Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Riziki Shahari Mngwali (28 total)

Mapendekezo ya Mpango wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali katika Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. RIZIKI S. MNGWALI. Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nianze nami kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia hiki alichotujalia ambacho hatukukipata kwa ujanja wetu, bali matakwa yake. Pia nikishukuru chama changu kwa kuniamini na kunifanya na mimi kuwa miongoni mwa wawakilishi wake hapa Bungeni.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze pale ambapo aliishia au point ambayo aliisema Mheshimiwa Jesca kuhusu suala la utawala bora, lakini naongeza pale kwamba huu Mpango wote umejiegemeza kwenye hali ya utulivu na amani. Sasa hili ni jambo ambalo tumekuwa tukiliimba sana Watanzania. Wataalam wa masuala ya amani wanatuambia negative peace siyo peace ya kujivunia. Kwamba kusema nchi haina vita, halafu mkajidai kwamba mna amani, nchi hii haina amani ya kuweza kuhimili mipango kama hii. Hiyo inawezekana imechangia kushindwa kwa hiyo mipango ambayo tulikuwa nayo huko nyuma ambalo si tatizo kuwa na mipango Tanzania bali ni utekelezaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, huwezi ukawa na mipango kama huna utawala bora. Suala la Zanzibar tumelisema humu, nalisema na tutaendelea kulisema, si sahihi Serikali ya Muungano kukaa kimya wakati inaona hali ya usalama Zanzibar inazidi kudidimia. Tunarushiwa taarifa kila siku, watu sijui wanaitwa mazombi, kule nyuma mnakumbuka kulikuwa na kitu kinaitwa janjaweed, wana-terrorize watu katika mitaa ya Zanzibar, Serikali ya Muungano imekaa kimya, tunaimba tuna amani, hatuna amani kwenye nchi hii. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, utawala bora hauendi, labda mtueleze Serikali Kuu, kwa nini hatuna Meya Jiji la Dar es Salaam mpaka leo? Kwa nini mnashindwa kuthamini mapenzi na mapendekezo na maamuzi ya wananchi? Hilo ni kwamba nasema mpango wote huu umejiweka mahali sipo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna masuala maalum machache ambayo pia ningependa kuyazungumzia. Suala la miundombinu kwa mfano, kumetajwa humu bandari na niliwahi kusema hapa wakati ule wa semina, kwamba tunajivunia vipi sisi bandari zetu au tunazitumia vipi sisi bandari zetu kuonesha kwamba kweli, tunanufaika na eneo letu au kuwepo kwetu kijiografia. Nchi ambayo ina pwani ndefu tu, lakini pia tumezungukwa na majirani wengi ambao ni land locked countries. Sasa hii economic diplomacy yetu inakwenda wapi ikiwa tunashindwa kutumia fursa hata hizi ambazo tunazo kihistoria. Nchi zinazotuzunguka tuna historia nazo ndefu za mahusiano, lakini tumeshindwa kutumia nafasi yetu hii ya kijiografia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika miundombinu pia wakati mwingine naona kwa mfano, kwenye mwelekeo; kama kunazungumziwa au kunatajwa variables mchanganyiko. Kwenye eneo la anga wakasema katika mambo yaliyofanyika ni kujenga uwanja wa ndege wa Mafia. Sasa ule uwanja wa ndege wa Mafia ni kwa ajili ya watu wa Mafia au wale watalii wanaokwenda kule na ni ndege gani hizo hizi za tropical sijui za watu 12, 13 hizi. Ndiyo kweli tunaeleza kama ni success story! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wa Mafia wanaendelea kudhalilika na usafiri, usafiri wa maji ni mbovu kabisa, wala hatujui kwa nini Serikali bado inaendelea kuangalia hali kama ile. Ndege siyo ile inayozungumziwa hapa na kiwanja cha Mafia kile siyo kwa manufaa ya watu wa Mafia. Kwa taarifa yenu tulishaahidiwa uwanja wa Kimataifa wa ndege na wala hatujauona.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la ukusanyaji wa mapato. Ukiangalia sioni jipya, mpaka wanazungumzia sasa kuhakikisha, kuorodhesha ile, kwamba majengo yote, sasa haya mambo mbona ni yale yale tu, hakuna jipya kwenye maeneo hayo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, specifically pia nataka kuzungumzia hili suala la kuondoa utaratibu wa retention. Jamani tunataka kuua na hizi Taasisi. Sasa Serikali hii ya Awamu ya Tano ni mabingwa wa kushtukiza, sasa nawaomba wazee wa kushtukiza, msishtukize kwenye retention. Taasisi hizi zilipokuwa zina-retain some money, angalau zilikuwa zinajiendesha jamani, OC haiendi kwenye taasisi hizi miezi mitatu, minne mpaka mitano. Sasa mnatarajia ziende vipi hizi Taasisi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, huko nyuma kuna mwalimu alirudisha watoto wa boarding nyumbani, akasema hana chakula, wakamjia juu hapa, ndiyo hali halisi. Hizi taasisi za umma, kikiwemo Chuo cha Diplomasia, mimi nimetoka kule na tulikuwa tuna hali ngumu, OC haziji halafu mnaondoa na retention, naomba mkae makini kabisa, msije mkaziua na hizi taasisi, mkazikosesha uwezo wa kufanya kazi na kutimiza majukumu yao ambayo mmewapa kisheria.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la afya. Orodha hii hapa inasema lakini sioni wapi wamezungumza specifically kuweka wafanyakazi wenye sifa vile inavyopaswa. Huwezi tu ukazungumzia kwamba nitahakikisha dawa zinapatikana. Hivi mnajua kuna zahanati ambako wale watoa dawa hawana sifa za kutoa dawa na siyo tu kwamba anatoa dawa yeye ndiye anamwona mgonjwa halafu yeye ndiye anasema wewe mgonjwa ukapimwe nini, halafu yeye anainuka anakwenda kumpima mgonjwa na kisha anasoma kile kipimo alichopima mwenyewe, halafu anakuja kuandika dawa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa suala si dawa tu, hizi dawa nyingi kwenye zahanati zetu huko kwingine, ni sumu kwa sababu zinatolewa na watu ambao si wenye sifa. Zahanati kadhaa Mafia zinahudumiwa na wahudumu wa afya, sio hata matabibu au wauguzi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa jamani tuwe makini, kwa sababu huu mpango wenyewe wote unasema pamoja na yote lakini unataka maendeleo ya watu. Maendeleo ya watu gani hayo ambao wale tulioko pembezoni, Mkoa wa Pwani pembezoni, sasa Mafia pembezoni mwa pembezoni. Haitufikii mipango kama hii, haionyeshi kwamba humu kweli yale masuala mahususi yanayotajwa au yanayogusa au yanayoathiri maisha ya wale maskini zaidi au walio pembezoni zaidi yanabebwa katika mipango kama hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie labda la mwisho, nizungumzie suala ambalo niliacha kulitaja pale kwenye miundombinu, kwamba tunaposoma watu wa Mafia kwamba kinatafutwa kivuko cha Dar es Salaam – Bagamoyo, wakati sisi hatuna meli ya kututoa Mafia kutuleta Dar es Salaam, tunaona tunazidi kunyanyasika katika nchi yetu hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa taarifa yenu tu niwaambie kwamba kuna gati kule limejengwa la mabilioni na limekamilika toka mwaka 2013 lakini mpaka leo hii wananchi wa Mafia hawana usafiri wa kuaminika wa meli na humu sioni ile investment yote ile imetajwa itashughulikiwa vipi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana mwanafunzi wangu mwema wa Chuo cha Diplomasia. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nami nianze na ada ya kumshukuru Mwenyezi Mungu muumba mbingu na ardhi ambaye kwa utashi wake ametuchagua mimi na nyote mliomo humu ndani kuwa na afya njema na kuwa hapa kwa wakati huu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nami naomba nichangie kwa kiasi Mwenyezi Mungu atakachoniwezesha kwenye mjadala huu wa Wizara hii muhimu sana. Nianze kwa kuwaombea dua au kuwatakia kheri wale waliopewa jukumu hili na kuwapa nasaha kwamba walichukue hili kama ibada, wanalifanya kumridhisha muumba wao lakini pia wanalifanya kama wajibu wao wa kijamii ambao wamekabidhiwa na wamekabidhiwa kwa sababu wameonekana wanaliweza. Mimi na wengine wengi tunawaombea Mwenyezi Mungu awawezeshe katika kutekeleza jukumu hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wengi wamechangia nami kila nikifuatilia nazidi kupata wasiwasi. Nikasema labda tuna haja ya kubadili hata hii approach ya kufanya hizi budgeting. Nilikuwa nimesema labda ianzie kule mwanzo kabisa, kuna need ya some sort of brainstorming session ya hawa Mawaziri wetu na watendaji wao wakuu, ile tuliyokuwa tunaita semina elekezi lakini wakae pamoja wakaja na kitu kuna wataalam wanakiita mind map, inakuwa huge thing ambayo inatoa matawi chungu nzima, katikati pale ipo Tanzania halafu kuna hizi Wizara sasa, kila Wizara ipo peke yake inatoa mkia mmoja halafu kila Wizara ina nini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachoona hapa tukifanya hili zoezi, mwisho wa yote hayo iwe kwamba, lile jambo linatutengenezea system ambayo itakuwa inafanya kazi in a very integrated way yaani iunganeungane. Isiwe kama sasa hivi nahisi kama vile afya wako wenyewe wakija na bajeti yao inaanza upya, elimu wapo wenyewe wakija hapa na bajeti yao inaanza upya kama yenyewe isolated thing siyo kama party of the whole thing. Nadhani tuna haja ya kufanya hicho na vilevile iendane na periodic assessment. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, inanisikitisha hii na bahati mbaya ndiyo nimeingia kwa mara ya kwanza, bajeti inakuja hapa halafu tunaambiwa katika maelezo mwaka jana tulipangiwa shilingi bilioni kadhaa, Bunge likaidhinisha shilingi bilioni kadhaa, lakini tulichopewa ni shilingi milioni kadhaa. Halafu mwakani tukija tunaacha yote yale tunaanza upya, mwaka huu tunaomba kadhaa, sasa hivi hatuendi. Lazima tukishajenga hii system inapokuwa na input process, output na feedback, feedback itumiwe tena kama input tunapoanza second round ya ile process. Isiwe kila mwaka kama tunaanza upya mambo ambayo kwa kweli nadhani hayatatufikisha mahali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba tuliangalie hilo kwa upana zaidi na tuone namna gani tunaifanya hii system yote ifanye kazi kwa pamoja, kwa sababu mwisho wa yote ni Serikali hii moja ambayo ndiyo inatakiwa ihudumie wananchi hawa wa Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, yamesemwa mengi masuala mahsusi nami naomba nianze kwa lile suala la kuwa na mahitaji ya ma-specialist wetu. Niwapongeze kwanza wafadhili wetu, they are really friends in need and they are friends indeed kwa sababu kama wanatusaidia kwenye program kama hizi ambazo Dkt. Othman na timu yake wanafanya sasa hivi katika Kanda mbalimbali za kuhudumia watoto wetu wenye vichwa vikubwa. Kwa kweli ni msaada mkubwa na hawa watumishi wetu pia tunawapongeza na tungependa kuwe na mifano kama hii mingi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wale ma-specialist wetu wa maeneo mbalimbali waje na some sort of a proposal kwamba wanawezaje wakafanya kazi, labda Serikali na wapenzi wetu wengine watusaidie kutafuta funds ili hawa wataalam wetu, ma-specialist watakuwa wana-move. Kwa kweli ni msaada mkubwa sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, imagine watoto hawa wote wabebwe na mama hawa kutoka mikoa mbalimbali wakajazane pale MOI - Muhimbili hali ingekuwa vipi? Tunawapongeza na tunawaombea Mwenyezi Mungu awalipe kwa hayo mnayoyafanya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuongelea Taasisi ya Saratani Ocean Road. Nimeangalia kwenye bajeti yao kwenye hili book kama ndiyo liko sahihi, kuna zero zero, eneo la preventive and cure, actually hata sehemu ya cure pale kwa Ocean Road kuna zero bajeti. Ukiangalia pia kwenye zero budgeting issue nyingine iliyotajwa ni ya HIV/AIDS na kwenyewe kuna zero, sasa nikasema hii kidogo inaleta wasiwasi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, taasisi hii ya saratani ni moja ya maeneo yale very sensitive. Niliwahi kuzungumza na mtu ambaye yeye aliishi Ujerumani akasema Ujerumani ndiyo mabingwa sana wa haya mambo ya saratani. Hata hivyo, kuna marafiki zake walitutembelea, walipokwenda kwenye taasisi yetu ile wakasema hata vile vifaa vyenyewe havifai kufanyia hiyo tiba tunayofanyia sasa hivi. Nikapata wasiwasi kwamba kama hiyo ndiyo taasisi tunayoitegemea countrywide kuhudumia wagonjwa wetu hawa, halafu na bajeti yenyewe inakwenda hivi, kwa kweli ni hali ya hatari sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye taarifa ya Kamati pia wameeleza vizuri mambo haya. Sidhani kama inaleta maana sana kusema vinahitajika vifaa vya shilingi bilioni sita lakini tumewapa shilingi bilioni mbili. Nina imagine lidude kama X-ray machine kama ni ya shilingi bilioni nne umewapa shilingi mbili sasa wanunue kipande au inakuwa vipi? Kama tumepewa hizi shilingi bilioni mbili mara hii, kwa hiyo tuziweke na je mwakani bei inakuwa ile ile au vipi? Nadhani tunatengeneza environment ambayo tunaji-defeat sisi wenyewe pamoja na kuwa na mipango mingi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kabisa Taasisi ya Saratani iangaliwe upya. Iangaliwe upya pia hata kuwasaidia kujipanga wenyewe namna wanavyotoa huduma. Nimesikia vilio vya wagonjwa au wasindikizaji wao wanasema eti wanaamka alfajiri makwao wanakwenda kusubiria pale kupimwa au kupata huduma na inaweza ikafika saa tatu ya usiku hawajahudumiwa, jamani tuwaangalie hawa wenzetu. Kwa kweli ni hali mbaya na tuwasaidie hawa watendaji wetu wawe kwenye environment ambayo kidogo ni rafiki isijekuwa mwisho wa siku na wao pia tukawa tunawadhuru kwa sababu ya kufanya kazi kwenye mazingira ambayo siyo sahihi. Kwa hiyo, naomba sana taasisi hii iangaliwe. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda niseme kwa uchache kuhusu ndoa za utotoni. Kwa sababu niliwahi kujiwa siku moja yaani watu wana jambo linawakera kweli kweli, nini mwalimu tukasaidiane, kitu gani kuna ndoa za utotoni. Kwa nini mimi, aah kwa sababu Waislam tumeonekana ndoa ziko nyingi. Nikamwambia kama ndoa Waislam wanafanya ndiyo ibada kwa sababu ndoa ni nusu ya dini yao lakini ni sunna. Sasa nikasema kama ni Waislam hawatokimbilia kwanza kwenye ndoa watakimbilia kwenye elimu kwa sababu elimu ni faradhi yaani jambo la lazima, sasa wanapataje matatizo haya Waislam? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tatizo linarudi pale pale kwamba kila kitu tunachukua in isolation. Kama tungekuwa na mfumo ambao watoto wetu watasoma pamoja na wasichana wetu mpaka form four, a minimum atakuwa tayari ana miaka 17 akija kuolewa mwakani ana miaka 18 mpaka akipata ujauzito ana miaka 19 ndiyo amewahi huyo. Sasa tutazungumza lini haya mambo ya ndoa za utotoni. Kwa hiyo, hili jambo linakuja kwa sababu approach na mambo yetu tunafanya kwa namna ambayo siyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna waliowahi kusema hapa, tutengeneze mifumo ambayo watoto wetu wote watapata hizi huduma za lazima katika ule umri wao na tunawakuza hivi watakapofikia mahali wanapoanza utu uzima ndiyo haya majukumu mengine ya kiutu uzima na wao yanaendana nao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, siyo suala tu kwamba kuna ndoa za utotoni lakini naona zaidi tatizo ni mimba za utotoni kwa sababu nilikwenda Muhimbili siku moja, Manesi tena wanawachekea hasa, wanasema wapisheni hao chekechea, nawauliza chekechea ni akina nani? Wasichana wale ambao wamejifungua wote wapo kwenye wodi, watoto wao wako huko chini sijui kwenye incubators lakini majority of them wala hawakuolewa. Kwa hiyo, tatizo ni mimba hizi na wala siyo ndoa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia twende mbali zaidi tu-define huyo mtoto ni nani kwa umri wake ambao sikuona humu kwenye kitabu cha Mheshimiwa Waziri. Tukimsema huyo mtoto ni nani, halafu tujipange sasa kuhakikisha huyu mtoto tuliyem-define tunamuwekea mazingira mpaka amalize utoto wake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 20 16/2017 - Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora
MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Bismillah Rahman Raheem, Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, muumba mbingu na ardhi, aliyenijalia mimi na sote tuliomo humu ndani uzima na tukawa hapa leo, kwa matashi yake tu na siyo kwa ujanja wa yeyote katika sisi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia nishiriki kidogo kuchangia katika mada ambazo ziko mbele yetu hapa. Nianze kwa nasaha, nafanya hivi kwa sababu kuna wenzangu kadhaa walipokuwa wakichangia wameonesha kama kukata tamaa; kwamba tunasema tu Mheshimiwa Mtolea mpaka akasema it is boring kusema hilo hilo, kweli wana falsafa wengi tu wanatuambia, kufanya jambo lile lile kwa namna ile ile, ukatarajia mambo tofauti kuna tatizo. Lakini mkubwa zaidi kwenye falsafa Mwenyezi Mungu, pia naye anaonya kuhusu hilo, kwa kemeo kubwa kabisa kwamba hao anawaita ni wale ambao wana mioyo hawaelewi kwa mioyo, wana masikio hawasikii kwa masikio hayo, wana macho hawaoni kwa macho hayo, na hilo ndio Mwenyezi Mungu anasema ni dalili na ndiyo njia ya kuangamiza jamii, hebu tusiende huko. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa na kwa nini tunaendelea kusema, tunaendelea kusema kwa sababu Mwenyezi Mungu huyo huyo, ametuambia kumbusha. Hakika ukumbusho huwafaa wenye kuamini na mimi naamini sote humu ndani tunaamini, kwa itikadi zetu tofauti, kwa sababu tulishika kitabu cha Mwenyezi Mungu, kwa kila mtu kwa imani yake, tukiamini na tukiahidi kwa yule, nguvu hiyo ya juu, kwamba atusaidie kuendesha nchi hii kwa uadilifu na kwa maslahi ya sisi tuliopo na mustakabali wa vizazi vijavyo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba nianze pia kwa kusema kwamba katika mambo ambayo hayapendezi ni kufanya haya mambo as formality, budgeting is a very serious process activity kwenye nchi jamani, kupanga ni kuchagua. Sasa tunafanya bajeti gani hapa ya kuigiza igiza tu, tunapitisha pitisha tu, hata tukisema hili halijakaa sawa twende tu, amesema mdogo wangu Sophia pale, tunakwenda kwa mambo ya kiitikadi za vyama, vyama tutaviacha hapa, siku ya siku utaulizwa wewe na kile kitabu ulichokishika pale na siyo chama chako.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mambo mengi siyo halisia humu, kuna takwimu zinatajwa, kuna maelezo yanatolewa yale maelezo tumekuwa tukiyasema, tukiyasoma, tukiyasikia siku zote hakuna kilichobadilika. Kwa nini tuwe ni jamii ya kwenda kwa kauli mbiu na misamiati, mara kasi mpya, mara kasi zaidi, mara hapa kazi tu, tuko pale pale, tubadilike ndugu zangu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme elimu inasemwa hapa, elimu bure kila mtu anapiga makofi, kwenye Jimbo langu la Mafia nilipokuwa natembelea shule kadhaa zote zipo kwenye hali taabani. Mwalimu mmoja akaniambia Mheshimiwa sasa tunarudishwa analogue, ametumia term hiyo, akasema sasa kwa hii mnayotuambia elimu bure mmeturudisha analogue, hatuwezi tena kuchapa hata karatasi tuza mtihani wa mwisho wa mwaka. Ule uwezo mmetunyanganya, mmetuletea wanafuzi hatuna mahali pa kuwaweka, walimu wenyewe hatuna mahali pa kukaa, tunasema elimu bure, watu wamependa hawakupenda wafanye nini, hebu tuseme na mioyo yetu katika haya tunayoyafanya. Tusishangilie namba tu, quantity haina maana yoyote. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mafia nilipokuwa na shule moja ya sekondari sikupata division one, sasa hivi kuna shule sita hakuna division one. Tofauti kati ya watoto 39 na watoto 400 haipo, kwa nini tunashangilia hii namba isiyokuwa na maana? Hebu tuende kwenye quality, tusisingizie tu kwamba mbambo yamekaa sawa, mambo hayajakaa sawa na kuna mengi wengine wamesema kuhusu elimu, matatizo yaliyopo, wala sina haja ya kuyarudia kwa sababu muda wenyewe haupo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu afya, Serikali ya Wilaya ya Mafia ndiyo zahanati ya kijiji cha Kilindoni, na ndiyo kituo cha afya cha kata ya Kilindoni. Maabara yake kwa wakaguzi wa Wizara ya Afya haifai ilikuwa ifungwe, Maabara ya Wilaya ya Mafia, hospitali yake kwa vigezo vya wakaguzi kutoka Wizarani Serikalini kwamba ile ni unqualified kabisa ifungwe. Lakini tunaifunga? Tunao madaktari? Hatuna x-ray sasa hivi, hatuna ultra-sound. Kibinadamu tunasema tulimpoteza mtu kwa sababu hiyo tu. Alipata ajali ya kugongwa na pikipiki, ikashindikana kumfanyia x-ray, usafiri Mafia hakuna, ndege hizo tunazosifia na airport sijui ni wale private wanaleta watalii wao basi, mpaka alipopata ndege siku ya pili amekata roho kabla hata hajafika Kilwa kwa sababu ndege ilikuwa inapita Kilwa kabla ya kuja Dar es Salaam. It is a Coastal Air wanapeleka watalii wao kwanza, kabla ya kutoa huduma kwa Watanzania. Jamani hii ndio hali ambayo tunakwenda nayo, tunashangilia humu, haifai. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niliwahi kusema wakati fulani, kuna zahanati ambayo inafanya kazi ya kituo cha afya, mbaya zaidi anayetusaidia pale ni Medical Attendant, is not even a Medical Officer, au ni nurse not even a nurse, a Medical Attendant. Halafu mwenyewe huyo anamuona mgonjwa, akimaliza ile karatasi yake pale anaenda kumpima maabara, akishamaliza yeye anasoma yale matokeo aliyoyapima, halafu yeye anamuandikia dawa huyu, nimesema hapa miezi miwili iliyopita.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni nchi gani, hii ni Serikali gani isiyokuwa na huruma na watu. Hapa halafu tunazungumzia utawala bora, utawala bora gani ambao una watumishi ambao ni very insensitive, ina watumishi na watendaji na viongozi ambao wanagawa jamii kimaeneo. Sisi watu wa pembezoni tutaendelea kuwa wa pembezoni, inagawa watu kijinsi wanawake waendelee kufa tu kwa sababu afterall ni 400 tu, kiitikadi na kidini, kwa nini tunakuwa na nchi ya namna hii, utawala gani huu usiofuata sheria, usiojali haki za binadamu? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Mashekhe limesemwa siyo leo, siyo jana, wala siyo juzi, kosa lao nini, hatuambiwi. Sijui kama nitauruhusu mshahara wa mdogo wangu kaa vizuri tu, tutaelezana vizuri. Tunaambiwa kuna memorandum of understanding, waislam wamelalamika jamani wamepewa upande mmoja tu, sisi hatuna hatupewi majibu, tunafanyiwa kejeli. Waislam walilalamika pia kuhusu NECTA, kwamba hawakuwa na imani na Mtendaji Mkuu pale, ikaundwa Kamati kufanya uchunguzi, hatukuambiwa matokeo yake lakini mtu huyo huyo amekwenda nafasi ya juu zaidi na mbaya katika eneo lile la elimu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mnataka waislam wasimame wapi, waielewe vipi Serikali hii, sipendi kuzungumza maneno yanayoonesha division, lakini is a very serious thing, ukiwa na Serikali ambayo ni very sensitive, ukiwa na watendaji ambao in very sensitive, hiyo tunajichimbia shimo jamani, tutaangamia na binadamu akifikishwa pahala ambako he has got nothing to lose ila roho yake wala haoni hata hiyo thamani ya roho. Roho ina thamani kama itaishi maisha ambayo ni quality, lakini roho ambayo inaishi maisha ya kubangaiza, maji hajui, kula yake hajui, vaa haijui, nyumba anayokaa haielewi hayo siyo maisha ndugu zangu tutumie budgeting process seriously, tupange mambo kwa ajili ya jamii yetu, tuweke vitu vyenye kueleweka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa muache Mafia kuendelea kuifanya sehemu ya pembezoni, hivi kweli mnanipangia DAS Office budget ya usafiri in country laki nne. Tumelia mara ngapi jamani msitumie kigezo cha watu tu, tumieni geographical factors pia. Kumsafirisha mtumishi kutoka Mafia afike headquarter ya Mkoa wa Kibaha, ni ghali kuliko kumsafirisha mtumishi kutoka Kinondoni akaenda Morogoro, sasa nawaambia kama mnaona laki nne zenu ni nyingi sana, au kama watumishi wa Mafia hawaitaji maslahi mazuri, pesa yenu bakini nayo, nitatoa pesa mara nane yake, hiyo mliyopanga ninyi nitatoa quarterly kwa ajili ya kuiwezesha Halmashauri yangu ifanye kazi, hata hili jamani hebu tuhurumieni. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mambo mengi mahsusi ambayo ningeweza kuyachangia lakini nina wasiwasi sana na suala la muda. Watumishi sasa hivi sijui hii by-law imetoka wapi, kwa nini hii TAMISEMI Head Office isiwe ndiyo mwajiriwa wale watumishi, walimu, watumishi wa afya na wengine, badala ya kuiweka Halmashauri ambazo baadae zinanyanyasa watu. Mwalimu amekaa kituoni miaka kumi, anaambiwa huondoki mpaka ulete mbadala, yaani mwajiriwa akatafute mwajiriwa mwenzie akamlete Mafia, kama yeye anapaogopa yule mwingine atakujaje? Hebu jamani tuwe na utaratibu.
MWENYEKITI: Mheshimiwa muda wako umekwisha.
MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti nakushukuru, ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, muumba wa mbingu na ardhi kwa kutujalia sisi sote uhai, uzima na fursa ya kuwa hapa leo.

Pia nakushukuru wewe kwa kunipa fursa ya kuchangia mada ambayo iko mbele yetu leo hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi nianze kwanza kwa kupongeza Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii kwa taarifa yao nzuri kabisa na nipongeze Kambi Rasmi ya Upinzani kwa hotuba yao nzuri kabisa. Waingereza wanasema; they have said it all. Ni matarajio yangu kwamba Waziri atafanyia kazi document hizo mbili, kwa uadilifu ili Taifa letu lifike litakapofika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wala siachi kumshukuru wifi yangu Mheshimiwa Waziri kwa kazi anayoifanya na Naibu wako na timu yake yote. Pia nikupongeze kwa kuchagua partner ndiyo kwa sababu ulikwenda Kusini ungekwenda Kaskazini yale maneno leo usingeyasema hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli haya mambo kama alivyosema Mheshimiwa Mbatia yanaturudisha mle mle kila siku. Halafu tunafanya trial and errors hata kwenye elimu! Halafu Bunge kama imepanga ratiba vizuri, jana tumezungumzia mambo ya maji hapa, maji ni uhai, leo tunazungumzia elimu, elimu ni ufunguo wa maisha, lakini tunauchezea ufunguo huu, matokeo yake Taifa hili litaangamia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jana nilikuwa najitahidi sana nipate fursa ya kuuliza swali la nyongeza wakati swali namba 199 likipatiwa majibu. Mimi muda wote nasema nchi hii tuna tatizo la ukosefu wa uadilifu, hatufanyi mambo kwa uadilifi. Mheshimiwa Mbatia kasema vizuri pale, hizi itikadi zetu za chama zitatupeleka pabaya. Ikisemwa hapa, ndiyoo, waliosema ndiyo wameshinda, waliosema sio wameshindwa halafu matokeo yake tunapitisha mambo mwisho wa yote yanaturudia wenyewe tunaangamia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mambo ni mengi lakini nianze na hili la mambo ya vyuo kwa sababu limenigusa mimi binafsi. Hivi Wizara inapokuja kutuambia kuna vyuo visivyo na sifa lakini vilisajiliwa, vilisajiliwa vipi? Mimi nilikuwa Chuo cha Diplomasia, ni chuo cha Serikali, tulizungushwa miaka miwili na NACTE kwa sababu tu hatuna push door yaani mlango ule tunaambiwa mlemavu hawezi ku-access miaka miwili chuo cha Serikali kilichoanzishwa miaka karibu ishirini iliyopita. Vyuo binafsi hata mlango wenyewe haupo vinapata usajili, halafu hapa wanakuja kutuambia kuna vyuo visivyo na sifa vilisajiliwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama vile haitoshi wanatumbia vitabu vyenye maudhui siyo vipo, hilo ni tatizo la uadilifu. Tunaona kwenye tv zetu hapa programu za kijinga kabisa, watoto wanazini pale mbele ya screen, lakini TCRA kuna Kamati ya Maudhui hawalioni hili? Tatizo ni uadilifu. Tunawaweka watu siyo kwenye taasisi ndizo, tubadilike. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, NECTA na vyeti fake. Kwenye kikao cha mwaka jana hapa nilisema, mimi nimepoteza cheti changu cha form four na form six, nakwenda NECTA naambiwa nenda kule ulikosoma mwalimu wako mkuu akuandikie barua. Nikawaambia mimi nimetoka Kisutu mwaka 1977, huu mwaka 2011 Mwalimu Mkuu gani wa Kisutu ananijua mimi lakini wewe NECTA ndiyo uliyenipa mimi namba ya mtihani na ndiye unayejua kituo changu cha mtihani, you stand a better position and chance ya kuni-clear mimi kuliko huyo mwalimu. Sasa hapa mmeanzisha hili zoezi wenyewe mnaliita uhakiki wa vyeti fake, kisiasa kabisa watu wanaathirika, wengine wala hawahusiki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, labda niwaambie moja tu. Mimi sasa hivi naitwa Riziki Shahari Mngwali lakini hili nimelipata na nimelisajili rasmi kwa sababu nimeenda kutafuta deed poll. Watanzania wangapi wanajua hilo? Mimi miaka yangu yote naitwa Riziki Shahari, majina mawili tu. Hata nilipokwenda chuo kikuu kuomba niwe admitted kwa ajili ya programu nyingine nikaambiwa hilo jina la tatu hatulikubali kwa sababu ulisoma hapa digrii ya kwanza kwa majina mawili, tutakusajili tena kwa majina hayo hayo mawili. Sasa hivi vyuo vyetu vingesaidia hivi kuliko kuwaadhiri na kuwatesa watu bila sababu ya msingi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika lile swali nililolisema la jana namba 199 kulikuwa na issue ya wenyewe watalaam wanaitwa LOI - the Language of Instruction, imesemewa mpaka na programu maalum ilikuwepo chuo kikuu pale. Profesa Koro wame-research na wameandika bado tunali- discuss hapa. Jana likaja hapa linasemwa na leo hivyo hivyo ndiyo tunaona vitabu hapa vinakwenda kushoto kulia, kulia kushoto, pembeni kati, tatizo hatujui tunataka nini. Basi hata kuamua tu lugha gani tutumie kufundishia watoto wetu kwenye ngazi zote za elimu yetu lakini pia tuweke msisitizo wa kuwafundisha foreign languages not only English, French, Spanish, Arabic na bado watoto watafaulu watatoka na elimu nzuri na bado watakuwa na qualification za foreign languages tunazozitaka, tujipange tu vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la hizi programu maalum kwenye ukurasa 77, 78, P4R, TESP na mengine, nitoe tahadhari ile ile ambayo nilishawahi kusema kwingine this is donor dependence ya kutisha kabisa. These are very special programs (programu maalum) na ni nzuri kwa kutengeneza mfumo wetu wa elimu, lakini zinafadhiliwa kwa sehemu kubwa kabisa kama siyo sehemu yote. Ni kama vile wewe ili umlee mtoto wako mzuri atoke jirani huku aje akuambie mwanao akiwa na afya nitakupa pesa, mwanao akisoma vizuri nitakununulia gauni, mambo gani haya? Hebu haya mambo mengine tujiwekee sisi wenyewe tuone tunakwenda wapi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nisije nikaishiwa muda bila ya kusema suala la motisha kwa walimu na baadaye tutali- discuss kwa watumishi wetu wote wa umma. Jamani mwalimu anafanyiwa stihizai, anapandishwa cheo mwezi huu analipwa mshahara, mwezi unaofuata halipwi, kimya, hapelekewi barua wala hajulishwi chochote, hivi tunategemea hawa watu wafanye kazi namna gani? Mwalimu mnamtoa Kigoma mnampeleka akafundishe Mafia, hapewi nauli wala stahiki zake nyingine, mnatarajia atafanyaje kazi, hata kweli atakuwa na moyo wa kufundisha watu huyu? Watu wengine mnazungumzia mazingira magumu, wana allowance nyingine hazina hata na majina lakini walimu wanasahaulika. Nani awatetee hawa walimu na siyo kwamba hawana watetezi, watetezi wapo wanasema hapa lakini nani anajali kushughulikia hayo ambayo yanasemwa kwa ajili ya mustakabali wa nchi yetu hii? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jamani Mheshimiwa wifi hebu badilikeni. Kweli tunakuona mfanyaji kazi, mara hii tunazo kweli timu za akina mama, mmekaa kwenye Wizara, Mheshimiwa Ummy yuko pale na wewe na Naibu wako mmewekwa Wizara moja hebu fanyeni kazi tuone kweli wanawake mtaleta mabadiliko ambayo kweli sisi tutakaa tujivunie. Elimu tukiichezea, Taifa tumelichezea na kuliangamiza. Jamani tubadilike na tufanye kazi inavyotakiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Waziri Kivuli amezungumzia suala la wataalam wa TEHAMA na mimi pia niliseme. Mimi nilishtuka kwamba eti tunaenda kuazima wataalam kwingine waje watutengenezee programu yetu sisi, mimi nikasema what a shame! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nilikuwa kwenye Tume ya Warioba, tulipata vijana wa IT mashallah walitengeneza programu pale ya kurekodi zile taarifa zote, mikutano tunayofanya, Hansard tulichukua wataalam wa hapa Bungeni, kulitokea programu mpaka siku moja Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Salim Ahmed Salim, mwenyewe alikuwa ananiita jirani maana ofisi zetu zilikuwa floor moja, akaniambia jirani hawa watoto ni wa Tanzania? Nikamwambia tena mmoja ni Mpemba, walitengeneza programu mpaka mtu unashangaa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa leo tunaenda kuwatafuta watu wa Rwanda, sijui na watu gani. Hivi tutawasifia lini watoto wetu, tuta-recognize lini sifa zao na tutawa-motivate vipi watoto hawa? Watoto excellent kabisa wengine wame-graduate hapo St. Joseph, hapo hapo mlipopafunga mwaka jana, watoto wazuri, watoto ambao TTCL wanawagombea. Ukipeleka mtoto kufanya field TTCL wanamuuliza wewe ni wa St. Joseph au wa chuo gani, kwa sababu wanajua watoto wale wamefundishwa sio elimu ya darasani lakini hands on, ile competence base ni kweli wamejifunza, lakini yote haya hatuyaangalii tunazidi kuwakatisha tamaa watoto wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho nilisema hapa tunahitaji an integrated process, budgeting, planning and even understanding. Tukiwa na uelewa wa pamoja tunapanga mambo yetu pamoja, migongano gongano hii haitakuwepo tatizo kila kipande kinatengenezwa peke yake halafu kinakuja kulazimishwa kukaa kwenye kipande kingine. Kwa namna hii hatutafika na kila siku tutakuwa tunaanza palepale kwa sababu mambo yetu tunayapanga kipande kipande halafu tunakuja kulazimisha kuwa pamoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Nami nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na ardhi, aliyetujalia sote hapa uhai na uzima na kutuwezesha kufanya hili tunalolifanya. Baada ya hapo nitoe shukrani za kipekee kwa wazazi wangu wawili Mwenyezi Mungu awarehemu huko waliko na awahurumie kama wao walivyonihurumia mimi nilipokuwa mdogo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa namna ya kipekee kabisa naomba niyatambue, niyashukuru na niyaenzi malezi ya Walimu wangu wa darasa la kwanza mpaka la saba kama ifuatavyo:-
Mama Clara wa darasa la kwanza na la pili; Mrs Mganga wa darasa la tatu; Mrs. Makundi wa darasa la nne; Mrs Matata wa darasa la tano; Miss Komba wa darasa la sita; na Mr. Mabula wa darasa la saba waliongozwa na ma-head waaminifu, mama Kehemere, Mzee Mwamugunda na Mzee Lukoo. Naomba kwa namna ya kipekee niwaenzi Walimu wangu Wakuu wa Kisutu sekondari 1974-1977 marehemu mama Chale, mpenzi wangu mama Tegisa, Mama yangu Mrs. Munuo na Miss Kassim. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, niwaenzi pia Walimu wangu Wakuu wa Korogwe Sekondari mama Msemakweli na Mwalimu Chisongela, kwa malezi yenu nimefika hapa, nawashukuru sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nianze kuzungumzia mada hii kwa kuangalia Taasisi zilizomo na nianze na NECTA. Katika mambo yanayotia uchungu kwenye Taasisi hii ni credibility yake. Hii ni Taasisi ambayo it makes or destroys Mtanzania. NECTA inatoa maamuzi mwanafunzi anapotoa mitihani yake lakini je, kweli Taasisi hii ina uadilifu wa kutosha kuweza kufanya kazi hiyo? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kwa ruhusa yako niwasome watoto hawa halafu nitakwambia kwa nini. Kuna hafidhi Hassan Arkam Salum, Nassoro Shaban, Ali Alhabi, Abdulhamid Ahmed, Zamha Abdallah Rashid, Damtu Mohamed Tahir, Fatma Vuai Muhidini, Mwanaharusi Ally, Sabrina Suleiman Ally, Ruwaida Ally Ahmed. Hawa watoto walidhalilishwa mbele ya umma wa Tanzania katika watoto waliofutiwa matokeo yao, hawakufanya vizuri, wamekopia mitihani.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mwenyezi Mungu alichowajalia watoto hawa ni kwamba wazazi wao wana uwezo. Walichofanya wazazi wa watoto hawa, waliwapeleka Arusha Modern na pale wakaamua wafanyiwe mitihani ya Cambridge, mtoto Hafidhi Hassan Ali, alitoka na distinction lakini kama vile haitoshi, ule mtihani wake wa Kiswahili ulipewa A* na A* kwa Cambridge ni kwamba iko beyond 89. Hasa ni Global wise na hiyo A* yake ya Kiswahili ni globaly, worldwide huyu mtoto alitoka Arusha modern, lakini kwa mfumo wetu kwa assessment ya NECTA huyu mtoto kama mzazi wake asingekuwa na uwezo tungeshamsahau sasa hizi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, na hawa wote waliomfuatia katika orodha hii walipata merit. Kwa hiyo, ni watoto na naombeni m-google muangalie how Cambridge wanaweka hizo classification zake, distinction, merit na pass halafu muone sisi tunaingia wapi pale. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kama hilo halitoshi kwa NECTA, lingine ni kwamba hawa NECTA wakishakufelisha ukitaka kukata rufaa ukate kwao, mlisikia wapi? Mahakama ya Mwanzo, hiyo hiyo Mahakama ya Hakimu Mkazi na Mahakama ya Rufaa ni hiyo hiyo, tunafanyaje haya. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nina kesi mbili ambazo walifelishwa niseme na wakakata rufaa. Uzuri hawa walipata msaada wa Walimu wao wenyewe, kama huyu kijana mmoja yeye alipofanya mitihani ya A-level pale Benjamin Mkapa, wazazi wake wakasema haiwezekani Abdulkarim afeli, kupata division III ni Walimu wake waliomsimamia na ziliposahihishwa akapata division one, sasa hivi ni Mhasibu, yuko Arusha Municipality, hiyo ndio NECTA yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa NECTA katika kasoro nyingine wasifanye kazi kwa uzoefu. Nimepata bahati mbaya ya kupoteza vyeti vyangu, vya O-Level na A-Level, lakini baadaye nikapa hamu ya kwenda kujiendeleza nifanye PhD nilipokwenda shuleni Vietnam, Taasisi zetu za elimu ya juu na NECTA, chuo kikuu wananidai mimi vyeti vyangu vya form IV na Form VI nikawaambia ninyi mnisamehe kwa sababu degree yangu ya kwanza niliipata hapa chuoni kwenu na mlini-admit kwa credential zangu za O-level na A-level, lakini wakaniambia tunakuweka lakini hutopata cheti, huto-graduate mpaka utuletee.
Mheshimiwa Naibu Spika, nilipokwenda NECTA wananiambia niende shule yangu ya O-level, niende na shule yangu ya A-level wakathibitishe kama mimi nilikuwa mwanafunzi wao pale. Mimi nimeondoka Kisutu 1977, nimeondoka Korogwe Girls 1980. Mwalimu gani ambaye ataweza kuthibitisha zaidi kuwepo kwangu mimi kuliko NECTA ambao wao waliitambua shule, wakanitambua mimi, wakanipa examination number. Haya mambo gani ya kufanya kazi kwa uzoefu? NECTA wabadilike katika utendaji kazi wao. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ambalo linaingia kwenye Wizara hii pia ni suala la Mheshimiwa Kuchauka alichangia siku moja akasema, uwekwe msisitizo katika kufundisha jiografia na historia, lakini nimekuwa nikisema mara kadhaa hapa kwamba, watendaji wetu wanatakiwa wapate dozi ya know your country. Hii nairudia tena leo hapa kwa mfano mdogo kwamba, watu hawa watakapoijua nchi yao, watajua makundi maalum yaliko yanayotengeneza ile jamii kubwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo watakapofikiria kupanga shughuli maalum kama hizi za michezo kwa mfano, UMISHUMTA sijui, UMISETA na hata SHIMIWI, hawawezi wakayapanga mwezi wa Ramadhani kwa sababu wanajua kuna kundi kubwa la jamii ya Watanzania kushiriki kwao michezo ile itakuwa muhali, basi hata hili nalo jamani tuambiwe, wakati kalenda tunaZIpata mwezi Januari au hata kabla tukaona mle na huwa wanaweka star kabisa kwamba tarehe hizi inaweza ikawa Idd el fitri, kwa hiyo maana yake mwezi before ndiYo Ramadhani, sasa mambo kama hayo yazingatiwe. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba pia nichangie katika, mimi nimeliita the big scandle in town, hili tuliloambiwa hapa, la TCU na Saint Joseph. Hili limetokea kwa haya ambayo Wabunge wengi wamesema na kaka yangu Mheshimiwa Mbatia amemalizia kusema na amekuwa akilisema miaka mingi ya kuchezea elimu yetu na mfumo wetu wa mafunzo katika nchi hii, mahodari wa kuunda Taasisi, kuzipa majina, halafu tukakoroga yale majukumu yake, mwisho wa yote hatupati chochote. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, namwomba Mheshimiwa Waziri na kwa namna alivyom-introduce best half wake jana mimi nakuwa wifi, kwa hiyo, nisikilize kwa umakini zaidi, siyo tu Mbunge lakini wifi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ajijulishe kuhusu kitu kilitwa NAMDEC ilikuwepo huko, National Managament Development something ikaundwa HEAC, lakini baadaye nikadhani baada ya kuunda TCU na NECTA na VETA, nikajua sasa ule mkorogo tuliokuwa nao kwenye NAMDEC na ile HEAC kwa maana ya Higher Education Accreditation Council yatakwisha, kwa nini? Kwa sababu zile Taasisi za mwanzo zilikuwa zinachanganya chuo kikuu kimo, kisichokuwa chuo kikuu kimo, lakini ukishasema TCU (Tanzania Commission For Unviversity) ukasema NACTE sijui National Technical Edecucation something; VETA Vocational Education yashajulikana, lakini tunafanya nini?
Mheshimiwa Naibu Spika, Taasisi zilizokuwa chini ya NACTE na zenyewe zinakwenda zinataka kutoa degree zijiite chuo kikuu; Taasisi zile za chuo kikuu zenyewe nazo zinashuka mpaka chini zinataka kutoa vyeti, sasa ni nini? NACTE kwa mfumo wao wanasema wao ni competency based kwa maana nyingine wanatutengenezea hawa watu wa hands on, wale wataoshughulika practically na wao ndio maana kwao…
MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Naibu Spika, basi nakushukuru.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara hii inahitaji kufanya marekebisho ya msingi katika mfumo wetu wa elimu na mafunzo nchini.
Naomba Mheshimiwa Waziri asome kwa makini sana Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, Hotuba ya Kambi ya Upinzani kwa Wizara hii na ripoti ya Profesa Mchome ya mwaka 2013 kufuatia mass failure ya watoto wetu katika mitihani ya Form IV mwaka 2012. Naamini hizi zote zitamsaidia katika kazi nzito iliyo mbele yake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, namuomba Mheshimiwa Waziri alipitie upya suala au sakata la TCU na wanafunzi wa Chuo cha St. Joseph. Kwa kiasi kikubwa tatizo liko katika utaratibu ambao Serikali imeuweka. Mabaraza yetu ya NACTE, NECTA na TCU yanatakiwa yafanye kazi zao kwa kuzingatia mipaka yao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kiutaratibu vyuo viilivyo chini ya NACTE vinadahili wanafunzi waliopata minimum ya D nne (4) katika mtihani wa form four kwa kozi ya NTA 4 katika chuo chochote. Wanafunzi waliofukuzwa St. Joseph College wamekidhi hili. Tatizo liko wapi? Kupata diploma watasoma miaka mitatu na wakiendelea mpaka digrii watalazimika kusoma miaka mitano, hili ndilo walilokuwa wanafanya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, narudia kusema Mheshimiwa Waziri apitie kwa makini taasisi zilizo chini ya Wizara yake ili kuitendea haki nchi yetu na hasa vijana wetu. Lazima iwepo nidhamu na utaratibu maalum kwa taasisi zetu wakati wanatekeleza majukumu yao. Pamoja na nidhamu, uadilifu ni muhimu zaidi. Vijana wetu wengi wameharibiwa maisha yao au ndoto zao kwa maamuzi ya NECTA kwa miaka mingi na sasa tunashuhudia hili la TCU.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.
Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, vituo vya televisheni hasa Clouds, vinaonesha miziki ambayo haiendani kabisa na mila na utamaduni wetu. Wasanii hucheza miondoko isiyofaa. Pia mavazi ya wasanii wanawake (wanenguaji) na hata baadhi ya waimbaji yamekithiri kwa utovu wa maadili na vigezo vya mila zetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri Kamati ya Maudhui ya TCRA iwajibike ipasavyo. Inasikitisha sana kuona wasanii wakiwa uchi (wengine wakiwa na nguo za ndani tu) wakioneshwa na televisheni zetu, tena muda wa mchana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara na TCRA ni lazima wawajibike ipasavyo haraka iwezekanavyo.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara hii ni miongoni mwa Wizara zenye umuhimu wa kipekee kwa nchi yetu. Mafanikio ya utendaji kazi wa nchi hii unategemea uwezeshwaji katika rasilimali zote (rasilimali watu na rasilimali fedha). Tabia iliyozoeleka ya Hazina kutoa pesa iliyoidhinishwa na Bunge kwa Wizara zetu ikiwemo hii ya Mambo ya Nje imekuwa kikwazo kikubwa kwa watendaji wa Wizara yetu. Ifike wakati sasa Bunge liheshimiwe kwa kutekeleza maamuzi/maelekezo yake na Wizara zetu zitendewe haki kwa kupewa bajeti walizoidhinishiwa na Bunge lako Tukufu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa rasilimali watu yenye sifa stahiki ni muhimu sana kwa utekelezaji wa majukumu ya Wizara hii muhimu, Serikali inabidi iweke mkazo wa kipekee kuandaa Mabalozi wetu wanaotuwakilisha nje ya nchi na watendaji wa Wizara. Lazima foreign service officers wapewe mafunzo maalum ya muda mrefu (angalau mwaka mmoja) ili kupata vyote, Regional and functional specializations kwa watendaji wetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Regional specialization ni lazima ijumuishe mafunzo ya lugha kuu ya eneo (region) husika. Kwa mfano, Watendaji wetu kwa Kurugenzi ya Mashariki ya Kati (Middle East and North Africa) ni lazima wawe na umahiri wa lugha ya Kiarabu. Kurugenzi ya Ulaya wajue Kifaransa na Ki-Spanish na kadhalika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni muhimu Wizara hii pia itoe umuhimu wa kipekee kwa Chuo cha Diplomasia ili kiwe na hadhi stahiki. Kwa sasa Chuo kiko katika hali mbaya, miundombinu yake kwa kweli hairidhishi, lakini hata Walimu wa Chuo cha Diplomasia hawapatiwi mafunzo stahiki ya kuwajengea uwezo kwa kuandaa watendaji wa Wizara hii. Kozi fupi nje ya nchi kwa Walimu wa Chuo hiki ni muhimu sana ili kuwajengea uwezo katika kutekeleza majukumu yao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika harakati/jitihada za kubadili hali ya Chuo cha Diplomasia iliwahi kuundwa Tume ya Profesa Ishumi iliyojumuisha Wataalam mahiri wakiwemo Profesa Daudi Mukangara. Ni muhimu taarifa ya Tume hii ifanyiwe kazi. Kuwa na Wakuu wa Chuo wenye sifa bila ya kufanyia kazi masuala mengine muhimu haitoshi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni jambo muhimu sasa Wizara ibadili utendaji kazi wake na utoaji taarifa zake za kila mwaka ikiwemo Hotuba zake za Bajeti za kila Mwaka. Wizara isitoe descriptive report tu, ni lazima kutoa taarifa zinazoonesha kuwa Wizara ilikuwa na malengo yanayopimika (measurable goals/objective). Hili liwe pia kwa Balozi zetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lazima Balozi zetu zipewe malengo maalum ya kuyafikia na malengo hayo yazingatie maeneo waliko kulingana na maeneo/nchi wanazotarajia kupata wawekezaji, watalii na kadhalika. Kwa mfano, malengo ya Wizara kwa mwaka ujao wa fedha hasa Kifungu cha 193 (i, ii, iii na iv) yangeweza kuboreshwa na kutaja vigezo mahususi.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2016 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Niruhusu nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, muumba mbingu na ardhi, aliyetujalia sote uhai, afya na uzima na kutuwezesha kuwa hapa tukijadili hili suala tunalojadili kwa mara ya pili sasa katika kipindi hiki au awamu hii ya uongozi tuliyonayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nifuatilize kwa jambo jema kabisa ambalo limewahi kutendwa hapa duniani ambalo ni kuhusiana na kuusia mema na hasa kuusia kumcha Mwenyezi Mungu. Basi na mimi niwausie kama ninavyousia nafsi yangu kumcha Mwenyezi Mungu kwa namna inavyopasa kumcha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naipongeza Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni chini ya uongozi thabiti wa Mheshimiwa Mbowe, akisaidiwa na mimi hapa ndugu yake, lakini pia chini ya usaidizi mkubwa kabisa wa Mwenyekiti Mwenza, kaka yangu mpenzi, Mheshimiwa James Mbatia. Ama timu ya UKAWA inafanya kazi na kwenye ukweli siku zote uongo hujitenga. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika pongezi ambazo ningependa kuzitoa leo hii kwa uzito wa kipekee kabisa, nimpongeze kiongozi wangu mwadilifu, mcha Mungu, muungwana, mpenda amani na yeye mwenyewe ni kipenzi cha watu; huyu sio mwingine ni Katibu Mkuu Mwenza wa UKAWA, Mheshimiwa Maalim Seif Sharrif Hamad ambaye yeye siyo tu ana dhamira ya kuendeleza amani, bali anafanya kwa kitendo. Anatekeleza suala hili, anaendeleza amani na maelewano katika nchi hii na kwa kweli penye ukweli pasemwe. Laiti Maalim Seif angekuwa kama viongozi wengine wa Afrika wale ambao wana maslahi binafsi au wana ubinafsi, basi Bunge hili inawezekana ingekuwa saa hizi tunajadili mengine au nchi hii kwa ujumla wake ingekuwa katika hali tofauti na hii tunayoiona sasa hapa. Nampongeza sana, namwomba Mwenyezi Mungu amzidishie subira na ucha Mungu na kwa hakika yeye ni miongoni mwa wenye kufaulu duniani na akhera. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi wala si mtaalam sana wa takwimu lakini masuala mengine yamekuwa tabled hapa wiki iliyopita na kwa vigelegele kabisa mpaka watu wakasimama wima mimi nilikuwa nashangaa na naamini ulikuwa unaniona, nilikuwa nashangaa hivi kweli hotuba hii inastahiki kusimamiwa, kwa lipi lililomo mle jipya? Walichojitahidi sana ni kucheza na maneno, semantics genetics tu, sarakasi za maneno lakini hazina jipya lilotuletea hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, semeni kwa ukweli wa dhati wa mioyo yenu Waheshimiwa hivi unapoongeza tozo kwenye mafuta ya taa nia yako hasa ni nini? Wapiga kura wetu walio wengi lile wenyewe wanaita jiko la mchina ndiyo gesi yao na ndiyo electric cooker yao. Hivi unavyowaongezea hiyo gharama ya kununua mafuta ya taa unataka waende wapi? Unaongeza bei ya mafuta wakati ambapo tunakaza nati kwenye masuala ya mazingira na kuwazuia kukata miti, hao wananchi waishi maisha ya namna gani hebu niambieni Waheshimiwa? Nakuomba sana Mheshimiwa Waziri ukija hapa tuambie hawa walala hoi wa Tanzania wewe unataka waishi maisha ya aina gani mwaka huu wa 2017/2018? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesahau yule Malkia wa Ufaransa alikuwa wa mwaka gani lakini katika kituko chake cha ile kuonyesha kiasi cha yeye kuwa mbali na realities na uhalisia wa mambo, wananchi walipoandamana wakasema hatuna mikate akawaambia why don’t you eat cake, hamna mkate kuleni keki. Kumbe wenzie wanasema hawana mkate yaani hawana hata kile cha kuendesha maisha ya kawaida, sasa ndiyo tunachokifanya hapa. Tumeshindwa kutafuta shilingi trilioni zile pungufu 29 leo tunasema tunataka shilingi trilioni 32 tunazitoa wapi kwa hali halisi? Halafu hatuonyeshi mbadala ulio mahsusi na makini wenye kueleweka kwamba hivi ndiyo vyanzo ambavyo vinakuja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jamani nakusihi sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango, hebu soma kwa uadilifu bila hiyana maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ambayo Masha Allah leo kijana wangu Silinde kaya-present yakiwa kwenye fomu yake hasa. Yapitie kwa umakini kabisa, utaona mapendekezo gani yamo mle kuhusu vyanzo vya mapato, lakini pia kuhusu ipi iwe ndiyo budget figure yetu. Tuache kucheza na maneno hapa, tuache kuwadanganya walimwengu lakini mwisho wa yote tunajidanganya sisi wenyewe. Hivi unaposema nitakimbia kilometa saba ukashindwa ukaishia mbili na nusu halafu unakuja tena unasema sasa mara hii nataka kukimbia kilometa kumi, inatokea wapi mambo hayo? Jamani kwa nini tunajidanganya hivi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwalimu Bilago pale kauliza huyo aliyeturoga nani huyu? Sisi kule kwetu wanasema ukiona hali kama hii huyo aliyekuroga kafa maana angekuwa hai angekuhurumia. Laiti yule aliyeturoga Watanzania angekuwa hai akatuona tunavyodhalilika humu, tunavyosema mambo ambayo hayana kichwa na miguu wala hayana mbele wala nyuma angetuhurumia. Basi akapunguza, wanasema anapunguza ile dozi, basi na sisi tungepata ahueni. Waheshimiwa Wabunge nawasihi sana tumwogope Mwenyezi Mungu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwalimu wangu mmoja wa jiografia nilipokuwa O-level, Mrs. Seif, Mwenyezi Mungu ambariki sijui yuko wapi sasa hivi, katika ufundishaji wake mzuri sana wa geography ya maeneo alikuwa anatupandisha ndege na meli lakini tuko Kisutu Sekondari. Anatuambia fumba macho leo tunaondoka Zanzibar kwa boti namba fulani tumeingia baharini, mawimbi yanafanya vile, fumba macho na kweli tunafumba macho tuna-internalize ile safari yote mpaka lile aneo jipya tunalokwenda. Hebu na sisi tufumbe macho tu-internalize haya mambo, tu-internalize hii bajeti process yetu kila figure, tumvute kwenye picha hii kubwa kila mtu ambaye anaguswa na bajeti hii, tusijifikirie sisi wenyewe tu Waheshimiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mambo ambayo mimi naamini au katika vitu ambavyo ninajua kabisa bila hata kufundishwa wanasema, I am spill of effect au trickling down effect ni masuala ya mafuta. Unapoongeza tozo kwenye diesel na petrol unatarajia hao wenye mabasi yao akina Mheshimiwa Shabiby watawacha nauli ile ile, si watapandisha? Madaladala si watapandisha nauli? Mwalimu Bilago kasema hapo unadhani bidhaa itakayotoka Dar es Salaam mpaka ikafika huko Kakonko sijui itakuwa bei ile ile, itakuwa bei juu. Sasa sisi tunafanya nini jamani mbona tunagusa mahali sipo!

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini tunafanya jambo kama hili wakati tunadai eti tunataka kuwasaidia walalahoi, hatuwasaidii walalahoi. Labda mniambie mmekuja na system ambayo mtatengeneza kwenye vile vituo vya mafuta ile gari ikienda inakuwa detected, hii ni ya Mheshimiwa Ashatu mkate huyu, hii ni gari la daladala usikate labda iwe hivyo lakini kama tunaweka hii blanket amount halafu kwa system hii ya kawaida kwa kweli tunakwenda kuwaumiza watu wetu na walio wengi wataanza sasa kutumia hii tunaita TZ eleven, watatembea kwa miguu badala ya kutumia vyombo vya usafiri kwa sababu hawatamudu kutoa gharama hizo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, waswahili wanasema kama ilivyo dawa ya jipu kulitumbua dawa ya deni kulipa. Msitumie maneno lihahimilika, linavumilika, linahamishika, linakwenda wapi? Bado linabaki ni deni letu la taifa, tulilipe, tuwe na clean slate halafu tunaanza upya. Watu tumelalamika hapa na Mheshimiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti kasema kuhusu riba, riba tena inatuning’inia rohoni hapa hatujiwezi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitawaambia jambo lakini ninyi mtakasirika kwa sababu lilishaingia Bungeni humu likaleta siasa na chuki, go OIC ambapo tunapata mikopo haina riba. Kama OIC mnaiona ina ukakasi, mimi naamini kama hiyo economic diplomacy yetu tungeitumia vizuri wangetutafutia partners ambao wangeweza kutupa mikopo kwa bei nafuu kabisa. Naamini hao watu wapo, hizo nchi zipo kwenye Bara la Ulaya tungeweza kupata hao partners ambao wangetupa arrangements zenye unafuu sana na mikopo ambayo kweli tungeweza kuhimili. Siyo hii mikopo ambayo tunaenda kukopa kibiashara kwenye arrangements ambazo zinatutoza riba kubwa mwisho wa yote capital hatulipi na wala hiyo riba inayoongezeka kila mwaka hatulipi, tunaendelea kubadilisha maneno hapa mara leo linahimilika, kesho sijui litavumilika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba sana Mheshimiwa Waziri husika hebu atuambie vizuri haya maneno hasa mwisho wake nini na nini anapotuambia tunaweza kuhimili deni ili mwisho wake iwe nini. Atuambie tu hii bajeti yake inajibu vipi vilio vile ambavyo tulivisikia hapa wakati tunajadili Sectorial Ministries. Tulipokuwa tunasema maji, kila mtu hana maji na Mheshimiwa kaka yangu Almas anamalizia hiyo imekwisha, Wizara ya Maji ilishapita na hii bajeti haina hata maji humu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumejadili hapa kila kitu elimu matatizo, afya mtihani, maji ndiyo hayo, barabara hazisemeki, kila kitu kila kitu hakipo. Hii bajeti hii hapa hii ukiondoa hiyo dhamira ya kuendeleza amani ambayo wala haipo mnafanya nini ku-address vilio vyote vile ambavyo vimesemwa katika Bunge lako hili Tukufu kuhusu maisha ya Watanzania kwa mustakabali wa nchi yetu.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa fursa nami niweze kuchangia kidogo kwenye Wizara hii. Nianze kumshukuru Mwenyezi Mungu muumba mbingu na ardhi, aliyenijaalia mimi na ninyi wote kuwa na afya njema na kuwemo humu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nina machache vilevile ya kuchangia kama wenzangu wengi walivyosema, labda nami nianze nalo hilo hilo kwamba, pamoja na makandokando yake yote kaka yangu Mheshimiwa Lukuvi, lakini naona hii Wizara anaiweza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme kwa yale yaliyosemwa na hotuba ya Kambi ya Upinzani kwamba tunachohitaji ni system, lazima uwepo mfumo! Siyo tu kama alivyosema Mheshimiwa Yusuph kwamba Mheshimiwa Lukuvi yeye ni binadamu, lakini pia kawekwa na binadamu. Nani anajua kwamba atakaa hapo miaka yote mitano? Anaweza akahamishwa kesho kutwa. Je, akihamishwa wakati yuko katikati ya hii mikakati yake, tutafanyaje? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nisisitize hilo kwamba tunahitaji mfumo na huu mfumo sijui unatoka wapi! Usidhani Waziri mwenyewe anaweza akasema mfumo nimeutengeneza huu na utafuatwa na wengine wanaokuja, kwa sababu historia haituoneshi hivyo, imekuwa kila awamu ikija, inakuja na misamiati yake na taratibu zake na mambo yake na mbaya zaidi ni kama vile inafumua lote lililokuwa kabla ya hapo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ninalotaka kusema, limesemwa pia na wachangiaji wengine kadhaa kuhusu masuala ya mipango Miji. Taratibu, akili ya mwanadamu iliyo sawa huwa anarudia lile lililokaa sawa, wenye lugha yao wanasema kuna success stories. Sasa unapokuja kufanya mambo, unafuata zile success stories.
Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wameimba sana hapa kuhusu Kigamboni Development Agency, mpaka mwanafunzi wangu Mheshimiwa Mary Mwanjelwa akasema this is a non starter, yaani hakuna pa kuanza, hakuna pa kuelekea. Hivi tuliigiza nini tukaweka ile?
Mheshimiwa Mwenyekiti, CDA ime-fail for more than 40 years. Miaka 40 CDA haijulikani kama inatambaa au imekaa kitako au inasimama dede wanasema, lakini bado tukaanzisha mamlaka nyingine kwenye eneo dogo halafu na hotuba zote zimesema mpaka ya Kamati kwamba mmeanzisha dude halifanyi kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pesa hiyo hiyo ndogo iliyopo tunasema tunabana matumizi, tunapeleka kule kule; pesa inatumika hakuna productivity. Sasa sijui ndiyo siasa safi na uongozi bora! Sijui, lakini kuna kasoro kubwa katika haya. Tunahitaji kujiangalia kwa kina na tuseme hasa na tuamue tunataka nini kwenda mbele? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, toka nimeanza kuja hapa Dodoma Bungeni kila nikitoka kichwa changu huwa kinapata wasiwasi na mpaka juzi nadhani, sikumbuki nilikuwa na nani, nikamwuliza hivi hili jengo la Bunge kuwekwa hapa, nani aliamua? Hii ndiyo barabara!
Mheshimiwa Mwenyekiti, unajua kile kikao cha kwanza nilipofika, nimekaa pale nje getini, nikaona mabasi yanapita yanafuatana. Nikasema haya mabasi yanakwenda wapi? Wakasema hii ndiyo barabara kuu, ndiyo hiyo ulipotokea Dar es Salaam, ndiyo huko inakwenda stand hapo. Naambiwa na jengo la Bunge liko hapa. Kwa nini liliwekwa eneo kama hili? Sasa nikauliza, wana mipango ya kuhamisha watu wa huku au wana mipango ya kuhamisha hili lipelekwe huko mbele ya safari? Jamani, tunafanyaje mambo kama haya? Tunapangaje? Hivi kweli wanaoitwa wapangaji, hawa watu wanaotupangia haya nao wamesoma? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna siku baba mkwe wangu aliniuliza, akaniambia wewe mama ulikwenda kusoma Marekani, umesoma umefaulu kweli au? Kwa sababu anachosema yeye kwamba, tukisharudi huku na degree za huko huko, bado tunawaita wale wataalam tuliosoma nao kule kuja kutusaidia huku. Sisi wenyewe hatuwezi. Kuna tatizo hapa, halafu watu tunakaa tu kama vile mambo yamekaa sawa. Jamani mambo haya hayajakaa sawa. Bado kunahitajika kazi ya kina.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi sijui, kwa sababu hatujaingia huko na wala hamtushirikishi kwenye mambo yenu, tunaona tu vision na misamiati ya hapa kazi, ya kasi zaidi, kasi mpya lakini tunabaki pale pale. Sijui tunahitaji kufanya nini, lakini ilikuwa vizuri tu mngekuwa waadilifu 2015 mngetupisha kwa sababu naamini UKAWA tulifanya performance nzuri sana na hii ingekwenda vizuri kabisa. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna lingine ambalo limegusa suala mahususi kuhusu Jimbo langu la Mafia. Naishukuru Serikali na Wizara hii kwa kwenda kutusaidia angalau shamba moja kati ya mawili ambayo Wilaya ya Mafia tulikuwa na migogoro nayo. Mafia jamani ni ndogo, anapokuwepo mwekezaji sijui au mmiliki mwenyewe wa shamba pori hili la ekari karibu 4,000 na kitu kwa miaka tu linakaa hivi hivi, wananchi wanakuwa hawana mahali; sasa angalau mmetusaidia kwenda na nimeona kwenye taarifa humu kwamba shamba lile limerudishwa kwa wananchi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi langu, Mheshimiwa Waziri atusaidie uhamisho huu ukamilike. Kwa sababu tunapozungumza sasa hivi, huyo mwenye nalo ameshatushtaki, kwa hiyo, tuna kesi na kwa bahati mbaya ni kesi ambayo inabidi tuje kuisemea Dar es Salaam na kwa bahati mbaya Mafia hatusafiri ila kwa ndege kwa sababu hatuna meli ya kuaminika. Ndiyo pale nikagomba sana kuhusu sh. 400,000/= mlizotupangia TAMISEMI kama usafiri, kwa sababu ile ni safari moja tu na nusu kwa sababu ndege sisi tunalipa return kwa 350,000. Sasa ni wazi kabisa hii kesi sisi itatushinda. Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Waziri achukulie hii kama special case ili jambo hili liishe haraka iwezekanavyo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nyongeza katika hilo, liishe pia kwa kutuwekea mipaka ya vijiji vyote vitano vinavyozunguka pale, kwa sababu nimeona kwenye hotuba humu ya Mheshimiwa Waziri, amesema ni vijiji vitatu, sasa pia sivijui ni vijiji gani. Lile shamba la Tumaini linagusa Vijiji vya Jojo, Kirongwe, Baleni, Gonge na Kithinge. Sasa sijui vitatu vipi vimepimwa na viwili vipi vimebaki, lakini ingekuwa ni vizuri zaidi hili tukalikamilisha liishe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna hiyo pia ndiyo itakuwa mwendo mzuri sasa wa kushughulikia masuala, tusiwe tunafanya hii nusu nusu; tunagusa, halafu tunaacha halijakamilika, tunaliachia katikati. Kwa hiyo, naomba tena kwa msisitizo kabisa, suala hili likamilike kwa haraka iwezekanavyo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, naomba nizungumze kidogo kuhusu masuala ya huduma ya upimwaji ardhi. Sijui kwa nini niliposoma kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri naona hata hao wahitimu kwenye fani hii ni wachache. Najiuliza ni kwa nini? Sikuona, labda kama ipo, wahitimu wa Chuo Kikuu cha Ardhi, sikuona. Nimeona Chuo cha Morogoro na Tabora nadhani. Ni wachache mno! Hawa watu wanahitajika, tatizo ni nini? Hatuwafundishi. Vyuo hivi havina miundombinu ya kutosha kusomesha watu wengi au ni nini hasa tatizo?
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia lingine niulize, hivi Serikali inashindwaje kubeba jukumu la kutoa huduma hii? Tatizo ni nini mpaka tunaletewa sasa wapimaji binafsi ambao nao wanakuja na masharti magumu sana, wananchi wanashindwa? Utaambiwa shamba lako kama ni ekari tatu, watakwambia sijui watakutumia heka ngapi uwape na wao sehemu ama wanakutajia pesa nyingi na wananchi wanashindwa. Nilidhani hii ni huduma ya msingi kabisa Serikali ibebe na ifanye kwa taratibu kabisa. Kwani Serikali inashindwa nini kusema mwaka huu tunapima labda mikoa miwili, mwaka ujao mikoa mengine! Kwani nchi yenyewe ni kubwa ya kiasi gani Mheshimiwa Waziri? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba sana suala hili la ardhi hebu lishughulikiwe kama walivyosema wengi kwamba ardhi ndiyo kila kitu. Tunahitaji ardhi tuwekeze, tunahitaji ardhi tuishi tu humo kwenye majumba yetu na mambo mengine yote yanahitaji ardhi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Naomba tu nami nimalizie kwa kusema tena kwamba, naunga mkono hotuba ya Kambi ya Upinzani kwa sababu imeonesha reality na tuifuate. Ahsante sana.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa fursa. Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na ardhi aliyetujaalia sisi sote uzima na afya na akatupa upendeleo maalum kutuweka kwenye jengo hili tujadili kwa niaba ya Watanzania mamilioni kile ambacho kina mustakabali mwema kwa nchi yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niruhusu nisome tafsiri ya maandiko matakatifu kutoka kwenye kitabu wanachofuata Waislamu cha Qurani na kiongozi wao Mtume Muhammad (SAW). Kuna hizi aya mbili, moja wapo nakumbuka nilishawahi kuisema hapa lakini nitairudia tena, ya kwanza iko katika Sura inaitwa Sura Hajj ni aya 46 ambayo inasema; “Hivi hawatembei katika ardhi, wakawa nyoyo ambazo wanafahamu kwa nyoyo hizo? Au masikio wakasikia kwa masikio hayo? Kwa hakika yanayopufua si macho bali ni nyoyo zilizomo ndani ya vifua.”
Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu kuna aya nyingine iko kwenye Sura Araf na ni aya ya 179 hii inasema; “Hakika tumeumba moto wa Jehanum kwa ajili ya watu wengi na majini pia kwa sababu...” wataalam wanasema pale kiunganishi “...kwa sababu wana nyoyo lakini hawafahamu kwa nyoyo hizo, wana macho lakini hawaoni kwa macho hayo, wana masikio lakini hawasikii kwa masikio hayo, hao ni sawasawa na wanyama bali wao ni wapotevu zaidi kuliko wanyama kwa sababu hao ni wenye kughafilika.” Hadithi ya Mtume (SAW) ikasema; “mapambano yaliyo bora zaidi ni neno la haki mbele ya mtawala jeuri.” (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, huyu mtawala ana ngazi, tunaweza kumzungumzia Rais, mkuu wa utawala wa muhimili mmoja naweza kuwa Spika na wasaidizi wake muhimili mwingine, anaweza kuwa Jaji Mkuu na wengine wanaomsaidia. Lakini pia kwenye ngazi za Mawaziri na wote ambao kwa pamoja wanatengeneza utawala. Katika wazungumzaji mmoja jana alisema; “Aah! nina wasiwasi kama vile hatuelewi tunachotakiwa kufanya kwa sababu kila anyesimama analalamika,” hatulalamiki, ndiyo tunachangia! Na ile inakuja kwa sababu ya hali halisi. Tulisema mwaka huu huu tukipitisha, tukijadili bajeti kwamba jamani mbona hapaoneshi kwamba kuna integrated system ya haya tunayo yajadili? Wa viwanda akisimama anaruka ruka, anachachatika, hatuoni viwanda! Akisimama wa Miundombinu na Maji utadhani maji yatatoka kesho kwenye mfereji wanasema jamaa zangu, hakuna kitu! Akisimama wa usafiri ATC imefufuliwa, Bombardier zimenunuliwa, ziko wapi? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa Mafia siku chache kabla ya kuanza vikao vya Kamati nikawapigia simu watoto wangu nyumbani hebu harakisheni ATC mkanifanyie booking ndege ya Dodoma. Wakaniambia mama hazijaanza kwenda! Aaah! Mimi nilidhani ndiyo ingekuwa kituo cha mwanzo hapa! Wateja tupo wengi wa uhakika, haipo. Lakini hii Mpango unasema tena kufufua ATC watu wanapiga makofi, watu wanashangilia, jamani hebu tuone kwa nyoyo zetu kwa sababu ni hizi nyoyo ndiyo zilisimama pale zikaapa. Kila mmoja wetu na katika kiapo kile tunaweka ahadi na huyo mwenye mamlaka zaidi na pia ndiyo tunakubali kwamba hayo mamlaka yapo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana kupitia kwako hebu tuzingatie ile sala tunayoomba hapa kila asubuhi, lakini pia kupitia kwako hebu jengeni mazingira ya kuwa tunamkumbuka Mwenyezi Mungu kila wakati, labda itatujengea hofu na kusema kweli tuna dhima kubwa hapa ndani ya jengo hili, isiwe ushabiki tu! Tunasema jamani haya mambo yako so broad! Yaani ni mapana kiasi kwamba inasikitisha hata kusoma, alisema msemaji hapa kwamba huu ni mwaka wa pili na ni mwaka mmoja, kulikuwa na mwaka kabla yake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, laiti tungepata assessment ya mwaka ule japo miezi michache tu ile ndiyo ikawa msingi sasa wa kufanya huu mwaka huu, humu background information nadhani kuna majedwali mengi hapa ukurasa wa 18 mpaka 24; hivi unapozungumzia mpango wa mwaka mmoja tu mwaka wenyewe ni 2017/2018 unapotoa data za mwaka 2013 ambazo wala hazisaidi hata ule Mpango wenyewe wa miaka mitano ambao mkubwa ndiyo ukatolewa huu mdogo. Sasa nikasema huu ni mpango wa mwaka huu au ni nini na tatizo ni nini? Ndiyo hiyo copy and paste au ni kwamba taarifa tu ilimradi buku lijae iletwe? (Makofi)
Mheshimiwa Mweyekiti, nadhani hatutendei haki, tuletewe mpango ambao ni mahsusi na niliposema hapa kikao kilichopita kwamba mbona hamna kile wanachoitwa wataalam measurable targets yaani tukiangalia hapa tunasema hapa tumesema mwaka huu tutatoka point moja twende point mbili. Niliguswa zaidi wakati ule na suala la afya na nikasema mahsusi suala la vifo vya akina mama linalotokana na uzazi, wakati ule kulitokewa na figure pale, sijui 400, kati ya watu 100,000, nikawauliza jamani sasa kwa mwaka huo mmoja mmepanga kitu gani hapa? Mbona ni namba tu ambayo haina mwelekeo wowote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, aliposimama mjibu hoja, akasema jamani kweli hamna humo tena kwa ile sauti yake kama vile kaonewa au mtu anasema uongo, sasa mara hii ndio limekuja broad kabisa, katika ukurasa 54 mpaka 55 kipengele 6.4.2 afya na ustawi wa jamii wanasema kupunguza vifo vya akina mama vinavyotokana na uzazi basi mara hii hata namba hamna.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vifo vyenyewe peke yake viko aina chugu nzima hivyo vifo vya uzazi viko aina chungu nzima, kwa mwaka huu ni vifo gani mnavitarajia kuvifanyia kazi, na kutoka vingapi mpaka vingapi huu mwaka mmoja tu, mbona haya mambo yanakuwa hivi jamani halafu mnasema tunapanga na kuna wanaosema maneno wanasema if you fail to plan, you plan to fail. Tukishindwa kupanga ina maana tunapanga kufeli au kushindwa, hivi kweli Taifa hili tunakaa watu mamia humo tumeacha mambo mengine yote kuja kujadili hili, jamani hebu tuitendee haki nchi hii, hebu tuwatendee haki wananchi wetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango huu haukubali kwamba hali ya uchumi umeshuka jamani kwa ukweli wa dhati ya mioyo yenu hivi kweli Watanzania wangapi sasa hivi wana purchasing power ambayo inafanana kidogo tu na ile ya mwaka jana, yaani ule uwezo tu wa kumiliki yeye maisha yake mwenyewe kwa kile kipato anachokipata kuanzia mama ntilie mpaka maprofesa wa chuo kikuu, ni wangapi kweli purchasing power yao ni kweli inawawezesha hawa kuishi maisha ya kuaminika au maisha angalau kidogo yanampa mtu ahueni, akasema nina mshahara, nina kazi, nina kibarua, nina kipato cha kuaminika. Tunafanya uigizaji sekta isiyo rasmi kila mtu ajiajiri, sekta isiyo rasmi inajengwa na sekta iliyo rasmi. Viwanda vinaeleweka, wafanyakazi idadi fulani inaeleweka, mshahara wao unaeleweka kwa hiyo tunajua kiasi fulani cha pesa kitaingia kwenye mzunguko. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hatuweki mambo tu hivi hivi, na ndio maana hata huu mpango wenyewe wote ukasimama wanasema wasemaji matofali ya barafu ambayo wala hayajengi nyumba.
Mheshimiwa Mwenyekiti, miongoni mwa mambo yanayotajwa kwamba ni msingi ambao mpango huu umesimamia ni amani, usalama, utulivu ndani ya nchi kweli. Nchi hii ina amani? Wataalam wa amani wanasema peace is not the absence of war yaani kukosekana vita sio kwamba mna amani, lazima kuwepo na mifumo mizuri ya kijamii ambayo ina mhakikishia kila mtu haki yake inampa utulivu, inamhakikishia maisha yake ya kila siku, nani nchi hii leo hii, Mbunge hana uhakika kama nikitoka hapa Dodoma nitafika Dar es Salaam bila kukamatwa na askari, nitadaiwa pesa isiyokuwa na mbele wala nyuma.
MWENYEKITI: Ahsante.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kushukuru kuwa nimepata nafasi ya kuchangia kwa kuzungumza kuhusu hoja hii jana tarehe 2 Novemba, 2016.
Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo la kuwa na mpango wenye malengo mapana yasiyopimika limejitokeza tena katika Mpango wa 2017/2018 kama ilivyokuwa kwa mpango wa 2016/2017. Inasikitisha sana kuona kuwa Serikali inadhani inajua kila kitu na kwamba inachokisema na inachoandaa ni sahihi. Tunapochangia hoja za Serikali, nia huwa ni kuboresha hoja husika kwa maslahi ya nchi yetu na si vinginevyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile tatizo la kukosekana utengamano (integration) wa Wizara mbalimbali linaonekana tena katika mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2017/2018, kama ulivyokuwa kwa ule uliotangulia. Hili ni tatizo kubwa kwani ndicho chanzo cha kuwa na mipango isiyotekelezeka na bajeti isiyowezeshwa. Vipaumbele vinakuwa vingi mno kutekelezeka katika mwaka mmoja na hata kwa miaka mitano.
Mheshimiwa Naibu Spika, huu Mpango unarudia kusema kuwa miongoni mwa misingi inayoisimamia na kuendelea kuidumisha ni amani, usalama, utulivu na utengamano wa ndani wakati ukweli ni kuwa yote hayo hayapo. Serikali ya Awamu ya Tano inatumia mabavu na vitisho kukandamiza mfumo wa Vyama Vingi na demokrasia iliyojengeka nchini kwa miongo miwili sasa. Vyama vya Upinzani viko katika mazingira magumu sana na mara nyingi inatokea misuguano isiyo na lazima na vyombo vya dola.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni ukweli kuwa Serikali haioneshi kuwa na utashi wa kujenga utengamano kati ya Tanzania Bara na Zanzibar. Tatizo la kuvurugwa kwa Uchaguzi Mkuu wa 2015 na kesi ya Mashehe wa Zanzibar walioko mahabusu ya Tanzania Bara ni vielelezo tosha vya hali hiyo. Kilichojitokeza kwa suala la Mashehe ni kuwa Tanzania Bara inatumika kama Guantanamo ya Zanzibar.
Mheshimiwa Naibu Spika, Kiongozi Mwandamizi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar alisikika akisema hadharani kuwa wataoleta fujo Zanzibar watapelekwa bara kama wenzao akina Farid waka…
Mheshimiwa Naibu Spika, katika hali kama hii, huwezi kusema nchi ina amani, amani ni neno pana na halina maana ya kutokuwepo vita tu. (Peace is not absence of war) mifumo ya kuleta amani na utulivu inavunjwa na kuharibiwa na Serikali zote mbili zilizo madarakani. Naamini Wazanzibari wengi hawafurahishwi na hali hii, kinachotisha zaidi wamekaa kimya. Serikali inajiaminisha kuwa ukimya huu unaashiria amani, mimi siamini hivyo kwa sababu hiyo. Naishauri Serikali kujenga amani ya kweli nchini ili kujenga mazingira mazuri (wezeshi) kwa utekelezaji wa masuala muhimu mbalimbali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii nchini ukiwemo Mpango wa Maendeleo unaopendekezwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, wachangiaji wengi wamezungumzia suala la mdororo wa uchumi, na mimi naunga mkono. Nashauri Serikali isijivunie takuwimu za kupanda uchumi bila ya kuangalia ni vipi takwimu hizo zinajionesha katika maisha ya wananchi. Ni lazima mabadiliko au hali ya uchumi mkubwa (Macro-economy) ihusiane na uchumi mdogo (micro-economy) ambao unagusa hali ya maisha ya mwananchi mmoja mmoja.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli alilizungumzia suala hilo wakati alipokutana na watendaji wa Benki Kuu, kwa kweli ni jambo lenye mantiki. Haiwezekani Serikali ijivunie kuimarika hali ya uchumi wa nchi wakati hali ya maisha ya wananchi walio wengi inadidimia au haiendani na hali hiyo ya nchi/Taifa.
Mheshimiwa Naibu Spika, namsihi Mheshimiwa Waziri husika na Serikali kwa ujumla kuzingatia mapendekezo mbalimbali yanayotolewa na Waheshimiwa Wabunge ambayo kama nilivyosema awali yanatolewa kwa nia njema na kwa manufaa ya nchi.
Mheshimiwa Naibu Spika, siungi mkono hoja na badala yake namshauri Waziri Mpango, aisome kwa umakini taarifa ya maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2017/2018.
Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 - Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa
MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichangie kwa kutoa masikitiko yangu katika maeneo mawili tu. Moja ni suala la kutumia vibaya Jeshi letu la Ulinzi (JWTZ). Si sahihi hata kidogo kwa jeshi letu kutumiwa kuvuruga shughuli za kidemokrasia nchini hasa chaguzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hali ni mbaya na ya kutisha Zanzibar. Binafsi nilipata fursa ya kuwa Zanzibar wakati wa uchaguzi mdogo wa marudio Jimbo la Dimani. Nilishuhudia malori ya JWTZ yaliyobeba “mazombi” watu waliovalia sare za jeshi na soksi usoni (wakijificha) walioshikilia silaha juu yakienda na kurudi barabara ya Fumba. Kwa hakika nilishtushwa sana na tukio hili na kwa heshima kubwa namwomba Mheshimiwa Waziri akomeshe vitisho hivi na matumizi mabaya ya jeshi letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili linalonisikitisha ni Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kushindwa kujitegemea kiuchumi na kulisaidia Taifa. Hili ni jeshi lenye makambi karibu nchi nzima na nguvu kazi ya kutosha ya vijana wetu wanaokwenda huko karibuni muda wote. Jeshi lina mashamba makubwa, miradi ya mifugo, ujenzi na kadhalika. Ni vipi Jeshi hili lishindwe kuendesha kilimo cha kisasa na chenye tija? Waziri kwa kweli alifanyie kazi suala hili ipasavyo. Kwa wataalam wa fani mbalimbali waliojaa JKT ni aibu kubwa kuwa na jeshi la aina hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine dogo ninalopenda kuchangia kwa leo ni kuomba Bunge kuipa Wizara hii hadhi yake stahiki yaani kuwa Wizara ya Muungano. Kwa hadhi hii Wizara hii inastahiki kupewa muda wa kutosha kwa Wabunge kuchangia kwa nafasi badala ya kupangiwa siku moja tu ambayo inaanza kwa kipindi cha maswali na majibu. Nililisema Mkutano wa Bunge la Bajeti ya mwaka uliopita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili ni Bunge la Jamhuri ya Muungano na siyo la Tanzania Bara. Imekuwa ni tabia/ mazoea ya Bunge hili kutumia muda mwingi (mpaka siku tatu) kujadili masuala ya Tanzania Bara tu (Kilimo, TAMISEMI, Afya na kadhalika) badala ya masuala ya Muungano (Ulinzi, Mambo ya Nje, Ofisi ya Makamu wa Rais na kadhalika).

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho naomba Waziri mhusika aipitie vizuri hotuba ya Kambi ya Upinzani, kwa uadilifu na bila hiyana kwa maslahi mapana/ya jumla ya nchi yetu na maslahi mahsusi ya walinzi wetu (wanajeshi) wa majeshi yote mawili –JWTZ na JKT.

Mheshimiwa Mwenyekiti nakushukuru na naunga mkono hotuba ya Kambi ya Upinzani na kumtakia kila la kheri Waziri wa Ulinzi kwa jukumu nyeti na muhimu alilopewa na nchi yetu.
Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nianze kwa kusema kwamba naunga mkono hoja… MWENYEKITI: Dakika tano wote. MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nianze tu kwa kusema kwamba nawapongeza Wajumbe wa Kamati zote tatu kwa kazi nzuri waliyofanya lakini nitachangia zaidi taarifa ya Kamati ya Ulinzi na Usalama na Mambo ya Nje. Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kusema ufike wakati sasa hili Bunge lijione kwamba ni Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa hiyo zile Wizara za Muungano zipewe kipaumbele, hadhi na uzito na ustahili. Wizara ya Ulinzi na Usalama na Wizara ya Mambo ya Nje ni Wizara za Muungano lakini siku zote huwekwa pembezoni na matokeo yake haijadiliwi ipasavyo. Ukiangalia hivi vijitabu tulivyopewa cha Mambo ya Nje na Ulinzi ndiyo kibaya kuliko vyote, hata pini hazijakaa sawa, maandalizi yake hovyo, wakati ni mambo muhimu sana ya Jamhuri ya Muungano. Naomba hili lizingatiwe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu hiyo basi hata zile taasisi zilizoko kwenye Wizara ya Mambo ya Nje kwa mfano na zenyewe pia hazipewi uzito unaostahili. Chuo cha Diplomasia ni taasisi nyeti sana. Nchi yoyote ile taasisi inayohusika na masuala ya mambo ya nchi za nje inapewa uzito.
Chuo hiki kimekuwa chuo utadhani sijui cha kutengeneza watu gani! Hakina miundombinu mizuri, hakina vifaa vya kufundishia, Walimu wake wako so local! Mtu anafanya first degree mpaka PhD Mlimani pale hatoki mpaka anastaafu – huyu mtu atafundisha vitu gani jamani? Lazima walimu hawa wapewe exposure, wapelekwe nje, wapewe in service training periodically ili waandaliwe na wao waweze kuandaa foreign service officers wetu ipasavyo. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, msongamano magerezani. Wamesema waliotangulia kwamba kuna watu wanawekwa mahabusu miaka. Tumeimba kesi chungu nzima, ya Masheikh tumeisema, sasa ni miaka minne ni mahabusu, kesi hazisemwi, watu mnaambiwa kumerundikana! Serikali haiamui, Serikali haiko serious. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati za Bunge haziwezeshwi ipasavyo. Nilitarajia Kamati ya Mambo ya Nje ionane na wadau, miongoni mwao wawepo pia wanafunzi wetu wanaosoma katika nchi mbalimbali basi angalau hao walioko kwenye nchi jirani hapa za Afrika Mashariki. Nimesikia baadhi ya wanafunzi wakilalamika wanavyokuwa mistreated, bahati mbaya ni katika nchi moja jirani mwenzetu Afrika Mashariki kwamba hawa wanalipishwa ada tofauti na vile ambavyo wangelipishwa na vilevile hawapati treatment kama amember country ya East African Community. Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna hiyo Inter-University Council ya East Africa ambayo inasemekana inashughulikia masuala haya, lakini ni muda mrefu sana hayapati ufumbuzi. Kwa hiyo, naamini kama hizi Kamati zingewezeshwa watu kama hawa wangeweza kufikiwa na Kamati za Bunge na masuala yao yangeweza kushughulikiwa ipasavyo. Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia nizungumzie kidogo kuhusu…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nianze kwa kurudia masikitiko yangu niliyoyatoa katika Mkutano wa Bajeti ya mwaka jana kuhusu muda mchache unaotengwa kujadili hoja ya Wizara hii muhimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukumbuke kuwa Bunge lako Tukufu ni Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo si haki kulinyima muda wa kutosha kujadili suala hili muhimu la Muungano. Ifike muda uongozi wa Bunge ubadili utaratibu uliozoeleka wa kutenga muda mchache wa kujadili Wizara za Muungano, zikiwemo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, pamoja na Wizara ya Muungano, (Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano).

Mheshimiwa Mwenyekiti, inatia uchungu kusikiliza na kusikia yaliyosemwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu hali ya utendaji ya Wizara hii na hali ya Balozi zetu nje ya nchi. Hivi ni kweli Serikali haioni umuhimu wa kuwa na majengo mazuri yenye hadhi kuwakilisha taswira ya nchi yetu? Ni aibu kubwa kwa nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimuombe Waziri husika aisome kwa makini hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani na ayafanyie kazi yaliyomo kwa uadilifu mkubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni jambo la kusikitisha kuona Wizara na Serikali kwa ujumla kuendelea kufanya kazi kwa mazoea. Bado Wizara hii haiainishi mkakati madhubuti wa kutekeleza Sera yetu ya Mambo ya Nje hasa kuhusiana na diplomasia ya kiuchumi. Hotuba ya Waziri haina taarifa yoyote kuonesha mkakati wa kuhakikisha nchi yetu inapata wawakilishi nje ya nchi na watendaji kwenye Wizara husika wenye sifa na walioandaliwa ipasavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, watendaji wa Wizara yetu ya Mambo ya Nje wanatakiwa kuandaliwa katika maeneo mahsusi ya maeneo (regional specialization), kisha watendaji hawa walioandaliwa ipasavyo ndio wapande ngazi Wizarani na hatamae kuwa wawakilishi (mabalozi) wetu nje ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, inakuwa ni mazoea, kwa Serikali kuteua mabalozi wa kutoka nje ya Wizara. Hii inakatisha tamaa watendaji wa Wizara lakini pia inadhalilisha fani ya mambo ya nje (foreign service). Foreign service ni profession kama zilivyo professions nyingine. Wahusika hupata mafunzo na kukidhi vigezo maalum.

Mheshimiwa mwenyekiti, wengi wamesema kuhusu Chuo chetu cha Diplomasia - Kurasini. Chuo hiki kitendewe haki, kipewe hadhi stahiki kwa kuhakikisha kinawezeshwa kujenga mazingira ya kufundisha maafisa wetu na vijana wetu kwa ujumla. Wizara ikisaidie Chuo kuwa na walimu mahiri na wenye maslahi mazuri.
Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi; nami nianze kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia neema kubwa ya uhai na uzima na afya na tukawa hapa. Nimpongeze kaka yangu aliyemaliza kuzungumza Mheshimiwa Maji marefu kwa kutimiza ada muhimu sana. Mafunzo yanasema ukitendewa jema basi mshukuru yule aliyekufanyia jema mpaka ahisi kwamba ameshukuriwa. Naamini Waheshimiwa Wabunge na wote uliowashukuru walihisi kwamba umewashukuru na sisi tunamshukuru Mungu kukurejesha tena hapa hata tukawa na wewe. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, babu zangu wa Kimwera wanasema hizi Kamati hizi they have seen it all. Kwa kweli Kamati zimefanya kazi, Wenyeviti wao wametuletea hapa taarifa, hakuna kilichobaki humu; na wachangiaji walionitangulia nao wamechangia, wamesema waliyoyasema, sasa hayo nitakayoyasema mimi itakuwa ni nyongeza tu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na suala la kuchezea elimu. Elimu nchi hii tunaikoroga, elimu nchi hii tunaichezea na hatujiamini bado kama elimu ndiyo ufunguo wa maisha ingawa huo msemo upo kila mahali, elimu ni ufunguo wa maisha, lakini matendo yetu hayaendani na hilo. Naomba tu kwa msisitizo kabisa, hebu Serikali ibadilike. Waheshimiwa Wabunge humu wameshasema sana kuhusu suala la elimu, its time now.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali hii ya CCM miaka yote hiyo iliyopita ni CCM tu hakuna ya Rais huyu, Serikali ya CCM, sasa ibadilike, ione kwamba ina jukumu la kusimamia elimu na elimu ni kweli iwe ufunguo wa mambo yetu yote yanayofuata. Dada zangu mmepewa Wizara hili tutawapima tu! Kwa hiyo, Profesa na Msaidizi wake wajipange kwenye elimu, mabadiliko tunayataka, yenye uweli si haya ya kutubadilishia mara mtaala, mara nini, hapana!
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la UKIMWI; na hili nalisema kwenye kipengele cha utegemezi. Wataalam wameimba kuhusu madhara ya kutotumia dawa ipasavyo. Mgonjwa wa UKIMWI ukishamkatizia dozi yake, iwe ile ya dozi yenyewe au ile inayoitwa dawa za kuondoa magonjwa nyemelezi, unamuathiri zaidi kwa sababu vile vijidudu vinajenga usugu; sasa tunashangaa nini inapoonekana kwamba haya maradhi hayaondoki na maambukizi yanazidi kwa sababu hata hiyo tiba yenyewe hatuifanyi swa sawa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la utegemezi; kila mahali Kamati imetuambia hapa; kuanzia utafiti, kutoa hizo huduma zenyewe za madawa tunaambiwa wafadhili ndio wafanye hivyo. MCC hiyo arijojo, imeshaondoka sasa sijui tuna nini mbadala kwenye suala hili ambalo kwa kweli ni janga.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ujumla wake taasisi zetu za huduma muhimu haziko sawa. Tunajua hali za hospitali zetu, zahanati zetu, vituo vyetu vya afya, wamesema hapa na Kamati zimesema; lakini pia tunajua hali ya shule zetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, miezi kadhaa nilipita mahali kule Jimboni kwetu, kuna eneo Kaskazini kunaitwa Bweni nilikuwa nakwenda Bweni sasa hapo katikati unapita mahali panaitwa Kirongwe. Tulikuwa tunapita kwa haraka kwa gari lakini nikaona watoto kama wanacheza cheza hivi kwenye majengo mabovu sana. Sasa nikawa nauliza wale wenzangu, hiki hapa ni nini? Wakaniambia ndiyo shule ya msingi Kirongwe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikasema watoto wanakuja kwenye majengo haya? Hizi ndiyo shule zetu lakini hapa Serikali Kuu inatuambia kwamba Halmashauri ndizo zishughulikie hizo, Halmashauri ambazo tayari zimeshaondolewa uwezo wa kusimamia hayo kwa maana ya kupunguziwa vyanzo vyao vya mapato. Sasa sidhani kama kweli tunataka kuleta maendeleo kwenye jamii hii kwa sababu mambo yetu maneno ni mengi kuliko utekelezaji na matendo yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna wimbo huu wa ufinyu wa bajeti na sasa umekuwa wimbo wa kutopeleka pesa zilizopangwa, sasa kuna haja gani ya kufanya hii budgeting process?
Mheshimiwa Mwenyekiti, mkutano uliopita nilisema hapa kwamba hivi hii bajeti ya nchi yetu kwa nini isiwe mchakato unaojitegemea, yaani uliounganika yaani intergraterd process ya budgeting? Ndiyo maana tunapata haya matatizo. Tunazungumzia hiyo semina elekezi, semina elekezi si lazima tuambiwe A, B, C lakini semina elekezi pia isaidie kupanga pia vipaumbele.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hawa Mawaziri wote wakikutanishwa pamoja waka-brainstorm kwa pamoja jamani vipaumbele mwaka huu ni nini? Haya matatizo, kwamba kule hakukupelekwa, huku hakikutolewa hayatotokea tena, au angalau yatapungua kwa asilimia kubwa; lakini kila mtu hapa anakaa peke yake, anasema ana vipaumbele, vipaumbele vyenyewe vinakuwa zaidi ya 20.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kila anayesimama hapa kipaumbele, kipaumbele mwisho wake tunaimba hii kila siku nenda rudi ni yale yale hatubadiliki, tatizo ni nini jamani? Wasomi ndio hao na kama kuna Serikali imejaa maprofesa ndiyo hii, hebu tuone basi mabadiliko. Hizo elimu na ujuzi wenu wekeni kwenye vitendo ili tuone kweli ninyi mnataka, mnaambiwa mainjinia; tulikuwa tunawaita ma-spanner boys; basi na wao wafanye kazi ya vitendo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, limezungumzwa pia suala la kutaka ufafanuzi kuhusu kuwepo au kutokuwepo kwa madawa; tena hili mimi naomba litolewe maelekezo kweli kweli. Huo ufafanuzi uwe ufafanuzi wa kweli. Kwa sababu Serikali ikizungumza kupitia Mawaziri wake iwe wa Afya au wa TAMISEMI unaona pepo kabisa kwenye zahanati, lakini wakisimama wale watumishi wetu walioko kule ma-DMO na wengine unaona ufukara uliokithiri, tatizo ni nini hapa? Mawaziri wanatuambia madawa yamejaa, sijui basket fund imeleta kila kitu, DMO akisimama akikwambia unaona kabisa ana-negative wala hata siyo zero, hili tatizo liko wapi? Hebu watupe maelekezo ya kutosha kwamba dawa zipo au hazipo?
Mheshimiwa Mwenyekiti, labda nimalizie kwa kusema kwamba na mimi ni-declare interest na mimi ni Mwalimu. Dada yangu Mwalimu Susan amesema Walimu wamedhalilishwa kiasi cha kutosha na kuonewa kiasi cha kutosha, sasa huu msemo unaishia kusema na tunasema sasa basi. Hebu Walimu wa nchi hii wapewe hadhi yao, wapewe haki zao, Walimu hawa wanadhalilika. Niliwataja siku moja hapa Walimu walionifundisha toka shule ya msingi wengine wakasema wako hai, wako hai baadhi wa miaka 70 na, lakini ukiwaona unaona huyu mtu aliishi na anaendelea kuishi japo ameshazeeka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, walimu wetu wa sasa ndio watu dhalili, dhalili mpaka kwenye jamii yenyewe hawathaminiwi. Mwalimu anafika mahali anamwogopa mwanafunzi wake kwa sababu mwanafunzi anatoka kwenye hali ya juu kuliko Mwalimu. Kwa sababu gani Walimu wetu wanafanywa kuwa ombaomba, watu dhalili, watu wasiothaminiwa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, mateso wanayopata Walimu; Mwalimu Susan amesema kama unataka kuboresha elimu anza na Mwalimu. Mwalimu ambaye mmemjali yuko tayari kuchukua watoto wake akawafundishia chini ya mwembe na wakapata elimu bora, lakini Mwalimu ambaye umemdhalilisha, umemdharau, hata ungemjengea chumba ambacho kina feni na viyoyozi hatafundisha na watoto wale wakafundishika. Jamani hebu tuangalie mzizi wa tatizo uko wapi na tuutatue ule, tusihangaikie matawi, matawi hayajengi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa nafasi uliyonipa na niwapongeze tena Kamati hizi kwa kazi nzuri na niseme naunga mkono hoja yao. Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake pamoja na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018.
MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Nianze kwa kumshukuru zaidi Mwenyezi Mungu kwa kutupa uhai na uzima na afya na kutuchangia sisi kuwa miongoni mwa waja wake ambao leo wameweza kuendelea na shughuli zao ambazo wamejipangia.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nianzie hapo ambapo Mheshimiwa Mtolea ameishia; na hili; mimi bahati niko kwenye Kamati ya Katiba na Sheria; tulilizungumza na tulisema pia kwenye Kikao cha Kamati, kwamba kuna taasisi za Serikali ambazo ziko chini ya ofisi nyingine kubwa za Serikali, utendaji wao kazi unakuwa ni mbaya na mbaya kiasi cha kuweza kuhataraisha hata usalama wa nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, yanayofanywa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa yana hatari kwa sababu, kwanza yanahatarisha hata muungano wetu kwa sababu wanachezea chama ambacho kina nguvu sana upande mmoja wa muungano na chama ambacho kwa sababu
yake watu wengi wa upande huo wa muungano waliteseka, walikufa na wengine bado wana vilema vya kudumu mpaka hivi sasa. Anachezea Chama cha Wananchi – CUF, taasisi ambayo imeundwa kwa miaka mingi, watu wamejitolea nafsi zao na kila kitu chao kwa ajili ya taasisi hii. Hii ni taasisi kubwa ambayo watu hao hawatakubali kuona inaharibiwa namna hii na watakapofikishwa mwisho, kile ambacho watakifanya kitakuwa na hatari. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, niliwahi kusema hapa, kwamba hata namna Serikali inavyofanya kazi inatujengea uhasama na inatuvunjia udugu kati ya pande mbili za muungano, kwa sababu upande mmoja unatumia kama ndio torturing centre au camp ya upande mwingine. Kwa sababu zilitolewa kauli kwenye Bunge hili au na baadhi ya viongozi wa siasa wa juu kabisa wakasema wanaofanya makosa upande mmoja wa muungano waletwe upande mwingine ambako watashughulikiwa ipasavyo. Hii ni hatari. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kinachoniumiza zaidi ni ile kuona kwamba hizi taasisi ni subsidiaries tu, yaani ni taasisi ndogo, kama nilivyosema mwanzo, zinasimamiwa na taasisi nyingine, lakini Ofisi ya Waziri Mkuu binafsi sioni inafanya nini kukemea ofisi hii ambayo iko chini yake. Msajili wa vyama vya siasa anavuruga, lakini katika majukumu makubwa ya Ofisi ya Waziri Mkuu ni kujenga mahusiano mema kati ya
Serikali na vyama vya siasa. Hebu tupate maelezo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, wanalifanyaje hili wakati wanaona wazi Ofisi ya Msajili wa Vyama inavuruga vyama vya siasa, inahatarisha au inaharibu mahusiano mema kati ya Serikali na vyama vya siasa? Tupate maelezo ya kina na hasa katika hili linaloendelea ndani Chama cha Wananchi – CUF.
Mheshimiwa Naibu Spika, labda niongeze zaidi kwenye hili itaeleweka zaidi, kwamba, hizi taasisi ambazo ziko chini zinapoachiwa namna hii ndio tunaona hata ufisadi. Tumeambiwa hapa, kwenye ripoti nyingi tu, ya mkaguzi na hata taarifa zinazotolewa na Wizara husika, kwamba kwa
mfano mashirika yetu ya umma mengi hayafanyi kazi vizuri au yanafanya kazi katika namna ambayo, zile bodi zenyewe zinashindwa kusimamia mashirika, lakini Wizara mama pia, zinashindwa kusimamia mashirika! Vinginevyo tusingekuwa tunaona taarifa hizi zinazoitwa ma-scandle sijui ya NSSF na wengine au taasisi kama hizi security funds kuwekeza kwenye miradi ambayo haina tija.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu, pamoja na kwamba, taasisi hizo zina bodi zao, lakini pia hizi zinakuwa chini ya Wizara mama. Ofisi ya Waziri Mkuu ni mojawapo inasimamia NSSF, lakini katika mambo ambayo yalikuwa yamesemwa hapa ya kasoro kiutendaji ni hivyo. Sasa
tunajiuliza hivi inakuwaje kwamba, yule anayekabidhiwa ulezi hatazamwi tena yule mtoto anamlea vipi?
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu, haya yote yanatokea mpaka tukafikia hapo Bodi inawezekana zimeshindwa kufanya kazi, lakini Wizara mama ndio zimeshindwa zaidi kwa sababu, zimeshindwa kuchukua hatua kabla ya kufikia uharibifu mbaya. Nasema tena kwa msisitizo, suala hili linalofanywa na Msajili wa Vyama vya Siasa Ofisi ya Waziri Mkuu iwajibike ipasavyo na itupe maelezo ya kina.
Mheshimiwa Naibu Spika, lingine litakuwa ni masuala haya ya ujumla tu, namna gani vijana wa nchi hii wanavyokosa uhakika wa maisha yao na tuna wizara kama hii, lakini wakati mwingine mimi nikasema labda haya maneno yamekuwa mengi kwenye hii Wizara. Ofisi ya Waziri
Mkuu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, Watu Wenye Ulemavu, yote haya yako mahali pamoja na sasa hivi naona mwanangu Mheshimiwa Mavunde kabaki peke yake Msaidizi wa Waziri, sasa sijui haya mambo yanakwendaje? Vijana wa nchi hii wanatakiwa kuhakikishiwa usalama wao, wanatakiwa kuhakikishiwa heshima yao, wanatakiwa kuhakikishiwa kweli hiyo tunayoita hawa ndio Taifa la kesho au Taifa in the making, basi kweli wawe hivyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, vitisho wanavyopata vijana wetu sasa hivi vya kutekwa, vya kupotezwa, kwa kweli vinasikitisha. Binafsi niliwahi kuwa karibu na ndugu Ben Saanane, mwanangu Ben Saanane, katika kama siku tatu hivi. Kwa hiyo, kila linapotajwa jina lake hapa mimi naleta picha mama yake Ben, najiweka mimi kwenye nafasi ya mama yake Ben, anafanya nini mwanamke yule sasa hivi? Hebu wanawake wa Bunge hili, tuungane kumdai Ben kwa ajili tu ya mama yake Ben na si kwa sababu nyingine yoyote. Hebu Serikali itwambie kijana huyu na vijana wengine hawa wanaokamatwa na kurushwarushwa kila wakati wanafanyiwa nini na wategemee nini kutoka kwenye nchi yao hii? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tuelezwe vijana wetu na hasa Ben Saanane na nawaomba tena wanawake wa Bunge hili tumsemee mama yake Ben. Kila jina hili likitajwa mimi naamini wanawake ambao tumepitia labor ward, tunarudishwa kwenye machungu yale, kwa hiyo hili lifanyiwe
kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, taasisi nyingine ambayo iko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ni hii Kamisheni ya Usuluhishi wa Migogoro. Nitatafuta ile kesi mahsusi nitampa mtendaji yule kwa sababu aliniomba, lakini kuna taarifa hizi za jumla pia ambazo nilikuwa naomba sana wazifanyie kazi. Kwamba utendaji wa taasisi hii unaonekana kama vile hausaidii sana upande wa Serikali, kwamba kesi zinazopelekwa kule hazishughulikiwi vile ambavyo tungetarajia. Kwa hiyo, Serikali inabeba mzigo zaidi wa kulipa gharama na fidia kwa ajili ya wale ambao wanakwenda mbele ya Kamisheni hii kwa ajili ya kutatuliwa migogoro yao. Kwa hiyo, hilo naomba pia Serikali itupe maelezo juu ya namna gani hii taasisi nayo inatusaidia.
Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho kabisa niizungumzie Tume ya Uchaguzi. Kama taasisi nyingine zilizo chini ya Ofisi hii na yenyewe nayo ina mazonge yake mengi. Tunashuhudia amani ya nchi hii inahatarishwa sana na ujumla wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, kwa maana ya hizi taasisi zake ndogondogo zilizoko humu. Tume yetu ya Uchaguzi lazima iwe na maelekezo, iwe kwenye nafasi inayostahiki. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nathubutu kusema kwamba, uchaguzi wa kuchagua Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, pia umevurugwa sana na Tume ya Uchaguzi, kwa sababu msimamizi wa uchaguzi ule alikuwa ametwambia kwamba yeye pia alikuwa anataka kupata taarifa zaidi za uthibitisho kwamba, nani ndiye, nani siye kutoka Ofisi ya NEC. Inavyoelekea NEC ikampa maelezo kwamba kutoka Chama cha Wananchi – CUF watu wanne wote wanafaa waje hapa na wagombee na tuliwaona mbele hapa.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa napata wasiwasi kwenye taasisi muhimu kama hizi ambazo tunazikabidhi majukumu muhimu kama haya ya kuendesha nchi hii yanavurugwa, lakini kama nilivyosema tena, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi inayolea haitoi kauli wala haioni kama inaguswa na matatizo haya.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa ujumla basi, kama itakuwa kupitishwa bajeti, tunasema ile value for money iwe pia kwenye huduma. Je, tunapitisha bajeti kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu kwa huduma hizi inazotoa? Nini inafanya mpaka kweli ituhakikishie sisi kwamba, inastahili kupata pesa hizi kwa ajili ya hizi taasisi zake zifanye kazi wakati huduma yenyewe inayotolewa mimi ninaiita ni chini ya kiwango?
Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Katiba na Sheria
MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, Muumba wa mbingu na ardhi ambaye kwa matakwa yake mwenyewe ametuchagua sisi kuwa miongoni mwa waja wake ambao amewatunuku uhai na uzima na akili timamu na akawajalia pia kufanya kile ambacho wamejipangia wenyewe kukifanya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa imani ya dini yangu, katika mambo ambayo tunaambiwa tuyafanye kwa wingi sana ni kukumbushana kwa sababu katika kukumbusha hutoa msaada kwa wale wenye kuamini. Nami nalifanya hilo nikiamini kabisa kwa dhati ya moyo wangu kwamba nyumba hii imejaa wenye kuamini. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kitabu ambacho kwa dini yangu nakiamini, Kitabu cha Quran, kuna aya ya 54 iko katika Sura ya 36 na sura hii kwa jina lake mahsusi inaitwa “Surat Yaseen” na kwa hadhi yake hii sura ndiyo inaitwa ndiyo moyo wa Quran. Katika hiyo aya ya 54 inasema:-
“Iangalieni ile siku ya hukumu ambapo haitadhulumiwa nafsi chochote na wala haitolipwa isipokuwa yale ambayo imeyatenda”. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niliseme hili kama tahadhari kwetu sisi sote, iko siku ambayo hakuna chochote ambacho tutaulizwa isipokuwa kile ambacho tumekitenda hapa. Kwa imani ya dini yangu, maisha ya kila siku, mahusiano yetu, kusoma kwetu, kuwa Wabunge kwetu yote haya yataulizwa siku hiyo na hayo ndiyo katika hayo ambayo tunayatenda. Kwa hiyo, naomba nitoe hiyo tahadhari na nimwombe Mwenyezi Mungu ashuhudie kwamba nimewakumbusha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niendelee kuchangia kwa kusema kwamba naunga mkono hoja hotuba hii ya Waziri Kivuli wa Kambi ya Upinzani lakini pia mengi yaliyomo kwenye taarifa ya Kamati ya Katiba na Sheria hususani yale ambayo yameelezwa ukurasa wa 18 na 19 kuhusu msisitizo wa kuangalia masuala mazima ya haki za binadamu hasa yakiendana na namna ambavyo vyombo vya kutoa sheria ikiwemo Mahakama vinavyotakiwa vitende haki. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi sitaki kuhoji Mahakama zinafanyaje kazi lakini nataka kuhoji sera za nchi hii, sheria na taratibu kuhusu masuala ya haki za binadamu. Mheshimiwa Waziri amesema hili na Kamati imesema na Waziri Kivuli amesema namna gani kesi zinacheleweshwa, namna gani mahabusu na wafungwa wanateseka katika nchi hii lakini tumenyamaza kimya au hatuchukui hatua inavyostahiki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Mashekhe ambao wanaoza mahabusu kwa miaka minne sasa ambapo suala lao linapigwa danadana hilo sijui kama siyo suala la haki za binadamu au siyo katika zile kesi ambazo taarifa zote hizi zimesema lazima masuala ya upelelezi yakamilishwe katika wakati ambao ni reasonable. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jana Mheshimiwa Waziri huyu ambaye yuko leo na hoja yake Mezani lakini jana alikuwa anatupa utaalam kama Profesa wa Sheria, alipokuwa anazungumzia Sheria ya Ndoa alisema kwamba, kuna kitu kinaitwa legal anthropology. Ombi langu ni kwamba hii legal anthropology sipati maneno sahihi lakini ninachotaka kusema ni kwamba isiangalie tu masuala ya abstract, zile values ambazo huzioni, lakini pia iangalie masuala ambayo ni real and tangible, yale unayoyaona.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hili, inapokuja suala la dini, viongozi ni katika values hizo. Sasa tunapoona viongozi wetu wa dini wanadhalilika, wananyanyasika kwa miaka nenda, rudi, mjue mnatukwaza kiimani na mnateteresha hivyo vitu ambavyo mnasema legal anthropology inaviangalia kwa umakini sana. Kaka yangu Mheshimiwa Profesa Kabudi utanisamehe huko mwishoni kama nitashika shilingi ya mshahara wako. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Profesa Kabudi kama ambavyo Waziri Kivuli amesema hapa kwenye ukurasa wa nne kwamba hakuna shaka yoyote kwamba Ripoti ya Tume ya Warioba na Rasimu ya Katiba Mpya ina alama za vidole vya kitaalam vya Profesa Kabudi, ni kweli. Ninachoongeza tu ni kwamba alikuwa ana wasaidizi wake kama proof-readers wake, wanawake wawili, mmoja napenda nimtaje Mheshimiwa Kibibi Mwinyi Hassan, mwingine kwa leo nahifadhi jina lake, walifanya kazi ile kwa kukesha, tukatoka na document zile na mimi nilibahatika kuwa katika Tume ya Warioba.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Ripoti ile haikuzumngumzia tu pendekezo la Katiba Mpya lakini kuna masuala kadhaa ya kijamii, kisheria, kitaratibu ambayo Tume ya Warioba iliandaa kwa volumes na zikakabidhiwa Serikalini. Laiti mchakato ule ungefikishwa mwisho haya mambo yote hapa tunayozongwazongwa nayo sasa hivi yasingekuwepo. Taratibu zingekaa sawa, Katiba Mpya ingepatikana masuala yote haya tunayosema huyu asitajwe, huyu asifanywe hivi yalishajadiliwa na wananchi kwa kina kabisa mpaka suala la viroba na zile suruali ambazo vijana wetu wanavaa, wananchi walilisema. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kama tungeupeleka mchakato mpaka mwisho wake yale yote yasingekuwa issue sasa hivi, lakini imekuwa hivyo kwa sababu suala la Katiba Mpya limekuwa kizungumkuti, sasa sijui nikisema limepigwa kaputi nalo nitaambiwa msamiati siyo, lakini ni katika lahaja tu na nadhani Waziri anayehusika na utamaduni alisimamie hili. Lugha yetu ya Taifa ni Kiswahili, tutumie utajiri wa lugha hii, tutumie lahaja ambazo zinaleta ladha masikioni, lugha ina ladha yake masikioni. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika suala hilo la Katiba Mpya masuala ya maadili ya kijamii, mila na desturi zetu, tunu hizi za Taifa ikiwemo lugha yetu, uongozi na mihimili hasa mihimili hii mitatu versus masuala ya vyama vya siasa yamefanyiwa kazi vizuri kabisa. Wananchi walisema hatutaki kumuona Spika ambaye ni m-NEC, hatutaki kumwona Rais ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Siasa na walitaja kwa vitu specific lakini hatukulifanyia kazi sasa hivi tunahangaishana hapa kila kinachosemwa kinaambiwa sicho, kila kinachoandikwa kinaambiwa kifutwe, lakini kile kisu cha jana kile kwa bahati mbaya kimebaki humu na kinaendelea kutesa watu, mimi sijui kisu gani. (Makofi/ Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeshuhudia humu asubuhi haki ya msingi kabisa ikitetereshwa ambayo ni haki ya kujieleza. Hivi Mbunge, Waziri Kivuli anapozongwazongwa, anapokatazwa kueleza kile ambacho yeye ana imani nacho inashangaza. Mimi nitashangaa sana ikiwa Mawaziri Vivuli wa Kambi hii watarudia yale hotuba za Mawaziri wa upande ule itakuwa kituko! Yule Waziri akisema tumefanya kila kitu na Waziri Kivuli naye aseme Serikali ile imefanya kila kitu, itakuwa kiini macho gani hicho? Hebu tupewe haki hii ambayo tunaizungumzia hapa, haki za binadamu, utawala wa sheria uachwe utekelezwe katika nchi hii. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kaka yangu Mheshimiwa Profesa Kabudi amevishwa viatu au sijui amevishwa kilemba hiki ambacho inabidi akifanyie kazi sawasawa. Namshauri asisite kushauri mamlaka husika kuhusu utawala wa sheria unavyotakiwa kufanya kazi kwa sababu sasa hivi tumefikishwa mahali ambapo hatujui twende kwa sheria au kwa matamko.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria inasema, vyama vya siasa vipewe ruzuku vifanye kazi, vifanye shughuli za kisiasa ikiwemo mikutano ya hadhara. Matamko yanasema, hakuna kufanya kazi za siasa, hakuna mikutano ya hadhara mpaka tarehe fulani, kipi ni kipi? Hii haifai na haikubaliki katika nchi ambayo tunasema tunafuata utawala wa sheria, tuna demokrasia ya vyama vingi lakini zaidi tunasema kila siku tuombeane dua, tuombeane Mungu, hatuwezi … (Makofi)
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
HE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa fursa na mimi kama ada nianze kumshukuru Mwenyezi Mungu muumba mbingu na ardhi, aliyetujalia uhai, uzima na afya na akatuwezesha kuwa hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nianze hapo alipomalizia Mheshimiwa Halima kwa kuzungumzia suala la kunusuru akina mama na vifo wakati wa ujauzito. Mimi nimeogopa kweli labda kwanza nianze kusema naipongeza Kamati ya Bunge husika kwenye Wizara hii kwa ripoti yao hii na naunga mkono hoja hii ya wao walichosema na pia ripoti ya Kambi Rasmi ya Upinzani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukurasa wa 33 Kamati inasema bajeti hii inayoitwa Support to Maternal Mortality Reduction imepungua kutoka shilingi bilioni 13 mpaka shilingi bilioni nane. Mheshimiwa mdogo wangu Ummy ana lile tangazo lake anatoka sana kwenye televisheni “Kama
Halmashauri zinataka kuona kipaumbele cha kunusuru wakina mama watatenga pesa.” Wizara yenyewe inapunguza bajeti, Halmashauri itatenga pesa za kutosha kutosha kutoka wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jamani tuishi yale tunayoyasema, kama kweli tunataka kunusuru akina mama hawa wanaotimiza jukumu la msingi, kweli tuwatengenezee mazingira ya kuwanusuru na tusiwanusuru kwa maneno tu. Hii inauma na haikubaliki, mdogo wangu Mheshimiwa Ummy nakuelewa, nakufahamu na ninakuamini katika utendaji kazi wako, hili lirekebishe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine linaloendana na Halmashauri kubebeshwa mzigo ambao hawauwezi ni haya masuala ya kuhakikisha huduma za msingi kama afya zinatolewa ipasavyo. Ajira zinatangazwa Serikali Kuu, watu wanaomba halafu wanapangiwa kwenye Halmashauri, kisha watu hao wanatakiwa washughulikiwe na Halmashauri. Halmashauri hizi hazina uwezo, mbaya zaidi hii tofauti ya uwezo wa Halmashauri inajenga matabaka ya watendaji wa kada moja katika sehemu mbalimbali za nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nani midwife professional ataenda kukaa Mafia ambako Halmashauri yenyewe hohe- hahe aache kukaa Kinondoni kwenye mabilioni huku? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali Kuu ishughulikie wafanyakazi wa kada hizi nchi nzima. Nurse wa Mafia, nurse wa Kinondoni na nurse wa Ilolangulu huko wote wapate hadhi sawa, kwa maana ya mishahara na stahiki nyingine. Vinginevyo yale maeneo ya pembezoni yataendelea kuwa ya pembezoni na watumishi watatukimbia kila siku. Hili lirekebishwe watu wapate stahiki zinazostahili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mafia in particular jamani ni kisiwa, tena kisiwa kile kilichosahauliwa. Hatuna usafiri wa kuaminika ambao watu wengi wangeweza kutumia wa meli, Hospitali ya Wilaya x-ray hatuielewi na vipimo vingine sijui vitendanishi na vitu gani, mpaka kumpima mama mjamzito kuangalia tu mkojo wake, ile kama sijui kuna vidude gani vingine visivyotakiwa, sukari na vitu vingine hakuna vitu vya kuwezesha kufanya hivyo. Sasa watu hawa wakipata dharura tunawapeleka wapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mafia huko hospitali hiyo haijiwezi, majeruhi chungu mzima wanaovunjika, tunawafanya nini? Hata tukimudu kuwatia kwenye ndege, ndege zetu zinazokwenda ni hivi vidogo vya private companies vya eight seaters sijui 13 seaters; kumuingiza mgonjwa mle aliyevunjika mguu au aliyevunjika ni mtihani, angalau maeneo kama haya yangepewa kipaumbele. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii Serikali inayofanya mambo kwa jumla bila kuangalia specific case kama hizi kwenye masuala kama haya ya afya na mengineyo naona siyo sahihi lazima Serikali ibadilike katika kuweka mipango yake na kutuambia wananchi kwamba kweli wanataka kutupa huduma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilisema kwenye kikao kilichopita tubadilike kwenye budgeting process yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, niruhusu nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Waziri kwa mageuzi makubwa aliyoyafanya na anayoendelea kuyafanya katika Wizara hii. Namtakia kila la kheri na ni matarajio yangu kuwa tutafika mahali pazuri pa kuwa na Wizara na Taasisi zinazowajibika ipasavyo. Katika sekta hii muhimu sana kwa maendeleo ya kijamii katika nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na pongezi na dira hizi naomba nimshauri Mheshimiwa Waziri, kupitia kwa kina bila hiyana hotuba ya Kambi ya Upinzani na kuyafanyia kazi mengi ya mapendekezo yake. Sote katika Bunge lako hili Tukufu tupo kwa maslahi ya wananchi wetu na si vinginevyo na hivyo tukishirikiana itapatikana tija zaidi nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia nimshauri Mheshimiwa Waziri, kushughulikia kwa kina suala la kuwapatia na kuwahakikishia watumishi wa umma nchini makazi bora na ya uhakika katika maeneo mbalimbali. Hivi sasa NHC inaonekana kuweka mkazo zaidi katika kujenga na kuuza badala ya kupangisha hata kwa watumishi wa umma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, watumishi wa umma kwa asili yao si watu wa kudumu katika maeneo yao ya kazi bali katika maeneo yao ya kuzaliwa. Hivyo msisitizo unapowekwa katika kuwauzia nyumba watumishi panatengeneza mazingira ya kuwafanya watumishi wa umma, kutaka kubaki maeneo waliyopangiwa na wakati mwingine kutumia hata njia chafu kuhakikisha kuwa hawa hawahamishwi. Hali hii si zuri kwa kujenga kada ya watumishi wa umma waadilifu na walio tayari kutumikia popote nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata Wabunge wako wengi nikiwemo mimi mwenyewe, tumehangaika kwa zaidi ya mwaka na nusu sasa kutafuta makazi ya kukaa hapa hapa Dodoma, Makao Makuu ya Serikali. Hii ni dalili wazi kuwa Wizara hii na Serikali kwa ujumla haijatoa kipaumbele au haijajipanga ipasavyo katika eneo la makazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana.
Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kuwa nilipata dakika chache za kuchangia kwa kuzungumza, hivyo, maelezo haya ni nyongeza ya mchango wangu huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ndiyo Taifa lenyewe. Bila ya afya, bila mazingira mazuri ya wazee wetu na watoto wetu, bila mfumo nzuri wa jinsia - mahusiano ya wanawake na wanaume maendeleo ya jamii hayatapatikana. Kwa masikitiko makubwa Wizara hii imekumbwa na tatizo sugu la utendaji wa Serikali ya CCM tatizo la kutopeleka fedha zinazoidhinishwa na Bunge kwa Wizara na Taasisi husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Taarifa ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii inasema katika ukurasa wa 19 kuwa, bajeti ya Wizara hii kwa mwaka 2016/2017 haijatekelezeka kwa asilimia 60%. Hii ni kwa mujibu wa takwimu za mwaka 30 Machi, 2017. Hii ni kucheza na uhai na maisha ya Watanzania/wananchi wetu. Katika mjadala wa bajeti kwa mwaka 2016/2017, nilishauri kuhusu kubadili mfumo/utaratibu/mchakato wa bajeti nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchakato wa bajeti unafanyika kama ni jambo la kawaida tu kufanyika miaka nenda rudi matatizo na kasoro zile zile zinaendelea kujitokeza lakini Serikali haioneshi dalili za kubadilika ili kuwa na mchakato wa bajeti inayotekelezeka na unaoweza kuleta tija katika jamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ambalo napenda kuishauri Wizara na Serikali kwa ujumla kulifanyia kazi kwa umuhimu wa kipekee ni takwimu kuhusiana na upungufu wa wataalam wa afya zilizotolewa na hotuba ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani kwenye ukurasa wa saba. Picha hii inatisha sana na si jambo la kupuuzia hata kidogo. Tukibadili mchakato wa bajeti na kuufanya kuwa ‘integrated’ itasaidia kuwa na vipaumbele vichache vya Taifa badala ya huu utaratibu wa sasa unaokuwa na vipaumbele vingi kwa kila Wizara, matokeo yake ndiyo hili tatizo sugu la bajeti zisizotekelezeka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, intergrated budget process itasaidia kuondoa tofauti kubwa za kimaendeleo na utoaji huduma za msingi za jamii. Kujenga barabara za kisasa, flyovers na usafiri wa mwendo kasi katika Jiji la Dar es Salaam, kwa kigezo cha mchango wake katika pato la Taifa ni sawa lakini muhimu vilevile kuangalia spill-over effects zake kwa maeneo mengine na haki ya Taifa. Maeneo mengi ya vijijini likiwemo Jimbo langu la Mafia yanaendelea kubaki nyuma katika maendeleo na upatikanaji wa huduma muhimu zikiwemo za afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Hospitali ya Wilaya ya Mafia ina matatizo lukuki kuanzia wafanyakazi mpaka vifaa, inafikia wakati Nesi mmoja anapangiwa wodi mbili. Uwepo wa hospitali iliyo kamili/inayojitosheleza ni muhimu sana kwa Wilaya ya Mafia kutokana na jiografia yake kuwa kisiwani. Wilaya ya Mafia haina usafiri wa kuvuka kwenda Dar es Salaam au Mkuranga ili kupata huduma kama za X-ray au rufaa husika. Namwomba Mheshimiwa Waziri aiangalie Hospitali ya Wilaya ya Mafia kwa jicho la kipekee.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hotuba ya Kambi ya Upinzani na taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge. Hata hivyo, nawapongeza sana Waziri na Naibu wake kwa uwajibikaji wao mahiri. Ni matumaini yangu Serikali itawapa mazingira mazuri ya kufanya kazi hii adhimu. Nashukuru sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Fedha na Mipango
MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia uzima hadi kufikia wakati huu tukijadili bajeti ya pili toka niingie katika Bunge lako Tukufu. Katika mjadala wa bajeti wa mwaka huu wa fedha tunaomalizia, 2016/2017, nilisema humu katika Bunge lako Tukufu kwa namna wataalam na hivyo Wizara hii mahsusi inayohusika na suala hili wanavyofanya suala hili muhimu kimazoea tu. Hii maana yake ni kuwa Wizara hii inaonesha kushindwa kutekeleza majukumu yake muhimu kama Waziri alivyoorodhesha katika hotuba yake hasa yale ya ukurasa 75 mpaka ukurasa wa 80.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara hii inahusika au ndiyo yenye jukumu la uandaaji na usimamizi wa utekelezaji wa Bajeti ya Serikali? Mheshimiwa Waziri atueleze ni vipi jukumu hili muhimu sana kwa uhai na mustakabali wa nchi yetu wamelitekeleza? Wizara zote zilizowasilisha bajeti zao zimeonesha hali ya kusikitisha kwa namna mipango, matarajio na utekelezaji wa malengo na majukumu yao ulivyokuwa chini sana. Eneo la bajeti za maendeleo kwa Wizara zote ndiyo limeathirika zaidi kwa kutopelekewa fedha ambazo Bunge lako Tukufu liliidhinisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hali imekuwa mbaya katika maeneo yanayogusa moja kwa moja maisha ya wananchi kama vile afya, maji na huduma za usafiri, lakini pia katika eneo ambalo linabeba hadhi ya nchi yetu katika Jumuiya ya Kimataifa kwa maana ya Wizara ya Mambo ya Nje. Hotuba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Taarifa ya Kamati husika ya Bunge ameeleza hali za Balozi zetu nje ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara hii inaandaaje bajeti zisizotekelezeka? Bajeti ya Serikali maana yake ni hizi bajeti za Wizara moja moja. Wimbo umekuwa ni ule ule miaka nenda miaka rudi. Kutenga fedha, kutopeleka fedha kunakohusika, kushindwa kutekeleza yale yaliyopangwa. Hebu tufike mwisho kwenye hili. Serikali ipeleke fedha zinazoidhinishwa na Bunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilisoma bajeti iliyopita na Waheshimiwa Wabunge wengine na hasa Kambi Rasmi ya Upinzani wanasema kwamba tuwe na vipaumbele vichache vinavyotekelezeka badala ya wataalam kuachia Wizara kuwa mipango isiyotekelezeka. Hivi wataalam hawajui au ni nini hasa kinachoendelea?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna uwezekano kwa sehemu nyingine za hotuba hii ya Mheshimiwa Waziri kwamba imerudia tu yale ambayo imekuwa ikiripoti miaka yote (i.e. cut and paste). Mheshimiwa Waziri anasema katika hotuba yake, ukurasa wa 75 aya 125, kuwa katika mwaka 2017/2018 itafanya uchambuzi na tathmini ya miradi ya kuondoa umasikini ngazi ya Wilaya na Vijiji. Hivi ni kweli muda wote huu uchambuzi na tathmini haijafanyika/haikufanyika? Utekelezaji utakuwa lini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mengi yamesemwa na Waheshimiwa Wabunge wengi waliopata fursa ya kuchangia kwa kuzungumza kuhusu masuala halisi kama vile deni la Taifa kutovumilika, viporo visivyomalizwa kama Tume ya Pamoja ya Fedha, mfano ya wastaafu, riba za mabenki kwa mikopo kwa wananchi, ahadi ya milioni 50 kila kijiji na mengine yote yakionesha kushindwa kutekeleza yanayopangwa au yanayoahidiwa na Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimalize kwa kuiomba Wizara hii ibadilike, ijipime kwa namna inavyotekeleza majukumu yake. Hivi ni kweli inaridhika na utendaji huu? Mbona Mheshimiwa Waziri na Mheshimiwa Naibu Waziri wake ni watu makini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.
Muswada wa Sheria ya Upatikanaji wa Habari wa Mwaka 2016
MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu muumba mbingu na ardhi ambaye kwa mapenzi yake mwenyewe ametupangia na ametuamulia na akatuchagua sote kuwa hapa leo, lakini kubwa akatupa uzima na afya njema.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nifuatie kwa kukushukuru wewe kwa kunipa fursa hii na mimi nichangie kilichopo mezani kwetu japo kwa uchache kwa sababu mengi yameshasemwa toka jana. Baada ya kukushukuru niseme jambo moja na lenyewe ni kitendo ambacho kinasemwa ni kitendo bora kufanywa hapa duniani, kitendo hiki ni kuhusiana kumcha Mwenyezi Mungu.
Kwa hiyo, na mimi nachukua nafasi hii kuwausia pamoja na kuusia nafsi yangu kumcha Mwenyezi Mungu. Maana yangu ni kwamba tunapousiana hivyo basi tunausiana kuchunga mipaka katika kila tunalolifanya na katika kila tunalolitamka, kwa sababu wale wanaoamini kama mimi kwa upande wetu, tunaamini kwamba kila tunalolifanya hapa duniani haliishii hapa, hiyo siku tunayoiita siku ya hukumu tutaulizwa pia. Naomba niliseme hilo ili siku hiyo nitasema niliwakumbusha wenzangu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Muswada huu kama nilivyosema pale awali yamesemwa mengi, lakini nifuatishe kwa nasaha kwamba tunatengeneza sheria hapa, sheria ambazo wenye lugha yao wanasema; they can either break or make hii jamii yetu, kwa hiyo, tuwe na tahadhari sana. Tusije tukatoka na sheria ambazo badala ya kutengeneza zikabomoa, badala ya kusaidia zikaumiza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wasemaji wanasema sana kuhusu wenyewe wanaziita claw back clauses kwenye kutengeneza sheria au hata kama zile ambazo zimo kwenye Katiba. Ukiangalia Muswada ambao uko mbele yetu hapa leo una hizo claw backs clauses nyingi tu, kwamba jambo linasemwa vizuri lakini kikija kifungu cha sita ukikiangalia mwanzo mpaka mwisho unaona kama jambo lenyewe kumbe halitakiwi. Ukienda kwenye kifungu cha 10 unaambiwa uandike, ufanyeje! Ufanyeje, sasa kwa nini wakasema yote yale kwa mfano kwenye hicho kifungu cha 10 na kwa nini tusijikite tu kwenye kifungu cha 10(4) ambacho kinasema, nadhani ndiyo hicho kinatoa ruhusa kwamba asiyeweza kuandika na mambo mengine kwamba atasema tu pale kwa mdomo huyo mhusika anaweza yeye akajaza basi iwe hivyo. Tunakwenda kwenye maofisi fomu iko pale, mimi naitwa fulani nataka taarifa, kinachukuliwa kikaratasi kama hiki tunachoomba hapa kuchangia, unajazwa jina lako na ile taarifa unayotaka inapelekwa hapo.
Mhehimiwa Mwenyekiti, wengi wamesema kuhusu muda, hivi kuna haja ya kusema tusubiri siku 30 na hilo litatumika. Hao wenye taarifa watalitumia hilo. Mimi nakwenda kituo cha polisi, naenda kumuona OCD kwa sababu kuna watoto vijana wamepotea kwenye Wilaya yangu, kwenye Jimbo langu. Wazazi wanalalamika, wanasema hata tukienda hatusikilizwi, najipiga kifua nakwenda mimi kama Mbunge, naambiwa eehh mama sasa tuandikie hapo, tuandike nini? Watoto fulani na fulani wa nyumba kadhaa wamepotea na wamepotea kwa sababu wamechukuliwa na askari wako Mheshimiwa OCD niambie, naambiwa niandike. Hivi hizo taarifa nazo ni za kuandika?
Sasa labda tuseme ni taarifa za namna gani kama itabidi huu Muswada ushughulikie yote hayo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapata taabu sana kwamba masuala kama haya ya Miswada na bahati hii Mwenyezi Mungu ametusaidia katika Wizara ya Katiba na Sheria yupo msomi wa sheria, ambaye mimi siyo tu ninamheshimu kama kaka yangu, lakini pia huwa napenda kumpa daraja ya mwalimu wangu, ingawa hakunifundisha lakini marafiki zake wa karibu Profea Mahalu, Profesa Peter na Profesa Kabudi wamenisomesha, kwa hiyo Mheshimiwa Mwakyembe pia napenda kumpa heshima ile. Ninampa heshima hiyo kwa sababu miongoni mwao hawa wanamtaja kwa uzuri, napenda sana ule uzuri ninaousikia kwa wale wenzake ujioneshe hapa kwenye kazi hii, kwenye mamlaka haya, kwenye jukumu hili alilopewa kulisimamia. (Makofi)
Mheshimiwa Mwakyembe tuongoze tutoke na miswada ya sheria na tuje tutengeneze Sheria kwenye Bunge hili ambalo tutaishi sisi na vizazi vyetu waje waseme yes! tulikuwa na Ph.D kwenye Wizara ya Katiba na Sheria na these are the laws ambazo zilifanywa kwa wakati huo, nakusihi sana tusaidie hilo. Kwa maana hiyo basi tutaanza na muswada huu, Kamati ya Kudumu ya Bunge imesema, Kambi ya Upinzani imesema tutengeneze sheria ambayo kweli inatufaa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kifungu cha sita kina utata sana, kifungu cha 19 kina walakini mwingi tu. Kifungu 19(2) kinasema; “Mkuu wa Taasisi ndani ya siku 30 baada ya kupokea maombi yaliyofanywa chini ya kifungu kidogo cha (1) ataamua maombi kwa mujibu wa taratibu walizojiwekea.” Taasisi wamejiwekea wenyewe taratibu, mimi ninayekwenda kuomba taarifa sijui taratibu hizo lakini ninabanwa na taratibu hizo. Maslahi ya umma, umma ni nani kama syo mimi? Pia kuna hizo zinazobana. (Makofi)
Mheshimwa Mwenyekiti, kwa hiyo kwa kweli napenda tuuangalie huu muswada kwa namna ya kipekee na nilikuwa nawauliza wenzangu wanaojua zaidi taratibu na sheria hivi kusoma mara ya pili na mara ya tatu na kuhitimishwa na kupitishwa maana yake nini? Kama hatuna ulazima huo tuurudishe ufanyiwe kazi. Nasema hivyo kwa uzoefu mdogo pia niseme kwamba mara nyingi hizi kazi zinafanywa kwa speed ya ile kama tunazima moto vile. Tunawa-overwork wataalam wetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niliwahi kupata uzoefu kidogo nikiwa kwenye Tume ya Mheshimiwa Warioba, wale vijana tulikuwa tunawa-overwork mpaka wengine wanakuja asubuhi unamhisi mtu anatetemeka hivi, kwamba hajapata hata muda wa kupumzika, na nilivyowaona wachache waliokuja kwenye Kamati yetu unahisi hivyo, wana mengi hawa vijana, kama tunapanga hizi sheria kwa ajili yetu, jamani tuzipe muda, wataalam wetu tuwape muda walete mambo ambayo kweli yanasaidia na siyo kama haya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, seriousness inaonekana pia katika kuamua mnafanya nini. Hii karatasi hii inaitwa order paper au imeandikwa Orodha ya Shughuli za leo inasema tunajadili Muswada wa Sheria ya Upatikanaji Habari. Hii imeandikwa leo, jana Mheshimiwa Waziri kasema ni Muswada wa Upatikanaji Taarifa, sasa tunasema ya jana taarifa au ya leo habari? Tunachojadili hasa ni Muswada upi? Kama kweli tunataka kuwa precise na kujua tunajadili na ndiyo maana unatuona humu tunaogelea, kwamba wanaokuwa na upande wa habari unaonekana habari lakini taarifa nayo inatofautiana vipi na hiyo habari nayo pia haieleweki.
Kwa hiyo, sasa hayo pia ni masuala ambayo tungependa sana tuyaone yakifanyika katika Bunge lako hili, wengine tunapata hofu zaidi kwa sababu tulisimama pale, tukashika kitabu, tukaapa na kila siku siku asubuhi humu tunaapa kwamba tutatumia busara zetu, tutatumia hekima yetu ili tutengeneze sheria ambazo zina maslahi na zinaleta haki na usawa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, je, tujiulize hizo sheria ambazo tumeshazitengeneza au zimeshatengenezwa na Bunge lako zimesaidia vipi, hizi sheria kama hizi ambazo zinaletwa kisha zikajadiliwa katika mihemko ya kisiasa na kebehi na maneno ambayo hayajengi na wengine wanatoka kabisa nje ya mada tena unawavumilia halafu unawaambia kwa uwezo wako ulivyojadili na kuchangia, sijui kama inatusaidia kweli. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ningeomba sana labda kwa uzoefu wangu wa kuwa mwalimu na huu uzee unaonikaribia nakuwa very conservative, lakini kuna mambo ambayo ningependa kabisa seriousness i-prevail, tujadili haya mambo kwa maslahi ya Taifa letu, kizazi hiki na kizazi kijacho. (Makofi)
Mheshimiwa MWenyekiti, sidhani kama nina mapya mengi labda nikushukuru na nina hakika wengine pia watachangia zaidi na kama nilivyoomba, nafasi zaidi itatolewa who to shelf kwa muda tutoe muda zaidi ili tuje na Muswada na baadae sheria iliyo nzuri zaidi.
Ninakushukuru na nimalizie tu kwa lile jambo bora kwamba nawausia pamoja na kuiusia nafsi yangu tumche Mwenyezi Mungu na kwa maana hasa ya kumcha. Nakushukuru.
Muswada wa Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo, wa Mwaka 2016
MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu Muumba mbingu na ardhi kwa kutujalia afya na uzima. Kisha nakushukuru kwa kunipa fursa nami ya kuchangia Miswada ambayo tunayo mbele yetu. Mengi yamekwishasemwa kwa hiyo, nami nitakuwa na machache tu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kuilinganisha yote miwili nikiwa na uelewa kwamba taasisi hizi mbili ambazo sheria zake tunazitengeneza hapa zina uzito sawa na zinatarajiwa zitendewe haki sawa na Serikali hii. Sasa kwanza zenyewe ukiziangalia zote mbili, Miswada yote miwili, ukiangalia sababu za kuundwa kwake na ukiangalia jina lake, kuna walakini. Kwa hiyo, sitaki kwenda kwenye details kwa sababu ya muda, lakini naomba na kumsihi Mheshimiwa Waziri apitie kwa utaratibu kabisa na kwa kina, aangalie pale zinapoelezwa sababu na madhumuni, halafu aangalie na title. Kwa kweli nimeona kwa kupitia tu, haziendi sawa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo liko kote, nimeona suala la maslahi au posho. Sasa kwenye hizi documents mbili, moja inazungumzia posho kwa Wajumbe, lakini nyingine inazungumzia marupurupu. Sasa kwa kile nilichosema mwanzo kwamba tunatarajia ziwe treated equally, huwezi ukazungumzia posho halafu mwingine ukasema unampa marupurupu; hayo ni mambo mawili tofauti.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kwenye suala hilo hilo la hayo malipo au marupurupu, kwingine kunawekwa Msajili wa Hazina anahusika lakini kwingine inasemwa Waziri tu na Bodi. Sasa nadhani kuna mambo ya kuyapitia tena ili tuweze ku-harmonise ili mwisho wa siku tukitoa sheria ziwe kweli sheria zile ambazo tunazitarajia, unless Waziri aseme kwamba taasisi hizi hazitarajiwi kuwa na hadhi sawa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie pia suala lingine la ujumla la gharama. Kwenye moja ya document hii inaelezea sababu mojawapo ni kuondoa duplication, yaani kurudiarudia na vilevile kupunguza gharama. Sasa the mere fact kwamba tunaanzisha hizi independent institutions kila mahali, hiyo by itself ina maana tunaleta gharama na kuna uwezekano mkubwa wa ku-duplicate haya mambo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge wengi waliochangia pia wameeleza hayo; wanauliza, kwa mfano, nani anasimamia hizi mwisho wa siku? Kwa sababu ziko nyingi mno. Kwa suala la gharama peke yake, unapoanzisha Bodi, kuna Mwenyekiti, Makamu wake, Wajumbe hao wote wana haki na stahiki mbalimbali; hizo zote ni gharama Waheshimiwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna Mheshimiwa mmoja alizungumza, nafikiri ni Mheshimiwa Jitu kwamba kwenye nchi nyingine za wenzetu, masuala kama haya unayakuta yako embedded kwenye higher learning institutions. Vyuo vikuu vyetu vyenyewe zinakuwa ni research based universities; most of them.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hii inasaidia siyo tu kujenga human resource ambayo ni skilled na ina uwezo mkubwa, lakini pia inaimarisha vyuo vyetu kwa sababu vinakuwa vina research ambazo zinafanyika kwa muda wote. Wale walimu na ambao wengine wanakuwa specialized kama researcher professors only, lakini wanakuwa na kazi hiyo ya kufanya ambayo pia inawajengea uwezo wanafunzi wetu. Hii inapunguza gharama kama nilivyosema, lakini pia inajenga uwezo wa watu wetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye Muswada wa Kilimo. Waheshimiwa Wabunge wengi hapa wamezungumzia suala la masoko, sasa kwa kuwa huu Muswada wenyewe hauna uhakika sana, ukisoma, kwa sababu hata pale kwenye item, kwenye ukurasa huu wa 61 ambapo kunataja maeneo ya utafiti; 61 inaendelea mpaka 62, hata pale kwenye ile item (8) ambayo inazungumzia utafiti wa uchumi, jamii na masoko, hakuna masoko pale. Kuna ki-item kimoja tu ndiyo kinazungumzia masoko, lakini mengine yote siyo masoko. Hayo masoko yenyewe, kuna document nyingine samahani siwezi kuwa very specific, inasema kuimarisha hayo masoko.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sisi kwa mifano tuliyoiona kwenye TV wiki iliyopita tu na wiki hii, tunaimarisha masoko au tunatakiwa tutafute masoko? Ikiwa nyanya tu za Moshi na Kilosa pale zinaoza, unaimarisha soko kweli au hatuna hata hilo soko? Kwa hiyo, nadhani tuwe makini tunataka kusema nini hasa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, hizi kwa uelewa wangu ni very serious institutions, kwa hiyo, yale majukumu tunayotarajia yafanywe na hizi taasisi kweli yawe specific na ule u-specific wake uende kwenye ku-address the needs kama alivyosema Mheshimiwa Waitara. Research ni lazima ziwe zinajibu yale masuala yaliyopo au zinatatua changamoto na matatizo yaliyopo. Sasa hizi documents je, zina-address hayo? Haya yaliyoorodheshwa humu kama majukumu ya taasisi hizi, hapo zitakapoanzishwa kama hizi sheria zitapita, je, kweli zitakuwa zinatupa majibu ya yale maswali ambayo sisi kwenye jamii hii yanatugusa kwa sasa hivi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye huu Muswada wa Uvuvi, nashukuru dada yangu Mheshimiwa Paresso aligusa hilo. Nilipoangalia kwenye headings kule kwenye ile Kiswahili version nikapata wasiwasi, nikasema huu sasa umekuwa mseto. Hili linaendana na suala ambalo nilishawahi kulisema hapa kwamba Watendaji wetu hawa wanakuwa overworked most of the time, ndiyo maana hata hizi documents ambazo nilidhani zingekuwa identical twins lakini zina tofauti ambazo sidhani kama they were intended kuwa na hizo tofauti, lakini inaweza ikawa ni kwa sababu hiyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwenye suala hili la Muswada wa Uvuvi nilikuwa na swali ambalo Mheshimiwa Waziri ningependa ajibu, anijulishe baadaye kwamba ni vigezo gani vilitumika, kwa mfano, kutaja hivi vituo vinne; kimojawapo kikiwa Dar es Salaam na vingine Mwanza, Kigoma na Kyela?
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikasema hivi Dar es Salaam kunawekwa Kituo cha Uvuvi, research kwa ajili ya bahari au kitu gani? Vipi mahali kama Mafia ambapo kuna lukuki ya matatizo yanayohusu uvuvi, hakuna hata ile thinking kwamba mahali kama pale panahitajika ule utafiti ukawa karibu zaidi kwa sababu kule kuna mahitaji mengi mahsusi. Kwa hiyo, naona kwamba kuhusu namna gani tunaamua, wapi kikae nini, pia ingekuwa ni suala ambalo tunalipa fikra zaidi ili mwisho wa yote tuwe na kitu ambacho kweli kinakidhi haja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, zinapotajwa sifa za Wakurugenzi hawa, pale inapokuwa sifa hii au hii, sasa kwa mfano kwenye suala la fisheries, mimi sio mzoefu sana, lakini napata tabu kuelewa kwamba mtaalam wa fisheries anaweza akawa sawa tu na yeyote ambaye amesomea viumbe vya majini. Sasa uvuvi na labda viboko na mamba vinaendana vipi? Sisi tunataka mtaalam ambaye amebobea kwenye uvuvi, masuala yanayohusu uvuvi, masoko na kila aina za uvuvi; lakini tunaambiwa hata yule aliyesomea viumbe vingine tu vya kwenye maji anaweza akasaidia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia hapo Mheshimiwa Waziri labda wakati anajumuisha angetupitisha akatueleza hasa ni nini ambacho kinatakiwa hapa? Ni kweli tunataka wataalam ambao ni very specific and specialized kwenye hizo areas ambapo hizi research institutes zitakuwa zinashughulika nazo, au tunataka tu mtu yeyote ambaye angalau ana ujuzi au uelewa wa masuala hayo? Hii nadhani sitarajii kupata suala lile la jumla kama ambalo tulitolewa kwenye ile Miswada iliyopita juzi pale kwamba yoyote tu, hata chemistry inaweza kuwa chemistry lakini na biology pia ikawa ni chemistry, kwa hiyo, nilikuwa nimeomba sana Mheshimiwa Waziri atupe hayo majibu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna makosa madogo madogo tu ya spelling, kuna mahali wataalam wanaitwa wataaluma au vitu kama hivyo…
MWENYEKITI: Ahsante.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) wa Mwaka 2016
MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti nakushukuru, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa uhai na uzima na kutuwezesha kuwa hapa mchana huu ili kujadili mambo kadhaa.
Mheshimiwa Mwenyekiti kama alivyosema Mzungumzaji wa Kambi ya Upinzani, kazi tulinayo mchana huu si ndogo na kwa kuwa mimi pia ni Mjumbe wa Kamati ya Katiba na sheria hata sisi kwenye Kamati tulijiona kwamba tuna kazi kubwa. Sheria ni nyingi, kwa hiyo ilituchukua muda na vikao kadhaa kuweza angalau kufikia pale tulipofikia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya marekebisho ambayo Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameyaleta kama alivyosema Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria yametoka kwenye mapendekezo ambayo Kamati tulikuwa tumeyafikia kwa sehemu kubwa sana na nyongeza ndogo tu ya kufanya katika maeneo mawili tofauti.
Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo moja ni lile linalohusu mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu na mengi katika ambayo yamesemwa ni namna ya kuwaweka waajiri mahali ambapo panawapa majukumu au panawaingiza katika makosa wakati wao mwanzoni hawakuwa sehemu ya mkataba huu. Kwa hiyo, maoni ya wengi ilikuwa ni kwamba waajiri waenziwe lakini pia…
MWENYEKITI: Waheshimiwa tunaomba utulivu kwenye Bunge.
MHE. RIZIKI S. MNGWALI: ...lakini pia wapewe masharti nafuu sana ili na wao waweze kushiriki vyema katika zoezi hili la kusaidia kukusanya mikopo na wasitishwe wala wakaona wanabebeshwa majukumu makubwa zaidi kuliko wale wenyewe ambao hawakuwa sehemu ya mkataba. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wale wanaopewa mikataba wanawadhamini wao, kwa hiyo, wadhamini wangekuwa wanabeba sehemu kubwa ya kuhakikisha kwamba mikopo hii inarejeshwa. Pia ni jambo ambalo linatakiwa lichukuliwe kwa tahadhari sana kwamba ikiwa tutawapa masharti magumu sana waajiri, basi tuwe na tahadhari kwani hii inaweza ikarejea kwa vijana wetu ikawa wanaonekana kama ni watu wasumbufu badala ya kuwasaidia pamoja na elimu zao ikawa tumewapa jukumu kubwa tena la kuwa wazururaji wa mitaani kwa kuwa waajiri wengi watakataa usumbufu na kwa hiyo watawaacha vijana wetu ambao ni wanufaika wa mikopo hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba sana haya tuyaangalie kwa umakini mkubwa yasije yakaturudia sisi ikawa ni hasara badala ya faida ambayo tunaitarajia. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, point nyingine ni kuongeza tu fikra katika suala la SUMATRA. Hili tulilijadili sana kwenye Kamati maeneo yale ya kutoza faini na Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria ameiweka hapa kwamba tahadhari kubwa ichukuliwe kwamba ile faini inalipwa vipi. Vile vile huyo anayetozwa faini, hilo neno kukubali kosa nalo pia linatakiwa liwekewe tahadhari kubwa kwa sababu na niliwahi kusema hapa kwamba, sentensi hiyo pia inatumiwa na Jeshi letu la Polisi wa Usalama barabarani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, dereva unapofanya kosa barabarani, unajaziwa fomu halafu unaambiwa usaini kwa sababu fomu yenyewe imeshajazwa kabla ya kuulizwa wewe mhusika na vile vile wanamlazimisha mhusika yule alipe fani pale pale kwa yule askari tofauti na ambavyo ile karatasi inaeleza kwamba faini ile inaweza ikalipwa ndani ya siku saba katika ofisi husika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hili kwa SUMATRA pia linahusika kwamba SUMATRA wasiwe wao wakusanya pesa barabarani tu na wala hii kumfanya mhusika wa kosa kulazimishwa kwa maana ya kujaziwa makosa kabla au kama ilivyowekwa kwenye hii Sheria kwamba wanamshawishi mtu eti kwa kumpunguzia adhabu alipe nusu ya faini ikiwa atakubali kulipa pale. Sidhani kama hii ni namna nzuri sana ya kuweka sheria ambazo tunatarajia zidumu na zilete ufanisi na zilete mtangamano katika makundi mbalimbali ya jamiii yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti nakushukuru.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali, 2017
MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Bismillah Rahman Rahim.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi. Pia namshukuru Mwenyezi Mungu Muumba Mbingu na Ardhi aliyetupa afya na uzima sisi zote tuliomo humu na nazidi kumwomba ajalie kikao hiki kifupi kitoke na maamuzi ya busara kwa ajili ya maslahi mapana na ya muda mrefu wa nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hili suala tunalojadili hapa ni muhimu kama ambavyo tumejadili mengine na sidhani kama nitakuwa na maneno tofauti sana ya kusema mbele yako, bali kurejea yale kwamba tumche Mwenyezi Mungu kwa namna ya kumcha na katika imani yangu tumefundishwa kukumbushana kwamba kukumbusha hakika kunawasaidia wenye kuamini na nawakumbusha Waheshimiwa wote mliomo humu kwamba tumwogope Mwenyezi Mungu, tutunze viapo vyetu na naamini ninyi ni waumini, kwa hiyo ukumbusho huu utawasaidia.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala hili, mimi ni mjumbe wa Kamati ya Katiba na Sheria, nilikuwa nashangaa hapa nikimwangalia prince wangu wa Madaba Mheshimiwa Mhagama, nikimwangalia na prince Mheshimiwa Rashid Shangazi wanashangilia nasema wamebadilika lini, nilikuwa najiuliza mwenyewe hapa, wamebadilika lini? Kwa sababu siku ambayo Waziri husika alikuja kwenye Kamati, hakuwa na hoja za msingi, kabisa. Mwisho tukamwambia kwa hali tuliyonayo sasa hivi kwa namna technology ipofikia hata tukikwambia utuletee report monthly, weekly, hutaweza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo hakuna sababu ya msingi hoja ya maana kwamba eti sasa mkileta ripoti baada ya miezi sita itakuwa ya maana zaidi kuliko ya miezi mitatu, si kweli. Naomba Mwenyezi Mungu nishuhudie nasema si kweli. Utaratibu tuliouweka mwanzo ndiyo unawezesha hiki ambacho kimesemwa hapa kwenye taarifa ya Kamati yangu kwamba marekebisho hayo yaongeze uwezo wa Bunge kugundua haraka.

Mheshimiwa Naibu Spika, utagunduaje haraka wakati muda wenyewe umeshauweka mrefu? Vipaumbele ambavyo havijatekelezwa matumizi yasiyo na tija, vyanzo vya mapato visivyofanya kazi vizuri. Umeshaondoa ule muda wawewe kukufanya ukagundua hilo haraka, ambao ni miezi mitatu unasema ukae mpaka miezi sita haraka iko wapi Waheshimiwa. Waheshimiwa haraka iko wapi unapotoka kufanya kazi miezi mitatu, useme tusubiri mpaka miezi sita.

Mheshimiwa Naibu Spika, hii si haki, narudia tena, si haki, Waheshimiwa tuiheshimu nchi hii, tuwaheshimu wananchi waliotuweka huku na tuweke maamuzi na tufanye kazi hii kwa ajili yao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa hii, hayo marekebisho hasa hayo yanayobadilishwa kwamba utoaji wa taarifa hizi kwa kweli si wa haki. Si wa haki hata kidogo na tusijidanganye hapa hicho ulichokisema Mheshimiwa Naibu Spika kwamba tuache vyama nje ni kweli tuache vyama nje, hapa tuwaangalie Watanzania, hapa tuangalie Serikali yetu, hapa tuangalie mamlaka yetu Bunge ni vipi tunaweza kutekeleza mamlaka hayo, vipi tunaweza kutekeleza majukumu hayo kwenye mazingira ambayo kweli yanawezesha hilo. Mimi wala sitajali hata nikiambiwa Bunge tutakutana mara moja kwa mwaka, lakini muhimu yale majukumu yetu ya Bunge tuyafanye. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, haiwezekani, tunaliua Taifa hili, tunajenga uzembe katika utendaji kazi wa Serikali kwamba mkae tu tusiwakague, mkae tu tusiwakague kwa miezi sita, maana yake ripoti itakuwa inatoka mara moja tu. Kwa sababu by the time mid year ya pili inakamilika mwaka mwingine umeshakamilika, whether uwe mwaka wa kifedha au mwaka wa kalenda, jamani tunakwenda wapi au tunaipeleka wapi nchi hii! (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakubaliana kabisa na yaliyoletwa na Kambi Rasmi ya Upinzani kwamba hii Serikali tubaki pale pale kwenye kuletewa taarifa kila baada ya miezi mitatu.

Mheshimiwa Naibu Spika, aliyekuwa Kiongozi wa Cuba aliwahi kusema wakati wa yale mapinduzi makubwa ya 1950s kwamba condemn me I don’t care history shall observe me. Semeni mtakayosema lakini ukweli utabaki kuwa ukweli. Tuiteni majina; tuiteni nyati, tumbili, kobe whatever the name you like to call us, lakini ukweli utabaki kuwa ukweli.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwanangu Kafulila aliitwa majina hapa wakati wa Escrow, Escrow iko wapi sasa hivi, ukweli utabaki kuwa ukweli kwa sababu ukweli ndiyo kauli ya Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu ni mwadilifu, kwa hiyo kauli hata siku moja haitokwenda vibaya.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli sina maneno hata kama muda bado upo lakini ni lile lile kwamba turudi pale pale tulipo tuletewe ripoti kila baada ya miezi mitatu, lakini muhimu zaidi tumwogope Mwenyezi Mungu na tutunze viapo vyetu hapa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru.
Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Maliasili wa Mwaka 2017.
MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi ya kuchangia mjadala huu unaoendelea.

Mheshimiwa Naibu Spika, toka taarifa ile ya Katibu wa Bunge kusema sasa wadau watoe maoni ilipotolewa nilikuwa nashangaa na naendelea kushangaa namna hili jambo zito sana lilivyoshughulikiwa. Mheshimiwa Profesa Kabudi kaka yangu anajua tulikuwa wote kwenye Tume ya Warioba namna gani Watanzania walisema kwa uchungu mkubwa kuhusu rasilimali hizi. Namna gani tulikwenda mpaka Buhemba tukaona mahandaki yale yaliyoachwa pale, watu wameachwa dhalili kuliko udhalili wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lilipotolewa lile tangazo nikasema Alhamisi tangazo, Jumamosi utampata vipi mtu wa Buhemba, utampata vipi mtu wa Mahenge, hawa ndio


walioko kule, waje watoe maoni yao? Nikasikia kauli tena kutoka mamlaka ileile kwamba niliowaalika mimi nimewapa barua na nakala za Miswada, kumbe kuna watu selected few ndiyo tuliowataka kwenye zoezi hili? Sidhani kama tunawatendea haki Watanzania, sidhani kama tunajitendea haki sisi wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuchanganyikiwa kote huku napata faraja kwenye maneno ya Mwenyezi Mungu, anasema hakika wale wanaoharibu wakiambiwa mnaharibu kwa kiburi wanasema sisi tunatengeneza. Tunaharibu. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Swadakta.

MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mnaharibu wenye mamlaka mnaharibu na tunawaambia mnaharibu. Fungeni macho kama yale aliyonifundisha mwalimu wangu Mrs. Seif, funga macho internalize.

My former boss Profesa Safari aliwahi kuandika makala anasema, ‘Liberating the Court Language’, kwamba ile Mahakama Kuu acheni kusema kiingereza semeni kiswahili kwa sababu ndiyo lugha ya Watanzania ili twende pamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, walikuja watu tukawaonyesha kwamba wao ni dhalili kwa kulalamikia lugha tu. Hili suala linawagusa wao, limeletwa katika lugha ambayo haieleweki kwao, lakini pia si lugha ya Taifa lao, wapeni haya masuala kwenye lugha yao, wa-internalize, waweze ku-participate fully. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sikutarajia katika maisha yangu kuona Mbunge anamdhalilisha mpiga kura. Wale wananchi waliokuja pale tukawadhalilisha ni wapiga kura, ni wananchi wa Tanzania. Tunashangaa vipi hizi taasisi nyingine kama polisi na kadhalika kutudhalilisha sisi? Sisi wenyewe tunadhalilisha Watanzania. Ni msiba mkubwa na imenisikitisha. (Makofi)


Mheshimiwa Naibu Spika, muda haupo wa kutosha kujadili suala hili muhimu. Nilitarajia tungepata uelewa wa pamoja kwanza kwamba what are the issues in debate kuhusu matatizo haya. Grievance za wananchi ni zipi hasa? Sisi wote tupate uelewa wa pamoja kisha tuambiwe hizi sheria zilizopo kwani simekosea nini na zina upungufu gani, tulete hayo mapendekezo mapya tuone yanaleta nini hasa ambayo ni so substantial ambayo kweli ita-take care of the limitation ambazo ziko sasa hivi lakini hatufanyi haya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, masuala madogo tu, tunaulizana je, hii sheria tunayoitengeneza ita-apply retrospectively? Hilo peke yake wengine wanasema ndiyo, wengine wanasema siyo uelewa wa hilo pia hatuna. Pia katika wataalam kuna waliotuambia kwamba mbona hii mikataba yenyewe ya sasa hivi inaruhusu reviews, why we didn’t do the reviews? Hilo pia hatuna uelewa, jamani tunafanya nini? Tunaleta ushabiki kwenye suala hili? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nawaambia hamjafika Buhemba mkawaona wananchi dhalili walioachiwa mashimo yale. Mwanangu Mheshimiwa Bashe aliwahi kusema hapa wameachiwa mashimo ambayo hayatojaa mpaka kwa miaka 200, nchi bado ipo? Jamani tuwe serious na masuala haya. Hayahitaji kupigana vijembe, hayahitaji kuonyeshana ushabiki na siku moja nilikuwa kusema hapa kwamba hayahitaji kujificha behind technicalities. Wenye mamlaka wanatuambia ndiyo Kikatiba, kitaratibu, kikanuni tunawakaribisha wadau lakini hatulazimiki kuwasikiliza wala hatulazimiki kufuata wanayosema. Come on are we serious, wasting time? Wabunge wanakaa hapa Jumamosi na Jumapili watu waje waseme eti lakini after all hatulazimiki kuwasikiliza au kufuata wanayosema, ya nini tunafanya hayo? Mimi sidhani kama kweli hiyo nia aliyonayo Mheshimiwa Rais ya kutuletea mabadiliko tumeitendea haki, hatukuitendea haki. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika waandishi waliowahi kuandika kuhusu vita vya Rwanda, alishangaa akauliza, how could all these people agree to kill but how all these people


accept to be killed? Watu walishawishiwa tu wakaambiwa kwamba ueni wakaua na maelfu tena malaki yanakaribia milioni na wao wakakubali wakauliwa. Kwa sababu anatoa scenario ambayo Mchungaji au Kiongozi mkubwa wa Kanisa anamwandikia meseji mtu mkubwa wa mamlaka anamwambia, we wish to inform you that tomorrow we will be killed. Yaani wamefungiwa Kanisani wanajua wanakuja kuuliwa kesho na anapeleka hiyo note.

Mimi nauliza hivyo hivyo, how could all of us accept to be fooled and how all of us accepted to be robbed?

Mheshimiwa Naibu Spika, sikuzungumzia suala la juzi na leo, nimezungumzia all that time kwamba wakati huo wote vipi sisi tulikubali kupumbazwa na mikataba tuliyoingia na tukakubali kuibiwa na mikataba tuliyoingia, sikuzungumzia hili la leo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba mnisamehe kwa hilo, kama mmenielewa vibaya sikuzungumzia hilo, nimezungumzia how…

KUHUSU UTARATIBU...

MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Naibu Spika, kila niliposema hilo la kiingereza lilifuatia la kiswahili pamoja na nilipotoa ufafanuzi kwamba namna gani tulikubali kupumbazwa na namna gani tulikubali kuibiwa kwa mikataba ambayo tuliingia sisi wenyewe tukiwa na wataalamu wetu na tukiwa na akili zetu timamu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ndio hicho nilichosema mwanzo, hili si suala la ushabiki wala si suala la kushindana kwa semantics, misamiati ambayo haitupi tija. Tunajadili suala hili naamini ndani ya moyo wangu kabisa kwamba huu mchakato ulihitaji muda wa kutosha tuwape nafasi walioguswa moja kwa moja na siyo mimi na ninyi tunaosikia kupitia kwa mtu mwingine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa msisitizo kabisa kwamba mchakato huu hatukuutendea haki na yanaonekana hapa. Katika kauli ambayo imenipa ukakasi zaidi ni ile ya kusema after all tunatengeneza si tutabadilisha tu. Hiyo peke yake ni false start yaani ni mwanzo mbaya sana huo kwamba mnatunga sheria kwa sababu kuna nafasi ya kurekebisha, hiyo siyo sababu ya kutunga sheria. Tunatunga sheria mioyo yetu ikiamini kabisa ni katika yale maamuzi ambayo Bunge hili kama yalivyo Mabunge mengine duniani yamepewa mamlaka kwa niaba ya wananchi kutengeneza vitu pamoja na sheria ambazo ni makini sana ama ikitokea kasoro ndiyo tunasema ni human error kwamba ni binadamu hatuko wakamilifu, lakini siyo kwa makusudi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimewahi kusema hapa tunafanya mambo ya kanyaga twende, hapana haifai, sisi
ni watu muhimu bana, hii taasisi ni muhimu sana. Tumetumwa hapa kwa kazi maalum na hilo la utungaji wa sheria ndiyo haswa kazi yenyewe. Kwa hiyo, tunapoitekeleza kazi hii ni lazima tuwe makini sana na zaidi jamani tunaswali hapa kila asubuhi, unless kama tunafanyia stihizai Mwenyezi Mungu. Kama kweli hii swala tunayoiomba hapa asubuhi kweli tunaitia ndani ya mioyo yetu naamini tutabadilika na tutafanya kazi zile ambazo tunatakiwa kufanya.
Muswada wa Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi wa Mwaka 2017.
MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi ya kuchangia mjadala huu unaoendelea.

Mheshimiwa Naibu Spika, toka taarifa ile ya Katibu wa Bunge kusema sasa wadau watoe maoni ilipotolewa nilikuwa nashangaa na naendelea kushangaa namna hili jambo zito sana lilivyoshughulikiwa. Mheshimiwa Profesa Kabudi kaka yangu anajua tulikuwa wote kwenye Tume ya Warioba namna gani Watanzania walisema kwa uchungu mkubwa kuhusu rasilimali hizi. Namna gani tulikwenda mpaka Buhemba tukaona mahandaki yale yaliyoachwa pale, watu wameachwa dhalili kuliko udhalili wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lilipotolewa lile tangazo nikasema Alhamisi tangazo, Jumamosi utampata vipi mtu wa Buhemba, utampata vipi mtu wa Mahenge, hawa ndio


walioko kule, waje watoe maoni yao? Nikasikia kauli tena kutoka mamlaka ileile kwamba niliowaalika mimi nimewapa barua na nakala za Miswada, kumbe kuna watu selected few ndiyo tuliowataka kwenye zoezi hili? Sidhani kama tunawatendea haki Watanzania, sidhani kama tunajitendea haki sisi wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuchanganyikiwa kote huku napata faraja kwenye maneno ya Mwenyezi Mungu, anasema hakika wale wanaoharibu wakiambiwa mnaharibu kwa kiburi wanasema sisi tunatengeneza. Tunaharibu. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Swadakta.

MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mnaharibu wenye mamlaka mnaharibu na tunawaambia mnaharibu. Fungeni macho kama yale aliyonifundisha mwalimu wangu Mrs. Seif, funga macho internalize.

My former boss Profesa Safari aliwahi kuandika makala anasema, ‘Liberating the Court Language’, kwamba ile Mahakama Kuu acheni kusema kiingereza semeni kiswahili kwa sababu ndiyo lugha ya Watanzania ili twende pamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, walikuja watu tukawaonyesha kwamba wao ni dhalili kwa kulalamikia lugha tu. Hili suala linawagusa wao, limeletwa katika lugha ambayo haieleweki kwao, lakini pia si lugha ya Taifa lao, wapeni haya masuala kwenye lugha yao, wa-internalize, waweze ku-participate fully. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sikutarajia katika maisha yangu kuona Mbunge anamdhalilisha mpiga kura. Wale wananchi waliokuja pale tukawadhalilisha ni wapiga kura, ni wananchi wa Tanzania. Tunashangaa vipi hizi taasisi nyingine kama polisi na kadhalika kutudhalilisha sisi? Sisi wenyewe tunadhalilisha Watanzania. Ni msiba mkubwa na imenisikitisha. (Makofi)


Mheshimiwa Naibu Spika, muda haupo wa kutosha kujadili suala hili muhimu. Nilitarajia tungepata uelewa wa pamoja kwanza kwamba what are the issues in debate kuhusu matatizo haya. Grievance za wananchi ni zipi hasa? Sisi wote tupate uelewa wa pamoja kisha tuambiwe hizi sheria zilizopo kwani simekosea nini na zina upungufu gani, tulete hayo mapendekezo mapya tuone yanaleta nini hasa ambayo ni so substantial ambayo kweli ita-take care of the limitation ambazo ziko sasa hivi lakini hatufanyi haya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, masuala madogo tu, tunaulizana je, hii sheria tunayoitengeneza ita-apply retrospectively? Hilo peke yake wengine wanasema ndiyo, wengine wanasema siyo uelewa wa hilo pia hatuna. Pia katika wataalam kuna waliotuambia kwamba mbona hii mikataba yenyewe ya sasa hivi inaruhusu reviews, why we didn’t do the reviews? Hilo pia hatuna uelewa, jamani tunafanya nini? Tunaleta ushabiki kwenye suala hili? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nawaambia hamjafika Buhemba mkawaona wananchi dhalili walioachiwa mashimo yale. Mwanangu Mheshimiwa Bashe aliwahi kusema hapa wameachiwa mashimo ambayo hayatojaa mpaka kwa miaka 200, nchi bado ipo? Jamani tuwe serious na masuala haya. Hayahitaji kupigana vijembe, hayahitaji kuonyeshana ushabiki na siku moja nilikuwa kusema hapa kwamba hayahitaji kujificha behind technicalities. Wenye mamlaka wanatuambia ndiyo Kikatiba, kitaratibu, kikanuni tunawakaribisha wadau lakini hatulazimiki kuwasikiliza wala hatulazimiki kufuata wanayosema. Come on are we serious, wasting time? Wabunge wanakaa hapa Jumamosi na Jumapili watu waje waseme eti lakini after all hatulazimiki kuwasikiliza au kufuata wanayosema, ya nini tunafanya hayo? Mimi sidhani kama kweli hiyo nia aliyonayo Mheshimiwa Rais ya kutuletea mabadiliko tumeitendea haki, hatukuitendea haki. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika waandishi waliowahi kuandika kuhusu vita vya Rwanda, alishangaa akauliza, how could all these people agree to kill but how all these people


accept to be killed? Watu walishawishiwa tu wakaambiwa kwamba ueni wakaua na maelfu tena malaki yanakaribia milioni na wao wakakubali wakauliwa. Kwa sababu anatoa scenario ambayo Mchungaji au Kiongozi mkubwa wa Kanisa anamwandikia meseji mtu mkubwa wa mamlaka anamwambia, we wish to inform you that tomorrow we will be killed. Yaani wamefungiwa Kanisani wanajua wanakuja kuuliwa kesho na anapeleka hiyo note.

Mimi nauliza hivyo hivyo, how could all of us accept to be fooled and how all of us accepted to be robbed?

Mheshimiwa Naibu Spika, sikuzungumzia suala la juzi na leo, nimezungumzia all that time kwamba wakati huo wote vipi sisi tulikubali kupumbazwa na mikataba tuliyoingia na tukakubali kuibiwa na mikataba tuliyoingia, sikuzungumzia hili la leo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba mnisamehe kwa hilo, kama mmenielewa vibaya sikuzungumzia hilo, nimezungumzia how…

KUHUSU UTARATIBU...

MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Naibu Spika, kila niliposema hilo la kiingereza lilifuatia la kiswahili pamoja na nilipotoa ufafanuzi kwamba namna gani tulikubali kupumbazwa na namna gani tulikubali kuibiwa kwa mikataba ambayo tuliingia sisi wenyewe tukiwa na wataalamu wetu na tukiwa na akili zetu timamu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ndio hicho nilichosema mwanzo, hili si suala la ushabiki wala si suala la kushindana kwa semantics, misamiati ambayo haitupi tija. Tunajadili suala hili naamini ndani ya moyo wangu kabisa kwamba huu mchakato ulihitaji muda wa kutosha tuwape nafasi walioguswa moja kwa moja na siyo mimi na ninyi tunaosikia kupitia kwa mtu mwingine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa msisitizo kabisa kwamba mchakato huu hatukuutendea haki na yanaonekana hapa. Katika kauli ambayo imenipa ukakasi zaidi ni ile ya kusema after all tunatengeneza si tutabadilisha tu. Hiyo peke yake ni false start yaani ni mwanzo mbaya sana huo kwamba mnatunga sheria kwa sababu kuna nafasi ya kurekebisha, hiyo siyo sababu ya kutunga sheria. Tunatunga sheria mioyo yetu ikiamini kabisa ni katika yale maamuzi ambayo Bunge hili kama yalivyo Mabunge mengine duniani yamepewa mamlaka kwa niaba ya wananchi kutengeneza vitu pamoja na sheria ambazo ni makini sana ama ikitokea kasoro ndiyo tunasema ni human error kwamba ni binadamu hatuko wakamilifu, lakini siyo kwa makusudi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimewahi kusema hapa tunafanya mambo ya kanyaga twende, hapana haifai, sisi
ni watu muhimu bana, hii taasisi ni muhimu sana. Tumetumwa hapa kwa kazi maalum na hilo la utungaji wa sheria ndiyo haswa kazi yenyewe. Kwa hiyo, tunapoitekeleza kazi hii ni lazima tuwe makini sana na zaidi jamani tunaswali hapa kila asubuhi, unless kama tunafanyia stihizai Mwenyezi Mungu. Kama kweli hii swala tunayoiomba hapa asubuhi kweli tunaitia ndani ya mioyo yetu naamini tutabadilika na tutafanya kazi zile ambazo tunatakiwa kufanya.