Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Peter Joseph Serukamba (43 total)

Hotuba ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Kufungua Bunge la Kumi na Moja
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa, nafasi na mimi niweze kuchangia Hotuba hii ya Mheshimiwa Rais. Kwanza naomba niwashukuru kwa dhati kabisa, wananchi wa Kigoma Kaskazini, kwa heshima kubwa waliyonipa, naweza kusema namuomba Mungu nisiweze kuwaangusha hata kidogo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, hotuba ya Rais ni nzuri sana. Hakika hotuba ile ilikuwa inaonesha dira ya miaka mitano. Lakini pia baada ya hotuba ile Rais ameanza kutekeleza, wazungu wanasema, he is walking the talk, ameanza kutekeleza aliyoyasema tarehe 20 Novemba hapa Bungeni. Sasa unaanza kuona nchi ambayo inachukia rushwa kwa vitendo. Tunaanza kuona ahadi zetu zikitekelezwa, tunaanza kuona tukielekea kwenye nchi ile ya ahadi tuliyoitarajia. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Rais anavyofanya kazi unaona Taifa letu likienda sasa kuanza kufanya kazi. Lakini wako wanazuoni wanasema, pamoja na yote, no gain without pain and this is leadership. Kwa hiyo, unaweza ukaona mambo yanavyokwenda, pain itakuwepo, lakini hatuwezi kufanikiwa bila kuwa na pain.
Mheshimiwa Rais ameongea mengi, mimi nitachangia machache la kwanza, maji. Mimi ninaamini kama kuna vita ya tatu ya dunia itatokea itasababishwa na maji. Tatizo la maji nchini ni kubwa sana, hasa katika Jimbo langu la Kigoma Kaskazini, Kata ya Kalinzi hatuna maji, Kata ya Mkigo hakuna maji, Kata ya Kagongo hakuna maji, Kata ya Ziwani hakuna maji, Kidahwe hakuna maji na Mayange hakuna maji. Lakini naomba nitumie nafasi hii kuishauri Serikali. Ukiangalia matatizo tunayokumbana nayo ya mazingira duniani, tunakoelekea mito mingi itaanza kukauka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ningeomba, niiombe Serikali ilifanya uamuzi mkubwa kutumia maji ya Lake victoria, lakini sisi tumebarikiwa tuna Lake Victoria, tuna Lake Tanganyika na tuna Lake Nyasa. Mimi ningeshauri Serikali, umefika wakati, waone umuhimu wa kutumia maziwa haya ili kuweza kupeleka maji katika maeneo mengi ya nchi yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni Sheria ya Ununuzi, Mheshimiwa Rais alisema, kama kuna sheria mbaya ni Sheria ya Ununuzi, na mimi nasema sheria ile ni mbaya sana, inatumia pesa nyingi sana kama walivyosema watu wengine. Tukipitisha Bajeti mwezi wa saba, inaanza kutumika Bajeti ya Serikali, Wizara zote zikianza kufanya manunuzi, mpaka mkandarasi anaingia kazini, siku anaanza kutangaza na hapo wameenda wamefata sheria ni miezi sita, haiwezekani! Kwa hiyo, ina maana tunatumia miezi sita yote tunafanya kazi za procurement. Halafu wakati wanataka kuanza kutekeleza mvua ni nyingi kubwa sana nchini, kwa watu wa barabara wanajua matokeo yake pale wanasimama, kwa hiyo tunamaliza mwaka, kwa kweli kazi nyingi hazijafanyika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, UN System wana kitu kinaitwa Universal Procurement List. Ningeomba nishauri Serikali umefika wakati na sisi tuandae Tanzania Procurement List. Maana yake nini, maana yake ni kwamba tunaenda kununua vitu vyote kwa supplier mwenyewe kwa manufacturer mwenyewe, tuta-serve pesa nyingi, tutapata vitu kwa bei ambayo ni ya chini, lakini na quality itakuwa ni kubwa. (Makofi)
Leo hii, hii habari ya list evaluated bidder, inafanya bei iwe kubwa, kalamu ya shilingi 1000 tunainunua kwa shilingi 5000, mtu amefuata sheria na tumeibiwa tunaangalia iko within the law, ningeiomba Serikali wailete sheria hii haraka sana.
Mheshimwa Mwenyekiti, lingine ni suala la PPP. Toka nimeingia Bungeni huu ni mwaka wa kumi naenda mwaka wa 15, tunaimba PPP, mpaka leo haijatekelezwa. Ningeomba niishauri Serikali, haiwezekani tukafanya maendeleo makubwa ya haraka kwa kutumia pesa za Serikali. Kama kuna mtu anadhani Serikali hii tunaweza tukafanya kwa pesa zetu wenyewe, ni tatizo kubwa. Na wenzetu we are not inviting the will, wenzetu wameanza.
Mheshimimiwa Mwenyekiti, ningeomba sana kwa mfano, reli, bandari, umeme, barabara, hasa barabara kubwa ya Dar es Salaam kwenda Arusha, Dar es Salaam kwenda Mwanza, Dar es Salaam kwenda Mbeya, kwa kweli kujenga barabara hizi kwa fedha zetu wenyewe hapana. Tuwape watu wajenge, waweke road toll, tutalipia, lakini tutapata barabara nzuri, na tutapunguza ajali. Wenzetu Malaysia wanafanya, South Africa wanafanya, sisi tatizo ni nini? Ningeomba Serikali walitatue tatizo hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hili Tanzania tumebarikiwa sana. Tuna uchumi wa kijiografia, naombeni Serikali tumesema inatosha, tutumieni nafasi yetu ya kijiografia, Tanzania tuko well located kijiographia, Tanzania Mungu ametujalia kwa sababu ya Chama chetu kuna amani na utulifu, naombeni hii amani na utulivu iwe ni resorces ya kuleta maendeleo. Hatuwezi kuwa kila siku tunaimba, nchi yetu ni ya amani na utulivu, mambo hayaendi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho katika hili, hatuwezi kuendelea bila private sector, niwaombe watu wa Serikali nimeanza kusikia sentiments za kuona wafanyabiashara wanatuibia, wafanya biashara ni watu wabaya, naombeni tuondoe hizi sentiments. Haziwezi kutupekeka popote, sungura wetu bado ni mdogo. Kama tunataka tuondoke hapa tulipo na wengine wote wamefanya lazima tuitumie private sector.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mifugo. Tanzania Mungu ametubariki, lakini laana hii ya mifugo haitusaidii sana, ndiyo maana tunauana kila siku kwa sababu ya mifugo, ningeomba mifugo hii tuitumie vizuri.
Mheshimiwa Mwenyekti, kilimo. Kilimo natamani ningekuwa na muda mrefu sana. Lakini itoshe kusema mwaka 2005 tulitumia bilioni 7.5 kwa ajili ya ruzuku, tukapata mazao ten million tones za mazao ya chakula. Mwaka 2015 tumetumia bilioni 299, tumepata mazao tani milioni kumi na sita. Ni investiment tunatupa bure. Ningeomba tumefika wakati twende kwenye commercial farming, tusiogope, haiwezekani kila mtu alime, haliko Taifa la namna hiyo. Tunaogopa commercial farming umefika wakati twende kwenye commercial farming, itatusaidia sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho ni elimu. Naipongeza sana Serikali, inafanya kazi kubwa kwenye elimu bure, lakini mimi bado nina tatizo pamoja na elimu bure mimi nadhani umefika wakati tuunde Tume ya Elimu. Ili tuangalie matatizo yetu ya elimu, ipitie mfumo wetu wa elimu kuanzia vidudu mpaka university. Tuangalie watu wanaomaliza darasa la saba wameelimika? Wanaomaliza form four wameelimika? Wanaomaliza Chuo Kikuu wameelimika? Haiwezekani tutakuwa tuna-solve watu hawawezi kulipa school fees tuwatolee bure, vitabu tuwanunulie, bado hatujapata tatizo letu la mfumo wa elimu ni nini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi siyo wa kwanza, Wamarekani mwaka 1981 wakati wa Rais Reagan waligundua mfumo wao wa elimu unashindwa duniani, wakaunda Commission ya Elimu. Watu wote mkaangalie, wakatoa ripoti mwaka 1983 inaitwa A Nation at Risk, waliona Taifa lao linaenda kwenye majanga. Kwa sababu tusipokuwa na elimu bora viwanda tunapiga story tu hapa. Kilimo tunapiga story, uvuvi tunapiga story, kama hatuja-solve tatizo la elimu na elimu watu wetu waelimike na you might have all the Professors lakini hawajaelimika!
Mheshimiwa Mwenyekiti, ningeomba sana niishauri Serikali umefika wakati tuuangalie upya mfumo wetu, na ndiyo maana anakuja Waziri wa Elimu leo analeta GPA, mwingine anakuja kesho anaondoa GPA, kwa sababu gani hatujui tatizo letu ni nini. Hatujui kwa nini watu wanafeli, kwa hiyo mimi ningeshauri Serikali, atakuja Ndalichako leo amesema turudi kwenye division, Ndalichako kesho anaondoka anakuja mwingine watu wanafeli sana anajenga hoja anadhani ndiyo solution tunarudi kule tulikotoka. Ni kwa sababu hatuja-diagnosis tatizo letu la elimu nchini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naunga mkono speech ya Rais. Nampongeza Mheshimiwa Rais, tunamuombea kila la kheri, aendelee kufanya kazi, aendelee kutumbua majipu, ninaamini Watendaji wa Serikali sasa wataanza kutekeleza wajibu wao. (Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali katika Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia Mpango huu. Mpango huu ni mzuri, hivyo nina mambo machache sana.
La kwanza, ujenzi wa reli mpya ya kati kwa kiwango cha Kimataifa cha standard gauge. Namwomba Mheshimiwa Waziri aseme ni ujenzi wa reli ya kutoka Dar es Salaam mpaka Tabora mpaka Mwanza, kutoka Tabora mpaka Kigoma, kutoka Kaliua mpaka Mpanda mpaka Kalema, kutoka Uvinza kwenda Msongati na kutoka Isaka kwenda Keza. Haya mambo ya kutosema ndiyo baadaye tunabaki hatuna hata pa kumuuliza. Ningemwomba Mheshimiwa Waziri aje kwenye Mpango atakapouleta maana haya ni mapendekezo, aseme. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili ni suala la retention scheme. Mheshimiwa Waziri, nakuomba sana usiingie kwenye historia ya kuua taasisi za nchi hii. Viwanda vya nchi hii vilikufa miaka ile kwa sababu kila fedha inakusanywa inapelekwa Hazina, wanaomba kuagiza raw material mpaka fedha zitoke Hazina, by the time wanapewa pesa ndiyo viwanda vikaanza kufa. Leo mnakuja mnataka kuua Halmashauri, mnataka kuua Taasisi za Serikali! Naomba Wabunge mnikubalie tupinge habari ya kuondoa retention. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitasema, leo mnasema fedha zote ziende Central Bank. Nataka nimuulize Waziri wa Fedha, fedha zinazokusanywa na Pension Funds, wasipoziwekeza Pension Funds hazifi hizi? Pension Funds zinakusanya fedha mnapeleka Hazina, watazalishaje, watalipaje pension? Leo mnasema retention scheme za kwenye airport zote ziende Hazina, kitakachotokea mtawafukuza watendaji, kwa sababu ndege zitashindwa kutua, mtakuwa hamjapeleka OC kwa sababu hela mmekusanya, mmepeleka Hazina.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri zinakusanya fedha za own source, mnasema peleka Hazina, hizi Halmashauri zitakufa, mnasema leo own source zote za TANAPA, za nani ziende Hazina. Kitakachotokea, Mbuga za nchi hii zitaanza kufa mbuga moja baada ya nyingine. Mnataka Bunge hili tuingie kwenye historia ya kuua mbuga za nchi hii? Halafu kama hoja ni kuweka hela Hazina hawajaanza leo. Hebu tukumbushane ilikuwaje miaka ya nyuma.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati BOT imeungua, ndiyo wakati hela ziliondoka Hazina, zikapelekwa NBC, alivyokuja Gavana yule Rashid akasema sasa sizitaki hizi fedha. Urasimu ulikuwa ni mkubwa sana. Nasema kama ni fedha za Serikali za Bajeti weka Hazina hakuna atakayekupinga, lakini fedha zinazozalishwa huku, mkisema zote ziende Hazina, mtaua taasisi moja baada ya nyingine. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu, hatuwezi kuwa na contradiction, mnasema D by D, D by D gani sasa? Unless mniambie kwamba sasa hatuzitambui Halmashauri zote. Kwenye Vyuo vya Maendeleo, kwenye shule za sekondari watoto wanalipa pesa wanunue chakula, mnasema peleka pesa zote peleka Hazina, muda wa kununua chakula utakuwa wapi? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho Mheshimiwa Waziri, nchi hii inaongozwa kwa sheria. Ziko taasisi zimeletwa kwa sheria, mnatakaje kuleta mambo kwa decree, mnaamua tu bila kufuata sheria? Ningeomba Waziri wa Fedha, tuletee sheria zote zilizoanzisha taasisi hizi ambazo kwenye sheria kuna mambo ya retention, tuangalie ili tubadilishe sheria za nchi. Haiwezekani mnakaa na TR mnaandika barua, fedha zote zitapelekwa Hazina kesho Jumatatu. Hii ni nini? Mnapewa sekunde.
Mheshimiwa Mwenyekiti, yapo mashirika kufungua akaunti lazima muwaite Board Meeting leo ninyi mnawapa siku nne, wawe wamepeleka fedha BOT. Kuna haraka kweli? Nasema na nawaomba sana Wabunge, hili la Retenteion tulipinge, tunalipinga kwa sababu We have a cause, tunataka kuzuia watu kuua mashirika ya nchi hii na ni kwa sababu watu wa Hazina hamtaki kufikiri. Chenge one, imewapa vitu vya kukusanya mapato, hakuna hata kimoja mmekiandika humu. Bahari kuu iko wapi, kila siku mnatuambia habari ya bahari kuu, tutakwenda kufanya utaratibu, mpaka lini huo utaratibu?
Mheshimiwa Mwenyekiti, shida ya pale Treasury watu hawataki kufikiri. Angalia vyanzo vya mapato ni vilevile toka nimeingia Bungeni havijawahi kubadilika. Naomba sana niseme tulikubaliana wakati tunaanzisha VAT kwamba VAT itapungua na ningeomba twende 16 wanavyokwenda Wakenya ili tuweze kushindana na Kenya, lakini tumekaa rigid, matokeo yake tunapambana. Nasema viwango vya kodi visiposhushwa hatuwezi kupata compliance, viwango vya kodi vya nchi hii vinatuma watu kukwepa kodi kwa sababu viwango ni vikubwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wa TRA najua wametembea duniani kote kuangalia viwango vya kodi, wakienda duniani kuangalia viwango vya kodi wanaangalia nini? Ukienda Mauritius kodi ziko chini na wanakusanya zaidi yetu, wako mpaka fifteen percent hadi cooperate tax na wanakusanya zaidi, sisi tumekalia kupandisha rate na mnajua kwa nini tunapandisha rate, ni kwa sababu hatutaki kufikiri kutafuta tax base zingine. Tumeji-zero in kwenye tax base ile ile.
Mheshimiwa Mwenyekiti, narudia tena, suala la reli kwetu sisi ni kufa na kupona. Naomba niwaambie Waheshimiwa Wabunge, Walvis Bay wanajenga reli kwenda Congo, Nakara wanajenga reli kwenda Zambia, Wakenya wanakwenda Kigali. Reli zote zikiisha Tanzania hatuna cha kwetu. Haiwezekani Mungu ametuumba Tanzania imewekwa hapa geographically Mungu ana sababu na sisi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumezungukwa na nchi nane, lakini hatutaki kutumia hizo opportunity, tatizo ni nini? Halafu mtatuambia kujenga reli, tukope maana Waziri wa Fedha juzi anasema, hatuwezi kujenga reli hii ni fedha nyingi, nani kasema, fedha nyingi nani anazitoa, fedha ziko duniani tukazitafute….
MWENYEKITI: Mheshimiwa Serukamba, muda wako umekwisha.
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuchangia Wizara ya Viwanda na Biashara.
Mheshimiwa Naibu Spika, leo naomba nianze kwa kumuuliza swali Waziri wa Viwanda na Biashara. Waziri wa Viwanda na Biashara nataka ulijibu Bunge letu, unataka kujenga viwanda vya nini? Focus yetu ni viwanda gani? Maana unapotaka kujenga viwanda, ukisema unataka kila kitu niweke kiwanda tumeanza na kushindwa. Nilidhani umefika wakati tuamue focus yetu iwe kwenye maeneo ambayo tuna comparative advantage. Ukiniambia leo tunaweza tukashindana na China, India na nchi zile ambazo zimefanya vizuri tutapata tatizo.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninachomwomba Mheshimiwa Waziri atusaidie, atuambie kwa hali ya dunia inavyokwenda, Tanzania tunaweza tukaanza na viwanda vya namna gani. Ukienda leo pale Silcon wameanzisha teknolojia lakini wana invest kwa ajili ya teknolojia hii, wanafanya research, wameandaa mazingira kwa ajili ya viwanda vya teknolojia. Ukienda Auto Mobile duniani inajulikana, siyo wote wana Auto Mobile. Ninachouliza kama Tanzania tunatakiwa twende kwenye viwanda vya namna gani? Mimi nimesoma hapa, ukiangalia mwanzo mpaka mwisho sioni tunakwenda kwenye viwanda vipi, yaani focus yetu ni nini. Tusipokuwa na focus tutarudi kule kule tulikotoka miaka ya nyuma. Ndiyo maana unasema leo mara unataka uanzishe hiki, uanzishe hiki, hatuwezi kufika.
Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niulize, maana yako mambo ambayo tusipoyaweka sawa tutakuja kushindwa huko baadaye. Mimi nasema kama nchi tunge-concentrate kwenye viwanda vya agro-industries kwa sababu tuna malighafi. Leo tukiamua kama nchi, maeneo manne tu tufanye kweli kweli, mfano Kiwanda cha Mbolea, kiwanda kikubwa ambacho tuna uhakika tutazalisha mbolea ambayo itatumika Sub-Sahara Africa, tutapata fedha nyingi sana kama nchi na tuta-save dola nyingi sana za ku-import mbolea. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, cha pili, ni viwanda vya sukari, hizi kelele hizi ni kwa sababu hatujaamua ku-invest kwenye viwanda vya sukari. Tukiamua ku-invest kwenye viwanda vya sukari Tanzania tuna hekta karibu milioni nne unazoweza kufanya irrigation, tunaweza kuzalisha karibu tani milioni mbili za sukari, tutatumia ndani na nyingine tutauza nje na tutafaidisha sana wakulima wetu ambao wako kwenye hayo maeneo. Namba tatu, mafuta ya kula, tuna michikichi, tuna alizeti, tu-concentrate hapo kwa kuanzia. Namba nne ni leather industry kwa sababu tuna mifugo mingi sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri akija hapa anasema kila mtu atajenga kiwanda awe na uhakika atashindwa, kwa sababu viwanda vinahitaji Serikali tuungane, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Waziri wa Fedha na Mipango, Waziri wa Nishati na Madini lazima wote tuongee lugha inayofanana. Ukisoma vitabu hapa, ukasoma Mpango, lugha haifanani. Sasa tunataka kujenga viwanda gani? Imefika wakati lazima tuambiane, tunawaunga mkono lakini lazima kuwe na coordination unity ambayo inawaunganisha tujue direction ya namna moja. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Waziri wa Fedha anataka kukusanya kodi, lakini kuna wakati lazima tutumie kodi kutoa incentive ili viwanda viweze kujengwa. Ili viwanda viweze kujengwa wenzetu wamefanya research, kuna mambo lazima tuhangaike nayo, lazima uangalie micro-stability ya nchi. Micro-stability yetu inasemaje? Kama huangalii hili investor haleti fedha zake! Lazima uangalie skills and education, hapa kwako mambo ya elimu yakoje? Lazima uangalie infrastructure kwa maana ya umeme, maji na transport system. Lazima uangalie teknolojia, hali ya innovation na teknolojia wewe unafanyaje, kwako pakoje?
Mheshimiwa Naibu Spika, njia ya kupata teknolojia ziko njia tatu, moja kutoka nje, mbili through FDI, tatu research and development ili kupata teknolojia ambazo ni locally made. Kama viwanda tutasema tu tutarudi kule tulikotoka na nina hakika hatutoweza kufanikiwa. Tukiamua kuungana tukajiweka kwenye viwanda ambavyo malighafi tunazo Tanzania ambazo ni agriculture tutabadilisha maisha ya watu wetu vijijini na nchi hii itaweza kupata fedha nyingi za kigeni na tutaweza kwenda mbele.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa ni Waziri wa Viwanda na Biashara, hali yetu ya biashara ni mbaya. Ukiangalia cost of doing business in Tanzania, kwa ripoti ya World Bank ya 2016 tuna rank ya 139 katika nchi 189, hili siyo jambo jema. Kwa hiyo, lazima Waziri wa Viwanda na Biashara ufanye kazi ya kufanya biashara zikue Tanzania.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukisoma Ilani ya Chama cha Mapinduzi wamesisitiza kuhakikisha tunaanzisha Bodi ya Kusaidia biashara ndogo ndogo (SMES) wala sioni ukieleza thoroughly, kwa sababu hiyo ndiyo itakayowaokoa hawa wafanyabiashara wadogo wadogo, wataajiri watu wengi, tutapata kodi nyingi sana. Kama haturasimishi biashara tunalo tatizo.
Mheshimiwa Naibu Spika, nitamwambia Mheshimiwa Waziri kwa mfano, wanasema ukitaka kuanza biashara Tanzania sisi tunachukua nafasi ya 129 katika nafasi 189, ukitaka kupata construction permit tunakuwa wa 126, kupata umeme wa 83, ku-register property wa 133, kupata credit wa 152, kuwalinda minority investors wa 122, kulipa tax wa 150, trading across borders wa 180 kati ya 189, enforcing contract wa 64 na resolving insolvency sisi ni wa 99. Waziri wa Viwanda na Biashara lazima uhangaike kuhakikisha unajenga mazingira ya biashara kukua Tanzania. Tusipojenga mazingira ya biashara kukua Tanzania maana yake ni moja tu, hata hivyo viwanda tunavyoviongea havitapatikana, wawekezaji hawatapatikana.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nasema Waziri anaposhughulika na suala la viwanda na biashara lazima ajue analo jukumu la kuhakikisha biashara inaenda vizuri isidumae. Ili isidumae lazima uondoe hizi bottlenecks! Tanzania tumeumbwa tuna nchi karibu nane zinatuzunguka, hii ni advantage kwetu kiuchumi, je, tunaitumiaje? Lazima mipango yetu iende towards kwenye kuleta biashara na siyo tu biashara hata kufanya biashara Tanzania isiwe tatizo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba Waziri wa Viwanda ukae na Waziri wa Fedha, concentration yetu isiwe kukusanya kodi tu, lazima tutumie kodi kukuza uchumi. Unakuza uchumi kwa wafanyabiashara, kwa kuweka mazingira ya watu kuleta fedha zao kwako na hatuwezi kuamini kwamba tunaweza tukaleta mageuzi ya viwanda kwa kutumia fedha za bajeti, haiwezekani! Tukidhani unaweza ukatumia fedha za bajeti mjue tunaelekea kwenye kushindwa. Ili mwenye fedha zake aje, asiende Mozambique, Kenya, Rwanda lazima uweke mazingira ya kumkaribisha aone kwamba Tanzania nikienda nitapata zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sisi tumehangaika kule Kigoma, Wahindi wanataka kuleta Kiwanda cha Sukari, wamezungushwa mambo ya ardhi karibu sijui miaka mingapi, inawezekanaje? Huku tuna matatizo ya sukari in the country, kuna mtu anataka kuja kuweka kiwanda anazungushwa tu. Lazima haya Waziri wa Viwanda uhangaike nayo.
Mheshimiwa Naibu Spika, ningeomba Serikali iunde committee ambayo itahusisha watu wa Wizara ya Fedha na Mipango; Kilimo, Mifugo na Uvuvi; Viwanda, Biashara na Uwekezaji; na Nishati na Madini, ili mkikaa muwe mnajua hali inavyokwenda nchini kwa maana ya kuhakikisha mnaondoa bottleneck za biashara nchini ili watu waweze ku-invest Tanzania.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimalizie kwa kusema Waziri nakuunga mkono, lakini nasema ukisoma mipango yako naona unataka kuanzisha kiwanda everywhere as if viwanda ni jambo rahisi, suala la viwanda siyo rahisi kama tunavyotaka kuiweka, unaweza ukaweka viwanda kesho vyote vikafa. Ndiyo leo unataka kufufua General Tyre, is it our priority? Huo mpira wenyewe umeanza kuulima? Maana unaweka bajeti leo kwa ajili ya General Tyre shamba hujaanza kulima, je, hayo matairi yako yanaweza yaka-compete kwenye biashara nyingine duniani, unaweza u-compete na wengine? Ukiangalia cost zako unaweza uka-make money ama tunataka kurudisha General Tyre out of prestige kwamba na sisi tumefufua, prestige! (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, biashara jamani ni economics tuache kuchanganya siasa, biashara na viwanda. Suala la viwanda na biashara, tukachanganya na siasa, nina hakika, hatutakwenda tunakotaka kwenda. Nakuamini Waziri, Serikali ina nia njema, lakini kaeni muwe more focused, tuanze vile tunavyoviweza ambavyo raw materials zake ziko Tanzania na tukizalisha vizuri tutaweza kuuza angalau regionally kabla hatujaenda huko nje.
Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja na nakushukuru.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2015, Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, nami naomba nikupongeze, nimpongeze Waziri wa Fedha na watendaji wote na nashukuru kwa nafasi hii uliyonipatia.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nianze kwa kumwomba Waziri wa Fedha. Rais alipokuja Kigoma moja ya jambo ambalo alituahidi ni suala la tozo kwenye zao la kahawa ambalo lina tozo 26. Alisema hizi tozo lazima ziondoke. Namwomba Mheshimiwa Waziri atakapokuja kujibu, atuambie kwa nini hakuona umuhimu wa kutoa tozo hizi kwenye zao la kahawa? Ni kwa nini tunaomba tozo hii zipunguzwe? Ni kwa sababu bei ya soko la kahawa imepungua duniani. Namna ya kuwasaidia wakulima wetu ni kupunguza tozo hizo ili waweze kufaidika na zao la kahawa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, la pili ni suala la maji kwenye Jimbo la Kigoma Kaskazini. Tatizo la maji ni kubwa sana, lakini tuna Lake Tanganyika. Namwomba sasa Waziri wa Fedha aje na mipango atuambie lini tutaanza kuyatumia maji ya Lake Tanganyika; siyo kwa Kigoma Mjini, ni kwa ajili ya Jimbo la Kigoma Kaskazini pamoja na Mkoa mzima wa Kigoma? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nimpongeze Waziri wa Fedha, anapeleka asilimia 40 kwenye maendeleo. Kwa vyovyote vile haya ni mageuzi makubwa sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimetafakari sana asilimia 40 maana yake nini? Asilimia 40 Mheshimiwa Waziri wa Fedha, maana yake unaenda kutengeneza umeme, majenereta utayanunua nje, kwa hiyo, tuta-save fedha zetu, tutatoa dola kupeleka nje kupata umeme. Tutatoa dola kutengeneza reli, maana itabidi tuchukue kwanza shilingi, tutawalipa wakandarasi, kwa vyovyote vile watakuwa wa nje. Kwa hiyo, hela itakwenda nje; tunanunua ndege, fedha itakwenda nje. Maana yake ni nini? Tuna-save kama nchi kwa shilingi yetu; itabidi tununue dola kununua hizi services. Ili tuweze ku-strike a balance lazima na sisi tuwe na eneo ambalo litatuingizia dola nchini. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hapa ndipo ambapo wachumi wetu tungewaomba watusaidie. Ninayo maeneo makubwa matatu ambayo nataka niwashauri watu wa Serikali.
Mheshimiwa Naibu Spika, eneo la kwanza ni suala la tourism. Wanaoshindana na sisi kwenye utalii ni Kenya, Uganda, Rwanda, Mauritius na South Africa. Wenzetu hawajaweka VAT kwenye utalii, maana yake tunaifanya Tanzania iwe destination ambayo ni gharama na utalii mtu hawezi kuja.
Mheshimiwa Waziri wa Fedha, tukiweka VAT uwe na uhakika katika watu ambao wataumia zaidi ni Wazanzibar na uchumi wa Zanzibar. Kwa sababu uchumi wa Zanzibar unategemea tourism na tourism ya Zanzibar iko packed pamoja na utalii wa Kaskazini. Mtu angependa aende Zanzibar, aende na Serengeti; aende Mikumi aende na Zanzibar. Naombeni hili jambo tuliangalie kwa umakini mkubwa sana.
Sehemu ya pili ambayo itatuingizia dola ambayo lazima wachumi wetu tukubaliane, ni suala la kwenye masoko ya mitaji. Dar es Salaam Stock Exchange tuliamua kuwapa incentive kwenye capital gain ili watu wengi wapeleke, waende waka-list pale. Waki-list kwenye DSE maana yake ni nini? Maana yake ni mitaji tutapata liquidity, maana yake ni job, ndiyo tutafanya uchumi uchangamke.
Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza Gavana wa BOT, ame-liberalize account ya nje ndiyo maana sasa DSE kuna watu wanatoka nje wanakuja kununua share; lakini ukiweka hiyo kodi maana yake watu wataondoka Dar es Salaam Stock Exchange. Hata anachotaka kukipata, hakitafanikiwa.
Kwa hiyo, nakuomba sana Mheshimiwa Waziri, walioamua kuweka zile incentives kwa ajili ya soko letu lichangamke, naamini walifikiri vizuri. Haiwezekani tuziondoe leo sisi, nakuomba sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, siyo hiyo tu, hata kukusanya hiyo kodi ni ngumu sana; maana capital gain tax ni wakati gani? Mimi nina share 200 nimeuza, pale nikizidisha ndiyo unakuja unakata, kwa sababu watu wote hatuuzi share at a time. Kwa hiyo, unachotaka kukipata unaweza usikipate mwisho wa siku. Kwa hiyo, suala hilo litakuwa ni gumu sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, eneo la tatu, jana Mbunge mwenzangu wa Kahama amelisema, sijui kama nitafanikiwa kulieleza kama alivyolieleza. Ametuambia jambo jipya, lakini limekuwepo, mwaka 2011 Kamati ya Madini na Nishati walilisema kwamba umefika wakati tufungue soko la dhahabu Tanzania. Tunalifunguaje? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sisi tuweke mazingira kwamba kila anayekuja na madini yoyote Tanzania, halipi hata shilingi moja. Halipi kodi yoyote, lakini atakayetaka kuyatoa madini hapa Tanzania, tusichukue kiasi kikubwa, unaya-export 1% tu.
Mheshimiwa Waziri wa Fedha ngoja nikwambie kitakachopatikana; tukiamua kufanya hivyo, unayo hakika kwa mwezi tutapata siyo chini ya tani 20 za dhahabu peke yake. Watu watakaokuja kununua hapa, ile dhahabu moja kilo moja ni dola 40,000. Maana yake ni nini?
Mheshimiwa Naibu Spika, unapozi-export maana yake unachukua dola 40,000 unazidisha kwa hizo kilo 20,000 utapata karibia dola milioni 800; ukizidisha kwa hela ya Tanzania ni 1.6 trillion. Maana yake ni nini? Asilimia moja ni shilingi bilioni 16. Kwa hiyo, kwa mwaka una hakika utapata shilingi bilioni 200. Shilingi bilioni 200 ni Wizara ngapi umezipa fedha? Ni nyingi sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, hawa watu watakaokuja hapa, watanunua vyakula vyetu, tutapata kwenye VAT, tutapata kwenye hoteli zetu, watanunua kwenye masoko yetu. Naombeni wachumi wetu wakati wa kutumia mambo ya kwenye vitabu, tuanze na mambo ambayo ni practical, tuyasimamie, tutabadilisha nchi yetu. Ndiyo maana tunataka kuweka kodi kila eneo kwa sababu tunataka kufikiria maeneo yale yale.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nasema ile 48% ambayo tutaipeleka kwenye maendeleo, tutafute namna ya kuirudisha ndani. Namna ya kuirudisha ndani Mheshimiwa Waziri wa Fedha, tunaomba twende kwenye tourism, tuanzishe soko la dhahabu, lakini pia tuwe na incentive kwenye Dar es Salaam Stock Exchange ili watu wengi waweze kuja hapa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ningependa nichangie baada ya kutoka hapa Mheshimiwa Waziri wa Fedha, ni suala la viwanda. Bajeti yako inaimba neno “viwanda.” Nakuomba sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha, ukisoma historia ya watu ambao wameendelea juzi tu kwenye viwanda, kuna mambo lazima tukubali kuyakosa. Ni aidha upate viwanda ama upate kodi. Ukianza na kodi hatuna viwanda; tukubaliane! (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, leather industry, kwa maana ya Leather Industry in Ethiopia. Wanasema imefanikiwa kwa sababu one, hakuna kodi kwenye capital goods; hakuna kodi kwenye construction materials; kuna cheap electricity; kuna cheap labour. Wamepewa miaka sita kutolipa income tax. Wamepewa holiday! (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, unachotafuta kwenye viwanda, kitu cha kwanza ni ajira. Watu wetu wakishakuwa na ajira watakuwa na purchasing power. Kwa hiyo, kodi yako utaipata, ni indirect tax, utaipata tu! Cha pili, ni bidhaa ziwepo sokoni. Kodi ni sehemu ya tatu unapoongelea kwenye ule mnyororo wa viwanda. Target ya kwanza ni ajira, bidhaa, ndiyo unakuja kodi na unakuja kuangalia GDP yako.
Mheshimiwa Naibu Spika, naiomba sana Wizara ya Fedha, tuliangalie hili eneo. Kama hatujajiandaa, tutasema sana kwenye vitabu, lakini tunaweza tusifanikiwe na nia yetu ni kufanikiwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna suala la sunflower. Sunflower imeongezeka, ilianza kidogo, sasa hivi imefika tani 180,000; maana yake industry inakua. Sasa tukiweka kodi kwenye crude oil maana yake unasema hakuna haja nilete crude oil, acha nilete refined oil ili nilipe 25% niuze; lakini utakuwa umepoteza ajira za watu wangapi?
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna vitu vingine tunavifanya ili kulinda viwanda, ili kulinda ajira, hili ndiyo la msingi kama Taifa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lingine nilitaka niongelee suala la PPP. Suala hili linasemwa sana kwenye vitabu, lakini kwenye matendo halionekani. Namwomba sana Waziri wa Fedha, sheria ipo, kanuni zipo, tuanze. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niwaulize Waheshimiwa Wabunge wenzangu, hivi kweli karne hii leo tunaweka bajeti kununua ma-generator ya umeme, wakati ukitangaza, utapata watu wengi tu wa kununua majenereta ya umeme. Kwa nini tuweke hela ambayo tungeipeleka kwenye afya, elimu na maji? Ni jambo ambalo ukiwaita wawekezaji watakuja, unachotakiwa kuweka ni tarrifs ambazo watu wako watafaidi kama Taifa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tuweke mazingira ya kusema, unataka kuja kuleta umeme Tanzania? Eeh, lazima uwe na Mtanzania mwenye 30% mpaka 40%. Haya tukiyafanya, tutaenda mbali. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tuna Mashirika ya Serikali, mimi nitatoa mfano wa shirika moja tu. Mafuta ya ndege Tanzania, Puma ndiyo wana-manage 90%, lakini eti tunampa mtu mwingine aagize ndiyo amletee Puma na sisi tuna share kule 50%. Hivi nani ambaye hajipendi? Lazima tufike maeneo mengine tufanye maamuzi kwa sababu tuna interest kule.
Mheshimiwa Naibu Spika, juzi tumemwona Waziri wa Fedha anapokea dividends. Maana yake ni nini? Kwamba, tukiwapa biashara kubwa, tutapata fedha nyingi kama Taifa. Tukipata fedha nyingi, tutachangia kwenye uchumi wa nchi, tutachangia kwenye maendeleo yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nawaomba watu wa Serikali, tusaidieni. Yale maeneo ambayo tuna interest kama Taifa, tusione aibu kutumia makampuni yetu. Tusione aibu hata kidogo, kwa sababu tukiogopa tunafanya nini? Tutakuwa tunaongea huku, mkono huu tunafanya kitu cha ajabu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, cha mwisho nataka niongee suala la Kurasini Logistic Centre. Nimesoma hapa suala la Kurasini. Suala hili ni jema sana, lakini nataka niwaambie Waheshimiwa Wabunge, ukisoma kwenye Mpango wa Miaka Mitano, Waziri wa Fedha anasema kwenye mpango ule kwamba kuna kampuni za Kichina zitakuja kufanya biashara pale Kurasini; jambo jema, tutapata bidhaa za bei rahisi; lakini mnajua maana yake? Maana yake tumewaua Wakinga, tumeua Wachaga, Kariakoo tumeiua. Maana yake hawawezi ku-compete.
Mheshimiwa Naibu Spika, wale watakaoleta mizigo yao kutoka kule China watapewa export guarantee, watapewa incentive na nchi zao, anakuja anauza bei ambazo umeweka wewe; wewe utakuwa na gharama. Sisi tutakuwa ni expensive; watu wote watakwenda pale. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, najua argument ya baadhi ya watu wanasema, ukifungua Logistic Centre ile kitakachotokea nchi zote zilizotuzunguka zitakuja kununua Tanzania. Sawa nakubali, lakini zikinunua Tanzania, yule anayeuza ni Mchina, sio Mtanzania! Maana yake fedha zile zinakwenda China. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tukubaliane jamani, moja ya mambo ambayo tusipokuwa waangalifu tukiwaondoa hawa wafanyabiashara wa katikati, tunaua economy yetu. Tukubaliane, hatuwezi kuendelea bila Watanzania wengi kuwa matajiri.
Mheshimiwa Naibu Spika, hii habari ya kufikiria Watanzania wakiwa maskini ndio tutaendelea, haiwezekani. Tutapata kodi nyingi wakiweko wafanyabiashara wengi zaidi. Tuweke mazingira ya kukusanya kodi, lakini tuweke mazingira ya kulinda biashara za watu wetu. Tulete mazingira ambayo kule ambako tunafanya biashara kama Serikali, tuhakikishe tunawapa biashara. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tusipofanya hivyo, Mungu ametupa jiografia nzuri sana Tanzania; maeneo haya tuliyopewa kama nchi tuyatumie kibiashara. Tanzania tuna amani, Tanzania tuna mvua, Tanzania tuna maji, tuna mito, tuna lakes, tuna everything! Sasa kwa nini tusitumie jiografia yetu hii kwa ajili ya maendeleo yetu? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nawaomba wachumi wetu wakae tufikiri; tusidhani tutakuwa tunafanya mambo kama tunavyofanya miaka yote, mambo yamebadilika sana. Naiomba sana Wizara ya Fedha itusaidie. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho na mimi niliseme, nimesikitika kidogo. Mheshimiwa Waziri wa Fedha anasema, katika mikoa maskini ni Kigoma, Mwanza na mingine aliyoisema. Hapa tuulizane Waheshimiwa Wabunge; hivi kweli jamani Mwanza ni maskini kuliko Katavi? Mwanza ni maskini kuliko Lindi? Mwanza kweli kuliko Pwani! Maana Pwani ni nchi katika nchi ambazo zimefanya vizuri sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, nataka Mheshimiwa Waziri wa Fedha, atuambie vigezo vyake vya kupima umasikini ni vipi? Ni idadi ya watu au ni nyumba? Ni kitu gani kinapima umaskini?
Mheshimiwa Naibu Spika, Mwanza ambako wana ng‟ombe; Mwanza ni wavuvi; Mwanza kuna dhahabu; inawezekanaje wawe maskini kuliko watu wa Lindi? Inawezekanaje? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ukiniambia Kigoma, Mwanza, nitaelewa. Kigoma maskini nakubali; lakini hata mimi ukiniambia Kigoma ni maskini sikubali sana; ndiyo Mkoa pekee hatujawahi kupewa chakula toka uhuru wa nchi hii. Halafu watu hawa eti ndio maskini. Tunakuwaje maskini? Kwa hiyo, naomba data zetu tuziangalie upya. Naamini liko tatizo kwenye kuandaa hizi data zetu za watu wa Mipango. Kabisa! (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho kabisa ni suala la pensheni. Nimwombe Waziri wa Fedha, suala la pensheni…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Peter Serukamba, dakika zako 15 zimeisha na zile ulizokuwa umepewa pia umeshazimaliza.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nikushukuru kwa kunipa nafasi.
Mheshimiwa Naibu Spika, leo nitachangia maeneo matatu ambayo Waziri ameyasema kwenye kitabu chake. La kwanza amesema page ya 11 kusimamia Deni la Taifa, la pili kusimamia Taasisi za Mashirika ya Umma na la tatu Kusimamia Sera ya Ubia Kati ya Serikali na Sekta Binafsi.
Mheshimiwa Naibu Spika, Deni la Taifa ni jambo ambalo lazima tuhangaike nalo vizuri sana, tusipohangaika nalo tunaweza tukajikuta juhudi zote zinazofanywa na TRA kukusanya kodi nyingi zisionekane kwa kiasi kikubwa katika kupeleka maendeleo kwa watu wetu. Katika kuangalia suala la Deni la Taifa, naomba nijikite kwenye suala la interest ambazo tunalipa kwenye madeno haya tunayoyachukua.
Mheshimiwa Naibu Spika, na nitaomba Waziri atakaponijibu aniambie wanampango gani. Interest ni risk management, risk management inahitaji kila siku tuangalie kinachoendelea kwenye uchumi wa dunia. Sisi tunakopa dola, so kitakachotokea kwenye uchumi wa Marekani wale watu woote wanaokopa dola lazima kiwa-affect,sasa tunafanyaje? Ukienda kwenye mikataba yetu yote ya Wizara ya fedha ambayo tumekopa pesa kwa ajili ya kuendesha bajeti jambo jema, interest zetu zote ni liable fractuate ni floating interest, uki-float interest maana yake nini? Unapofanya floating interest maana yake uchumi wa Marekani uki-tilt kwenda juu au kwenda chini utaku-affect kwa sababu kwanza unakopa kwa dola lakini kwa maana nyingi ni kwamba haijawahi kutokea ishuke sana kwamba ile uliyo-float wewe uta-benefit mara nyingi sisi tunapoteza.
Mheshimiwa Naibu Spika, nitatoa mfano tumewahi kuchukua kwenye Swiss Credit, ukiangalia interest ya mwezi wa kwanza ni 1.3% lakini ukienda nayo mpaka unamaliza inafika mpaka five percent unafanyaje, ukimuuliza leo Waziri wa fedha mwezi kesho utakapokuwa unalipa ile mshahara, ile first charge ambayo ni interest atuambie ni shilingi ngapi atalipa kama interest Waziri wa Fedha hajui, kwa sababu itategemea situation ya economy ya wakati ule anataka kulipa tunafanyaje sasa kama nchi.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kumshauri Waziri wa Fedha umefika wakati watu wa Idara ya Madeni waangalie trend za interest zinaendaje. Wanachofanya wenzetu kuna kitu kinaitwa swapping, una-swap interest rate unazi-swap ili uzi-fix ukifanya fixed rate maana yake unaweza uka-determine cash flow yako.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo wakati unapanga unajua mwezi ujao mshahara kiasi fulani, sijui majeshi kiasi fulani, interest kiasi fulani kwa sababu unajua una uhakika kwa hiyo, ni rahisi katika ku-manage budget ya Serikali, lakini ukiruhusu tukaenda kwenye floating ambayo ukienda kuangalia inavyo fractuate by the end of the year itafika 0.894 maana yake ni nini, Kidata atakusanya pesa nyingi sana, zile fedha zikija nyingi zinakwenda kwenye kulipa madeni mpaka tutaanza kuulizana mbona makusanyo yameongezeka lakini mbona hela haziendi nyingi kwenye Halmashauri, ni kwa sababu hatu-manage interest rate.
Mheshimiwa Naibu Spika, nataka Waziri wa Fedha aje ani-critisize hapa kwamba tunafanyaje kwenye suala la ku-budget interest rate ili ku-manage budget ya nchi, ku-manage cash flow zetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, la pili nataka kuchangia ni suala la PPP. Waziri wa fedha anasema kwenye kitabu chake page ya 11, kusimamia sera ya ubia kati ya Serikali na sekta binafsi maana yake ni PPP. Ukienda page ya 29, Waziri wa fedha huyo huyo anasema, kwenye suala la kuchukua madeni anasema masharti nafuu ambayo inakopa kwa uangalifu kutumika kwenye miradi yenye vichocheo vya ukuaji wa uchumi ikiwemo ujenzi wa miundombinu, barabara, reli, ujenzi wa mitambo ya kufua umeme, ujenzi wa viwanja vya ndege pamoja na bandari na kadhalika. Maana yake ni nini? Huku unasema unataka ku-embrase PPP, huku unasema nataka nikope kujenga miundombinu, niambieni ni nchi gani Waziri wa Fedha atuambie unaweza ukaleta PPP kama siyo kwenye miundombinu? Tell us? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hivi kweli kama Serikali kwa nini leo uweke hela kwenda kununua majenereta wakati ukitangaza wako watu wengi sana watanunua majenereta halafu ile fedha ambayo ungenunua majenereta peleka kwenye elimu, peleka kwenye maji, peleka kwenye shule, peleka kwenye kulipa wanajeshi, lipa mapolisi wetu, hii ndiyo management ya economy.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye suala la PPP naomba tujifunze kwenye aspect moja na Wabunge nataka mnisikilize kwenye suala la simu. Leo vijijini kwetu nani anayeuliza simu hii ni ya nani? Si kila mtu anataka kuwa na simu? Nani anauliza simu hii ni ya Serikali au ni ya nani? Leo tumeweka legal frame work yenye clarity watu wameweka fedha, wamefanya nini leo simu ziko mpaka vijijini, tunapata ajira, tunapata kodi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, bado kwenye mambo mengine tunaona wagumu kweli kuleta watu wa nje ama kuleta PPP na ukiamua ili u-benefit watu wako Waziri wa Fedha, kama nia ni kusaidia private sector ya Tanzania hii ndilo eneo la kusaidia watu. Waambie unataka kujenga bandari, siwezi kukupa kujenga bandari mpaka uwe na Mtanzania, unataka kufungua umeme mpaka uwe na Mtanzania hii ndiyo namna tutaweza kuukuza huu uchumi na ikatusaidia kwa maendeleo ya nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tukidhani Serikali inaweza ikafanya kila kitu, Serikali hii tutaichosha. Tutashindwa kununua dawa hospitalini, tutashindwa kupeleka hela kwenye education kwa sababu leo hii tunasema elimu bure maana yake ni nini, watoto wengi sana wana-access watakuwa wengi tutahitaji kujenga madarasa, tutajenga kila kitu, hii ni hatari sana kwenye economy. Nikuombe Waziri wa Fedha, tulipitisha sheria ya PPP mwaka 2009, tuanze kuitekeleza sasa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine nilitaka kulizungumzia ni suala la Mashirika ya Serikali. Taasisi za umma, naombeni Waziri wa Fedha na hii kazi ya Waziri wa fedha pamoja na kukusanya kodi lazima ufanye jukumu la kukuza uchumi wa nchi. Utaukuza uchumi wa nchi kama tuta-embrase biashara. Kama bandari wanafanyabiashara waacheni kuwaingilia, waacheni wafanye kazi za biashara. Kama TANESCO wanafanya biashara waambieni wafanye maamuzi ya kibiashara, ninyi kazi yenu mwisho wa siku muwaulize tu though TR tunaomba dividend mwisho wa mwezi.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini Serikali kuna baadhi ya maeneo tuna-share. Kwa mfano nitasema PUMA Serikali ina asilimia 50 lakini Waziri wa fedha naomba nikwambie kwenye bulk procurement hamjawahi kutumia Kampuni yenu ya PUMA hata siku moja. Kwenye kununua mafuta mnanunua kwa watu wengine hii ni nini? Huku mna-share, mnapata dividend lakini mnapoanza kununua mnanunua kwa watu wengine, hivi nani asiyejipenda? Ukienda South Africa leo hakuna mfanyakazi wa Serikali ambaye hapandi Ndege ya South African Airways. Leo tunaingiza pesa, tunajenga ndege kitakachotokea kwenye ticket mtapanda Emirates, maana tunaulizana maswali hapa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kama tunataka mashirika haya na taasisi za Serikali yachangie kwenye uchumi wa nchi tuyaache yafanye kazi kibiashara. Naombeni sana bila kufanya hivyo hatutokwenda, naombeni tuanze kazi ya kuamini wafanyabiashara nao ni watu na niombe Waziri wa Fedha, tuache kufikiria wafanyabiashara ni wezi. Tuweke mazingira ya kuzuia wasikwepe kodi lakini tujue ni watu tunaowahitaji kwa maendeleo ya Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ninalotaka kusema ni suala la bei ya mafuta, again narudi kwenye interest pale pale, bei ya mafuta duniani imeshuka weee, imefika mpaka barrel kwa pipa shilingi dola 29, leo imefika dola 50. Maana yake ni nini kwenye uchumi? Sisi tumekaa tunasubiri tu dunia iamue mafuta yakipanda sawa yakishuka sawa. Kazi ya Waziri wa Fedha, Idara yako hiyo ya Sera na ya Madeni ni kuangalia vitu hivi kinachotokea kwenye uchumi kila siku. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, leo tulichotakiwa tufanye, tungefanya oil hedging baada ya mafuta tulivyoona yanaanza kurudi, yameanza kufika ishirini na tisa, thelathini tunge-hedge tukasema mafuta yetu ya miezi sita tuta hedge kwa dola 30 per barrel. Na uki-hedge wanafanya watu wote, kama watu binafsi wanafanya, watu binafsi wanapata interest ndogo, kwa nini Serikali tusipate? Ni kwa sababu tunataka kufikirie vilevile tulivyozoea. Uki-hedge Waziri wa Fedha, maana ukiacha, mafuta yakiendelea kupanda maana yake bajeti yako inakuwa tilted, yale uliyoyapanga kununua mafuta haitawezekana, itabidi ubane. Rais amekuja na jambo zuri sana, Rais ameweka austerity measure kubwa, ana-manage economy, anapunguza matumizi, sasa tumsaidie.
Tumsaidie kwa kuangalia trend za market kwenye dunia. Leo mafuta mwaka jana…
Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nashukuru kwa kunipa nafasi. Kwanza niwapongeze Kamati ya Bajeti kwa ripoti yao nzuri na kwa kweli vitu vingi wamevielezea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaongea machache. Moja, ni deni la Taifa. Naamini, nilisema wakati wa bajeti na leo naomba nirudie tena. Kama kuna eneo ambalo tusipolisimamia vizuri juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano, hatutaziona.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kila unapoongelea deni la Taifa, tunaambiwa deni letu ni himilivu (sustainable) kulingana na viwango vya Benki ya Dunia na IMF. Naomba tufikiri tofauti kidogo. Deni hili tunatumia GDP kujua kama deni la Taifa linahimilika. GDP ni sawa, ndiyo mali zote tulizonazo, zinajumlishwa, halafu unaangalia percentage ya deni ulilonalo. Unapoanza kulipa deni, hutumii ile GDP sasa, unalipa deni kutoka kwenye mapato yako. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, unakusanya kila mwezi ukishakusanya, first charge mshahara, first charge, deni la Taifa. Wizara ya Fedha watatuambia, tumefika sasa tunakusanya makusanyo; asilimia 86 ya makusanyo yanaenda kwenye mshahara na deni la Taifa. Maana yake ni nini? Hatutapeleka hela kwenye maendeleo. Kwa hiyo, lazima tubadilike; tunapotaka kuliangalia deni letu, tuli-peg na revenue base yetu. Tukifanya hivyo, tutaweza kwenda huko tunakotaka kwenda.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kwenye deni la Taifa, tumeshafika hapa. Hilo la kubadilisha namna ya ku-calculate, tuamue sasa kama Serikali, tutumie revenue ratio ili tuweze kujua tunaweza ku-manage deni la Taifa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo litaleta shida, mikopo yote ambayo tumeichukua, hasa ile ya kwenye mabenki, kuna kitu kinaitwa floating libor, wakubwa wanaenda kukopa kwenye mabenki wanatuambia chukua floating libor kwa sababu kwa hii inaweza interest zikashuka ama zikapanda; lakini trend imekuwa, ni interest zinapanda. Kwa sababu huwezi ku-control wewe. Ikishakuwa floating libor huwezi ku-control wewe, mwezi kesho unalipa nini kwenye interest rate? Anaye-control ni bwana mkubwa Marekani. Reserve Bank ya Marekani mwaka 2016 imeongeza kutoka 0.25% to 5%. Maana yake nini? Interest zetu nazo zikapanda. So we are here tumekaa, tunasubiri the mercy ya wengine. Lazima twende kama wanavyofanya wenzetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye bajeti nilisema nikajiwa hapa, kwamba unachosema sawa, lakini nahitaji a complicated work force. Hii complicated ya wapi? Duniani wanafanya, kuna kitu kinaitwa swap interest rate. Ukifanya swap, utalipa kingi mwezi wa kwanza, baada ya pale, interest yako unayoilipa inakuwa ni constant kila mwezi. Kwa hiyo, kama Taifa, utakuwa unajua kila mwezi ni shilingi ngapi nalipa kwenye deni la Taifa. Leo hii tukimwuliza Waziri wa Fedha, mwezi kesho atalipa shilingi ngapi kwenye deni la Taifa, hajui kwa sababu sio yeye anaye-control. Ni uchumi mwingine ndiyo una-control kwa sababu tu tumekwenda kwenye floating libor.
Mheshimiwa Mwenyekiti, unajua kinachotokea? Wanakuja wale wenye mabenki wanakwambia ukienda kwenye floating libor interest rate mwezi wa kwanza utalipa 0.1% au 1.3%, lakini ukienda kwenye fixed anakwambia itakuwa ni 1.75%. Kwa hiyo, wewe as a country una-save kwenda kwenye 1.3%! Uliza mwezi wa Pili, mwezi wa Tatu au mwezi wa Nne inakuwaje? Unakwenda kila mwezi unaongezeka, utatoka 1.3% mpaka 5%, lakini yule aliyelipa 1.75% ataendelea kulipa hiyo mpaka mwisho wa hilo deni.
Mheshimiwa Mwenyekiti, haya tunayoyasema wenzetu wamefanya, sisi sio wa kwanza. Nawaombeni sana watu wa Wizara ya Fedha, tufike sehemu tufikiri tofauti kidogo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, ni suala la investment model ya growth ya economy yetu. Naomba sana Serikali, tusirudi tulikotoka miaka ya nyuma. Nawaombeni sana. Wenzetu wote wanakwenda kwenye private sector ndiyo engine ya growth. Tukidhani Serikali hii inaweza ikafanya kila jambo, nawaambia hatutafanikiwa. Mwalimu Nyerere alifanya hapa, alijenga kila kiwanda, leo viko wapi vyote? Kwa sababu, mambo haya ya viwanda, mambo haya ya investment, lazima uingize hela kila wakati. Siyo kila wakati utapata faida! Kitakachotokea leo utapata hasara, kesho unafanyaje? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi zilizoendelea hivi karibuni baada ya miaka ya 60, nchi kama Malaysia wanatumia hela za watu kufanya uwekezaji. Wewe unachotaka kama nchi, unataka huduma. Nchi inataka umeme megawati 5,000; kuna mtu anaweza akaleta fedha zake akaweka umeme, shida yetu ni nini kumpa? Ni lazima kila kitu kifanywe na TANESCO? Mtu anataka kujenga barabara kutoka Dar es Salaam; Swiss Dual Carriage, mpaka Dodoma, aweke road toll, sisi hatutaki. Maana yake ni nini?
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeongea habari ya PPP, tumeweka Sheria, lakini soma Ripoti za Wizara ya Fedha; kama kuna jambo hawana interest ni suala la private sector. Private Sector ni wezi hawa. Naomba sana tubadilishe mentality ili twende kwa kasi. Kwa kasi ya Rais Magufuli, tukimsaidia tukaanzisha miradi ya private sector tutaenda kwa kasi sana ya maendeleo. Naomba sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati wa bajeti tulisema kuhusu bei ya mafuta. Niliwaambia jamani eeh, bei ya mafuta duniani inapanda na wenzetu wana-hedge na hata Kenya wame-hedge, kwa nini sisi hatu-hedge? Watu ni kama vile tunaongea, tunayaacha hapo hapo. Ilikuwa wakati ule ni dola 44 per barrel, leo inakaribia dola 60 per barrel, tuko hapa hapa! We are at their mercy, tumekaa tunasubiri tu. Kwa hiyo, inaweza ikapanda mpaka ikafika 100, wakishakuja wanakwambia, unajua viashiria vya mwaka huu, bei ya mafuta duniani inapanda; lakini inapanda ukiwa unaangalia. Naomba watu wa sera wa Wizara ya Fedha mtusaidie. Vitu hivi wenzetu wanafanya, haiwezekani sisi tusifanye. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie kilimo. Naomba sana, kilimo chetu tumelima namna hii miaka 50, karibia 60 ya uhuru tunaendelea kulima namna hii. Mvua ikitetereka kidogo tunaanza kupiga kelele. Ni kwa sababu hatu-embrace commercial farming. Naomba tu-embrace commercial farming, ndiyo itakayotutoa hapa kwenda mbele.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano rahisi wa commercial farming ndugu zangu, twende Zimbabwe. Bwana mkubwa yule wa Zimbabwe aliamua akafukuza wale Wazungu kwa sababu ya uzalendo wa ardhi, leo wanakufa njaa. Maana yake nini? Kilimo kinahitaji uwekezaji mkubwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeongea habari ya pembejeo hapa, mwaka huu pembejeo hakuna. Tumetoka shilingi bilioni karibu 80, mwaka huu tumeweka shilingi ngapi za pembejeo? Tunatarajia kupata nini? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ili tuweze kutoka hapa, ni lazima tuone namna bora tuwe na mashamba haya ya akina mama yake na Peter, ambayo wanalima miaka yote hawajawahi kujitosheleza, lakini tuwe na mashamba ya mabwana wakubwa wenye fedha ambao watajitafutia wagani wao, watanunua pembejeo za kwao, wataweka umwagiliaji, watatafuta mbegu bora, hawatasubiri Serikali. Hapo kama Taifa, tutatoka hapo tulipo, tufike tunapokwenda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaongea habari ya viwanda, tunaingiza mifuko ya jamii kwenye viwanda. Tuwe waangalifu sana. Tukizubaa mifuko hii tutaipoteza. Nilidhani mifuko iingie kama kuweka mtaji, shughuli ifanywe na wengine, lakini mkitaka waingie wafanye wenyewe, nawaambieni wataanza ku-provide losses hapa, tutashangaa baada ya miaka michache ijayo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, duniani kote hawafanyi. Wanachofanya, wanaingiza kwenye investment program. Kama Ilovo anaweza akalima shamba, ana uwezo wa kutengeneza sukari, unanunua mtaji, unaweka hela kule kwa sababu yeye ana ile experience. Tukiamua kufanya wenyewe, muwe na hakika tutakuja kuulizana hapa siku moja. Tuko tayari kuzibeba losses hizo? Kwa sababu, biashara ina faida na losses. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho ni mabenki yetu. Nawaomba sana, suala hili la Financial Sector tuwe waangalifu sana. Quarter ya pili, karibu benki 15 zime-provide loses. Majibu tunayopewa inawezekana ni majibu sahihi, lakini twende mbali zaidi tujiulize: Je, ni sahihi kwa uchumi wetu? Money supply kwenye market imepungua. Mwaka jana 2016 ni 4.6% wakati mwaka uliopita 2015 money supply ilikuwa almost 14.6%. Maana yake ni nini? Hela imetoka kwenye money supply. Kwa hiyo, hii ni shida. Lazima uchumi uende unaongeza, unatoa, unapunguza, then ndiyo tuta-stabilise.
Mheshimiwa Mwenyekiti, najua wanafanya kazi nzuri sana. Kamati imetuletea mapendekezo mazuri sana; ni matarajio yangu kwamba mapendekezo haya Serikali itaenda kuyafanyia kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalize kwa kusema, nawaombeni watu wa Hazina twendeni tukafanye analysis proper kuhusu deni la Taifa. Tusiposimamia deni hili, muwe na hakika mtakusanya kwa juhudi kubwa, hela yote inakuja inakwenda kulipa deni, maana kulipa ni lazima. Tunasema tunaenda kwenye miundombinu, tumekopa madeni haya yanakwenda kwenye miundombinu, sawa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, umeme, bandari, baadhi ya barabara, naomba tuweke private sector wafanye. Hata viwanja vya ndege. Private Sector ndiyo inayoleta biashara. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana watu wa Wizara ya Fedha, ni dhambi sana kujivunia kufunga biashara. Serikali serious, huwezi kusimama unasema nafurahi biashara zaidi ya 2000 zimefungwa. Hili siyo jambo la kusema. Tafadhalini sana wenzangu! Kama kweli Serikali you are serious, Waziri wa Fedha unasema mwaka 2016 tumefunga biashara 2000 ni jambo la kujisifia, hili siyo jambo la kujisifia hata kidogo, tunyamaze. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, shughuli ya Serikali, shughuli ya Watu wa Wizara ya Fedha ni kusaidia biashara zianzishwe nyingi zaidi kwa sababu, biashara zikianzishwa nyingi zaidi maana yake ni ajira, maana yake kodi itaongezeka, maana yake maisha ya watu yataboreka. Kama kweli, mnataka tukae hapa tunasema wale tumewafungia maana walikuwa wanakwepa kodi, mtu wa kodi unamwita, una-negotiate naye unamwambia bwana wewe nakudai. Sasa nitakukata mwakani. Mna-negotiate! Ndio kazi ya taxation! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naombeni watu wa tax, kazi ya kukusanya kodi ni sayansi of its own. Haiwezi kuwa kazi yetu ni kufunga biashara, ni kuwashtaki, hapana! Ukifunga biashara zote, kitakachotokea ni nini? Wewe utapata kodi?Hatutapata.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono mapendekezo yaliyoletwa na Kamati ya Bajeti.
Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. PETER J. SERUKAMBA – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba niwashukuru Waheshimiwa Wabunge wote kwa kuchangia hoja yetu ya Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Wabunge waliochangia kwa kusema humu Bungeni Wabunge 32 na Wabunge waliochangia kwa maandishi ni Wabunge 20. Kwa kweli wote waliochangia, waliochangia humu ndani wamekubali mapendekezo yetu na wote ukiangalia wameeleza, walikuwa wanachangia kule ambako sisi tumeweka haya mapendekezo kama Kamati.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mambo ambayo ningependa kulitambulisha Bunge lako, ni muhimu sana tulifahamu mwanzo kabisa. La kwanza, Waheshimiwa Wabunge, Tanzania sensa ya mwaka 2012 ilisema kama Taifa tunakuwa kwa 2.7 percent, sasa maana yake tunaongeza Watanzania wenzetu karibia milioni mbili kwenye population yetu. Unaposema hivyo maana yake gharama za afya lazima ziongezeke, lazima gharama za education ziongezeke, sasa hii ndiyo changamoto tuliyonayo na changamoto yetu hii kubwa ni ya kifedha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili ambalo Wabunge wengi sana wamesema na wote waliochangia humu walikuwa wanaongelea matatizo yaliyopo kwenye zahanati, kwenye vituo vya afya, kwenye hospitali za wilaya, matatizo yalipo kwenye shule za msingi, yaliyopo kwenye shule za sekondari. Moja ya mapendekezo yetu tuliyotoa kama Kamati na ninaomba Waheshimiwa Wabunge tuitafakari upya, tuangalie mfumo wetu wa D by D. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge wote waliosema, zaidi ya asilimia 80 tulikuwa tunaongea mambo ya TAMISEMI, hatukuongelea sana mambo ya Waziri wa Afya, mambo mengi ya Waziri wa Elimu. Lakini kwenye Kamati yetu wanaokuja mbele ya Kamati yetu ni Waziri wa Afya; Waziri wa Elimu na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, lakini wanaoshughulika na utendaji wa kila siku wako TAMISEMI. Wanafunzi wakifeli sana tunasema Waziri wa Elimu hatoshi, lakini Waziri wa Elimu anaishia kwenye sera; walimu wanafundishaje, wanaajiriwaje, whether kuna madarasa, whether kuna chaki, hazipo, yeye Waziri wa Elimu hajui. Vituo vya afya vinasimamiwa na Halmashauri zetu, kukitokea leo ugonjwa mkubwa watu wakafa au madaktari, tutahangaika na Waziri wa Afya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge, kwa nini nasema hili, nataka kama Bunge tutafakari upya mfumo wetu wa kutoa elimu na afya nchini. Ni nia ya Serikali kuhakikisha kila kituo cha afya kina daktari, kina theatre ili tuweze kupunguza vifo vya akina mama na watoto. Lakini anayewaajiri hao ni nani, yuko TAMISEMI. Pendekezo letu linasema na ninaomba Waheshimiwa Wabunge mtuunge mkono kwamba umefika wakati sasa watakapokuja mbele ya Kamati, Wizara ya Afya aje na mtu wa TAMISEMI, kama ni Wizara ya Elimu aje na mtu wa TAMISEMI ili matatizo yale tuwe tuna watu wawili ambao mmoja anashughulika nayo kisera na mwingine anashughulika nayo kwenye utekelezaji. Mimi hili naliona ni tatizo ambalo lazima tulipatie majawabu na wanaoweza kutoa majawabu hayo ni sisi Waheshimiwa Wabunge, naombeni tutekeleze wajibu wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya hilo ambalo mimi niliona ni la kijumla zaidi, na mimi kwangu hili ndiyo tatizo ninaloliona zaidi, nilikuwa namsikiliza dada yangu Mheshimiwa Jacqueline, anaongea mambo ya Tunduru, lakini yote anaongelea kituo chake cha zahanati, anaongelea kituo chake cha afya, anaongelea hospitali yake ya Wilaya, lakini kwa kweli aliyekuwa anamwambia sio kwenye Kamati yetu, alikuwa anamwambia mtu wa TAMISEMI, na watu wengi ambao wameongea humu ndani wameongea mambo yanayotokea kwenye Wilaya zao. Kwa hiyo ni muhimu sasa tuuangalie mfumo wetu upya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo ya mfumo, nilitaka niongee suala la ufaulu kwenye shule za sekondari kwa sababu sisi huko tumelisema ili tuone tunaendaje kwenye suala la ufaulu. Nikisema suala la ufaulu nitaomba niunganishe na shule za binafsi na za umma, na katika mapendekezo yetu tumesema kuhusu shule za binafsi na za umma.
Waheshimiwa Wabunge, kwa wale ambao wamefuatilia matokeo ya form four haya yametoka juzi; Ukihesabu shule ya kwanza mpaka ya 200, shule za umma ni shule 17 tu. Ukichukua shule ya kwanza mpaka ya 100, shule za umma ni shule saba. Hili ni tatizo lazima tutafute ufumbuzi. Kwa hiyo, niwaombe sana Waheshimiwa Wabunge na hili linatokea na mimi ninasema ni muhimu sana sasa Wizara ya Elimu, shule hizi za binafsi pamoja na kwamba wanafanya biashara lakini wanatusaidia Watanzania.(Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunalo jukumu kama Bunge ya tuhakikishe zinatoa elimu bora. Waziri amesimama hapa anasema; shule ya Feza haina wanafunzi wengi, akailinganisha na shule ya Kibaha yenye wanafunzi wengi, ukilinganisha hivyo yes, lakini tumekuwa na seminari zina wanafunzi 40 zinaongoza miaka yote. Hoja yetu hapa, naombeni kama Bunge tuhakikishe tunatenga fedha nyingi ili shule za umma ziwe na fedha waweze kusimamia ili tuweze kupata ubora kwenye shule zetu za sekondari.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwahiyo niwaombe Watu wa Wizara ya Elimu kwenye moja ya pendekezo letu, tunaomba Wizara ya Elimu wajikite kwenye kuhakikisha tunapata ubora kwenye Shule zetu za umma. Na mimi hapa Waheshimiwa Wabunge mnikubalie na Kamati yangu, nimpongeze sana Rais Magufuli kwa kuamua kuleta elimu bure. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ameleta elimu bure maana yake nikusaidia watoto wa maskini, wale wasio na uwezo. Sasa niwaombe watu wa Wizara ya Elimu tuhakikishe tunaboresha hizo sekondari zetu. Ikitokea sasa mzazi ameamua kuacha shule ya bure ameenda shule ya kulipia hilo ni tatizo lake. Haiwezekani sisi tuanze sasa kusema, shule za kulipia tuwapangie school fees, hapana. Sisi ndiyo maana kama Serikali nadhani mliangalia busara ya hali ya maisha ya watu mmesema shule zetu ni za bure. Hapa kuna mzazi ameamua kuacha shule ya bure ameamua kupeleka mtoto kwenye shule ya kulipia tumuache alipe anavyoweza kwasababu ni maamuzi yake. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitaka niongelee suala la afya. Wizara ya Afya Wabunge wengi sana wameongelea suala la dawa. Waheshimiwa Wabunge kwanza niipongeze Serikali na sisi Kamati tumeipongeza sana. Ukiangalia bajeti ya mwaka huu iliyowekwa kwa ajili ya dawa, ndugu zangu tukubaliane kama Bunge tuwapongeze Serikali bajeti ni kubwa sana. Challenge ambayo nawapa watu wa Wizara ya Afya na Wizara ya Fedha, Wizara ya Fedha, fedha mnajua mtawapa na tunapeleka shilingi bilioni 20 kila mwezi kwa sababu dawa lazima kuna process ya kuyanunua, naiomba Serikali hasa Waziri wa Fedha, tuna mifuko yetu ya jamii tunapoanza mwaka tuiombe iipe pesa kule MSD wanunue dawa, lakini kila mwezi wanapoleta disbursement yao iende kurudisha hela kwenye Mifuko ya Jamii maana yake ni nini? Tutakuwa tumetatua tatizo la uwepo wa dawa ili ziende kwa wakati na kwa jinsi hiyo tutaonekana tumefanya kazi kubwa sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, na hapo tunarudi kwenye dawa ni pale pale sasa TAMISEMI kuna dawa nyingine wananunua wenyewe Waziri wa Afya hajui kwahiyo yeye atakapo report ata-report hali ya dawa ambayo yeye ni custodian wake lakini kule TAMISEMI wanaweza wakanunua bila kumwambia Waziri wa Afya, kwa hiyo, cha msingi hii mifumo tuiunganishe ili tuweze kujua hali halisi ya dawa nchini. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, vifaa tiba na niwaombe sana Waheshimiwa Wabunge, najua hili Serikali linakigugumizi nalo sana, lakini niwaombe sana Serikali dunia ya leo hatuwezi kununua vifaa vyote kwenye hospitali zote, hatuwezi. Ziko taasisi kubwa duniani watakuja hapa, wataleta vifaa tiba, watafunga kwenye hospitali zote, wataviendesha lakini sisi tusimamie wasitoze bei kubwa. Teknolojia ikibadilika watabadilisha wao. Lakini sisi tukisema lazima tununue safari yetu ya kwenda kila Mkoa tutatumia miaka mingi sana kwa sababu vifaa hivi ni bei ghali sana. Niwaombe Serikali imefika wakati twende kwenye PPP kwa ajili ya kupata hizi mashine kubwa na ambazo advantage zake ni tatu; moja ni unahakika utapata the latest technology; pili, teknolojia ikipitwa na wakati watabadilisha na tatu, watu wetu watapata huduma bora zaidi kwa sababu watu hawa watakuja na watu wa kuviendesha vyombo hivyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani hili ni suala la Serikali naomba muende mkalisimamie ili tuone namna ambavyo tunaweza tukafanikiwa katika mambo yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ambalo tumelitolea kama Kamati ni suala la Bima ya Afya. Bima ya Afya ni jambo jema sana lakini inaumiza sisi Wabunge una kadi ya Bima ya Afya eti hapa Tanzania tu kuna hospitali hawapokei Bima ya Afya, haiwezekani.
Mimi ni matarajio yangu Serikali sasa muende mkaliangalie angalau tunapokwenda kwenye universal coverage, lakini hata hii iliyopo ya kwanza iwe na maana kwa maana kwamba popote nitakapoenda hawataniambia kadi hii siipokei. Kama suala ni fedha muongeze ili wanaochangia wachangie fedha nyingi, lakini waweze kupata huduma bora zaidi na muanze kufikiria suala la kwenda mpaka huko kwa Afrika ya Mashariki. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ambalo Waheshimiwa Wabunge mmelichangia kwa nguvu zote ni suala la mikopo wa elimu ya juu. Waheshimiwa Wabunge sisi Kama Kamati tumesema kuhusu namna bora ya kuangalia kuhusu suala la mikopo ya elimu ya juu. Moja ya jambo ambalo tumesema lakini hakuna Mbunge ambaye alili-pick up, lakini mimi naona kwetu ni muhimu sana; suala la kuanzisha scholarship program.
Waheshimiwa Wabunge, nchi zote wanaotuzunguka kuna scholarship program, ikiwezekana tuiite Magufuli Scholarship Program ili wale watoto ambao wamefaulu sana form six awe mtoto wa tajiri, awe mtoto wa maskini lakini ni mtoto ambaye ana kipaji, amefaulu sana kwenye yale maeneo ya vipaumbele watoto hawa wapewe scholarship.
Mheshimiwa Mwenyekiti, itasaidia kuonyesha kwamba hatujawabagua. Kwa hiyo wale watoto ambao wamepata point tatu, mtoto amepata point nne kwenye PCM hata kama ni mtoto wa nani ni muhimu sana Serikali iangalie uwezo wa kuanzisha scholarship program. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa suala la vigezo; naomba sana watu wa Wizara ya Elimu, vigezo vya mikopo visibadilishwe badilishwe. Maneno mengine yanaletwa kwa sababu kila mwaka kuna vigezo vyake. Ni vizuri vigezo viwe vinajulikana, vikishajulikana ni rahisi lakini ukishaanzisha na scholarship program itasaidia sana kwa wale watoto ambao wamefanya vizuri zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu madai ya walimu; tumesema hapa ndani, tunaomba sana Wizara ya Elimu, Wizara ya TAMISEMI na hili naomba Waziri Mkuu wewe upo hapa ikiwezekana Waziri Mkuu watu hawa wawili wakae, vyombo hivi viwili ama vitatu; Chama cha Walimu, TAMISEMI pamoja na Wizara ya Elimu tukae tulijadili suala la madai ya walimu ili tujue madai ya walimu kiukweli ni kiasi gani, yahakikiwe, tusiwe na figure mbili mbili na baadaye sasa Serikali kadri itakavyokuwa na uwezo iweze kuwalipa hao walimu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hayo ndiyo mambo mengi ambayo Waheshimiwa Wabunge kwa suala la Wizara ya Afya na Elimu wameyasema sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mengine ni suala la ugonjwa wa saratani ambalo kwa kweli wengi wamelisema, ndugu zangu tukubaliane ugonjwa huu unakuja kwa kasi sana. Tumeweka kwenye pendekezo letu, tuombe sasa Serikali ianze kuwekeza fedha nyingi kwa ajili ya kutatua tatizo hili. Ni ugonjwa mkubwa, ugonjwa unaotumia fedha nyingi lakini hatuna choice lazima tuhangaike kuwasaidia Watanzania hawa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, TBC; Waheshimiwa Wabunge wamesema kwa kweli chombo chetu cha TBC ndugu zangu Wabunge naomba mniunge mkono kwenye bajeti ijayo tuhakikishe wanapata fedha za kutosha ili angalau TBC waweze kusikika kwenye Wilaya zote Tanzania, redio yetu ya Taifa iweze kusikika kwenye Wilaya zote za Tanzania maana kupata habari ni jambo muhimu sana kama Taifa. Naombeni tuungane mkono ili tuweze kupata bajeti ili waweze kufanya vizuri. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ambalo Waheshimiwa Wabunge wamelisemea ambalo ni kupongeza kuhusu Muswada wa Habari lakini kikubwa zaidi, Mheshimiwa Devotha Minja anasema suala la diploma katika uandishi wa habari kwamba sasa kuweka kigezo cha uandishi wa habari lazima awe na elimu kwanza ya diploma Mheshimiwa Devotha anasema ni jambo kubwa hili na ni jambo jema anaamini safari yetu ya kuleta weledi kwenye uandishi wa habari Tanzania tunaanza kuelekea huko. Tunaipongeza Serikali, tunaomba tutekeleze.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho ni suala la michezo; Mheshimiwa Kadutu anasema, ili tuweze na sisi kushangilia kwenye Michezo hatuna shortcut lazima tuwekeze. Tuwekeze kuanzia kindergarten mpaka watoto wanapopanda huku juu; na ili tuweze kupata mafanikio hayo ambayo tunayataka lazima tuwekeze na kwa kweli ndugu zangu michezo ni ajira. Tukifanikiwa kama nchi na sisi tukafika wakati ambapo tutakuwa tunatoa Watanzania wasiopungua hata wanne, watano kwenda kucheza Kimataifa maana yake tutakuwa tumesaidia sana kwa vijana wetu na fedha zile zitakuja kwenye uchumi wetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho ni suala la mfumo wa Elimu. Waheshimiwa Wabunge wamelisema sana na sisi kwenye pendekezo letu tumesema tunaomba sasa Serikali iende ikakae, ikaungalie mfumo wetu wa elimu ili wautatue tutakapokuja kukutana baadaye watuambie wamefanya nini, kwa sababau matatizo haya tusipoyaangalia kwa upana, hatuwezi kuyatatua vizuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo Waheshimiwa Wabunge naomba sasa niweze kutoa hoja ili Bunge lako tukufu liweze kupitisha mapendekezo yetu yote ya Kamati, naomba kutoa hoja Waheshimiwa Wabunge.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nashukuru kwa kunipa nafasi kuchangia bajeti ya Wizara ya Kilimo. Leo ni mara yangu ya kwanza nachangia bajeti, naomba na mimi nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa anayofanya ya kurudisha nidhamu Serikalini. Nina hakika sasa tunaenda kwenye mstari ulionyooka na Taifa letu litaanza kushuhudia maendeleo kwa kasi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, niwashukuru wananchi wa Mkoa wa Kigoma hasa Kata ya Kigoma Kaskazini kwa heshima kubwa waliyonipa kunirudisha Bungeni kama Mbunge wao. Nina hakika sitawaangusha, ahsanteni sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ambalo napenda kuliongelea ni kahawa. Pale Kigoma Kaskazini tunalima kahawa hasa maeneo ya Kalinzi pamoja na Nyarubanda kwenda mpaka Buhigwe, Manyovu wanalima kahawa aina ya organic coffee. Zaidi ya wakulima 435 walichukuliwa kahawa yao, imepelekwa Kilimanjaro kwa ajili ya kubanguliwa mpaka leo hawajapata fedha zao. Nataka Waziri aje aniambie lini wananchi hawa watapata malipo yao hayo ambayo yamekaa muda mrefu sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili kwenye kahawa tatizo ni tozo. Kwenye mazao yetu tozo za wakulima ni kubwa sana na bei ya kahawa duniani imeshuka. Kwa hiyo, lazima Serikali tujipange kwa sababu bei hatuwezi ku-control lakini tozo tunaweza ku-control ili wakulima wetu waweze kupata mazao na waweze kulima na kufaidika. Kwa sababu nia yetu ni kuondoa umaskini, bei kwenye soko la kahawa hatuwezi kuisimamia kwa sababu ni suala la demand and supply, wenzetu Brazil wanaleta kahawa nyingi sana, namna ya kuwasaidia hawa wakulima wa Tanzania ni kupunguza tozo kwenye zao la kahawa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sekta ya kilimo inaendelea kushuka katika ukuaji. Mwaka 2015 kilimo kimeshuka kwa asilimia 2.3 ambapo mwaka 2014 ilikuwa asilimia 3.4 maana yake ni nini? Kama kilimo ambacho ndiyo kinabeba watu asilimia 75 ukuaji unashuka lazima tujiulize tunafanya nini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimuombe sana Waziri tuanze na tukubali kwamba kwa asilimia 90 kilimo ni sayansi na sio juhudi. Kama ni juhudi mama yangu amelima toka nazaliwa kwa juhudi kila mwaka lakini hajawahi kujitosheleza kwenye chakula. Kama kilimo ni sayansi maana yake ni uwekezaji. Kuna Abuja declaration lazima asilimia 10 ya bajeti yetu iende kwenye kilimo kama tulivyokubaliana kwenye Azimio la Abuja. Naomba sana Waziri na Serikali tuende kule ambapo tulikubaliana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kilimo ni sayansi tunahitaji uwekezaji, hatujapata fedha tunafanyaje kama Taifa. Lazima nimuombe Waziri tuanze sasa kuleta commercial farming in Tanzania. Tukileta commercial farming tunaunganisha na out growers. Tumeona Kilombero kuna baadhi ya maeneo unaona maisha ya watu yamebadilika kwa sababu kuna commercial farming pale na kuna wakulima wadogo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wale commercial farmer’s watakachofanya watakuja na mbegu zao, watafanya utafiti wenyewe, watatafuta wagani, hawatahitaji tuwape mbolea wala ruzuku. Kama Taifa ili tuweze kufanikiwa niombe sana tuhakikishe angalau kila mkoa tuwe na commercial farming kubwa ndiyo itawasaidia wakulima wetu wadogo wadogo. Tunaona kila mwaka tunaanza kuhangaika na mbolea na ruzuku umefika wakati wa kuleta commercial farming. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ili commercial farming Tanzania iweze kufanikiwa mambo mawili yafanyike, kwanza, ni umilikaji wa ardhi, lazima tuziangalie upya sheria zetu za ardhi. Pili, ni kuangalia namna ya kuwasaidia hawa wakulima kuweka incentive ili watu waende kwenye ukulima. Kwa sababu hiyo, tutaweza kupata malighafi kwa ajili ya viwanda vyetu. Commercial farming wataweza kufanya value addition, pia watatafuta masoko lakini tusipofanya yote haya tutasema tuna mavuno makubwa lakini wakulima wetu hayo mazao yao hawawezi kuuza popote. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la mkonge, sasa hivi duniani mkonge umepanda bei sana. Tani moja ya singa ya mkonge ni dola 2500, hata ukiondoa gharama za kuzalisha hiyo tani moja hazizidi dola 1,000 kuna faida zaidi ya dola 1,500. Leo watu wanakuja kununua mkonge shambani, wanalipa pesa in advance. Niiombe Serikali na Waziri wa Kilimo sasa hivi tuhangaike kuhakikisha kila shamba ambalo linaweza kulima mkonge tupande mkonge. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tukipanda mkonge tutapata fedha za kigeni, tutaajiri watu wengi sana kwenye kiliomo kwa sababu mkonge unahitaji watu wengi sana kwenye yale mashamba, lakini hauhitaji mvua, ni kitu rahisi kulima. Ukisoma hapa hotuba ya Wizara ya Kilimo suala la mkonge limetajwa paragraph moja tu wakati ndiyo zao ambalo leo lingeleta pesa nyingi kuliko zao lolote Tanzania. Zao la mkonge ukishaondoa singa yale yaliyobaki yote unaweza ukaanzisha viwanda vya kutengeneza tikira kwa ajili ya pombe, syrup kwa ajili ya wangonjwa wa sukari, kwa ajili ya umeme, kwa ajili ya mbolea haya yote yanawezekana kama tutajielekeza kwenye suala la mkonge. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee mifugo, hapa ni masikitiko makubwa. Ukisoma hotuba ya Waziri katika mifugo anaongelea majosho, dawa, migogoro ya wakulima na wafugaji. Kama kuna jambo ambalo tukiamua kufanya tutabadilisha nchi hii kimaendeleo ni suala la mifugo. Mifugo tusiione ni dhambi. Leo hii ukitaka kujua thamani ya mifugo hebu fikirieni kama Taifa tungekuwa hatuna mifugo ingekuwaje? Leo ingekuwa Tanzania hakuna ng‟ombe, kuku wala mbuzi Taifa hili lingekuwaje, mngetumia mabilioni ya pesa kuagiza nyama duniani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hii biashara ya nyama ili ziweze kufanikiwa naombeni kama Serikali tuanzishe National Abattoir kubwa na kama Serikali haiwezi tutafute private sector waanzishe National Abattoir kubwa ambayo kazi yake itakuwa ni kuchinja mifugo na kusambaza nyama nchini na kuuza nje ya nchi na kuchukua zile ngozi kuwapelekea wenye viwanda vya ngozi. Kazi nyingine wawepo watu katikati wafugaji ambao watafanya kazi ya kunenepesha ng‟ombe, hiyo ndiyo itakuwa kazi yao. Kwa kufanya hivyo chain ya biashara ya mifugo itakuwa kubwa sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la NFRA, kila mwaka tunatafuta kuongeza hela kwa ajili ya strategic reserve. Sasa imefika wakati tuanzishe private sector ambao na wao watanunua mazao ya wakulima wetu. Ikitokea leo mavuno ni wengi hakuna mnunuzi wa mahindi yao kwa sababu mnunuzi ni mmoja. Kwa hiyo, tutafute mtu mwingine ambaye anaweza akafanya biashara hiyo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho uvuvi, mnaenda mnawachomea nyavu wavuvi wetu wa Kigoma, Lake Victoria, Lake Nyasa, swali langu ni moja naomba Waziri atujibu nyavu hizo zinatoka wapi? Kwa nini nyavu hizo wasizizuie toka kiwandani? Nyavu zinazalishwa viwandani au zinakuwa imported wanauziwa wavuvi wetu ndiyo mnakwenda kuwakamata mnawachomea, hapana. Naomba Mheshimiwa Waziri mpige marufuku kuleta nyavu hizo, mpige marufuku kuzalishwa na hiyo ndio itaondoa suala hili la nyavu mbaya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho ni tumbaku, naomba tupunguze tozo kwenye zao hili. Pia wakulima wangu wa kule Matendo, Kidaghwe anayekuja kununua tumbaku ni mtu mmoja anapanga bei anayotaka matokeo yake wakulima wetu wanaendelea kuwa maskini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naomba nimalizie kwa kusema naunga mkono bajeti lakini naomba Serikali ijielekeze kwenye kuamini bila sayansi kilimo hakiwezi kuondoka hapa. Hata tukisema kilimo ndiyo uchumi, ni mgongo wa Taifa, mali ipo shambani kama huweki sayansi yatakuwa maneno matupu, hatuwezi kwenda tunakotakiwa kwenda. Zama hizi ni za mabadiliko, naombeni tubadilike, tuamini kulima ni sayansi, bila sayansi hatuwezi kwenda tunapotaka kwenda. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naomba kuunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia Wizara hii muhimu sana. Kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Waziri Kitwanga kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya ndani ya nchi yetu. Tumeziona juhudi zako za kupambana na ujambazi, madawa ya kulevya, kusafisha pale Uhamiaji, Waziri Kitwanga endelea na kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo nimekishangaa sana Kiti chako kwa sababu, labda Kanuni zinawezekana zimebadilika. Wenzetu wa upinzani walipewa nafasi ya kutoa maoni ya upinzani. Wameamua wenyewe kwa mapenzi yao, kuondoa hotuba yao mezani. (Kicheko/Makofi/Kelele)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa wale ambao hili Bunge wanalifahamu, hii siyo mara ya kwanza, Wapinzani kuambiwa kutoa maneno wakatoa. Hii siyo mara ya kwanza! Mheshimiwa Tundu Lissu aliwahi kuleta wakati wa bajeti, miaka mitano iliyopita, akaambiwa maneno haya hayafai na kwa sababu ni muungwana akaenda kuyatoa akaja akasoma speech yake. Leo kwa sababu wanayoyasema kwanza hawayaamini, hawana uhakika nayo, ndiyo maana hawawezi kuyatoa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, na sisi ngoja tuseme suala la Lugumi.
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti…
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichukue nafasi hii nimpongeze sana Mwenyekiti wa Kamati ya PAC kwa kazi kubwa anayoifanya. Mambo mengine yalikuwepo huko nyuma, kuanzia mwaka 2011 hakuna aliyeyaona; mwaka 2012, hayakuonekana; 2013 hayakuonekana; 2015 hayakuonekana. Hayakuonekana kwa sababu Kamati hizo waliokuwa wanaongoza wanafahamika. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti…
nimepewa na mdogo wangu, kwa bahati mbaya leo naikataa kwa sababu angesubiri nimalize angeweza kunisikiliza vizuri. (Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Aeshi amefanya kazi kubwa sana kwenye Bunge hili. Amechukua hatua, jambo analifanyia kazi, Kamati zinazunguka nchini kufanya kazi. Sasa leo anapokuja mtu mwingine, anasema amekuja na maswali, ningetamani niyasikie. Maswali hayo, huyu mtu anawahisha shughuli na inawezekana nia yake siyo njema. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaposema nia ni kuisimamia Serikali, Serikali inasimamiwa kwa utaratibu. Wengine inawezekana wamekuja jana ndiyo maana hata heshima ya Kiti hawaijui. Upande wa CCM watu wameongea hakuna watu waliokuwa wanazomea; lakini kwa sababu ya ugeni, mnadhani mkizomea mnafanikiwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ya Aeshi inafanya kazi, tuiache ifanye kazi. Nakuomba Mheshimiwa Waziri, ukiona adui yako anasema anakupenda, ujue huyo ndiyo mbaya wako. Maana kama mtu mmekwenda mmealikana, mmekula chakula, wakati mnaalikana hamkutuambia, lakini mnavyokuja leo mbele ya Bunge hili kusema mliyoyaongea, siyo mapenzi hayo! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri endelea na kazi na bahati njema yote yanayosemwa, kwa namna yoyote ile huhusiki na hili Bunge litasimama kwenye haki. (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichukue nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Rais Magufuli… (Kicheko/Makofi)
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba unilinde..
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana nichukue nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa anayofanya nchini. Mheshimiwa Rais anarudisha discipline ndani ya nchi yetu, anasimamia mapato ya nchi yetu, kazi hii kubwa anayoifanya siyo wengi wangependa, lazima waumie. Naomba tumpe moyo, aendelee kufanya kazi ili apeleke nchi yetu kule tunakotaka iende. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niwapongeze Polisi wa nchi yetu. Jeshi la Polisi linafanya kazi kubwa sana. Nchi yetu leo ina amani kwa sababu vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinafanya kazi, vinaheshimika sana duniani. Hakuna jambo la hovyo kama tunavyokutana kama Bunge, tunaanza kukejeli vyombo vyetu vya ulinzi vinavyofanya kazi nchi hii. (Makofi/Kelele)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nawapongeza sana watu wa uhamiaji kwa kazi. Leo hii ukiwa unataka kuomba passport utaipata baada ya muda mfupi sana, hili ni jambo jema, naomba liendelee. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia maslahi ya vyombo vyetu vya ulinzi na usalama yaangaliwe upya ili maslahi yao yaongezwe. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naomba niunge mkono hoja. Mheshimiwa Waziri Kitwanga endelea kufanya kazi, Bunge hili linakuamini na tuna hakika utatupeleka tunakotaka kwenda. Naunga mkono hoja hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nashukuru kwa kunipa nafasi. Moja ni suala la Ubalozi huko tuliko kwenye viwanja vyetu. Nikuombe Mheshimiwa Waziri, viwanja maeneo mazuri Nairobi; ukienda nyumba yetu pale London; ukienda Sweden; kote ninaamini tukiweka uwekezaji tutapata fedha za kuendesha Balozi zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, nampongeza Mheshimiwa Waziri kwa suala la kufungua Ubalozi na watu wa Israel na tumeona faida zake, sasa tumeanza kupata watu wanakuja kutalii kutoka Israel. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la tatu, niwaombe sana Waheshimiwa Wabunge, mimi kama mwanasiasa, ukiona mtu ambaye ni adui yako umefanya jambo akakusifia, ujue liko tatizo. Ukiona umefanya jambo adui yako akasema umekosea, maana yake umepatia sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili ni Taifa. Nami naomba sana nimpongeze Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa aliyofanya. Niwambie Waheshimiwa Wabunge, naomba niwambie duniani kote, extractive industry inaenda kubadilika na atakayekuwa kwenye historia amebadilisha extractive industry ni Mheshimiwa Rais Magufuli. Leo duniani kote, kwenye kila mgodi mambo yatabadilika kwa sababu sasa ilikuwa ni vitu vinatengenezwa, mnaambiwa kuna tatizo, lakini sasa amefungua mlango. Nina hakika kila ambako kuna extractive industry, mambo yatabadilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwambieni Watanzania tusiogope. Kwenye hili lazima kama nchi tuwe nyuma ya Mheshimiwa Rais, tumuunge mkono aendelee. Ninayo hakika wawekezaji watakuja mezani. Wakati fulani ili watu waje mezani lazima na pa kuanzia. Kama ni suala la ku-negotiate, ume-negotiate toka mwaka 1999, hatujapata vya kutosha. Nadhani umefika wakati, hii ndiyo ilikuwa njia ya kuleta haya mabadiliko ambayo nina hakika tutayapata kama Taifa.

Mimi niwaombe sana Waheshimiwa Wabunge, tumuunge mkono Mheshimiwa Rais, huu siyo wakati wa kutupiana maneno.

Ni wakati wa kufikiri. Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru umenipa nafasi nichangie mpango huu. Nimekuja na mipango mitatu, nimekuja na Mpango wa mwaka 2016/2017; 2017/2018 na 2018/2019.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naanza na Deni la Taifa. Kwenye Mpango wa 2016/2017 tuliambiwa ilipofika Oktoba, 2015, Deni la Taifa lilikuwa dola bilioni 19 ikilinganishwa na dola bilioni 18 za mwezi Oktoba, 2014. Tulipokuja Mpango 2017/2018, tukaambiwa Deni la Taifa limekua dola bilioni 18, ongezeko la asilimia 9.76. Sasa mwaka uliopita ilikuwa bilioni 19, mwaka unaofuata tunaambiwa ni bilioni 18, lakini kuna ongezeko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hawakuishia hapo, wanasema ongezeko hili wanalinganisha na dola bilioni 16 za kipindi cha 2015. Kwenye mpango huu wa mwanzo wanasema Oktoba ilikuwa bilioni 19, kwenye mpango huu wa pili wanasema Oktoba ilikuwa bilioni 16. Sasa kwenye mpango huu mpya wanasema Deni la Taifa limefika bilioni 26 ukilinganisha na Dola bilioni 22 za mwaka 2016 Juni, lakini kwenye ripoti ya Juni tunaambiwa dola bilioni 19.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, moja ya tatizo tunalo hapa ni data hizi zinazoletwa na Wizara ya Fedha. Data ni za kwao haiwezekani tukawa na fatal mistakes za zaidi ya Dola bilioni tatu, jamani hatusomi documents hizi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, maana yake ni nini ninachotaka kusema, ukiangalia mipango yote mitatu kwa kweli, ni copy and paste. Ukipitia yote wamebadilisha language, kinachosemwa ni kile kile. Kwa hiyo, hapa tunapanga, lakini ni kwa sababu, ni Katiba lazima tupange, yanayokwenda kufanyika wao wanajua, Bunge lako haliyajui. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema deni la Taifa linapanda. Sasa hivi linapanda kwa trilioni nne kwa mwaka kulingana na ripoti za BOT. Maana yake ni nini? Maana yake tumeamua, kama Serikali kwamba, kila kitu kinafanywa na Serikali, hatuwezi kuendelea! Halipo Taifa duniani ambalo kila kitu wanajenga kwa fedha zao. Kwangu hata ukikopa ni fedha zako sina shida, ukikopa bado ni fedha zako. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wewe shahidi tumekwenda Moscow uwanja wa Moscow International unajengwa na mtu binafsi. Hivi humu ndani tunasema tutafanya PPP, ukitafuta miradi ya PPP haipo, Serikali hii haiamini katika private sector.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka Bunge hili tukubaliane Waziri wa Fedha atuambie Serikali hii haikubaliani na private sector kwa sababu mipango yake Mheshimiwa Waziri mwanzo mpaka mwisho haongelei private sector. Kama tumerudi kwenye ujamaa tuambiane wote tujue, lakini haiwezekani tunaimba ujamaa halafu tunataka matokeo ya Kibepari, haiwezekani! Hakuna katikati. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, soma mpango huu hakuna production. Hatuongelei kukuza tija, angalia kwenye kilimo, angalia mazao yote ya kilimo hakuna anayeongelea kukuza tija, maana nilitarajia wangesema mwaka huu tumezalisha tani fulani za mahindi, mwaka kesho ni tani fulani za mahindi, hakuna! Pamba hakuna, kahawa hakuna, tumbaku hakuna, korosho hakuna, sasa tunapanga nini? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli tunapanga vizuri sana, lakini mwisho wa siku ukiangalia mpango uliopita yale yale yamesemwa. Huku kwenye mipango yote wanasema wataweka fedha TIB, fedha hizo zisaidie ku-leverage kwenye miradi, toka wameanza kusema hawajaweka senti tano TIB. Naomba watusaidie mambo ambayo wanajua hawawezi kuyafanya wasiyaandike unless wanaamini Bunge halisomi documents hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda humu ndani utaona kabisa kwamba, kwa mfano leo tunaongelea bei ya mahindi. Naomba nikwambie bei ya mahindi kinachofanya bei imeshuka watu hawataki kusema, Zambia wameanzisha Commercial Farming, wamelima mahindi mengi sana sasa yanauzwa mpaka Somalia, kwa vyovyote hatuwezi ku- compete kwa sababu wao wanaongeza production, hatuongelei production, sisi tunahangaika kubanakubana, sasa mmegeuza ni uchumi wa kubana tu, leo tunaleta sheria hapa ya kubana! Hakuna anayeongelea kupanua! Hakuna. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, unaweza ukaanzisha kiwanda cha pamba una marobota 240,000 kwa mwaka. Bangladesh kiwanda kimoja kinatumia marobota milioni tano, leo tunaongelea viwanda vya pamba kwa marobota 240,000, tunamdanganya nani hapa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwonea huruma sana Mheshimiwa Rais anahangaika, lakini wenzake hawamwambii ukweli, mtanisamehe. Leo Rais anakwenda kuwaambia viwanda ndio vizalishe sukari, lakini tumesema hapa siku zote hakuna aliyetuelewa kwenye hili Bunge, lakini kwa sababu Rais amesema viwanda vitazalisha sasa.

Mheshimiwa Spika na Waheshimiwa Wabunge, twende kwenye records tumesema, waongezeeni maeneo walime. Ilovo waliomba maeneo wakanyimwa, Ilovo wameenda Zambia leo ni number two kwa sugar production in Africa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania ardhi tunayo ni over regulations ni over regulations. Humu ndani Waziri anaongelea kodi tu, haongelei kukuza biashara, anaongelea kukusanya kodi peke yake, tunakusanya kodi kwa nani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo mabenki yanakufa, mabenki yote yana-record less profit hata mabenki makubwa. Uchumi unaofanya vizuri unaangalia mambo haya mawili, performance ya banking industry na performance ya stock exchange. Go to Dar es Salaam turn over ya Stock Exchange Dar-es-Salaam imeshuka kutoka bilioni 20 mpaka bilioni mbili na no one is talking about 85 percent, Waziri wa Fedha hasemi wala sidhani kama ana interest na sioni yeyote mwenye interest na hili jambo, ni nini hii? Jamani hii nchi ni yetu wote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawaombeni, haiwezekani viwanja vya ndege tujenge kwa pesa, reli kwa pesa zetu, umeme kwa pesa zetu, barabara kwa pesa zetu, hivi sisi ni nani? Dunia yote imeenda kwenye private sector, the whole world! China kuna toll road, Malaysia kuna toll road, kokote unakokwenda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho ni mambo mawili, moja; tunaleta hapa sheria ambayo humu ndani hawajasema ya kuleta NASACO, unajua kwa sababu gani, tunaongelea Tanzania tuna-manage ma-container 600,000 Singapore wana-manage ma-container milioni 34. Badala ya kuongelea kuongeza mzigo, tuongeze ma-container yatoke laki sita yaende milioni nne hadi milioni tano, tunafikiria ku-regulate hayo, kulinda hizo hizo laki sita zetu, ni nini hii? Hakuna anayewaza kuongeza biashara, kuongeza production, hakuna! Soma mwanzo mpaka mwisho hatuongelei kukuza biashara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii ukienda kwenye mabenki kila kitu kimeshuka, everything. Naomba nikupe data mbili au tatu. Personal landing mwaka 2015 ilikuwa asilimia 25.5, leo ni asilimia nane. Trade 2015 ilifika asilimia
24.6 leo ni asilimia tisa. Manufacturing it was 30 percent, leo ni asilimia tatu. Hakuna anayesema, tunaona mambo ni mazuri, ukisema tutaanza kupewa majina. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mambo hayako sahihi kwa sababu moja tu, ukiangalia sababu yetu ni moja tu, mpango wetu wa mwaka huu ndiyo wa mwaka jana, ndiyo wa mwaka juzi na ndiyo wa mwaka unaokuja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana Bunge lako tuamue, tuiombe Serikali iseme sasa inataka ujamaa twende kwenye ujamaa per se, kama ni ubepari au uchumi wa soko tuende kwenye uchumi wa soko per se, short of that ukivichanganya hatuwezi kwenda kama Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho, nataka kusemea suala la Kigoma, REA. Alisema jana Mheshimiwa Obama, kinachoendelea REA leo kwa watu wa Kigoma ni dhambi. Kigoma tumepata mkandarasi amepewa kazi, ni Kigoma na Katavi, anataka kuanza CRB inakuja inasema huyu hafai. Hivi CRB Mikoa yote hamkuona umuhimu wa kuangalia procurement, mnaangalia kwa ajili ya Mkoa mmoja na kwenye Sheria ya Procurement CRB inakujaje? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sababu tunazijua, aliyekuwa anataka kazi ya Kigoma na Katavi ndiye Mwenyekiti wa CRB, ni conflict of interest na Mawaziri leo, Waziri Kamani hawezi kuamua ana kigugumizi, Waziri Mbarawa hawezi kuamua ana kigugumizi kwa sababu wote tunazijua. Watu wa Kigoma mnatuweka wapi, kwani sisi siyo Watanzania? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, unfortunate, hivi sisi ni nani? Nataka kusema suala la REA na suala la Kigoma kwenye REA III naombeni mfanye maamuzi. Kama suala labda kumpa huyo ambaye najua ni mpendwa ambaye yuko CRB, mpeni tufanye kazi, yule maskini mwenzetu ambaye alifanya REA II leo hamwoni wa maana mnyang’anyeni basi mpeni mnayemtaka ili twende watu wa Kigoma wasipate hasara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, lakini mipango yetu kwa kweli ni ya mwaka jana ndiyo ya mwaka juzi. Sielewi maana yake ni nini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017
MHE. PETER J. SERUKAMBA - MWENYEKITI KAMATI YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Nimesimama mbele ya Bunge lako Tukufu niweze kutoa baadhi ya maelezo na niweze kuhitimisha hoja yangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niwashukuru sana Waheshimiwa Wabunge, Wabunge waliochangia humu ndani kwa kuongea ni Wabunge 21 na Wabunge waliochangia kwa maandishi ni Wabunge 15. Nawashukuru sana mmefanya kazi kubwa ya kusaidia kuboresha report yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mambo makubwa yaliyoongelewa nitaomba nianze kwa sababu tuna Wizara tatu nitaanza na suala la Wizara ya Elimu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu ina mambo makubwa matatu:-
(1) Mitaala
(2) Ubora wa Elimu (quality assurance)
(3) Examiner (Mtahiniwa mwenyewe)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema haya kwa sababu kila Wabunge waliochangia hapa ndani wameeleza matatizo tuliyonayo kwenye elimu na sisi kwenye Kamati tumeeleza baadhi ya mambo ambayo tunayaona yapo kwenye elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upande wa mitaala maana yake huko utaongelea Walimu, majengo, vitabu, vifaa vya kufundishia, muda wa kusoma na wanafunzi wenyewe. Pia kwenye quality assurance ni suala la ukaguzi na baadaye tunakuja Baraza la mitihani ambalo kazi yake ni kutunga na kusahihisha mitihani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nimeanza na hili? Nimeanza na hili kwa sababu kwenye ripoti yetu tumeonesha hali ya ufaulu nchini Tanzania. Ukiangalia hali ya ufaulu kwa Tanzania kuanzia mwaka 2013, division one ilikuwa ni asilimia 2.8; mwaka 2014, division one ilikuwa asilimia 4.2; mwaka 2015; asilimia 3.0; 2016, asilimia 3.7; na 2017, asilimia 3.5.
(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia division two tulianza na asilimia 8.0; tukaja asilimia 14; tukaja 11 au 12 na sasa ni 14.9. Kwa hiyo, unachokiona kwa miaka hii yote, watoto wetu wanafaulu kwa division one mpaka three hawajawahi kuzidi asilimia 30.

Waheshimiwa Wabunge kwangu mimi hili ni kubwa sana, tunafanya nini sasa kama Taifa? Huko nyuma tulitoa maelezo sasa tuna shule za binafsi, tuna shule za Serikali. Kuna watu wamechangia hapa ukiangalia matokeo ya mwaka huu shule za Serikali katika shule 100 ni shule nne, naimi nataka nimpongeze sana Mheshimiwa Rais kwa kuleta elimu bure. Ameamua, ni uamuzi mkubwa kuleta elimu bure maana yake wazazi wa Tanzania wamepewa uchaguzi, wamepewa choice. Ukiwa mzazi una watoto wako, upande mmoja Serikali inasema zaa unavyoweza tutakusomeshea mpaka darasa la 12, upande mwingine una watoto wako unaweza ukasema mimi watoto wangu kwenye bure siendi nakwenda kuwasomesha kwa kuwalipia, ni choice Watanzania wamepewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa sisi Kamati tunataka tuiombe Wizara ya elimu, Wizara ya Elimu inaboresha shule zake ni jambo jema sana. Sasa kwa wale ambao wameamua wao wenyewe, kwa mapenzi yao kuwapeleka watoto wao kwenye shule za private, wakifika pale wanasainishwa mikataba kwamba bwana wewe umemleta mtoto wako hapa, masharti yetu sisi ni haya, mtoto wako asipofaulu kwa kiwango hiki hapandi darasa, lazima alipe school fees kiasi hiki. Sasa anakuja mtoto, wazazi watoto wake amefukuzwa tunakimbilia Wizara ya elimu kuomba msaada.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilidhani Wizara ya Elimu ingesema “Mzee mtoto wako amefukuzwa? Eeeh!, Lakini mbona tuna shule za bure kwa nini usimpeleke kwenye shule za bure?” Why tunataka tuwa-punish hawa wenye shule? Mtanisamehe kwa wale ambao walisoma seminary mimi nilisoma seminary. Seminary sisi tulianza 58, waliomaliza form four ni watu 23, maana yake ni nini? Ni choice, hujapata asilimia 50 hupandi darasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuangalie upande mwingine wa shilingi, wale ambao wanawasimamia hawa watoto ili wasome kwa bidii ndiyo hizi division one tunazoziona za asilimia tatu. Naomba Serikali hili tulitafakari kwa kina, naamini shule hizi zinasaidia Taifa letu. Sasa Serikali ifanye nini? I-set standard, ifanye monitoring, na ifanye followup, lakini Serikali isianze ku-supervise process ya hizi shule. Serikali ijishughulishe zaidi kwenye shule za Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wengi ambao wana umri wa miaka 40 kwenda juu, zamani ilikuwa usipofaulu kwenda shule ya sekondari unarudia ili uende ukasome shule ya Serikali kwa sababu shule za Serikali zilikuwa zinafanya vizuri. Zamani mtoto kwenda shule ya private ulikuwa unachekwa kijijini kwamba wewe huna akili, lakini hali imebadilika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niiombe Serikali ni muhimu sana kwenye suala la elimu mfanye consultations na hao wenye shule ili kutatua matatizo badala ya kutunishiana misuli ya kuandika waraka kama barua. Nataka niiombe sana Serikali kwenye jambo hili walisimamie vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ambalo tumelisema kwenye Kamati yetu, Baraza la Mitihani kila mwaka wakimaliza kusahihisha mitihani wanaandika ripoti ya watoto walivyofaulu na kila somo. Niiombe sana Wizara ya Elimu na Wizara ya TAMISEMI, ripoti hizi zikisambazwa kwenda kwenye Halmashauri zetu mhakikishe zinasimamiwa zinakwenda kwa kila Mwalimu Mkuu ili aangalie hali kwa nini watoto ili mwaka ujao tuongeze idadi ya watoto waliofaulu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kilichopo ripoti zile kila mwaka zinaandikwa tuna-shelf kwa sababu ukienda mwaka ujao, matatizo yaliyosemwa mwaka huu, mwaka kesho yanasemwa hayo hayo. Niiombe sana Serikali hasa Idara ya Ukaguzi, wanaosimamia quality assurance report hizi ni muhimu sana ili mwaka ujao tujue tunafanya effort wapi ili watoto wetu waweze kufaulu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ambalo tumelisema kwenye Wizara ya Elimu; narudia tena tulilisema mwaka jana na mwaka huu tumelisema, naombeni sabna Serikali mlitafakari. Umefika wakati watoto wetu wanaofanya vizuri sana darasani Mataifa yote yanatoa scholarship; Kenya kuna President Kenyatta awards, ukienda Uganda ipo, ukienda Rwanda ipo kwa nini Tanzania nchi kubwa na uwezo wetu wote huu hatuna Presidential awards? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, faida ya kuwa na Presidential awards unawafanya watoto wasome kwa bidii wakijua kwamba nikipata point three, point nne, point tano Serikali yangu itanisomesha na wenzetu wamekwenda mbali zaidi, ukienda hizo Tiger countries; China, Malaysia, Singapore watoto wote waliofanya vizuri sana wanapelekwa kwenye Western countries, kwenye heavy league universities, maana yake ni nini kule watakwenda kupata degree, watakwenda kujifunza na culture, wakirudi wanakuwa ni vijana, lakini hata wasiporudi hawa atafanya remittance nyumbani kwao. (Makofi)

Mhesimiwa Mwenyekiti, mtoto aliyemaliza degree Harvard akapata kazi Wall-street ni uhakika kama ni mtoto wa Kalinzi kijijini kwetu atajenga nyumba kijijini hata akiwa Harvard. Niwaombe sana Serikali mlitafakari angalau tuanze na watoto hata 100 huko nyuma ilikuwepo, kumetokea nini mwaka huu tumeamua kuiondoa? Baada ya kazi hii nzuri, Rais Magufuli anasomesha bure, nina hakika Serikali mkimuambia hawezi kuacha kuweka Presidential awards kwa watoto waliofanya vizuri sana regardless ni mtoto wa tajiri ama ni mtoto wa maskini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la MSD; Waziri amesema kuhusu MSD wanafanya kazi nzuri sana, ningeomba suala la MSD, sasa kazi imekuwa kubwa. Kwenye zile hospitali ambazo hasa Muhimbili na hospitali hizi kubwa za rufaa waachiwe wanunue madawa wenyewe ili MSD wahangaike zaidi na hospitali za Mikoa, za Wilaya na zahanati mpaka kwenye vituo vya afya, nina uhakika wakifanya hivyo tutaweza kufanya vizuri zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ambalo wachangiaji wengi wamesema ni kuhusu suala la NHIF. NHIF Serikali imesema wataleta Sheria, nampongeza sana Waziri lakini Sheria hii ni muhimu ije haraka sana. Dunia ya wenzetu kwa sababu matibabu ni gharama sana kinachosaidia ni kuwa na insurance. Nadhani umefika wakati tuweze kuwa na insurance.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni suala la kuimarisha huduma za Mama na Mtoto wanasema wao wanatafuta fedha tunawapongeza ni vizuri waendelee kufanya suala hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni suala la kupata wahudumu; Madaktari, Manesi na Walimu. Niombe sana Wizara ya ya Utumishi suala la kuajiri watu hawa ni muhimu sana kwa sababu hali vijijini kwetu kwenye hospitali zetu za vijiji, vituo vya afya na wilaya hali ni ngumu sana. Nadhani umefika wakati tuhakikishe watu wetu wanakwenda kufanya huko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ambalo tutachangia na tumelieleza vizuri ni suala la vitabu. Waziri ametuonesha vitabu vilivyotengenezwa, hoja yetu Kamati inasema; kuna vitabu vibovu vimeshasambazwa mashuleni, tunaomba vitabu hivyo vikaondolewe mashuleni, basi, halafu hivi vipya vipelekwe kwa sababu kuendelea kufundishia watoto wetu kwa vitabu vya zamani nadhani siyo jambo zuri sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niipongeze Serikali kwa suala la uboreshaji wa Chuo kikuu hasa kuanza ujenzi wa Bweni la tano na la pili ni kazi nzuri sana lakini nimpongeze Waziri kwa kusema amesema hapa hawana mpango wa kuifuta Open University, nadhani ni vizuri sana tuendelee kuinunga mkono ili iweze kusaidia maeneo ambayo tuna hakika yatasaidia kwenye elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la TBC, niiombe sana Wizara iendelee kusaidia TBC ili iweze kufanya vizuri zaidi na TBC kinachotakiwa ni uwekezaji. Naombeni, hiki ni chombo chetu, Serikali iwekeze kwenye jambo hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Sheria ya BMT ni muhimu sana Sheria ya BMT ije kwa sababu ni Sheria toka mwaka 1971, haiwezekani leo miaka 47 baadaye bado tunatumia Sheria ya mwaka 1971 kwa sababu mambo ya michezo yanabadilika sana huko duniani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge, michango ilikuwa ni mingi kwasbabu ya muda siwezi kuieleza yote, lakini kwa hakika niwashukuru sana Waheshimiwa Wabunge kwa michango yenu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho hasa ambalo liko tulilisema mwaka jana naomba tulirudie, naamini umefika wakati Serikali tukatafakari tulete, tuunde Tume ya Elimu. Nasema hili la elimu kwa sababu moja tu, elimu ndiyo uhai wa Taifa lolote. Tutajenga viwanda, tutajenga barabara, tutafanya kila kitu kama Taifa letu watoto hawajaelimika tutakuwa hatujafanya jambo lolote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naamini umefika wakati twende tukaangalie mfumo wetu wa elimu in totality hata haya tunaanza kubishana private schools ni kwa sababu tu, nadhani tukishaungalia mfumo wetu katika mapana yake tunaweza kujua tunakwenda wapi kwa sababu watu wamechangia hapa tuna watu wengi sana ni unskilled labour, tunafanyaje kupata skilled labour ili kufanya hiyo kazi kwenye viwanda ambayo mmeanza nayo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili la kuanzisha Tume ya Elimu siyo la kwanza. Mwaka 1981 Rais Regan alianzisha Tume ya Elimu baada ya kuona Marekani inafanya vibaya sana kwenye elimu. Ukienda ku-google iko report tena jina lake inaitwa “A Nation at Risk” ilielezea hali ilivyokuwa mbaya inakwenda huko Marekani kwa suala la elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wao walifikia point mpaka ku-test output, watoto waliomaliza degree wanawa-test wameelimika hawa? Wakakuta asilimia 60 ya watoto waliomaliza degree hawakuelimika. Kwa hiyo na sisi leo tukiamua ku-test output yetu, ndugu zangu tutashangaana watoto wetu wengi wanamaliza kweli lakini output siyo tuliyoitarajia. Nadhani umefika wakati kama nchi tuamue kuweka Tume ya Elimu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naomba sasa nitoe hoja kutaka Bunge liweze kuyakubali na kuyapitisha yale yote tuliyoyaleta kwenye Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/2017.
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nikushukuru kwa kunipa nafasi na nianze na kumshukuru Waziri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, moja, Rais alipokuja kutafuta kura moja ya jambo alituahidi pale ilikuwa ni barabara ya Mwandiga - Chankele – Kagunga. Naomba atakapokuja kujibu hoja utuambie status ya barabara hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, Rais alipokuwa Simbo alisema atatupa kilometa kumi za lami kutoka Simbo – Ilagala. Naomba Waziri atakapokuja kujibu hoja napo utusaidie status ya suala hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu, Mheshimiwa Rais aliongelea suala la kuwalipa fidia wale ambao hawakulipwa kwenye barabara ya Mwandiga - Manyovu. Nalo naomba kujua status yake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nne, nataka nipate status ya gati la Kagunga na watu wanaolipwa fidia. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine kubwa ambalo leo nadhani nitatumia muda wangu mrefu ni suala la viwanja vya ndege na ATC pamoja na reli. Reli ndiyo inayoweza kukuza uchumi wetu kwa haraka sana. Mimi naomba niwaambie Waheshimiwa Wabunge kama kuna jambo ambalo Rais Magufuli ataenda kwenye historia ya miaka 100 ni kujenga reli kwa kiwango cha standard gauge. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la reli ni legacy ya Rais Magufuli. Mimi namuomba Waziri, unless hataki tuandike legacy ya Mheshimiwa Rais Magufuli, naomba tujenge reli ya kiwango cha standard gauge kutoka Dar es Salaam kwenda mpaka Mwanza, kutoka Tabora kwenda mpaka Kigoma, kutoka Isaka kwenda Keza, kutoka Kaliua kwenda Mpanda, Mpanda kwenda Karema na Uvinza kwenda Msongati. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tubadili tabia, tukienda kwa hali hii tutaongea tutamaliza miaka mitano hatujaanza kujenga. Nchi zinazotuzunguka za Afrika, Kenya ilikuwa ni jambo la siku mbili, tatu leo wanajenga reli yao, Uganda nao wanajenga, Ethiopia wamejenga, Senegal wamejenga na wote hawa wamekwenda China kuchukua fedha. Naomba sana Mheshimiwa Waziri najua atasema ameweka shilingi trilioni moja, trilioni moja huwezi kujenga reli hii. Ni matarajio yangu shilingi trilioni moja hii ni sehemu ya fedha ya Serikali kama mchango wetu kwenye huo mpango mkubwa zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nawaombeni watu wa Wizara, Rais Magufuli tutamtofautisha na Marais wote tukijenga reli. Akijenga barabara na Kikwete alijenga, Marais wote walijenga barabara. Tunachotaka Rais Magufuli fanyeni kila mnaloweza tuache longolongo tujenge reli kwa standard gauge. Naomba Waziri unapokuja kujibu hapa atuambie jambo ambalo linaeleweka. Kama anakuja anasema anataka watu washindane, naombeni tusiwe wafungwa wa sheria zetu, hili suala ni la uchumi, ni la maendeleo, naomba tujenga reli ya kati. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni suala la ndege, mimi nampongeza Mheshimiwa Waziri ameanza kutengeneza ndege, lakini naomba tuseme tunataka kujenga airline ya namna gani? Kama tunataka kujenga airline kwanza lazima tuje na Shirika la Ndege ambalo ni imara. Wengine wanasema hamna wapanda ndege, ngojeni niwaambieni, tukiweka viwanja vya ndege mikoa yote, bei za ndege zitashuka na watu wote watapanda ndege. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tena mimi nachosema mikoa ambayo imeanza juzi ya Geita, Simiyu, Katavi, Songwe tujenge viwanja vya ndege. Viwanja vya Bukoba, Kigoma, Tabora, Singida, Dodoma vyote vijengwe. Tukishakuwa na viwanja tukawa na network, hilo shirika letu la ndege la ATC likawa lina-fly mikoa yote, kitakachotokea bei zitashuka, watu wengi watapanda ndege na shirika hili litapata faida. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mikoa lazima tujenge viwanja vya ndege, hiyo mikoa mipya ya wenzetu, Shinyanga tujenge, kiwanja cha Mwanza ni muhimu sana, tupanue kiwanja cha Kigoma na tupanue kiwanja cha Tabora. Kwa kufanya hivyo, tunayo hakika hili shirika tunalotaka kutengeneza litakuwa na maana na litatupeleka mbele tutapata faida. Kama unaleta shirika la ndege unataka ukashindane na mashirika yaliyoanza muda mrefu umeanza na kushindwa. Lazima tuanze kwanza ndani ili kama walivyosema wenzangu, leo unakwenda unapanda FastJet kweli inaonekana bei rahisi lakini ukiwa na begi unalipa shilingi 100,000 au shilingi 200,000 inawezekanaje? Siyo ndege rahisi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata tiketi yenyewe wanakuambia labda ni shilingi 90,000, unakuta tiketi za bei hiyo ni nne au tano nyingine zote ni za shilingi 400,000 mpaka shilingi 500,000, ni kwa sababu hatuna ushindani. Anayeweza kuleta ushindani ni shirika letu la ndege. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni suala la minara vijijini. Nimesoma hapa suala la UCSAF naona Wazri sasa hivi halichangamkii sana. Tulianzisha sheria hapa, tukasema tuweke huko ili UCSAF wapeleke minara vijijini. Haiwezekani minara tukaletewa na hawa Halotel, Halotel ni wafanyabiashara kama yalivyo makampuni mengine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naombeni kama Serikali tuendeleze mipango yetu ya kuhakikisha tunawapa fedha watu wa UCSAF ili kasi ya kuleta minara iwe kubwa. Mheshimiwa Waziri anajua kuna vijiji vyangu vya Kata ya Ziwani, vijiji vyote saba hakuna minara na tumelisema hili, tunaomba sasa lifanyiwe kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho ni suala la bandari ya Dar es Salaam. Kuna kitu kinaitwa VAT kwenye transit cargo, Waziri najua atajibu atasema VAT haitozwi lakini kwenye sheria ipo, tuliipitisha mwaka jana kwenye Finance Act. Kwa sababu tuliipitisha mwaka jana, yule anayetaka kutumia bandari ya Dar es Salaam anachukua sheria, una muda gani kwenda kumwambia hatutozi. Tuitoe kwenye sheria ili wajue hakuna VAT kwenye transit cargo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, bandari ni ushindani, naombeni sana tuiache bandari ya Dar es Salaam ifanye biashara kama biashara zingine zozote duniani. Kama kuna sehemu tunatakiwa tusiweke siasa ni kwenye bandari ya Dar es Salaam. Tumecheza na siasa, tulianza mwaka 2008 tunaongelea habari ya gati 13 na 14 leo ni mwaka 2016 hatujajenga. Tulikwenda China na watu wa Mombasa, Mombasa wameshamaliza kujenga wanaanza kwenda Lamu, sisi bado tunajiuliza tu tutumie modal gani. Nadhani muda umetosha, nakuomba sana Waziri umefika wakati tuache siasa kwenye suala la bandari ya Dar es Salaam. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, bandari ya Dar es Salaam lazima itafute masoko, lazima waende huko kwenye masoko wakaiuze bandari. Naombeni muondoe urasimu ili watu wa masoko waende huko, ndiyo kazi yao kwa sababu tunashinda, mzigo wenyewe siyo mwingi sana duniani. Ni kweli sasa hivi kuna downturn ya economy duniani, mzigo umeshuka lakini sisi hata kama mzigo umeshuka duniani lazima kuwe na sababu za kwetu, kama sisi hatutekelezi majukumu yetu kwetu utashuka zaidi na Mungu ametupa bandari hii tuitumie kwa maendeleo yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, namuomba Waziri atakapokujibu hoja atuambie kwa uhakika tuweze kumwelewa lini tunaanza ujenzi wa reli ya kati? Lini tunaanza kuandika historia ya Rais Magufuli ya miaka 100 ijayo ya kujenga reli ya standard gauge?
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naomba niunge mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Fedha na Mipango
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kwanza nimpongeze Waziri lakini nianze kwa ku- quote maneno aliyoyasema Deputy Managing Director wa IMF Dar es Salaam kuhusu kodi. Pamoja na kutusifia lakini alisema maneno yafuatayo:

“It is crucial to mobilize more private public resource within Tanzania especially by strengthening tax collection and fair and predictable tax regime. Ametumia maneno, strong, fair and predictable tax regime. Anasema, this is an area where Tanzania has fallen behind its neighbours. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kusema la kodi kwa sababu biashara, Waziri wa Fedha naomba hili likae kichwani, wafanyabiashara wote Tanzania ni partner wake, wafanyabiashara wa nchi hii ni partner wa nchi hii na nitasema kwa nini ni partner. Wafanyabiashara wa nchi hii wanatupa asilimia 30 ya corporate tax kila mwaka, kwa hiyo, maana yake na sisi tunazo sababu za kufanya biashara iendelee.

Mheshimiwa Mwenyekiti, biashara ikienda vizuri, Serikali inapata asilimia 30, Serikali itapata Pay As You Earn, itapata kwenye insurance, itapata kwenye pension funds. Kwa hiyo, tunalo jukumu kama Serikali na niwaombe sana watu wa Wizara ya Fedha, tufanye kazi ya kukuza biashara Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda leo Kariakoo, yuko mfanyabiashara mmoja ni mdogo sana, natoa mfano, mwaka 2005 alikuwa anaingiza makontena manne kila mwezi analipa shilingi milioni 72, leo hii mambo yamekuwa magumu anaingiza kontena moja kila baada ya miezi miwili,
aliyepoteza ni nani? Ni sisi Serikali. Hii nasema lazima niwaombe sana tujitahidi tuwalee wafanyabiashara. Kudhani wafanyabiashara ni wezi, wanatuibia siyo sahihi sana, naombeni sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili wameanzisha task force, task force inakwenda kwa wafanyabiashara imerudi mpaka 2009. Wanajua maana yake ni nini? Kwa sababu walikwepa kodi kule zamani wakiwaambia leo wailipe, yes watalipa lakini hao wanakufa kibiashara. Kwa hiyo, mwezi unaofuata hawataweza kulipa kodi. Ama kitakachotokea ile task force, wanakwenda wanakaa mezani, ni rushwa! Mtu atakuja anadaiwa shilingi bilioni tano hajalipa miaka sita, anaambiwa sasa sikiliza, lipa shilingi bilioni moja, tupe shilingi bilioni moja, shilingi bilioni tatu tunakusamehe, ndiyo kinachoendelea huko mtaani. Niwaombe sana watu wa Wizara ya Fedha, tuamue sasa, tusiende nyuma, tuanzie sasa kwenda mbele kuhakikisha kila mtu analipa kodi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni Sheria ya VAT. Sheria yetu ya VAT haitambui vivutio tunavyowapa wawekezaji, kwa maana ya capital goods na deemed capital goods. Nimwombe Waziri, tutoze kodi kwenye bidhaa siyo kwenye production. Tukianza kudhani unataka kuwekeza leo unataka uanze kupata, hakuna atakayewekeza. Mimi nasema jamani haya yanayofanyika, duniani wenzetu wanafanya, ukimuachia mtu azalishe, Dangote alienda pale Ethiopia akaambiwa tunakupa umeme rahisi, vivutio, baada ya kuanza kuzalisha bei ya cement ikashuka by 60% maana yake watu wengi wakajenga, utapata kodi kule mbele. Kwa hiyo, niwaombe wenzetu wa Wizara ya Fedha tuyasimamie haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine naomba tu- harmonise NIC pamoja na Sheria ya Fedha. Kama inatokea NIC inatoa vivutio under TIC, Sheria ya Fedha inakuja hapa haivikubali ni contradiction, hatueleweki. Ndiyo maana tumeambiwa our tax regime is unpredictable, wenzetu ndivyo wanavyotuona. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni suala la TIB, Waziri wa Fedha, naomba leo atuambie anaihitaji TIB ama haihitaji? Kutoweka fedha TIB mimi sielewi maana yake ni nini. Duniani kote wanaweka hela kwenye Benki zao za Maendeleo ili zisaidie katika maendeleo hasa ya viwanda na kila kitu. Sisi tunasema tuna maendeleo ya viwanda, tunataka kwenda kwenye viwanda lakini hakuna hela TIB. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninacho kitabu cha maendeleo cha mwaka mmoja, TIB imetajwa by the way. Hakuna anywhere imetajwa TIB inawekwa pesa. Tuliambiwa watapewa shilingi trilioni moja, najua mwaka huu wamepanga kuwapa shilingi bilioni 94, watafanya nini kwenye maendeleo? Jamani ukienda China, Brazil, wapi wana embrace Development Banks zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawaomba sana watu wa Wizara ya Fedha, waweke commitment hapa. Leo TIB ukimpa shilingi trilioni moja anazi-leverage atapata hata zaidi ya bilioni nyingi tu, anakwenda kwenye masoko nje, analeta through DIF, anachangia kwenye maendeleo yetu. Mimi sijui kuna nini pale Wizara ya Fedha, hawataki kuisaidia TIB. Watuambie, kama hawaitaki tuifunge lakini kila siku ukisoma kwenye vitabu humu inashangaza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni suala la investment model yetu. Waziri wa Fedha, lazima tuchanganye tax, debt na investment. Kwa nini nasema investment, ili sasa uweze kuleta PPP. Ukisoma kwenye kitabu PPP haisemwi, ukisoma kwenye hii ya maendeleo, hakuna PPP tunaisema by the way. Hivi mbona wenzetu wote, China, Malaysia na kadhalika wana embrace PPP, what is wrong with us? Hatuwezi kujenga nchi hii kwa kodi peke yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wenzetu barabara, umeme, wanajenga kwa hela za watu, unaweka legal framework yenye clarity. Hata agriculture, mimi nawasikia wenzangu wanasema tuweke hela kwenye agriculture, tusipo-embrace kwenye commercial farming hatutaendelea. Commercial farming ni more capital, itaajiri watu wengi na italeta hela kwenye products za kwenye viwanda lakini wakubwa hawasemi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, deni la Taifa, wanasema linahimilika, linahimilika yes, kwa sababu wanachukua debt sustainability ratio, fine. Mimi naomba, umefika wakati tuliangalie deni la Taifa na revenue base yetu ndiyo watajua kwamba deni letu halihimiliki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni transit trade, VAT. Jamani tumesema mwaka jana, auxiliary VAT kwenye transport inaua hii industry. Waziri hapa anasema uchumi umekua kwa asilimia saba na moja ya mchango ni kwenye transport, Waziri wa Fedha, transport imeshuka. Aende akaulize wenye malori, malori yaliyokuwa yanakwenda nje yalikuwa 23,000 leo yamebaki malori 11,000.

Yakibaki malori 11,000 maana yake ni nini? Mafuta hawanywi, madereva hawana kazi, tairi hakuna, magari 12,000 yako nyumbani, mabenki hayalipwi kwasababu tumeua hii industry. This is our dear country, naombeni tufanye wanavyofanya wengine. Nimesikia auxiliary VAT hawataki kuitoa, hawataki kuitoa kwa sababu gani? Wanapata nini kwa kuiweka? Ni kama vile ambavyo tunasema suala la kuwakusanyia Congo kodi tuache, haitusaidii ni disincentive kwenye economy yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni deni la ndani, Waziri naomba tulipe deni la ndani. Leo hali iliyoko nchini ni kwa sababu hatulipi deni la ndani. Naombeni sana tuhangaike na kulipa deni la ndani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni suala la Federal Reserve zimepanda interest rate. Mimi niliisema mwaka jana, naomba leo niiseme, najua watu wa Wizara ya Fedha hili hawataki hata kulisikia. Leo hii Federal Reserve imepanda to
0.75 maana yake ni nini? Kwa sababu mikopo yetu yote ni faulting libel maana yake inakwenda kupanda, maana yake Waziri wa Fedha utakapoanza kulipa deni la Taifa kesho siyo hela uliyolipa mwaka huu, revenue inashuka, deni la Taifa linapanda kwa sababu ya interest rates, what do we do? Wenzetu wana-swap, let us fix this interest. Jamani wote wanafanya, Kenya wamefanya, Uganda wamefanya, wamezi-fix interest rates kwa sababu vitality kwenye economy ya Marekani ni kubwa, inatu-affect sisi ambao tumekopa kwa dola lakini wenzetu hawataki kusema. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la mifuko, nasikia mnataka kuunganisha mifuko ya pension fund, jambo jema lakini niwaombe Waziri wa Fedha, kabla hawajaiunganisha tulipe madeni yao yote. Maana hii itakuwa ni kukwepa majukumu yetu. Mifuko inaidai Serikali, hakikisheni mifuko yote inalipwa, tufanye hesabu za mwisho ndiyo tuamue kuiunganisha. Kwa kufanya hivyo, tutafanya vizuri sana kama nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nimalizie kwa kusema suala la mwisho na narudia kwa kweli ni suala la biashara. Nawaombeni sana wakubwa, tu-embrace biashara Tanzania. Ukienda leo Kariakoo jamani siyo Kariakoo ya miaka mitatu iliyopita. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi niwaambieni kwa mtu aliyesoma tax, somebody akiwa analeta makontena 100, akakwepa makontena 50 akalipa kodi ya makontena 50 anaingiza kwenye market, uwe na hakika atakapoenda mwezi ujao ataleta makontena 150. Kwa hiyo, anapokuja anakukuta umejiandaa unampiga kodi makontena 120 maana yake wewe base yako ya kodi imepanda. Akileta 100 ukasema lazima ulipe yote, fine, it is a good idea lakini mwezi unaokwenda ataleta makontena 70, aliye-loose ni wewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lazima tutengeneza utaratibu wafanyabiashara wakue na sisi tukue. Ukidhani unaweza ukafunga milango kwamba hapa hakitoki kitu ni jambo jema lakini mwisho wa siku we will be a looser as a country. Kwa sababu ukiangalia trend ya kodi imekuwa
inapanda, kama inaanza kushuka lazima tujiulize haraka sana, tatizo kwa vyovyote vile ni suala tunavyo-handle business as a country.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana na naunga mkono hoja.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi.
Niwapongeze kwa speech nzuri, nina mambo matatu.
Mheshimiwa Naibu Spika, moja, nililisema na nazidi kulisema ili angalau wenzangu wa
Serikali huko walielewe. Sisi tuna madini mengi sana, lakini nchi hii katika wanaotuzunguka sisi
hatuna soko la madini. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika na Waheshimiwa Wabunge, leo Tanzania tukiweka soko la
madini kwamba mtu yoyote anayekuja pale sokoni hatumuulizi madini ameyatoa wapi lakini
yule anayekuja kununua anapoondoka tunaweka export levy, tutapata fedha nyingi sana kama Taifa. Fedha zile zitaingia kama kodi ni nyingi sana na tutapunguza kodi nyingi hizi za kero.
Lakini kila tukisema suala la madini, kwa sababu leo tunawachimbaji wadogo wadogo, hivi
wanauza dhahabu wapi? Nani anajua wanauza wapi? Kwa hiyo, inawezekana wanachimba
kwetu wanaenda kuuza kwingine kwa hiyo faida inaenda kwa wengine, lakini tuna uwezo wa
kuanzisha soko la madini Tanzania na watu wote wakaja wanunuzi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa naongea na mtu mmoja hapa anasema, ukienda leo
Telaviv-Israel, moja ya biashara yao kubwa ni diamond na diamond wala haichimbwi Telaviv.
Walichofanya wameweka soko la diamond, so everybody ine the world anakwenda kuuza
diamond pale Telaviv. Kwa hiyo, na sisi kama Tanzania tukiweka soko hapa, tuna hakika
Wakongo wataleta dhahabu, nani ataleta dhahabu halafu watu wanaponunua
wanapoondoka ndiyo tunaweka export levy, tutapata fedha nyingi sana na hawa wanunuzi
watakaa kwenye hoteli zetu, watakula chakula chetu na wale Wauzaji wakishauza dhahabu
watanunua bidhaa so triple down effect kwenye economics itakuwa kubwa sana kama
Tanzania. (Makofi)
Lakini tunalisema hakuna anayetaka kulielewa, naomba sasa Profesa Muhongo, fanya
hili jambo liwe legacy yako. Anzisha soko la madini Tanzania watakukumbuka tu kwa sababu
utakuwa umeanzisha jambo kubwa sana na itakuwa ni source ya fedha nyingi sana kwa nchi.
Mheshimiwa Naibu Spika, la pili ni suala la mafuta, tumesema hapa bei za mafuta
duniani zinapanda na kushuka. Kama nchi lazima tuwe na strategic reserve ya mafuta ili
tukishakuwa na strategic reserve ya mafuta tunaweza tuka-survive kwa miezi sita bei ya mafuta
inayo treat haitatu-affect sisi kwa sababu tutakuwa tuna mafuta yetu ambayo tunatumia miezi
sita ama mwaka mmoja. Na hii haihitaji fedha nyingi sana kwa sababu tunayo TIPPER, tunayo
PUMA ambayo tuna asilimia 50, TIPPER tuna asilimia 50, ni suala la kuamua tu na hapa Serikali
itapata faida maeneo matatu:-
(i) Itapata faida kwenye TIPA kwa sababu tuna asilimia 50 kwenye reserve.
(ii) Itapata faida kwenye PUMA kwa sababu tuna asilimia 50.
(iii) Itapata faida ya mafuta tutaweza ku-control inflation, tuta-control bei ya mafuta
ambayo ni kubwa sana kwa maana ya nchi. (Makofi)
La mwisho ni suala la PPP project kwenye barabara, niombe sana, umefika wakati,
tumeongea habari ya PPP project ya barabara. Huu mwaka wa kumi niko Bungeni, tunaifanya
Dodoma kuwa Makao Makuu lazima tuifanye Dodoma iwe accessible. Lazima Dodoma iwe
karibu, hatuwezi kutegemea watu wote wapande ndege. Tutegemee kwamba wanaokuja
Dodoma atakayekuja kwa treni awahi, atakayekuja kwa gari awahi, atakayekuja kwa ndege
awahi, tunafanyaje? Lazima fedha zetu tuweke fedha ya watu binafsi wajenge super high way,
wata-charge...
Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru huo ndiyo mchango wangu.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 6) wa Mwaka 2019 (Toleo la Kiingereza)
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 50(1) Kanuni za Bunge Toleo la 2016 naomba kutoa maelezo binafsi mbele ya Bunge lako Tukufu.

Mheshimiwa Spika, nimesimama kwa sababu kuu moja ambayo ni kufafanua na kisha kuomba radhi Chama changu na Viongozi wangu wa Chama cha Mapinduzi kutokana na matamshi niliyoyatoa wakati nikichangia hoja hapa Bungeni mwezi Juni, 2019. Wakati nikihitimisha hoja yangu, nilitumia neno “Ujamaa” katika mukhtadha ambao baadaye nilikuja kubaini ulisababisha taharuki iliyotokana na tafsiri ambayo sikuimaanisha.

Mheshimiwa Spika, sentensi ya mwisho katika hoja, ilikuwa ni maneno yafuatayo: “kama kuna jambo siliamini, ni Ujamaa.”

Mheshimiwa Spika, msingi wa hoja yangu haikuwa kuupinga Ujamaa kama itikadi ya kisiasa ya kujenga uchumi wa Kitaifa na badala yake ililenga kuchochea mjadala wa kujenga uchumi wa kijamaa unaotambua mchango wa Sekta Binafsi katika juhudi za kukwamua kilimo chetu.

Mheshimiwa Spika, mimi ni zao la Chama cha Mapinduzi ambacho kinaamini katika dhana ya Ujamaa na Kujitegemea na hivyo, haiwezekani mimi tena nikakaririwa kwa makosa na hata kutafsiriwa ninaukana msingi wa kuwepo kwangu Bungeni na ndani ya CCM. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi ni mjamaa kwa kulitambua hilo na kwa ajili ya maslahi mapana ya Taifa, napenda tena kukiomba radhi Chama changu, Viongozi wote wa CCM kwa usumbufu uliotkana na matamshi yangu ambayo yalitafsiriwa katika muktadha usio sahihi.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba na mimi nichangie Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na naomba nianze kwa kutoa pongezi kubwa kwa kazi kubwa ainayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa barabara zaidi ya kilometa 17,000 huwezi kutenganisha na Mheshimiwa Magufuli. Ujenzi wa viwanja vya ndege nchini unaoendelea, huwezi kuacha kumtaja Mheshimiwa Rais Magufuli; umeme vijijini ambapo tunamalizia vijiji hivi, huwezi kumuacha Mheshimiwa Rais Magufuli; mabasi yaendayo kwa kasi Dar es Salaam ni kwa sababu ya Rais Magufuli, ujenzi flyover leo Dar es Salaam, kwa kweli ni Mheshimiwa Rais Magufuli; Daraja la Mkapa, Daraja la Kikwete, Daraja la Kigamboni, Daraja la Kilombero huwezi kuyatenganisha na Mheshimiwa Rais Magufuli. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa reli ya kati ya kisasa (standard gauge) ambayo mara ya mwisho reli hii imejengwa mwaka 1906 leo Mheshimiwa Rais Magufuli anaandika historia ya kujenga reli Tanzania. Kuimarisha Shirika la Ndege la ATC ni kazi ya Mheshimiwa Rais Magufuli, kudhibiti matumizi ya Serikali ni Mheshimiwa Rais Magufuli, ukusanyaji wa mapato ni Mheshimiwa Rais Magufuli. Leo tunaona elimu bure, ni Mheshimiwa Rais Magufuli, mabweni ya University of Dar es Salaam ni Mheshimiwa Rais Magufuli. Upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam na Mtwara ni Mheshimiwa Rais Magufuli, kuanza kujenga upya uchumi wa viwanda ameanza Mheshimiwa Rais Magufulina na kudhibiti maliasili ni Mheshimiwa Rais Magufuli. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ninayo hakika kwa kazi kubwa inayofanyika ya miumbombinu, safari ya kuondoa umaskini wa Watanzania Mheshimiwa Rais Magufuli ameianza. Pia naomba niwaambie Waheshimiwa Wabunge, ninayo hakika atayekuja kuandika historia ya Tanzania nina hakika jina la Mheshimiwa Rais Magufuli litaandikwa kwa wino wa dhahabu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, naomba sasa nichangie baadhi ya maeneo; barabara ya Mwandiga - Chankere kwenda Kagunga, nampongeza sana Mheshimiwa Waziri ameipandisha lakini fedha iliyowekwa ni kidogo sana kwa sababu barabara hii ni ndefu na inapita kwenye milima mikubwa sana. Pia suala la barabara ya
Mwandiga, fidia Mwandiga - Manyovu nakuomba sana Mheshimiwa Waziri Mbarawa, usimchonganishe Mheshimiwa Rais Magufuli na watu wa Kigoma Kaskazini. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Rais Magufuli alikuja kwenye kampeni, aliahidi kwamba lazima atawafidia ambao hawajafidiwa kwenye barabara hiyo ya Mwandiga
- Manyovu na barabara ya Mwandiga - Kidahwe. Nakuomba sana utekeleze ahadi hii. Pia barabara ya kutoka Simbo kwenda Ilagala kilometa kumi za lami naomba zianze kujengwa, Mheshimiwa Rais Magufuli alihaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, na mimi kwa nini nasema hivi? Mheshimiwa Rais Magufuli akiahidi anatekeleza. Naombeni ninyi watu wa Serikali, Wizara msimchonganishe Rais, kwa sababu aliahidi naombeni mtekeleze hizi ahadi zake. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu Bandari ya Kagunga, nawapongeza sana watu wa bandari kujenga gati ya Kagunga. Nawaomba sana watu bandari, ili bandari ya Kagunga iwe na maana kibiashara ni lazima na soko la Kagunga mlichukue muweze kulifanyia kazi. Halafu baadaye Halmashauri ya Kigoma tutaungana na bandari, tutafanya revenue sharing, mkishamaliza kutoa fedha zanu, then mtaturudishia jengo lile, lakini nina hakika bandari ile itakuwa na maana kama tutakuwa na soko la Kagunga. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naiomba sana Serikali, pale kwenye Soko la Kagunga tupafanye kuwa free trades zone area ili watu wote wapeleke bidhaa pale. Nina hakika Warundi na Wakongo watakuja pale kwenye soko lile na tutapata fedha nyingi sana kama nchi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho nilitaka niliseme vizuri sana, ni suala la barabara vijijini na TANROADS. Nimesikia Serikali inataka kuanzisha Wakala wa Barabara Vijijini. Nashauri na naomba sana tayari tunayo TANROADS, inafanya vizuri sana, hivi badala ya kuanzisha Wakala mwingine ambao ni matumizi, ni fedha, ni mzigo, badala yake kwenye TANROADS pale fuwafanye waende mpaka Wilayani.
Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wabunge wote hapa ndani mmekuwa mnaomba barabara zipandishwe, sasa kama tunaomba barabara zipandishwe, basi tuamue.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Bunge, tuamue niombe Serikali kwamba sasa custodian wa barabara nchini iwe TANROADS peke yake ili fedha zote za mafuta tunazokusanya, badala kumpelekea TANROADS asilimia 67, tumpelekee asilimia 100 kwamba suala la barabara Tanzania tunashughulika na TANROADS peke yake. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashuri yapo mambo mengi ya kufanya, tuwanyang’anye hili la barabara. Nina hakika Wakala huu tukiupanua tukawapa fedha zote mtu mmoja, kwanza tutakuwa tume-save fedha za administration kwa sababu itabaki ni ile ile; kama ni Mkuu wa Taasisi atabaki ni yule yule, Wakurugenzi watabaki ni wale wale. Tukianza taasisi nyingine, hizi ni gharama. Na mimi ninaamini spirit ya Serikali hii ni kupunguza matumizi. Nani anataka kuleta habari ya kuanzisha mawakala wengi, wakati tunaweza kuamua ma-engineer wote tunawapeleka na one umbrella, wao ndio wafanye kazi ya kuhakikisha nchi yetu barabara zinajengwa na mtu mmoja. (Makofi)
Mheshimiwa naibu Spika, mwisho ni suala la barabara ya kutoka Kibondo kuja Kasulu kwenda Manyovu. Nawaomba sana, nimeona kwenye kitabu mmeandika kwamba ipo under NEPAD. Habari ya NEPAD tumeisikiliza huu ni mwaka wa saba. Nadhani imefika wakati sasa, na kwa kweli jamani, tuliobaki hatujapata barabara ni sisi watu wa Kigoma. Naombeni sana mjitahidi tumalizie barabara hizo za watu wa Kigoma. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho kabisa nataka kuwakumbusha tu watu wa Serikali, inawezekana Mheshimiwa Waziri Mbarawa labda hili hulijui vizuri sana. Reli
ya kati Tanzania; definition ya reli ya kati toka wakati wa Mjerumani ni Kigoma - Dar es Salaam. Toka 1906 ni Kigoma – Dar es Salaam. Halafu kuna matawi ya Tabora - Mwanza kuna matawi ya kutoka Kaliua kwenda Mpanda, haya ndiyo matawi. Naombeni tusi-diverge from the original reli ya kati. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, na mimi kwa nini nasema Kigoma? Ni kwa sababu moja tu; kwa sababu Kigoma tunayo bahati; Kigoma tuna Burundi na Kongo ambako huko kuna mzigo wa biashara. Investment hii inayofanyika ni kubwa sana, lazima tuanze kuifikiria kibiashara. Tutumie jiografia yetu kutengeneza pesa. Mungu ametuunga geographically tuko well located, tuitumie nafasi hii kufanya vizuri zaidi.
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, naomba sana nimpongeze tena Mheshimiwa Waziri na watendaji wake kwa kazi kubwa sana wanayofanya. Nawapongeza watu wa bandari, wanafanya kazi kubwa sana. Tumeongea habari ya gati 13 na 14 nikiwa Bunge hili karibu miaka kumi. Sasa naona kuna mwanga, gati 13 na 14 linaenda kutekelezwa; gati namba moja mpaka saba inatekelezwa, kupanua mlango na kuchimba dragging ya Dar es Salaam inatekelezwa. Naombeni miradi hii iende kwa kasi ili nasi tuweze ku-compete katika biashara ya huko mbele tunakokwenda. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, naomba kuunga mkono hoja ya Mheshimiwa Waziri.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Spika, nami nakushuru sana kwa kunipa nafasi niongee kwenye Bunge lako Tukufu, kwa kweli toka tumeanza nilikuwa sijachangia. Leo naomba nianze kwa kuipongeza Serikali, nimpongeze Rais Mheshimiwa Dkt. Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya, nimpongeze Waziri Mpango, nimpongeze Katibu Mkuu wa Fedha, Naibu Waziri, rafiki yangu Ndugu Kichere wa TRA na task force yote kwa kazi kubwa wanayoifanya.

Mheshimiwa Spika, mchango wangu leo nitaanza na page 47 ambapo Mheshimiwa Waziri ameamua jambo kubwa na la kihistoria kupunguza corporate tax kwa ajili ya viwanda vya ngozi na viwanda vya madawa kutoka asilimia 30 mpaka asilimia 20. Namwomba sana Mheshimiwa Waziri aende zaidi; kwa viwanda vya ngozi vilivyopo, vinavyokuja, na viwanda vya madawa afanye zero corperate tax. Akifanya zero corporate tax kitakachotokea Tanzania itakuwa hub ya biashara ya madawa. Viwanda vyote vya madawa vitakuja Tanzania kwa sababu itazalisha kwa wingi waende wakauze nchi zote zinazotuzunguka. Viwanda vya ngozi tutaweza kuwa competitives kwenye soko la dunia, lakini tutapata ajira na production itaongezeka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wenzetu huko duniani tunashindana na Mheshimiwa Spika umesema kuhusu Kenya lazima twende kwa kasi zaidi. Kwenye suala la ngozi naomba tuondoe asilimia 10 ya export levy tukiondoa na tu-ban tuhakikishe hakuna kusafirisha tena ngozi ambayo ni raw. Uki- ban raw halafu ukatoa 10 percent na umeondoa corporate tax ni zero, unayo hakika viwanda vyetu vya Tanzania vitazalisha ngozi na vitakwenda kushindana kwenye soko la dunia.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, hapo kwenye kiwanda nataka niongeze na Kiwanda cha Mbolea. Naombeni Mheshimiwa Waziri tuamue, tuondoe corperate tax iwe zero rated ili watu wote duniani waje wajenge viwanda vya mbolea. Wakijenga viwanda vya mbolea Tanzania kitakachotokea Tanzania ndiyo tuta re- export mbolea kwenye Afrika yote, leo mbolea yote inanunuliwa Morocco, why? Tanzania tuna Gesi, Tanzania tuna Bandari, tunayo sababu tuweke huo mkakati, nina hakika viwanda hivyo vikiwekwa tutapata ajira, production itaongezeka lakini na bei ya mbolea Tanzania itashuka na kwa sababu hiyo tutakipa thamani kilimo.

Mheshimiwa Spika, suala lingine ambalo leo nitachangia liko page ya 52. Mheshimiwa Waziri ame- introduce electronic stamp, namshukuru na kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri. Nampongeza na naomba nianze kwa kusema kwenye tax kuna task evasion na tax avoidance. Tax evasion ni kosa la kijinai, tax avoidance ni mtu anatumia sheria zako za kikodi anakwepa kodi na hilo wala siyo kosa la jinai. Tufanye nini ili kuzuia tax avoidance? Mambo mawili lazima yafanyike.

Mheshimiwa Spika, kwanza, kuweka sheria ambazo zitazuia watu wasiweze kukwepa kodi, pili ni kuweka infrastructure ambayo itazuia ama kuweka system watu wasiweze kukwepa kodi. Kwa kufanya hivi tutakuwa tumeenda mbali sana, Waziri wa Fedha ameliona na amelifanya, hongera sana ndugu yangu.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, wako watu watapinga huu mfumo, siyo kwa sababu nyingine yoyote. Mfumo huu unakwenda kufanya yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza, mfumo huu unakwenda kufanya production count, kila kitakachozalishwa kwenye kiwanda chochote, TRA wanaona. Jambo la pili kubwa ambalo litatokea kwenye mfumo huu ni revenue itakua. Kila walio-embrace teknolojia hii ya electronic stamp, nchi 47 ninazozifahamu kodi ilipanda kwa asilimia 40 mpaka asilimia 65. Kwa hiyo, naamini mwaka kesho tutakapokutana hapa kodi itakuwa imepanda kwa kiasi kikubwa sana, lakini jambo kubwa ambalo litatusaidia ni bidhaa feki. Kwa wale ambao ni wanywaji kama mimi naomba waniambie ukienda kwenye spirit watu wetu wanakufa sana kwa vinywaji feki. Kwa sababu zile stamp za karatasi kila mtu anaweza akazitengeneza, lakini hapa ni stamp siyo za kutengeneza, kwa hiyo tutaondoa vitu feki na tukiondoa feki wenye viwanda watapata mapato zaidi kwa sababu mapato yao yalikuwa yanashuka kwa sababu ya vitu feki.

Mheshimiwa Spika, wako Watu wanasema tuna hand over sovereignty, sovereignty gani tuna hand over? hapa tunachofanya tunakwenda kuzuia ili Serikali ipate mapato makubwa. Naomba Serikali iendee itekeleze jambo hili na ikiwezekana ipeleke kwenye kila bidhaa, wametuibia inatosha umefika wakati tupate mapato makubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hii ndiyo PPP inayosemwa na kuna wenzetu wanaomba PPP lakini PPP zikija naomba hii muitambue hapa amekuja mtu ana fanya self-investment lakini sisi tutapata na yeye atapata, ndiyo maana ya PPP hawezi mtu kuja na technology halafu asipate, haiko dunia ya hivyo. Mtu huyu ameleta hela zake, ameleta techology yake, wewe ghafla unasema na mimi naweza nikafanya mbona hukufanya jana?

Mheshimiwa Spika, ninachoomba sana kwa Serikali jambo hili ni zuri litaongeza ajira. Kubwa zaidi huyu anayekuja kufanya ataajiri Watanzania above all atalipa corporate tax, kwa hiyo revenue itaongezeka both side. Kwa hiyo niombe Mheshimiwa Waziri hili mlisimamie haraka ili liweze kuanza tuweze kupata mapato.(Makofi

Mheshimiwa Spika, jambo lingine nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri, toka nimeingia Bungeni mwaka 2005 kila mwaka kwa wale tulikuwepo na Mheshimiwa Spika wewe utasema. Kila mwaka tuliongeza excise duty ya bia, soda, maji pamoja na vinywaji vikali na sigara kila mwaka mpaka tukawa magazeti yanaandika bajeti ya sigara, bajeti ya pombe. Mheshimiwa Waziri wa Fedha ametanzua jambo hilo kwa mara ya kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nampongeza sana Mheshimiwa Waziri na naipongeza sana Serikali ya Awamu ya Tano. Kwa kufanya hivyo maana yake ni nini? Maana yake production itaongezeka, maana yake matumizi yataongezeka, nilikuwa nawatania wenzangu kwa kutoongeza excise duty wale ambao tulikuwa tunakunywa bia mbili sasa tutakunywa tatu kwa sababu zitabakia kwenye bei zile zile tutaweza kutumia hizo bia zetu.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine ninalotaka kusema ni kuhusu mafuta ya kula, Waziri wa Fedha amechukua very good measure kupandisha kwenda asilimia 35 na asilimia 25. Sasa nimwombe Mheshimiwa Waziri wa Fedha lipo jambo la kufanya. Jambo la kwanza lazima aje na extensive master plan ya agriculture ya michikichi pamoja na alizeti. Tusipofanya hivyo bei hizi zitapanda, Wabunge tutarudi hapa kupiga kelele. (Makofi

Mheshimiwa Spika, tumeamua kufunga mkanda, tukitaka kuulegeza mkanda lazima sasa kilimo cha michikichi, kilimo cha alizeti tukipe bajeti. Kwa bahati mbaya sana ukisoma bajeti ya Wizara ya Kilimo hakuna hata senti tano moja inayokwenda kwenye michikichi. Kwa hivyo, inawezekana hii measure ni nzuri lakini ikawa counterproductive.

Mheshimiwa Spika, nami niseme ulikuwa unasema kwa nini Kenya wako mbali? Moja ya sababu ni Kenya wana- embrace commercial farming. Narudia tena mimi siyo muumini wa ujamaa, kama tunataka kilimo kitoke lazima tuanzishe commercial farming. Ukianzisha commercial farming utatoa ajira nyingi zaidi, production itaongezeka kwa sababu yule anayeleta fedha zake atatafuta Wagani wake, atatafuta mbolea na ataongeza production.

Mheshimiwa Spika, ukienda leo michikichi ya Kigoma yote imezeeka, haizalishi mawese tena, ili uweze kuokoa kilimo cha michichiki Kigoma lazima ugawe mbegu mpya. Tukigawa mbegu mpya ndani ya miaka miwili, mitatu tutaweza ku-clear hili gap na mafuta yataongeza.

Mheshimiwa Spika, lingine ni suala la transit trade. ukisoma record za uchumi, sekta mbili zilizoleta fedha Tanzania ni bandari na tourism. Maana yake ni nini? Ili bandari ifanye vizuri zaidi lazima tu-embrace transit trade. Tuondoe vikwazo ili watu wengi watumie bandari ya Dar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, kwa mfano mafuta yanayokwenda transit trade, mafuta yakiwa yanakuja yakifika Dar es Salaam baada ya siku 30 hayajatoka tunawaambia waya-localise. Ukienda Beira ni siku 90, ukienda Durban siku 120, Walvis Bay siku 90, Mombasa siku 60 maana yake ni nini? Tanzania siyo sehemu ya kwenda kupitisha product hiyo. Tukiongeza siku zikawa 90 maana yake destination ni Dar es Salaam, tutaongeza ajira, tutapata wharfage tutapata storage. Tukipata storage maana yake bandari iende fast, bandari ijenge storage capacity ili tuweze kuweka mafuta hayo. Storage capacity tuliyonayo ilijengwa mwaka 1970, leo ni miaka 47 Taifa limebadilika sana. Ninaomba hilo tulifanye kwa haraka ili tuweze kufanikiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala lingine nataka kusema PPP project, nimesema kila nilipoingia kwenye Bunge hili, naombeni tubadilishe sheria, naombeni tufanye PPP itatusaidia to easen budget. Hili nalisema kwa sababu nataka leo wenzangu muangalie ukienda page ya 78 ya kitabu cha Waziri wa Fedha ameonesha mfumo wa bajeti ya mwaka wetu. Ukichukua first charge pesa ambazo lazima hata afanyeje Waziri lazima alipe ni trilioni karibu 27 hizi hana choice lazima alipe.

Mheshimiwa Spika, ukienda kwenye revenue ukatoa mikopo fedha ambazo anaweza akakusanya na hapa maoteo yamepata kwa asilimia 100 ni trilioni 23. Sijaweka OC, sijaweka hela za Development. Unafanyaje katika situation hii? Situation hii lazima uje na PPP, PPP lazima u- embrace concession loan. Kwa mfano, leo Mheshimiwa Rais Magufuli ame-embark kwenye kufanya mambo makubwa mawili ya kihistoria, moja kujenga Reli ya Kimataifa, mbili kujenga Stiglers Gorge jambo kubwa la kihistoria na kwa kweli naamini historia itamuandika Rais Magufuli kwa kufanya miradi hii mikubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nitoe ushauri kwa haya yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, miradi hii tunaijenga kwa fedha za ndani, miradi hii tunaijenga kwa kukopa commercial loans, tukikopa commercial loans maana yake ni moja tu, ukikopa mkopo wa kibiashara unaanza kuulipa ndani ya miezi sita, wakati unaanza kuulipa hata miradi hii haijakwisha, miradi hii haijaleta fedha. Tumeweka seven trilioni mpaka Dodoma lakini mpaka leo tunalipa deni lakini reli haijafika Dodoma. Sasa ili tuweze kupata concession loans lazima tufanye yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, naomba sana, mimi Rais Magufuli namuamini, Rais lazima aende, akutane, afanye mambo ya kidiplomasia. Akutane na Xi Jinping wa China, akutane na Angela Merkel wa German, akutane na Shinzo Abe wa Japan, akutane na Donald Trump wa US, akutane Vladimir Putin wa Urusi, akutane na Theresa May wa UK maana yake nini? Watu wawili wanakutana na mimi najua uwezo wa Rais Magufuli atakwenda na nchi at heart ata-re-negociate for the country tutapata concession loans.

Mheshimiwa Spika, tukipata concession loans maana yake ni moja tu, maana yake tutapata fedha, tutajenga reli yetu, wakati huo hatulipi mpaka baada ya miaka 15 tuwe tunaanza kulipa deni. Maana yake ukienda kwenye figure za bajeti pale kwenye eneo la deni la Taifa la trilioni mbili litapungua, likipungua Waziri wa Fedha atapata fedha sasa ya kupeleka kwenye maendeleo ya vitu vingine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, haya yote wenzetu wamefanya, hapa Ethiopia wamejenga reli juzi, tena ni reli inayoenda kwa umeme, wamekopa China concession loan tena one percent. Wakenya wamechukua concession loan, sisi ni nani? Naamini halijaelezwa vizuri, naamini uwezo mkubwa alionao Rais Magufuli hili jambo akiamua litatokea kesho. Tutapata fedha za concession loans, tutafanya miradi mikubwa na maana yake bajeti yetu ya Serikali tutawarahisishia watu wa Wizara ya Fedha ku-balance bajeti.

Mheshimiwa Spika, jambo la mwisho ambalo naomba leo nichangie ni suala la Small Business Act. Waziri wa Fedha naomba awape zawadi Watanzania, zawadi hiyo ya kuwapa Watanzania alete Small Business Act. Ni nini maana yake? Tuamue sasa kwenye corporate tax tuweke kitu kinaitwa brackets za kodi kwamba kwa mtu ambaye ana mtaji wa milioni 10 mpaka milioni 100 mtu huyu alipe kodi labda asilimia tano. Kwa mtu ambaye labda ni milioni 100 mpaka bilioni moja alipe asilimia kumi, maana yake ni nini? Tunawa-include watu wote kwenye uchumi. Tukiwa- include watu wote kwenye uchumi tutapata mapato mengi zaidi kuliko yalivyo sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwisho nikuombe sana nimalizie la mwisho kwangu mimi ni la muhimu sana. Kwenye hoja hii ya viwanda nikuombe kuna measure kubwa wenzetu wa Kenya ambao ni washindani wetu wameweka. Wakenya wameondoa asilimia 30 ya bei ya umeme kwenye manufacturing. Maana yake ni ili viwanda vyao viweze kuwa competitive, tunajenga viwanda, lazima tuweke competition na sisi, tukiondoa hata tuondoe asilimia 40. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nimalizie kwa kusema wakati wanajenga kiwanda cha saruji kikubwa Ethiopia, Ethiopia alipewa punguzo la umeme la asilimia 60. Alipopewa punguzo hilo, bei ya saruji ilishuka kwa asilimia 70, here yamefanyika, we are not inventing the wheel. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimalizie kwa kusema nakushukuru sana, naomba niunge mkono hoja, Waziri wa Fedha namuunga mkono, bajeti yetu hii mwaka huu ni nzuri sana ni bajeti inayokwenda kujibu matatizo ya viwanda na matatizo ya kukuza biashara Tanzania.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia bajeti ya Wizara ya Elimu. Niwaombe Waheshimiwa Wabunge, tunakwenda kuandika historia kwamba na sisi tunashiriki mazishi ya kuua elimu ya Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nayasema haya nina vitabu hapa na namshukuru sana Mheshimiwa Biteko aliyeanza kulisema hili jambo. Waheshimiwa Wabunge ukiangalia vitabu hivi kwa namna yoyote ile huu ni wizi. Kwa namna yoyote ile hii ni kuua kizazi cha kesho, lakini vitabu hivi vimepitiwa na vimewekewa ithibati. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi hawa watu wa Tanzania Institute of Education, naomba leo niliombe Bunge hili tuazimie wote walioandika vitabu hivi waende gerezani, haiwezekani! Vitabu hivi wamekaa watu ma-specialist wamevitunga, wameviangalia, wanavipitisha, vinasomwa na watoto wetu, haiwezekani. Waheshimiwa Wabunge ukichukua vitabu hivi, nitawasomea sentensi chache, ‘which is wrong between a pen and a ruler’, 21st Century? Huku ndani kila unakoenda unajiuliza ni Tanzania hii kweli? Haiwezekani Waheshimiwa Wabunge. Nawaomba sana Waheshimiwa Wabunge suala la vitabu hivi tusilifanyie mzaha hata kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna sehemu hapa wanasema, ‘When, End and How”. Hata neno ‘and’ hawawezi kuandika na ni specialists walikaa wamepitisha vitabu hivi, vina makosa. Hiki kitabu cha Kingereza, hiki ni kitabu cha Jiografia. Kuna sehemu carbon dioxide imeandikwa canon dioxide, kweli jamani! Hapa kuna kitabu, standards wenyewe mmesaini, lazima kiwe na gundi, hapa wamebandika tu stepple pin na hiki chenyewe cha kujifunza na kusoma hakina hata ithibati, kina mhuri tu wa Tanzania Institute of Education. Waheshimiwa Wabunge, ukisoma makosa hapa ni mengi sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, makosa haya ni aidha hawa walioandika hivi vitabu na waliovipitisha, nadhani watakuwemo kwenye orodha ya watu wa vyeti fake. Kama hawa hawamo, then tuna tatizo kubwa zaidi. Maana haiwezekani mmekaa na mnajua Waheshimiwa Wabunge zimetumiwa shilingi ngapi, shilingi bilioni 108. Shilingi bilioni 108 za Watanzania zimeandika vitabu ambavyo havisomeki. Hivi siyo vitabu! Halafu mnataka Wabunge tukae hapa tushangilie kama mambo ni mazuri, hili lazima tulikatae. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ukishakosea kwenye kitabu tunaua generation ya kesho unless tumeamua kuwa wabinafsi. Naomba sana tuache ubinafsi, tuombe kwanza vitabu hivi viondolewe kwenye circulation ya Wizara ya Elimu. Pili, naomba sana, watu wote walioshughulika na vitabu hivi lazima waende kwenye mkondo wa sheria. La tatu, tuombe Waziri wa Elimu anapokuja hapa, hawa watu lazima walipe shilingi bilioni 108 za Watanzania, haiwezekani. Haya yanatokea kwa sababu hatujali na inawezekana kwa sababu watoto wetu hawasomi huko ndiyo maana hatuoni kama ni jambo kubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini liko suala hapa linasemwa la shule za binafsi. Nataka niwarudishwe kwenye historia, siku za nyuma miaka ya 80, 90 shule za sekondari za Serikali hazikuwepo zilikuwa chache hawa watu wa private wakaja wakatoa huduma kwa Watanzania hawa. Leo tumejenga Shule za Kata, haiwezekani sasa zile hazifai tuzitupe kwamba wale ni wafanyabiashara tuachane nao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono tuanzishe Regulatory Authority ya kusimamia standard za elimu Tanzania ili kama shule iwe na wanafunzi 45 ndiyo standard, iwe ya Serikali iwe ya private ambayo imezidisha ichukuliwe hatua. Maana sasa zinazochukuliwa hatua ni za private, zile za Serikali hawana vyoo ni sawa, hawana Walimu ni sawa, wanafunzi wako 300 ni sawa, haiwezekani! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nasema lazima tufike sehemu tutoe huduma lakini pia naomba shule hizi za private tuziangalie kwa jicho lingine. Jamani, watu hawa kwanza wanatoa service kwa Watanzania, lakini pia wanaajiri watu na wanalipa kodi. Kwa hiyo, tutengeneze utaratibu tuwapunguzie mzigo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho ni suala la kurudia darasa. Mimi nimesoma seminari wakati tunaanza tulikuwa wanafunzi 51, by the time tunafika form three tumebakia 28. Wengine wanabaki huko nyuma kwa sababu pale seminari ili upande darasa ni lazima upate wastani wa 50. Wakati tunafanya mtihani wa form two ili upande form three Serikali ilikuwa wastani ni D, seminari waliweka wastani ni C, wameamua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, cha msingi ambacho tumesema kwenye Kamati, Serikali muweke standards ili mtoto anayekwenda shule ya private anapoanza tu ile form one aambiwe kwamba hapa usipopata marks hizi hupandi darasa, mzazi akikubali amechukua choice yake yeye mzazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi kweli mnataka liwe Taifa ambalo watoto wanasoma moja kwa moja mpaka form four? Wakipata division four tunasema mwaka huu kufaulu ni kwingi sana lakini ukifanya analysis ya kufaulu ni division four. Hili Taifa ni letu wote, naombeni Waheshimiwa Wabunge tulisimamie, tusiache kuna watu pale Wizara ya Elimu wanafanya wanayoyataka sisi tunanyamaza, haiwezekani! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, maana Wizara ya Elimu ukienda kila mtu anatoa circular. Zinakuja circular nyingine hata Waziri hajui, lakini circular ilishakwenda. Ukienda TAMISEMI wanafanya wanachotaka, kila mtu anafanya anachotaka, hapana. Jamani Taifa lolote ili lionekane limeendelea ni elimu ya watu wake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naombeni sana tuzisimamie vizuri lakini tupunguze utitiri wa kodi kwenye shule za private, hawa wanatoa huduma, wanasomesha Watanzania. Kazi hii wamefanya kwa muda mrefu, haiwezekani leo ghafla tuwaache, wameajiri watu. Naombeni sana Serikali, nendeni mkakae muwaite watoa huduma hawa muongee mkubaliane vitu vya kufanya vile ambavyo Serikali inaweza kusaidia isaidie kwa sababu tutapata kwingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho niwaombe Waheshimiwa Wabunge, Waziri anapokuja kuhutubia leo aje na majibu ya kutuambia hivi vitabu vinatoka kwenye circulation. Aje na majibu ya kutuambia kwamba haiwezekani hivi vitabu vinasomwa na watoto wa Kitanzania. Lazima hawa walioandika vitabu hivi, nasikia kuna wengine mpaka vyeo wamewapa, how?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kweli, unampa cheo kwa kitabu hiki cha Kiingereza au ndiyo maana wanataka kila mtu aongee Kiswahili saa hizi maana Kiingereza imekuwa tabu. Ndiyo maana kila mtu anasema Kiswahili, Kiswahili, Kiswahili, Kiswahili, ni kwa sababu wameshafanya haya? Waheshimiwa Wabunge tusikubali kuingia kwenye historia na sisi tulishiriki kuua kizazi kijacho. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Naomba nisiunge mkono hoja mpaka Waziri atakapokuja hapa kuniambia hivi vitabu wanavifanyaje? Nakushukuru sana.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018
MHE. PETER J. SERUKAMBA – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII: Mheshimiwa Spika, nikushukuru kwa nafasi hii uliyonipa na nawashukuru wachangiaji wote, ripoti yetu imechangiwa na watu 25. Yameongelewa mengi sana, nitajitahidi kuongea yale machache ambayo wameongea watu wengi zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la kwanza ambalo Kamati yetu imelisisitiza na Waheshimiwa Wabunge wamelisema ni umuhimu wa Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote. Bado tunaiomba Serikali kama kuna zawadi Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli na Serikali yake tunaweza tukawapa Watanzania ni kuleta Bima ya Afya kwa Watu Wote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala la pili ni watumishi wa afya. Tumefanya kazi kubwa sana ya kujenga vituo vya afya na zahanati. Bahati nzuri kaka yangu Mheshimiwa George Mkuchika ametuahidi, ni muhimu sana kupata watumishi wa afya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala la tatu nataka kuipongeza Serikali kwa dhati kabisa. Serikai imefanya kazi kubwa katika uwekezaji mkubwa hasa Hospitali za Muhimbili, Jakaya Kikwete, Mloganzila, Benjamini Mkapa, MOI na Ocean Road. Pia tumejenga hospitali za mikoa, hospitali za wilaya na vituo vya afya. Kwa vyovyote vile haya ni mafanikio makubwa. Naomba niipongeze Serikali kwa kazi hiyo kubwa wanayofanya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine ambalo kama Kamati tunaiomba sana Serikali, umefika wakati tuanze kuhangaika na kinga. Wanasema kinga ni bora kuliko tiba. Tukihangaika na kinga tutapunguza gharama kubwa za afya. Ili tuweze kuhangaika na kinga lazima tuhangaike na watu wanaoitwa Community Health Workers. Hawa ndiyo wako vijijini, wanaishi na wananchi, watatoa elimu, watasaidia kwenye chanjo na wataeleza umuhimu wa usafi. Naomba nieleze tuliyoyaona Rwanda, wao hawa Community Health Workers wamesaidia kupunguza vifo vya akina mama kwa asilimia 80. Kwa hiyo, niiombe Serikali tuhakikishe tunaiangalia kwa makini kada hii na kuwasaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine ni suala la elimu. Tumeandika kwenye ripoti yetu na kila mwaka tumekuwa tunaandika na tutaendelea kuandika. La kwanza, Serikali inafanya vizuri sana kwenye kutoa mikopo ya watoto wanaokwenda vyuo vikuu. Ukiangalia nchi zote zinazotuzunguka wanazo tuzo kwa maana ya scholarship award. Naomba sana Serikali umefika wakati sasa tuanzishe scholarship award.

Mheshimiwa Spika, maana yake ni nini? Scholarship award ni watoto waliomaliza form six waliopata point tatu na point nne. Kama Serikali tuwaoneshe appreciation kwamba tumekubali wamefanya vizuri na watasomeshwa na Serikali. Tunapendekeza scholarship award hii ingeitwa Magufuli Scholarship Award. Hii itaongeza morale shuleni na kwa vijana wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine ni suala la university classification. Tuna universities nyingi sana, nadhani imefika wakati sasa tuanze ku-classify vyuo vikuu vyetu. Duniani huko universities ziko classified. Ukienda Marekani wanaitwa Ivy League maana yake ukisoma chuo hicho, hata mtu ukimwambia nimesoma Harvard kuna maswali haulizi. Kwa hiyo, nasi tutengeneze Harvard ya Tanzania kwamba labda nimesoma University of Dar es Saalam, kama ndiyo high classified hata mwajiri anasema hapa ni pazuri. Kwa hiyo, naomba tuanze kuona umuhimu wa suala hili.

Mheshimiwa Spika, niipongeze sana Serikali ya Awamu ya Tano imefanya kazi kubwa sana kwenye elimu. Wazungu wanasema access, tumetoa access, watoto wote wa Tanzania wana access kwenye education, watoto wote wa Tanzania wanapata elimu bure. Baada ya hii ya access imekuja na changamoto ambayo itaenda kwenye ubora, vyumba vya madarasa na walimu.

Mheshimiwa Spika, kwa nini nalisema hili? Tulilisema siku za nyuma, najua wengine inawezekana hawajalitafakari vya kutosha, amelisema Mheshimiwa James Mbatia na Waheshimiwa Wabunge wengi wamelisema. Nadhani umefika wakati, baada ya haya mafanikio makubwa tuliyonayo ya elimu hebu tuangalie upya mfumo wetu wa elimu, tujue kama tuna matatizo yako yapi, je, tatizo ni financing, walimu, vitabu, ni mitaala ama ni muda wa kufundisha? Tukifanya hivyo tutakuwa tume-solve tatizo la miaka 50 ijayo kama Taifa.

Mheshimiwa Spika, huwa napenda kutoa mfano, mwaka 1981 Rais Reagan aliangalia hali ya Marekani ilikuwa inadorora kwenye world stage kwenye education wakaanzisha Tume ya Elimu ambayo ilifanya kazi kwa miezi 18 ikaja na ripoti na ripoti hiyo famous, inaitwa ‘A Country at Risk’. Taifa kubwa liliangalia likaona hapana tunakokwenda tutashindwa kuangalia.

Mheshimiwa Spika, sasa na sisi imefika wakati wa kuliangalia suala hili la elimu yetu. Watoto wetu wanamaliza chuo kikuu hebu tu-taste output. Maana wakati unafanya huo uchunguzi wata-taste output, je, lazima watoto wote waende university hakuna tertiary education? Maana tuna tatizo la ajira na tuna watoto wengi wana degree lakini pamoja na tatizo la ajira hatuna mafamasia, mafundi mchundo na wafanyakazi wa hoteli wazuri. Haya yote yatawezekana iwapo tutaunda Tume ya Elimu na kwa kweli itatusaidia sana na tutakuwa tume-solve tatizo la miaka mingi ijayo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala la walimu wa hesabu na sayansi, tunarudi hapo hapo. Inawezekana tukasema tatizo letu ni walimu wa hesabu na sayansi lakini inawezekana hilo si tatizo peke yake. Pengine tunasema tatizo ni maslahi ya walimu inawewezekana siyo tatizo peke yake. Tunaishawishi Serikali ione umuhimu wa kuleta Tume ya Elimu ili tuangalie mfumo wetu wote wa elimu kuanzia kindergarten mpaka university tuone kama liko tatizo liko wapi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tumefanya vizuri sana wanasema kwenye hard infrastructure. Tunajenga reli, umeme na barabara; these are the hard infrastructures. Umefika wakati tuwekeze vya kutosha kwenye soft infrastructure ambazo ni pamoja na education. Nchi zote zilizoendelea miaka ya 60 siri yao namba moja ni elimu. Kwa hiyo, niombe sana tulifanyie kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine ni suala la utafiti. Tulikubaliana tupeleke asilimia moja ya GDP. Hata hiyo tunayoipeleka inazidi kupungua. Suala la utafiti ni muhimu sana.

Mheshimiwa Spika, nimalize kwa mambo mawili. Moja, hapa Bunge wakati tumeanza 2016 tulitunga Sheria ya Vyombo vya Habari. Nimuombe sana Waziri wa Habari, Michezo, ile sheria ilipigiwa kelele sana lakini ilikuwa ni sheria nzuri sana kwa ajili ya kusimamia waandishi wa habari na vyombo vya habari. Tunajua Kanuni zimetungwa na sheria ile ilitaka tutunge vyombo fulani vya kusimamia wandishi wa habari, mpaka leo vyombo vile havijatungwa. Kwa hiyo, niwaombe Serikali wajitahidi watunge vyote vile ili tuanze kusimamia hii kada na tuendeleze weledi katika vyombo vya habari.

Mheshimiwa Spika, mwisho ni michezo. Nimewasikiliza Waheshimiwa Wabunge wengi sana waliozungumzia suala la michezo. Michezo ni ajira. Mwezi Aprili tunakwenda kwenye mashindano ya AFCON lakini tuulizane maswali, timu yetu iko kambini?

WABUNGE FULANI: Hapana.

MHE. PETER J. SERUKAMBA – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA
JAMII: Tunawezaje kushinda ikiwa mpaka leo hatujaenda kambini? Michezo iko Aprili leo ni Februari, mnataka tushindane tukiwa tumeanza kambi wiki moja kabla? Ni lazima kama nchi tuwekeze kwenye michezo na tuongeze bajeti ya Wizara ya Michezo. Tukifanikiwa hapo ninayo hakika vijana wengi watakwenda kucheza kimataifa wataleta dola nchini na kwa kweli itakuwa ni ajira ya uhakika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, nami niwashukuru sana wote waliochangia na kwa vyovyote vile wamekubali tuliyoyapendekeza kama mapendekezo yetu ya Kamati. Pia niwashukuru sana Mawaziri, Mheshimiwa Waziri Ummy, Mheshimiwa Profesa Ndalichako na kaka yangu Mheshimiwa Harrison Mwakyembe. Nawashukuru sana kwa ushirikiano mnaotupa kwenye Kamati yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimemsikia Mheshimiwa Waziri Profesa Ndalichako anasema hukukosea kutuunda Guantanamo na naamini Mheshimiwa Spika hukukosea. Watu wanajituma sana na unajua ukishatengwa na ukapelekwa gerezani inabidi muungane ili mfanye vizuri zaidi. Hiyo ndiyo huwa sifa ya watu waliotengwa, wanaungana na wanafanya vizuri zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naomba nitoe hoja kuomba Bunge lako Tukufu liweze kupitisha mapendekezo yetu yote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi)

MHE. MWANNE I. MCHEMBA: Mheshimiwa Spika, naafiki. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru kwa kunipa nafasi, leo ntaongelea kodi. Mheshimiwa Mwijage anafanya kazi nzuri sana kutafuta wawekezaji, lakini wawekezaji ili waweze kuja Tanzania ni lazima tuangalie mfumo wetu wa kodi. Mfumo wetu wa kodi si rafiki kwa wawekezaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukijenga kiwanda ukataka wakati unajenga uanze kupata kodi haiwezekani. Duniani kote wameondoka kutoza kodi kwenye production, unatoza kodi kwa yale yatakayotokea baada ya ku-produce. Sasa sisi tunataka mtu anafika siku ya kwanza tu na kodi ianze, matokeo yake Tanzania hatutabiliki katika mazingira ya uwekezaji. Mabadiliko ya Tanzania yanakuja kila mwaka; mwaka huu tutasema tunaondoa vivutio, mwaka kesho vinarudi, mwaka kesho kutwa vinaondoka, hakuna ambaye anaweza akaja.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitawapa mfano wa vitu vichache. Mwaka 2009 tuliondoa vivutio kwenye kodi ya deemed capital goods, uwekezaji ukashuka. Mwaka uliofuata tukarudisha, uwekezaji ukapanda. Hata hivyo, sisi tuna TIC ambayo inatoa certificate, lakini TIC inatoa certificate ambayo Waziri wa Fedha haitambui. Sasa, tuko kwenye Serikali moja, niwaombe watu wa Serikali; Waziri wa Viwanda na Biashara pamoja na Waziri wa Fedha tukubaliane vivutio gani vinawekwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimemsikia hapa Mzee Deo Sanga anaongelea habari ya Mchuchuma na Liganga, Mzee Sanga tatizo ni vivutio, utapiga kelele, lakini haiwezekani; kwa sababu TIC wamewapa vivutio, Waziri wa Fedha hajakubali, sasa tunafanyaje? Kwa hiyo, niwaombe na ningekuwa na muda ningesema hata vifungu ambavyo vinakubalika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna suala la VAT; Sheria yetu ya VAT haitambui suala la bidhaa za mtaji na capital goods na deemed capital goods hawatambui. Juzi walikuja wale ambao wanatengeneza magari Kenya, Volkswagen walitaka kuja Tanzania, walikutana na Mheshimiwa Mwijage mmekubaliana weee, walipofika sasa kwenye vivutio, Waziri wa fedha akaweka nanga, wakaondoka. Mwisho wake sasa tunamlaumu nani?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nasema kwamba naamini nia ya kuleta uwekezaji ni njema, nia ya kukuza viwanda ni njema, lakini nia njema hii tuipeleke kwenye sheria ili hadi kuanzia chini Mkuu wa Wilaya mpaka mtu wa juu aongee kivutio cha namna moja. Unapoongelea Tanzania tukisema vivutio, across the country tunaongea jambo moja. Leo kuna vivutio vya Mwijage, kuna vivutio vya TIC na kuna vitutio vya Waziri wa fedha inawezekanaje kwenye nchi moja?

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sana sana na matokeo yake sasa ya kutokuwa na kutabirika; moja, wawekezaji mahiri hawawezi kuja Tanzania; mbili, wawekezaji walioko kwenye sekta ambazo bidhaa zake hazitambuliwi na VAT hawawezi kuja Tanzania; na tatu, tumeumiza usafirishaji na tourism in Tanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, usafirishaji mwaka 2015 wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne tulikuwa na malori 23,000 yanafanya kazi kwenda kupeleka mizigo, leo yamebaki malori 11,000 kwa sababu gani kwa sababu ya VAT kwenye auxiliary basi, kwa sababu gani kwa sababu ya single custom ya Congo, sasa tunamuumiza nani? Naomba Serikali mkae, sheria zetu tuzioanishe ili ziweze kufanya kazi ili tuweze kwenda mbali katika kujenga uchumi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitatoa mifano michache; nimelisema hili la Mchuchuma nadhani wenzangu wamelisema. Ethiopia, Dangote alikwenda Ethiopia akapewa vivutio, akapewa na bei ndogo sana ya umeme watu wakashangaa akazalisha cement, bei ya mfuko wa cement ikashuka kwa 60%. Watakaofaidi ni watu gani? Ni wa Ethiopia.


Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, unakosa kodi hapa unapata kule mbele, production ikiwa kubwa watu watajenga nyumba sana watu watanunua cement, tutapata tu kule mbele, unless mtuambie hii shule ya uchumi mliyosoma nyie ni ipi ambayo wengine hatuijui? Mtuambie leo. Ningetamani Mheshimiwa Waziri wa Fedha awepo hapa leo, asimame atuambie shule yake ya uchumi ambayo wengine wote hatuijui ni ipi? Maana haiwezekani tunaenda huku tunarudi? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye suala la ngozi na Mheshimiwa Mwijage amekwenda Ethiopia, Ethiopia leo ni big exporter wa product za ngozi kwa sababu gani? Nendeni m-google wanatoa incentive, wanatoa tax holiday kwa asilimia nyingi sana, lakini matokeo yake export imeongezeka, dola inakuja nyingi in the country wana-manage their economy. Sisi tunataka tupate kodi leo kabla haiwezekani haiko dunia unayoweza ukapata kodi kabla hujazalisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini juzi kwenye suala la wafanyabiashara Mheshimiwa Rais amesema maneno yafuatayo:- Rais amewaambia Watanzania mkishindwa kujenga viwanda, mkishindwa kufanya uwekezaji Tanzania wakati wangu, hamtoweza wakati mwingine wowote. Sasa maneno makubwa haya ya Mheshimiwa Rais yawekeni kwenye sheria, kayawekeni kwenye utekelezaji, maana tutaonekana huku tunaongea maneno mazuri, ukija na fedha zako unaanza kupigwa maneno.

Mheshimiwa Naibu Spika, Tanzania tuna ardhi, Tanzania tuko well located as a country, tuna madini, tuna gas, tuna misitu, tuna tourism, kutokwenda kwa kasi hatuna maelezo na hatuna maelezo kwa sababu moja tu, kwa sababu hatuna vivutio, hatuna strategy. Ukisoma mkakati wetu mzuri sana na sisi Mungu alitujali, ukisoma development plan ya miaka mitano, ya mwaka mmoja superb, ukisoma ripoti hapa ya Mwijage superb lakini nenda kwenye utekelezaji hapo ndio penye mashaka.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, namwomba sana Waziri akae na wenzake Serikalini waviangalie hivi vivutio, waangalie haya mazingira ya uwekezaji…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, ningesema habari ya NEMC, NEMC nayo ni kikwazo kwenye uwekezaji nchini NEMC, inakwaza nchi hii...

NAIBU SPIKA: Haya. Ahsante sana,
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa uliokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili nichangie kwenye Mpamgo wa Taifa wa mwaka 2020/2021. Kwanza naomba nimpongeze Waziri wa Fedha kwa kuja na mpango mzuri, leo nitatoa ushauri kwa badhi ya mambo. Nimeusoma mpango wetu, nashauri sasa nadhani umefika wakati kwenye mpango ningetamani tuoneshe mwaka kesho baada ya mwaka mmoja kama ambavyo tumesema tutajenga barabara, tunajenga madaraja, lakini nataka tuoneshe production, kwa sababu ili tuweze kupata fedha nyingi tuweze kuendelea cha kwanza lazima tuhakikishe production yetu kwenye mpango wetu ionekane na hapa nitatoa mfano kwenye kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kila mwaka tunakaa hapa tunapitisha Bajeti ya Kilimo, nadhani umefika wakati kwenye mpango basi tuseme kwa mfano kwenye kahawa; kwenye kahawa tunataka tuafanye kazi ili mwaka kesho tutoke kwenye tani 50,000 twende kwenye tani 200,000, lakini hili kwenye mipango yote haionekani na ndiyo maana kwa miaka yote minne kahawa haijawahi kuzidi tani 60,000, lakini wenzetu Uganda ni tani 2,88,000. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, twende kwenye chai; tunazalisha chai tani 19,000, tani 20,000 au 25,000; wenzetu Kenya hapa ambao sisi tuna ardhi zaidi, wanazalisha tani 350,000. Sasa lazima na sisi tunapokuwa tunapanga, tupange kwa kuweka matarajio, haiwezekani tunajadili tu kilimo, lakini tuweke deliverables ili tuweze kuwapima hawa wenzetu. Tukifanya vizuri kwenye kilimo nina hakika tutapata export nyingi, tutapata fedha za kigeni na kwa sababu hiyo balance of payment itaondoka kwenye negative. Tanzania kama nchi katika vitu ambavyo ni advantage kwetu cha kwanza tuna ardhi kubwa sana, Tanzania tuna maji mengi sana, Tanzania tuna mifugo, sasa kama tuna vitu vikubwa hivi vitatu, lakini zaidi ya hapo tuna jiografia ya Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lazima tunapopanga tupange kuona ambavyo vitu hivi vitatu kwenye mifugo, itatuletea nini baada ya mwaka mmoja, bada ya miaka mitano, hatuwezi kuwa tunasema kuwa ni wa pili Afrika tuna mifugo lakini ukienda kwenye mchango kwenye GDP, ukienda kwenye mchango wa pesa ya mmoja mmoja siyo kubwa. Tuna uvuvi, wenzetu tukienda kujifunza hata pale Namibia, wanafanya uvuvi mkubwa sana kwenye bahari kuu, sisi tuna eneo kubwa la bahari kuu lakini tujiulize maswali, mwaka huu tulivua kiasi gani mwaka kesho tutavua kiasi gani. Kama hatujiwekei namna ya kwamba mwaka huu tutoke hapa kwenda pale, tutakuwa kila siku tunajadiri tunamaliza mpango tunakwenda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nakuja na mawazo kwamba umefika wakati Wizara ya Fedha inapokuwa inapanga mpango tuwekeane, wakae na Mawaziri wasainiane mikataba kwamba tunataka kwenye kilimo, kwenye kahawa iwe hivi, kwenye katani iwe hivi, kwenye mkonge iwe hivi. Kwa mfano mkonge sasa hivi, una bei kubwa sana kwenye soko la dunia, lakini unajua tunazalisha tani ngapi? Tunazalisha tani 34.6 kwa mwaka, wakati ardhi tuliyonayo tunaweza tukazalisha tani milioni moja na hela hii ikaingia kwenye economy. Ardhi tuliyonayo tunaweza tukatoka, leo korosho inaleta fedha nyingi sana, lakini korosho ni tani ngapi, laki mbili, laki tatu, lakini uwezo tulionao tunaweza tukaenda tani milioni moja. Sielewe watu wanaopanga mipango yetu kwa nini hatujiwekei target, tukiweka target nina hakika tutafanya vizuri sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania haikuwa bahati mbaya kuwepo hapa ilipo, jiografia yetu lazima tuitumie kukuza uchumi; hatuwezi kuwa tunasema tuna amani, nchi imetulia, tuna jiografia nzuri, lakini inaleta nini, tuangalie tunafanye biashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine nimelisema kila nilipoingia kwenye Bunge hili, ni suala la miradi ya PPP. Kwenye miradi ya PPP sielewi kuna ukakasi gani Serikalini, kwa sababu PPP wako watu wanasema tumeshajaribu PPP ukisikia inatajwa wanataja TANESCO, haikuwa PPP ilikuwa ni management, wanataja RITES, RITES haikuwa PPP ilikuwa ni management, wanataja maji ya Dar es Salam City Water, hiyo haikuwa PPP, it was a management. PPP ni lazima mtu alete fedha, awekeze, azalishe, mgawane na mfano thabiti wa PPP ni daraja la Kigamboni, tumefanya, Serikali na NSSF na watu wanalipa pale, lakini wananchi hawajazuiliwa kwenda kupanda pantone, mwenye haraka ataenda kwenye daraja. Tukifanya hivi tuta-leverage haya tunayofanya leo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitatoa mifano, leo Mheshimiwa Rais anafanya miradi mikubwa sana mmoja ukiwepo mradi wa maji wa Nyerere wa Rufiji, jambo jema, jambo nzuri sana. Hata hivyo, lakini ukisoma sera ya Tanzania ya mwaka 2003 sera ya energy inasema energy mix maana yake nini? Tuna geothermal, tuna upepo, tuna gesi, tuna makaa ya mawe, mpango wetu unasemaje? Kama hatuna fedha kwa sababu tunafanya kwenye maji tutafute watu wafanye, wakifanya tutagawana zile fedha na Tanzania tutapata umeme mwingi. Nataka niwaambie leo wenzangu umeme ni bidhaa, umeme ni biashara, nina hakika tukizalisha umeme mwingi tutauza Kenya, tutauza Uganda, tutauza Rwanda, Burundi, Kongo, Zambia na Malawi, tunaweza, lakini hatuwezi kuyafanya yote kwa wakati mmoja lazima mengine yafanywe na PPP.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo barabara, tumekalia tunataka kila kitu kijengwe na Serikali, wewe umetembea duniani barabara za express way zipo; hivi tunaona tabu gani kujenga express way ya Dodoma Dar es Salam halafu hii barabara ya zamani iendelee kuwepo mwenye haraka atakwenda kwenye kulipia, wako watu wanakuja na hoja kwamba tunajenga SGR hakuna ya barabara siyo kweli hata kidogo, nenda China bigger as it is population one point four billion people wanajenga mabarabara, wanajenga reli yanaenda kwa kasi, reli haiwezi kuchukua nafasi ya barabara, wala haiwezi kuchukua nafasi ya ndege, vyote tunavihitaji kama Taifa. Ili mtu akitoka hapa aende Mwanza haraka, akitaka aende taratibu kuna barabara hii atakutana na ma Traffic, hii ya haraka atalipa, shida iko wapi? Leo wenzetu Uganda kutoka Entebbe kuja Kampala wamejenga express way, maana yake kule watu watalipia, lakini ile barabara ya zamani itaendelea kuwepo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niwaombe wenzangu PPP ni lazima, ndiyo way to go kama nchi. Kama na kwa sababu PPP itatusaidia, leo Serikali inajenga sana hospitali kila mkoa, kila wilaya, hivi tunaona tabu gani kuingia PPP mtu akaleta vifaa; kwamba vifaa vile yeye ndiyo anahangaika na vifaa, teknolojia ikibalika atalipisha yeye, kinachotokea yeye anaweka hela zake. Kwa hiyo maana yake tunaweza tukajenga hospitali nyingi zaidi kwa sababu vifaa ni gharama, lakini somebody yes will do it for us. Kwa nini wenzetu hawataki kuhangaika na PPP? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niongelee miradi mitatu, ukisoma kwenye Mpango haitajwi sawasawa. Mradi wa kwanza ni wa LNG plant wa gesi kule Lindi, Mradi wa pili ni Mchuchuma na Mradi wa tatu ni Engaruka. Nataka wenzangu tuelewane miradi hii mitatu leo ingekuwa inatekelezwa ni zaidi ya bilioni 40 zingekuwa kwenye economy yetu. Leo Tanzania kila mtu angekuwa ana kazi, leo Tanzania shilingi yetu ingekuwa na thamani kwa sababu kuna dola nyingi zingekuja in our economy.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo ukienda Msumbiji muuza hata toilet paper ni tajiri pale Msumbiji kwa sababu ya Mradi wa LNG, watu watasema tatizo ni mikitaba, mimi nasema mikataba kwa Awamu ya Tano ya Mheshimiwa Magufuli itakuwa mizuri tu, kwa nini tusi-negotiate, hatuwezi kuwa tunakaa tunasema tatizo letu ni mikataba mibaya, hapana, mikataba tuisahihishe mbona mkataba wa Barrick tumeubadilisha. Tunaogopa nini ku-negotiate vizuri na haraka kwenye LNG, huku kwenye Mchuchuma huku kwenye Engaruka, tunaogopa nini? Tatizo ni nini na hatutumii fedha zetu somebody yeye si analeta pesa. Pia kinachotokea tukitekeleza hii miradi, mradi wa PPP wa reli kutoka Mtwara kwenda huku Liganga utawezekana, lakini kama Liganga haiwezekani hiyo reli haitokuwepo. Hata Mradi wa Bagamoyo tukiamua kufanya hii miradi tuka-renegotiate upya, tuwaondoe wale wezi tulete watu wazuri, hii miradi tunaihitaji kwenye hii economy. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme mambo mawili makubwa; naomba sana wenzetu mpango wetu lazima uje na mambo makubwa mawili, lazima mpango uwe clearly kwenye job creation, mpango lazima uwe clearly kwenye foreign currency tunazipata wapi, kwa maana exports, kwa sababu kama hatutengenezi jobs, tunasomesha kila siku hizo kazi zitatoka wapi? Lazima PPP ndiyo ije na ili PPP ije mambo mawili yafanyike; moja, lazima tuangalie sheria zetu upya, tuweke legal framework yenye clarity, pia tuhangaike na education kwa maana kuandaa skills zitazofanya kazi kwenye hivyo viwanda vipya, kwenye hiyo miradi mikubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa wale mnaojua trend ya dunia, trend ya duni sasa hivi kule China gharama za kazi zimeanza kupanda kwa sababu wanakwenda first world; Asia, India gharama za kazi zinapanda maana yake ni nini? Wanakuja Afrika lakini watakakokuwa wamejiandaa, ndiyo maana leo unaanza kuona viwanda vikubwa vinatoka China vinakuja Ethiopia kwa sababu wamejiandaa, wameweka mazingira wezeshi na kwa kufanya vile wanapata jobs, wanapata technological transfer, pia above all wanaweza kupata hela za exports. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya yanawezekana, naamini tukiamua haya yanawezekana, naomba mpango wetu uhangaike na haya mambo, kwangu mimi ni makubwa sana. Niseme, umefika wakati siyo vibaya ku- copy vitu vizuri, ukisoma historia nchi zote zilizoendelea miaka ya 60; China, India, Singapore, Malaysia, South Korea, vitu vitatu vimewapeleka haraka sana. Cha kwanza wame-embrace free market na free trade, wameweka tu governance ya kuhakikisha inafanya kazi vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, cha pili ni pragmatism, hii means yake what? Maana yake ni kwamba, hutojali kama huyo paka ni mweusi ama ni mweupe, cha msingi akamate panya tu. Kama mtu anaweza akaja akajenga barabara, express way kwa hela zake, shida yetu nini? Mtu akishajenga barabara hawezi kuibeba akaondoka nayo, mtu akija akawekeza LNG plant hawezi ku-assemble akaondoka nayo haiwezekani, lakini pia lazima tuanze ku- impress meritocracy, tuanze kuhangaika na watu wenye maarifa, tutengeneze Taifa ili lihangaike na watu wenye maarifa, tuweze kwenda haraka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naamini kama Tanzania kipindi hiki cha Mheshimiwa Rais Magufuli, ni Rais anayefanya maamuzi, ni Rais mwenye nia ya kutaka kuleta maendeleo kwa kasi, ni jukumu letu sisi Wabunge na watu wa Serikali, tumsaidie aende kwa haraka. Haya anayoyafanya lazima yawe leveraged na kitu kingine na kwa sababu anafanya maamuzi haraka, naombeni Serikalini na ninyi mfanye maamuzi haraka. Nchi hii itaenda kwa kasi sana kwa sababu tuna kila kitu unachoweza kusema hapa duniani, tuna madini, tuna gesi, tuna everything, kwa hiyo mipango yetu iwe ya kusaidia kwenda haraka kwenye maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho ni suala la, kuna kitu kimeletwa Serikalini Mheshimiwa Waziri Mkuu amekianzisha kinaitwa MTAKUWA. MTAKUWA ni utaratibu wa kuhangaika na kuondoa unyanyasaji wa akinamama na watoto ni initiative kama ilivyo initiative ya UKIMWI, lakini nimesoma mpango wote hawaongei chochote kuhusu MTAKUWA. Taifa lolote lenye heshima ni Taifa ambalo linajali haki za watoto, haki za akinamama na haki za jinsia yote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo naomba kwenye Mpango na bajeti ijayo kila Wizara ije na gender budget statement, tuoneshe tunavyojiandaa kuhangaika na mambo haya, huu ndio ustaarabu, hamwezi kuwa na Taifa la watu kila siku akinamama wananyanyaswa; watoto wananyanyaswa; ukiyasikiliza yanayotokea huko ndani, sio Taifa la Tanzania. Naombeni tukusanye nguvu za kifedha, za mikakati, za kisheria, kuhangaika na unyanyasaji wa akinamama na watoto. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi na naunga mkono hoja. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Spika, na mimi nakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuchangia Bajeti ya Serikali, kwanza naomba kwa dhati kabisa nimpongeze Waziri wa Fedha kwa speech nzuri sana, lakini pia nimpongeze kwa kusikia kilio cha Wabunge toka tumeanza kuondoa tozo zote, tozo 54. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini pia nimpongeze Waziri wa Fedha kwa mara ya kwanza tumekuja tunafanya bajeti, siyo bajeti ya pombe, siyo bajeti ya sigara, hongera sana ndugu yangu, lakini la pili niipongeze Serikali kwa barabara ya Kigoma - Nyakanazi; naishukuru sana Serikali kwa kutukumbuka watu wa Kigoma, nadhani umefika wakati sasa tuhangaike na barabara ya Mwandiga, Chankere, kwenda Kagunga kwa sababu tutapitia pale gombe ambayo itasaidia sana kwa maana ya utalii nawashukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini nimesoma vitabu vyote hivi vya bajeti, nimesoma Mpango wa Taifa kuna maeneo mimi nadhani ningeomba Serikali tuyawekee mkazo unaostahili, tukiyawekea mkazo unaostahili tutapata fedha nyingi sana na mimi leo nataka nijikite kwenye growth na production. Nadhani umefika wakati Serikali tuhangaike na growth na production kwenye kilimo nimeingia Bungeni hapa huu mwaka Mungu akinijaalia mwaka kesho utakuwa mwaka wa kumi na tano, haiwezekani kila mwaka nimechukua mazao machache, kila mwaka uzalishaji wa kahawa, hauzidi tani 50,000; uzalishaji wa chai, tani 19,000; pamba haizidi tani 300,000; mkonge haizidi tani 36,000 na korosho haizidi tani 210,000. Nimeamua kuchukua haya machache. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nadhani Waziri wa Fedha umefika wakati ukae na Waziri wa Kilimo tupeane utaratibu kwamba ili tumpime Waziri wa Kilimo mwaka kesho tunataka aongeze tani za kilimo akishindwa then tujue wewe hutufanyii kazi yetu, sasa yeye ndiyo aseme hili niweze kuzalisha tani hizo nyingi ninahitaji uwekezaji huu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naona suala la growth hatuhangaiki nalo, siyo sawa, maana hata hii kodi tunayotafuta kama hakuna growth, hakuna production ni kwamba tutaendelea kushikana mashati tu, wenzetu wanafaidi kwa sababu ya economies of scale kwamba hata bei ya dunia ikianguka kwa sababu umezalisha sana bado hutopata taabu.

Suala la pili ni suala la samaki, ukisikiliza hapa ni suala la Waziri wa Uvuvi anahangaika na wavuvi kuchoma nyavu, kukimbizana nao, toka tunaingia ndio kazi tunafanya, lakini leo wenzetu Kenya na Uganda wameanza namna mpya ya kufanya uvuvi, wanafanya vizimba. Maana yake ni nini kwa kufanya vizimba Uganda wamekwenda wamechukua wataalamu Kenya wamewapeleka Uganda kufundisha namna ya kutengeneza vifaranga na kuvigawa bure kama Serikali Kinachotokea leo Uganda na Kenya wataanza export samaki kuliko sisi hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sisi tuna Tanganyika, tuna Lake Victoria, tuna Nyasa kwa kweli kutohangaika na hili hatuhangaiki kuondoa umaskini wa watu, tukihangaika na suala la vizimba (cage) wanasema fishing caging fishing ninayo hakika kama Tanzania tutaongeza fedha nyingi za kigeni kwa ku-export samaki, lakini angalia nguvu zetu zinaenda wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwenye kuchoma nyavu, kwenye kukamata watu na vipuri vyao, kukamata watu na mashine zao, huko ndiyo nguvu tumepeleka, huko ambako tungepeleka tupate pesa wala hatuendi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tukifanya vizimba niwaambie kitakachotokea uvuvi ndani ya maziwa yetu kwa maana ya samaki wataendelea kuwapo kwa sababu ukishakuwa na cage unalisha pale moja kwa moja vinaanguka chini na samaki wengine kule chini wanakua, haya hatufanyi. Kupata kibali cha kuanzisha caging ni shughuli kubwa sana sasa mimi sielewi tunafanya nini? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine ni suala la utalii, hivi leo tuulizane Waheshimiwa Wabunge na hii naisema kwa nia njema kabisa, ukiindoa Zanzibar fikiria tungekuwa hatuna Muungano huu, maana yake tungekuwa hatuna utalii wa bahari, beaches Tanzania hazipo, lakini we have the longest beach kuanzia Tanga mpaka Mtwara tunafanya nini? Beach zipo Mungu ametuumba nazo lakini we do nothing. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, so nadhani umefika wakati watu wa Wizara hii waje na mkakati wa kufanya tuwe na beach hotels, tuwe na beach tourism Mungu ametupa, hajatupa kwa bahati mbaya.

Mheshimiwa Spika, kutotumia ni dhambi na mimi nataka leo ni-suggest Serikali tuna mbuga nyingi sana Spika wewe hili unalijua sana, mimi nataka niishauri Serikali tuamue kwamba Ngorongoro na Serengeti ukitaka kwenda kule tuweke kwa watu wenye fedha, tuseme ukiingia kule ni dola 1,000, dola 2,000; tutapata pesa tutashangaana hapa, wale ambao hawana uwezo, hawana fedha iko Mikumi, Selous, Tarangire, iko wapi waende huko, kwa sababu wanyama watawaona, iko Katavi, Ruaha waende huko, lakini ukitaka kwenda Serengeti, Ngorongoro tuseme ni for high and kitakachotokea na mimi nasema hii imetokea Rwanda. Rwanda hawana vitu vya maana, wana nini, wana chimpanzee peke yake, walianzisha dola 750 kwa ajili ya kwenda kuona, ikawa over subscribe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Kagame amekwenda Marekani kakutana na watu pale seekerville wakamwambia unaweka hela ndogo ndiyo maana wengine hatuji, wameweka dola 1,500 bado kunajaa, maana yake nini, matajiri hawapendi kubanwa, matajiri hawapendi kuzungukwa na watu wengi. Kwa hiyo bado unaweza ukasema kwa mbuga zetu hizi mbili nitaweka tu hawa na nina hakika watajaa na tutapata pesa nyingi sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala la biashara, nimemsikia rafiki yangu hapa amesema vizuri sana Mbunge wa Gairo.

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Shabiby.

MHE. PETER J. SERUKAMBA: ...Mheshimiwa Shabiby na mimi nataka niende kwenye angle moja, juzi Mheshimiwa Rais alifanya jambo kubwa la kihistoria alikutana na wafanyabiashara, moja ya mambo muhimu sana Rais amesema sijui kama naona hamna anaye-pick up, Rais amesema anatamani akimaliza muda wake atengeneze mabilionea 100. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Rais anatamani Watanzania waende kuwekeza Kenya, waende kuwekeza kwenye SADC, waende kuwekeza kote Afrika, sasa ukitaka kwenda kuwekeza leo nje ya Tanzania, kupata vibali pale BOT ni shughuli kubwa mno, leo una fedha zako kwenye bank account, there is a business unataka kwenda kuwekeza Burundi, brother kupata vibali BOT ni shughuli kubwa mno, kuna over regulation, ukiweka over regulation huwezi kuendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hizi nchi ambazo bado tunakua lazima kuwe na flexibility, leo hapa amesema habari ya magari yote yanakwenda yanaji-register Rwanda na Zambia, nikwambie ukiwa na magari ya transport Rwanda unalipa kodi hii, moja tu shilingi milioni moja basi, hakuna Corporate Tax, hakuna nini, ni shilingi milioni hii mmemalizana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo ukiwa na magari 100 wana milioni yao mia moja unaenda unalipa shughuli imeisha, wewe ungekuwa mfanyabiashara utaacha kwenda huko, njoo hapa kwetu, kuna Corporate Tax, kuna OSHA, kuna nani, kuna service levy yote haya ni huyo mwenye magari. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo kwa maana ya mfanyabiasha yeyote atakwenda huko, nataka kusema kama tunataka kwenda huko lazima tufanye kama wenzetu, lakini nataka nipendekeze na amesema hapa Mheshimiwa Shabiby suala la VAT kwenye petrol stations mimi niwaombe Serikali na Waziri naomba hili ulitafakari sana, hakuna mwenye petrol station ambaye anajiuzia mafuta? Wote mafuta wanachukua kwenye depot, kama wewe ni mtu wa PUMA unachukua PUMA, kama ni TOTAL unachukua TOTAL. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo leo Serikali ukienda pale PUMA ukamuuliza swali moja tu una petrol stations ngapi atakwambia 50, nipe sales zao au walivyoagiza mafuta kwa mwaka anakupa list yako, akishakupa anakupa na cost unaijua kwa sababu una EWURA, maana yake ni nini, unajua kwa kituo hiki kwa mafuta aliyouza labda lita milioni moja kwa mwaka alipata faida kiasi hiki, atakuonesha cost zake analipa kodi, rahisi tu, rahisi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini hii tunaweka, haya amesema naweza mafuta yasifike kwenye petrol station na bado hiyo EFD mashine wala isifanye kazi, so mimi ninachosema tutafakari umefika wakati tupunguze gharama za kukusanya kodi, kwa sababu gharama za kukusanya kodi nazo kubwa sana, kwa hiyo niombe hilo watu wa Wizara ya Fedha mtusaidie. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi niseme, namshukuru Rais na amesema vizuri sana, tunahitaji tuwe na marafiki na wafanyabiashara, naombeni sana unajua kwa miaka minne hii, nimekuwa namsikiliza sana Naibu Waziri wa Fedha akiwa anajibu hoja Bungeni hapa, siku zote suala la biashara kufungwa halijawahi kumshtua huyu mama hata siku moja, anasema biashara zitafungwa, tunafungua zingine. Ni sawa, lakini jamani hivi kuna nyongeza mbaya? Kama biashara ipo halafu ukafungua zingine hivi ni dhambi? Kwa nini ujidai kwa kufunga? Kama unaona ni faraja nimefunga why? Lakini tunasahau biashara inayoanzishwa leo haileti kodi hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini tunasahau, biashara ikianzishwa leo haileti kodi hiyo, biashara ikianzishwa leo hailipi kodi, lakini yule aliyekuwepo huyu tuna historia naye. Kwa hiyo mimi ningewaomba sana Waziri ndugu yangu tujitahidi tusifunge biashara na hii habari na mimi naomba sana, hii habari ya kuwa-involve TAKUKURU, watu wa vyombo vya ulinzi kwa ajili ya kodi siyo sawa. Kodi tuwaachie wafanyakazi wa kodi, kodi tuwaachie watu waliosoma kodi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, maana leo unasikia pale Wizara ya Fedha wamepangishwa foleni wafanyabiashara, kwani ungemuita Ofisi ya TRA akaenda akakutana na mtu wa TRA kuna dhambi gani, why uwatishe, saini hapa, tunakupa siku saba, uwe umelipa, hii siyo sawa, hii siyo sawa na naamini Mheshimiwa Rais hili halijui, kwa sababu Rais anataka dialogue kwamba wewe njoo ufanye biashara na mimi nifanye biashara na wewe. Naombeni watu wa kodi tubadilike. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la mwisho naomba sana suala la Marekani kuna kitu wanaitwa Small Business Act, Waziri wa Fedha naomba utafakari kuleta Small Business Act, kwamba Corporate Tax ni thirty percent, inawezekanaje ACACIA alipe thirty percent na Serukamba Company alipe thirty percent ni watu wawili tofauti hawa, tutengeneze utaratibu kulingana na mitaji ya watu. Tunasema kuanzia mtaji wa milioni mpaka milioni 20 blacket yake iwe hii, kutoka milioni 20 mpaka milioni 100 iwe hii, kutoka milioni 100 mpaka bilioni moja iwe hii, bilioni moja and above iwe hii, maana yake ni nini, watu wana- graduate akifanya vizuri zaidi anapanda kule, on doing this tutawa-incoporate watu wote wataingia kwenye wigo wa kodi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimalizie kwa kusema na mimi hii nairudia tena, Watanzania wengi wote, Watanzania wote wanalipa kodi, tofauti yetu kuna anayelipa direct tax kuna anayelipa indirect tax. Mtu yeyote anayenunua sukari analipa kodi, ukinunua soda unalipa kodi, ukinunua mkate unalipa kodi, wote na ndiyo maana nchi zilizoendelea kama kuna eneo wanahangaika nalo ni suala la employment. (Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Spika, ukihakikisha watu wako wana kazi, maana yake wana purchasing power, wakishakuwa na purchasing power watatumia, wakitumia watalipa kodi. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana.

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo na mimi namshukuru sana Waziri wa Fedha, nampongeza sana yeye na watu wake Wizarani kwa kazi kubwa wanayofanya, nakushukuru. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Maji na Umwagiliaji
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ya kwangu ni machache, moja, Jimbo langu la Kigoma Kaskazini tuna vijiji 46, katika vijiji 46 vijiji ambavyo maji yanatoka ni vijiji 14. Ningemuomba sana Mheshimiwa Waziri atusaidie na sisi watu wa Kigoma Kaskazini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kigoma na mikoa mingine, niombe sana Mheshimiwa Waziri umefika wakati tuyatumie maji ya Lake Tanganyika kwa ajili ya kupeleka maji Kigoma na all the way mpaka Tabora. Kwa sababu kutumia mito, mito inakauka. Ukienda leo uangalie Malagarasi ng’ombe walioingia mle na hali ya Malagarasi tukitumia kama itasaidia kwa wengine ni nguvu sana.

Mimi niombe Waziri, imefika wakati tufanye maamuzi ya kuchukua maji ya Lake Tanganyika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bajeti ya Wizara ya Maji. Nimewasikiliza sana wenzangu hapa ndani, bajeti haitoshi. Kwangu bajeti hii inatosha, nitasema kwa sababu gani. Watu wote humu ndani naomba tuchukue Kitabu cha Nne, ukichukua Kitabu cha Nne nenda kila mkoa kwenye sub vote 3280 kuna Rural Water Supply, kila mkoa kuna fedha, lakini hizo haziko kwenye Wizara ya Maji. Naweza nikataja baadhi ya mikoa, Ruvuma wana shilingi bilioni nane, Kilimanjaro wana shilingi bilioni nne, Kagera wana shilingi bilioni nne, Tanga wana shilingi bilioni mbili, Kigoma wana shilingi bilioni tatu. Ukizijumlisha zote hizi na ukaja na za bajeti, bajeti ya maji inatosha. Sasa ambalo nataka Mheshimiwa Waziri wa Fedha atupe commitment, fedha hizi zitoke zote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli mwaka wa jana ilikuwa bilioni 900, zimekwenda asilimia 19; na Waheshimiwa Wabunge tusipende ma-figure makubwa sisi tujaribu kuhangaika fedha tunazopitisha ziende. Haya ndiyo maswali ya sisi kujiuliza, kwa sababu kama tunakaa hapa miezi mitatu tunapitisha bajeti halafu zinakwenda asilimia 19 halafu mwaka ujao sisi tunasema hapana bajeti haitoshi iongezeke. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi mbona hatuongelei asilimia 80 ambazo hazijaenda? Kwa hiyo mimi nasema kama ni bilioni mia sita ikitokea zikaenda zote mwaka huu maana yake ni kwamba tutakuwa tumefanya asilimia 75 ya yale ambayo tungefanya mwaka jana, asilimia 75 ni pakubwa mno. Kwa hiyo,…

T A A R I F A . . .

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, huyu ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, ananishangaza kidogo. Mimi sijaongelea habari ya tozo hapa, naongelea habari ya bajeti, anataka kuniambia shilingi bilioni 900 za mwaka jana zote zilikuwa za tozo, unataka watu wote hapa tuamini kwamba shilingi bilioni 900 zilikuwa za tozo? Sijaongelea jambo hilo, ninachoongea mimi, naongelea bajeti ya Serikali…

T A A R I F A . . .

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niwakumbushe Waheshimiwa Wabunge nilichoongea mimi hapa hakuna ninayempinga hata mmoja. Ninachosema, nataka kuwaonesha Waheshimiwa Wabunge kwamba kwenye fedha zinazokwenda mikoani kwetu nyingine ziko kwa ma-RAS, hakuna anayesema mwaka jana, mwaka juzi zilikuwepo. Kwa hiyo, tunapoongelea bajeti ya maji ya mwaka jana ilikuwa ni shilingi bilioni 900 plus hizo za mikoani na ninavyosema mwaka huu ni shilingi bilioni 600 plus zilizo kwa RAS na fedha za RAS hazipiti Kamati ya Kilimo, kuna Kamati ya TAMISEMI; Kamati ya TAMISEMI Ndiyo inaangalia fedha zote za TAMISEMI.

Mheshimiwa Mwenyekiti, TAMISEMI kule kuna fedha za elimu, kuna fedha za maji, kuna fedha za kilimo, kuna fedha za kila kitu, kuna fedha za afya. Unapotaka kuongelea maji in Tanzania huwezi kusema zile unaziondoa, na zenyewe ni sehemu ya kutatua tatizo la maji kwenye mikoa yetu. Argument yangu ni fedha ziende, kwamba Waheshimiwa Wabunge tusikae hapa eti Mheshimiwa Waziri akija ameweka 1.4 trillion tusimame tumpongeze halafu mwaka unaofuata zimeenda shilingi bilioni 200, tunapata nini? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachosema hapa, fedha iliyopangwa iende, ikienda nina hakika hali ya maji kwenye nchi yetu itabadilika. Lakini tukianza kunyoosheana vidole, yule amepangiwa nyingi mimi chache haina maana. Sisi twende kwenye plan yetu, zimetoka shilingi bilioni 600 tuiombe Serikali kwa mara ya kwanza waweke commitment kwamba zote shilingi bilioni 600 zitakwenda; na baada ya shilingi bilioni 600 ninazoongelea kuna nyingine kwenye mikoa yetu. kwa hiyo unaweza ukakuta tunaongelea bajeti ya maji in totality zaidi ya shilingi bilioni 800 si fedha ndogo.

heshimiwa Mwenyekiti, mimi nilitaka kusema kwamba jambo la msingi tuhangaike fedha zetu ziende, na hii itatusaidia sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho ni suala la DAWASCO na DAWASA. Umefika wakati kwa spirit ile ile ya kubana matumizi, nikuombe vyombo hivi viunganishwe ili viweze kubana matumizi viweze kufanya kazi nzuri katika Mji wa Dar es Salaam...

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nianze kukushukuru kwa kunipa nafasi. Naipongeza Wizara ya Fedha, nimpongeze Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na wenzake kwa bajeti nzuri sana. Kwa kweli ukiangalia bajeti ya mwaka jana na bajeti ya mwaka huu tofauti naiona ni kubwa. Bajeti hii wametusikiliza vizuri sana, hongereni sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, China wameanza miaka mingi sana, maendeleo unayoyaona leo China yameanza mwaka 1978 baada ya Deng kuchukua ile nchi. Deng amechukua nchi lakini kwenye Serikali zilizopita alikuwamo. Brazil unayoiona leo maendeleo yameanza mwaka 1998 baada la Lula kuchukua ile nchi, kabla ya hapo alikuwa ni Kiongozi. Malaysia unayoina leo maendeleo yameanza mwaka 1980 baada ya Mahathir Mohamad ambaye kule nyuma alikuwa ni kiongozi alipochukua nchi. Sohat wa Indonesia baada ya kuchukua nchi ndio tuameanza kuona maendeleo makubwa ya Indonesia. Ethiopia unayoina ya leo yameanza mwaka 1992 baada ya Meles Zenawi kuchukua nchi, naweza nikataja Mataifa mengi sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naanza na hili kwa sababu gani Waheshimiwa Wabunge. Lazima Taifa lolote yuko mtu ambaye atakuja ndio atasababisha Taifa hilo liendelee. Nami naomba leo niseme kwamba ninayo hakika Rais Dkt. Magufuli atatupeleka kwenye uchumi wa kati.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Marais wote hawa nimewataja ambao wamefanya vizuri sana kwenye Mataifa yao wana sifa kubwa tatu, wote kwa maana ya Singapore Malaysia, Indonesia kote, kazi ya kwanza walifanya waliwekeza kwenye elimu, unaona Rais Magufuli ameingia kazi ya kwanza aliwekeza kwenye elimu. Wote kazi ya pili ni kusimamia nidhamu ya utekelezaji wa kazi, tunaona leo Serikalini kuna nidhamu kubwa sana. Sifa ya tatu ya Marais hao waliobadilisha nchi zao ni suala la kusimamia mapato na rasilimali za nchi zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Rais Dkt. Magufuli ameamua kusimamia kwa uthabiti kabisa rasilimali na mapato ya nchi yetu kwa sababu naamini Rais anatupeleka kwenye Taifa la maendeleo. Hata hili la makinikia, hili la madini ni katika ule mwendelezo wa kusimamia mapato na kusimamia rasilimali za Tanzania. Nilisema siku ile Rais Magufuli, anaenda kubadilisha namna ambavyo uchimbaji wa madini duniani utakavyofanyika. Kwa hiyo, yeye ndio atakuwa chachu alichofanya Rais Magufuli atazisaidia Kenya, Mali, Guinea atasaidia nchi zote kwa sababu sasa wote wanakwenda kwa kuamka na ninayo hakika sasa tutapata share yetu na tutaendelea kama nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nimewasilikiza sana Wapinzani. Hakuna hata Mpinzani mmoja ambaye amesema Rais Magufuli anakosea, hakuna! Hata hivyo, Wapinzani kama walivyo Wapinzani wao wameamua kuwa Thomaso. Wanataka waone yatapotokea. Kwa hiyo, nawaelewa, mashaka yao nayaelewa ni mashaka ya Thomaso. Yesu amefufuka, Thomaso anamwambia Yesu naomba niangalie mahali palipochomwa mkuki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nawaelewa wenzetu na ndiyo maana nasema, wao wanaonesha wasiwasi lakini hawasemi kama tumekosea. Nami naamini kazi anayofanya Mheshimiwa Rais, Dkt. Magufuli, anafanya kazi nzuri sana na Rais Mheshimiwa Magufuli anaendeleza pale walipoacha wenzake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilisema kule nyuma kila Rais ataandika kitabu chake, Rais Dkt. Magufuli anaandika kitabu chake na kitabu cha Mheshimiwa Dkt. Magufuli kitakuwa kitabu ambacho nina hakika kwenye historia ya nchi yetu ndio Rais tutakayesema alitutoa third world kutupeleka kwenye uchumi wa kati kama Taifa. Jukumu letu kama wanasiasa, tumuunge mkono ili aweze kufanya vizuri zaidi huko anakokwenda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, sasa nirudi kwenye bajeti. Naipongeza sana Serikali kwenye kubadili mfumo wa kukusanya Road License. Wako watu wanasema Road License imeondolewa; hapana, haijaondolewa. Road License imeletwa ili iwe rahisi kuikusanya na iwe rahisi kwa sisi tunaochangia lakini pia itozwe kwa magari yanayofanya kazi. Naipongeza sana Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ambalo naiomba Serikali tulikazanie, ni suala la deni la ndani. Leo hii ukienda nchini, malalamiko ni kwamba pesa hazipo, wanasema liquidity haiko kwenye market. Liquidity haipo kwa sababu watu wengi ambao wamefanya biashara na Serikali wanatudai. Naiomba Serikali ije na mkakati wa kulipa madeni ya ndani. Tukifanya hivyo, uchumi wetu utaanza kukua kwa kasi kubwa zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawapongeza kwa suala la asilimia 18 ya VAT kwenye auxiliary. Sasa mnaisaidia bandari yetu, lakini naomba suala la single custom na DRC tuliondoe ili single custom itusaidie na watu wengi watumie Bandari za Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine Mheshimiwa Rais ameamua kwa dhati kufufua Shirika la Ndege la Tanzania na amenunua ndege kubwa. Zile ndege kubwa zitakuwa zinasafiri kwenda kwenye Mataifa makubwa duniani. Moja ya gharama kubwa ya ndege ni mafuta ya ndege. Tumeamua wenyewe kama Serikali; kama Afrika Mashariki, mafuta ya ndege yasitozwe kodi yoyote na yasitozwe RDL. Sisi bado tunang’ang’ania kuweka tozo hiyo. Tukiweka tozo hiyo, tunaongeza gharama za ndege. Tukiongeza gharama za ndege, tunaiumiza tourism yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu ambacho naomba leo niseme, shirika ambalo linatoa mafuta haya ya ndege ni Puma. Puma, Serikali ina asilima 50. Ukiliongezea gharama maana yake ni nini? Maana yake, profit and loss yao inakuwa kubwa, maana yake dividend itapungua, corporate tax itapungua na yote haya yatapungua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali; na bahati nzuri Kamati ya Bajeti kwenye ukurasa wa 41 mmeliandika hili jambo; nawaombeni sana mwende kwenye Finance Bill. Hii ni element ndogo sana, tukaliondoe ili nasi tuweze kuwa competitive na sisi ndege nyingi ziweze kuja kunywa mafuta hapa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kuikumbusha Serikali, kila wanapoongelea reli ya kati wanaongelea Dar es Salaam
– Mwanza. Naombeni mkumbuke ni Dar es Salaam – Kigoma na matawi yake ya Mpanda na Mwanza lakini central line ni kwenda Kigoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo la maji ni kubwa sana, naombeni sana tuweke bajeti kubwa ya maji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni suala la soko la dhahabu. Musukuma amelisema hapa, tulisema mwaka 2016 na Bwana Kishimba, naombeni tuweke soko la dhahabu, halafu kwenye soko lile tuwaambie kila atakayeleta dhahabu msimwulize ameitoa wapi? Isipokuwa watakaokuja kununua ndio tuweke export levy. Tutakusanya pesa nyingi sana kama Taifa. Wala siyo hii asilimia tano ya wachimbaji wadogo. Wachimbaji wadogo watakwepa, hatutoikusanya hii hela; lakini tukiwafanya waje kwenye soko, wanunuzi wakaja, tutapata fedha nyingi sana kama Taifa. Naombeni mwende mkalifanyie kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni suala la ten percent ya crude oil. Jamani, Kenya na Uganda hawana crude oil. Kitakachotokea, sisi tutakuwa soko la Kenya na Uganda, nasi hatuna mafuta mengi sana nchini jamani! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pale Kigoma tuna michikichi, lakini angalia mafuta ya michikichi yanayozaliwa Kigoma, huwezi kutumia hata kwa mwezi mmoja, ni machache. Nawaombeni sana tuwekeze kwenye mbegu na utafiti ili tuweze kuzalisha michikichi mingi na tuweze kuzalisha alizeti nyingi sana. Bila hivyo… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Fedha na Mipango
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Spika, nami nawapongeza Wizara ya Fedha kwa kazi kubwa wanayofanya. Nawapongeza watu wa TRA kwa kazi kubwa wanayofanya.

Moja, ni suala la TR Office, naiomba sana Wizara, kama kuna eneo tukilisimamia vizuri tutapata fedha nyingi kama Taifa ni kwenye TR Office, kwa sababu TR Office ndiye ambaye anakwenda kutukusanyia dividend. Kwa hiyo, ili tupate dividend lazima tuwekeze, lazima tusaidie hayo makampuni.

Mheshimiwa Spika, natoa mfano wa kampuni mbili. Moja ni TIPER. Tujitahidi sana watu wengi watumie facility yetu ya TIPER kwa sababu TIPER sisi tunapata dividend. Kwa hiyo, tunalo jukumu kama Serikali kuwasaidia TIPER.

Pili, PUMA, leo sisi tuna asilimia 50, lakini tumeleta sheria ya local content. Kwa hiyo, ina maana kote kwenye migodi PUMA anaondoka kwa sababu tu ya asilimia 51. Huyu anatupa dividend. Leo tunajenga reli kwa hela nyingi, kazi kubwa tunafanya, lakini kampuni za Serikali hatutaki zipate biashara, kwa sababu gani? Hatusimamii. Namuomba Waziri wa Fedha, nina uhakika dividend hizi anazihitaji. Ili tuweze kuzipata lazima kampuni ambazo Serikali ina share zisaidiwe zipate biashara, ili zikue na tuweze kupata dividends. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la tatu ni suala la PPP. Tumeongea sana kuhusu PPP. Namwomba ndugu yangu Waziri wa Fedha, kama kuna zawadi anayoweza kuwapa Watanzania ni kusimamia miradi ya PPP na mfano tunao. Naomba leo nitoe mfano mmoja. Tuna mfano wa Daraja la Kigamboni, tunatengeneza fedha nyingi sana kwa sababu Serikali haikuweka hela pale, wananchi wamepata huduma, tumepata daraja na pesa tunapata. Hivi leo barabara ya kutoka Dar es Salaam mpaka Dodoma ambayo ni Makao Makuu kwa nini tusiweke road toll? Kwa nini? Tunaongea leo ni mwaka wa 15 mimi niko ndani ya Bunge hili.

Mheshimiwa Spika, naomba sana, dunia yetu, kote wenzetu hata Wachina wakubwa wanaondoka kwenye kufanya kila kitu kama Serikali. Baadhi ya mambo yanafanywa na PPP. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine ni suala la biashara ndogo ndogo. Namwomba sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha, kama kuna jambo tutawasaidia Watanzania, tukuze biashara. Tukikuza biashara, kodi itaongezeka. Kodi ikiongezeka, tutapata ajira, nchi itaendelea kwa kasi kubwa zaidi kuliko inavyofanya sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la mwisho, ni transit trade. Mungu alituweka Tanzania akatuweka kwenye jiografia yetu hii, haikuwa bahati mbaya. Tunazungukwa na nchi nane. Hiki ndiyo kiwanda kikubwa kuliko kiwanda chochote Tanzania.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ni lazima tuje na sera ambazo zinatasaidia watu wote waje Dar es Salaam, waende Mtwara, waende Tanga. Wanaendaje? Lazima tuweke sera rafiki. Wanaendaje? Kuwe na miundombinu mizuri, tuwe marafiki kwa wafanyabishara ili watu wote waache kwenda China na Dubai, we should create Dubai of Tanzania na ilishaanza hiyo kazi Kariakoo. Sasa kwa trend tunayoenda nayo, tumeanza kutokuwa marafiki. Naomba sana watu wa Serikali, transit trade ndiyo itakayotuondoa hapa kama Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nitakupa mfano wa mafuta. Mafuta yanayoenda nje ya nchi tunasema lazima yawe yametoka Tanzania baada ya siku 30, maana yake ni nini?

Maana yake kwa sababu kule nchi za nje kwa wenzetu siku 30 ni chache, ukienda Daban siku 120, ukienda Beira siku 120, ukienda Holdens Bay siku 120, Tanzania siku 30. Maana yake ni nini? Watu hawatokuja. Tukiongeza tukafanya siku 120, maana yake Dar es Salaam ni karibu, watakuja, lakini biashara, transit trade itaongezeka. Malori yatafanya biashara, watu watakunywa mfuta, tutapata kodi, tutapata ajira. Naomba sana wenzetu wa Wizara ya Fedha tulisimamie hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimalizie kwa kuwaunga mkono kwa kila wanachokifanya, lakini niwaombe sana, dunia hii inaenda kwa kasi sana. Tukiendelea kujiuliza kila siku, wenzetu watatuacha.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema haya, naomba niunge mkono hoja.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi nianze kwa kumpongeza sana Waziri wa Fedha na timu yake kwa mpango huu mzuri sana. Mpango huu mimi naukubali wote kama ulivyo shida yangu mimi ipo kwenye ku-finance kama kuna eneo tukubaliane vizuri ni namna ya haya tuliyoyapanga tutayatekeleza namna gani? Hapa kwangu mimi ndiyo napaona ukienda page ya 50 na mwenyewe amesema mpango huu unatarajiwa kugharimiwa na sekta ya umma na binafsi kupelekea uwekezaji wa moja kwa moja au kwa njia ya ubia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesoma mipango yote sijaona popote ambapo tunajadili kama miradi hii itatekelezwa kwa ubia ama miradi hii itatekelezwa na private sector na mimi Mheshimiwa Waziri hili ninaliamini nitalisema kila nitakapo simama, nina amini iko miradi ingeweza kutekelezwa na private sector na bado tukapata mambo mazuri zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, duniani kote ukienda, China, Malaysia, kote nchi zimeendelea juzi wanatumia sana PPP kwenye miradi mingi hasa hii ya kiuchumi. Kwa bahati mbaya sijaelewa tunatunga sheria na juzi umeleta sheria nzuri sana, lakini sioni miradi ambayo tuna i-push kwa ajili ya PPP. Kwa mfano, barabara ya kutoka Dar es Salaam kuja Chalinze utmeongea huu mwaka wa 10 ambao mimi ninaamini barabara hii tukiamua ku-push tutapata mtu wa kuijenga na kwa kweli tukitafuta private sector kitakachotokea tutapata fedha nyingi ambazo tutapeleka kwenye social services kwa maana ya elimu, kwa maana ya maji, kwa maana ya afya na tutapandisha mishahara ya wafanyakazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kama tutaamua miradi yote hii mikubwa tunafanya kama Serikali peke yake, madhara yake yako kwenye social services. Mipango hii ni mizuri sana kwa hiyo mimi ningeomba Mheshimiwa Waziri jambo hili kubwa na miradi hii umeipana vizuri, vipaumbele ni vizuri lakini umefika wakati tubadilishe mindset yetu, twende kutafuta watu tutakaosaidiana nao kufanya miradi hii ya maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, umeme, pamoja tunaenda kutengeneza umeme mwingi sana mimi nakubali jambo kubwa, lakini tufanye energy mix, tukipata mtu mwingine akazalisha kwenye jua, akazalisha kwenye upepo, akazalisha kwenye gemotheo, sisi tunazalisha kwenye maji maana tutakuwa na umeme mwingi kama Taifa labda megawatts
5,000/10,000 ambao tutaanza ku-export na mwingine tutatumia ndani, lakini bado tutakuwa tume-achieve kama nchi, lakini tukitafuta kitu kimoja tu mimi nasema ningeomba sana umefika wakati tujandiliane suala la kutumia private sector. Lakini private sector ije Tanzania cha kwanza lazima sheria zetu ziwe predictable, pesa zetu za kodi ziwe predictable kila kiwe kinaaminika, lakini kama tunabadilisha magoli kila siku ni kweli baadhi ya investors hawawezi kuja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu hawana hakika kesho tutafanya nini? Kwa hiyo mimi nina amini nchi yetu ina resorce nyingi sana, Mungu ametubarikia kila tu, naombeni sana imefika wakati tutumie private sector ili tuweze kwenda mbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni suala la kilimo tunakiongea sana hapa ndani, lakini mimi nasema kilimo tulichoongea miaka yote jambo moja Serikali naona hatufanyi kwa nini nimesoma humu ndani, hatuongelei commercial farming, bila commercial farming matatizo ya kilimo hayatakwisha, matatizo yote ya kilimo yatatatuliwa na mashamba makubwa, sisemi tunyang’anywe mashamba. Mungu katupa ardhi bado ardhi hii watu watakuja wenye uwezo mkubwa. Mtu mwenye shamba lake kwa mfano hili jambo la korosho hivi kwa mfano mtu ambaye ana hekari 10,000; amelima korosho zake hawezi kumtafutie soko ninyi, hata omba pembejeo, kwa hiyo nasema tufike sehemu haya mawazo kila mtu anaweza akalima, haiwezekani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nasema tumeanza ku- push command economy hata hili la korosho, naomba mimi mwenzangu silielewi sana, Serikali ituache demand and supply ifanye kazi. Serikali kuingia ku-detect terms sio sawa, ndiyo matokeo yake wataingia watu katikati, watatuvuruga. Bei kuanguka za mazao imekuwepo hivyo duniani, kote kwa sababu inategemea soko la dunia. Lakini tuongelee zao moja, watu wa mahindi hali ni mbaya, mtama hali ni mbaya, kahawa hali ni mbaya, chai hali ni mbaya, why?

Kwa hiyo, mimi nasema ningeiomba Serikali jambo hili tuache market force ndizo ziamue bei, ikitokea bei safari hii imekuwa mbaya mwaka kesho mnatafuta namna kutoa incentive ili kuwainua wakulima, lakini tunaanza kuangaika wote just because kuna eneo moja mazao yameanguka haiwezekani? Kwa sababu bajeti ya kununua tunaitoa wapi? Tukiamua kununua sisi tunatowa wapi bajeti? Bajeti tumeipitisha hapa ndani kwahiyo, mimi ningeiomba Serikali tuache market force zi-determine biashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe Serikali, tuache biashara tupo kwenye soko huria, kurudi kwenye command economy maana yake itabidi tuanze kuleta tume ya bei, tukileta tume ya bei, tukileta tume ya bei tutarudi kule kule, wako watu wanasema tu-own sisi unajuwa maana on lazima uweke mtaji, ukipata hasara lazima uweke mtaji mwingine, kitakachotokea tutashindwa kufanya yale makubwa ambayo ni ya Kiserikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni suala la watu wa TRA, task force nilishalisema huko nyuma, jamani naombeni biashara zinafungwa, niwaombeni biashara ni mahusiano. Mwaka 1987 Mahathir aliulizwa na Rais Mwinyi kwanini Malaysia inafanya vizuri, jibu lake ilikuwa nini? Wakiwa kwenye Commonwealth ya Zimbabwe akasema mimi ninafanya vizuri kwa sababu kuna asilimia 30 ya kila anayefanya biashara kwenye Malaysia yangu.

Kwa hiyo ninachosubiri ni asilimia 30 kazi yangu ni kuweka mambo mazuri ili tupate asilimia. Juzi ameingia at 94 anaulizwa anasema shughuli yangu mimi ni kulinda 24 percent kwamba wafanyabiashara anawawekea mazingira mazuri wao ndiyo partners wangu na sisi partners wetu ni wafanyabiashara, tunalo jukumu la kuwalinda, tunalo jukumu la kuweka mazingira mazuri ili wakifanya vizuri tutapata faida asilimia kubwa itaongezeka nchi itaenda mbele.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami niwapongeze sana Mwenyekiti wa Bajeti na Mwenyekiti wa PIC kwa ripoti yao. Pia niipongeze Serikali kwa kazi kubwa wanayofanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri Mkuu wa Malaysia alivyoshinda uchaguzi juzi Mahathir akiwa na miaka zaidi ya 90 aliulizwa swali moja, utafanya nini ili kuendeleza maendeleo ya Malaysia. Alijibu jambo moja tu alisema kazi yangu ni kuhakikisha asilimia 24 zinaendelea kuwepo. Maana yake ni nini? Anasema kila biashara iliyoko hapa nchini kwetu Serikali inapata asilimia 24. Kwa hiyo maana yake sisi ni shareholder wa kila biashara. Nami ningetamani niwaombe wenzangu Serikalini tuseme kila biashara ya Tanzania, sisi tuna asilimia 30. Kwa hiyo tunalo jukumu la kulinda hii asilimia 30 iendelee kuwepo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu gani nasema haya, nasema biashara ikienda vizuri, kama kodi tumefika asilimia 88, tutafika asilimia 100 tutafika asilimia 180, hivi jambo likiongezeka ni mbaya? Kuna ziada mbaya kweli jamani. Mimi niwaombe wenzangu Serikalini tuanze kubadilika kwamba wafanyabiashara ni partners wetu. Wafanyabiashara ni partners wa Serikali hii. Ninayo mifano ya makampuni mengi sana ambayo ukiangalia kodi wanazolipa, ukiangalia wanavyoajiri watu, wanaleta fedha nyingi kwenye uchumi wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, iko tabia imeanza kukua kwamba tunadhani wafanyabiashara ni wezi, ni wahuni, ni watu wabaya, maneno haya yanasemwa na viongozi, hili siyo sawa. Juzi Mheshimiwa Rais amesema tunawahitaji wafanyabiashara. Kwa hiyo ningeomba na wale wengine ambao mnamsaidia Mheshimiwa Rais muanze kuona umuhimu wa wafanyabiashara. Leo Kariakoo imekufa, nitasema sababu chache za Kariakoo kufa. Ya kwanza ni tariff, Serikali yetu wafanyabiashara wadogowadogo anaenda India, anaenda China analeta glass ya shilingi elfu moja na kuna glass ya shilingi elfu kumi, akija mtu wa kodi anasema glass zote hizi ni shilingi elfu kumi, lakini watu wengi wanatumia glass za shilingi elfu moja matokeo yake commoditie zinazokuja ni bei ghali na matokeo yake watu wanaondoka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili angalia, ni harassment tunayowapa, anakuja Mzambia anakuja na fedha zake, anafika Kariakoo anakutana na TAKUKURU, anakutaka na Polisi anakutana na TRA, huyu hawezi kurudi. Shughuli ya kodi inasomewa, watu wanakaa darasani wanapata degree ya kodi, hawa watu wanafanya TRA, tuwaombe Polisi na vyombo vyote vya ulinzi ya usalama wafanye kazi walizosomea. Yako madhara yako madhara ya kuwapa watu wakafanye kazi ambayo hawakusomea. Madhara haya ni makubwa, tunaharibu uchumi wetu wenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Kariakoo mabenki yote yanafungwa, mnajua kwa sababu gani? Kila branch ya Kariakoo inafungwa, kwa sababu hakuna biashara tena, biashara yote imehamia wapi, Zambia, Kenya na Uganda. Hii siyo sawa, Mungu alituweka Tanzania geographically, Tanzania tuko mpakani ni kwa nia njema, tuutumie mpaka huu kwa maendeleo yetu lakini tunafanya nini. Tuangalie trade angalia transit trade, angalia vizingiti vya barabarani, lori mpaka lifike Zambia limesimamishwa zaidi ya mara 30, polisi wako everywhere, watu wa mizani wapo, sasa hizi tunaambiwa lazima tufuate sharia, lakini hii sheria ametunga nani, si sisi leteni tuibadilishe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ni suala la Afrika Mashariki, Kenya wanatudanganya, kwa sababu Kenya biashara yao haiko Zambia, haiko Kongo. Tanzania sisi wanaotuletea fedha ni Zambia, ni Malawi, ni Kongo, ndio watafuata Burundi kidogo, watafuata na Rwanda. Niwaombe sana Serikalini biashara hii isipokua, maana leo Waziri wa Fedha tutampiga maneno tu hapa, lakini Waziri wa Fedha tusipomsaidia biashara ikakua, hawezi kukusanya, hawezi kuleta hela ya maendeleo, tutaaanza kulalamika hapa. Kwa hiyo niwaombe wenzetu wazingatie hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi kwenye World Economic Forum bosi wa IMF ameulizwa anasema ili nchi ifanye vizuri mambo machache sana, moja kubwa lililosemwa ni growth, kwamba lazima tulete fedha za kukuza uchumi, tukuze kilimo, tukuze biashara, tukuze kila jambo. La mwisho akasema ni suala la private sector, ndugu zangu tukidhani Serikali inaweza ikafanya kila kitu, kuna mtu tunamdanganya sio kweli. Nenda kuanzia China, nenda kote unakokujua ambako wameendelea juzi kilichofanya waendelee ni private sector.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi niwaombe sana, unajua niwaambieni hakuna nchi iliyoendelea kwa kuwa na maskini peke yake, haipo, no single country imeendelea kwa kuwa na maskini peke yake. Tufanye jukumu la kupunguza umaskini, tufanye jukumu la kuondoa wanyonge kwenye uchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mtu mmoja akiwa na pesa, leo Mbunge mmoja akiwa amepata Ubunge na niwaulize Wabunge wenzangu kuna watu wamepata Ubunge ndio ameajiri dereva, ameajiri Katibu na kadhalika kwa sababu ya nini tuna income zaidi. Uchumi pia unafanya kazi hivyo hivyo, akitokea mtu akawa tajiri, huyu mtu ataajiri watu wengi. Bakhresa hajasoma, lakini ameajiri wenye PhD ni kwa sababu ana uwezo wa kifedha. Kwa hiyo, kudhani wafanyabiashara ni watu wabaya siyo sawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, liko suala hapa limesemwa na naomba sana amesema Mwenyekiti wa PIC tunayo mashirika zaidi ya 11 yametupa dividend bilioni 35. Nasema hizi hazitoshi, tuyasaidie mashirika haya yafanye vizuri zaidi. Nami ningemwomba Mwenyekiti atakapokuja mwaka kesho asiishie kwenye dividend, nataka atuonyeshe mashirika haya yamechangia shilingi ngapi kwenye uchumi. Watuoneshe maana kuna watu wanadhani ile Kampuni naweza nikaifuta tu, wewe unafuta kampuni assume leo watu wamesema hapa habari PUMA, tukiamua hapa leo kuifuta PUMA unajua maana yake ni nini? Unapoteza zaidi ya bilioni 400 kwenye uchumi wako, sasa unapata nini ukiifuta. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimalizie kusema jambo moja la ATC. Nataka nichukue nafasi hii kabisa kupongeza uamuzi wa kuwa na Shirika letu la ndege na niwaombe wenzangu tusiwe na haraka ya kupata faida, tunachotakiwa ni kuangalia multiplier effect ya kuwa na airline. Ukishakuwa na airline yako muuza mafuta atakupa dividend, muuza mafuta ya ndege utapata corporate tax utapata tax faida, lakini ameuza mafuta mengi kwa sababu una ndege, utapata ajira kwa sababu una ndege, utapata kodi kwa sababu una ndege, lakini utafanya biashara ichanganye Dodoma hukai masaa manane barabarani utawahi, uje ufanye biashara urudi. Hii ndio faida ya kuwa na airline in the country.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda pale Airport mtu akipita pale atanunua kitu yule mwenye duty free utapata kodi kule, matokeo yake ndio faida ya kuwa na Airline.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, nakushukuru na naomba niwashukuru Wenyeviti kwa kazi nzuri waliyofanya. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Spika, nami nawapongeza viongozi wa Kamati zote mbili walioleta report yao hapa ndani. Naomba nijadili zaidi kwenye kilimo. Toka tumepata uhuru kuna mazao ndiyo mazao ya kimkakati Tanzania kwa maana ya kahawa, katani, chai, korosho pamoja na pamba pamoja na palm oil. Nimeamua kuangalia uzalishaji wetu wa haya mazao na ili twende mbele kiuchumi lazima tuongeze uzalishaji. Uzalishaji wa kahawa Tanzania ni tani 100,000; kwa nchi 10 bora duniani Brazil wanazalisha tani 2,500,000; Vietnam tani 1,650,000; Colombia tani 800,000; Indonesia tani 600,000; Ethiopia ambayo ni ya tano duniani inazalisha tani 4,84000.

Mheshimiwa Spika, kwa nini nasema haya? Nataka sasa kama Taifa tuanze kujielekeza kwenye uzalishaji, tuache kuhangaika na kutatua matatizo ya siku, maana mwaka jana 100,000, mwaka huu 100,000, mwaka keshokutwa, hii siyo sawa. Leo hii tuna matatizo ya fedha za kigeni, tutazipataje; ni kwa ku- export mazao yetu haya ya biashara. Ili tuweze kuongeza uzalishaji, najua hili jambo wengi hawalipendi, lakini ni lazima tuanzishe mashamba ya biashara, lazima tuanzishe commercial farming in Tanzania kwa sababu ardhi tunayo, maji tunayo, lakini tusipo-embrace commercial farming na commercial farming ina faida zifuatazo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwanza watahangaika na ubora; pili, watahangaika na quantity; watahangaika kutafuta soko, watatoa ajira, watatoa mafundisho, watatoa pembejeo, watatafuta za kwao, lakini watalipa kodi, lazima kama Taifa tuseme tunapoenda ndani ya miaka mitatu ijayo, tutaondoka kwenye kahawa kutoka 100,000 kwenda 500,000 na unajua maana yake nini? Maana yake unaingiza fedha nyingi za kigeni hata bei ya dunia ikianguka kwa sababu quantity inakubeba bado itakusaidia kama Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nitakwenda kwenye katani, katani iliyokuwa inazalishwa miaka ya 1970 leo haipo, leo katani duniani bei imepanda, lakini tunazalisha tani 50,000, lakini tuna uwezo wa kuzalisha tani 1,000,000, tufanye nini? Ni lazima tuhangaike, tuondoke kwenye 50,000 ili twende kwenye tani angalau 500,000 na tukifika tani 1,000,000 maana yake tutaingiza dola milioni 700 kwenye uchumi wa Tanzania, lakini ili tufike tuhakikishe watu wengi household nyingi zinalima mkonge, tuhakikishe financing inakaa vizuri. Lakini ili commercial farming ifanye kazi lazima tulete wanasema Wazungu legal framework with clarity.

Mheshimiwa Spika, Mfalme wa Dubai wakati anafanya mabadiliko Dubai Baktoum familia yake walimfuata wakasema wewe mzee mbona unagawa ardhi yetu ya Dubai kwa Wachina, Wahindi na Wazungu; aliwaangalia akawajibu jambo moja tu, siku ambapo Mchina na Mhindi yuko Airport anaondoka na ghorofa lake mniite, hata sisi akija mtu tukampa ardhi, akalima, tukiamua kumfukuza haondoki na ardhi hawezi kuibeba, kwa hiyo lazima tubadilishe mindset kwenye agriculture, we can’t go like this.

Mheshimiwa Spika, nitakwenda kwenye chai, Tanzania tunazalisha tani 19,000 tu, wakati Wakenya ambao wana eneo dogo kuliko sisi wanazalisha tani 300,000 na leo Kenya ni ya tatu kwa chai duniani, maana yake ni nini; kwa sababu wame- embrace mashamba makubwa, wamewekeza na ukitoka tani 18,000 ukafika tani 300,000 tu, maana yake unaingiza kwenye economy dola nyingi sana na GDP ya kilimo itatoka kutoka asilimia 30 mpaka 50 kwa sababu tunayo ardhi, tuna watu na tuna mvua. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nitakwenda kwenye korosho, nasikiliza kelele za korosho, unajua maana yake nini, ni kelele za kitu kidogo wanataka kupigania watu wote. Tanzania tunazalisha tani 210,000, lakini kwenye korosho Vietnam wanazalisha tani milioni 1,200,000; Nigeria tani 900,000; India tani 600,000; Cote d’Ivoire tani 600,000; maana yake ni nini? Sisi Tanzania tunayo capacity ya kutoka 200,000 kufika 1,000,000. Leo ukitoka hapa 200,000 ukafika 1,000,000, 200,000 unapata dola milioni 600 kwenye economy dola maana yake ukienda 1,000,000 unaongelea shilingi ngapi ni six time five that is three billion dollars kwenye economy yako. Tunapambana kupigania umaskini wetu, lakini ili watu wa korosho walime wengi, tutengeneze commercial farming, wale wenye commercial farming, wanatafuta soko duniani na watawachukua hawa wachache, tutakwenda mbali kama Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, namalizia suala la pamba angalia pamba leo mwaka jana tumezalisha tani 200,000, lakini kama nchi tuna uwezo wa kufika hata tani 500,000. Mimi nasema lazima mawazo ya Mheshimiwa Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Waziri wa Ardhi na Mheshimiwa Waziri wa Fedha tubadilike sasa tu-invest kwenye grove, bila grove ndugu tutabakia hapa hapa, tunatafutana kwa nini hatuendi mbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, palm oil Tanzania tuna import asilimia 55.5 ya edible oil karibia dola milioni 300 zikaenda kwenye ku-import mafuta ya kula, lakini tuna eneo zuri la palm oil Kigoma pamoja na Kyela, tuna eneo mikoa yote ya katikati kulima alizeti na siyo kwamba tumejitosheleza kwenye edible oil lakini na Tanzania tungeanza ku- export edible oil. Balance of employment, export tusipo-invest kwenye ukuzaji na uzalishaji, bado tutabaki tunahangaika ku-solve matatizo ya siku inayofuata. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tuna suala la ng’ombe, suala la maziwa Uganda pekee yake wanazalisha lita 1,000 000 ya maziwa, sisi wenye ng’ombe wengi, wenye ardhi kubwa lita 100,000 na angalia tunachohangaika nacho, hata wale watu ambao wana vi-ranch badala ya kusema tuwasaidie wazalishe zaidi tunakwenda kuongeza kodi za per square meter maana yake waondoke, maana yake wao hawana malisho, na hiyo kodi unayoitaka mwisho wa siku hutoipata, lakini ungeunganisha wale wafugaji wakazalisha maziwa mengi ukaja na viwanda, leo tungekuwa mbali sana.

Mheshimiwa Spika, juzi Uganda mtoto wa Museveni wa kike amefungua kiwanda kimoja tu anazalisha lita 100,000 za maziwa kwa siku, wala hawatuzidi ng’ombe wengi, hawatuzidi maarifa, hawatuzidi land, tatizo letu ni nini? Lazima tubadilike kama Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimalizie kwa kusema tatizo la maji; kama dunia itakuja kupigana vita ya tatu ya dunia italetwa na maji, lakini kwa bahati nzuri Tanzania Mungu katupa baraka ya maji, moja ya 16 ya maji yote safi ya kunywa duniani yako Lake Tanganyika, lakini watu wa kilometa tano kutoka Lake Tanganyika hawana maji, ukienda Mwandiga hakuna maji, ukinda vijiji vyote vya Simbo hakuna maji, ukienda Kalinzi, Mkiva, Nyarubanda hakuna maji lakini tunazungukwa na Lake Tanganyika. Niombe sana tuhangaike na suala la maji.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naunga mkono hotuba zote za Kamati zote. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru wka kunipa nafasi niwe wa kwanza leo, nianze kwa kumpongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na wafanyakazi wa wote wa Wizara kwa kazi nzuri wanayofanya. Naanza, nina mambo matatu kwa kweli, moja ni suala la barabara ya kwangu kule Mwandiga kwenda Kabunga ni barabara mpya barabara ambayo Mheshimiwa Rais aliahidi kwenye kampeni, ningetamani sana tutakapoenda kwenye kampeni mwaka kesho hilo lisiwe swali, naomba sana waziri tujitahidi barabara hii tuweze kuimaliza na barabara hii ina faida zifuatazo:-

Mheshimiwa Spika, barabara hii ikiisha maana yake Gombe watu hawataenda kwa njia ya boti; barabara hii ikiisha TPA wamejenga bandari kule Kagunda ili bandari ile iwe na maana lazima barabara hii iishe TPA na halmashauri wanajenga soko Kagunga ili soko lile liwe na maana kwa biashara ya Burundi na Uvira, lazima barabara hii iishe, niombe sana Wizara tujitahidi barabara hii iishe kwa kweli ni barabara ya kiuchumi ni barabara ya kiulinzi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili, ni suala la PPP. Nimesoma kitabu hiki cha Waziri sijaona popote tunapoongelea barabara za PPP au mradi wowote mkubwa wa PPP. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hili ningeomba sana watu wa Serikali watusaidie. Mimi naamini tunapoongelea barabara Tanzania, Rais Nyerere alijenga barabara, Mwinyi alijenga barabara, Mkapa alijenga barabara, Kikwete alijenga barabara, Magufuli anajenga barabara. Mimi leo nataka tumtenganishe Magufuli na Marais wote waliopita kwenye barabara. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ili tuweze kumtenganisha lazima tuje na mawazo mapya. Umefika wakati barabara za nchi hii tuanzishe super high way ambazo hatutumii fedha zetu. Tutajenga barabara ambazo tutalipa kwa road toll. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wako watu fulani Serikalini wanasema kwa kujenga standard gauge barabara haina maana, siyo kweli.

MBUNGE FULANI: Siyo kweli.

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Spika, Dodoma Jiji, ili Dodoma iwe accessible lazima tujenge super high way from Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha. Maana yake ni nini? Kama kuja Dodoma ni saa nane, maana yake Dodoma haiwezi kukua kwa haraka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi nasema reli hata ikiisha kazi yake ni mizigo. Kama mnadhani tunajenga reli kwa ajili ya kusafirisha watu nadhani siyo sahihi. Kwa hiyo, tunasema tujenge barabara na hizi barabra duniani kote wanatumia hela za PPP, Malaysia, Marekani na China wanatumia PPP, tatizo letu ni nini? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi na wewe tulikwenda kwenye mkutano wa IPU, Urusi. International Airport ya Urusi (Moscow) ni ya mtu amejenga, siyo Serikali lakini service zinapatikana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, najua sana mambo ya barabara kwa sababu na mimi nimekulia humo ndani, naombeni tumfanye Magufuli awe tofauti na wenzake. Namna bora ya kuwa tofauti ni moja tu: Amekuwa tofauti kwenye reli, wote hawakujenga reli yeye anajenga reli; amekuwa tofauti kwenye umeme wa Stiegler’s wote hawakufanya yeye anafanya, naombeni tumpe na utofauti wa barabara, tujenge super high way nchi nzima ambazo watu watakuja kwa kulipa. Chalinze high way tumeiondoa, why? Ukiwauliza watu wa Serikali wanasema Chalinze high way tumeiondoa kwa sababu kuna standard gauge, hapana, havina mahusiano hata kidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, siyo lazima watu wote watapanda reli. Haiwezekani kilometa 100 tunakwenda saa tatu, kiuchumi siyo sawa. Kwa sababu infrastructure ndiyo inayoleta uchumi, ndiyo enabler wa economy. Sasa kama infrastructure ndiyo enabler wa economy lazima tufanye vitu ambavyo vitasababisha goods zifike mapema, tuweze kwenda kwenye maeneo yetu mapema, twende kwenye biashara tuwahi kurudi. Sielewi kwa nini Serikali haitaki miradi ya PPP. Naamini kama tunataka twende haraka lazima twende kwenye PPP. Wenzetu wote wanatumia fedha za watu, hii kwamba lazima tufanye wenyewe siyo sawa.

Mheshimiwa Spika, matokeo ya kufanya wenyewe ni haya yafuatayo. Barabara ya kutoka Nyakanazi kwenda Kabingo Kilometa 50 tunajenga huu mwaka wa 10. Barabara ya kutoka pale Kidahwe - Kasulu huu mwaka wa 10. Maana yake ni nini? Tuna shida nyingi sana tunataka kufanya yote. Namna bora ili tuweze kwenda kwa kasi, maeneo mengine tuwaachie wengine wafanye. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naamini Watanzania hawawezi kushindwa kulipa road toll, hawawezi. Kama natoka na basi Kigoma saa 12.00 asubuhi, nina uhakika nitakuwa Dar es Salaam saa 10.00 kuna shida gani ya kuweka toll? Nani atakataa kulipa toll? Sielewi kuna nini Serikalini. Sielewi why Serikali hawataki miradi ya PPP, sielewi.

Mheshimiwa Spika, napenda Waziri atakapokuja atuambie hivi sisi ni tofauti na watu wengine? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo ukienda Marekani hata uki- google, mtu pekee anayekumbukwa kwenye barabara Marekani ni Rais Franklin Roosevelt? Kwa sababu gani? Baada ya vita kuu ya pili ya Dunia aliamua kuunganisha states zote 50 kwa super high way na watu wanalipa kwenye toll. Kwa nini hatutaki kufanya hivyo? Kwa hiyo, mimi ningeomba sana Serikali, najua jambo hili linawawia ugumu lakini sioni ugumu wake ni nini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala lingine ni viwanja vya ndege. Mimi hili naleta ushauri Serikali mlitafakari upya, nadhani umefika wakati viwanja vya ndege viachiwe kazi ya kujenga na kuendesha. Habari ya kuchukua viwanja vya ndege unapeleka TANROADS, inawezekana ni nia ya kudhibiti lakini kuna ucheleweshaji. TANROADS wana kazi kubwa, wana madaraja, barabara na kila kitu. Ningeomba suala la viwanja vya ndege tuvirudishe. Pale tumepeleka CEO mzuri sana, Engineer Ndyamkama is one of the best, tumpe kazi hii ataifanya na kwa haraka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini pia tuweke taa kwenye viwanja vyetu. Tumenunua ndege lakini ili ziweze kufanya kazi mara nyingi tunahitaji taa. Hii kusubiri jua tu maana yake ndege zetu hazifanyi kazi at its capacity. Kwa hiyo, naomba sana hili nalo liangaliwe.

Mheshimiwa Spika, lingine ni suala la bandari. Naomba nichukue nafasi hii kuwapongeza sana viongozi wa bandari kwa kazi kubwa wanayofanya. Hata hivyo, kazi kubwa inayofanyika bandarini naomba tuwasaidie tuondoe vizingiti barabarani.

Mheshimiwa Spika, kwenye transit trade, biashara hii tupo na wenzetu sasa kama kila baada ya dakika tano kuna Polisi, tunaifanya bandari yetu isiwe attractive. Kwa sababu gani? Bandari itafanya kazi vizuri, inatoa mizigo kwa wakati lakini lori likishaingia mpaka kufika Tunduma ni shughuli ya siku nne au tano. Wafanyabiashara wanataka waende haraka warudi, hii ndiyo maana ya biashara. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hapa kwetu kuna point nyingi za kukaguliwa unapotoka Dar es Salaam mpaka Kigoma na unapokwenda kwenye mipaka yetu nawahurumia wale wanaoendesha haya malori kwa sababu wanasimamishwa kila baada ya kilometa 3 au 4, trafiki wapo. Rais amesema jamani eeh, Polisi haiwezekani mkasema kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro kuna point mbili za kukagua, huku kwingine kote wanasimamishwa, biashara haiwezi kutusubiri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ndiyo maana sasa bandari yetu inapambana na ushindani wa Mombasa na Beira kwa sababu bandari ina-perform lakini kama wale wengine hatuisaidii itaonekana imeelemewa. Kwa hiyo, naomba sana watu wa Serikali tuwasaidie sana watu wa bandari kwa maana ya ku-enable ili kazi yao iweze kufanya vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la mwisho ni suala la fedha za barabara hasa za GOT. Naomba sana Serikali, ukiangalia trend yetu, barabara ambazo zinajengwa na GOT zinatumia muda mrefu sana. Maana yake ni nini? Zikitumia muda mrefu, interest rate, idle time, kwa barabara ambayo ungeijenga kwa shilingi bilioni 50 unaijenga kwa shilingi bilioni 100, siyo sawa. Atakuja mtu siku moja tutapata shida. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naomba na mimi niunge mkono hoja, nakushukuru sana.
Azimio la Bunge la Kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC na kuendesha vyema Mkutano wa 39 wa Jumuiya hiyo
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Spika, nami nashukuru kwa kunipa nafasi niweze kuunga mkono azimio lililoletwa leo asubuhi. Kwanza nami nimpongeze sana Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kwanza kwa kukubali mkutano kufanyika Tanzania. Ni kweli mikutano ya SADC ni rotational lakini angeweza kukataa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili, kama hali yetu ya pili isingekuwa nzuri, bado hata wenyewe watu wa SADC wasingeleta mkutano Tanzania. Kwa hiyo, ni vizuri tuelewe mkutano umekuja Tanzania kwa sababu ya utayari wa Rais wetu, ulikuja kwa sababu Tanzania tupo tayari. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, napongeza kwa sababu kwanza kama walivyosema wenzangu, Tanzania ndiyo kitovu cha ukombozi wa Bara la Afrika hasa upande wa Kusini mwa Afrika; na kwa wale mnaokumbuka, wakati wa liberation struggle, ile committee ya liberation struggle, Katibu Mtendaji wa kwanza alikuwa Marehemu Balozi George Magomba baadaye akafuatiwa na Ndugu Brigadier Hashim Mbita. Kwa hiyo, Tanzania tumefanya kazi kubwa sana kwa ukombozi wa Kusini mwa Afrika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naunga mkono na nikiomba Mheshimiwa Rais, Mwenyekiti wetu mpya wa SADC, kazi ya ukombozi Kusini mwa Afrika imekwisha, nadhani umefika wakati na Rais amesema huu ni wakati wa ukombozi wa uchumi wa Kusini wa Bara la Afrika. Nina uhakika Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli atalisimamia hili kama Mwenyekiti mpya wa SADC kuhakikisha tunaondoa vikwazo vya kufanya biashara kati ya nchi wanachama. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mwalimu Nyerere alipokuwa anafungua Bunge la South Africa mwaka 1994 aliwaambia wa South Africa msijigeuze kuwa kaka wakubwa, South Africa hamna jirani, jirani yenu ni sisi Waafrika wenzenu. Akasema ili block hii iweze kuendelea, lazima tufanye biashara ndani ya wanachama wenyewe. Kwa hiyo, ni matarajio yangu na ninayo hakika Mwenyekiti mpya wa SADC atafanya yafuatayo: moja, akisaidiwa na Waziri wa Mambo ya Nje kuhakikisha tunaondoa vikwazo vya kufanya biashara ndani ya nchi wanachama. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pili, ili tuweze kufanya biashara na wananchi wanachama, umefika wakati lazima tutafakari, hivi kwenda Kongo ni lazima niwe na visa? Hivi Mkongoman lazima awe na visa kuja Tanzania? Hivi Wamalawi lazima wawe na visa kuja Tanzania? Tukifanya hivyo, nina hakika biashara kwenye nchi hizi itashamiri na ninayo hakika hii ndiyo itakuwa legacy atakayoiacha Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli.

Mheshimiwa Spika, ninapongeza kwa sababu mkutano wenyewe umefanyika kwanza kwa utulivu mkubwa sana, lakini pia umefanyika kwa ushirikishwaji wa watu wengi sana. Kwa mara ya kwanza mkutano wa Kitanzania; na ninawapongeza walioandaa mkutano huu, tumeona private sector ikishiriki kuhakikisha mkutano huu unafanikiwa.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, nami nashukuru sana na ninamtakia mema Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa hiyo aliyoianza. Moja legacy ya kwanza kama mnavyofahamu Bunge hili, kazi ya kwanza Rais amefanya kwenye SADC ni kufanya Kiswahili ni kuwa lugha ya SADC. Kwa hiyo, mtu yeyote mwenye wasiwasi wa legacy ya Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwenye SADC, legacy ya kwanza ni Kiswahili. Ninaamini legacy ya pili itakuwa ni biashara ndani ya nchi ya wanachama na legacy ya tatu nina hakika itakuwa kuhakikisha katika nchi za SADC kunakuwepo na utulivu na amani kama ilivyo Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema haya, naomba niunge mkono azimio hili. Namtakia maisha mema Mheshimiwa Rais na Mwenyekiti mpya wa SADC.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Kuhusu Shughuli za Kamati Kwa Mwaka 2019 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2019
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Spika, nami naomba niwapongeze Wenyeviti; Mwenyekiti wa Kamati ya Madini na Nishati kwa ripoti zao nzuri sana. Nawapongeza sana Wizara ya Nishati na Wizara ya Madini kwa kazi kubwa wanayofanya.

Mheshimiwa Spika, kama alivyosema ndugu yangu Mheshimiwa Mzee Keissy kazi ya umeme inayofanyika Tanzania ni nzuri sana, naipongeza sana Serikali. Nataka niseme jambo moja ambalo nadhani kama Bunge lako, hatujalipa nafasi ya kutosha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika na Waheshimiwa Wabunge wenzangu, kilichofanywa na Rais, kilichofanywa na Serikali kuingia makubaliano mapya na wawekezaji wakubwa wa madini, kwa vyovyote vile ni jambo ambalo sisi kama Bunge tunapaswa kuipongeza Serikali. Wako wanaosema ambao mimi naelewa kwa nini wanasema, lakini najaribu kuangalia tutakachopata kama nchi kwa makubaliano haya makubwa na kwa uchumi wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, cha kwanza ukisoma kwenye yale makubaliano ambacho watu wengine wanaweza wakaona ni kidogo, ofisi za Barrick London, ofisi za Barrick Johannesburg, zote zinafungwa, zinakuja Tanzania. Maana yake wafanyakazi wale watakaa kwenye nyumba za Watanzania, watalala kwenye hoteli za Watanzania, watakula kwa Watanzania. Maana yake uchumi mkubwa katika nchi utaongezeka sana. Bado hapa sijaongea habari ya ajira. Ninayo hakika, leo ukienda Dar es Salaam na mikoa ya Mwanza na Arusha bei ya nyumba zimeshuka, lakini unapopata Kampuni kubwa kama Barrick, wafanyakazi wake wanakuja kukaa Tanzania, maana yake nyumba zetu zitarudi bei kuwa juu, kwa sababu wale watu wana- income kubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia ziko faida za kiuchumi. Moja ya faida kubwa, ukiangalia pale, Serikali ina asilimia 16, lakini Tanzania tutapata cooperate tax 30%. Tutapata karibia 3% kwa ajili ya Local Government. Maana yake kwa uchumi tunakwenda kupata kila mwaka mapato ya zaidi ya 50% kwa revenue ya kampuni hii. Kwa vyovyote vile Mtanzania yeyote ukisimama unalaumu jambo hili, then maana yake hufahamu uchumi mpana unavyofanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vile vile naangalia social responsibility ambapo kwa watu ambao wanazunguka na madini kule ambako madini yapo watafaidi zaidi kuliko Halmashauri nyingine za mbali ambazo sisi tunakaa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia nataka niwaambie wenzangu, mimi nimeangalia vizuri sana, tunaanzisha kampuni mpya ya Twiga, ukiingalia watu watasema unapata 16% lakini mkishakuwa na kampuni maana yake baadaye ikiishaanza kufanya biashara, tutaipeleka kwenye stock exchange, kwa sababu ni kampuni mpya hii. Tukiipeleka kwenye stock exchange, watakaofaidi ni mimi na wewe na sisi. Haya ni mageuzi makubwa ya kishujaa ya kimapinduzi. Tanzania tume-set tone Africa. Leo hii Waafrika wote wanakuja kujifunza tuliyoyafanya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, habari ya smelter, hata kama isipojengwa hapa, ambayo naamini baadaye itajengwa, bado kwa sababu tumeweza ku-identify a new company, watu wetu watakuwemo kwenye Bodi, ofisi zitakuwepo hapa, usimamizi bado kama nchi tutafaidi ndugu Wabunge. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naangalia, kwa mara ya kwanza, tutakuwa na Board Members kwenye kampuni hiyo Watanzania ambapo naamini jambo hili ni kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia kubwa zaidi ambalo wote hamlisemi, tulitunga sheria mwaka 2010 hapa; moja ya jambo kubwa tulilotunga, makampuni haya…

(Hapa Mhe. John W. Heche alisimama)

SPIKA: Mheshimiwa Heche, naomba utulie. Halafu wanaogeuza kiti nyuma kwa Spika wanakosea. Mnatakiwa wote muwe mnamwona Spika anavyopendeza. (Kicheko/Makofi)

Tusikilize shule inayoshushwa na Mheshimiwa Peter Selukamba.

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Spika, moja ya jambo kubwa lililofanyika, kuna maamuzi makubwa ambapo tulitunga Sheria ya Madini Mwaka 2010, kwamba makampuni yote ya madini fedha zao wataweka kwenye benki za Tanzania. Maana yake ni nini? Wakiweka fedha kwenye benki za Tanzania; NMB, CRDB na benki zote, fedha zile Watanzania wote tutazi- access kwenye mikopo. Maana yake fedha za Barrick, pamoja na kwamba zitafanya kazi ya kuchimba, zitafanya na kazi ya uchumi kwa Watanzania. Hili ni jambo kubwa, uncles wenzangu hatuelewi maana ya fedha kuja kwenye benki za Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa sababu wakileta; kwa mfano, leo najua watu kama GGM fikiria fedha zao zote wanaweka kwenye benki moja ya Tanzania, Barrick; maana yake ni nini? Siyo kwamba fedha zile ni kwa ajili ya kumpa Barrick or Geita peke yake, maana yake fedha zile kwa sababu ziko kwenye benki zitatumika na masikini wa nchi hii kuwakopesha kufanyia biashara. Huu ndiyo uchumi mkubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, muhimu zaidi leo nataka niseme, kwa muda huu ambao walikuwa wamesimamisha biashara, nenda leo kaangalie Kahama, Shinyanga na Mwanza utaona tofauti. Tumefaidika kidogo baada ya Waziri wa Madini ambaye nami nampongeza sana ndugu yangu Mheshimiwa Doto kuhakikisha wachimbaji wadogo wanapewa nafasi ya kufanya kazi kubwa. Kama leo ingekuwa wachimbaji wadogo hawapo, tungekuwa na hali ngumu kiuchumi mikoa ile ya Kanda ya Ziwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, fikiria, tuna wachimbaji wadogo, tumewawekea regulation, tumewawekea masoko, wanaleta fedha, tunapata kodi na on top of it tunawaleta na wachimbaji wakubwa wanaanza kufanya biashara yao. Kwa vyovyote vile hili ni jambo kubwa. This is a game change of the economic Tanzania; na sisi kama Wabunge tunapaswa kuwa watu wa mwisho kuinyooshea kidole Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, rafiki yangu Mheshimiwa Heche amesema kwamba Wabunge wa CCM tunatakiwa kuona aibu. Nadhani kuna maeneo haelewi vizuri. Anasema tunabadilisha sheria. Wewe umekaa muda mrefu na wengine wachache wamekaa muda mrefu, kila mwaka tunabadilisha sheria. Miscellaneous maana yake nini? Miscellaneous tunaleta tubadilishe sheria ambazo aidha tulitunga tukakosea, tumefikiria, tunatunga upya. Suala la kubadilisha sheria halimaliziki leo. Mbona sheria nyingine hawasemi? Kazi ya Wabunge ni kutunga sheria. Ukitunga sheria leo, ukaanza kuitumia, ukaona haikuletei ulichokuwa unakitaka, prudence yoyote, unaleta unabadilisha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tumetunga sheria nyingi hapa za fedha, tunakwenda tunagundua haifai, tunaileta tunaibadilisha. Kwa nini Sheria ya Madini tukiibadilisha iwe nongwa? Ni nongwa! Mimi naelewa kwa nini ni nongwa. Ni kwa sababu wanaona Chama cha Mapinduzi kinafanikiwa sasa. Ni nongwa kwa sababu wanaona Chama cha Mapinduzi na Serikali yake kimeanza kuelewa na kuleta mageuzi makubwa ambayo kasi ya uchumi itakuwa kubwa, nafasi yao inazidi kupungua kadri siku zinavyoenda mbele. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nawaomba watu wa Serikali, msiogope. Kama kuna maeneo tulifanya tukadhani hayatuletei faida, leteni tubadilishe, ndiyo kazi yetu. Nasema tuleteeni! Moja ya kazi kubwa tukibadilisha sheria hii, maana yake tuna-attract more investors. tuki-attract more investors, maana yake uchumi wa Tanzania utakua; na ile dream ya Mheshimiwa Rais Magufuli ya kwenda kwenye uchumi wa viwanda, kwenda uchumi wa kati, tutai-realize kwa kuandika sheria nzuri.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naomba kuunga mkono hoja ripoti ya Kamati. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii
MHE. PETER J. SERUKAMBA - MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza niwashukuru Waheshimiwa Wabunge wamejadili vizuri ripoti yetu, wamechangia Wabunge 22 na wajumbe watano wameandika kwa maandishi, kwa sababu ya muda nitaomba nisiweze kuwataja.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitaanza na Wizara ya Afya; nimewasikiliza Waheshimiwa Wabunge wote jambo moja ambalo nadhani Serikali mtakubaliana na Waheshimiwa Wabunge moja, ni kuhusu watumishi wa afya. Umefika wakati, tumewekeza fedha nyingi sana kwenye vituo vya afya, kwenye zahanati, hospitali za mikoa, hospitali za wilaya na hospitali za kikanda. Uwekezaji huu ili uweze kuwa na maana ni muhimu sana kuwa na wafanyakazi, niwaombe Serikali mpo hapa tujitahidi sana tupate wafanyakazi kwenye Idara ya Afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ambalo wengi wamelisema na sisi kwenye mapendekezo yetu tumeliweka ni jambo la bima ya afya. Mimi nawaomba sana Serikali kama kuna jambo, na Mheshimiwa Spika alisema tutakuwa tumeleta ukombozi kwa Watanzania ni kuleta Sheria ya Bima ya Afya kwa wote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye hili naomba sana watu wa Serikali tusipate kigugumizi kuleta sheria hii. Kamati yangu ilikwenda Rwanda, Rwanda kila Mnyarwanda ana bima ya afya, lakini kwa sababu wanajua kuna watu maskini wameweka social stratification, wamewagawa watu. Katika wote kuna asilimia karibu nne hawana uwezo kabisa, hao Serikali inawalipia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wenzetu ukilipiwa na Serikali hutakiwi hata kuwa na bank account, so lazima wajue kweli wewe ni maskini kweli kweli. Kwa hiyo, mimi naomba sana Serikali suala hili la bima kwa wote, na mimi nasema siyo suala la NHIF, ni suala la bima ya afya kwa wote. Ukiipata kwenye private sector sawa, ukiwa nayo kwenye Mfumo wa Serikali sawa, cha msingi kila Mtanzania awe na bima ya afya.

Mimi naomba sana Serikali mlete, na hii mtakuja jambo la misamaha, kuna Wabunge wamesema habari ya maiti kukataliwa, lakini jamani gharama za matibabu ni kubwa sana. Ni kweli wanasamehewa watu wengi, ni kweli Serikali haipeleki ruzuku, kwa hiyo kinachotokea sasa hizi hospitali hazitoweza kutoa huduma bora katika mazingira ambayo bajeti yake haifai. Kwa hiyo niwaombe wenzangu Serikalini jitahidini sana ili kupambana hili la misamaha lazima tulete bima ya afya kwa wote.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Afya pia kuna suala la kinga na lishe, nadhani imefika wakati tuwekeze fedha nyingi kwenye kinga pamoja na lishe, tutaokoa magonjwa mengi sana. Ili tuweze kuwekeza kinga lazima turudi kwenye drawing board, tuajiri watu wa social workers waende huko vijijini, hawa ndiyo watasaidia katika haya mambo.

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ambalo wamechangia watu wengi ni kwenye elimu, mimi nataka niseme kidogo kwenye elimu na nina mambo makubwa mawili/matatu; moja, leo dunia inaenda kwa kasi sana, yuko mwanazuoni mmoja anasema; “we stand on the blink of technological revolution will fundamentally alter the way we live, work and relate to one another”.

Kwa nini nimesema hivyo, leo tunakwenda kwenye fourth industrial revolution, tunakwenda kwenye dunia ya teknolojia, kwa hiyo, lazima Wizara ya Elimu turudi tuangalie elimu tunayotoa inaweza kwenda kupambana na mabadiliko haya makubwa ya kiteknolojia?

Mheshimiwa Naibu Spika, nimemsikia Mheshimiwa Naibu Waziri hapa anasema wanatafuta utaratibu kuowesha mitaala, kuangalia mambo ya, jamani! Bado mimi kama Mwenyekiti na Kamati yangu tunaomba Serikali muendelee kutafakari umuhimu mkubwa kuhakikisha tunapitia mfumo upya wa elimu. Tuje na mfumo ambao kuanzia kindergarten mpaka university, tuangalie je, elimu tunayofundisha, mitaala, uwekezaji, fedha vinajibu matakwa ya sasa? Kama hatuhangaiki na hilo tutapata taabu sana huko tuendako.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kuna suala la kuboresha elimu, mimi ningeomba sana watu wa Wizara ya Elimu ili kuboresha elimu kunaendana, unaposema tunaboresha elimu lazima hiyo kazi ifanywe na shule za umma na shule za private. Lazima watu binafsi watusaidie kwenye kuboresha elimu yetu, lakini naomba sana Serikali mtafakari, umefika wakati suala la shule za binafsi, kwamba usimamizi wa shule zote liwe chini ya Wizara ya Elimu, tuondoe TAMISEMI. Kwa sababu TAMISEMI naye ana shule kwa hiyo TAMISEMI kuna conflict of interest, kwa hiyo, kuna maamuzi atafanya TAMISEMI kwa sababu anajua anapendelea shule zake. Kwa hiyo, ili kuondokana na hilo jambo mambo yote ya usimamizi wa elimu Tanzania yarudi Wizara ya Elimu, lakini watoa elimu watakuwepo wa binafsi, itakuwepo TAMISEMI kwa maana ya shule za umma. Mimi nadhani hii itatusaidia sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, nia nyingine ni kuhakikisha kuwa tuna quality na access, lakini hayo yote yatapatikana kama hatutafanya vurugu kwenye shule hizi za binafsi, lakini pia tuangalie uwezekano wa kutoa kodi kwenye shule za binafsi ili tuweze kuzisaidia.

Pia kuna suala la walimu wa sayansi ni jambo kubwa limesemwa na Wabunge wote, tuangalie pia mitaala ya vyuo vya ufundi na mMimi nasema jamani tumesema tunakwenda kwenye uchumi wa viwanda, uchumi wa viwanda unahitaji ….. education so lazima tuangalie upya; je, mitaala yetu ya ufundi inajibu huko tunakotaka kwenda? Kuna shule zinapoteza hawa walimu?

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho ni suala la TBC. TBC ni muhimu sana, lazima tuendelee kuwekeza ili TBC ndiyo pride ya Tanzania, ndiyo pride ya Serikali. Kwa hiyo, lazima tuwekeze kwenye chombo hiki cha kwetu cha Watanzania. Pia na vyombo vya binafsi lazima tuendelee kuvisaidia ili vitusaidie kutoa elimu kwa Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo sana naomba kutoa hoja. (Makofi)

MHE. JULIUS K. LAIZER: Mheshimiwa Naibu Spika, naafiki.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kucahngia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Mheshimiwa Spika, kwanza nianze kabisa kabisa kumpongeza Waziri Lukuvi na Wizara nzima ya Ardhi. Waziri Lukuvi mimi nakuombea heri sana, angalau ni kati ya Mawaziri wachache ukienda ofisini kwake atakusikiliza na utaondoka na jawabu. Mimi huwa najiuliza Lukuvi aidha labda hana kazi sana ama Lukuvi anawapenda Wabunge na anapenda kutatua matatizo. Kwasababu Mawaziri wengine kwa kweli wako busy kweli, ukikutana naye ana haraka na hakusikilizi vizuri. Mheshimiwa Lukuvi mimi naomba niseme nakupongeza sana.

Mheshimiwa Spika, na kwa kiasi kikubwa unaweza ukaona matatizo ya ardhi mengi sana yametatuliwa kipindi hiki cha Mheshimiwa Waziri Lukuvi. Nakushukuru sana Waziri Lukuvi, nawashukuru watendaji wote wa Wizara, Naibu Waziri na Katibu Mkuu kwa kazi kubwa mnayofanya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi nina mambo mawili tu ya kuchangia kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, la kwanza ni suala la National Housing. Nimesoma hapa ndani kwenye kitabu Mheshimiwa Waziri amesema kuhusu National Haousing. Mimi nataka nikushauri Mheshimiwa Waziri; nadhani umefika wakati National Housing iwe na department mbili. Moja ihangaieke na nyumba kwa ajili ya wafanyakazi wa Tanzania ambao ni kwa ajili ya punagisha, na ndilo lilikuwa dhumuni la Shirika hili. Mbili, kuwe kuna wing ya biashara ya kujenga nyumba kwa ajili ya kuuza. Nina uhakika National Housing wakifanyakazi hizi; lakini mkataka wafanye kazi za nyumba za kuuza, nyumba za kupangisha tunawachanganya na ndiyo maana leo kuna miradi mikubwa sana pale Dar es Salaam imesimama.

Mheshimiwa Spika, ningemwomba Mheshimiwa Waziri, ile miradi tukiiacha isimame sisi tunapata hasara kwasababu wale wakandarasi wako site tayari. Kama hamuwalipi wao wanapata interest, wanapata idle time; kwahiyo at the end of the day looser ni Serikali. Whether mikataba ilikuwa mibaya, whether mikataba ilikuwa ni mizuri lakini it is our interest tuhakikishe tunamaliza kazi za majumba yote ya Dar es salaam; kwasababu Shirika limekopa Benki, Shirika limeweka collateral. Sasa kama hatuwezi kumalizia zile nyumba maana yake hizi collateral zinakuaje? Na leo kinachoonekana kama vile National Housing imendoka na Nahemia Mchechu, that is the vibrancy ya National Housing haionekani. Is it true kweli kwamba ni mtu mmoja ameondoka mabo yamebadilika?

Mheshimiwa Spika, mimi sitaki kuamini hayo, nataka kuamini kwamba ningeomba Serikalini turudi kwenye drawing board, kwanza tumalize yale tuliyoyaanza halafu ndipo tuje na mpango mpya; lakini tukisema tunakuja na mpango mpya yale tuliyoyaanza tunayaacha barabarani kwa kweli tunajichoma wenyewe hatima yake collateral zetu zitaanza kuuzwa; nani atalipa hii gharama? Maana project zikisimama zina-accrue interest, kitakachotokea ni nini? Maana yake gharama ni kubwa na Shirika letu tunaliingiza kwenye madeni makubwa. Kwahiyo niwaombe Serikali kwa umoja wenu nawaombeni tatizo la National Housing tulitatue, tuipe nguvu National Housing ifanye kazi yake.

Mheshimiwa Spika, la pili, nataka nizungumzie suala la mortgage financing. Toka nimeingia kwenye Bunge hili tulitunga Sheria ya Mortgage Financing lakini bado interest za benki ni kubwa sana. Matokeo yake ndiyo maana mortgage financing haishamiri, nchi za wenzetu ukimaliza university ukipata kazi siku ya pili tu ziko nyumba za kwenda kupanga ambazo unauziwa kwa interest unalipa baada ya miaka 20, baada ya miaka 30, namna hiyo tutaweza kuwasadia wafanyakazi wa Tanzania. Kama mortgage financing hii ninayoijua ambayo ni benki zimeamua yao, ambayo interest ni kubwa bado mortgage financing Tanzania safari yetu ni ndefu sana. Ningeomba turudi kwenye drawing body tuangalie hizi interest rate, kama interest rate tuziongezee miaka mingi ya kurudisha fedha nina hakika tutakuwa tumewasaidia wafanyakazi wa Tanzania na Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la mwisho, nataka kuzungumzia suala la Land Bank; marehemu Mzee Mungai aliwahi kusema hapa Bungeni kwamba tunatamba sana tuna ardhi kubwa sana, Watanzania tuna ardhi yetu, Wakenya wanatuonea wivu kwa ardhi yetu, kila mtu anatuonea wivu ardhi yetu lakini ardhi isiyoleta mali ya nini. Leo tuna ardhi tunatamba nayo halafu tunakufa njaa, tuna ardhi tunatamba nayo ukiangalia kwenye GDP growth kutoka kwenye agriculture ni ndogo. Nilitarajia tumepata ardhi hii, iwe ni kichocheo kikubwa cha uchumi wa Tanzania. Kwa nini nasema hivyo? Angalia kahawa Tanzania tunazalisha tani 50,000 nchi nzima hapo Uganda tani 288,000, wana ardhi ndogo kuliko sisi tuna ardhi kubwa lakini hakuna ni kwa sababu gani tunataka kila mtu alime. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hatuwezi kuendelea hatuwezi kuja na commercial farming, kama tunataka kila mtu alime matokeo yake itakuwa ni umaskini tu, mama yangu kijijini analima miaka yote lakini hajawahi kujitosheleza kila mwaka anazo heka mbili, heka tatu zinamsaidia nini, hivyo, ningeshauri Mheshimiwa Waziri Lukuvi umefika wakati tupime ardhi yetu tuwe na maeneo ya ardhi ambayo ni kwa ajili ya large plantations, kwa ajili ya commercial farming, hili ndio itatufanya Tanzania tuilishe East Africa, tuilishe Afrika kwa sababu Mungu ametupa ardhi na ametupa maji. Hata hivyo, kama hatuna mpango miji tunadhani nia yetu ni kila mkulima, kila Mtanzania awe na kipande chake kidogo cha ardhi mwisho wa siku kukitoa draught tutakufa njaa.

Mheshimiwa Spika, yako mazao ambayo tulipaswa Tanzania tuwe tuna read kwenye hilo continent, kwa mfano kahawa tuna eneo kubwa sana tulitakiwa tunashinda Ethiopia. Angalia mkonge tuna uwezo wa kuzalisha tani 1,000,000 za mkonge lakini tunazalisha tani 19,000 na tuna ardhi yote hii, kwa nini? Kwa sababu hatuja-embrace commercial farming, hata kule ambako kuna mashamba tunaseme tuwape watu wadogo yeye si ndio atalima mahindi, kesho anaendelea kuwa masikini tu.

Mheshimiwa Spika, haya kwenye chai tuna maeneo makubwa sana ya land ambayo tunaweza tukalima chai, unajua tunazalisha tani ngapi za chai kwa mwaka, tani 19,000, Kenya tani 3,80,000, hivyo ikitokea bei ya chai imeanguka duniani sisi inatuumiza kwa sababu hatuna economics of scale. Sasa mimi sielewi naomba wenzangu watusaidie.

Mheshimiwa Spika, suala la pareto, suala la korosho, korosho tuna tani 210,000, Nigeria wana tani 890,000, ukiangalia hata ugomvi wetu wote ni kwa sababu tunagombania kidogo tulichonacho, lakini tunayo ardhi ya kuweza kulima na tuka-benefit kwenye economics of scale. Hivyo ningeomba Mheshimiwa Waziri Lukuvi umefika wakati na najua hili analiweza, umefika wakati tutengeneze ardhi hata tukiwatafuta investors wakatuambia nataka ardhi ya kulima kitu Fulani, unamwambiwa ardhi hii hapa.

Mheshimiwa Spika, leo akija investor anataka kulima kwa mfano makademia ambao ni very higher product, kuna Wakenya wanakuja hapa kutafuta ardhi, hawaoneshi lakini tunaimba ardhi tunayo. Kama ardhi hii haituletei maendeleo, ardhi haituletei uchumi, nadhani tunaji-contradict na hakuna maana ya kuwa na hii ardhi kama haiwezi kutuletea maendeleo, kwa sababu ardhi ndio maendeleo ya watu.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naomba kuunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Fedha na Mipango
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Spika,na mimi nianze kwa kumpongeza Waziri wa Fedha kwa speech yake nzuri sana.

Mheshimiwa Spika, mimi nitaongelea kwa kweli jambo moja biashara na financial institutions. Asilimia 97 ya kazi Tanzania zinakuwa-offered na private sector, kwa hiyo, nataka tuelewane hapa vizuri kama kuna mwajiri wa kwanza mkubwa Tanzania ni private sector, so lazima huyu mwajiri huyu tumlinde, lazima tuje na instrument za kufanya huyu afanye vizuri zaidi.

Mheshimiwa Spika, tuna benki za biashara tuna benki ya maendeleo ama investment benki kazi yake ni nini. Kazi ya benki hizi ni kuchochea uchumi na biashara hata kama watapata faida lakini cha kwanza ni biashara wachochee. Sasa kinachotokea tungalie investment bank tunaifanyia nini ili iweze kufanya hiyo kazi vizuri. Lazima tuandae mazingira ili hii development bank ifanye vizuri zaidi watu wakope, wawekeze ili biashara ichangamke. Kwenye commercial bank biashara haiwezi kwenda kama commercial bank haziendi.

Mheshimiwa Spika, leo Ndugai umeanzisha biashara utanisamehe, umeweka mkopo benki/umeenda kukopa mkopo benki umeweka mortgage ukishaweka mortgage unapewa pesa. unakwenda kufanyabiashara unashindwa kulipa deni, ukishindwa kulipa deni benki inasema tunauza nyumba TRA wanakuja wanaweka kitu kinaitwa ganesh order kwamba sasa kabla hujachukua hela zako benki huyu tunamdai kodi, tupe kodi yetu, kinachotokea benki inafanyaje NPL zinapanda so leo TRA kwa... kwenye mortgage wao ni super power kuliko aliyetoa fedha maana yake ni nini, maana yake ni moja tu. Watu wengi hawatokopeshwa kwenye mabenki kwa sababu itabidi utajikuta wanaokopeshwa ni hao hao breweries, wakina Azam wale wale wakubwa, wadogo inaanza kuwa shida tukija hapa mbele tunasema kuna mikopo chechefu. Lakini wakati huo huo mabenki yanatoa fedha ikitoka hapo watu wanaenda mahakamani wanaweka order hawezi ku-escute ile order so mahakama inashughulika na banks, TRA inashughulika na banks, NPL zinapanda mabenki yanafanya nini yataanza kufunga branches, yataanza kufanya nini yataanza kupunguza wafanyakazi, yataanza kufanya nini fedha ambazo walikuwa wanalipa za cooperate tax zitaanza kupungua.

Sasa naomba Serikali au contract firming mtu anataka kujenga barabara anakuja anachukua mkopo anapewa anajenga barabara TRA wanakwenda TANROADS huyo mtu huyo tunamdai kabla hujamlipa kule benki tupe hela zetu kabisa, so the priority now is TRA kwa maana ya revenue ni jambo jema, lakini tusisahau kama hizi financial institutions zisipochangamka biashara haitochangamka.

Mheshimiwa Spika, mimi nasema kwa sababu ndiyo maana leo BOT wameshusha treasury bills rate, lakini bado kama unajua interest rate hazijashuka za mikopo kwa sababu gani? Risk bado ni kubwa na ni kwa sababu ya sera hizitunajichanganya. Kwa hiyo, mimi naomba jamani biashara ndiyo itakayofanya nchi hii twende kwa kasi .

Mheshimiwa Spika, kwa mfano mwaka 2015/2016 fedha iliyokuwa inakopwa kwa ajili ya agriculture ilikuwa asilimia 11.2, mwaka 2018 ikashuka to negative four, 2019 kumetokea jambo zuri na ningependa baadaye Waziri atuambie tumepanda kwa asilimia 45. Je, tumepanda 45% kwenye sekta moja hiyo ya korosho tu au na mazao mengine?

Mheshimiwa Spika, personal lending mwaka 2015/ 2016 ilikuwa asilimia 37.2; leo hii personal lending imeshuka kwa asilimia 17.5 maana yake ni nini? Kuna retrenchment watu hawaaminiki, kwa hiyo hawakopesheki. Waziri wa Uwekezaji anisikie mwaka 2015 investment kwa GDP ratio ilikuwa asilimia tano, leo investment imeshuka kwa 2.3 to ratio.

Mheshimiwa Spika, kwa nini nayasema haya maana environment ya biashara ndiyo itafanya kodi iongezeke, ndiyo itafanya tuweze kupata ajira. So lazima tunapotenga policy zetu tulinde biashara na Waziri amesema vizuri sana nimemsikia leo anasema katika sekta ambazo zimekua sana ya Mwakyembe na nyingine, lakini kilimo hakijakua sana, lakini kilimo ni 80% yaani population yetu wanaolima ni asilimia 80 hawa asilimia 80 growth yake asilimia tano sababu ni nini?

Mheshimiwa Spika, sababu ya kwanza tumeendelea kuwa na traditional agriculture bila ku-embrace commercial farming hatuwezi, mifano ipo Zimbabwe ni mfano madhubuti kwa kiburi cha Mugabe aliua commercial farming, leo wanakufa njaa na mashamba/ardhi si wanayo tuna ardhi kubwa sana nilisema juzi, lakini lazima tuje na mkakati wa growth, tujiulize maswali kwenye tumbaku tumekuwa? Kwenye kahawa tumekua? Kwenye pamba tumekua? Kwenye korosho tumekua? Twende huko lazima Waziri wa Fedha mwambie Waziri wa Kilimo tuanze kupambana kwa growth kwamba mwaka kesho seme tumetoka tani tano tumeenda tani kumi haya ndiyo maendeleo, lakini kama hakuna growth leo pamoja Tanzania tuna ardhi kubwa tunazalisha tani 50,000 za kahawa. Uganda tani 288,000 maana yake ni nini kuna kitu hatujafanya na ndiyo narudi kule tukifanya mabenki yafanye vizuri watakopesha wakulima, watakopesha wafanyabiashara, tutapata growth kwenye biasharara na tutapata growth kwenye kilimo.

Mheshimiwa Spika, kilimo ndiyo jambo pekee litakalofanya industrialization iwezekane, maana kilimo ndiyo raw material. Sasa lazima tuulizane hapa, hivi kweli tuna ardhi kubwa tunazalisha tani 19,000 za mkonge wakati tuna capacity installed ya tani milioni moja shida ni nini tunachukua mashamba tunakwenda kuwagawia watu wadogo wadogo, na mimi nasema mimi jamani naomba leo ni- declare kama kuna jambo siliamini ni ujamaa, siamini. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana.

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Baada ya kusema hayo lakini nimalizie kwa neno moja tu, jambo moja, Waziri wa Fedha mwaka jana alitoa amnesty ya watu walipe kodi ambao hawajalipa kodi za nyuma, kuna watu wamelipa asilimia 50, asilimia 70 mpaka kwenda juu, ningemuomba Waziri wa Fedha wale ambao wameonesha interest ya kulipa over 50% a-extend time kwa sababu hawa wana nia hawajamaliza kwasababu hali ya biashara ngumu.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo naomba kuunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 – Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Spika, nikushukuru sana kwa kunipa nafasi hii niweze kuchangia hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Naomba nianze na yafuatayo. Kwanza nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kazi kubwa anayoifanya. Mimi nimepata bahati nimekaa Bungeni hapa muda mrefu kidogo, sijamuona Waziri Mkuu ambaye imekuwa rahisi kwenda kumuona ukiwa na shida na alivyo na uwezo wa kusikiliza. Mungu amjalie sana kwa wema huu na kwa tabia hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nikupongeze sana wewe. Kwa miaka hii mitano umetuongoza vyema sana. Wewe ni mnyenyekevu, Job Ndugai niliyemjua mwaka 2005 ndiyo Job Ndugai mpaka leo mwaka 2020. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia na mimi nichukue nafasi hii kuipongeza sana Serikali ya Awamu ya Tano. Rais Magufuli alivyochaguliwa moja ya mambo kama mnakumbuka alianza mwanzoni ilikuwa ni kubana matumizi, safari za nje, watu kunywa chai na kwenda kwenye semina mahotelini. Kwa kawaida watu wengine hawakuelewa, mimi sasa leo baada ya miaka mitano naona faida za kazi kubwa aliyofanya ya kubana matumizi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, amesema Mheshimiwa Nape kuhusu umeme. Tuna vijiji 12,000, tunapofika Juni, 2020 tutakuwa tumeweka umeme katika vijiji 10,000. Maana yake ni nini kwenye uchumi mpana? Maana yake sasa watoto wetu watasoma vizuri mashuleni, afya itawezekana lakini pia ndiyo modernity ya maisha kwamba tunatoka kwenye kipindi ambacho tulidhani ni mtu tajiri ndiye mwenye umeme, sasa Mheshimiwa Magufuli amefanya umeme ni essential kwa maisha ya binadamu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini pia amefanya kazi kubwa kwenye barabara, aliianza zamani. Naweza nikataja barabara nyingi sana lakini mimi itoshe kusema nampongeza sana kwa barabara ya Kigoma kwenda Nyakanazi. Watu wa Kigoma tunalo deni kwa Mheshimiwa Rais Magufuli. Inawezekana wengine hamjui thamani ya barabara ile, barabara ya Kigoma - Nyakanazi inaenda kutuunganisha watu wote wa Kigoma. Kwa hili, tunayo hakika tutatoa shukurani zetu mwezi Oktoba. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia kwenye afya, kwa bahati nzuri nimekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, ndugu zangu Waheshimiwa Wabunge hakuna kipindi ambacho nchi hii imefanya kwenye afya kuliko miaka hii mitano ya Mheshimiwa Magufuli. Leo hii Hospitali yetu ya Muhimbili imeanza kutoa huduma ambazo huko nyuma zilikuwa lazima uende India, uende South Africa, uende Ulaya; Mheshimiwa Rais Magufuli amefanikiwa huduma hizo sasa zinapatikana hapa kwetu. Nimpongeze sana Mheshimiwa Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia kwenye maji, tumeanzisha RUWASA, Waheshimiwa Wabunge mtakubaliana nami ndani ya miaka mitatu ijayo mtaona huduma za maji vijijini zitaongezeka sana kwa sababu ya RUWASA. Leo hii ukiangalia vijijini hata kwangu kule kuna miradi midogomidogo inasimamiwa na RUWASA, inafanya vizuri sana, nimpongeze sana Mheshimiwa Rais na Serikali kwa kazi kubwa waliyoifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunaangalia uchumi mkubwa, ukiangalia macro-economic stability ya nchi nawapongeza sana watu wa Wizara ya Fedha, bado inflation imebakia chini kwenye single digit, wameweza ku- control exchange rate, wameweza ku- control uchumi mkubwa ule na ndio maana leo sasa unaweza ukaona tunajenga barabara, madaraja na tunaweka maji; hii ni kwa sababu uchumi mkubwa umesimamiwa vizuri sana. Kwa hili naomba mnikubalie, ni ya kiupendeleo kidogo, lakini nimpongeze kaka yangu Mheshimiwa Dkt. Mpango kwa kazi kubwa. Nataka niwasaidie mwelewe na hilo ndio standard za Kigoma, kwa hiyo Mheshimiwa Magufuli alivyomchagua Mheshimiwa Mpango mnaweza mkaona standard za Kigoma, ndio hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo hii angalia kwa sababu ya uchumi kusimamiwa vizuri tunajenga meli Ziwa Nyasa, Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika; ni kwa sababu ya kazi kubwa ya kusimamia uchumi mkubwa. Leo tunaanza kufanya kazi ya infrastructure ambayo ikiisha ninayo hakika Tanzania ya viwanda sasa itawezekana, leo hii Tanzania inawezekana kwenda digital kwa sababu Tanzania tuna mkongo wa Taifa kila Wilaya, kwa hiyo tunayo hakika Tanzania kama nchi tutakwenda digital muda sio mrefu sana. Kwa hiyo kazi yote hii imefanywa na Serikali ya Awamu ya tano kwa usimamizi wa Mheshimiwa Waziri Mkuu pamoja na Mawaziri na Serikali nzima, nawapongeza sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, natoka Kigoma kuna wavuvi; sasa nataka nimwombe rafiki yangu Mheshimiwa Waziri wa Uvuvi, kuna nyavu za TBS na kuna nyavu za Wizara, wale wavuvi tumewachanganya hawajui hii nyavu ni ya TBS ama hii nyavu ni ya Wizara. Niombe sasa waende wakatoe clarification ili watu wangu wa Mwamgongo, Kagunga na Ziwani waweze kupata hizo nyavu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la mwisho, nataka niongelee suala la corona, ni janga kubwa lakini nimekuja na ushauri nimwombe Mheshimiwa Waziri wa Fedha. Corona ni jambo kubwa baya, lakini tutafute opportunity na sisi kama nchi zinaezoendelea, nimesikia African Union wameanza movement, naombeni na sisi kama Tanzania tuwaombe wakubwa wanaotukopesha, lenders wote wasimamishe sisi kulipa madeni ili fedha ambazo tunalipa deni la Taifa zitumike kwenye athari za uchumi zinazoletwa na corona.

Mheshimiwa Spika, corona naiangalia kwa side mbili; moja ni suala la afya na utabibu, linasimamiwa vizuri sana; upande mwingine ambao ni mbaya zaidi ni upande wa uchumi. Leo hii amesema hapa mtu dhahabu tunayo, hatuna pa kuuza kwa sababu wanunuzi hawawezi kuja. Leo hii tunalima, tutaanza kuvuna mazao yetu ya biashara, tutavuna lakini hatutakuwa na pa kuuza kwa sababu wanunuzi hawawezi kuja, hii ni hatari sana kwa uchumi wetu.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo niwaombe leo hii hoteli zinafungwa, migahawa inafungwa, hali ni mbaya ningemwomba Mheshimiwa Waziri wa Fedha atusaidie aongee na Benki ziwasaidie wafanyabiashara Watanzania hasa wale ambao wamepata matatizo Benki zisimamishe loan repayment kwamba sasa hivi kwa mtu anayeta mizigo toka China, kwa mtu mwenye baa, hoteli, mtu mwenye hoteli, transporter, watu wa mafuta, watu wa biashara za kwenda mfano mtu anayeuza maua leo hana pa kuuza maua, lakini ana mkopo benki lazima aendelee kulipa, kwa hiyo ni wakati mgumu, niiombe Serikali iwaombe Benki angalau kwa miezi mitatu yasimamishe loan repayment, kwa sababu hapa tutapata tatizo jingine tutapata corona ya umaskini , tutapata matatizo makubwa zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tuna tatizo la kiafya, lakini tatizo linaloletwa na uchumi linakuwa kubwa sana, kwa hiyo niwaombe watu wa Benki watukubalie kwamba umefika wakati angalau na wao wapate hii pinch wasimamishe loan repayment kwa miezi mitatu tukiangalia hali inavyokwenda.

Mheshimiwa Spika, nimalize kwa kusema tena, nakupongeze sana wewe, Mheshimiwa Waziri Mkuu nampongeza sana kwa kazi kubwa ya kusimamia Serikali, tumeona kazi waliyoifanya pia watuplekee pongezi zetu kwa Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa ya kizalendo, ya kimapinduzi na mtu anayeona mbali. Mheshimiwa Rais Magufuli anaona mbali na ndio maana ya kiongozi na nina hakika Watanzania watamchagua tena mwaka 2015 ili amalizie kipindi chake cha miaka mitano na nina hakika ataipeleka nchi yetu kwenye uchumi wa kati. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naunga mkono hoja ya Mheshimiwa Waziri Mkuu na nakushukuru sana. (Makofi)
The Written Laws (Miscellaneous Amendment) Bill, 2016
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ili nichangie Muswada huu, mabadiliko haya madogo madogo ya sheria hasa hii Sheria ya Uanzishwaji wa Mahakama ya Mafisadi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza unikubalie nianze kwa kumpongeza sana Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuleta Muswada huu. Zaidi nimpongeze Mheshimiwa Rais Magufuli kwa kutekeleza yale ambayo aliyasema wakati wa kampeni. Rais Magufuli alitembea nchini, moja ya jambo alilolifanya na alilolisema ni kwamba, atakapoingia madarakani katika mambo atakayoyafanya mwanzoni ni kuleta Mahakama ya Mafisadi. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais.
Mheshimiwa Naibu Spika, Wazungu wanasema alikuwa na hasira kwamba suala la rushwa limekuwa ni jambo kubwa, limeisumbua sana nchi yetu, nadhani sasa mabadiliko haya ya sheria yatatusaidia kuondoa tatizo hili la rushwa nchini. Niombe sana na nimpongeze Mwanasheria Mkuu wa Serikali na nimwombe yafuatayo kuhakikisha tunaanza kwenda mbele ili Mahakama hii ianze, lakini lazima tuiwezeshe Mahakama ili mashauri haya sasa nayo yasikilizwe.
Mheshimiwa Naibu Spika, nasema hivyo kwa sababu tunazo sheria, ilikuwepo ya wahujumu uchumi na tumeona, tumekuwa na trend sheria zinachelewa sana Mahakamani, kesi zinachelewa sana Mahakamani, moja ya sababu imekuwa ni fedha. Sasa ili kutimiza nia njema hii ya Rais ya kuleta sheria hii, nawaombeni sana watu wa Serikali tujitahidi Mahakama tuzipe uwezo, tuzipe nyenzo ili kesi hizi ziweze kusikilizwa na ili sasa watu waanze kuona makali ya sheria ya uhujumu uchumi na kupambana na ufisadi, itakuwa haina maana tumeleta sheria hii nzuri halafu kesi zinasuasua Mahakamani.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia niwapongeze kwa sababu mmeweka minimum ya bilioni moja kwa sababu pia ingetokea kesi zote za shilingi 200 au 500 zinakwenda kwenye Mahakama hii inge-loose maana yake na ule uzito wa Mahakama hii. Kwa kuamua kuweka ile threshold ya one billion, maana yake sasa tumeamua kupambana na rushwa kubwa. Niombe sana …
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Peter Serukamba, samahani. Waheshimiwa Wabunge, ninazo nafasi mbili zaidi za kuchangia, kwa hiyo, kama mtu anataka kuchangia aniletee jina, Mheshimiwa Peter Serukamba endelea.
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa nasema, niombe sana Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya DPP, suala la kesi za ufisadi liwe ni jambo la priority katika Mahakama zetu. Tunajua tunatoka PCCB tunakwenda kwa DPP, kesi zingine zitakwenda kwa DPP, DPP ataamua otherwise. Tumeamua kuanzisha vita hii ya kupambana na rushwa, basi ningeomba vyombo vyote vya haki vifanye kazi ya kupambana na rushwa. Kwa maana ya kuhakikisha kesi zinafika Mahakamani, Majaji wanakuwa na fedha ili fedha zikipatikana kesi ziamuliwe. Hiyo itatusaidia sana kama Taifa kuona kwamba sasa tumeanza kwenda mbele kupambana na vitendo hivi vya rushwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ambalo nataka kuchangia ni suala la kuandaa kanuni, kwa maana nimesikia watu wa Kamati wanasema kwenye kutunga kanuni angeachiwa Jaji Mkuu peke yake. Bado mimi nasema kwa nia ya kutaka jambo hili tulipe nguvu ya kisiasa na kwamba ionekane nchini vita ya rushwa inaanzia kwa Rais mpaka kwa chini, siyo jambo baya hata kidogo, Rais kuhusishwa wakati wa kuandaa kanuni ashirikiane na Jaji Mkuu. Hii maana yake ni moja tu, ni kutaka kuonesha kwamba, sasa hii vita watu wote tupo kwenye gari moja, tunataka kupambana na vita ya kukomesha rushwa nchini Tanzania. Kwa hiyo, bado nasema kwenye hili sioni tatizo kubwa, ningeomba sana tulifanyie kazi.
Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho ambalo nataka niseme kwenye suala hili, ni kwamba, Mahakama ziko nyingi na kesi nyingi, niwaombe watu wa Serikali tusije tukapeleka message kwamba sasa Mahakama hii ya Mafisadi yenyewe ianze kupata fedha wakati kule kwenye Ardhi, Commercial Court na kesi za kawaida wasiwe na fedha. Hiyo itakuwa ina imbalance na haitotusaidia tutawa- demoralize Mahakama in its totality. Naomba kesi zote zipewe uzito unaostahili, wapewe fedha ili Majaji wetu waweze kutoa haki, maana wanasema haki iliyocheleweshwa nayo huwa nayo siyo nzuri sana, ni vizuri haki iweze kutolewa kwa haraka, lakini ili iweze kutolewa kwa haraka wanahitaji wapate nyenzo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, nimpongeze sana kaka yangu Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuleta sheria hii na mabadiliko haya na kwa kuyaleta haraka. Ninachoomba sasa waende, kanuni zitungwe haraka ili Mahakama hii ianze, wapewe nyenzo ili tuweze kutekeleza kwa vitendo nia njema hii ya Rais wetu ya kutaka kupambana na rushwa nchini. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, naunga mkono hoja.
Muswada wa Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo, wa Mwaka 2016
MHE. PETER A. P. LIJUALIKALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi hii. Pia nachukua nafasi hii kwa kuwa ni mara ya pili kuzungumza, lakini mara ya kwanza tangu baada ya kuwa nimeshinda kesi ya uchaguzi, pamoja na kwamba mapolisi walijaa Ifakara kwa kila aina ya dhana zote za kijeshi, lakini nashukuru kwamba Mahakama imetenda haki. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nachangia Muswada huu unaoanzisha Taasisi ya Utafiti wa Kilimo nikiwa natambua msimamo wa Serikali ya Awamu ya Tano kwenye uanzishaji wa viwanda. Nachangia Muswada huu nikiwa natambua ni Watanzania takribani asilimia 73 wataathiriwa na Muswada huu ambao ni wakulima wa mazao mbalimbali. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma sheria inayoanzisha, hasa pale inapozungumza Mkurugenzi atapatikana vipi; Mkurugenzi atapatikana kwa Rais kuteua. Sisi tumekuwa tukisema sana kwamba mamlaka hii ambayo tunaitoa kwa Rais ya kuteua Wakurugenzi, kuteua viongozi wa taasisi mbalimbali za Serikali, ni madaraka makubwa sana. Kwa kuzingatia asilimia 73 ya Watanzania watakaokwenda kuathirika; kwa kuzingatia msimamo wa Serikali ya Awamu ya Tano ya ujenzi wa viwanda, napata mashaka; tena na katika Muswada huu Rais wetu anapewa mamlaka mengine makubwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, huu Muswada ni wa kitaalam, it’s pure research, pure academic na tumeona miaka hii ya sasa hivi zile posts ambazo ni za kitaalam wakipewa watu ambazo wana kadi za CCM. Hii tumeiona!
Mheshimiwa Mwenyekiti, tukianzia kwenye uteuzi; uteuzi ulikuwa ni Wakurugenzi wa Halmashauri mbalimbali na juzi ameteuliwa mtu mmoja hapa Manispaa ya Dodoma kuwa Mkurugenzi wa Jiji ambaye kwa sababu tu ana kadi ya CCM, sheria inasema kabisa uteuzi uzingatie vigezo vifuatavyo; na hapa tumeweka vigezo, tumeweka…
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nitashangaa sana…
Taarifa...
MHE. PETER A. P. LIJUALIKALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, hii taarifa siipokei. Nilichokisema kimo kwenye Muswada. Nazungumzia sifa za wanaoteuliwa. Ukisoma mwongozo wa kumchangua DAS anatakiwa kuwa mtu ambaye amefanya kazi kwenye Utumishi wa Umma miaka siyo chini ya 10.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nipo kwenye hoja, nazungumzia sifa za wanaoteuliwa. Nimesema huu Muswada unakwenda kuathiri asilimia 73 ya Watanzania, siyo kitu kidogo, lazima vitu hivi vifuate taratibu. Leo hapa tupo kwenye sheria, lakini kuna maamuzi mengine yanafanyika hayafuati sheria; na huu ni ukweli uko wazi. Kwa hiyo, naomba sasa tutunge sheria hii, kile ambacho kinapita hapa ndiyo kifanyiwe kazi, lakini siyo utafute kadi za watu, kwa sababu ya kadi ndiyo achaguliwe kuwa Mkurugenzi. (Makofi/Kelele)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia niseme jambo lingine. Kule kwangu Ifakara kuna Kituo cha KATRIN, ni kituo cha utafiti. Kituo hiki kinafanya tafiti ya mambo ya mpunga na nini, lakini ni kama vile kimekufa. Hakina nguvu, hakina fedha, hakifanyi kazi yoyote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nadhani labda kwa sheria hii jinsi ilivyo, inaweza kusaidia na ndiyo maana nasema kwamba hii sheria inakwenda kuathiri watu wengi. Kwa hiyo, tunapoongea haya mambo, siyo kwa sababu ya mtu kumsema, tunasema kwa sababu haya mambo yanakwenda kuathiri Watanzania wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia niseme jambo lingine kwamba sheria inasema taasisi hii itakuwa na uwezo wa kushtaki na kushtakiwa. Pia inasema Taasisi hii itakuwa na uwezo wa kumiliki mali za kila Taasisi, kila kituo ambacho kilikuwa kinafanya tafiti; lakini sheria inasema kwamba hakuna mtu atakayetakiwa kushiaki ikiwa hajapeleka notice ya siku 90 kwenda kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Asipofanya hivyo, maana yake ni kwamba anakosa haki ya kwenda kushtaki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kipengele hiki kinawanyima Watanzania wengi watakaokwenda kudhulumiwa haki zao na ukizingatia sasa hivi kuna migogoro mingi ya ardhi. Kwa mfano, kule kwangu Ifakara, Kituo hiki cha KATRIN kina migogoro mingi sana ya ardhi. Leo ukimwambia Mtanzania asiishtaki KATRIN, ashtaki taasisi kwa kutoa notice ya siku 90, maana yake ni kwenda kumdhulumu Mtanzania huyu asiweze kupata haki yake kisheria na ya Kikatiba.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika sheria hii, huku mbele kwenye mambo ambayo yanahusu utafiti, inasema kwamba kutakuwa na tafiti wa kutafuta masoko. Ningekuwa mimi ndiyo Waziri wa Kilimo, leo ningejiuzulu. (Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, haiwezekani miaka 50 wakulima wa Dumila wanalima, nyanya zinaoza na Serikali ipo. Haiwezekani Serikali inayosema Hapa Kazi Tu, Watanzania wanalima nyanya, wanatumia nguvu zao, wanatumia fedha zao, wanatumia akili yao, wanatumia kila kitu na Serikali hamtoi hata senti 10, wanapata mazao halafu eti baadaye soko hakuna, ng‟ombe wanakula, Waziri wa Kilimo yuko hapa amekaa analipwa mshahara! Ni Taifa la Tanzania ndipo unaweza ukaona hali kama hii. Hiyo hapa kazi tu iko wapi? Kama Wakulima wanatumia nguvu zao, wanatumia fedha zao, wanalima, wanajitoa halafu soko hakuna; Serikali imekaa, sijaona tamko hata la Waziri! Sijaona Waziri akisema ni kwa nini na amechukua hatua gani kunusuru watu wa Dumila waweze kupata haki yao, waweze kupata soko? Serikali imekaa, hamna tamko. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme, ukiangalia dunia ya leo, huu Muswada nilitegemea ungetoa majibu ya namna gani wananchi wanakwenda ku-access information. Nilitegemea sheria itasema tutakuwa na integrated system ambayo inafanya kila mtu aweze ku-access. Yaani SUA wakifanya research kuhusu kilimo, sehemu nyingine wakifanya research kuwe na system inayopokea taarifa zote hizi ili mtu leo akiamua kufanya research sehemu yoyote anaingia kwenye hiyo system, kwenye hiyo database ana-access information.
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo SUA wanafanya yao huko, leo tena tunakaa hapa Wabunge, hii sheria inapitishwa hawa watafanya huko, hawa watafanya kule; dunia ya leo ambapo information is power, sioni kwenye huu Muswada. Ni kama vile tuko miaka 60 nyuma. Yaani hii system ya nchi haiko intergrated, kila mtu na sehemu yake anafanya kazi yake peke yake. Hawa wanafanya vitu huku, hawa wanafanya huku, where is technology kwenye hii nchi yetu?
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa niseme kazi ambayo iko tu hapa, watu wakisikia UKUTA, basi vurugu; Mapolisi mtaani, lakini kazi ambayo ni tangible ambazo unaziona kabisa za kutumia akili; hatuwezi kuwa na nchi ambayo, yaani kitu kidogo kama hiki anakuja mtaalam na Muswada anashindwa kusema kwamba research which is pure academic; tunashindwa kuwa na system ambayo watu wanaweza ku-access information vizuri na tukafanya research zetu vizuri kwa maendeleo ya kilimo na kadhalika?
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa na hayo tu, ahsante sana.
Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari za Mwaka 2016
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze kwa kuunga mkono hoja hii. Leo mwenzenu Waheshimiwa Wabunge nina furaha kubwa sana. Nina furaha kubwa, nitumie maneno machache sana kuonesha kwamba nina furaha; yametimia, lile jipu lililowashinda wengine kwa miaka 23, leo tunakwenda kulipasua. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Waheshimiwa Wabunge wa Bunge hili tujisifie, kazi ambayo iliwashinda wote sisi tunakwenda kuifanya leo. Waheshimiwa Wabunge mkitaka kujua kwamba Muswada huu ni mzuri sikilizeni waliochangia wote kuanzia jana mpaka leo. Kila aliyechangia hapa, kama kuna mtu asimame aliyepinga vifungu, wote waliamua kucheza siasa tu hapa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maana ya sheria yenyewe, hakuna aliyehangaika kuweka neno kwa sababu kila kitu kimefanywa. Kwa hiyo, nilikuwa nawasikiliza lakini kwa sababu sisi ni wanasiasa, ukipewa jukwaa lazima ucheze nalo, na kila mtu akawa anaamua staili yake. Hata hivyo, naomba kusema, nimesoma ripoti ya ndugu yangu wa Kambi ya Upinzani. Soma ile ripoti mambo yote anayoyasema kwenye Muswada yameshafutwa, lakini yeye ameyaleta. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimewasikiliza wengine wote wanayoyasema kwenye Muswada hayamo. Tumebaki tunasema wadau hawakushirikishwa, naomba niseme Waheshimiwa Wabunge, kama kuna wadau ambao wanasema hawakushirikishwa ni kwa sababu hawakutaka kushiriki. Narudia tena, wadau ambao hawakushiriki ni kwa sababu hawakutaka kushiriki na hawakutaka kushiriki kwa makusudi. Maana wanasema Muswada hawajausoma, kesho unawaona kwenye kipindi cha TV wanaujadili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wamekuja kwenye Kamati, wanasema mmetupa siku tatu hatujamaliza. Baada ya siku mbili wako ITV wanajadili kifungu kwa kifungu. Walitaka kuendeleza tabia ileile ya kuuondoa Muswada Bungeni, sasa wamesahau hii ni Awamu ya Tano, Awamu ya Tano hatutishwi, basi. Niwaambieni Mwenyekiti huyu hatishwi. Tumeambiwa tufanye kazi tu, kazi yetu ni kutunga sheria, naombeni Wabunge tutunge sheria hii. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna watu wengine tena nawaheshimu kweli wanasema unajua uandishi wa habari ni moyo tu! Eeh, kweli? Uandishi wa habari ni passion tu basi, lakini kuwa Mchumi si passion! Kuwa Engineer si passion! Kuwa Accountant si passion kweli! Tunataka tupate sifa rahisi sana hizi, tusiwadanganye waandishi wa habari. Sheria hii imeweka vifungu vinavyowasaidia Waandishi wa Habari wa Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mtu anapinga accreditation hapa. Jamani tumesema tutaweka vigezo vya nani apewe leseni pamoja na Press Card, lakini wale ambao hawana leseni, hawana Press Card hawazuiliwi kuandika. Wale wenye passion anaowasema Mheshimiwa Zitto wataendelea kuandika, lakini hawatakuwa accredited kama ambavyo mimi ni Accountant kama sina CPA siwezi kusaini Financial Statements, lakini hainizuwii kuandika vitabu vya uhasibu. Ukiwa Mwanasheria hujashinda Uwakili Mahakamani huendi, lakini kazi za Sheria huwezi kuacha kufanya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naombeni tusiwadanganye Watanzania. Tusiwadanganye waandishi wa habari, wasaidieni wandishi wa habari, sheria hii inakwenda kusaidia journalists in Tanzania. Mambo yote ya printing yameondoka, 20(3) ambayo yalikuwa yana tatizo yamendoka, kila ambacho kina tatizo kimeondoka! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, yuko rafiki yangu mmoja mwandishi wa habari alinipigia simu, ni rafiki yangu wa siku nyingi sana, nikamuuliza swali niambie Muswada huu una tatizo gani? Akaniambia umesoma kifungu cha 20(3)? Nikamwambia nimesoma kina matatizo tutakiondoa. Akasema mengine sina shida, lakini namwona kwenye TV anasema Mheshimiwa Serukamba jipu! Ndugu yangu, sasa jipu kwa sababu ya 20(3)? Bahati mbaya jipu lenyewe hili halitumbuliki, ndiyo bahati mbaya sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mnajua Waheshimiwa Wabunge hawa jamaa walitaka tuuondoe Muswada na wakaamua kushirikiana na baadhi ya wenzetu kwamba, waje na pressure tutoe Muswada, ukiwauliza sababu hawana! Ukiwaambia kifungu gani kibaya, hawakisemi! Sheria kandamizi, sheria ya mwaka 28, sheria ya kikoloni! Hata rafiki yangu msomi Mheshimiwa Tundu Lissu anaongea hapa, twambie Mheshimiwa Tundu Lissu kifungu namba fulani kina matatizo, ndiyo kazi ya kutunga sheria.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nawaelewa, jana Mheshimiwa Sugu alisema hivi, naomba niwakumbushe. Rafiki yangu Mheshimiwa Joseph Mbilinyi (Sugu) jana alisema maneno yafuatayo, alisema, naomba nisome tu najua Muswada huu utapita, Muswada huu utasainiwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Waheshimiwa Wabunge wa CCM, tuongee ki-CCM, tufanye kazi hii kwa sababu tuko wengi. Naomba wana CCM tumfanyie kazi na Rais ametuambia wana CCM tumalize hii kazi, akasaini, tumalize leo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi niwaambieni ukiona unaleta jambo zuri wanaokupinga wakasema zuri, ujue jambo lenyewe baya; ukiona unaleta jambo wale wanaokupinga wanapiga kelele, maana yake jambo lenyewe zuri. Maana ukiangalia wote waliosimama hapa, hata ambao walikuja kwenye Kamati wakachangia mawazo yao yakaingia, rafiki yangu Mheshimiwa Devotha hapa kuna mambo yameingia yalikuwa ni mawazo yake yeye, leo anayakataa hapa ndani! Hii ni nini? Hebu tufanye kazi ya kutunga sheria (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ningeweza kwenda kifungu baada ya kifungu, ningeweza kusoma vyote, lakini ninachoweza kusema Serikali imekuwa sikivu, tumefanya hii kazi, tumetunga sheria nzuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimalize kwa kusema, Waheshimiwa Wabunge leo tunakwenda kumaliza hii kazi, tutunge hii sheria, naomba tuunge mkono Serikali. Isingewezekana na niwakumbushe Wabunge wa CCM, hivi Wabunge wa CCM ni lini kitu kililetwa hapa ndani wale wakatuunga mkono, lini? Maana bajeti ya Serikali walikimbia! Bajeti za Mawizara walikimbia! Mlitegemea leo watuunge mkono humu ndani? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tutekeleze wajibu wetu. Bahati njema sana kwenye suala hili wengi ndio wanaoshinda, mtapiga kelele, lakini sheria itatungwa. Mtatutukana, lakini sheria itatungwa, wala haina shida tukaneni tu, lakini sheria itafanyaje, itatungwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru.
Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Maliasili wa Mwaka 2017.
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, muda ni mdogo, lakini Waheshimiwa Wabunge leo ni siku muhimu sana, ni siku ya mapinduzi ya kiuchumi. Ukisoma sheria zile mbili ni siku ambayo Watanzania tumeamua kwa sauti moja kwamba mali zilizopo Tanzania ni za kwetu. Kwa namna yoyote ile maamuzi haya lazima tumpongeze Mheshimiwa Rais Magufuli. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Rais Magufuli amefanya kazi hii, amezidi kuthibitisha uzalendo wake lakini amezidi kuonesha nia njema ya kutaka kuliendeleza Taifa letu. Nilisema siku ile wakati nachangia Wizara ya Ujenzi kwamba naamini watakaokuja kuandika historia ya Tanzania, jina la Rais Magufuli litaandikwa kwa wino wa dhahabu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu ya muda, nataka nimpe angalizo Waziri wa Sheria. Waziri wa Sheria tunatunga sheria hii leo, hizi ndogo mbili, ambazo tunakwenda kutambua ukuu na mali za Tanzania. Ninayo hakika wakubwa duniani watalalamika, wawekezaji wakubwa watalalamika, Bretton Woods Institutions zitalalamika, nikuombe Waziri Profesa usije ukaenda ukapata pressure za hao wakubwa ukaja hapa kufanya amendments, nitaongoza kukupinga. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, narudia tena, tunatunga sheria hizi ambazo ni ukombozi wa nchi yetu, muende huko mkakutane na wakubwa halafu Waziri wa Sheria uje kutaka kufanya amendment, nina-register nitakupinga. Ni vizuri tuwe tayari yatakayotokea tujifunge mkanda. Mwalimu wa Taifa alituambia sisi ni Taifa lazima tuwe tayari kujifunga mkanda. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wako wanaosema wakubwa watanuna, sawa, wanune, waende, mali ni yetu. Watakuja watachimba hata watoto wa watoto wangu. Maana haya tumeamua, haya ni maamuzi makubwa, amesema Mheshimiwa Zitto kwamba haya ni maamuzi makubwa na mimi nasema leo Bunge hili tumeingia kwenye historia kufanya maamuzi makubwa.

Naombeni Wabunge tusirudi nyuma, wanaosema tuna haraka, mlitaka tuanze lini? Tumeibiwa vya kutosha, hili jambo halitakiwi tuulizane kuhusu dharura, kwanza limechelewa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, yamekuwepo malalamiko kwamba tunaibiwa na tatu tumepewa opportunity ya kwenda ku-renegotiate mikataba yote iliyokwishapita, tunataka nini kama Bunge? Tumepewa opportunity kama Taifa, naombeni Bunge tufanye kazi yetu tuhakikishe tunakwenda ku-renegotiate. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wanasema tunakwenda kupata shareholding, mimi nataka muende mbali zaidi Mheshimiwa Waziri, naomba tukubaliane hapa kama Bunge madini yote yaliyobaki tufanye exploration wenyewe. Tukifanya exploration wenyewe anayekuja tuta-determine sisi tuwe na percent ngapi. Nafuu kila hata baada ya miaka mitano tufanye exploration moja, tuanze mgodi mmoja, lakini tutaanza na asilimia 50 tutapata fedha nyingi kama Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine nataka kumpongeza Mheshimiwa Waziri kwa suala la kuamua watu wote wanaofanya biashara ya resources Tanzania wafungue akaunti zao hapa. Maana yake ni nini? Fedha watakazoweka kwenye benki zetu na sisi Wabunge tutazitumia, tutakwenda kukopa, ndiyo banking inavyofanya kazi, kwa hiyo, uchumi wetu utachanganya kwa wao kuweka fedha zao kwenye akaunti zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wako wanaosema wamechukua mikopo duniani, yes! Mikopo wamechukua, bado hata ukikopa nje unaweza ukalipa kutokea kwenye benki ya Tanzania, it is normal, ni TISS tu. Kwa hiyo, tunachosema sisi kopeni huko nje, lakini fedha leta weka Tanzania ili na sisi Watanzania tufaidike na fedha hizo ambazo ziko kwenye uchumi wetu. Nakupongeza sana Mheshimiwa Waziri kwa kuleta hili na kwenye Ripoti ya Bomani najua hili lilikuwa moja ya sharti la Ripoti ya Bomani kwamba lazima wafungue akaunti zao hapa Tanzania.
Muswada wa Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi wa Mwaka 2017.
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, muda ni mdogo, lakini Waheshimiwa Wabunge leo ni siku muhimu sana, ni siku ya mapinduzi ya kiuchumi. Ukisoma sheria zile mbili ni siku ambayo Watanzania tumeamua kwa sauti moja kwamba mali zilizopo Tanzania ni za kwetu. Kwa namna yoyote ile maamuzi haya lazima tumpongeze Mheshimiwa Rais Magufuli. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Rais Magufuli amefanya kazi hii, amezidi kuthibitisha uzalendo wake lakini amezidi kuonesha nia njema ya kutaka kuliendeleza Taifa letu. Nilisema siku ile wakati nachangia Wizara ya Ujenzi kwamba naamini watakaokuja kuandika historia ya Tanzania, jina la Rais Magufuli litaandikwa kwa wino wa dhahabu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu ya muda, nataka nimpe angalizo Waziri wa Sheria. Waziri wa Sheria tunatunga sheria hii leo, hizi ndogo mbili, ambazo tunakwenda kutambua ukuu na mali za Tanzania. Ninayo hakika wakubwa duniani watalalamika, wawekezaji wakubwa watalalamika, Bretton Woods Institutions zitalalamika, nikuombe Waziri Profesa usije ukaenda ukapata pressure za hao wakubwa ukaja hapa kufanya amendments, nitaongoza kukupinga. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, narudia tena, tunatunga sheria hizi ambazo ni ukombozi wa nchi yetu, muende huko mkakutane na wakubwa halafu Waziri wa Sheria uje kutaka kufanya amendment, nina-register nitakupinga. Ni vizuri tuwe tayari yatakayotokea tujifunge mkanda. Mwalimu wa Taifa alituambia sisi ni Taifa lazima tuwe tayari kujifunga mkanda. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wako wanaosema wakubwa watanuna, sawa, wanune, waende, mali ni yetu. Watakuja watachimba hata watoto wa watoto wangu. Maana haya tumeamua, haya ni maamuzi makubwa, amesema Mheshimiwa Zitto kwamba haya ni maamuzi makubwa na mimi nasema leo Bunge hili tumeingia kwenye historia kufanya maamuzi makubwa.

Naombeni Wabunge tusirudi nyuma, wanaosema tuna haraka, mlitaka tuanze lini? Tumeibiwa vya kutosha, hili jambo halitakiwi tuulizane kuhusu dharura, kwanza limechelewa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, yamekuwepo malalamiko kwamba tunaibiwa na tatu tumepewa opportunity ya kwenda ku-renegotiate mikataba yote iliyokwishapita, tunataka nini kama Bunge? Tumepewa opportunity kama Taifa, naombeni Bunge tufanye kazi yetu tuhakikishe tunakwenda ku-renegotiate. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wanasema tunakwenda kupata shareholding, mimi nataka muende mbali zaidi Mheshimiwa Waziri, naomba tukubaliane hapa kama Bunge madini yote yaliyobaki tufanye exploration wenyewe. Tukifanya exploration wenyewe anayekuja tuta-determine sisi tuwe na percent ngapi. Nafuu kila hata baada ya miaka mitano tufanye exploration moja, tuanze mgodi mmoja, lakini tutaanza na asilimia 50 tutapata fedha nyingi kama Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine nataka kumpongeza Mheshimiwa Waziri kwa suala la kuamua watu wote wanaofanya biashara ya resources Tanzania wafungue akaunti zao hapa. Maana yake ni nini? Fedha watakazoweka kwenye benki zetu na sisi Wabunge tutazitumia, tutakwenda kukopa, ndiyo banking inavyofanya kazi, kwa hiyo, uchumi wetu utachanganya kwa wao kuweka fedha zao kwenye akaunti zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wako wanaosema wamechukua mikopo duniani, yes! Mikopo wamechukua, bado hata ukikopa nje unaweza ukalipa kutokea kwenye benki ya Tanzania, it is normal, ni TISS tu. Kwa hiyo, tunachosema sisi kopeni huko nje, lakini fedha leta weka Tanzania ili na sisi Watanzania tufaidike na fedha hizo ambazo ziko kwenye uchumi wetu. Nakupongeza sana Mheshimiwa Waziri kwa kuleta hili na kwenye Ripoti ya Bomani najua hili lilikuwa moja ya sharti la Ripoti ya Bomani kwamba lazima wafungue akaunti zao hapa Tanzania.
Muswada wa Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma wa Mwaka 2017
MHE. PETER. J SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kwanza na naomba kwanza niishukuru Serikali kwa kuleta muswada huu. Kipekee kabisa namshukuru Mheshimiwa Rais. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma historia ya muswada huu, ilianza mwaka 2004 huko, lakini wote hawakufanya decision hii, Rais huyu amechukua maamuzi haya magumu lakini maamuzi mazuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, nilitaka kusema kwamba sheria hii tunayotunga leo, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, guarantor ni Serikali, tusije tukasahau hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda kusoma standard za ILO, minimum ya pensheni ya ILO ni asilimia 40; Ulaya Magharibi ni asilimia 42 mpaka asilimia 74; Ulaya Mashariki ni asilimia 46 mpaka asilimia 63. Latin America ni asilimia 46 mpaka 77; Tanzania kwa wale ambao labda hawajui ni kati ya nchi chache zenye kiwango kikubwa sana cha pensheni. Tanzania ni asilimia 72.5. Tumewazidi wengi katika continent hii. Naipongeza sana Serikali kwenye hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nimeamua kusema hili kwanza? Nataka tuelewane, sisi Kamati tumewaomba Serikali wako wachache watesema otherwise, lakini unanimously Kamati tulisema formula iwekwe kwenye kanuni. Sababu zetu ni moja, mbili, tatu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sababu ya kwanza, tumesema watakapotunga sheria hii wakafanya actuarial valuation. Actuarial valuation inafanywa na SSRA, siyo na mifuko yenyewe. Huweze kumwambia mtu aku-access wewe mwenyewe. Regulatory akafanye hiyo kazi, access hiyo mifuko, baada ya pale wakutane kwenye utatu mtakatifu, waweze kuandaa formula na lazima formula hii iwezeshe mifuko hii kuendelea kuwapo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imefanya maamuzi haya kwa sababu ya kutatua matatizo tuliyokuwa nayo ili wafanyakazi wa Tanzania wasipate shida. Kwa hiyo, bado naomba Serikali ifanye kazi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la tatu, nimemsikiliza dada yangu wa upinzani, aliyekuwa anasoma, nadhani hajasoma muswada huu mpya. Serikali imeamua haitahamisha member yeyote. Members watabaki kule walikokuwa. Wanasheria wenzangu mnajua, hatutungi retrospective law. Waajiriwa wapya ndio watakwenda kwenye hiyo mifuko mipya. Hii ni kwa sababu ungewahamisha leo, unawahamisha na contribution, investment zao unafanyaje? Liabilities zao anabaki nazo nani? Kwa hiyo, ilikuwa ni lazima wabaki, halafu tuweke cutoff, wale wanaokuja mbele, wataingia kwenye sheria hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, umuhimu wa SSRA, watu wanaweza wasilione, ndiyo maana tumependekeza mifuko yote ya hifadhi ya jamii iwe chini ya mtu mmoja, NHIF iende huko, CHF iende huko na mifuko yote ili kuwe na regulator ambaye anasimamia shughuli hii. Kwa hiyo, ni muhimu sana kwa ajili ya maendeleo ya mfuko wa jamii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ambalo tumelisema kwenye kamati na naomba personally niliseme, ni suala la Makatibu Wakuu. Makatibu Wakuu ndio Maafisa Masurufu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wewe umekaa Serikalini; kwa kweli niwapongeze kwanza hata hao Makatibu Wakuu na watu wa Serikali. Maana wangekuwa wanajifikiria wao, wasingeileta hii sheria. Kwa sababu sheria hii ilikuwa inawa- benefit wao, hasa waliokuwa kwenye PSPF. Kwa sababu ya kuangalia mbali, kuangalia Taifa, wameileta hii sheria. Naomba sana Makatibu Wakuu wenyewe hawafiki 20. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaongelea yule ambaye amefanya kazi mpaka siku ya kustaafu ni Katibu Mkuu. Hawa ndio wanatunza pesa, otherwise tusipowa-consider, naomba Serikali mkatafakari, wataanza kujitafutia pensheni yao pembeni. Tunazuia haya, maana haiwezekani mimi ni Katibu Mkuu, aliye chini yangu amekuwa taken care, bado hatueleweki.

Naiomba Serikali iende kulitafakari namna tunachoweza kufanya kuhusu Makatibu Wakuu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu umesema tupunguze muda, ukiangalia sheria hii, kwanza naipongeza Serikali kwa sababu karibu amendments zote ambazo Kamati tulitoa, kwa kweli zimeingizwa. Unaweza ukaona aliye na ule muswada wa Oktoba na huu, tofauti ni kubwa sana. Serikali imeanzisha mafao mapya, lakini imehakikisha mafao yanayotolewa mifuko yote ni sawa, lakini under section 29 inasema, bodi ikiona inataka kuanzaisha fao lingine, wao ndiyo wataangalia wataweka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho ni suala la wale waliokuwa wana-benefit hasa kwenye fao la elimu. Kama Serikali inaona hilo fao hapana, naombeni wale watoto ambao wazazi wao labda hawapo, ni maskini, wamefariki, waliokuwa wanasomeshwa kwenye arrangement hizo, tusiwaache barabarani. Wale ni watoto wa Tanzania, twende tuhakikishe mifuko hiyo inayowachukua, iende iwafanyie kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho naiomba Serikali ihakikishe inasimamia wafanyakazi wote wasipoteze ajira zao. Naamini wakifanya job evaluation, wakaangalia mifuko yote miwili, wakaangalia NHIF, wakaangalia Workers Compensation, bado unaweza ukawa-rearrange wafanyakazi walioko kwenye hii mifuko yote na kila mtu akapata kazi na kama Taifa tukaenda mbele. Baada ya kusema hayo, naunga mkono hoja hii na niwaomba Waheshimiwa Wabunge, tunaandika historia, tunatunga sheria ambayo itafanya hifadhi ya jamii Tanzania iendelee kuwepo kwa muda mrefu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
Muswada wa Sheria ya Bodi ya Kitaalam ya Walimu Tanzania wa Mwaka 2018
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi, lakini naomba nitoe shukurani zangu za dhati na furaha kubwa sana niliyonayo leo. Leo tunaandika historia kama Bunge, tunaenda kutambua hadhi ya mwalimu Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninayo hakika Marehemu Mheshimiwa Bilago angekuwepo angeanza na maneno yafuatayo. Siku zote aliniambia ukimaliza Uenyekiti hujatupa Teachers Professional Board utakuwa hujawatendea haki walimu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nawaomba Waheshimiwa Wabunge tusiwafanye walimu ni watu hohe hahe, tusiwafanye walimu ni jambo tu la kupita. Bunge hili limetunga Sheria ya Bodi ya Wahandisi, Bodi ya Wanasheria, Bodi ya Wakandarasi, hata juzi tu tumetunga Bodi ya Wasaidizi wa Madaktari. Ni kosa kubwa sana Waheshimiwa Wabunge kuukata Muswada huu. Tunaweza tukausahihisha Muswada huu lakini tusichanganye taaluma ya ualimu na maslahi ya malimu, hivi ni vitu tofauti sana. Namshukuru sana Mheshimiwa Prof. Ndalichako kwa kuleta jambo hili. Ni jambo ambalo vyama vyote na wote waliokuja mbele ya Kamati yetu walikuwa wanalitaka miaka yote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tumeshuhudia watoto wetu wanafundishwa na walimu ambao sio walimu na ukikosea kwenye kufundisha watoto huu ndiyo msingi wa kuwa na elimu bora. Ndiyo maana leo tumeona walimu kwenye shule za private wanafanya vituko lakini hakuna cha kuwafanya. Mikono ya Waziri wa Elimu imefungwa, hawezi kushughulika na mwalimu aliyeko kwenye private school. Mwalimu aliyeajiriwa kwenye Shule ya Sekondari ya Serukamba anafuata masharti yangu mimi. Hiki tunachofanya leo Waheshimiwa Wabunge, tunataka tutambue hadhi ya walimu, profession ya ualimu lakini tuwawekee makatazo. Ukifanya makatazo hayo, tutakunyang’anya cheti cha kufundisha. Ndicho kilichofanywa na Muswada huu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakubali yako matatizo ya walimu; mishahara midogo, hawapati stahiki zao, hiyo ndiyo shughuli ya TSC. Tanzania Service Commission ina shughuli moja kuhakikisha inahangaika na maslahi ya walimu walioajiriwa Serikalini lakini Bodi hii inakuja kutambua nani ni mwalimu. Ukishamaliza ualimu, tumependekeza wasianze na provisional registration, waende moja kwa moja wasajiliwe kwa sababu ukishawasajili utakapokuja kwenye leseni ndiyo tumeweka masharti sasa utuambie umefundisha mwaka mmoja. Kama umefundisha mwaka mmoja, tutakuwa tumeangalia tabia yako, tumefuatilia unavyoji- conduct, then tunakupa leseni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine, sasa tutawapa walimu ajira. Sasa hivi walimu hawatategemea kuajiriwa na Serikali peke yake, kwa sababu walimu wote waliosajiliwa, walimu wenye leseni tunakwenda kuwapa hadhi kama Taifa. Akishakuwa na leseni yake anaweza akaenda Afrika Mashariki akafundisha. Tumeona juzi Rwanda ilitaka walimu wa Kiswahili Watanzania hawakuajiriwa, unajua sababu? Hawana leseni ya kufundishia. Hao wote mnaosema wanasajiliwa na TSC ni walimu wanaoajiriwa na Serikali, ndiyo wamewa-register kule, wamefanya iwatambue. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, matatizo mengine hapa tusiyachanganye matatizo ya mfumo na Bodi. Kwenye Bodi ya Injinia siyo Injinia wote wanafanya kazi TANROADS, TAMISEMI au Bunge, mainjinia wote kokote waliko wanatambuliwa kama mainjinia na wana Bodi yao. Hatuwezi kukaa hapa Waheshimiwa Wabunge tupinge Bodi hii ya Walimu, hapana, tutakuwa hatuwatendei haki walimu. Yako mambo hata kwenye Kamati tumesema, tuangalie kwenye leseni, fee yao isiwe kubwa sana kwa sababu walimu ni wengi, fee ipungue, lakini lazima tusimamie maadili ya ualimu, taaluma ya ualimu lazima tuisimamie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mnakumbuka juzi kwenye mitandao, tumesema hapa, mwalimu mmoja anatembea na watoto wa kike wamemlalia hapa, imezagaa lakini hakuna cha kumfanya. Tungekuwa na Bodi hii, leo tungeshamnyang’anya leseni, yule asingekuwa mwalimu. Nawaomba sana wenzangu, Bodi hii ni jambo kubwa, tumefanya mageuzi makubwa kwa kada ya ualimu Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali iende mbali zaidi, Mheshimiwa Waziri Prof. Ndalichako tuanze ku-define
nani anakuwa mwalimu sasa? Haiwezekani aliyepata Division Three au Division Four ndiyo aende kufundisha watoto wetu, tubadilishe. Umefika wakati kwamba ukifaulu, ukipata Division One, kazi yako ya kwanza mwalimu, ziko nchi zimefanya. Kwa kufanya hivyo, tutaanza sasa kuupa hadhi kubwa zaidi ualimu lakini pia tutapata walimu ambao watafanya kazi nzuri zaidi, lakini as it is now walimu wapo, vyuo vipo sasa tuanze kwenda mbele zaidi; tumeshaandaa Bodi na baada ya Bodi tuanze sasa kuhangaika na kuweka watu gani wanakuwa walimu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wako watu wanasema kuna kazi za TSC. TSC ina kazi zake, inahangaika na walimu walioajiriwa na Serikali, ikahangaike kuhakikisha walimu sasa wanapata stahiki zao, mishahara na vyeo. Hii ndiyo kazi ya Tanzania Service Commission.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba sana Serikali, tunakoenda, nimeona hapa kwenye Bodi, naomba Mheshimiwa Waziri akalete amendment, Mwenyekiti iteuliwe na Rais, kwa sababu Bodi zote zinateuliwa na Rais. Kwa kufanya hivyo, tutaendelea kuipa hadhi Bodi hii kwa sababu ukisema wewe uteue Mwenyekiti wa Bodi na wajumbe, nadhani siyo sahihi. Utaratibu wa Bodi zote, Mwenyekiti anateuliwa na Mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalize kwa kusema, ukiangalia pale kwenye registration, sheria inasema, registration
lazima uwe umefanya kazi mwaka mmoja.

T A A R I F A . . .

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni bahati mbaya sana, Mheshimiwa Halima ni Mbunge wa muda mrefu lakini haelewi utaratibu. Ripoti hii ya Kamati ni ya Wajumbe wote. Ripoti hii ya Kamati tuliyoiandika Mheshimiwa Susan ni sehemu yake, lakini Mheshimiwa Susan mwenyewe ameleta amendment. Nami hapa naongea kama Peter siyo kama Mwenyekiti. Unajua watu wanahangaika kupata kick hapa, ndiyo tatizo letu hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, siipokei taarifa yake, kwa sababu najua anakotaka kunipeleka, siwezi kwenda. Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, naomba kuunga mkono hoja.