini vilevile lazima tukubali nia ya Serikali ni kufanya matumizi ya umeme yawe makubwa ili return irudi Serikalini. Nimeona baadhi ya maeneo kijiji kinapelekewa umeme lakini unakuta vijiji vinne watu wanne ndiyo wamevuta umeme au watano au sita, maeneo mengine yote wananchi wanaangalia umeme. Sasa nasema hivi lazima waangalie vipaumbele katika maeneo ambayo watu wanahitaji umeme na wanataka kuutumia.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano Jimbo langu la Kwela lina vijiji 115, mpaka sasa hivi ni vijiji 16 tu vilivyopata umeme sawa na asilimia 18.4, vijiji 99 havijapata umeme sawasawa na asilimia 81.6 na Mheshimiwa Naibu Waziri anafahamu kabisa amepita katika eneo lile karibu kila kijiji ni kama mji watu wanataka umeme na kutokana na uwezo walionao walishaweka solar ila solar wanashindwa matumizi mengine makubwa. Kwa hiyo tunaomba sana waweze kutupelekea umeme katika Jimbo letu la Kwela.

Mheshimiwa Naibu Spika, utakumbuka mwaka 2014, REA II, walichukua umeme Sumbawanga wakapitisha kwenye Jimbo langu wakapeleka Katavi, wakaacha karibu vijiji sita bila kuweka umeme jambo ambalo kwa wananchi linawaumiza. Mpaka sasa katika Jimbo langu kuna Kata 16 hazijapata umeme; Kata za Kilangawana, Kaoze, Kapenta, Ilemba, Nankanga, Milepa, Zimba, Kalumbaleza, Mwadui, Mfinga, Msandamuungano, Kaengesa, Kanda, Lyangalile na Mnokola, Kata 16 havijapata umeme hata vijiji vyake. Sasa jamani lazima tufike mahali tuangalie hawa watu wanahitaji umeme na bahati nzuri Jimbo langu wananchi wanataka umeme, wafanyabiashara wameshaanza kufunga viwanda vya mashine za kukoboa mchele, lakini wanasubiria umeme wameshafunga viwanda zaidi ya 20 lakini umeme hakuna.

Mheshimiwa Naibu Spika, ningeomba juhudi ile ile ya Naibu Waziri alipofika kule Mto Wisa alisema lazima umeme uwake. Umeme uliwaka pale Mto Wisa lakini waliruka Vijiji vya Kalakala, Uzia, Kifinga, Mkamba, Mwela, havijapata umeme na kule Kilyamatundu alipohimiza kweli umeme umeshawaka lakini haujasambaa kwenye zile Kata nyingine na Mheshimiwa Waziri alifika kule Nyangalua, akahimiza umeme ukawashwa na alisema vijiji vyote vinavyozunguka maeneo yale lazima vipate umeme, lakini mpaka sasa hivi vile Vijiji vya Tunko, Kamsamba, Kavifuti, Movu, Mkowe, havijapata umeme.

Mheshimiwa Naibu Spika, namwomba Mheshimiwa Waziri wahimize na naomba Meneja wetu wa Mkoa wa Rukwa kama kuna bajeti ameleta ya kuomba pesa ya kujaziliza, wampe bajeti ya kutosha, anatusaidia sana na anaweza akawaokoa sana hata kuchelewa kwa wakandarasi, huyu Meneja ana uwezo mkubwa sana, tena nafikiri wakati mwingine angeweza kupewa fedha huyu angeweza kufanya haraka zaidi kuliko hata mkandarasi. Huyu Meneja wametuletea Meneja kweli kweli, anawajibika, si kwa Jimbo moja kwa mkoa mzima. Pia si kwa umeme huu wa REA hata wa TANESCO, anatoa majibu kila siku kwamba kuna tatizo hili na analishughulikia. Naomba sana kama amepeleka bajeti, wamsaidie bajeti yake ipite, atatusaidia sana katika kueneza umeme katika maeneo hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nahimiza sana Wizara wanajitahidi, Waziri anajitahidi, Naibu Waziri anajitahidi ila tunaomba sasa waongeze kasi na wanapopeleka umeme waangalie maeneo ya Jimbo la Kwela, wananchi wanahitaji umeme. Lile Jimbo hatuna shida, wanavuta hata umeme wa TANESCO kutoka Sumbawanga, itakuwa umeme wa REA? Watuletee umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo nashukuru sana na naunga mkono hoja. (Makofi)