Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Saada Salum Mkuya (4 total)

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukua fursa hii kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri ambayo ameanza na anaendelea kuifanya. Vile vile pongezi kwa Waziri Mkuu na Mawaziri wake kwa kumsaidia Mheshimiwa Rais kutekeleza majukumu yake. Naomba kutoa mchango wangu kwenye hotuba hii kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Utalii; nimefurahishwa na kupata moyo kwa hatua ambazo Serikali itachukua kuimarisha utalli. Utalii ni sekta ambayo ina potential kubwa sana kwa uingizaji wa fedha za kigeni. Kwa upande wa Zanzibar, Sekta hii ni leading sector kwa mchango kwenye pato la Taifa. However, watalii wamekuwa wakilipia katika nchi zao na hivyo kukosesha pato kwa upande wa nchi. Uelewa mdogo wa changamoto hii kwa upande wa Kampuni za Kitalii kwa hapa nyumbani, umesababisha tabia hii kuendelea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mkakati ambao utaandaliwa uhakikishe kwa kiwango kikubwa unashirikisha Makampuni ya Kitalii ya hapa nyumbani kuzungumzia changamoto hii na utatuzi wake. Vile vile kwa kuwa Zanzibar inategemea sana utalii, mkakati ushirikishe wadau wa Zanzibar kwa kiwango kikubwa cha majadiliano.
Mheshimiwa Mwenyekiti, UKIMWI; wakati tukiwa kwenye Kamati, imeonekana bajeti nyingi zimeweka eneo la mkakati wa kudhibiti UKIMWI, kama ni eneo ambalo linasubiri fedha kutoka kwa wafadhili. Hii ni hatari, afya za wananchi na matibabu yake, hayawezi kuwekwa katika mikono ya wafadhili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu ni kwamba, kwenye activities zetu ambazo tunazifadhili kwa fedha yetu ya ndani, issues za HIV/AIDS, Women, Climate change and environment, ziwe mainstreamed humo. Tusisubiri hadi fedha za wafadhili zifike.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Ukusanyaji wa Mapato; eneo hili ni gumu na lina changamoto nyingi, hata hivyo pongezi kwa Serikali kwa kulipa mtazamo maalum suala la ukusanyaji wa mapato. Matumizi ya mashine ya electronics (EFDs) ziambatane na mafunzo ya watu wetu katika matumizi hayo, hususan kwenye Halmashauri zetu. Eneo hili la ukusanyaji wa mapato ni eneo gumu sana, lakini ni muhimu kuliko yote. Maendeleo yetu bila ya mapato yatokanayo na vyanzo vyetu vya ndani yatakuwa ni magumu mno.
Mheshimiwa Mwenyekiti, approach ya utoaji wa elimu ibadilike now, ijielekeze sana kwa wananchi ili waelewe umuhimu wa ulipaji kodi kwa Serikali kwa kudai risiti wanaponunua bidhaa mbalimbali. Changamoto hii ikitatuliwa tunaweza kufika mbali zaidi. Vyombo vya habari vya Serikali na binafsi vione umuhimu wa jambo hili. Aidha, katika bidhaa za mafuta tuangalie jinsi gani tunaweza kupata fedha kwa kuongeza angalau shilingi mia ili tupate fedha ziingie katika Mifuko ya Maji na REA kama ilivyopangwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti,Viwanda; dhamira hii ni nzuri katika ujenzi wa Taifa na kiuchumi. Hata hivyo, viwanda vitakavyojengwa vitumie rasilimali zinazopatikana kwa wingi nchini ikiwemo rasilimali watu.
Mheshimiwa Mwenyekiti,karafuu ya Zanzibar ingepata viwanda vinavyohitaji, tuna hakika Zanzibar ingepata tija kubwa kuliko inavyopata hivi sasa. Liangaliwe hili kwa mapana yake.
Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 20 16/2017 - Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora
MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kupata nafasi hii ya kuchangia hoja ambazo ziko mbele yetu. Awali ya yote, nachukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu Subhana Wataala na kumtakia Rehema Mtume Muhammad (S.A.W).
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya hapo sasa najikita katika hoja ambazo ziko mbele yetu. Kwanza tunaanza na suala la ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri. Tunaipongeza sana Serikali kwa kuwa ni jambo ambalo wamelitilia mkazo mara hii na tunaamini kwamba mifumo ya electronic ambayo imefungwa katika Halmashauri nyingi zaidi ya asilimia 70 kama ilivyoelezwa itakuwa inakwenda kufanya kazi ile ambayo tumeitarajia.
Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hilo, Mheshimiwa Waziri tunaomba Public Financial Management Reform Programme iende ikajenge uwezo wa watu wetu kuweza kukusanya mapato kwa njia ya kielektroniki. Njia za elektroniki siyo kwa kutumia tu M-PESA na Tigo Pesa lakini ni uwezo wa watu wetu kuweza ku-intergrate hizi systems katika systems zetu za kufanyia kazi. Maana yake ni kwamba tunataka hata watu ambao wanakwenda kulipa kodi walipe kwa urahisi zaidi.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi tunatumia benki kwenda kulipa kwa mfano kodi ya ardhi lakini ukishapewa risiti ya benki inabidi mtu aende tena ofisini kupata risiti nyingine, kidogo utaratibu huu unaweza kuleta usumbufu. Kwa hivyo, ni lazima tuone ni jinsi gani tunaweza tukarahishisha mifumo hii ya kielektroniki kuweza vilevile kuwafanya watu waweze kulipa kodi hizi kwa hiari kwa kuhakikisha kwamba hawapati tabu wala vikwazo vyovyote vile wakienda kulipa kodi hizi.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini jambo lingine ni kuhusiana na masuala ya HIV/AIDS, tumeona katika Halmashauri nyingi zimeweka hizi component za ku-address hizi issue za HIV/AIDS, problem iliyokuwepo ni kwamba wengi wanategemea donors yaani miradi mingi ya ku-address issue hizi za UKIMWI zinategemea sana fedha za donors, nadhani huu utaratibu unaweza ukatu-cost baadaye. Sasa hivi kuna indication kwamba maambukizi ya UKIMWI yanaweza yakawa yamepungua katika maeneo fulani lakini inaweza ikatuathiri baadaye kwa sababu financing ya ugonjwa huu tunawaachia donors.
Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri katika kila component yetu ya maendeleo ni lazima issue hizi za HIV/AIDS ziwe addressed mle kwa kutumia fedha zetu za ndani. Kama jitihada hiyo hatutaifanya kwa kutegemea development partners waje watusaidie kwenye masuala haya ya UKIMWI hapo baadaye inaweza ikatuathiri.
Mheshimiwa Naibu Spika, niende katika suala la Tume ya Maadili, tuna-note kazi nzuri sana inayofanywa na Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma. Jambo langu katika Tume hii, isiishie tu kwenye masuala ya mali, madeni lakini vilevile iende ikaangalie behaviors za wafanyakazi. Jambo la msingi ambalo nataka kuli-note hapa hususani kwa watendaji wetu wa afya, sasa hivi tunatumia mitandao lakini utaona kwa mfano inawezekana mwanamke ameathiriwa labda na mumewe au amepata jambo ambalo si zuri anapigwa picha na tunajua kwamba hii picha imepigwa hospitali na imepigwa na mtaalam, anapigwa picha mwanamke yuko utupu kabisa, tunaambiwa huyu mwanamke mume wake amempiga kipigo wakati ni mjamzito yaani maelezo kama hayo, hili jambo siyo zuri.
Mheshimiwa Naibu Spika, tungependa tusikie issues kama hizo kwa ajili ya kuchukua hatua lakini vitu kama hivyo visichukuliwe kama ni starehe ama visichukuliwe kwamba watu ndiyo wanapashana habari. Jambo hili linakwaza hususan sisi wanawake kwa sababu vitu vingi ambavyo vinatumwa katika mitandao ya kijamii ni vile ambavyo vimemkuta mwanamke na vina udhalilishaji wa hali ya juu. Mitandao mingi utaona picha zingine mtoto amezaliwa labda moyo wake uko nje inatumwa kwenye WhatsApp, ni vitu vya hatari.
Mheshimiwa Naibu Spika, nadhani Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma iende mpaka ikaangalie behaviors za wafanyakazi wetu wanafanya nini hasa. Tunataka watu wahudumiwe na siyo kutumia zile athari ambazo wamezipata kupashana habari ulimwenguni, kuona kwamba hili ni jambo ambalo labda tunaweza tukaliona hivi hivi, iende katika hatua hiyo pia.
Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ni kuhusiana na Tume ya Ajira. Kwenye Kamati tulikwenda na tukaongea na Tume ya Ajira, wanafanya kazi nzuri sana. System zao ziko vizuri sana na ni system ambazo zimetengenezwa na Watanzania, tunawapongeza sana kwa kazi hiyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini changamoto iliyopo hapa Wazanzibari kwenye Tume ya Ajira wanapata tabu sana kufuatilia ajira ambazo wame-apply hususan katika Taasisi za Muungano. Siku za kufanya interview utawaona Wazanzibari wengi katika vyombo vya usafiri wanakuja Dar es Salaam. Jambo hili tumekuwa tukilisisitiza kuhusiana na facilitation ya Tume hii kule Zanzibar. Lazima kule Zanzibar kuwe na Ofisi za Tume ya Ajira ili iweze kuwafikia Wazanzibari bila kikwazo chochote.
Mheshimiwa Naibu Spika, hili jambo linasemwa mwaka hadi mwaka kwamba tutafungua Ofisi lakini hazijafunguliwa, kwa kweli vijana wetu wanapata tabu na wanahangaika sana. Kule kuna vijana wazuri tu, wasomi, wamemaliza degrees, they are very good lakini kwa kufuatilia hizi inawakwaza sana kwa sababu ni gharama. Vijana hawa hawajaajiriwa lakini inabidi watafute fedha za kwenda Dar es Salaam kufuatilia maombi ya ajira zao.
Mheshimiwa Naibu Spika, nakusudia kabisa kushika mshahara wa Mheshimiwa Waziri kama hatanipa commitment ambayo itatekelezeka kuona kwamba Tume ya Ajira aidha inafunguliwa Zanzibar au kunakuwa na Ofisi kwa ajili ya watu wa Zanzibar kufuatilia masuala ya kazi katika hizi Taasisi za Muungano.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni kuhusu hii asilimia 10 ya wanawake na vijana. Katika Halmashauri nyingi wanaona kwamba hili jambo ni hisani, hili jambo linaweza likafanyika katika leisure time, hii siyo sawa na hatutarajii iwe hivyo. Tunamwomba Mheshimiwa Waziri achukue hatua kwa wale Wakurugenzi wa Halmashauri ambao hawajatenga hii asilimia 10 na hawana maelezo yoyote. Maana wakati mwingine unaweza ukakuta tuna-review bajeti mtu hajatenga hii asilima 10 na hakuna maelezo ambayo tunaweza tukaridhika nayo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu hili siyo jambo la kufanywa kwa wakati wanaoutaka wao au kwa mapendekezo yao ndio waweze kutenga, wengine watatenga asilimia tano wengine asilimia mbili, hapana ni asilimia 10 kwa ajili ya kwenda kuwasaidia akinamama na vijana kujiinua kiuchumi. Wengi wanaona kwamba sehemu pekee ya kupata ajira ni Serikalini, Serikalini hakuna ajira, lakini tukiweza kuwapa mtaji pamoja na mafunzo ya ujasiriamali vijana wengi wanaweza wakatoka katika dimbwi la umaskini. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ni madeni. Kweli hili jambo ni kubwa kidogo, ukiangalia suppliers wengi hususan wale locals wamekuwa hawapati malipo yao kwa muda muafaka. Hii inaweza ikasababisha waka-perish katika mzunguko huu wa kiuchumi kwa sababu capital yao imeliwa. Hata hivyo, naipongeza sana Serikali imeona umuhimu wa kulipa madeni hususan ya wazabuni pamoja na watumishi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hili suala la wazabuni naomba priority kubwa wapewe kwanza wazabuni wale wadogo wadogo ambao wametoa huduma kwa Serikali lakini zoezi hili liende sambamba na uhakiki wa madeni hayo. Si kila mtu anayeidai Serikali anaidai kiukweli au si kila mtu pesa anayoidai Serikali imepitia katika mifumo sahihi ya manunuzi. Naomba utaratibu uwekwe ili wale watakaolipwa walipwe kwa viwango sahihi na lazima wawe na documentation zote ambazo zinawafanya walipwe.
Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ni hili ambalo tumekuwa tukilizungumza la viwanda. Tunaipongeza sana Serikali chini ya Rais, Dkt. John Magufuli kwa kuona kwamba sasa ni muhimu Tanzania iende katika uchumi wa viwanda. Viwanda vingi viko katika maeneo yetu…
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa umemaliza muda wako.
MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.
Mkataba wa Ubia wa Uchumi baina ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya.
MHE. SAADA MKUYA SALIM: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kupata fursa hii na mimi nichangie katika mjadala uliopo mbele yetu. Na mimi naunga mkono hoja hii ya Serikali kwamba tusisaini mkataba huu kama ulivyo.
Mheshimiwa Spika, kabla ya kuendelea mbele naomba ku-quote maneno ya Rais Mstaafu ambayo yalikuwa posted kwenye gazeti la East African, Mheshimiwa Mkapa alisema kwamba EPA is bad news for entire region. It is just bad news for entire region wala siyo for Tanzania, but for entire region.
Mheshimiwa Spika, mkataba kama huu kama ungekuwa una terms nzuri, basi nadhani ingekuwa faida kwa region, lakini faida vilevile kwa Tanzania. Terms zake hazifanani na haziendani. Mheshimiwa Rais Mkapa alisema vilevile kwamba the EPA for Tanzania and the EAC never made sense, the maths just never added up yaani zile hesabu zake haziendi kutokana na hali yetu ya kiuchumi.
Mheshimiwa Spika, pengine ingekuwa sisi kama East Africa tunahitaji zaidi EU wana soko la watu karibu milioni 700, East Africa tuna watu karibu milioni 300 plus, tungekuwa tunawahitaji zaidi kama angalau kungekuwa kuna ule uchumi unaoendana, lakini hatufanani. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, isipokuwa tumeuleta huu mkataba hapa na tutaukataa kabisa, lakini tuchukue hii kama ni nafasi ya Tanzania kuweza kujijenga zaidi.
Kwanza, kwenye viwanda, lakini pili pengine Mheshimiwa Waziri ulichukue hili iwe ni changamoto, ingekuwa vyema kwamba huu mkataba tunaukataa, lakini wataalam wetu watuletee alternative, yaani zile terms zinakuja, hizi haziwezekani, what do we want? Tunakoelekea regional integration ndiyo itakuwa inapata nafasi zaidi kuliko bilateral cooperation.
Mheshimiwa Spika, leo hatuuhitaji mkataba kama huu lakini ninaamini sera yetu ya kujenga viwanda itakapokuwa imefanikiwa, tutakuwa tunahitaji mikataba ya aina hii. Kwa maana hiyo, tutakapokuwa tunakwenda, tuone ni jinsi gani tunaweza kujenga uwezo wa watu wetu, kwanza, kuangalia critically mikataba ya aina hii, lakini secondly iendane na policy zetu ambazo pengine tungeweza ku-compete zaidi na mikataba mingine au na masoko ambayo yanaambatana na mikataba kama hii.
Mheshimiwa Spika, mkataba kama EPA unamaanisha nini? Tunakokwenda development cooperation inapungua na badala yake inakuja trade cooperation. Kwa maana hiyo, kama leo tutakuwa tunategemea zaidi development cooperation, kwa maana ya nchi matajiri kusaidia masikini, lakini kesho na nchi matajiri na wao zitataka ku-benefit kutoka kwa nchi masikini kama ilivyo sasa hivi.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, hii ni changamoto kwetu sisi. Tutakuwa tumeshinda leo, lakini ninaamini kwamba ni nafasi nzuri ya kujiweka vizuri zaidi kuona kwamba tutakapokuwa tunakwenda mbele, watakuja wengine na mikataba kama hii, tutaweza ku-face vipi? Hatuwezi kukataa kila siku, lakini ninaamini kwamba tunaweza kuchukua fursa hii kama changamoto na tukajiweka vizuri zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kupitia kwako namuomba Mheshimiwa Waziri, ninaamini kwamba mkataba huu utakwenda kuathiri development cooperation na EU. Nadhani tumekuja mwaka 2013, Mheshimiwa Waziri wa Fedha by then, tulikuja tukataka ridhaa ya Bunge kwa ajili ya kuridhiria Cotonou Agreement ambapo ndani yake tunapata misaada mbalimbali. Sasa kama sasa hivi tunakataa huu mkataba ambao ni trade related, sina uhakika wala hatuombi, lakini inawezekana tukaathiri aid cooperation na EU, wanatusaidia!
Mheshimiwa Spika, sasa namuomba Mheshimiwa Waziri, mkataba huu ambao tutaukataa hapa Bungeni leo, ninaamini afanye namna atakavyofanya aende akawaelimishe wananchi wa Zanzibar kupitia Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi. Kwa sababu ninaamini nao watafurahia jambo hili ambalo limekuwa decided na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Zanzibar kama sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wanapaswa kufahamu jambo ambalo linaendelea ambalo lina maslahi ya Kitaifa.
Mheshimiwa Spika, namuomba Mheshimiwa Waziri, Baraza la Wawakilishi linaketi mwisho wa mwezi huu, aende akawape semina Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ili na wananchi wa Zanzibar na wao waweze kuona kabisa kwamba Serikali pamoja na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limefanya jambo la maana kabisa kutoku-rectify mkataba kama huu.
Mheshimiwa Spika, la pili, hii inakwenda zaidi kwenye regional integration. Na sisi tunahitaji zaidi tu haya mahusiano. Sasa kwenye hili, pamoja na mambo mengine kama nchi tufanye jitihada zetu kuweza sana kuhimiza South South Cooperation, yale mahusiano yetu na nchi ambazo tunafanana nazo kiuchumi, kimazingira na kiitikadi ili tuone kwamba hatuendi tu mbele tukawa tuna mahusiano na European Union watu ambao tupo tofauti kiuchumi hata kiitikadi, lakini vilevile tuwe tuna sera madhubuti ya kuweza kuimarisha uhusiano wetu na nchi ambazo Kusini Kusini, yaani tunaita South South Cooperation. Mheshimiwa Waziri hilo nakuomba sana ulichukue.
Mheshimiwa Spika, vilevile Mheshimiwa Waziri la tatu; kwa vile tunategemea athari kubwa itatokana na kutoku-rectify hapa, bajeti yetu itakayokuja tuhakikishe kwamba ile miradi ambayo ilikuwa inafadhiliwa na EU, tuiwekee mikakati ili Serikali yetu iweze kuibeba iende ikafadhiliwe na Serikali yenyewe, ama angalau tutafute alternative. Zanzibar tumefaidika sana na Cotonou Agreement; tumejengewa bandari, vilevile kuna miradi mingi ya maji ambayo EU imesaidia, lakini vilevile kuna miradi mingi ya utawala bora kupitia NGOs imesaidiwa. Tunaomba sana Serikali ijipange ili tuweze kutafuta mbadala wa nani na vipi itasaidia kuweza kuendeleza miradi kama hii.
Mheshimiwa Spika, kwa maana hiyo, naunga mkono hoja. Yangu yalikuwa machache sana, kwamba Serikali isisaini, lakini tuchukue hii kama changamoto kuweza kusimama zaidi, kujiimarisha zaidi na watu wetu.
Mheshimiwa Spika, ningependa zaidi kwamba kama unakuja mkataba huu tunaukataa, lakini angalau kungekuwa na mapendekezo mbadala, yaani tuseme kifungu hiki hatukiwezi, hatukitaki, basi tuwe na kifungu kama hiki ili tuendane nacho. Kwa maana na sisi kama block tunawahitaji wenzetu. Leo huu ni mkataba, siyo mzuri, lakini ninaamini wakati ambapo sera zetu zitakaposimama sawasawa na kufanikiwa, tutawahitaji wao na wengine.
Kwa hiyo, naomba zaidi tuwe tunafanya kazi ya ziada. Technical Committees zinapokaa ziwe zinafanya kazi ya ziada na siyo kukataa, lakini vilevile walete mapendekezo kwamba ingekuwa bora jambo kama hili lingekuwa limekaa namna kama hii. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Namwomba Mheshimiwa Waziri, tunasubiri semina kule Zanzibar ili hili liweze kujadiliwa, lifahamike na wananchi nao wapate kufaidika kutokana na maelezo haya. Nashukuru.
Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari za Mwaka 2016
MHE. SAADA S. MKUYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Sina budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kutuwezesha leo kuwepo hapa asubuhi, kwa ajili ya kukamilisha majadiliano yetu. Nachukua fursa hii vilevile kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri pamoja na watendaji wote wa Wizara hii kwa kukamilisha mchakato huu na kuleta Muswada huu hapa Bungeni. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kalamu ni kitu ambacho muhimu sana. kama tutakitumia vizuri, tunaweza tukajenga nchi yetu na watu wake vizuri. Mwenyezi Mungu katika Sura ya 96, katika Quran kwenye aya ya nne anazungumza kwamba amemfundisha mwanadamu kuandika kwa kalamu, kwa kuonesha umuhimu na hii ni sura ya kwanza wakati inateremshwa Quran. Kwa hivyo kalamu ni jambo muhimu sana katika maisha ya mwanadamu ya kila siku. Kwa maana hiyo, katika content hiyo, nampongeza sana Mheshimiwa Waziri kwa kuwa na gut ya kusogeza Muswada huu hapa ambapo tunaujadili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kuongelea sana suala zima la uanzishwaji wa Mfuko wa Mafunzo wa Waandishi. Tumezoea sana zikija sheria hapa, pamoja na mambo mengine, kwamba zinakuja na uanzishwaji wa Mfuko. Lakini sheria zinatekelezwa au zimeendelea kutekelezwa isipokuwa utekelezaji wa Mfuko unachelewa sana sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nawaomba Wabunge wenzangu despite ya kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri, tunamwomba Mheshimiwa Waziri atakapokuja mwakani na bajeti Mungu akituweka hai na uzima, tuungane sote kwa pamoja tuhakikishe kwamba Mheshimiwa Waziri ametuambia source of fund ya Mfuko huu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu tukiwa tunazungumza tu kwamba, fedha zinazotokana na Mfuko huu ni fedha ambazo zitakazokuwa appropriate hapa na Bunge hii, nadhani haitakuwa sahihi. Maana yake, tunajua fedha ina mambo mengi na kama Mfuko haujawekewa source of fund specific kwa ajili ya implementation ya Mfuko huo, hatuendi mahali popote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri mbali ya mambo mengine tunampongeza, lakini Wabunge wenzangu tuhakikishe kwamba yale maslahi ambayo tunataka waandishi wa habari wayapate, mambo mazuri ambayo tumekuja nayo pamoja na sheria hii ili yatekelezeke, tumwambie lazima tumsimamie Waziri tuone kwamba, ametuletea source maalum ya fund kwa ajili ya utekelezaji wa Mfuko huu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri hizi sifa zote zinaweza zikapotea kama hili jambo litakuwa halijatekelezwa. Tunakuomba sana, najua utafanya hivyo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili vilevile naunga mkono hoja hii ya kuweko accreditation bodi. Mwandishi wa habari amechukuliwa kama kibarua tu wa kawaida every now and then, sote tumeshuhudia maskini waandishi wa habari ukitoka nje ukiandikwa usitoe pesa uwagawie, yaani wewe mwenyewe unawaonea huruma kutokana na hali ilivyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza hii accreditation bodi itampandisha value hata yeye mwenyewe yule mwandishi. Itampandisha value kwamba yeye ni mwandishi ambaye tayari amekuwa accredited yaani ni mwandishi ambaye amepata ithibati. Kwa maana hiyo, mategemeo yetu, maslahi yake kwanza yatakuwa mazuri. Vilevile hata taarifa na habari ambazo ataziandika zitakuwa ni habari ambazo zimetokana na mwandishi ambaye amekuwa accredited. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba sana hili ni jambo la msingi tukiachia tofauti zetu za kisiasa, lakini hili ni jambo la msingi sana. Kwanza kabla ya yote tunataka Mheshimiwa Waziri, mara tu Rais akishasaini hii, kanuni zisije zikachelewa. Tunaomba tupate na kanuni kwa haraka sana ili tuweze kutekeleza sheria hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo linatia mashaka kidogo Mheshimiwa Waziri na naomba sana tupate advice yako, ni kuhusiana na kazi ambazo zitakuwa zinatekelezwa na bodi. Hususan zile ambazo bodi itakuwa ina-advice the Government on training ya media, kuna media ama kuna journalist ambao watakuwa katika public sector, lakini wengine watakuweko private. Huu Mfuko ama hii bodi itaweza ku-advice vipi waandishi wa habari ambao watakuwa private na wao wakawa facilitated kwenye training ile. Sina uhakika hii itakuwa covered vipi kwa sababu the way it has been written in the Bill ni kwamba ime-accommodate.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajua Serikali ama Mfuko utakaoanzishwa sina uhakika how far utakwenda katika kuwasaidia waandishi wa habari, aidha, ambao ni freelancer au ambao wanaandikia vyombo binafsi. Kwa hivyo, hilo tunaliomba pia lifanikiwe. Naamini sana, kwa Muswada huu wa sheria tunaweza tukatengeneza Salim Kikeke wengi kutoka Tanzania kuliko ambaye yuko BBC. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile Muswada huu tukiutekeleza vizuri, Mheshimiwa Waziri tutatengeneza akina Christiane Amanpour ambao ni waandishi wa habari weledi tu katika dunia na ambao tunawaamini. Kwa hiyo, tunataka huo utekelezaji uanze mara moja, lakini with specifically kwenye fund kwamba ianze kutekelezwa na Mheshimiwa Waziri atuambie hasa source of fund hii inatokea wapi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Naibu Waziri ni mwanamke, hujatuambia kwenye sheria wala mimi napata ukakasi sana kama hii itakwenda kwenye regulation hajatuambia kwenye sheria hii bodi content ya wanawake iko wapi? Eeh! hajatuambia tunaweza kusema at least two lakini hata wanaweza wakawa watatu mpaka wanne, hii haijasema katika sheria na sijaona kwenye marekebisho yake, kama hili amelirekebisha (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba sana, waandishi wa habari hususan wanawake, kwanza ni watu ambao wanafanya kazi vizuri sana, vilevile mazingira tu yale yenyewe ya kufanyia kazi, ina-pro mwanaume kuliko mwanamke. Kwa hivyo, tunaona kwamba kuna umuhimu hasa katika bodi hii vilevile wawepo wanawake ambao wataweza kusimamia maslahi ya waandishi wa habari wanawake katika sheria hii. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine na la mwisho, kalamu hii, nimesema mwanzo, kalamu ni jambo ambalo lina-shape Tanzania yetu. Unaweza ukaandikwa vizuri kwenye gazeti na siku hiyo chart yako ikapanda. Lakini tumeona of recent Mwenyekiti wa Kamati hii alivyopata kiki sana maana yake kila kwenye gazeti anachambuliwa yeye, kutokana tu na Muswada huu.
Naamini kwa sababu na aidha wahariri au waandishi wenyewe hawakusoma na wakaona hasa kitu kilichopo na ndiyo maana kilikuwa kinaandikwa shell will.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa basi kwa maana hiyo, uandishi ni jambo ambalo litasimamia sana mwelekeo wa nchi yetu. Tumeona mwenzangu hapa Mheshimiwa Amina alitaja kilichotokea baada ya gazeti lile la…
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana naunga mkono hoja na natumaini Mheshimiwa Waziri atayatekeleza.