Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto (61 total)

Mapendekezo ya Mpango wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali katika Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE ZITTO Z. R. KABWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ya kuweza kuchangia mapendekezo yangu kuhusu Mpango wa Maendeleo kwa ajili ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2016/2017. Nina maeneo machache sana ambayo naomba yafanyiwe improvement katika Mpango.
Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la kwanza linahusiana na ujenzi wa uwezo wa watu kwa ajili ya kuwaandaa kwenye uchumi wa viwanda. Katika ukurasa wa 25 wa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa 2016/2017, kifungu cha 3.2.2; miradi mikubwa ya kielelezo, Serikali imezungumzia kusomesha vijana wengi kwa mkupuo katika fani za mafuta na gesi, wahandisi kemikali, viwanda vya kioo na afya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, napendekeza kwamba, hatuwezi tu kuwa na watu ambao wamesomeshwa katika ngazi ya Vyuo Vikuu na hatuna watu ambao wako kwenye ngazi za chini. Kwa hiyo, mapendekezo yangu ni kwamba, tuongeze katika vipaumbele vya miradi mikubwa ya kielelezo (flagship projects) uwepo kwa VETA na Vyuo vya Ufundi vya Kati, kwa maana ya Technical Colleges.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunahitaji mafundi wa kuwasaidia Wahandisi na bila kuwa na VETA za kutosha nchini, hatutakuwa na mafundi wa ngazi za chini na bila kuwa na Technical Schools za kutosha nchini, hatutakuwa na mafundi mchundo wa katikati, ambapo kila Mhandisi mmoja, anahitaji zaidi ya mafundi mchundo 25 ili kuwezesha kazi kufanyika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mapendekezo yangu ni kwamba, kwa sasa hivi, kuna low-hanging fruits. Nawaomba Waheshimiwa Wabunge tukubaliane kwamba kuanzia sasa, kila Kambi ya JKT, iwe ni Chuo cha VETA, iwe designated kuwa chuo cha VETA na wale vijana ambao wanakwenda JKT kwa hiari, wale wa miaka miwili wale, watoke na ujuzi badala ya kuwafundisha tu masuala ya kijeshi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pili, wapate mafunzo ya kuweza kwenda mtaani na kuweza kufanya kazi, itatusaidia kupunguza tatizo la ajira na kadhalika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hili, naomba tupate support Kigoma kule kuanzisha Chuo cha Ufundi wa Kati. Pendekezo langu ni kwamba angalau kila mkoa uwe na Technical School moja, maana yake sasa hivi vyuo ambavyo vipo, kama Dar Tech. imekuwa Dar es Salaam Institute of Technology, Mbeya Technology sasa hivi imekuwa ni Chuo Kikuu, vimegeuzwa kuwa Vyuo Vikuu. Kuna haja ya kurejea kila mkoa kuwa na Technical School moja na kila Wilaya iwe na VETA kwa maana ya Halmashauri ya Wilaya na kwa kuanzia tuanze na Kambi za JKT kuweza kuwa VETA.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pendekezo langu la pili ni suala la reli. Tunahitaji kupata tafsiri ya reli ya kati na baadhi ya Wabunge wamezungumza jana hapa na naomba niongezee nguvu tu, kwamba tunapaswa kuwa makini sana kwenye siasa za kikanda. Tusikubali maslahi ya nchi zingine yafunike maslahi ya nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ni lazima tuanze kwanza kuhakikisha mtandao wa reli ambao utaisaidia nchi yetu ndiyo ambao unakwenda sawasawa. Juzi nilisikia kwamba, tuna tatizo la fedha. Mwaka jana Bunge lilipitisha Sheria ya Railways Development Levy, kodi ya maendeleo ya reli ambayo kila mzigo unaoingia nchini, unatozwa asilimia 1.5 kama niko sahihi; naweza nikarekebishwa, kwa ajili ya reli. Kwa hiyo, ina maana kwamba tunacho chanzo cha uhakika cha fedha, tunachokihitaji ni kuhakikisha kwamba chanzo hiki kinatumika kwa madhumuni yale.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaomba tupate tafsiri ya reli ya kati na kwetu sisi, reli ya kati ni inayotoka Dar es Salaam mpaka Tabora, mpaka Uvinza kwenda Msongati Burundi, kutoka Kaliua kwenda Mpanda mpaka Kalema kwa ajili ya ujenzi wa Bandari ya Kalema na kutoka Isaka kwenda Keza, Ngara kwa ajili ya madini ya nickel ambayo yamegundulika kule Ngara ili yaweze kusafirishwa kupelekwa Bandari ya Dar es Salaam.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba jambo hili liweze kutazamwa, ni muhimu sana na ni priority. Naungana na wote walioongea jana kuhusiana na reli, ya kwamba bila reli na tafsiri hii, hakuna kitakachoendelea katika mfumo mzima wa bajeti ambao unakuja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo napenda kulipendekeza ni ukurasa wa 29, usafiri wa anga. Namba tatu pale ununuzi wa ndege mpya mbili za Shirika la Ndege la Tanzania. Watu wamezungumzia sana hili, lakini kuna haja, Serikali haiwezi kuwa kila wakati inanunua ndege za ATCL, lazima kulifanyia marekebisho Shirika na tunajua na tumewahi kuzungumza huko nyuma, Mheshimiwa Mwakyembe atakuwa anakumbuka maana yake alilianza kidogo hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna watu ambao wanafaidika na kuwepo kwa Shirika la Ndege. Hawa ni Taasisi zinazohusu utalii, lazima tuzihusishe hizi taasisi ziweze kuhakikisha kwamba zinashiriki katika kuwepo na national carrier. Hapa nazungumzia Ngorongoro, TANAPA, hawa kutokana na wingi wa watalii wanaoingia nchini wao wanapata mapato. Turuhusu mashirika haya yawe na hisa ndani ya ATCL ili kuweza kupata fedha shirika liweze kujiendesha kibiashara. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hili jambo siyo kama tunalianza upya, lilishaanza Mheshimiwa Mwakyembe anakumbuka, kuna maelekezo yalitoka, ni kiasi cha Waziri Ndugu Mbarawa kukaa na Msajili wa Hazina, wakubaliane utaratibu ambao unapaswa kuwa ili mashirika yenye ukwasi yaweze kusaidia mashirika ambayo bado yako chini ili tuweze kwenda mbele katika nchi yetu, kwa sababu hatuwezi kuwa tunapanga bajeti ya kununua ndege kila siku. Hizi mbili sawa zitanunuliwa, lakini kuna haja kubwa sana ya kuweza kuangalia huko mbele.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho, maana yake kengele imegonga ambalo ningependa nilichangie ni ukurasa wa 30. Ukurasa wa 30 huduma za fedha namba nne, Serikali inasema inataka kuanzisha Mfuko wa Mzunguko (Revolving Fund). Wakati wa kampeni tulisikia, kulikuwa kuna ahadi ya shilingi milioni 50 kila kijiji, naamini kila kijiji na mtaa na leo asubuhi Profesa Muhongo ametupa takwimu ya idadi ya vijiji nchini, 15,209 ndiyo vilivyoko nchini. Ukichukua 50,000,000 times idadi ya vijiji unapata zaidi ya shilingi bilioni 750 kwa mwaka ndiyo itakayokuwa ya 50,000,000 ya kila kijiji.
Waheshimiwa Wabunge naomba niwakumbushe, tulikuwa na mabilioni ya JK, mnakumbuka namna ambavyo yalitumika vibaya, kwa sababu hapakuwa na mfumo mzuri wa namna gani fedha hizi zitatumika. Naomba nishauri, moja ya kipaumbele ambacho Waziri wa Fedha jana amezungumza hapa ni Hifadhi ya Jamii. Naomba niwashauri kwamba, tutumie fedha hizi kama incentive ya watu kuwekeza kwa ajili ya social security, kwa kufanyaje? Tuweke incentive kwamba, raia wetu mmoja akichangia shilingi 20,000/= kuingia kwenye Mfuko wowote ule wa Hifadhi ya Jamii, Serikali imwekee shilingi 10,000/= zinakuwa ni shilingi 30,000/=.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa idadi ya fedha ambazo zitapatikana, mwanzoni nilikuwa napiga hesabu ya vijiji elfu kumi na mbili, maana yake ni kwamba ndani ya mwaka mmoja, tutakuwa na one point eight trillion ambayo iko kwenye saving ya social security ambayo Serikali mnaweza mkaitumia kwa miradi yoyote mikubwa mnayoitaka. Kwa sababu social security liability yake ni long term, kwa hiyo mnao uwezo wa kujenga madaraja, mnao uwezo wa kujenga irrigation schemes kwa sababu mtu akiingia kwenye mfumo wa social security now anakuja kupata yale mafao ya muda mrefu baada ya miaka 15, baada ya miaka 20. Kwa hiyo, naomba jambo hili liangaliwe na nitaliandika vizuri, tuweze kuona ni namna gani ya kwenda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi ninashukuru kwa kupata fursa ya kutoa mchango wangu kidogo katika makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara muhimu kabisa katika nchi na nchi yoyote ile duniani. Ukitazama kipimo cha maendeleo (Human Development Index) theluthi mbili zinachukuliwa na elimu na afya (afya theluthi moja, elimu theluthi moja).
Kwa hiyo, tukiweza kutatua matatizo haya mawili, afya na elimu, maana yake ni kwamba tunakuwa tumetatua theluthi mbili ya changamoto zetu za maendeleo katika nchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wabunge wenzangu wazungumzia falsafa tuliyokuwa nayo, falsafa ya elimu ya kujitegemea na mimi swali ambalo ninapenda tujiulize sisi kama nchi, falsafa yetu ya elimu sasa ni nini? Tunataka tuzalishe watoto wa namna gani? Tunataka tujenge Taifa la namna gani?
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi tunazungumzia viwanda, lakini tunajua hali yetu ya elimu ilivyo. Watoto ambao tunawazalisha sasa wataendana na Tanzania ya viwanda ambayo tunataka kuijenga? Haya ni maswali ambayo tusipopata majibu yake humu Bungeni kwa miaka mitano tutakuwa tunakuja, tunazungumza, tunapitisha bajeti, tunaondoka hali inabaki ni ile ile. Kwa sababu kelele hizi ambazo zinasikia leo na jana ni kelele ambazo zimepigwa sana huko nyuma. Iliwahi kufikia nchi hii asilimia 20 ya bajeti ilikwenda kwenye elimu, mwaka 2008. Lakini ukiangalia uwekezaji tulioufanya kwenye elimu na ubora ambao tunaupata kwenye elimu haviendani kabisa. Na hapo ndipo ambapo tunapaswa kuangalia ni namna gani ambavyo tunafanya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu ya kujitegemea ilitaka kujenga taifa kujenga Taifa moja. Elimu ya sasa tunataka kujenga nini? Haya ni mambo ambayo ni lazima tujiulize kama nchi na tuyapatie majawabu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tunavyozungumza katika watoto ambao wanamaliza darasa la saba asilimia 50 walipofanyiwa utafiti, 50 percent walikuwa hawawezi kupiga hesabu ya sita jumlisha tatu. 50 percent walishindwa kupiga hesabu ya saba mara nane. Na haya si maneno yangu, ni utafiti ambao umefanywa na vyombo mbalimbali. (Makofi)
Kwa hiyo tuna tatizo kubwa kwamba siku zote tunaangalia inputs. Bajeti, majengo, enrolments, hatuangalii outcomes ni nini. Na kwa hiyo ningemshauri Mheshimiwa Waziri kwamba sasa hivi tuanze kuji-focus, na si Waziri peke yake, sisi viongozi, wazazi na kadhalika tu-focus tuangalie kwenye matokeo ya elimu. Watoto wetu hawasomi, lakini si hivyo tu, walimu pia hawafundishi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Benki ya Dunia na REPOA wametoa taarifa inaitwa Social Delivery Indicators. Inaonesha kwamba ukienda ghafla kwenye shule zetu bila kutoa taarifa, the so called ziara za kushtukiza asilimia 49 ya walimu hawapo shuleni kabisa. Kwa hiyo, tunapozungumza tunataka tuwekeze kufanya walimu wawe motivated, wawe na hamasa wafanye kazi, tuwalipe vizuri lazima pia tuwaambie walimu wawajibike kufundisha watoto wetu. Kwa sababu takwimu zetu ni mbaya sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, iwapo nusu ya walimu hawaingii darasani maana yake ni kwamba hiyo inayoitwa mishahara hewa hii ndiyo mishahara hewa kweli kweli, kwa sababu nusu ya walimu hawafundishi, maana yake mishahara ambayo tunailipa, tunailipa bila watu kufanya kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nashauri, kwanza salary scale ya walimu tuibadilishe. Salary scale ya walimu tuiweke sawa sawa na angalau nusu ya salary scale ya Wabunge. Na tusim-judge mwalimu kwamba huyu anafundisha primary, huyu anafundisha sekondari, huyu anafundisha chuo kikuu, walmu wote salary scales zao zifanane, mishahara yao itofautiane kulingana na muda ambao wamefundisha na kulingana na kiwango cha elimu ambacho wanacho. Kwa maana hiyo ni kwamba tutakuwa tuna walimu wazuri, dedicated, ambao wanaanzia chini kabisa kwenda mpaka ngazi ya juu kabisa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vyuo vikuu vyetu ndiko hali mbaya kabisa. Juzi kuna taarifa imetoka inaonesha kwamba kuna vyuo vikuu bora 30 Afrika, Tanzania hatumo. Hata Makerere na Nairobi ambao tulikuwa tunawazidi sasa hivi wanatuzidi. Lakini hii inatokana na nini? Ni kwa sababu ukiangalia bajeti ya elimu, hivi vitabu vya bajeti ya elimu tukivishika utaona development budget kubwa sana, zaidi ya shilingi bilioni 500, lakini 80 percent of that ni mikopo. It is distorting na ndiyo maana Kamati imependekeza kwamba fedha za mikopo ya wanafunzi zitoke hazina ziende Bodi ya Mikopo moja kwa moja, zisipite kwenye vitabu vya Wizara kwa sababu inaonekana vibaya, bajeti inaonekana ni kubwa wakati haipo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni aibu nchi kama hii 0.001 percent ya bajeti yetu ndiyo inakwenda kwenye research and development, vyuo vikuu vinafanya kazi gani?
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuna commitment ambayo tumeweka, kuna commitment kwenye Five Years Development Plan, kuna commitment za matamko ya viongozi kwamba tutaweka asilimia moja ya Pato la Taifa kwenye research and development, kwa nini hatufanyi? Vyuo vikuu vyetu haviwezi kufanya research and development. Nilikuwa naomba nisisitize hili, na niwaombe Waheshimiwa Wabunge. Takwimu za GDP tunazijua. Waziri wa Fedha anaweza akatuambia GDP ya sasa hivi ni ngapi. Tuangalie bajeti. Leo hii tunatenga 500 billion kwenda kununua ndege, 500 billion, 500 billion kwenda kununua ndege, atakayerusha hizo ndege ni nani? Atakayezitengeneza hizo ndege ni nani? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, one percent ya GDP ni bilioni 59 tu. Tunyofoe kule, tuwaombe watu wa Kamati ya Bajeti wakae tunyofoe kule, tuweke kwa ajili ya reseach and development, watu wetu wafanye kazi ya utafiti tuweze kuzalisha na tuweze kuitengeneza nchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumalizia kwenye ufundi. Na Wabunge wengi wamezungumza hili. Kwa hiyo ni consensus, lakini nimeangalia bajeti hapa, tunazungumza kuhusu VETA kila Wilaya, tunazungumza kuhusu vyuo vya ufundi katika Mikoa, bajeti ha-reflect. Bajeti yetu hai-reflect hizi VETA tunazozitaka. Lakini tuna zaidi ya 50 percent ya watoto ambao wanamaliza kidato cha nne hawaendelei na elimu ya juu zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nilikuwa naomba tuwekeze kwenye VETA, tuwekeze kwenye vyuo vya ufundi mchundo na mimi hapa ninakuja kuomba ombi langu rasmi Mheshimiwa Waziri, naomba Chuo cha Ufundi Kigoma.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kigoma ni lango la Magharibi la nchi hii, Kigoma ndiyo center ya nchi zote za Maziwa Makuu. Ukitaka kufundisha watu utengenezaji wa boti Kigoma fits, ukitaka kufundisha watu maritine Kigoma fits, ukitaka kufundisha watu namna ya kuvua kisasa Kigoma fits.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa naomba Mheshimiwa Waziri katika mipango ambayo tunakwenda kuifanya kwa ajili ya kufungua vyuo vya ufundi yva kutosha tupate chuo cha ufundi pale ili tuweze kusaidia, kama jinsi ambavyo wengine wameweza kuomba.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa naomba kusisitiza kwamba tuwekeze kwenye matokeo, tuangalie namna gani ya kuboresha watoto wetu waweze kusoma. Watoto wetu hawasomi.
Naomba tuji-focus huko, tuondokane na inputs, tumeshawekeza sana kwenye inputs, tumeshawekeza sana huko, naomba sasa hivi tujikite sasa hivi kwenye outcomes na ili tuwe na outcomes nzuri ni lazima tuwe na mwalimu ambaye yuko motivated, na ni lazima tuwe na mwalimu ambaye yuko accountable, nashukuru sana.
Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa fursa ya kuchangia hotuba hii ya Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kwanza ninukuu sehemu ya hotuba ya Waziri ukurasa wa tano kuhusiana na dira, vilevile iki-reflect Mpango wa Maendeleo ya Taifa Ibara ya 14 kwamba tunataka kujenga Taifa lenye umahiri mkubwa katika michezo ifikapo mwaka 2025, lakini ukiangalia bajeti hii huoni tafsiri ya dira hii na fedha. Huoni fedha zikienda kwenye hili.
Mheshimiwa Naibu Spika, mfano dhahiri sasa hivi na nimeshangaa sana kwa kweli Mheshimiwa Waziri Nape amezungumza hapa kuhusu watu kama akina Samatta walivyoiletea sifa nchi na siyo hivyo tu, michezo ni mingi na ni lazima tu-support michezo yote, lakini mchezo ambao Watanzania wanaupenda zaidi kuliko michezo yote ni soka. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hotuba hii kuanzia neno la kwanza mpaka neno la mwisho, halina neno Taifa Stars. Waziri ana picha kwenye kurasa nne za hotuba yake. Hakuna hata picha moja inayohusu soka. Mwezi ujao Taifa Stars inacheza na Egypt hapa Tanzania ambapo kwenye kundi letu ndiyo tumebakia na mechi mbili na zote ni timu hizo against sisi. Egypt against sisi, Nigeria against sisi. Tukishinda mechi ya nyumbani mwezi ujao, tarehe tano au tarehe sita, mechi ya ugenini ya Lagos ni mechi ya kumaliza ratiba. Hotuba hii ya Waziri haina hata kuwa-wish mafanikio Taifa Stars. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tunakuwaje Taifa mahiri la michezo? Mheshimiwa Nape? Hata timu yako ya Yanga imeshinda juzi dhidi ya Angola umeshindwa kuwa-support humu, ambapo wakienda Angola kucheza wakifanikiwa wataingia round ya pili na Jerry Muro ameshaanza kututisha watapata hela, sijui na nini hata iwe nini, hata mshinde namna gani timu ya Kimataifa ni Simba tu!
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kupata maelezo ya Waziri kuhusu jambo hili la mchezo wa soka na namna gani ambavyo Serikali inajipanga kutengeneza Kina Samatta wengi.
Mheshimiwa Naibu Spika, tusisubiri watu wafanikiwe wao wenyewe tuje kuwapa sifa hapa lazima tuwatengeneze. Program ya kutengeneza sports academies nchi nzima iko wapi? Naiona kwenye Hotuba ya Kambi ya Upinzani. Viwanja vya michezo CCM imevikumbatia, viwanja vinaharibika, viwanja ambavyo vilijengwa na Watanzania wote kwa michango yao, Mheshimiwa Nape unashindwaje kuanzisha wakala wa viwanja vya michezo, viwanja vile viingie Serikalini, wala hayatakuwa maamuzi ya ajabu.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mwenyekiti wenu wa CCM alitoa Chimwaga kuwa Chuo Kikuu cha Dodoma mnashindwaje kuvifanya viwanja tukaanzisha wakala wa viwanja vya michezo ili watu wacheze! tutengeneze tuweze kwenda na sisi tuingie World Cup. Kweli Mheshimiwa Nape huoni aibu hotuba nzima haina neno Taifa Stars?(Kicheko)
Mheshimiwa Naibu Spika, bahati mbaya Waziri wa Fedha na Naibu wake hawapo hapa labda watapewa taarifa. Nchi zote duniani, fedha za bahati nasibu ndiyo huwa zinatumika kuendesha michezo. Leo hii Ujerumani waliweza kuwafunga Brazil bao saba, ile timu imetengenezwa kwa miaka 10 kwa fedha za bahati nasibu. Uingereza ni fedha za bahati nasibu, Australia ni fedha za bahati nasibu. Tunashindwa nini kuhakikisha kwamba Bahati Nasibu ya Taifa inasimamiwa chini ya Wizara hii ili Serikali isihangaike kutoa fedha za bajeti kupeleka kwenye michezo, fedha za bahati nasibu zitumike kuendesha michezo. Tunachoshindwa ni kipi?
Mheshimiwa Naibu Spika, jamani michezo ndiyo inayounganisha watu, tukienda pale Uwanja wa Taifa, Taifa Stars inapocheza, Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu wakifunga hamna CCM, hamna CHADEMA, hamna UKAWA, hamna ACT Wazalendo wote ni Tanzania, wote tuna bendera ya Tanzania. Kama unataka kuliunganisha Taifa ni michezo! Hebu tufanyeni maamuzi, tuhakikishe tunafanya maamuzi kuanzia Julai mwaka huu bahati nasibu itumike kuendesha michezo. Hatutahangaika hapa kumbana Mheshimiwa Nape na vibilioni mbili vyake anavyoviomba ambapo wala hatavipata! Tutapata fedha za kuendesha michezo. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Naibu Spika, wenzangu hapa wamezungumza suala la TBC. Mimi nashangaa sana, siku Waziri Nape ametoa kauli ya Serikali hapa kuhusu TBC tulibishana, Wabunge tukasimama, tukapinga, waliounga mkono wakasimama wakaunga mkono lakini Kiti chako kimetuita Wabunge wote tuliopinga kauli ya Nape kwenye Kamati ya Maadili. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jana mimi nimepata barua kwamba mnatubana kusema, mnazuia Bunge lisionekane, hata kutoa maoni ndani ya Bunge tunaenda kuhojiwa? Mnaturudisha nyuma namna hii? TBC ni public broadcaster, TBC siyo government broadcaster ni public broadcaster.
Inaendeshwa kwa fedha za walipa kodi na kama tatizo ni bajeti Mheshimiwa Nape, TBC kwa nini hamjifunzi BBC? TBC inayo uwezo wa kuendeshwa kwa leseni maalum, kwa kodi maalum, kwa levy maalum, muhimu tu isishindane na vyombo binafsi kwenye biashara ndiyo BBC wanavyofanya.
Mheshimiwa Naibu Spika, tuliwaambia wakati nilipokuwa Mwenyekiti wa PAC, tuli-commission report maalum ya financing public broadcaster na nilikwambia Mheshimiwa Nape kwamba TBC ni shareholder kwa Startimes. Nimeangalia report yako hapa kwenye randama ya Wizara yako hamna hata senti tano ambayo TBC inapata kutoka Startimes. Umefanya nini kuhusu mkataba kati ya TBC na Startimes? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, vinga‟amuzi peke yake vikiwekewa fedha kidogo hata shilingi 500 tu vinaendesha TBC na tutakuwa na hata TBC Bunge tutaangalia bila shida yoyote. Kwa nini hamuwi-innovative Mheshimiwa Nape? Wewe ni kijana unatutia aibu vijana wenzako. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Nape wewe ukifanikiwa kwenye majukumu yako ndiyo na sisi wengine tutatembea kifua mbele tutataka majukumu zaidi kwa sababu tutaonyesha vijana wanafanya vizuri, brother be innovative! Tufanye kazi, tuifanye TBC iwe kama BBC iwe public broadcaster, wala hatutagombana tena, wala hatutakuwa na masuala ya bajeti hapa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, leo hii ukifungua redio zetu, ukifunga tv zetu zote binafsi na za public ni nyimbo za nje. Lakini ninyi mnasafiri, mkienda nchi za watu kuna limit. Leo ukienda Lagos husikii nyimbo za Diamond kama yuko Diamond peke yake. Lazima awe Diamond na Davido wamepiga pamoja ndiyo utazisikia, wana-promote wasanii wao. Sisi hapa sijui ni ulimbukeni wa ukoloni haujatutoka baada ya miaka 50!
Mheshimiwa Nape hili liko kwako, unataka kuwatetea wasanii, unataka kuwalinda wasanii hili wala huhitaji kubadilisha sheria. Content, kanuni za content ziko chini ya Waziri. Toa kanuni TCRA wazibariki asilimia 80 ya nyimbo zinazopigwa kwenye redio zetu na tv zetu ziwe za wasanii wetu. Anayetaka nyimbo za nje kutakuwa kuna channel za malipo aende kwenye channel za malipo alipie, apate hizo nyimbo za nje.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia katika Wizara hii muhimu sana katika uendeshaji wa uchumi wetu kwa sekta zote ambazo ziko chini ya Wizara hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza ambalo napenda niweze kupata mikakati ya Serikali,ni suala la mahusiano kati ya madini tunayozalisha, thamani tunayopata ya uzalishaji ya hayo madini na mapato ya Serikali kutoka kwenye makampuni husika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa naangaliwa hotuba ya Mheshimiwa Waziri, ukitazama ukurasa wa 86 na 87 ametoa takwimu za sekta ya madini. Utaona mwaka 2015 dhahabu peke yake ilituingizia dola za Kimarekani bilioni 1.6 takiribani trilioni 3.5 kwa maana ya thamani ya mauzo ya dhahabu nje. Lakini ukienda kuangalia mrabaha na mapato ya kodi kwa maana ya kodi zote ambazo zinakusanywa; kwa maana ya corporate tax, value added tax, pay as you earn, skills development levy na withholding tax, utakuta kwenye kodi tumekusanya shilingi bilioni 351 na kwenye mrabaha tumekusanya dola za Kimarekani 63.2.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukichukua mapato haya, yaani revenue hii ya Serikali na fedha za kigeni ambazo makampuni ya madini yanapata kuuza dhahabu tu peke yake ni asilimia 15 tu ya dhahabu inayouzwa nje. Kwa hiyo, hii ni changamoto kubwa, najua tumetoka mbali tulikuwa tunapata chini ya hapo, tunahitaji kuongeza nguvu zaidi ili tuweze kufikia hatua kubwa zaidi ya mapato ambayo tunayapata.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo kubwa ambalo tunalo sasa hivi, ni tatizo la makampuni makubwa ya madini kutumia njia za kihasibu kuhamisha faida kutoka nchini kwetu kupeleka kule ambako wamesajiliwa, inaitwa base erosion and profit shifting. Hili ni jambo ambalo ni lazima tulishughulikie vizuri, na tukiweza kulishughulikia hatutakuwa na haya matatizo ambayo tunayo sasa hivi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo ningependa kuweza kupata maelezo ya Serikali, leo hapa tunapozungumza ndani ya siku tano zijazo, hakuna ndege ambayo inaweza ikatua nchini kwetu kwa sababu hatuna mafuta ya ndege (Jet A one) na hii inatokana na zabuni ambayo ilitolewa kutoka kwa kampuni moja ya kigeni, kampuni ile ikaleta mafuta, mafuta yale yote yameonekana yako contaminated hayawezi kuingia kwenye soko.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mpaka sasa Serikali haijachukua hatua yoyote ile, mafuta ambayo yalikuwa yaende Puma Energy peke yake,yana thamani ya dola za Kimarekani milioni 13 mpaka hapa tunapozungumza, hifadhi yetu ya mafuta ya ndege imebakia ya siku tano tu, baada ya siku tano kama hakuna hatua ambayo Serikali imechukua, nchi yetu hakuna ndege ambayo itakayotua kwa sababu hawawezi kutumia mafuta ambayo yako nchini hivi sasa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nilikuwa naomba nipate maelezo ya Serikali,ni hatua gani ambayo wanachukua haraka kuweza kuhakikisha kwanza tunashughulikia jambo hili, tuweze kupata mafuta ya ndege ili ndege ziweze kutua. Tusipate aibu duniani, tusikose watalii ambao wanakuja nchini, lakini pili nihatua gani ambazo zitachukuliwa dhidi ya watu ambao walitoa zabuni kwenye mafuta ambayo yameonekana hayafai kutumika katika nchi yetu? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo mimi nilikuwa naomba nipate maelezo hayo ya Serikali, na nina barua za Bulk Procurement Petroleum Agency, ambazo zinahusiana na jambo hili, kama Waziri akizihitaji kwa ajili ya ufuatiliaji naweza nikampatia ili aweze kulifuatilia jambo hili, na kuweza kuleta suluhisho.
Jambo la tatu ni suala la uzalishaji wa umeme. Nimeona miradi ambayo imeorodheshwa, ni miradi mingi na miradi ambayo inapaswa kuungwa mkono. Kwa sababu juhudi zozote zile za kwenda kwenye viwanda, kama haziendani na uzalishaji wa umeme wa kutosha zinakuwa hazina maana yoyote. Ndio maana leo hii sisi kule Kigoma tunahangaika kutafuta wawekezaji, Waziri wa Viwanda anahangaika kutafuta wawekezaji, lakini swali la kwanza ambalo mwekezaji atauliza kuna umeme? Hakuna umeme.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ndio maana tunapigana sana kuhakikisha kwamba mradi wa Maragalasi unafanikiwa na ninapenda niwapongeze kwa kuhakikisha kwamba mradi wa Maragalasi umeingia kwenye mpango na hili ni kilio cha watu wa Kigoma cha muda mrefu na napenda niwashukuru sana kwa niaba ya wananchi wa Kigoma na kwa niaba ya wabunge wengine wa Kigoma kuhakikisha kwamba mradi huu unakuja jinsi ambavyo unavyotakiwa. Hata hivyo umeme sekta ya uzalishaji (generation part) ya umeme is liberalized,ni eneo ambalo Sheria ya Umeme ya mwaka 2008 imeruhusu private sector kushiriki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kama tukitumia vizuri hiyo mix ya public na private, tutaweza kuhakikisha ya kwamba tunazalisha umeme wa kutosha. Kwa hiyo, nilikuwa namsihi Mheshimiwa Waziri kwamba mikataba ambayo tayari tumesaini, inaweza kuwa inahitaji review ni sawa, kwa sababu ni lazima tufanye review kuangalia maslahi ya nchi namna gani ambavo inakuwa. Lakini tusifanye makosa tuliyoyafanya nyuma kujikuta tunapelekwa mahakamani tunalipa gharama kubwa, nyote hapa mnafahamu kwamba ilibidi tuwalipe DOWANS kisiri siri zaidi ya bilioni 200, kwa sababu ya kesi ambayo tulipeleka mahakamani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tusiingie kwenye mtego wa kupelekwa mahakamani tena, Rais alitoa tamko pale siku anaweka jiwe na msingi la Kinyerezi kuhusiana na kuzalisha wenyewe, ni tamko sahihi kabisa, ni tamko la kizalendo kabisa, lakini halina maana ya kwamba tuingie kwenye migogoro na watu ambao tayari tuna mikataba nao, halafu tuanze tena ku-negotiate mahakamani, itakuwa ni distraction mtapoteza muda na Mheshimiwa Waziri itakuondolea muda wa ku-concentrate kuhakikisha ya kwamba tunapata umeme wa kutosha, vijijini na miradi ambayo tunayo hivi sasa. Kwa hiyo, nilikuwa nashauri kwamba Serikali ijaribu kuangalia jambo hili na kuweza kuhakikisha kwamba tunakwenda vizuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho ni suala la TMAA na Dkt. Kafumu amelizungumza. Mimi nadhani tunaweza tukaangalia vizuri, ni namna gani ambavyo tunae-reform TMAA ipanuke zaidi, isiwe ni suala la kuangalia migodi peke yake, iangalie pia suala zima la mikataba yetu ya gesi, kwa sababu hatuna chombo ambacho chenyewe kiko dedicated kwa ajili ya kuangalia cost accounting na makampuni haya yanaingiza gharama nyingi sana kwetu, ili kuweza kupata sehemu kubwa ya mapato baada ya revenue sharing.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba tuangalie namna gani ambavyo TMAA haitaangalia migodi peke yake, tuipanue iende ikiangalia mpaka kwenye mikataba yetu ya gesi badala ya kuivunja kama jinsi ambavyo Mheshimiwa Dkt. Kafumu anapendekeza. Muhimu ni kufanya reform ili kuweza kuifanya kazi yake iwe more relevant kuliko kwenda kuiondoa kwa sababu tunajua kazi kubwa ambayo wameifanya, ukaguzi mkubwa ambao wamefanya na mapato makubwa ya Serikali ambayo yameokolewa kulingana na jambo hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho kabisa ni suala la mafuta na gesi Zanzibar. Mpaka sasa tunapozungumza bado Katiba inatambua kwamba suala la mafuta na gesi ni suala Muungano. Mpaka sasa tunapozungumza bado TPDC ambayo siyo taasisi ya Muungano inashughulika na mafuta na gesi Zanzibar, kuna haja kubwa, kwa sababu consensus tayari ipo, ni vizuri hata kama bado hatujafikia nafasi ya kwenda kwenye referendum ya Katiba au kuanza upya mchakato wa Katiba angalau tufanye amendment ya kisheria sasa hivi ili suala la mafuta na gesi liweze kutendeka Zanzibar bila kukiuka Katiba, bila kukiuka sheria. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, najua kuna consensus,lakini leo hii kampuni yoyote itakayoingia makubaliano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ina madhara ya kupelekwa mahakamani kwa sababu Katiba bado inatambua jambo hili la Muungano na nadhani kwamba halina ubishi. Hakuna mtu ndani ya Bunge hili ambaye atapinga jambo la kuhakikisha kwamba Zanzibar inaweza ika-manage mafuta na gesi yenyewe.
Kwa hiyo, naomba na napendekeza kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali tufanye amendment hiyo ili tuweze kuondoa tatizo hili la kisheria tuweze kuruhusu ndugu zetu wa Zanzibar waweze ku-manage resource hii kwa ajili ya faida yao na kwa ajili ya kuendeleza blocks ambazo tayari ziko Zanzibar na tayari zimeshaingizwa kwenye soko tuweze kuhakikisha kwamba na wenyewe hawarudi nyuma katika jambo hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo hayo nakushukuru sana.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kupata nafasi ya kuchangia, ingawa umeniwahi sana, lakini nitajitahidi tu kuweza kuchangia yale ambayo naweza nikachangia kutokana na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa ya Mwaka 2017/2018.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza ambalo naomba nilizungumzie ni suala zima ambalo ndiyo imekuwa kama nguvu kubwa ya Serikali ya Awamu ya Tano katika mwaka huu mmoja na ndani ya bajeti hii ya kubana matumizi. Ni hatua nzuri kubana matumizi kwa sababu inasaidia kupata rasilimali fedha za kutosha kuzielekeza kwenye miradi ya maendeleo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jana hapa Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi ametupa takwimu za watumishi hewa ambao wameondolewa kwenye payroll ya Serikali na hivyo kupelekea Serikali kuokoa shilingi bilioni 19 kila mwezi kutokana na suala zima la watumishi hewa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nipate ufafanuzi kutoka kwa Waziri wa Fedha. Taarifa ya gharama za watumishi tunazipata kupitia taarifa ambayo kila mwezi Benki Kuu inaitangaza; inaiweka kwenye tovuti yake na kuigawa pia (Monthly Economic Review).
Mheshimiwa Mwenyekiti, Monthly Economic Review ya mwezi Agosti mwaka 2015 inaonesha kwamba wages and salaries ambazo Serikali ililipa mwezi Juni, 2015 zilikuwa ni shilingi bilioni 456. Monthly economic review ya mwezi Agosti mwaka 2016 inaonesha kwamba wages and salaries ambazo Serikali imelipa kwa mwezi Juni mwaka 2016 ni shilingi bilioni 534; kwamba kuna nyongeza ya gharama za mishahara ya kila mwezi ya shilingi bilioni 78. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri wa Utumishi jana ametuambia wanaokoa shilingi bilioni 19 kila mwezi kwa kuondoa watumishi hewa. Taarifa ya Benki Kuu inaonesha kwamba toka Serikali hii imeingia madarakani gharama za watumishi kwa mwezi zimeongezeka kwa shilingi bilioni 78 Mheshimiwa Mwenyekiti, watumishi hewa wameondolewa, ajira mpya hakuna, nyongeza ya mishahara imesimamishwa, lakini gharama za wages and salaries zimeongezeka kwa bilioni 78. Haieleweki! Kuna mmojawapo kati ya hawa wawili anadanganya umma. Ama zoezi la watumishi hewa ni publicity stunt au Serikali inatumia fedha kwa matumizi mengine halafu BOT inasema ni mishahara. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba nipate maelezo ya Waziri wa Fedha kuhusiana na jambo hilo, kwa sababu ni jambo ambalo umma ni lazima uelezwe na liweze kueleweka tunapopanga mpango kuelekea katika mwaka ujao wa fedha ambao unakuja. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ni Higher Education. Jana nimepitia Mpango wa mwaka jana 2015. Mwaka jana tulichelewa kidogo tukaupitisha mwezi Januari. Serikali inazungumzia kuongeza idadi ya vijana, wanafunzi wanaopata mikopo kwenye elimu ya juu. Mpango pia wa mwaka huu unazungumzia hilo hilo na imeongeza; inasema, kuimarisha Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ili kuongeza uwezo wa kutoa mikopo kwa wanafunzi wengi zaidi wanaokidhi vigezo, kuendelea kupanua matumizi ya TEHAMA na ukarabati, upanuzi na ujenzi wa Vyuo Vikuu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa tunapozungumza, idadi ya wanafunzi ambao wana uwezo wa kuingia kwenye Vyuo Vikuu hapa nchini na wanao-qualify kwa mikopo ni takriban 65,000. Watoto waliopata mikopo ni 20,000 tu. Nini ambacho kinaandikwa na nini ambacho kinatendwa? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia hapa napata tatizo kidogo la coordination ndani ya Serikali. Waziri wa Elimu alikuja kwenye Kamati. Kamati ya Huduma ya Maendeleo ya Jamii ili-dedicate siku nzima na kujadili tatizo la mikopo. Wizara kwa maana ya Serikali kwa kupitia Wizara ya Elimu na Kamati tukakubaliana, kuna mambo yanayopaswa kwenda kuangaliwa upya kuhusu suala zima la financing higher education ili tuweze kutatua tatizo hili la mikopo la muda mrefu. Hata hivyo, ukisoma Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo hukuti jambo hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa maelekezo ya Kamati kwa Waziri ni kwamba by mwezi Februari tutakuwa tuna utaratibu mpya. Wakati huo huo, wiki ijayo tuna mabadiliko ya sheria tunakuja kuyafanya ya mikopo ya elimu ya juu. Katika Miscellaneous Amendment kuna vipengele ambavyo tunaenda kuvibadilisha kwenye mikopo ambavyo vinabana upanuzi wa kupata mikopo zaidi. Sasa nashindwa kuelewa, kuna mazungumzo ndani ya Serikali kabla ya Serikali kuja ndani ya Bunge kuwasilisha Mpango kama huu? Baraza la Mawaziri linakaa ili kuhakikisha kwamba kila Waziri anaeleza new development ambayo imetokea kwenye sekta yake ili jambo linalokuja Bungeni liwe ni lile ambalo limekubalika ndani ya Serikali? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya jambo tulilozungumza ni kwamba, ukisoma Mapendekezo ya Mpango kuna kipaumbele kimewekwa kwenye masomo maalum; gesi, gesi asilia, sijui nishati, uhandisi na kadhalika. Kwenye vigezo vya mikopo vya mwaka huu vimetolewa ni kwa wanaosomea Udaktari, Uhandisi, Gesi Asilia na kadhalika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ni nchi gani duniani ambayo haina scholarship programs kwa watoto wake? Kama ninyi mnataka kujenga nchi ya viwanda, mnahitaji Wahandisi kadhaa; mnahitaji wahandisi wa mitambo kadhaa; mnahitaji wataalam wa mafuta na gesi kadhaa; si ni wajibu wa Serikali kutoa scholarship kwa watu hao ili mweze kuwapata hao wataalam? Halafu ili eneo la mikopo, bajeti ambayo mmeitenga kwa ajili ya mikopo ibakie kwa ajili ya watu wengine wote waweze kupata mikopo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda niwaulize Waheshimiwa Wabunge wenzangu, mnaweza mkasomesha Wahandisi wengi sana; mnaweza mkasomesha Madaktari wengi sana; hivi niambieni, kuna kiwanda hakina Afisa Utumishi? Kuna kiwanda hakina Mhasibu? Kuna kiwanda hakina Wachumi? Mnawezaje mkasema kwamba mwaka huu tutasomesha hizi hard sciences tu? The best way to do that, mnatoa scholarship kwa hizo priorities, hao wengine wanaendelea kupata mikopo kama kawaida. Hayo ndiyo mambo tuliyokubaliana kama Kamati na Wizara ya Elimu. Siyaoni kwenye Mpango; sasa hili ni tatizo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, jana Mheshimiwa Bashe amezungumzia Kurasini na Kariakoo. Tunafahamu kabisa kwamba suala la Kurasini limeongelewa muda mrefu; lakini wakati tunaongea suala la Kurasini hatukuwa na nguvu hii tunayoongea kuhusu viwanda. Niliwahi kusoma makala moja aliandika Mheshimiwa Dkt. Mpango wakati yuko Tume ya Mipango, ilichapishwa na jarida la REPOA kuhusiana na suala la staying the course, kwamba mmepanga kitu hakikisheni mnakifanya na sequencing. Alitoa mambo kama manane na moja nitalizungumza mwisho kabisa ambalo ni la kumsuta kidogo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kurasini inaenda kuwa ni ya biashara. Kama mnataka kujenga viwanda, kwa nini mnaruhusu uchuuzi huo kama lengo ni la viwanda? Kama kuna transition ambayo nakubali, lazima kuwe na transition; kwa nini tusiitumie Kariakoo kama hiyo transition? Kwa nini tuwaue Waswahili, wafanyabiashara ambao wameanza kukua na kukuza mitaji yao kwenda kuimarisha viwanda vya China na wafanyabishara wa China kuleta bidhaa zao Kariakoo?
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini tusiifanye Kariakoo kuwa ni free trade area; chochote kinachoingia Kariakoo kisitozwe kodi na kinachotoka kitozwe kodi? Kwa sababu Kariakoo Wazimbabwe, Zambia, Malawi, Congo wananunua pale, kila sehemu wananunua pale. Hili jambo naomba liangaliwe upya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, bahati nzuri sasa hivi, kwa mujibu wa Taarifa ya Kamati ya Bajeti, mwekezaji yule wa Kurasini ameshaondoka, hayupo tena. Kwa maana hiyo basi, tutumie hii opportunity tuweze kuona namna ya ku-link; na kuna matatizo makubwa pale Kariakoo. Maana yake sasa hivi TBS wameongeza viwango vya tozo na faini na kadhalika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wafanyabiashara wadogo wa Kariakoo wanahangaika sana, lakini tunapoenda kwenye transition ya kuelekea viwanda, hawa ndio watu ambao wanapata entrepreneurial skills through biashara zao baadaye waweze kuja kuwa na viwanda. Lazima tuone namna gani ambavyo tutawasaidia. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho kabisa, katika lile jarida moja ya jambo ambalo Mheshimiwa Waziri Dkt. Mpango wakati ule akiwa Katibu Mkuu wa Mipango, alisema lazima uongozi ujenge chini ya ushindi, kama atakuwa anakumbuka mwenyewe; a winning coalition ambapo kila mtu anaongea jambo moja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wewe ni shahidi. Serikali na Bunge hatupo pamoja katika utekelezaji wa mikakati ya nchi. Ama sisi Wabunge hatuielewi Serikali au Serikali haiwaelewi Wabunge; ni either of the two. Pia Serikali yenyewe miongoni mwa Mawaziri wenyewe, bado hawaelewani. Ndiyo maana kumekuwa na matamko ya kila mtu kwa kila kinachotokea utafikiri Serikali inakimbizana kupata front pages za magazeti. Nadhani kuna haja ya kuwa na cooling of period, tuweze kukaa soberly kabisa, Waheshimiwa Wabunge na Serikali tujiulize, wapi tunaenda sawa na wapi hatuendi sawa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge wanalalamika na wananchi wanalalamika kwamba hali ni mbaya. Mimi naelewa na any development economist anaelewa kwamba mnapopiga hatua fulani ya maendeleo lazima kuwe na maumivu. Ndiyo maana kuna dawa za maumivu; lazima kuwe na palliative measures, yale maumivu mpaka mfikie ile hatua ambayo mnayotaka kufika, hatuendi hivi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba through Mpango tupate nafasi tukae kama viongozi, tuweze kuona nchi inakwenda vipi. Pale ambapo kuna matatizo tukubaliane, matatizo haya ni ya lazima lakini tutayaepuka namna hii. Sivyo hivi ambavyo tunakwenda; tutanyoosheana vidole, tutarushiana madongo na hatutakwenda. Hali ya wananchi sasa hivi malalamiko ni makubwa sana. Ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais (TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora) kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, tangu tuanze mkutano huu wa bajeti mwaka 2016 kumekuwa na malalamiko kutoka kwa Wabunge na hasa Wabunge wa Kambi ya Upinzani Bungeni kuhusu ukiukwaji wa sheria mbalimbali za nchi katika masuala ya bajeti. Jana jioni Mwenyekiti wa Bunge Mheshimiwa Andrew Chenge alitoa changamoto kuwa Wabunge tuseme ni sheria gani zimekiukwa katika mchakato mzima wa bajeti ya nchi hii sasa. Kwa maoni yangu, kuna ukiukwaji kadhaa wa Sheria ya Bajeti, Sheria namba 11 ya mwaka 2015, katika mchakato wa bajeti ya mwaka huu. Nitaeleza kwa ufupi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kifungu cha (8) cha Sheria ya Bajeti kinaeleza namna ambavyo mfumo wa bajeti ya Serikali unapaswa kuwa. Kifungu cha 8(1)(b) na 9(1)(a) na 19(1) vinaeleza namna mchakato wa bajeti unavyopaswa kuwa. Vifungu hivi vinataka planning and budget guidelines zipitishwe na Bunge katika Mkutano wake wa mwezi Februari kila mwaka. Sheria inataka budget ceilings ziidhinishwe na Kamati ya Bajeti na baadaye linapokaa kama Kamati ya Mipango.
Mheshimiwa Naibu Spika, Bunge lilikaa kama Kamati ya Mipango na kupitisha Mpango wa Bajeti uliokuwa na Bajeti ya shilingi trilioni 23.7 kama ulivyowasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango hata hivyo bajeti inayojadiliwa sasa ni shilingi trilioni 29.5, tofauti kabisa na siyo tu viwango vilivyopitishwa na Bunge mwezi Februari bali pia hata vipaumbele vyake ni tofauti. Hili ni suala la utawala bora (governance issue) kwani taratibu za utungaji wa bajeti zimeainishwa na sheria na kama sheria hazifuatwi ni vigumu sana hata bajeti yenyewe kutekelezwa. Ili kurekebisha hali hii ni lazima Bunge likae tena kama Kamati ya Mipango na kupitisha upya viwango vya juu vya bajeti kabla ya mjadala wa bajeti kuendelea au angalau kabla ya kupitisha bajeti kuu mwezi wa Juni, 2016.
Mheshimiwa Naibu Spika, Ofisi ya Rais, Ikulu, inapaswa kuzingatia sana sheria na taratibu tulizojiwekea kwani madhara ya kutofuata sheria ni makubwa mno. Kwa mfano, hivi sasa bajeti za taasisi hazimo kwenye vitabu vya bajeti ya Serikali kinyume na Sheria ya Bajeti ambapo hivi sasa bajeti za taasisi zote za umma zinakuwa ni sehemu ya bajeti ya Serikali na Wabunge wanapaswa kuwa na nyaraka za bajeti hizo. Ofisi ya TRA kwa mujibu wa kifungu cha 17(a) cha Sheria ya Bajeti ilipaswa kuunganisha bajeti ya mashirika yote ya umma na kutoa kitabu chake kwa Wabunge.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inapaswa kutoa maelezo ya kina kwa Wabunge kuhusu masuala haya ili kuzuia ukiukwaji wa Sheria tulizojitungia wenyewe.
Mheshimiwa Naibu Spika, TAKUKURU na kesi za ufisadi mkubwa nchini; ufisadi wa hatifungati ya shilingi trilioni 1.2, Standard Bank ya Uingereza; tarehe 8 Machi, 2013, Serikali ya Tanzania ilikopa fedha $ 600 milioni (1.2 trilioni) kutoka nje kwa msaada wa Benki ya Standard ya Uingereza ambayo sasa inaitwa Standard Bank ICIC Plc. Mkopo huo wenye riba yenye kuweza kupanda (floating rate) umeanza kulipwa mwezi Machi mwaka huu (kama Serikali imeanza kutekeleza mkataba).
Mkopo huu utalipwa mpaka mwaka 2020 kwa mikupuo tisa inayolingana. Ifikapo mwaka 2020, Tanzania italipa deni pamoja na riba jumla ya $897 milioni (takribani shilingi trilioni mbili). Mkopo huu umegubikwa na ufisadi na kwa kuwa baadhi ya Watanzania wamefikishwa Mahakamani kuhusiana na sehemu ya mkopo huu, sitapenda kueleza upande wa waliopo Mahakamani. Kesi iliyopo mahakamani inahusu $6 milioni ambazo inasemekana (kwa mujibu wa nyaraka za Mahakama) kuwa zilitumika kuhonga Maafisa wa Serikali ili Benki hiyo ya Uingereza iweze kupata biashara iliyopata.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la kushangaza ni kwamba wanaosemekana kula rushwa hiyo, hawapo Mahakamani mpaka sasa. Vile vile waliotoa rushwa hiyo hawapo Mahakamani mpaka sasa. Waliopo Mahakamani ni wanaosemekana kutumika kupeleka rushwa. Mjumbe kushtakiwa lakini aliyemtuma hajashtakiwa na aliyepelekewa kilichotumwa hajashtakiwa. Hapa kuna tatizo la msingi ambalo tukilitatua Serikali yetu itaepuka masuala kama haya siku za usoni.
Mheshimiwa Naibu Spika, hapa mbele yangu nina barua ambayo kundi la Watanzania zaidi ya 2,000 kutoka kona zote za dunia wamesaini kutaka Benki ya Standard ya Uingereza ichunguzwe kwenye suala hili la hatifungani. TAKUKURU walitumia taarifa ya taasisi ya Uingereza ya SFO katika kuchukua hatua zinazostahili dhidi ya Watanzania wanaotajwa katika sakata hili.
Mheshimiwa Naibu Spika, SFO haikufanya uchunguzi dhidi ya Benki ya Uingereza ya Standard Bank. Hatujui ni kwa maslahi mapana ya Uingereza au ni kwa kupitiwa. Sisi Tanzania tumejikuta tunafuata matakwa ya Uingereza katika jambo hili, kiasi cha hata kutumia ushauri wa kitaalam wa Waingereza katika jambo hili. Leo hii TAKUKURU inasaidiwa katika kesi hii na wataalam kutoka Uingereza katika kesi inayohusu Benki ya Uingereza!
Mheshimiwa Naibu Spika, Watanzania walioandika petition kutaka Benki ya Standard kuchunguzwa wanataka ukweli wote kujulikana. Standard Bank walihusika kwa kiwango gani katika kutoa rushwa ili kupata biashara? TAKUKURU wanapaswa kufanyia kazi jambo hili kwa kuwafungulia mashtaka Standard Bank, mashtaka ya kutoa rushwa ili kupata biashara nchini. Hata hivyo, TAKUKURU inaogopa Wazungu, inaogopa kuwaudhi watu wanaowapa ushauri wa kitaalam kuhusu kesi za rushwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, maslahi ya Tanzania hapa ni makubwa mno iwapo tutafanikiwa kuonesha kuwa Benki ya Standard ilihonga kupata biashara nchini kwetu. Tukifanya hivyo, Tanzania itafaidika kwa namna mbili. Moja, itakuwa ni fundisho kubwa kwa Makampuni ya Kimataifa kwamba Afrika sio mahali pa kuhongana kupata kazi na kutoadhibiwa.
Mbili, Tanzania haitalipa mkopo huu na riba zake, tutakuwa tumeokoa zaidi ya shilingi trilioni mbili katika Deni la Taifa na kuelekeza fedha tulizokuwa tulipe riba kwenda kuhudumia wananchi wetu wenye afya na elimu. TAKUKURU waongozwe na maslahi mapana kwa Taifa badala ya kutafuta sifa ndogo ndogo za wangapi wamefikishwa Mahakamani. Ni lazima taasisi zetu sasa zianze kutazama mambo kwa picha kubwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, hii sio mara ya kwanza SFO kufanya ilichofanya dhidi ya Tanzania. Mnakumbuka kesi ya rada na Shirika la BAE la Uingereza. Safari hii Tanzania isikubali kubeba tu makubaliano ambayo SFO inafanya na Makampuni ya Kimataifa. Ni lazima tufanye uchunguzi wetu na tufungue kesi dhidi ya makampuni haya. Haiwezekani wawe ni Watanzania tu wanaoshtakiwa kwa rushwa na kuwaacha wanaotoa rushwa hizo wakiendelea na biashara zao kama kawaida.
Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa zilizopo sasa kwenye vyombo vya habari ni kwamba, Benki hii kupitia tawi lake la Tanzania (Stanbic Bank) siku ambayo walipata deal la Bond ndio siku hiyo hiyo walipewa kazi na Serikali ya kufungua akaunti ya ESCROW kuhusu fedha za bomba la gesi kutoka Mtwara. Kimsingi biashara hii ya ESCROW akaunti katika Benki hii ni kubwa zaidi kutoka ile ya mkopo kwani ni biashara ya kutunza fedha za Bomba kwa miaka 20!
Mheshimiwa Naibu Spika, Benki hii ilipata biashara kubwa kama hii bila ya kuwepo kwa zabuni yoyote ile na kuleta ushindani. Pia kama kulikuwa na umuhimu wa kufungua akaunti hii ni kwa nini Shirika la TPDC halikufungua akaunti hii katika Benki Kuu ya Tanzania? Haya ndiyo mambo ya TAKUKURU wanapaswa kuchunguza katika kulinda maslahi ya nchi yetu dhidi ya makampuni makubwa kutoka nje.
Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile kuna taarifa kwamba hata fedha ambazo zilipatikana kutokana na mkopo huu hazikufika kule kunakotakiwa. Nimewasilisha maswali Wizara ya Fedha kutaka kujua miradi ambayo fedha hizi zilikwenda. Hata hivyo, kutokana na orodha ya miradi niliyonayo na kutokana na habari za hivi karibuni za Serikali kudaiwa na wakandarasi, mradi wa Kinyerezi na hata mradi wa Kiwira ni dhahiri kuwa sehemu ya fedha zilizopatikana katika mkopo huu hazikupelekwa huko. Uchunguzi wa kina unatakiwa kwenye eneo hili ili kupata ukweli na kuzuia mambo kama haya kutokea siku za usoni.
Mheshimiwa Naibu Spika, nitatumia kanuni ya 120(2) kutaka Bunge lako Tukufu kuunda Kamati Teule kuichunguza Benki ya Standard ICBC ya Uingereza na kampuni yake dada ya Stanbic Tanzania kuhusiana na mkopo wa hatifungani $600m, matumizi ya mkopo huo na ufunguzi wa akaunti ya ESCROW ya Bomba la Gesi Mtwara – Dar es Salaam.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa nawasilisha mezani nyaraka zote nilizonazo kuhusiana na mkopo huu kwa ajili ya Bunge kupitia kabla ya kuwasilisha hoja ya kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge kuichunguza Standard Bank ICBC na Stanbic Bank.
Mheshimiwa Naibu Spika, uchunguzi wa IPTL Tegeta ESCROW Account, mwaka 2014 TAKUKURU waliijulisha Kamati ya Bunge ya PAC kwamba ilikuwa inachunguza na kumaliza uchunguzi kuhusu miamala ya kutoka akaunti ya Tegeta ESCROW Benki Kuu ya Tanzania kwenda Benki ya Stanbic Tanzania. Katika taarifa zote ambazo TAKUKURU inatoa kuhusu kesi za ufisadi, hakuna hata siku moja wanasema kuhusu uchunguzi huu na lini wahusika waliochota fedha za umma watafikishwa Mahakamani.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba tupate kauli ya Serikali kuhusu jambo hili kwani ni moja ya JIPU kubwa ambalo tunadhani Serikali inalikimbia. Serikali inaogopa nini? Serikali inamwogopa nani? Kwa nini kesi ya ufisadi wa IPTL inakaliwa kimya?
Mheshimiwa Naibu Spika, Tanzania ni mwanachama wa Open Government Partnership (OGP). Toka ianze, Tanzania ilisaini commitments mbalimbali kuhusu OGP ikiwemo kuwa wazi (online), taarifa ya mali na madeni ya Viongozi.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika hotuba nzima ya Waziri, suala la OGP halijatambulika kabisa. Serikali ina wajibu wa kulijulisha Bunge nini kinaendelea kwenye OGP.
Mheshimiwa Naibu Spika, Manispaa ya Kigoma Ujiji imechaguliwa kuingia kwenye OGP, Sub National Pilot. Hii ni heshima kubwa kwa Tanzania. Naomba Serikali itupe ushirikiano wa kutosha ili Manispaa ya Kigoma iweze kuwa taa kwenye OGP na kuipaisha Tanzania. Naomba Ofisi ya OGP Tanzania iandae mafunzo kwa Watendaji wa Manispaa kuhusu OGP.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kufahamu Serikali imefikia wapi kwenye utekelezaji wa Action Plan ya OGP? Naomba kupata maelezo kuhusu utekelezaji huo ili kuweza kufahamu maandalizi ya Action Plan inayofuata.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni maeneo gani ya Action Plan yametekelezwa na kwa kiwango gani? Je, Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea na OGP? Maana kwenye hotuba ya Waziri sijaona eneo lolote linalotaja OGP.
Mheshimiwa Naibu Spika, nadhani mpango huu ni mzuri sana kwa nchi yetu na itasaidia sana juhudi za Serikali katika kupambana na ufisadi kupitia uwazi katika uendeshaji wake.
Mheshimiwa Naibu Spika, naipongeza sana Taasisi ya TAKUKURU kwa kuongeza nguvu ya kupambana na rushwa na ufisadi. Mkurugenzi Mkuu mpya ameanza vizuri sana na kazi ya Taasisi inaonekana kutokuwa na majalada yaliyofunguliwa na kesi zinazofunguliwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, TAKUKURU inapaswa kutafsiri “inafanya kazi kwa maslahi ya nani?” Ni lazima TAKUKURU kwenda kwenye mzizi wa rushwa ya Kimataifa badala kutaka tu kuonekana kuwa “kesi zimefunguliwa.” Mfano, kesi ya Hati Fungani ya $600m. Bila kuingilia kesi iliyopo Mahakamani ya Ufisadi wa $6m, hivi kwa kesi hii maslahi ya nchi ni nini? Nadhani maslahi ya nchi ni mkopo ghali wa $600m ambao mpaka tutakaporudi kulipa, utagharimu Taifa $897m ifikapo mwaka 2020. Hii inatokana na mfumo wa riba uliotokana na Board hiyo. Nani anafaidika? Ni Benki ya Standard KIC PLC ya UK na investors 1/3.
Mheshimiwa Naibu Spika, ndani ya TAKUKURU kuna washauri kutoka Uingereza. Unategemea hawa Wataalam wa UK, wataangamiza Benki yao? TAKUKURU lazima iamke na kufanya jambo kubwa ambalo litaitingisha dunia kwa kuchunguza na kuishtaki Benki ya Standard kwa kutoa rushwa ili kupata biashara nchini kwetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, ufisadi wa Kimataifa una mtandao mpana sana. Nchi yetu imeingia kwenye deni kubwa la shilingi trilioni 1.2 na riba ya shilingi bilioni 600. Iwapo TAKUKURU ina nia ya dhati ya kumaliza rushwa ya Kimataifa, ni muhimu kuungana na Watanzania duniani ambao wametaka Taasisi ya SFO ya UK kufungua upya jalada la Standard Bank.
Mheshimiwa Naibu Spika, suala hili ni suala la national interest tukifanikiwa kwenye hili TAKUKURU itakuwa imeokoa deni la shilingi trilioni 1.8. Iwapo Standard Bank watashtakiwa, Tanzania haitalipa deni hilo, pia itakuwa somo kubwa kwa Makampuni ya Nje kuomba biashara kwa rushwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia kuna suala la waliopokea rushwa hiyo ya Hati Fungani, mbona hawapo Mahakamani? Benki ilitoa rushwa $6m, waliopokea rushwa ni wale walioleta biashara kwa Benki hiyo, lakini waliopo Mahakamani ni “madalali” wa rushwa. TAKUKURU inapaswa kutoa maelekezo ya kina sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kupata taarifa kuhusu uchunguzi wa suala la IPTL na Tegeta Escrow. TAKUKURU walimaliza uchunguzi tangu mwaka 2014. Naomba kupata taarifa ni kwa nini wezi, matapeli na Mafisadi wa IPTL hawajafikishwa Mahakamani?
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshmiwa Spika, naomba kuwasilisha maelezo yangu kwa maandishi na naomba yawekwe kwenye Hansard. Naomba mchango wa jana ubadilishe na huu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mnamo tarehe 9 Machi, 1967 aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alichapisha falsafa ya elimu ya kujenga nchi ya kijamaa. Falsafa hii ni elimu ya kujitegemea ambayo ilitaka kuleta mapinduzi ya elimu katika nchi yetu. Mwalimu Nyerere alisema shabaha ya elimu ni kutafsiri maarifa na busara kutoka kizazi kimoja kwenda kizazi kinachofuata na kuwaandaa vijana kwa ajili ya kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya nchi. Falsafa hii ilijenga kutatua changamoto za kutoa elimu yenye ubora tofauti kwa watu tofauti kulingana na kipato chao. Falsafa ya elimu ya kujitegemea ililenga kuondoa ugandamizwaji na wenye nguvu dhidi ya wanyonge na matajiri dhidi ya maskini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, miaka karibu hamsini sasa tujiulize mfumo wetu wa elimu unatoa maarifa muafaka kwa vijana wetu? Mfumo wetu wa elimu unaondoa matabaka katika nchi yetu? Ni dhahiri kwamba hivi sasa tuna elimu kwa ajili ya watu maskini na elimu kwa ajili ya watu wenye uwezo. Tuna elimu kwa ajili ya sisi viongozi na walimu kwa ajili ya wapiga kura.
Mfumo wetu wa elimu unajenga matabaka ya walionacho na wasionacho na kutokana na hali hiyo Serikali sasa inaanza hata kutaka kudhibiti bei za shule binafsi ili wenye uwezo wasipandishiwe bei zikawa kubwa zaidi hasa baada ya Serikali mpya kubana mianya ya kupata mapato yasiyo halali kuwezesha kulipa ada kubwa. Kazi ya Serikali kimsingi ni kusaidia wanyonge wanaosoma kwenye mashule yenye hali mbaya sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ifike wakati sasa tujiulize maswali magumu kuhusu elimu. Tujiulize changamoto za elimu ya Tanzania nini? Ni suala la bajeti ndogo? Ni suala la ubora wa elimu? Kama ni kuhusu bajeti ni kwa nini uwekezaji mkubwa uliofanywa kwa miaka kumi ya Serikali ya Awamu ya Nne ambapo zaidi ya shilingi trilioni mbili zimewekwa kwenye elimu na haujaboresha elimu yetu? Kama ni kuhusu ubora ni kwa nini tumeshindwa kulitatua na kila siku tunarudia na kurudia na kurudia? Ni nini nyufa katika mfumo wetu wa elimu wa sasa?
Mheshimiwa Mwenyekiti ni dhahiri tumekuwa tukitoa majawabu yale yale kwa tatizo la ubora wa elimu tukitegemea matokeo tofauti. Tumekuwa tukilalamika kuhusu bajeti, bajeti iliwahi kufika 20% ya bajeti mwaka 2008 lakini hakuna kilichobadilika. Tumekuwa tukilalamika kuhusu ughali wa elimu na tukapanua udahili kwa kiwango kikubwa lakini bado shida za elimu zipo pale pale. Hata sasa tumetangaza elimu ya msingi bila malipo na tunatuma fedha yote kwenye mashule (capitation grants), udahili umeongezeka kwenye baadhi ya maeneo mpaka 140%. Lakini elimu bado haitengemai.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jana niliuliza rafiki zangu kwenye mtandao wa facebook kuhusu mambo gani wanayotaka kufanywa ili kuboresha elimu nchini kwetu. Nimeambatanisha maoni yao na kuwasilisha kwako ili yaingie kwenye Hansards za Bunge. Maoni ni mengi yanashabihiana na hali halisi ya elimu yetu. Kila Mtanzania analalamika na kutoa mapendekezo ya namna ya kuboresha elimu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumetunga sera mpya ya elimu inayounganisha elimu ya sasa ya msingi na sekondari na kuitwa elimu msingi. Tumeweka miaka kumi ya watoto kusoma elimu msingi. Muono wa sera ni kana kwamba changamoto zetu ni miaka ambayo watoto wanakaa shule. Mwandishi mmoja kuhusu elimu kaandika kitabu cha Rebirth of Education: Schooling isn‟t learning. Mwandishi huyu anaitwa Lant Pritchett. Naomba watu wote wanaopenda elimu nchini na wanotaka kuleta mapinduzi kwenye elimu wasome kitabu hiki. Kimsingi Pritchett anasema kukaa darasani sio kupata elimu, kwenye nchi nyingi zinazoendelea ikiwemo Tanzania tumewekeza kwenye kufikia malengo ya idadi ya watoto wanaoandikishwa badala ya kuwekeza kwenye kutoa maarifa kwa watoto. Ndiyo maana hapa nchini kwetu takribani vijana 60% wanaofanya mtihani wa kidato cha nne hufeli kwa kupata sifuri na kwenye baadhi ya mikoa kama Kigoma 86% hupata sifuri na daraja la nne. Watoto wanakwenda shuleni lakini hawajifunzi, hawapati elimu. Sera ya elimu lazima itoe fursa ya kuzalisha watoto wanaopata elimu na sio kukaa darasani tu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, utafiti wa karibuni kabisa unaonyesha ni 40% pekee ya watoto wa darasa la nne wanaoweza kufanya hesabu hii, sita gawanya kwa tatu (6/3) au kuzidisha saba mara nane. Matokeo ya miaka na miaka ya uwezo yanaonyesha hali hiyo pia. Kwa mfano karibu 50% ya watoto wanaomaliza darasa la saba hawawezi kufanya mahesabu au kusoma hadithi ya darasa la tatu. Kwa nini watoto wetu hawajifunzi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, visababishi vya hali hii ni vingi sana, lakini kikubwa kuliko vyote ni mwalimu. Matatizo kuhusu mwalimu Tanzania ni lundo lakini tunaweza kuongelea mawili kwa leo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, uwepo wa walimu katika miaka ya karibuni nchi yetu imepiga hatua katika kusomesha na kusambaza walimu. Lakini walimu wengi waliopo mashuleni hawafundishi. Utafiti wa karibuni kabisa unaonyesha kuwa ukifanya ziara ya kushtukiza mashuleni ni 47% ya walimu waliopo shuleni ndiyo waliopo darasani kufundisha vipindi walivyopangiwa.
Aidha, walimu wanafunzi nusu tu ya muda wanaopaswa kufundisha. Matokeo yake ni kwamba asilimia 50 ya muda wa watoto shuleni unapotea bila kusoma. Kiuchumi maana yake ni kwamba tunapoteza asilimia 50 ya uwekezaji katika elimu ukizingatia kwamba pesa nyingi katika elimu zinaenda katika mishahara ya walimu. Utafiti ambao umetolewa leo uitwao Tanzania Service Delivery Indicators unathibitisha kuwa 49% tu ya walimu wanaingia darasani na kufundisha zaidi ya nusu hawapo shuleni kabisa au hawafundishi. Utafiti huu umehoji walimu 3,692 na wanafunzi 4,041 na umefanywa na REPOA na Benki ya Dunia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hali hii inasababishwa kwa kiasi kikubwa na motisha na usimamizi hafifu kwa walimu. Hivyo ni muhimu kufanya bidii kama nchi kutoa motisha kwa walimu lakini ni muhimu pia walimu wasimamiwe na wapewe mafunzo kazini ya mara kwa mara. Kwa sasa ni asilimia tano tu walimu wanakuambia wamewahi kuhudhuria mafunzo yoyote kazini katika miaka mitano iliyopita. Ndiyo maana tumekuwa tukidai kwa miaka mingi sana chombo cha kitaaluma cha walimu (Teachers‟ professional board) lakini Serikali imegoma kunyang‟anywa udhibiti wa walimu. Tuwekeze kwa mwalimu kama ninavyoshauri hapa chini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu ya juu hapo ni balaa kabisa, ubora wa vyuo vikuu umeanza kutia shaka. Katika utafiti wa juzi juzi wa Times Higher Education hakuna chuo hata kimoja cha Tanzania kilichopo katika orodha ya vyuo bora 30 Afrika. Tupo nyuma ya Makerere na Nairobi ambavyo tulikuwa tunavizidi, hatufanyi uwekezaji katika tafiti. Nchi ilishaamua kuwekeza asilimia moja ya Pato la Taifa katika utafiti lakini hadi sasa Serikali imetoa 0.001%. Vitabu vya bajeti vinaonyesha kuwa bajeti kubwa ya elimu inakwenda elimu ya juu lakini kwenye mikopo. Uwekezaji kwenye utafiti haufanyiki na tutaathirika sana kama Taifa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nini falsafa ya Rais Magufuli katika elimu? Rais anasema Tanzania ya Magufuli ni Tanzania ya viwanda, viwanda kwenye nchi ya wajinga? Nani anafanya kazi kwenye viwanda hivyo? Nani atasimamia mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kijamii na hata ya kisiasa yatakayoletwa na uchumi wa viwanda? Tunaposema tunataka nchi ya uchumi wa kati tunajua mahitaji ya elimu ya uchumi wa kati? Tunaelekeza rasilimali fedha katika kujenga rasilimali watu itakayoendesha uchumi wa viwanda? Tunaposema uchumi wa viwanda tunawasemea watoto wetu hatujisemei sisi, tunasemea kizazi kijacho. Tunakiandaa kwa Tanzania hiyo?
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mahusiana chanya kati ya elimu na ukuaji wa uchumi, vilevile kuna mahusiano chanya katikati ya ubora wa rasilimali watu (elimu na afya) na ukuaji wa uchumi. Tafiti zinaonyesha kuwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara zinaweza kwenda kwa kasi kiuchumi iwapo zitawekeza kwenye elimu na afya. Robo ya kasi ya ukuaji uchumi inaweza kuchangiwa ubora wa rasilimali watu pekee.
Hivyo tunapotaka kujenga uchumi wa viwanda na ili uchumi huo uwe na maana ni lazima kuwekeza vya kutosha kwenye elimu. Hata hivyo, ni lazima tuwekeze tukiwa na ushahidi wa kisanyansi kuhusu nyufa za elimu ya Tanzania (evidence based policy interventions).
Mheshimiwa Mwenyekiti, sekta ndogo ya elimu ya ufundi peke yake inahitaji Watanzania wenye ujuzi wa juu milioni tatu ifikapo mwaka 2025. Pia Tanzania inahitaji watu wenye ujuzi wa ufundi (kutoka VETA na Technical Schools) wapato milioni saba ifikapo mwaka 2025.
Ni muhimu sana kufungua macho na kufanya maamuzi mahususi kuhusu elimu. Tunahitaji uwekezaji wa angalau 20% ya bajeti yetu kwenda kwenye elimu kwa miaka kumi ijayo ili kuweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye elimu. Hata hivyo, kipimo cha msingi cha mafanikio katika mfumo wa elimu ni kama watoto wanaotoka kwenye mfumo huo wa elimu wana maarifa, ujuzi na uwezo wa ulimwengu watakaoukabili. Hatuwezi kupata mafanikio haya bila kufumua mfumo wetu wa elimu, kupanua demokrasia ya utoaji elimu na kuhakikisha walimu wanapata motisha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya motisha tunayoweza kuwapa walimu ni kuwalipa vizuri, kuwasimamia vizuri na kuwapa mitihani maalum kila wakati ili kuwapandisha madaraja.
Napendekeza salary scale ya walimu iwe sawa na angalau nusu ya salary scale ya Wabunge na viwango vya mishahara kati ya walimu wanaofundisha ngazi yoyote ile iwe sawa kulingana na usawa wa elimu, muda kazini na juhudi (performance based remunerations). Najua haya yaweza kuonekana magumu lakini naamini maneno aliyoyasema mwanaharakati wa elimu nchini Rakesh Rajani aliyepata kusema more of the same won‟t cut I anymore. Kama elimu ndio silaha kubwa ya kuleta maendeleo, ni lazima tufanye tofauti ili kuboresha elimu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja ya Kamati ya Bunge ya Huduma Maendeleo ya Jamii kwamba Taifa liunde Tume ya Wataalam ili kuweza kutafuta nyufa za elimu yetu na kutoa mapendekezo yanayotokana ushahidi wa kisayansi. Tuunde Tume ya Elimu sasa ili tuweze kuwa na muda wa kutosha wa kutatua changamoto za elimu nchini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika pendekezo la kuanzisha vyuo vya ufundi kila mkoa natoa maombi maalum kwa mkoa wa Kigoma kuanzisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujiji (Ujiji Institute of Technology – UIT). Mji wa Ujiji ni moja ya miji mikongwe nchini ambayo inasinyaa kama sio kufa. Uanzishaji wa chuo utakaoweza kudahili angalau wanafunzi 5,000 itakuwa ni chachu kubwa ya maendeleo mji huu na Tanzania kwa ujumla. Taasisi ya Teknolojia ya Ujiji itaweza kusaidia sana kuziba mianya ya wataalam wa katika kwenye sekta ya usafirishaji (logistics) kwa kuzingatia kuwa Kigoma ni lango la Magharibi la Taifa letu. Napendekeza kuwa Serikali ilitazame kwa kina ombi hili ili kuweza kuongeza wataalam wa kati katika nchi yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapendekeza pia Serikali itazame upya suala la sera ya vitabu ili kuhakikisha kuwa uwekezaji katika uchapishaji unaongezeka nchini. Nadhani ni wajibu wa Serikali kuhakikisha ubora wa vitabu badala ya yenyewe kuhangaika na kuandika na kuchapisha vitabu. Sera ya vitabu inazalisha ajira kwenye nchi na inawezesha Watanzania kutafuta fursa kwenye maeneo hayo pia. Wachapishaji wa ndani wanashindwa kukua kwa sababu Serikali imewabana. Serikali haipaswi kubana, inapaswa kuchochea ukuaji wa sekta ya uchapishaji.
Vilevile napendekeza sana tuwekeze kwenye maktaba za kijamii kwenye kata zetu na miji yetu. Maktaba hizi ziwe na vitabu na tuhamasishe watu wenye vitabu kutoa vitabu kwa maktaba hizi. Tujenge Taifa la wasomaji kwa kuhamasisha usomaji kuanzisha ngazi za chini kabisa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nasisitiza kuwa mapendekezo ya Kamati ya Bunge kuhusu namna ya kutoa mikopo na kuikusanya yachukuliwe kwa uzito unaostahili. Mikopo isiwe sehemu ya bajeti ya Wizara badala yake Bodi ipewe fedha moja kwa moja kutoka hazina (direct transfer) na mfumo wa malipo udhibitiwe. Ni lazima tufanye tafiti kuhakikisha kuwa ifikie wakati Bodi ya Mikopo iweze kujiendesha yenyewe kutokana na fedha zinazorejeshwa. Mfumo wa kutumia credit reference bureau na vitambulisho vya Taifa na hata mobile technology kuhakikisha mikopo inarejeshwa ni mfumo ambao utakuwa na mafanikio makubwa sana. Serikali ifanyie kazi pendekezo hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nasisitiza pia kuwa pendekezo la Kamati kuanzisha President Magufuli Scholarship Award lianze mara moja. Tuchukue watoto waliofanya vizuri angalau 50 kila mwaka na kuwasambaza kwenye vyuo vikuu vikubwa duniani. Ndani ya miaka kumi tutakuwa tumetengeneza mamia ya Watanzania wenye uwezo mkubwa kwenye nyanja zote nchini. Rais atakuwa ameacha jambo kubwa na la kukumbukwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji na nina maeneo machache kama matatu au manne hivi kama muda utakuwa umeniruhusu ili niweze kuchangia uboreshaji wa hotuba hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza katika Hotuba ya Msemaji wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Mheshimwa Komu, amezungumzia suala zima la discrepancy iliyopo kati ya vitabu vya Wizara, vitabu vya Wizara ya Fedha, kwa maana ya kitabu Na. 4 cha maendeleo na randama ya Wizara ya Viwanda na Biashara kuhusiana na mradi wa General Tyre, ambapo mpango wa maendeleo unasema fedha zitakazotengwa ni shilingi bilioni mbili, randama ya Viwanda na Biashara inasema fedha ni shilingi milioni 500 na kitabu cha bajeti ya maendeleo kinasema shilingi milioni 150.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niikumbushie hoja hii kwa sababu nadhani ni hoja muhimu sana ili tuweze kufahamu tunapopitisha bajeti hii ni nini hasa tunachokipitisha. Kwa sababu ni vyema tukajua ni shilingi milioni 150 itakayopitishwa na Bunge, ni shilingi bilioni mbili ambayo ipo kwenye Mpango wa Maendeleo kwa ajili ya General tyre au ni shilingi milioni 500 iliyoko kwenye randama ya vitabu vya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, nami nataka kurejea kauli ambayo Wabunge wenzangu Wamezungumza kwamba tunataka kujenga viwanda gani, kwa sababu ni lazima tuwe na focus na tuweze kuhakikisha kwamba tunaendana na ile focus ambayo tumeiweka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nilipokuwa napitia hotuba ya Waziri, nimeona katika Ibara ya 191 ya hotuba yake, anazungumzia malengo ya mwaka 2016/2017. Katika haya malengo yote, sioni lengo ambalo linaelekeza nchi yetu kwenda kuzalisha bidhaa ambazo wananchi wengi wanazitumia na hapa nazungumzia sukari, mafuta ya kula na nguo. Hizi ni bidhaa ambazo wananchi wanazitumia kila siku. Hata hivyo, katika malengo tisa ya mwaka wa 2016/2017 ya bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, sioni jambo hilo. Sasa nashindwa kuelewa, Wizara haioni kwamba kuna tatizo katika maeneo hayo na kwamba tuna haja ya kufanyia kazi jambo hili?
Mheshimiwa Mwenyekiti, kinachonisikitisha zaidi ni kwamba kuna tatizo la Wizara kutokusomana; yaani Wizara ya Kilimo inachokisema, hukioni kwenye Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji. Viwanda vyetu sisi kimsingi vinategemea sana malighafi za kilimo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hapa nina hotuba mbili, nina hotuba ya Wizara ya Kilimo na nina hotuba ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji. Katika hotuba ya Wizara ya Viwanda na Biashara, sukari siyo priority kabisa. Haitajwi kabisa! Katika hotuba ya Wizara ya Kilimo ukurasa wa 25, 44 na 63, anazungumzia mikakati ya kuondokana na tatizo la uhaba wa sukari. Mpaka kwenye kiambatanisho namba sita cha hotuba ya Wizara ya Kilimo, kuna mikakati na miradi mingi na mpaka mradi wa Mheshimiwa Kawambwa ambao ameuzungumzia leo wa Bagamoyo na changamoto zake, imeelezwa. Hiki unachokisoma huku, haukisomi Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa napenda kujua, Mheshimiwa Kaimu Waziri Mkuu yuko hapo, cabinet haikukaa kuweza kuwianisha Kilimo na Viwanda? Kwa sababu Waziri wa Kilimo akilima miwa, haiwezi kuwa sukari bila viwanda. Ukiangalia humu, miradi ambayo imeainishwa kwenye Wizara ya Kilimo, ni miradi ambayo inaweza kuzalisha tani milioni moja na nusu za sukari. Maana yake ni kwamba tutaweza kutumia ndani na kuuza nje na kwa bei ya sukari ya jana, tunaweza tukauza mpaka Dola za Kimarekani milioni 500 kulingana na miradi ambayo iko humu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini hiyo miradi ambayo ipo humu, huioni kwenye viwanda. Tunasema kwamba sisi tunachokitaka ni kuanza na bidhaa za kilimo ili wananchi wetu wapate ajira tuongeze thamani na kadhalika na nadharia za uchumi zinaonesha hivyo.
Sasa Waheshimiwa Wabunge wenzangu, naomba tukubaliane kitu kimoja ambacho kimo ndani ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, hata tukimpitishia Waziri fedha zake zote sasa hivi, tutarudi mwakani, sifuri. Kwa sababu hakuna tutakachoweza kuki-solve. Iwapo Wizara ya Kilimo na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, wakioanisha mipango yao, ndani ya miaka mitatu hatuna shida ya sukari tena nchini. Wala hatutamwangaisha tena Mheshimiwa Rais kutembea barabarani anatoa amri kuhusu sukari.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais anatoa amri kuhusu sukari kwa sababu Mawaziri hawafanyi kazi yao. Kwa sababu matamko ambayo Mheshimiwa Rais anayazungumza kuhusu sukari, ni matamko ambayo yalipaswa kuzungumzwa na Mawaziri. Kama kungekuwa na coordination kati ya Wizara ya Kilimo na Wizara ya Viwanda na Biashara wala tusingekuwa na shida leo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nawaomba Waheshimiwa Wabunge, kwa mujibu wa ibara ya 69 ya Kanuni zetu za Bunge, Mbunge anayependa mjadala unaoendelea juu ya hoja yoyote uahirishwe hadi wakati wa baadaye, anaweza kutoa hoja kwamba mjadala sasa uahirishwe na atataja mjadala huo uahirishwe hadi wakati gani na pia atalazimika kutoa sababu, kwa nini anataka mjadala huo uahirishwe. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachokiomba Waheshimiwa Wabunge na hapa tuwe beyond party politics, yaani tuwe zaidi ya Vyama vyetu. Nawaomba tuiombe Wizara ya Kilimo na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ziende zikakae, wafanye marekebisho ya Bajeti ya Viwanda na Biashara, halafu ndiyo baadaye turudi, kujadili suala zima la Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji. Vinginevyo hapa tunakuwa tumecheza. Bahati mbaya sana, tumeshapitisha Wizara ya Kilimo. Ilitakiwa zote mbili hizi, tusizipitishe kwanza, wakae, wazungumze watuletee program. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nawaomba Waheshimiwa Wabunge kwa mujibu wa Kanuni ya 69 ya Bunge, mjadala huu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji uahirishwe. Hulikuti jambo hili kwenye sukari peke yake, unalikuta kwenye nguo, Wizara ya Kilimo inazungumzia pamba, lakini uzalishaji wa pamba umeporomoka kwa asilimia 47. Wizara ya Viwanda inasema itaimarisha viwanda vya nguo, utatoa wapi pamba ya kuingiza kwenye viwanda vya nguo. Pamba imeshuka by six and seven percent. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji haijazungumza kabisa suala la bidhaa ya mafuta ya kula. Leo hii ukitembea unakwenda Singida, unawakuta wananchi wetu wanapigwa na jua barabarani wanauza mafuta kwenye madumu. Mafuta ya alizeti leo bei yake ni kubwa kuliko bei ya petroli katika Soko la Dunia, lakini hamna mpango, hakuna links kati ya kilimo na viwanda.
Kama tunataka tuzungumze kuwafurahisha wananchi kwamba tunakwenda kwenye uchumi wa viwanda tuendelee kupitisha hii bajeti. Kama tunataka angalau Bunge hili lifanye value addition katika kazi ambayo Serikali inafanya, tuombe hawa ndugu zetu watoke, Wizara ya Kilimo na Wizara ya Viwanda waende wakakae wawianishe mipango yao watuletee tuweze kupitisha. Tukipitisha hivi hivi, hatutaweza kufanya chochote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba nitoe hoja kwamba mjadala wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji uahirishwe ili Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji na Wizara ya Kilimo waende wakakae waweze kuwianisha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho kabisa, viwanda vinahitaji vivutio. Nitatoa hoja mwishoni. Kuna umuhimu mkubwa sana, maana yake nasikia sasa hivi kuna mvutano kati ya Wizara ya Fedha na Wizara ya Viwanda kwa ajili ya kutoa vivutio kwenye viwanda vya kimkakati. Sasa Mheshimiwa Rais yuko barabarani, anapiga kelele kuhusu sukari; mwekezaji anataka kujenga kiwanda cha sukari; mnatakiwa mkubaliane mtoe vivutuo kiwanda kile kiweze kujengwa, Wizara ya Fedha inakataa. Maana yake nini? Kwa hiyo, Mheshimiwa Rais analaghai wananchi? Haiwezekani! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ndiyo maana nasema kuna haja kubwa sana hawa watu wakakae tena. Naomba nitoe hoja kwa mujibu wa Kanuni ya 69, kwamba Bunge hili liahirishe shughuli za Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji mpaka hapo watakapoainisha mipango ya kilimo na mipango ya viwanda na biashara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitoe hoja na naomba mniunge mkono Waheshimiwa Wabunge.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna changamoto ya sukari; changamoto hii suluhisho lake ni uzalishaji. Tatizo ninaloliona ni kukosekana kwa utaratibu ndani ya Serikali. Hotuba ya Waziri ukurasa 140 ibara ya 191 inaeleza malengo ya kisekta ikiwemo viwanda. Hata hivyo, katika malengo tisa hakuna hata lengo moja kuhusu kuzalisha bidhaa zinazotumiwa zaidi na wananchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baadhi ya bidhaa hizo ni sukari, nguo na mafuta ya kula. Hata hivyo, ukisoma hotuba ya Wizara ya Kilimo ukurasa wa 25 na ukurasa wa 44; Wizara hiyo imeelezea mikakati ya kulima miwa kwa ajili ya kuzalisha sukari. Ili miwa iwe sukari, tunahitaji viwanda. Wizara ya Viwanda na Biashara haina malengo haya. Je, Serikali haina uratibu? Serikali inasema sema tu bila uhakika isemalo?
Mheshimiwa Mwenyekiti, orodha ya miradi kwenye Wizara ya Kilimo inaweza kuzalisha tani 1.5m za sukari kwa mwaka. Kwa bei ya jana ya sukari na kupata $500m za Marekani kama forex. Hii ni robo ya lengo letu la mpango wa maendeleo kwa sekta nzima ya viwanda. Naomba mlete addendum ya hotuba ili tuweze kuwa na lengo la kuzalisha sukari na kuondokana kabisa na tatizo la sukari. Napendekeza muongeze lengo katika ibara ya 191 amendment ukurasa wa 140, ongezea (i) na rekebisha (i) iwe (ii) na kuendelea.
(i) Kuhamasisha kuanzisha na kuendeleza viwanda vya bidhaa zinazotumika zaidi na wananchi kama sukari na mafuta ya kula. Hii ni pamoja na kuhamasisha viwanda vidogo vya wakulima kwenye maeneo yanayolima miwa ya ziada kama Kilombero na Mtibwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kufuatia mapendekezo hayo hapo juu, naomba pia kusisitiza kuhusu viwanda vya kusindika mafuta ya kula. Tanzania ina mawese na alizeti ambapo iwapo tukiweka nguvu kubwa kwenye kuzalisha mawese na alizeti tutaweza kuwa na mafuta mengi zaidi na hata kuuza nje.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Kigoma tuna mpango/mradi wa kulima hekta 100,000 za michikichi kwa mpango wa hekta moja kwa familia moja. Iwapo tutafanikiwa tutaweza kuzalisha tani 200,000 za mafuta kutoka nje yenye thamani ya dola milioni 240 kwa mwaka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Viwanda inabidi ifanye kazi na Wizara ya Kilimo na Mkoa wa Kigoma ili kufanikisha jambo hili. Mkoa wa Kigoma na Mkoa wa Singida inaweza kuwa Mikoa ya kimkakati ya kumaliza kabisa uingizaji wa mafuta ya kula kutoka nje. Mipango iwekwe kwenye mikakati.
Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo ambalo litaondoa kabisa tatizo la ajira muhimu ni viwanda vya nguo (Textile Industries). Ukisoma hotuba ya Wizara ya Kilimo, unaona namna uzalishaji wa pamba umeshuka mwaka 2014/2015 kwa 47%.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo azma ya Wizara ya Viwanda lazima iendane na malengo ya Wizara ya Kilimo kuongeza uzalishaji wa pamba nchini. Kuna hatua za kuchukua sasa hivi ikiwemo udhibiti wa ukwepaji kodi unaofanywa na waagizaji wa nguo nchini. Viwanda vya ndani vya nguo vinapata shida kubwa sana kutokana na magendo ya nguo. Pambaneni na magendo ya nguo ili tulinde viwanda vya ndani vya nguo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Viwanda ifanye kazi na Wizara ya Kilimo ili kuongeza uzalishaji wa pamba nchini na tuongeze thamani ya pamba kwa kuzalisha nyuzi, vitambaa na nguo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kumalizia; viwanda vya sukari, mafuta ya kula na nguo viwe vipaumbele vya juu kabisa kuanzia mwaka 2016/2017. Tuwe focused, tuwe na sequence; narudia; nguo, mafuta ya kula na sukari.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kushukuru kwa kupata nafasi ya kuchangia hotuba ya Wizara ya Afya. Nina maeneo manne kama muda ukiniruhusu kwa ajili ya kuboresha na kuhakikisha kwamba tunaimarisha huduma za afya katika nchi yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya kazi za mwanzo kabisa ambazo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Magufuli alizifanya ni kwenye sekta ya afya. Tulimwona alikwenda Muhimbili na kutoa maagizo na tuliona Mawaziri na watendaji wa Wizara wakihangaika kutekeleza maagizo yale. Kwa hiyo, watu wengi tulitarajia kwamba afya ingekuwa ni kipaumbele kikubwa sana kwa Serikali. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuona bajeti ya Wizara ya Afya utaona kwamba, kimsingi licha ya kwamba bajeti ya mwaka huu imeongezeka kutoka bajeti ya mwaka jana, ambapo bajeti ya mwaka jana ilikuwa shilingi bilioni 446 na bajeti ya mwaka huu ni takribani shilingi bilioni 870 lakini bado bajeti ni asilimia tatu tu ya bajeti nzima ya Serikali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali yetu ina commitments kwa Abuja Declaration ya asilimia 15 ya bajeti kwenda kwenye afya lakini ukichukua shilingi bilioni 870 ukagawa kwa shilingi trilioni 29.5 unapata asilimia tatu tu ya bajeti ndiyo imeelekezwa kwenye afya. Ukienda ndani zaidi utaona kwa mfano, Serikali imepanga bajeti kwa ajili ya ununuzi wa madawa, bajeti kwa ajili ya MSD shilingi bilioni 251, lakini katika fedha hizo shilingi bilioni 131 ni za kulipa madeni ya nyuma ya MSD. Kwa hiyo, kimsingi bajeti ya madawa iliyopangwa kwa mwaka huu ni shilingi bilioni 120 tu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mbaya zaidi Serikali humu Bungeni ilitamka kwamba madeni yote ya MSD yamechukuliwa na Wizara ya Fedha. Serikali ilitamka hivyo mwaka juzi wakimjibu Mheshimiwa Margaret Sitta alipokuwa Mwenyekiti wa Kamati. Serikali ikasema hivyo mwaka jana kwenye hotuba ya Serikali ya mwaka jana. Mwaka huu madeni yale yote yamerundikwa ndani ya Wizara ya Afya. Matokeo yake ni kwamba, bajeti ya Wizara ya Afya inaonekana ni kubwa lakini sehemu kubwa hasa kwenye madawa inakwenda kulipa madeni ya zamani ya MSD, kwa hiyo, kimsingi bajeti haijaongezeka. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, napendekeza tuangalie uwezekano wa kuongeza bajeti ya Wizara ya Afya angalau ifikie asilimia tano ya bajeti nzima ya Serikali ambayo ni shilingi trilioni 1.4. Hiyo, ndiyo rai ambayo naitoa kwa Waheshimiwa Wabunge.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kutokana na ufinyu huu wa bajeti kuna baadhi ya huduma ambazo Serikali imekuwa ikizitoa kwa msaada wa wafadhili hazifanyiki tena. Masuala ya damu salama yana tatizo kubwa sana sasa hivi kwa sababu wafadhili wamejitoa na Serikali haijaelekeza bajeti kwenye damu salama. Vilevile utafiti uliokuwa unafanyika pale Muhimbili kwa ajili ya watoto wanaozaliwa na sickle cell nao umeguswa kutokana na tatizo hili la bajeti.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu ni ya nne duniani kwa watoto wenye sickle cell baada ya Nigeria, Congo, India, Tanzania. Tuna watoto 12,000 nchini ambao wana sickle cell. Kwa kipindi cha miaka kumi kumekuwa kuna taasisi inaitwa Welcome Trust ya Uingereza ambayo ilikuwa inafadhili huduma hizi na utafiti wa sickle cell pale Muhimbili. Watu wale wameondoa ufadhili wao na Muhimbili hapa tunapozungumza wamesimamisha huduma za sickle cell. Huduma ambazo zilikuwa zinaendeshwa na daktari wa Kitanzania, msomi ambaye amepata Awards kubwa duniani kwa ajili ya utafiti wake kwenye sickle cell.
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii tunavyozungumza huduma ile imefungwa na yule ameambiwa aondoke pale Muhimbili kufanya huduma hiyo. Toka huduma hiyo imefungwa mpaka leo, kwa takriban mwezi na nusu tu watoto watatu wenye sickle cell wameshafariki kwa sababu nchi yetu haina clinic nyingine yoyote ya sickle cell hapa nchini. Kwa hiyo, leo watoto wakifika Muhimbili wanaambiwa nendeni Amana, Mwanyamala, Temeke wa mikoani wabaki mikoani lakini kule mikoani hakuna huduma hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ilipanga fedha za utafiti one percent ya pato la Taifa ambayo inaenda takribani shilingi bilioni 50 hivi, Wizara ya Afya na Muhimbili waangalie utaratibu, wazungumze na COSTECH tupate sehemu ya fedha hizi kuendeleza utafiti wa sickle cell na huduma ya sickle cell na huduma hiyo itolewe bure kwa watu wenye sickle cell, vinginevyo tutaendelea kupoteza maisha ya watoto wetu ambao wanazaliwa wakiwa na sickle cell. Kwa hiyo, jambo hili naomba Wizara ilitazame kwa umakini sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala hilohilo kwenye damu salama tuna tatizo wafadhili wamejitoa. Pia sasa hivi kuna mradi ambao unaendelea ambao unaendeshwa na Dkt. Othman kwa ufadhili wa mfuko wa GSM kwa ajili ya watoto wenye kuzaliwa na vichwa vikubwa. Mradi huu unafadhiliwa na wafadhili, mfadhili akiondoka na wenyewe utakuwa kwenye the same problem. Kwa hiyo, naomba Wizara ya Afya ijaribu kuona namna gani ambavyo tutaweza kushughulika na mambo hayo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo lingine kubwa ambalo tumekutana nalo kwenye Kamati na limeelezwa kwenye taarifa yetu ya Kamati na Mwenyekiti wetu, ni suala la watumishi wa afya. Tuna tatizo kubwa la watumishi wa afya. Takwimu zinatisha kuhusu watumishi wa afya na hasa watumishi wa afya kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitali za vijijini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tunavyozungumza wahudumu wa afya vijijini asilimia 93 ni uhaba, Madaktari kwenye hospitali za wilaya takribani asilimia 70 ni uhaba, hawapo. Mwaka huu Wizara haijaajiri, ruhusa ya kuajiri imetolewa lakini mpaka sasa Wizara ya Afya haijaajiri. Kwa hiyo, naomba Wizara ya Afya ijaribu kuangalia ni namna gani itashughulikia jambo hili maana tunaoathirika sana ni watu ambao tunatoka mikoa ya pembeni na pembezoni ambapo Madaktari wakipangwa hawaji na matokeo yake inakuwa ni tatizo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ni pendekezo kwa Wizara ya Afya kuhusiana na bodi ya kitaalam ya watu wanaofanya huduma za physiotherapy. Bodi hii itaweza ku-regulate license zao na shughuli wanazofanya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, ni bima ya afya. Nchi yetu hivi sasa ina Mfuko wa Bima ya Afya na baadhi ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ina mafao ya bima ya afya. Nadhani imefikia wakati, nitatoa mchango huu kwa maandishi ili Wizara iweze kunielewa zaidi, tuunganishe ili pasiwe na Mfuko ambao wenyewe moja kwa moja unaendesha fao lile la afya. Mifuko yote ambayo wanachama wake wanafaidika na bima ya afya tuiunganishe wa-limit fedha zao NHIF ili tuwe na one unity, one composite ambayo ina-deal na bima ya afya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa taratibu za ILO ukichangia kwenye hifadhi ya jamii percent fulani inapaswa kuwa ni fao la afya. Kwa hiyo, leo kuna baadhi ya wafanyakazi wa Serikali kwa mfano, wafanyakazi wanaochangia PSPF, wanachangia PSPF twenty percent inakwenda mchango wa mwajiri na mchango wa mfanyakazi lakini at the same time wanachangia NHIF three percent yake, three percent ya mwajiri. Kwa hiyo, unakuta mfanyakazi anatoa michango mingi sana wakati uleule mchango uliokwenda PSPF ilitakiwa percent yake iende bima ya afya kwa ajili ya huduma za bima za afya na kwa kufanya hivyo tutakuwa tumepanua sana bima ya afya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Wizara ya Afya waje Kigomba na Ruangwa, tuna mradi ambao tunafanya kwa kushirikiana na World Bank ambapo ndani ya miaka miwili tutakuwa na universal coverage health insurance. Hii itaweza kuwapa somo la namna ya kufanya katika nchi nzima kwa sababu ni lazima ifikie wakati nchi yetu watu wote wawe na bima ya afya. Kwa sababu matatizo ambayo tunayapata sasa hivi, allocation za madawa na kadhalika ni kwa sababu hatuna mfumo madhubuti wa bima ya afya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, reforms ambazo tumependekeza na nitawaletea zingine kwa maandishi mziangalie. Najua Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla aliunda timu ya wachumi na madaktari kwa ajili ya kuangalia possibility ya kuunganisha mfumo wa bima ya afya katika nchi yetu na kupata afya ya jumla, nitaweza kuangalia namna gani tutaweza kusaidiana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niishie hapo maana muda wenyewe ndiyo hivyo tena umekwisha au unaniongezea muda kidogo?
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu viwanda vya kukuza uchumi na ujenzi wa msingi wa uchumi wa viwanda, ukurasa wa 52, 6.3(e), nashauri iongezeke mafuta ya mawese. Tanzania inaagiza mawese tani 600,000 kwa mwaka inayogharimu dola milioni 450 ya fedha za kigeni.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mkoa wa Kigoma unaweza kuzalisha zaidi ya kiwango hiki iwapo wananchi watahamasishwa kulima michikichi na kuvutia uwekezaji kwenye viwanda vya mazao ya mawese. Manispaa ya Kigoma inahamasisha mfumo wa one family, 1hc ili kuzalisha tani 80,000 za CPO.
Mheshimiwa Naibu Spika, marekebisho, page 52 ya mapendekezo, barabara hii inapaswa kuitwa Manyovu-Kasulu-Kibondo-Kabondo na siyo kama ilivyoandikwa. Nashauri muwasiliane na Wizara ya Uchukuzi maana kuna mabadiliko kwenye jina la mradi.
Mheshimiwa Naibu Spika, pongezi, page ya 18, tafsiri ya Reli ya Kati imetolewa vizuri. Ni sawa sasa, hii ndiyo tafsiri sahihi.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukurasa wa 43, kilimo cha mpunga. Katika Mkoa wa Kigoma, Manispaa ya Kigoma-Ujiji kuna mradi wa kilimo cha umwagiliaji katika delta ya Mto Lwiche. Mradi huu unatarajiwa kufadhiliwa na Mfuko wa Falme ya Kuwait (Kuwait Fund) kwa gharama ya dola milioni 15. Hata hivyo, Serikali ya Tanzania inapaswa kutoa fedha za feasibility study na detailed design. Naomba mradi huu mkubwa sana wa hekta 3,000 uingizwe kwenye orodha ya ukurasa wa 43. Pia naomba upembuzi yakinifu na usanifu wa kina umalizike ili tuweze kupata mradi huu ndani ya 2017/2018.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake pamoja na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018.
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili na mimi niweze kuchangia hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, kuhusiana na mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali tukifahamu kwamba Waziri Mkuu kwa mujibu wa Katiba ndiyo mwenye udhibiti na usimamiaji wa ujumla wa shughuli za Serikali. Nina mambo manne kama nitapata muda wa kutosha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza ambalo nataka kulizungumzia ni hali ya uchumi. Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri Mkuu anaonesha kwamba hali ya uchumi ni nzuri, mfumuko wa bei uko chini asilimia 5.2 lakini jana tu NBS wametoa taarifa mpya ya mfumuko wa bei ambao
umepanda kwa kasi sana. Sasa hivi hali ya wananchi kwa kweli ni ya kupoteza matumaini, bei za vyakula zimepanda, sukari imefika mpaka shilingi 2,500 kwa kilo, maharage yamefika mpaka shilingi 3,000 kwa kilo, u nga kuna maeneo ya nchi umefika mpaka shilingi 2,200 kwa kilo. Kwa hiyo, kuna haja ya kuweza kuangalia taarifa ambazo Wizara zinapeleka Ofisi ya Waziri Mkuu kwa sababu inaonesha kwamba taarifa
ambazo Waziri Mkuu amezitoa katika ibara ya 20 ya hotuba yake ni outdated, siyo taarifa za sasa hivi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, Waziri Mkuu katika ibara ya 26 ya hotuba yake ameongelea ajira na kusema kwamba tumeingiza ajira mpya 418,000 lakini naomba ifahamike kwamba kwa mwaka Tanzania watu wanaoingia kwenye soko la ajira ni milioni 1.6. Kwa hiyo, kuingiza watu 418,000 maana yake ni kwamba kuna zaidi ya watu milioni 1.2 ambao hawajapata ajira na wako nje ya shughuli za kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini hata hivyo kuna ajira zimepotea. Ndani ya Manispaa yako Mwenyekiti, Manispaa ya Ilala jumla ya biashara 2,900 zimefungwa. Maana yake ni kwamba leo Ilala hamuwezi kupata service levy, leo Ilala hamuwezi kupata leseni za biashara, kwa sababu biashara zimefungwa kulingana na sera za Serikali ambazo siyo rafiki kwa watu kuweza kufanya biashara inavyotakiwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia matamko kwa mfano ya viongozi yanasababisha upotevu mkubwa wa mapato.
Mimi nafahamu na natambua juhudi ambazo Rais anazifanya, anataka tukusanye mapato zaidi kwenye madini, lakini Rais hafahamu na wasaidizi wa Rais pia hawafahamu kwamba tamko lake alilolitoa Mkuranga kuhusiana na mchanga limepoteza mapato ya Serikali kuliko mapato yoyote ambayo tungeweza kuyakusanya kwa miaka 20 iliyopita na nitawapa takwimu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kati ya mwaka 1998 tulipoanza uchimbaji mkubwa wa dhahabu mpaka mwaka 2016 tumeuza nje dhahabu ya Dola za Kimarekani bilioni 18 na makusanyo yetu kwa miaka yote hiyo ya kodi ni dola za Kimarekani milioni 833. Tamko alilotoa Rais Mkuranga, kwa sababu kulikuwa na mazungumzo ya kuuza Kampuni ya Acacia ambayo ingeingiza mapato mengi sana Serikalini kupitia capital gain tax ambapo tulipitisha sheria hapa, tumepoteza Dola za Kimarekani milioni mia nane themanini na nane.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Rais anazungumza kukusanya mapato, Rais huyu huyu anaipotezea nchi mapato. Haya ni mambo ambayo tunapaswa tuwe makini nayo sana na ningeomba viongozi hasa Mawaziri wajaribu kumshauri. Tunajua ana dhamira njema, lakini tuifanye kwa
namna ambayo haiathiri maslahi ya Taifa kama ambavyo imefanyika sasa hivi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo asubuhi hapa kulikuwa kuna mwongozo ambao umeombwa na Chief Whip wa Serikali ametoa maelekezo ambayo wewe umeyakubali.
Maelekezo ambayo Chief Whip ameyatoa na wewe umeyakubali hayaendani na Kanuni za Bunge. Suala la Mtanzania aliyepotea Ben Sanane, ni suala ambalo linapaswa kuchukuliwa kwa uzito wa hali ya juu sana, sio suala linalopaswa kuchukuliwa kisiasa. Sio suala linalopasa Wabunge wabebe uthibitisho waulete mezani kwako kwa sababu taarifa ambazo ziko sasa hivi na zipo Jeshi la Polisi zinaonesha kwamba Novemba 15, Ben Sanane kwenye mawasiliano yake ya simu kuanzia asubuhi alikuwa maeneo ya Tabata, akaenda maeneo ya Mikocheni, akatumia muda mwingi sana maeneo ya Mwenge, akapelekwa au akaenda Mburahati, saa nne usiku tarehe 15 Novemba, simu yake
ikapoteza mawasiliano na toka hapo hajawahi kuwa traced tena na haya maelezo yako polisi. Ukifuatilia Jeshi la Polisi wanakwambia sisi tumefikia mwisho, lakini mwelekeo wetu unaonesha kwamba waliomchukua Ben Sanane ni Usalama wa Taifa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wewe ume-save kwenye Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama na Mambo ya Nje, unafahamu sheria ya Usalama wa Taifa, kifungu cha 5(2) kinaipiga marufuku Usalama wa Taifa ku-enforce laws.
Usalama wa Taifa hawana mamlaka ya kukamata, hata wakimwona mwizi hivi, sheria inawakataza, kwa sababu ya kuepuka haya mambo ambayo tunayo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi kumekuwa na matukio hatuyapatii ufumbuzi. Ninyi mnafahamu na mnakumbuka aliyekuwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda, alikamatwa, akateswa, akaumizwa na leo jicho lake moja, halioni lakini mpaka leo hakuna hata
mtu mmoja aliyekamatwa kulingana na tukio kama hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa katika mazingira kama haya, hatuna namna na siyo kawaida ya Bunge hili ninyi wenyewe ni mashahidi ambao mmekaa Bungeni muda mrefu kujadili Usalama wa Taifa. Kwa mara ya kwanza tunaivuka hiyo taboo kwa sababu watu wamechoka. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kwa mujibu wa Kanuni ya 120 ya Bunge, natoa taarifa rasmi kwamba nitaleta Hoja Binafsi ndani ya Bunge ili Bunge liunde Kamati Teule ya kufanya uchunguzi wa matukio yote ya upoteaji, mauaji na matukio ambayo yanaweza kujenga taswira hasi dhidi ya Idara ya Usalama wa Taifa katika nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizikumbushe Kamati za Bunge, kuna masuala ambayo Kamati za Bunge hazipaswi kupelekewa na Spika, zinapaswa kufanya zenyewe, ndiyo maana Bunge lina utaratibu wa taarifa maalum.
Mimi ningetarajia Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama ingetuletea taarifa maalum kuhusu mambo haya badala ya kusubiri mpaka Wabunge wazungumze, tuanze kujianika na kama nilivyoeleza it was a taboo kuongelea Usalama wa Taifa ndani ya Bunge lakini leo tunaongelea kwa
sababu ya utendaji mbovu ambao unaendelea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nimetoa taarifa kwa mujibu wa Kanuni ya 120 ya kuunda Kamati Teule na ndiyo taarifa ambayo inapaswa kufanyiwa kazi kwa mujibu wa Kanuni. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, nataka nimkumbushe Mheshimiwa George anafahamu, ni rafiki yangu, ni ndugu yangu yaani ndugu kabisa, waliokwenda kuvamia Clouds Media ni Kikosi cha Ulinzi wa Rais na ninaweza kuthibitisha, aliyemtolea bastola Mbunge wa Mtama ni Afisa Usalama wa Taifa na ninaweza kuthibitisha. Kwa hiyo, kama Bunge linaweza likaunda chombo cha kutaka nikathibitishe hayo,
niko tayari kuthibitisha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimalizie, Mheshimiwa Waziri Mkuu ibara ya 31 ya hotuba yako imezungumzia kilimo na umezungumzia mavuno ambayo tumeyapata msimu uliopita wa 2014/2015. Naomba nikukumbushe Mheshimiwa Waziri Mkuu kwamba, taarifa ya
Benki Kuu ya Quarterly Economic Review inaonesha kwamba kilimo kimekua kwa asilimia 0.3 tu. Kwa hiyo, maana yake ni kwamba, wananchi wetu vijijini mwaka 2016, wengi wamekuwa maskini kwa sababu ya ukuaji mdogo katika sekta ya kilimo.
Mheshimiwa Mweyekiti, lakini Mheshimiwa Waziri Mkuu amezungumzia mbolea ambayo Serikali imenunua tani 30,000. Ni kazi nzuri sana mbolea imenunuliwa lakini naomba nikufahamishe katika kila mfuko wa mbolea ambao umenunuliwa kwa shilingi bilioni 10 Serikali ilizotoa, watu wako ama ni watendaji wa Wizara ya Kilimo au TFC wameongeza shilingi 15,000 kinyemela. Mnunuzi wa kawaida akinunua
mbolea Dar es Salaam ananunua kwa shilingi 55,000 mpaka ifike kwa mfano Rukwa, Kigoma au Katavi mbolea ile inauzwa kwa shilingi 60,000. Leo hii mbolea ambayo imenunuliwa kwa fedha za Serikali, kwa kampuni ya Serikali ikifika Sumbawanga, Mpanda, Kigoma ni shilingi 75,000.
Nakuomba Mheshimiwa Waziri Mkuu, jana nimekuona umechukua uamuzi katika mambo kama haya ya pembejeo, nakuomba umwagize CAG akague…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. Nimeweka pia kwa maandishi nitayaleta ili iweze kufanyiwa kazi kwa uzuri zaidi. Naomba Ofisi yako
imwagize CAG akague manunuzi ya mbolea ya shilingi bilioni 10 yaliyofanywa na kusambazwa katika msimu huu na taarifa hiyo uweze kuifanyia kazi, kwa sababu kuna shilingi 15,000 zimeongezwa kwenye mbolea zote zilizonunuliwa ile ya DAP na ile nyingine ya kukuzia. Kwa hiyo, naomba jambo hilo uweze kuliangalia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa Mheshimiwa Waziri Mkuu ibara ya 17 ameongea maneno mazuri sana kwamba tufanye siasa na naomba nimnukuu, ni maneno mazuri sana, anasema; “Ninatoa rai kwa wadau wa siasa kote nchini kujenga utamaduni wa masikilizano na
kuendesha siasa za maendeleo badala ya siasa za malumbano; siasa za kuunganisha watu wetu badala ya kuwagawa; na siasa za uwajibikaji badala ya siasa za mazoea.”
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini Mheshimiwa Waziri Mkuu mmetufungia kufanya siasa. Tunafanyaje siasa za kuwaunganisha watu wakati hatufanyi mikutano ya hadhara? Tunafanyaje siasa za maendeleo wakati hatufanyi mikutano ya hadhara? Tunafanyaje siasa za uwajibikaji wakati hatufanyi mikutano ya hadhara na mnafahamu kabisa kwamba ni kinyume cha Katiba. Namwomba Mheshimiwa Waziri Mkuu kama Waziri ambaye unahusika na suala la vyama vya siasa umshauri Rais.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nitoe shukrani zangu za dhati kwa Mamlaka ya Bandari Tanzania kwa kuendelea kuamini katika maendeleo ya Mkoa wa Kigoma na hususan Mji wa Kigoma kwa kuwekeza katika upanuzi wa Bandari ya Kigoma na ujenzi wa Bandari ndogo za Kibirizi na Ujiji. Pia nawashukuru sana kwa kumaliza kazi Bandari ya Kagunga baada ya kuhangaika nayo kwa muda mrefu sana tangu mwaka 2009.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeona zabuni za Bandari ya Kigoma - Ofisi ya Mkoa na pia taarifa ya kazi ya upembuzi yakinifu kwa upanuzi wa Bandari ya Kigoma. Nimeona zabuni ya Bandari ndogo ya Kibirizi na naamini kuwa zabuni kwa ajili ya Ujiji itakuwa imetoka ili kuwezesha gati kujengwa eneo la Ujiji na kuwezesha ndoto yetu ya kurejesha hadhi ya Ujiji katika maendeleo ya nchi yetu. Miradi hii itaingiza fedha kwenye mzunguko wa uchumi wa mji wetu, kutoa ajira kwa wananchi wetu na kupanua shughuli za uchumi za Manispaa ya Kigoma-Ujiji. Nampongeza Mkurugenzi Mkuu wa TPA kwa kuendeleza miradi hii na hii ni ishara ya imani yake kwa ukuaji na maendeleo ya mji wetu na Mkoa wetu wa Kigoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile napenda kumpongeza Meneja wa TANROADS wa Mkoa wa Kigoma kwa juhudi kubwa za kutekeleza miradi ya barabara katika mkoa wetu licha ya changamoto kubwa za fedha. Ujenzi wa mzunguko wa Mwanga Sokoni, taa za barabarani za umeme wa jua kuelekea njia panda ya Mwandiga na kuanza kuandaa zabuni kwa ajili ya barabara ya Bangwe – Ujiji ni juhudi ambazo zinatuunga mkono katika juhudi zetu za kufanya mabadiliko makubwa katika Mji wa Kigoma Ujiji. Namwomba Waziri wa Ujenzi ahakikishe kuwa barabara ya Kasulu katika Manispaa ya Kigoma-Ujiji ambayo inaunganisha Mji wa Ujiji na barabara kuu ya Kigoma - Nyakanazi, inajengwa sasa katika orodha ya ahadi za Rais. Barabara hii yenye urefu wa kilometa 7.5 ni barabara ya kimkakati kwani itaongeza barabara mbadala ya kuingia Kigoma badala ya sasa ambapo kuna njia moja tu ambayo ni hatari kiulinzi na usalama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na shukrani hizo hapo juu bado watu wa Kigoma wanalia na barabara yao kuu inayounganisha mkoa kuanzia Nyakanazi mkoani Kagera mpaka Kigoma Mjini. Eneo la barabara kuanzia Manyovu – Kasulu - Kibondo halina mradi wa ujenzi kwani bado mapitio ya usanifu yanafanywa. Kigoma ni mkoa pekee nchini ambao bado haujaunganishwa na mikoa mingine kwa barabara ya lami moja kwa moja bila maeneo ya vumbi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, natambua kuwa barabara ya Kigoma – Tabora - Singida (Manyoni) – Dodoma sehemu zake muhimu zote sasa zina fedha za wafadhili ikiwemo Nyahua – Chaya – Urambo - Kaliua na Uvinza - Malagarasi lakini kuna kilomita 41 kati ya Kazilambwa (Tabora) na Chagu mkoani Kigoma hazina fedha wala mradi. Serikali itazame upya vipaumbele vyake kwani haitakuwa na maana mtu asafiri kwa lami kutoka Kigoma - Dar es Salaam lakini kuwe na kilometa 41 vumbi. Serikali itafute fedha mahali kwingine na kuongeza kipande hiki katika miradi ya kuunganisha Mikoa ya Kigoma na Tabora na Mashariki mwa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, juhudi za ujenzi wa reli ya kati ni za kimaendeleo na hazina budi kupongezwa na kila mpenda maendeleo. Reli ina faida kubwa kwa nchi na kiongozi yeyote anayefanya maamuzi muhimu kama haya hana budi kupongezwa kwa dhati. Hata hivyo, Serikali ni lazima ifungue masikio kusikiliza maoni mbadala katika utekelezaji wa miradi mikubwa kama hii ambayo inatumia fedha nyingi na tumeamua kutumia fedha za ndani. Uamuzi wa kutumia fedha za ndani ni uamuzi mchungu kwani maana yake badala ya kuwekeza kwenye miradi ya kilimo ili kuongeza uzalishaji wa chakula na bidhaa za kuuza nje, tumeamua kujenga reli. Badala ya kuongeza vyuo vikuu na vyuo vya ufundi ili kuongeza maarifa na wataalam katika nchi yetu tumeamua kujenga reli. Badala ya kuwekeza kwenye kumaliza kabisa tatizo la mtindio wa ubongo (stuntedness) ambalo ni tatizo kubwa sana kwa nchi yetu kwa sasa kwani Watanzania 34 katika 100 wametindiwa ubongo tumeamua kujenga reli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupanga ni kuchagua. Mmeamua kwa niaba yetu kutumia rasilimali fedha zetu kidogo kujenga reli (na kununua ndege) na haya mengine yasubiri kwanza. Uongozi ni uamuzi. Mmeamua, hatuna namna. Hata hivyo, tusikilizeni sisi wawakilishi wa wananchi, mawazo yetu ni kusaidia kupunguza maumivu ya maamuzi yenu bila kuathiri utekelezaji wa miradi husika. Mimi binafsi naunga mkono uwekezaji kwenye reli lakini siungi mkono namna uwekezaji huu unavyofanywa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikiwa mwaka wa tatu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nilichagua kusoma kozi elective iitwayo Transport Economics lakini nilipoingia darasani chini ya Dkt. Natu Mwamba tulijikuta watatu tu darasani. Hatukutosha na kozi ile haikutolewa mwaka ule. Nilichagua kozi ile kwanza kwa sababu ya mwalimu aliyekuwa anafundisha hiyo kozi, wanafunzi tulimpenda sana. Pili, nimelelewa kwenye uchumi wa usafiri, Mji wa Kigoma (bandari, reli na mipaka ya Kongo na Burundi).

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kukosa kozi ile ikabidi nisome mwenyewe na mtu aliyebadilisha kabisa mwono wangu anaitwa Ndugu Ali Karavina, alikuwa Mbunge wa Urambo. Ndugu Karavina na wenzake waliandika kuhusu ‘Uchumi wa Jiografia’ ukijikita kwenye faida za ujenzi wa reli ya kati. Reli ya kati ni reli kutoka Dar es Salaam (bandarini) mpaka Kigoma (bandarini) na Tabora - Mwanza, Ruvu - Tanga na Kaliua - Mpanda ni matawi ya reli ya kati sio reli ya kati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika andiko lao ‘Uchumi wa Jiografia Tanzania‘, Ndugu Ali Karavina na wenzake walishauri reli ya kati kwa kigezo cha takwimu za mizigo na ndio maana walisema kwanza ijengwe Dar es Salaam - Kigoma kabla ya popote kutokana na mapato yatakayotokana na eneo hilo, ndio matawi yajengwe. Leo kwa mshangao mkubwa Serikali ya Awamu ya Tano imekuja na tafsiri yake ya reli ya kati kwamba ni Dar es Salaam – Isaka - Mwanza. Mimi ni Mtanzania, sina tatizo kabisa na Mwanza kwani siku ikifika nitataka kura za watu wa Mwanza lakini mimi ni mzalendo nataka kuona kuwa maamuzi ya kutumia rasilimali za nchi yanakuwa na faida kwa nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tutumie shehena za mizigo inayopita Bandari ya Dar es Salaam kujenga hoja kwamba Serikali imekengeuka na kufanya maamuzi ama kwa faida za kisiasa, maslahi ya kikanda au urafiki tu wa viongozi na kupiga teke maamuzi kwa vigezo vya faida za kiuchumi. Mwaka 2015/2016, Bandari ya Dar es Salaam ilipitisha mizigo jumla ya tani milioni tano kwenda nchi tunazopakana nazo. Katika mizigo hii, 34% ya mizigo ilikuwa ya Zambia, 34% ya DRC, 12% Rwanda, 6% Burundi na 2.6% Uganda. Lango la mizigo ya DRC na Burundi ni Bandari ya Kigoma (kimsingi kama reli inafanya kazi). Hivyo, Bandari ya Kigoma inaweza kupitisha 40% ya mizigo yote inayopita Bandari ya Dar es Salaam kwenda nchi jirani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lango la mizigo ya Uganda na Rwanda yaweza kuwa Isaka na Mwanza ambayo ni takribani 15% ya mizigo yote kutoka Bandari ya Dar es Salaam. Ikumbukwe kuwa hiyo mizigo ya Rwanda na Uganda ina ushindani wa bandari ya Mombasa (ambapo wanajenga reli kwenda huko) ilhali mizigo ya Kongo DRC na Burundi haina ushindani huo na hakuna reli wala mradi wa reli unaojengwa. Sasa, Serikali itueleze sayansi gani ya uchumi waliyotumia kutumia mabillioni ya fedha za ndani kupeleka reli mahali penye mzigo wa 15% ya mizigo yote na kuacha mahali penye mzigo wa 40% ya mizigo yote?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaweza kujenga hoja kuwa Bandari ya Mwanza itakua lakini ukitazama takwimu za reli utaona kuwa bandari inayokua kwa kasi hivi sasa kwa idadi ya mizigo inayohudumia ni Bandari ya Kigoma. Mwaka 2015/2016, Bandari ya Kigoma ilikua kwa 12% wakati Bandari ya Mwanza ilikua kwa -41.3%. Hizi sio takwimu zangu, ni takwimu za taarifa hali ya uchumi inayotolewa na Serikali yenyewe. Mkurugenzi wa Bandari (TPA), Mhandisi Kakoko ana ushuhuda wa juzi tu msafirishaji Azam Dewji kapata kazi ya kupeleka Kongo DRC tani 120,000 ya udongo ulaya (saruji) kwa mwaka na mzigo huu utapita Bandari ya Kigoma kwa urahisi na wepesi wa kufikisha eneo la mteja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi, Serikali inatumia nini kufanya maamuzi? Ujasiri wa kutopeleka SGR Kigoma kwanza kwa ajili ya faida za kiuchumi unatokana na nini? Serikali inajua nini ambacho sisi wengine hatujui? Njia sahihi yenye faida kwa nchi kwa reli ya kati ni Kigoma-Dar es Salaam na tawi la Uvinza Msongati, Burundi ili kwenda kubeba mzigo wa madini ya Nikeli. Awamu za Serikali hazina mashiko kiuchumi na ni lazima kubadilisha njia na kupeleka reli mahali penye mzigo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili kwenye reli ni hatua za ujenzi. Hivi sasa kazi ya Dar es Salaam-Morogoro imeanza, kilometa 205 kwa thamani ya dola za Marekani bilioni 1.2 (shilingi trilion 2.5). Kipande hiki cha reli kitabeba nini kutoka Morogoro kwenda Dar es Salaam na Dar es Salaam kwenda Morogoro? Mwaka 2016/2017 tumepanga bajeti ya shilingi trilioni moja lakini mwaka 2017/2018 tunapanga shilingi bilioni 900. Hivyo itachukua bajeti tatu kujenga kipande cha reli kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro cha kilometa 205. Hii reli itafika lini huko mtakapotaka ifike na muda huo uwe na uvumilivu wa kiuchumi? Serikali haioni kwamba ingekuwa na faida zaidi kama reli hii awamu hii ingefika Makutupora Dodoma, kilometa 500 halafu TPA wakajenga dry port hapo ili reli ianze kuzalisha mapato kwa kusafirisha mizigo mpaka Dodoma? Rwanda, Uganda, Burundi na DRC wachukulie mizigo yao Dodoma. Najua swali litakuwa ni fedha za kufika Dodoma. Ni lazima Serikali ianze kufikiria nje ya boksi la fedha za ndani na mikopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ya Ethiopia ilijenga bwawa la kuzalisha umeme 10,000 MW. Benki ya Dunia walikataa kuwapa fedha na China walikataa kuwapa fedha. Serikali ya Ethiopia ikawaambia wananchi wake wajenge kwa kuuza bond kwa wananchi na hasa wananchi wao waishio nje ya nchi hiyo (Diaspora). Serikali iuze railways bond kwa wananchi wa ndani na nje ili ku-finance kipande cha Morogoro – Makutupora sasa hivi. Serikali ilete Muswada Bungeni wa kuiweka bond hiyo kisheria kwa miaka 15 na kupanga/kutenga fedha kwenye bajeti kulipia riba ya bond hiyo mpaka iive ambapo tayari uchumi utakuwa umekua na kumudu malipo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali iwafanye Watanzania washiriki katika ndoto yake ya kujenga reli kwa njia hii. Tufikishe reli hii Dodoma na kuwepo na dry port Dodoma kwanza ndiyo tutaweza kupunguza gharama na kuanza kupata mapato kutoka katika mradi, mapato ambayo yataanza kulipia madeni au kulipa ujenzi wa kuelekea Tabora na Kigoma na baadaye Mwanza, Uvinza, Musongati na Kaliua na Mpanda. Hayo ndiyo mawazo yangu, mnaweza kuyachukua ama kuyaacha, lakini nashukuru Mungu nimesema na watoto wetu watakuja kufukua historia na kutuhukumu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho kwenye reli ni uchumi kufaidika wakati wa ujenzi. Miradi mikubwa kama hii huwa ina mikataba inaitwa Offsets Agreeements. Hizi offsets hutumika kwenye miradi mikubwa ya kijeshi na miradi ya kiraia. Tusirudie makosa ya Bomba la Gesi la Mtwara ambapo kila kitu kilitoka China. Serikali izungumze na wakandarasi ili vitu ambavyo vinaweza kutengenezwa hapa nchini viwanda vianzishe kutengeneza vitu hivyo, lazima tutumie miradi hii kutekeleza ajenda yetu ya viwanda. Serikali inaweza kutuambia viwanda vingapi vya ugavi kwenye bidhaa za ujenzi wa reli vitajengwa? Nashauri hili lifanyike kama halijafanyika. Haya ndio mambo ya local content na Serikali lazima kila mwaka ituambie ni makampuni mangapi ya Watanzania yamefaidika na ujenzi wa reli na kwa kufanya kazi gani. Wajerumani walibebesha babu zetu mataruma ya reli, Waturuki walibebesha watu wetu ujuzi na fedha tunayolipa sehemu ibakie humu nchini kukuza uchumi wa nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho ni hili la ndege. Leo nimetua uwanja wa ndege wa Dodoma nikitokea Jimboni Kigoma kwa kutumia ndege za ATCL. Hii ni hatua ya maendeleo kwa sababu sikuweza kufanya hivi mwaka jana tu. Ningeendesha zaidi kilomita 800 na kufika nimechoka. Hatua hii siyo ya kubeza bali ya kuungwa mkono. Hata hivyo, suala la manunuzi ya ndege za ATCL linahitaji uwazi mkubwa kutoka Serikalini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka jana tumetenga fedha za ndani shilingi bilioni 500 kununua ndege na mwaka huu pia kiasi kama hicho. Tumeambiwa kuwa tayari tumelipa 30% ya dola za Marekani milioni 224 kununua Boeng 787 -8 Dreamliner. Jumla ya fedha za ndege kwa miaka miwili ni trilioni moja. Ni maamuzi, hatuna chakula Ghala la Taifa tunanunua ndege. Watoto wanakosa mikopo ya elimu ya juu, tunanunua ndege. Ni maamuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna habari kuwa ndege tuliyonunua ni sehemu ya ndege za Boeng zilizokataliwa na mashirika mengine duniani kwa sababu ya ubora wake. Ndege hizi zinaitwa Terrible Teens Dreamliner ambazo zilikuwa 12 na zilikosa soko kwa sababu ni nzito na hazina viwango. Wenzetu Ethiopia wamenunua pia ndege hizi lakini kwa punguzo kubwa la bei kwa sababu ndege hazikuwa na soko. Hata hivyo, katika tovuti ya Boeng, Bwana Van Rex Gallard, Vice President, Latin America, Africa & Caribbean Sales, Boeing Commercial Airplanes(http://www.boeing.com/commercial/ customers/air-tanzania/air-Tanzania-787-oder. page) amesema kuwa tumenunua ndege hizi kwa USD milioni 224. Naomba maelezo ya Serikali kuhusu suala hili ili Watanzania wajue kama fedha zao zinatumika vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha na naomba kupata majibu sahihi kuhusu masuala niliyoeleza.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. KABWE R. Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza napenda kuongelea kuhusu kufungamanisha viwanda na kilimo. Kufunganisha viwanda na kilimo kungeepusha uhaba wa bei kubwa ya sukari nchini. Serikali ingesikiliza ushauri mwaka 2016, nchi isingesumbuka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo kwa mara ya tatu tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani Bunge linajadili na baadae kuidhinisha fedha kwa ajili ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa mwaka 2018/2019.

Kwa Serikali ya Awamu ya Tano, Wizara hii ndiyo Wizara mama inayotoa taswira ya kufeli au kufaulu kwa Serikali hii. Maana ahadi ya msingi ya Serikali hii kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ilikuwa ni kuwa itajikita kujenga Tanzania ya viwanda huku lengo kuu likielezwa kuwa ni kuiwezesha Tanzania kuwa na uchumi wa kati unaongozwa na viwanda ifikapo mwaka 2025. Bunge tunao wajibu wa kuhakikisha tunasaidia Serikali ili itimize ahadi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, azma hiyo ya nchi yetu kuwa nchi ya viwanda ni njema na ni yetu sote, kwa nafasi zetu tunasaidia kuifikia azma hiyo. Tulipitisha hapa Bungeni Mpango wa Pili wa Miaka Mitano wa Maendeleo wa Serikali (FYDP2), kwa miaka ya 2016/2017 - 2020/2021 na kwa hiyo ni mpango wa nchi. Hivyo sote kwa pamoja tunafanya kazi ya kuhakikisha tunafikia malengo ya mpango husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi wa upande wa upinzani tuna dhima kubwa zaidi ya Wabunge kutoka Chama Tawala. Tunao wajibu wa kukosoa pale ambapo tunaona walio kwenye Serikali wanakosea, kupendekeza sera bora zaidi za kutumia ili kufikia lengo (Tanzania ya viwanda) na kushauri mbinu nzuri zaidi za utekelezaji wa sera hizo. Naomba nitumie nafasi hii kukumbusha Bunge kuwa sisi upinzani tulitimiza wajibu wetu, ni hivyo tu Serikali haikusikiliza ushauri wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maana mengi ya matatizo ya karibuni ya Wizara hii, hasa kwenye suala la uhaba na bei kubwa ya bidhaa za mafuta ya kula na sukari, si mapya, ni zao la uongozi mbovu wa CCM. Serikali ya Awamu ya Tano imerithi, imeendeleza na pia imezalisha zaidi matatizo ya uhaba na bei kubwa ya sukari na mafuta ya kula.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2016 wakati wa bajeti ya Wizara ya 2016/2017 Wabunge wa Upinzani tulishauri njia za kutatua matatizo hayo. Ushauri wetu haukusikilizwa, tunakumbusha tena leo ili Serikali itatue matatizo ambayo ilipaswa iyatatue mwaka 2016. Mchango wangu wa bajeti ya mwaka 2016/2017 ulijikita kwenye kuishauri Serikali juu ya umuhimu wa kufungamanisha sekta ya viwanda pamoja na kilimo ili kuongeza thamani ya mazao ya wakulima wetu na kuhakikisha kuwa aina ya viwanda vyetu tunavyovianzisha nchini ni vile ambavyo vitategemea kwa kiasi kikubwa malighafi kutoka ndani ya nchi yetu hasa bidhaa za kilimo, ikiwemo sukari na mafuta ya kula.

Mheshimiwa Mwenyekiti, msingi wa tatizo la sukari nchini, ukurasa wa 140 wa hotuba ya bajeti ya Wizara ya Viwanda ya 2016/2017 unaeleza malengo ya Serikali kwenye sekta hii ya viwanda. Mambo tisa ya msingi yalipaswa kutekelezwa na Serikali ili kufikia azma ya kuwa na viwanda na katika mambo hayo tisa, hakukuwa na mpango mkakati wa kufungamanisha uzalishaji viwanda na bidhaa za kilimo zenye soko zaidi nchini (sukari na mafuta ya kula).

Mheshimiwa Mwenyekiti, kurasa za 25 na 44 za hotuba ya bajeti ya Wizara ya Kilimo na Uvuvi kwa mwaka 2016/2017 zinaeleza juu ya mikakati ya kukabiliana na uhaba wa sukari nchini. Kiambatisho namba sita cha hotuba hiyo kilieleza kwa kina changamoto nzima ya sukari na miradi inayopaswa kutekelezwa ili kumaliza kabisa suala la uhaba na kupanda kwa bei ya sukari nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimejumlisha miradi ile kutoka kila kona ya nchi na nimekuta ni takribani hekta 300,000 za kulima miwa. Kwa hesabu ya chini ya wastani wa kuzalisha sukari kwa kila hekta, miradi ile kama ingetekelezwa Tanzania ingeweza kuzalisha tani milioni 1.5 za sukari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiondoa sukari ya kutumia nchini, ziada ambayo ingeuzwa nje ingeweza kuliingizia Taifa fedha za kigeni USD milioni 500, sawa na asilimia 30 ya malengo ya mpango wa maendeleo kwa sekta ya viwanda wa kupata mapato ya fedha za kigeni kiasi cha USD bilioni tatu. Hapo ni bila kutazama kiwango cha ajira zitakazozalishwa, ukuaji wa biashara kwenye sekta nyingine, umeme na kadhalika (multiplier effect).

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa bajeti ile ya mwaka 2016/2017 hakukuwa kabisa na mafungamanisho kati ya ulimaji wa hekta hizo 300,000 za miwa na uzalishaji wa tani milioni 1.5 za sukari. Maana Wizara ya Viwanda na Biashara hata haikujua juu ya mkakati huo wa kupunguza uhaba wa sukari wa Wizara ya Kilimo. Wizara mbili zilizo ndani ya Serikali moja hazikuwa zikisomana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulishauri mambo matatu kama ifuatavyo:-

(i) Bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Kilimo kwa mwaka 2016/2017 iondolewe na ikapitiwe upya ili isomane na bajeti ya Wizara ya Kilimo ya mwaka husika. Tuliomba Wizara mbili ziwianishe na kuoanisha mipango yao kwa lengo la kuratibu ulimaji wa miwa na uanzishaji wa viwanda vya sukari vya kutumia miwa ile.

Serikali haikusikiliza, Rais akatoa tu matamko ya zuio la sukari kutoka nje wakati hakukuwa na mpango wa Taifa wa namna ya kufidia nakisi ya sukari itokanayo na uzalishaji mdogo wa bidhaa hiyo nchini. Matamko ya zuio ya Rais yaliishia kuleta uhaba wa sukari na kupandisha bei kutoka shilingi 1,800 mpaka shilingi 6,000 katika maeneo mbalimbali nchini na tangu hapo bei ya sukari haijashuka tena, imebaki kuwa shilingi 3,000 kwa kilo.

(ii) Kwenye sukari kuna suala la low hanging fruits, kila mwaka miwa yenye uwezo wa kuzalisha tani 50,000 ya sukari huoza huko Kilombero na Mtibwa. Mkoani Morogoro wakulima wanalima miwa mingi zaidi kuliko uwezo wa viwanda kununua, miwa hii inaishia kuoza tu bila kutumika. Bodi ya Sukari ilipaswa kutoa leseni ili vikundi vya wakulima au wawekezaji wadogo wazalishe sukari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hadi leo Bodi ya Sukari nchini haijatoa leseni kwa viwanda vidogo vya uzalishaji sukari nchini na wala Serikali haijahamasisha Watanzania kuwekeza kwenye viwanda vidogo vya sukari ili kuwezesha miwa yote inayozalishwa nchini itumike kutoa sukari. Kama jambo hili lingefanyika, tungeweza kupunguza nakisi ya sukari nchini kwa zaidi ya tani 50,000.

(iii) Uwekezaji wa bidhaa kama sukari unahitaji vivutio vya punguzo la kodi kutoka Serikalini. Kule Uganda, Rais Museveni tangu aingie madarakani aliweka vivutio maalum kwa viwanda kama Kakira Sugar ili wazalishe sukari ya kutosha. Viwanda vya sukari Uganda hata umeme hulipiwa na Serikali kwa asilimia 50 ili kupunguza gharama za uzalishaji na kuvilinda dhidi na ushindani wa sukari kutoka nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpaka leo Serikali haijaona kuwa vivutio (subsidies) kwa ajili ya kupunguza gharama za uzalishaji ili kuwezesha kuzalisha sukari, kutengeneza ajira na kupata faida ni jambo la lazima. Sisi Kigoma mwaka 2016 kuna mwekezaji alitaka kuzalisha sukari tani milioni moja kwa mwaka kwa kulima miwa Kasulu, Wizara ya Fedha pamoja na Wizara ya Viwanda walibishana kuhusu vivutio (kama wanavyobishana sasa juu ya mafuta ya kula), leo mradi ule wa uwekezaji umekufa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utafiti uliofanywa na Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) kwa kutumia Kampuni ya LMC International, ulibaini mahitaji ya sukari kwa mwaka 2016/2017 ni wastani wa tani 590,000 ambapo kati ya hizo, tani 455,000 ni kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na tani 135,000 kwa matumizi ya viwandani. Leo mwaka 2018 nakisi hiyo ya mahitaji ya sukari imekua zaidi, bei ya sukari iko juu zaidi ya shilingi 1,800 iliyokuwepo mwaka 2016 kabla ya Serikali kuweka zuio la kuagiza nje sukari bila kwanza kuwa na mpango wa kuondoa nakisi iliyopo, sasa bei ni wastani wa shilingi 3,000 nchi nzima. Serikali ingetusikiliza mwaka 2016 leo tusingekuwa hapa tulipo, hata miradi inayopangwa sasa kupunguza nakisi, kama ya Mkulazi, ingeanza mapema zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili, thamani ya fedha tunazotumia kuagiza mafuta ya kula kutoka nje ni zaidi ya bajeti ya Wizara ya Maji ya mwaka 2018/2019. Serikali ingekubali ushauri wa mwaka 2016 wa kufungamanisha sekta ya viwanda na kilimo isingesumbuliwa mwaka 2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili nchi iendelee, maendeleo ya viwanda yanapaswa kufungamanishwa na sekta nyingine za uchumi kwa sababu kuna kutegemeana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa Tanzania ili tuendelee ni lazima kufungamanisha shughuli za uchumi zinazohusisha wananchi wengi zaidi na sekta ya viwanda ili huo uchumi wa viwanda uwe na tija kwa watu. Sekta ya kilimo kwa ujumla ikihusisha uvuvi na ufugaji huhusisha asilimia 75 ya Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sekta za viwanda na kilimo kwa pamoja zinachangia nusu ya Pato la Taifa (GDP) na nusu nyingine ni sekta ya huduma. Nadharia za uchumi zinatuambia kuwa tija ikiongezeka kwenye sekta ya kilimo, inawezesha sekta ya viwanda kukua na kisha sekta ya huduma. Hapa Tanzania na nchi nyingine za Afrika, sekta ya huduma iliruka hatua hizi za ukuaji, hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa zaidi kwenye GDP kuliko kilimo au viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana tunaambiwa uchumi unakua lakini umaskini wa wananchi haupungui, ni kwa sababu ya huduma haiajiri watu wengi kama sekta ya kilimo na hivyo uchumi unaokuzwa na sekta ya huduma hauajiri watu wengi kama sekta ya kilimo na hivyo uchumi unaokuzwa na sekta ya huduma ni nadra kuondoa umaskini. Sekta za kuondoa umaskini ni kilimo na viwanda maana zinaajiri watu wengi zaidi. Hivyo ili tuendelee ni lazima kufungamanisha viwanda tunavyotaka kuvijenga na kilimo chetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ya Awamu ya Tano tuliieleza haya wakati wa mwaka wa fedha wa 2016/2017, mwaka wake wa kwanza wa bajeti lakini ikashindwa kusikiliza ushauri wetu. Hivyo kushindwa kufungamanisha kilimo chetu na viwanda tunavyotaka kujenga hasa vya bidhaa tunazozitumia zaidi kama mafuta ya kula, bidhaa ambayo ina mahitaji makubwa na sasa bei yake imepanda toka shilingi 55,000 mpaka shilingi 70,000 kwa ndoo ya lita 20 kutokana na masuala yanayohusu uingizwaji wake kutoka nje ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, msingi wa tatizo la mafuta ya kula nchini na utatuzi wake; suala la mafuta halina tofauti na suala la sukari, ukipanda gari ukapita njia ya Singida unaona wananchi wamepanga madumu ya mafuta ya alizeti wanauza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwetu Kigoma sisi ndio wazalishaji wakuu wa mafuta ya mawese nchini, lakini bado bei ni haba, uzalishaji wenyewe ni duni na hautoshelezi hata soko la ndani. Kimsingi tarehe 17 Mei, 2016 wakati wa kusomwa kwa bajeti ya Wizara hii kulikuwa na matatizo matatu makuu kwenye sekta ya mafuta ya kula nchini na niliyaeleza katika mchango wangu kama ifuatavyo:-

(i) Suala la unafuu mkubwa wa kodi kwa mafuta yanayoingizwa kutoka nje ambao Serikali iliutoa kwa waagizaji nchini. Unafuu huo ulivunja hamasa ya uwekezaji wa viwanda vya kuzalisha mafuta ya kula ndani ya nchi. Mazingira ya unafuu ule wa kodi yaliwafanya wafanyabiashara waone ni nafuu na kazi rahisi zaidi kuagiza mafuta nje kuliko kuzalisha ndani. Jambo hili la unafuu wa kodi kwa waagizaji wa mafuta ya kula kutoka nje likaua ushindani wa bei na viwanda vya ndani vikashindwa kushindana kwenye soko na hivyo kupunguza uzalishaji, jambo lililoifanya nguvukazi ya wananchi wanaolima mawese na alizeti (mazao makuu ya kuzalishia mafuta nchini) kupotea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati ule wa bajeti ya mwaka 2016/2017 tuliishauri Serikali iondoe unafuu huu wa kodi inaoutoa kwa waagizaji wa mafuta ya kula kutoka nje ya nchi ili kulinda na kunusuru viwanda vyetu vya ndani na tuchochee uzalishaji zaidi wa ndani wa mafuta ya kula, jambo ambalo lingechangia ukuaji wa kilimo cha mawese na alizeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mwaka 2016/2017 kodi kwenye mafuta ya kula kutoka nje ni 10% (imports duty) na 18% VAT tu. Tukashauri jambo hili libadilike. Mwaka huu ndiyo Serikali imekubali kubadili ushauri wetu wa kuondoa unafuu wa kodi kwa waagizaji wa mafuta ya kula kutoka nje baada ya kuwa tumepoteza zaidi ya mwaka mmoja na nusu wa kuviathiri viwanda vyetu vya ndani.

(ii) Kama ilivyo kwenye sukari, tuna nakisi kwenye uzalishaji wa ndani wa mafuta ya kula. Mwaka jana uzalishaji wa ndani wa mafuta ya kula ulikuwa ni tani 180,000 tu wakati mahitaji yalikadiriwa kuwa ni tani 400,000 mpaka tani 520,000 kwa mwaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uwezo wa uzalishaji ndani ukiwa ni asilimia 30 ya mahitaji na uagizaji wa mafuta ya kula kutoka nje ukiwa ni asilimia 70; pia asilimia 55 ya mahitaji ya mafuta ya kula nchini ni mafuta ya mawese (palm oil) yanayoagizwa kutoka nje ya nchi. Inakadiriwa kuwa mafuta ya alizeti yanayozalishwa yanatosheleza mahitaji ya ndani kwa asilimia 40 tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto kubwa katika uzalishaji wa mafuta ya alizeti na mawese nchini inatokana na upungufu wa mbegu zenye ubora stahiki wa kutoa mafuta kwa wingi. Pia uwepo wa viwanda vichache vya kuzalisha mafuta yatokanayo na mazao hayo. Hivyo fursa ya kuwafanya wakulima wetu kuzalisha zaidi na kuziba nakisi hii kukosekana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulishauri kuwa Serikali inapaswa kuwekeza kwenye uzalishaji wa ndani wa mafuta ya kula kwa kuhamasisha kulimwa zaidi kwa mazao yanayozalisha mafuta ya kula (pamba, karanga, alizeti na mawese) pamoja na kufungamanisha uzalishaji zaidi wa mazao hayo na sekta ya viwanda kwa kuweka unafuu wa kodi kwenye uagizaji wa mashine za kukamulia mafuta ya kula.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna hamasa ndogo ya Serikali kwa wakulima wawekezaji wa viwanda. Serikali imeshindwa kufanyia kazi ushauri huu tangu mwaka 2016, katika wakati ambao mahitaji ya mafuta ya kula yanapanda nchini, bado uzalishaji wa ndani umebaki ulivyo.

(iii) Kwa lengo la kujazia nakisi ya uzalishaji wa ndani wa mafuta ya kula uliopo, nchi yetu inatumia sehemu kubwa ya akiba ya fedha za kigeni kuagiza mafuta ya kula kutoka nje ya nchi. Kwa wastani kwa mwaka tunatumia USD milioni 340 sawa na shilingi bilioni 782 zaidi ya bajeti yote ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa mwaka 2018/2019 ambayo ni shilingi bilioni 727.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Kigoma ni miongoni mwa mikoa maskini zaidi nchini. Shilingi bilioni 782 tunazopeleka Malaysia kununua mafuta ya mawese kwa ajili ya kujazia nakisi yetu ya ndani zingeweza kabisa kufuta umaskini wa Kigoma. Tuna mradi Kigoma wa kupanda michikichi ili kuzalisha mafuta ya mawese ulio chini ya Serikali ya Mkoa. Mpango wetu ni kila familia kupanda hekta moja ya michikichi, lengo ni kuzifikia familia 100,000.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uzalishaji wa familia hizo za Kigoma kwenye kilimo cha mawese unaweza kuondoa kabisa suala la Tanzania kuagiza mawese kutoka nje maana tutaweza kuzalisha tani 200,000 za crude palm oil (CPO) kwa mwaka, kuzalisha ajira nyingi, kupandisha hali ya maisha ya wananchi/wakulima na kukuza biashara nyingine. Uzalishaji ni ndani ya miaka miwili tu tangu upandaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zaidi biashara ya uzalishaji wa mafuta ya kula ni fursa kubwa kwa nchi yetu ambayo ingetumika vyema ingeweza kufuta umaskini wa wananchi wetu. Leo hii ninapozungumza hapa Bungeni bei ya lita moja ya mafuta ya alizeti/mawese ni shilingi 4,000 ikiwa imepanda kutoka shilingi 3,500 na ni bei kubwa kuliko bei ya lita ya petroli kwenye soko la dunia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kutimiza lengo hilo Kigoma wanahitaji watu watakaowekeza kwenye viwanda vya kuzalisha mawese. Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ishirikiane na uongozi wa Mkoa wa Kigoma kuhakikisha tunazalisha mafuta ya kula ya kutosha ili kuondokana na uagizaji huu. Mawese na alizeti ndiyo suluhisho la kudumu la suala la mafuta ya kula. Ni imani yetu kuwa sasa Serikali itabeba ushauri huu ili miaka miwili kutoka leo tusijikite kujadili tena suala hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la tatu ni kwamba vyuma vitazidi kukaza tukipuuza fungamanisho la miradi mikubwa na ujenzi wa viwanda nchini. Serikali ibebe ushauri wangu wa mwaka 2017.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kukumbushia ushauri wangu juu ya namna bora ya kupunguza nakisi na kupunguza bei ya bidhaa za mafuta ya kula na sukari nilioutoa wakati wa bajeti ya Wizara hii kwa mwaka 2016/2017 sasa naomba pia nikumbushie jambo la tatu muhimu nililoishauri Serikali kuhusu hali ya uchumi wa nchi yetu, juu ya sababu ya fedha kupungua nchini (vyuma kukaza) na namna ya kuitumia miradi mikubwa tunayoifanya nchini kuendeleza sekta ya viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili nililieleza kwa undani wakati wa bajeti ya Wizara hii ya mwaka 2017/2018. Serikali haikuchukua ushauri ule, kwa sababu ya umuhimu wake, naomba niikumbushe tena Serikali juu ya umuhimu wa kuifungamanisha sekta ya viwanda na ujenzi wa miradi mikubwa tunayoifanya nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imejipanga kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo kama vile barabara, ndege, madaraja, mabomba ya gesi, mafuta na kadhalika. Fedha nyingi za ndani na za wafadhili zimetengwa kwa ajili ya kuendeleza miradi hii. Nitajikita kwenye kurudia mfano nilioutoa mwaka jana juu ya mradi wa reli ya kati kwa kiwango cha SGR. Kwenye mradi huu wastani wa shilingi trilioni 17 zinahitajika kukamilisha ujenzi wake kati ya Dar es Salaam na Mwanza (kilometa 1,200).

Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa kilometa moja ya reli unahitaji chuma cha pua (steel) chenye ubora wa hali ya juu kiasi cha tani 40 mpaka 60. Sisi tunajenga kilometa 1,200 za reli kwa sasa hivi na baadae zitaongezeka kwa vipande vya Tabora - Kigoma, Kaliua - Mpanda - Karema, Uvinza - Musongati na miradi mingine kama Mtwara - Mbamba Bay, Ruvu - Tanga, Tanga – Musoma - Kigali na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo basi, Tanzania inahitaji siyo chini ya tani 500,000 za chuma cha pua (steel) katika kipindi cha miaka michache ijayo. Kwa mipango iliyopo sasa ni kwamba mataruma ya reli yataagizwa kutoka nje na kuletwa nchini na hivyo kuzalisha ajira huko kwenye nchi za nje ambazo mataruma hayo yatazalishwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, fedha za miradi hii zitakwenda nje ya nchi, kama ilivyo kwenye fedha za mafuta ya kula na sukari, Watanzania hawatafaidika kabisa. Je, Serikali imeweka mikakati ya kufungamanisha maendeleo ya viwanda na miradi hii? Je, kuna mipango shirikishi ya kuhakikisha utekelezaji wa miradi hii unawasaidia zaidi Watanzania?

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, sekta binafsi ya Tanzania kwa ushirikiano na Serikali imeandaliwa kuzalisha bidhaa na malighafi zinazotakiwa kwenye miradi hii? Hivi Serikali imeambatanisha faida, ajira, mapato ya kodi na mapato ya fedha za kigeni kwenye fungamanisho la miradi hii ya maendeleo na sekta yetu ya viwanda? Maswali haya niliyauliza mwaka 2017 hayakupata majibu, nayarudia hapa ili Serikali ichukue hatua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miradi mikubwa yote duniani ina mikataba ya ziada iitwayo Offsets Agreements. Offsets Agreements ni makubaliano maalum kati ya Serikali na mzabuni wa miradi (kwa mfano ubia kati ya kampuni ya Yapi Merkezi ya Uturuki na Kampuni ya Contrucao Africa SA ya Ureno ulioshinda zabuni kipande cha reli kati ya Dar es Salaam - Morogoro) makubaliano ambayo huweka msukumo maalum wa kisera na kisheria ili kuhakikisha watu wetu wanafaidika wakati wa ujenzi wa miradi mikubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, faida husika huwa ni kwa kushirikiana kwenye uzalishaji wa sehemu ya malighafi zitakazotumika wakati wa mradi na pili katika kuhakikisha kuwa sehemu ya utaalam uliotumika wakati wa ujenzi unaachwa nchini ili kuhakikisha tunawajengea uwezo Watanzania wa kufanya miradi ya namna hii siku za usoni (transfer of knowledge).

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu ina chuma kingi sana kule Mchuchuma na Liganga na pia tuna makaa ya mawe ya kuchenjua chuma hiki ili kupata chuma cha pua (steel). Mradi huu wa reli peke yake ungeweza kuchochea maendeleo makubwa kwenye sekta ndogo ya migodi na viwanda vya chuma. Tungekuwa na mipango thabiti, sisi Tanzania tungekuwa ndio wazalishaji wakubwa wa chuma nchini na hata uzalishaji wa chuma cha kujenga reli kwenye eneo la Mashariki mwa Afrika na Maziwa Makuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huu wa reli unaweza kufungamanishwa na sekta ya kilimo nchini kwa bidhaa za ngozi na mkonge kutumika katika utengenezaji wa vitanda na viti vya mabehewa ya treni. Sekta yetu ya ngozi pamoja na ile ya katani zingeweza kufaidika sana kwa mradi huu mmoja tu wa reli kwa kuhakikisha kuwa mapambo ya ndani ya mabehewa yanakuwa ya bidhaa za ngozi na viti vinakuwa vya bidhaa za katani. Hivi ndivyo namna nchi nyingine zimeweza kuchochea viwanda kwenye mnyororo wa thamani. Najua tunatangaza zabuni ya mabehewa haya, tumetilia maanani jambo hilo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, uwepo wa hizi Offsets Agreements kati ya Serikali na Mzabuni kwenye mikataba kungehakikisha Serikali inawakutanisha wakandarasi wa reli na wazalishaji wa bidhaa za ngozi na katani na kungehakikisha uwekezaji kwenye sekta ya uchimbaji madini na viwanda vikubwa vya chuma. Tunaweza kufanya haya kwenye miradi mikubwa ya maji, ujenzi wa bomba la mafuta na kadhalika. Naisihi Serikali itazame hii miradi mikubwa na kuifungamanisha na mkakati wetu wa viwanda ili fedha za miradi hii zibaki zaidi nchini, zitumike kuinua sekta yetu ya viwanda, zitoe ajira kwa watu na zisaidie kuchochea mzunguko wa fedha na kupunguza ugumu wa maisha (vyuma kukaza).

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la nne ni kwamba tuwe na mkakati maalum ili kuingiza dola bilioni moja kwa mazao ya biashara na India. Mei 2016 tulipokuwa tunajadili makadirio na matumizi ya Wizara hii, viwanda vyetu vilikuwa vinazalisha na kuuza nje ya Tanzania bidhaa zenye thamani ya dola za Marekani bilioni 1.408 (takribani shilingi trilioni 2.6)

na hivyo, kuwa sekta ya pili kwa kuingiza fedha za kigeni nchini kwetu baada ya sekta ya utalii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mei 2017 hali hiyo ya uzalishaji na uuzaji wa bidhaa zitokanazo na viwanda haipo tena, tunaweza kusema kwa uwazi kuwa biashara hiyo imeshuka mno. Kwa mujibu wa taarifa rasmi za Serikali yenyewe, kupitia taarifa ya Benki Kuu ya sasa (BoT Monthly Economic Review), sekta ya viwanda inauza nje ya nchi bidhaa za thamani ya dola za Marekani milioni 879 tu (takribani shilingi trilioni 1.962). Hivyo sekta hiyo kushuka na kuwa ya tatu katika kuchangia mapato ya fedha za kigeni baada ya utalii na dhahabu. Ushukaji huu ni wa zaidi ya asilimia 38 yakiwa ni mapato kidogo zaidi tangu mwaka 2010.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Mei 2018 BoT hata hawaweki takwimu za mauzo ya nje ya bidhaa za viwandani maana hali ni mbaya zaidi. Serikali inaona aibu kuwa sera zake mbaya za kiuchumi zimeshusha uzalishaji kwenye viwanda na sasa imeamua kuwakataza BoT kutoa takwimu za mauzo ya nje ya bidhaa za viwandani. Ni kilio kwa wakulima wa mbaazi, choroko, dengu na giligilani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mauzo ya bidhaa za viwanda kwenda nje ya nchi siyo pekee yaliyoshuka, lipo pia eneo la biashara ya mazao ya kitaifa. Mchango wangu kwenye bajeti ya Wizara hii kwa 2018/2019 utajikita zaidi kwenye eneo la biashara ya kimataifa, hasa biashara ya mazao ya kilimo jamii ya mbaazi, choroko, dengu na giligilani kwenda nchini India.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sera mbaya za uchumi, utekelezaji mbaya wa diplomasia yetu na juhudi ndogo za Serikali kutafuta masoko ya bidhaa zetu kimataifa ndani ya miaka miwili na nusu ya Serikali ya Awamu ya Tano vimechangia kwa kiasi kikubwa katika kuanguka kwa biashara ya mazao hayo kimataifa na hivyo Taifa letu kukosa fedha za kigeni. Miongoni mwa biashara za kubwa za mazao nchini ni biashara ya mbaazi tukiwa na soko kubwa nchini India. Mwaka 2015/2016 mauzo ya nje ya mbaazi (kwenda India) yalifikia USD milioni 224 sawa na shilingi bilioni 515 yakiweka rekodi ya juu kabisa ya mauzo yetu ya mbaazi India na pia yakiweka rekodi kwa wakulima kuuza hadi shilingi 3,000 kwa kilo moja ya mbaazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tarehe 9 Julai, 2016 Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi aliwasili nchini kwa ajili ya ziara yake ya kwanza Afrika, ambapo alitembelea pia Msumbiji, Afrika Kusini na Kenya. Lengo la kuja nchini likiwa ni kuonesha uhusiano mzuri kati ya nchi hiyo na Tanzania na pia kusaini mkataba wa ununuzi wa mbaazi kati ya nchi zetu mbili hasa kwa kuwa Tanzania ilikuwa imeuza mbaazi zenye thamani ya nusu trilioni kwa nchi hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mkutano wake na Waziri Mkuu Modi, uliofanyika tarehe 10 Julai, 2016 Rais Magufuli alisema yafuatayo na nanukuu: “Mwaka jana (2015), Tanzania iliiuzia India tani 100,000 za mazao ya kunde ambayo yalikuwa na thamani ya USD milioni 200. India inahitaji tani milioni saba za mazao hayo kwa mwaka, kwa hiyo, kuna fursa kubwa ya kufanya biashara katika kilimo hicho.” Mwisho wa kunukuu na akawahimiza wakulima wa mbaazi kulima zaidi zao hilo kwa kuwa soko la uhakika liko India.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini Serikali yetu kwa zembe tu ilichelewa kusaini makubaliano hayo ya ununuzi wa mbaazi kati ya nchi zetu mbili mpaka muda wa kikomo iliopewa na India ulipopita. Jambo hilo la kuchelewa kusaini makubaliano hayo limetufanya tutolewe miongoni mwa nchi zinazoruhusiwa kuuza mbaazi India na hivyo kusababisha tukose soko la kuuzia mbaazi zetu kwa miaka hii miwili ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kuwa haikuwa na mkataba wa kuuza mbaazi India, kwa kuwa ilichelewa kusaini makubaliano, lakini Serikali ilikaa kimya tu na taarifa hizo, haikuwaeleza wananchi waliohamasika kulima zaidi mbaazi kwa sababu ya bei kubwa ya shilingi 3,000 kwa kilo ya mwaka 2015/2016 kuwa haina mkataba na India. Matokeo yake wakulima na wafanyabiashara wetu wameishia kupata mateso tu na kufilisika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mwaka 2016/2017 thamani ya mauzo ya mbaazi kwenda India ikashuka mpaka USD milioni 131 sawa na shilingi bilioni 303.3. Mapato yakipungua kwa zaidi ya bilioni 200. Kwa mwaka 2017/2018 mauzo ya mbaazi kwenda India yakishuka zaidi hadi kufikia USD milioni 75 sawa na shilingi bilioni 172.5 na kusababisha ufukara kwa wakulima, kiasi sasa kilo moja ya mbaazi kuuzwa kwa shilingi 150 kutoka shilingi 3,000 ya awali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo baya zaidi ni kuwa Serikali yetu imeshindwa kabisa kutumia mahusiano yetu ya kibiashara, kidiplomasia na kihistoria na India kuhakikisha tunamaliza jambo hili na kunusuru soko letu kimataifa. Katika wakati ambao hatuwezi kuuza mbaazi India, kwa mwaka jana tu India alisaini makubaliano na kununua mbaazi kutoka Nigeria zenye thamani ya USD bilioni mbili sawa na zaidi ya shilingi trilioni 4.6, wakati ambao mbaazi zetu zilibaki kuozea kwa wakulima. Utafiti wa Januari, 2018 uliofanywa na Taasisi za Tanzania Pulses Network na East Africa Grain Council unaonesha kuwa hasara iliyopatikana kutokana na mbaazi zisizouzwa ni kubwa mno, kipato cha mwananchi kikitajwa kushuka sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, si mbaazi tu hata giligilani hali ni hiyo, bei yake imeshuka kutoka shilingi 300,000 mwaka 2016 mpaka shilingi 150,000 kwa gunia kwa mwaka 2017 wananchi wa Mkoa wa Manyara wanaumizwa sana na hali hiyo. Hali hiyo ya maumivu na kilio ipo pia kwa wananchi wa Misungwi, Mkoani Mwanza ambao mwaka 2016 waliuza choroko kwa shilingi 300,000 kwa gunia lakini bei hiyo ilishuka mpaka shilingi 150,000 kwa mwaka 2017.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mazao mengine yaliyoshuka bei ni mazao ya jamii ya dengu, mwaka 2016 wakulima wa mazao haya waliuza kilo nne za dengu kwa bei ya shilingi 7,500 lakini tangu mwaka jana bei ya mazao haya kwa hizo kilo nne imeshuka mpaka shilingi 2,500 tu, soko la mazao haya likiwa ni India. Ukitazama kwa undani, ni dhahiri kuwa mazao haya ya mbaazi, choroko, dengu na giligili, yanao uwezo wa kuliingizia Taifa zaidi ya USD bilioni moja kama tutaweka mipango ya kuongeza uwezo wa uzalishaji pamoja na kutumia diplomasia na historia yetu na India kutatua changamoto ya soko iliyoko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nini kifanyike ili kufikia lengo la kuingiza fedha za kigeni, USD bilioni moja kupitia mazao haya maalum yenye soko India? Baada ya kuonesha upungufu wa Serikali ya CCM katika fungamanisho la kilimo na biashara ya nje, natoa pendekezo la jawabu la hali hii, kama ifuatavyo:-

(i) Tusahihishe mahusiano yetu na India. Tuna faida mbili za kimahusiano na India, ya kwanza ni historia kati ya nchi zetu tangu wakati wa Baba wa Taifa, Mwalimu na Waziri Mkuu Nehru. Pili, ni uwepo wa jamii kubwa ya wafanyabiashara wa Kitanzania wa jamii ya Kihindi wenye asili ya Jimbo la Gujarati ambapo anatokea pia Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi. Kuna kulegalega kwenye mahusiano yetu, tusahihishe.

(ii) Tuitumie vyema diplomasia yetu. Kwa vyovyote ni lazima Serikali yetu ifanye diplomasia ya hali ya juu sana na Serikali ya India kwenye suala la soko la bidhaa za pulses hasa mbaazi, choroko, giligilani na dengu. Nchi yetu haiwezi na haipaswi kuzidiwa na nchi nyingine za Afrika katika suala zima la soko la bidhaa zake nchini India. Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ambayo inahusika na biashara ya nje, inabidi ifanye kazi ya ziada kwenye eneo hilo, biashara ya nje ni diplomasia, tuitumie.

(iii) Tuhakikishe tunarudisha soko letu. Nguvu yetu ya historia na mafungamanisho na India pamoja na diplomasia yetu vitumike vyema kwa pamoja kuhakikisha tunarudisha soko letu la kuuza mazao haya. Hili la kurudisha soko linapaswa kuwa jambo la kufa na kupona kwa Wizara hii. Ikibidi Waziri, Mheshimiwa Mwijage aende tena kuonana na Waziri mwenzake wa Viwanda na Biashara wa India, Suresh

Prabhu hasa kwa kuwa alishindwa kuambatana na msafara wa Makamu wa Rais juzi kwenye Mkutano wa Jumuiya ya Madola kule London, mkutano ambao Waziri Mkuu Modi alihudhuria.

(iv) Tuongeze uzalishaji wa mazao haya. Juhudi za diplomasia ya kurudisha soko letu ziende sambamba na kuongeza uzalishaji wetu katika kulima mazao haya. Ni lazima kuongeza uzalishaji wa mazao haya ili kuweza kupata mapato zaidi ya fedha za kigeni kwa mauzo ya nje.

Pia biashara ya mbaazi, choroko, dengu na giligilani inaweza kuchangia kwenye juhudi za kuondoa umaskini wa wakulima wetu ikiwa tutaweka mkakati maalum wa uendelezwaji wa mazao haya. Mkakati huo unapaswa kuhusisha kuwahamasisha wakulima waliokata tamaa kuanza upya kulima mazao haya, kisha kuwaunganisha kwenye vyama vya ushirika, kuhakikisha vyama hivyo vya ushirika wa wakulima tunaviunganisha na masoko moja kwa moja bila kupitia watu wa kati (madalali wanaowanyonya) na kuongeza tija ya kilimo chao kwa kuwaunganisha kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na kuweka fao la bei kwenye mifuko hiyo ili kuwalinda pale bei ya mazao inapoanguka

Mheshimiwa Mwenyeikiti, tukifanya haya, ni imani yangu kuwa tutaweza kabisa kuongeza uzalishaji hata kwa tani tano tu kutoka sasa ili kufikia mapato ya USD bilioni moja ya fedha za kigeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, naomba kuwasilisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, sisi si Tanzania ya Nyerere, ni Tanzania mpya, Tanzania mbaya inayokalia kimya mauaji ya kinyama ya Wapalestina na kuunga mkono waonevu.

(i) Msimamo wa Tanzania kuhusu Palestine (aya 18 ya Hotuba ya Waziri), maelezo ya Serikali hayaendani na matendo. Tanzania imewatupa mkono wanyonge wa Palestine.

(ii) Msimamo wa Tanzania kuhusu Sahara Magharibi (aya 19 ya Hotuba ya Waziri), kuna dalili zote kuwa Serikali inataka kuwafukuza POLISARIO baada ya kuikumbatia Morocco.

(iii) Unafanyaje diplomasia bila wanadiplomasia? Vituo vingi nje havina FSOs.

Mheshimiwa Naibu Spika, msimamo wa Tanzania kuhusu mgogoro wa Israel na Palestina unaelezwa vizuri sana na nukuu hii ya Mwalimu Nyerere aliyoitoa mwaka 1967 na ndiyo umekuwa msingi wa Sera yetu ya Mambo ya Nje kwa miaka mingi kabla ya utawala wa sasa wa CCM mpya.

“….Tanzania’s position. We recognize Israel and wish to be friendly with her as well as with the Arab Nations. But we cannot condone aggression on any pretext, nor accept victory in war as a justification for the exploitation of other lands, or Government over other peoples.”

Mheshimiwa Naibu Spika, kwamba Tanzania inaitambua Israel na inapenda kuwa na urafiki nayo pamoja na urafiki na mataifa mengine ya kiarabu, lakini hatuwezi kukalia kimya uvamizi kwa namna yoyote ile, pia ushindi vitani hauhalalishi unyonyaji dhidi ya ardhi ya wengine au dhidi ya Serikali za watu wengine. Msingi huu unaendana kabisa na dhamira ya sasa ya Sera ya Mambo ya Nje. Hata hivyo, hali ni tofauti kabisa. Mambo tunayoyayafanya kwenye Sera yetu ya Mambo ya Nje yanamfanya Mwalimu Nyerere ageuke huko kaburini kwake.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitaeleza kwa mifano, 26 Oktoba, 2016 kulikuwa na kikao cha Wajumbe wa Nchi 21 zinazounda ‘Kamati ya Urithi wa Dunia’ ya UNESCO-Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni kupiga kura ya kupitisha makubaliano ya kuridhia kuupa hadhi ya urithi wa Dunia Mji wa Jerusalemu pamoja na moja ya majengo ya Mji huo (Temple Mount) na kufungamanishwa na uasili wake na si hali ya sasa inayotokana na uvamizi wa Israel juu ya eneo hilo lililoko Jerusalemu Mashariki (lililovamiwa mwaka 1967 na mpaka leo kutambuliwa na UN kama eneo la Palestina, ambao wanauona ndiyo Mji Mkuu wa nchi ya Palestina iwapo makubaliano ya ‘Two States Solution’ yatafikiwa).

Mheshimiwa Naibu Spika, ACT Wazalendo tulihoji juu ya jambo hili linalokwenda kinyume na Sera ya Nje ya nchi yetu. Msimamo wa Tanzania ni kukubaliana na UN kupinga uvamizi wa eneo hilo uliofanywa na Israel. Serikali ilitoa majibu mepesi tu, tena pembeni kuwa upigaji wa kura ule haukuwa msimamo rasmi wa nchi yetu ni ukiukwaji wa sera yetu ya Mambo ya Nje na kuwa ni jambo ambalo Afisa wetu kwenye mkutano ule wa UNESCO alilifanya kwa makosa na hivyo hatua zingechukuliwa dhidi yake.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni dhahiri hayo yalikuwa ni ghiliba tu, matukio ya karibuni yameonesha kwa uwazi sura mpya ya Taifa letu pamoja na msimamo mpya wa Sera yetu ya Mambo ya Nje. Kwenye diplomasia matendo ya nchi huwa na maana zaidi kuliko maneno ya wanadiplomasia wake, matendo yetu yafuatayo ya karibuni yameonesha kuwa Tanzania hatuiungi mkono tena Palestina.

(1) Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuwaangusha Wapalestina kule Paris kwenye Mkutano wa UNESCO, Serikali iliahidi kuwa ingemchukulia hatua Afisa yule wa Wizara ya Mambo ya Nje aliyekwenda kinyume na Sera yetu ya Mambo ya Nje, hatujafanya hilo zaidi tumempandisha cheo na kumteua kuwa Balozi Elizabeth Kiondo apige kura namna ile kule UNESCO na sasa tumempa cheo zaidi kwa kazi njema aliyoifanya. Jambo hili linaonesha kuwa kwa sasa tunawaunga mkono Waisrael na hatuko tena na Wapalestina.

(2) Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa tumeamua kufungua Ubalozi wetu Israel, Tel Aviv, kuongeza uchungu kwenye kidonda, tukachagua wakati huu wa maadhimisho ya miaka 70 ya uvamizi wa Israel ardhi ya Taifa la Palestina kuzindua ubalozi wetu huo. Jambo hili linafanyika kukiwa na tuhuma kuwa hata huo ubalozi unagharamiwa na Israel yenyewe, ndiyo maana tumepangiwa hata kipindi cha kuufungua.

Mheshimiwa Naibu Spika, kidiplomasia kuufungua ubalozi wetu katika wakati huu ni kuadhimisha uvamizi wa Israel katika ardhi ya Palestina. Maana tulikuwa na uwezo wa kuchagua wakati mwingine wowote kufanya uzinduzi wa ubalozi wetu, lakini kwa kuwa aliyegharamia uwepo wa Ubalozi huo (Israel) alitaka tuufungue wakati huu wa maadhimisho ya miaka 70 ya uvamizi wa Israel kwa Palestina, ilitubidi tufanye hivyo. Jambo hili limeonesha kuwa kwa sasa hatuungi mkono tena utu (Palestina) bali tunamtumikia kila mwenye kitu (Israel).

(3) Mheshimiwa Naibu Spika, wakati akiwa ziarani Israel, Balozi Dkt. Mahinga alifika sehemu ya miji inayokaliwa kimabavu na Israel ambayo inapakana na ukanda wa Gaza, na baadaye alihojiwa na Televisheni ya Taifa ya Israel ambako alionesha tu masikitiko yake kwa Waisrael wanaokaa maeneo hayo kwa kusumbuliwa na mashambulizi ya Hamas, lakini hakulaani kabisa uendelezaji wa Israel kujenga makazi kwenye maeneo hayo ya uvamizi kama wanadiplomasia wengine wa nchi zenye msimamo wa ‘Two States Solution’ kama sisi wanavyofanya.

Mheshimiwa Naibu Spika, Balozi Dkt. Mahinga mwanadiplomasia mzoefu na mbobezi, kutokulaani kwake makazi yale haramu ni jambo la makusudi kabisa, si bahati mbaya. Ni kitendo cha kutuma salamu kwa Wapalestina kuwa tunaunga mkono uendelezaji makazi wa Israel katika maeneo hayo iliyoyavamia.

(4) Mheshimiwa Naibu Spika, Tanzania imetajwa na vituo mbalimbali vya habari vya Kimataifa kuwa ni katika nchi 33 ambazo zilihudhuria ufunguzi wa Ubalozi wa Marekani Mjini Jerusalemu, Mei 14 kilele cha maadhimisho ya miaka 70 tangu uvamizi wa Israel katika maeneo ya Wapalestina. Chanzo cha taarifa ya Tanzania kuhudhuria ni Serikali ya Israel, ikitaja nchi ilizozialika na zilizohudhuria.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali yetu inasema inapinga uwepo wa Ubalozi wa Marekani Mjini Jerusalem, lakini hapo hapo inatajwa kuhudhuria uzinduzi huo. Picha tunayoitoa hapa kwa Wapalestina ni kuwa tunaunga mkono jambo hili la ufunguzi wa Ubalozi wa Marekani Mjini Jerusalem.

(5) Mheshimiwa Naibu Spika, siku ya uzinduzi huo wa ubalozi wa nchi ya Marekani Mjini Jerusalemu, Jeshi la Israel liliwaua kwa risasi zaidi ya watu 54 wa Palestina, wakiwemo wanawake, watoto, walemavu na hata wanahabari. Nchi mbalimbali duniani zimelaani mauaji hayo. Nchi ya Afrika ya Kusini imekwenda mbali zaidi kwa kumrudisha nyumbani Balozi wake aliyeko Israel. Tanzania tuliyoikomboa Afrika ya Kusini tumekaa kimya, tumeshindwa hata kutoa kauli ya kulaani mauaji hayo. Kuhudhuria kwetu ufunguzi wa ubalozi na kukaa kimya juu ya mauaji hayo kunaonesha tumewaacha rasmi Wapalestina.

Mheshimiwa Naibu Spika, mambo hayo matano yanaonesha kuwa sisi si tena ile Tanzania ya Mwalimu Julius Nyerere, sisi kwa sasa ni Tanzania mpya (kama yasemavyo matangazo ya Ikulu yetu) – Tanzania mpya inayosimama na waonevu wa dunia, wauaji na wavunja haki za wanyonge. Sisi si tena Tanzania ya kusimama na wanyonge, bali ni Tanzania ya kusimama na wanyongaji kwa sababu ya maslahi ya kiuchumi.

Mheshimiwa Naibu Spika, si ile Tanzania iliyongoza ukombozi wa Bara la Afrika kutoka kwenye makucha ya ukoloni, bali ni Tanzania mpya inayounga mkono na kushabikia ukoloni na uvamizi. Sisi si ile Tanzania yenye msimamo mkali tuliopinga Taifa kubwa la Marekani dhidi ya
uvamizi wake kwa wanyonge wa Taifa la Vietnam, bali sasa ni Tanzania mpya ya kuunga mkono uvamizi wa Taifa onevu la Israel kule Palestina.

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi si Tanzania ile iliyoitetea China ipate nafasi na Kiti chake stahili kule UN, bali sasa sisi ni Tanzania mpya inayowaacha watu wa Palestina bila utetezi wa hadhi, kiti na nafasi yake stahili kule UNESCO.

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi si ile Tanzania huru tena ya Mwalimu Nyerere, iliyowaheshimu watu na Mataifa kwa sababu ya utu wao na kuamini kwamba binadamu wote ni sawa. Sasa sisi ni Tanzania mpya, inayowapa heshima watu kwa sababu ya kitu inachotuhonga, tukiuza usuli wa Utaifa wetu kwa maslahi machache ya kifedha au kiuchumi.

Mheshimiwa Naibu Spika, hatuwashi tena Mwenge na kuuweka Mlimani Kilimanjaro, hatumuliki tena nje ya mipaka yetu, hatuleti tena matumaini pale pasipo na matumaini, hatupeleki tena upendo kule kuliko na chuki na hatuleti heshima pale palipojaa dharau. Sisi si Tanzania ya Mwalimu Nyerere, sisi sasa ni Tanzania mpya, Tanzania mbaya, Taifa lililokiuka misingi yake, Taifa linalowaacha Wapalestina wakiuawa kinyama na sasa linalosapoti waonevu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kujengewa uwanja wa mpira na msikiti visiifanye Tanzania likumbatie Morocco na kuacha kuiunga mkono Sahara Magharibi.

Mheshimiwa Naibu Spika, bado niko kwenye Sera ya Mambo ya Nje ya Nchi yetu, si hii ya Tanzania mpya bali ile Tanzania ya tangu wakati wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ya kusimama na wanyonge. Wakati tulipoamua kufuata ‘Diplomasia ya Uchumi’ bado msingi wetu huu wa kusimama na wanyonge ulibaki palepale. Ndiyo maana wakati wa Rais Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete bado tulibaki kuwa ni sauti ya Mataifa yanayoonewa kama Cuba (tukipinga vikwazo vya Marekani dhidi yao), Palestina na Sahara Magharibi.

Mheshimiwa Naibu Spika, msingi huo wa kusimama na wanyonge ni muhimu zaidi kwa Chama chetu cha ACT Wazalendo, ndiyo maana tulipinga ujio wa Mfalme wa Morocco hapa nchini tarehe 23 - 25 Oktoba, 2016. Kwa kuwa Taifa hilo bado linaikalia kimabavu ardhi ya wanyonge wa Sahara Magharibi, ndiyo msingi pia wa kutangaza wazi mahusiano yetu rasmi na Chama cha Siasa na Ukombozi wa Taifa hilo cha POLISARIO kinachopigania uhuru wa nchi ya Sahara Magharibi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Umoja wa Afrika (AU) uliamua kukubali ombi la Morocco kurudi bila masharti kwenye Jumuiya hiyo. Ikumbukwe kuwa kwa zaidi ya miaka 33 Morocco haikuwa na mahusiano na Jumuiya hiyo (tangu OAU mpaka sasa AU) baada ya kujitoa kwa kupinga OAU kuitambua Sahara Magharibi kama Taifa huru na kupewa Kiti rasmi ndani ya OA mwaka 1984.

Mheshimiwa Naibu Spika, uamuzi wa OAU wa kuiruhusu Sahara Magharibi kuwa mwanachama wa umoja huo ulitokana na hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (International Court of Justice-ICJ) ya mwaka 1975 iliyopinga madai ya Morocco kuwa ina mahusiano ya kihistoria na kisheria na Sahara Magharibi (na hivyo kuitawala kinguvu) na kutoa haki ya kujitawala kwa Taifa hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaheshimu maamuzi yale ya mkutano wa AU uliofanyika Januari, 2017 ulioirudisha Morocco kwenye AU, lakini tabia za Taifa hilo onevu bado hazijabadilika, hivyo ni muhimu tulieleze Bunge hili Tukufu masuala yafuatayo ili liweke msimamo wake kwa Serikali juu ya kuminywa kwa watu wa Sahara Magharibi:-

(1) Kikao cha AU cha tarehe 28 - 29Januari, 2018 kiliazimia kuwa Morocco iruhusu Kamati Maalum ya Uangalizi ya AU iende kwenye maeneo ya Sahara Magharibi ambayo inayakalia kimabavu ili kuja kuijulisha AU hali ya mambo ilivyo.

(2) Tarehe 29 Machi, 2018 Morocco iliwajulisha UN juu ya kutoruhusu waangalizi wowote wa AU kwenda kwenye maeneo yote ya Sahara Magharibi inayokalia.

(3) Tangu mwaka 1991 Morocco imetumia mbinu, hila na uzandiki ili kuzuia Tume ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kura ya maoni ya uhuru wa Sahara Magharibi (MINURSO) kufanya kazi yake kwenye maeneo inayoyakalia kimabavu ya Sahara Magharibi. Siku za karibuni Umoja wa Mataifa (UN) ulipitisha Azimio Na. 2414 (2018) la kuongeza muda wa mamlaka, uhai na madaraka ya MINURSO kwa miezi sita, Morocco imepinga jambo hilo na kutishia kufanya mashambulizi ya kijeshi kwenye maeneo ya Sahara Magharibi ambayo yameshakombolewa (Liberated Zones).

(4) Bado Morocco inaendeleza uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu kwa watu wote wa Sahara Magharibi wanaodai uhuru wao.

(5) Kurudishwa kwa Morocco kwenye AU kulienda pamoja na Taifa hilo kuridhia ‘AU Constitutive Act’ inayotaka Mataifa ya Afrika kuheshimu Maazimio ya AU na hata yale ya UN yanatolewa kwa ushirikiano na AU. Hata hivyo, kwa matendo yake tuliyoyaainisha hapo juu ni dhahiri kuwa Morocco haitaki usuluhishi na Sahara Magharibi, bado inataka kuitawala na kuikalia kimabavu, ndiyo maana imekataa hata kumpa ushirikiano msuluhishi wa mgogoro huu, Ndugu Horst Kohler Rais wa zamani wa Ujerumani.

(6) Matendo ya Serikali yetu kwa sasa yanaonesha hatuna msimamo kwenye mambo ya msingi ya kidiplomasia, namna tulivyoenenda kwenye mahusiano yetu na wanyonge wa Palestina ni mfano hai, sasa tukijali vitu kuliko utu kama ilivyo zamani.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo basi, nataka kulishawishi Bunge lako litoe mwongozo kwa Serikali juu ya kuenenda kwenye hili jambo la Morocco na Sahara Magharibi ili kuzuia ahadi ya kujengewa uwanja na msikiti na Serikali ya Morocco. Vitu visitufanye tuwaache ndugu zetu wanyonge wa Sahara Magharibi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi yetu ni kimbilio la nchi ya Sahara, Serikali yetu chini ya Mwalimu Nyerere ililitambua Taifa la Sahara Magharibi tangu siku za mwanzo kabisa za harakati zao, ndiyo maana wanao Ubalozi hapa nchini. Kumuenzi Baba wa Taifa na kulinda misingi ya Taifa letu ni lazima tusimame na watu wa Sahara Magharibi na tusiwatupe kama tulivyofanya kwa watu wa Palestina.

Mheshimiwa Naibu Spika, naliomba Bunge liibane Serikali ili itoe ahadi hiyo hapa Bungeni, pamoja na kuitaka Serikali kutumia ushawishi wake kule AU na UN kuibana Morocco iruhusu kura ya maoni ya kuamua mustakabali wa watu wa Sahara Magharibi kama ilivyoridhiwa kwenye Azimio la UN. Viva Sahara Magharibi, Viva POLISARIO, Mungu Ibariki Afrika.

Mheshimiwa Naibu Spika, hakuna Diplomasia bila wanadiplomasia, tuna uhaba mkubwa wa Watumishi kwenye Balozi zetu. Msingi wa tano wa Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania unatutaka tushirikiane kikamilifu na nchi, Mashirika pamoja na Taasisi mbalimbali katika nyanja za Diplomasia, siasa, uchumi, utaalam na teknolojia. Wizara hii ina jukumu la kubuni na kusimamia utekelezaji wa misingi yote ya sera yetu ya mambo ya nje.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia Wizara hii pia ina jukumu la kusimamia na kuratibu mahusiano kati ya Tanzania na nchi pamoja na mashirika mbalimbali. Utimizaji wa jambo hilo unafanyika kupitia Balozi zetu zilizotapakaa kwenye nchi mbalimbali ulimwenguni. Kwa sasa ufanisi wetu si mkubwa kwa sababu ya uhaba wa Watumishi kwenye Balozi zetu mbalimbali duniani.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa wastani ukimwondoa Balozi, kila kituo cha Ubalozi wetu nje ya nchi kinapaswa kuwa na Mhasibu, mtu wa TISS pamoja na mwanadiplomasia (FSO). Vituo vingi vya Balozi zetu havina kabisa Maafisa wa Diplomasia (FSO’s), wale wachache waliokuwepo awali walirudishwa nchini kwa sababu mbalimbali (ikiwemo kumaliza muda wao wa Utumishi Nje ya Nchi). Tumerudisha watu bila kupeleka mbadala wao.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye Balozi zetu mbalimbali Watendaji hasa wa kazi za Kibalozi na Kidiplomasia ni hawa Maafisa wa Diplomasia (FSO’s). Sasa kwa uhaba huu tunawezaje kufanya diplomasia ya nchi yetu? Hiyo Diplomasia ya Uchumi tunafanyaje bila kuwa na hao wanadiplomasia?

Mheshimiwa Naibu Spika, natoa tu mfano wa Balozi zetu chache ulimwenguni, China nchi ambayo ni mshirika wetu mkubwa kidiplomasia na kiuchumi, hatuna kabisa FSO huko, labda ndiyo sababu mauzo yetu kwenda China yameshuka mno, maana biashara ya nje ni diplomasia. Sasa wakati unamtaka ndugu yangu Charles Mwijage asafiri ni nani atakayemuandalia hiyo mikutano ya kupata wawekezaji huko China kama hatuna FSO hata mmoja? Wenzetu Uganda wana FSO’s nane huko China, Kenya na Sudani wao wanao tisa kila mmoja.

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi nyingine ambayo hatuna FSO ni Ethiopia-Makao Makuu ya AU, utaona tunavyodharau nafasi yetu katika Afrika. Pia hatuna FSO Afrika Kusini, nchi rafiki na moja ya zenye uchumi mkubwa Afrika, hatuna kabisa FSO Ujerumani, nchi kubwa zaidi kiuchumi katika Umoja wa Ulaya (EU). Hata India ambako tangu Bunge lianze Wabunge tunalalamikia kukosa soko la mbaazi kutoka huko nako hatuna FSO hata mmoja. Tumeufanya kuwa ubalozi wa kupokea wagonjwa tu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi za BRICS (ukiondoa China, India na Afrika Kusini ambazo hatuna kabisa FSO’s) zilizobaki, Brazili na Urusi tuna FSO mmoja mmoja tu. Hata DRC Congo nchi ambayo zaidi ya theluthi moja ya mizigo ya transit inapita kwenye bandari ya Dar es Salaam inatoka, nayo tuna FSO mmoja tu tofauti na watatu ilivyozoeleka.

Kenya nchi ya Afrika Mashariki tunayofanya nayo biashara zaidi nayo ina FSO mmoja tu.

Mheshimiwa Naibu Spika, hali iko hivyo karibu katika Balozi zetu nyingi ulimwenguni, FSO’s ndiyo Maafisa hasa waliyofundwa na kupikwa kutekeleza sera yetu ya Mambo ya Nje. Foreign Service Officers (FSO’s) ndiyo diplomats (wanadiploma wetu). Kama hawapo vituoni na hatuwatumii maana yake hatufanyi diplomasia na kwa kuangalia mbali tunaua diplomasia yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, sitapitisha bajeti hii mpaka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki itakaponihakikishia kuwa itapeleka Maafisa wa Diplomasia (FSO’s) katika vituo ambavyo hatuna kabisa na pia kuwaongeza katika vile vituo ambavyo wako wachache.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 20 16/2017 - Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora
MHE. KABWE Z.R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa fursa ya kuchangia na nina maeneo makuu mawili tu maeneo mengine ni madogo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza jana Mheshimiwa Chenge alitu-challenge hapa tulete vifungu gani vya sheria ambavyo vimekiukwa katika utaratibu wa bajeti. Waheshimiwa Wabunge mtakumbuka kwamba mwezi Februari Bunge lilikaa kama Kamati ya Mipango na kupitisha ceiling za bajeti na bajeti guidelines. Katika bajeti guidelines ambazo tulipitisha hapa mwezi Julai thamani ya bajeti ilikuwa ni shilingi trilioni 23 lakini bajeti ambayo tunaijadili sasa hivi ni shilingi trilioni 29 na Bunge halijakaa wakati mwingine wowote ule kama Kamati ya Mipango na kuweza kurekebisha hizo bajeti guidelines.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba Waheshimiwa Wabunge watazame Sheria ya Bajeti, Na. 11 ya mwaka 2015, vifungu vya nane (8), tisa (9) na 19 ambavyo vyote vinaeleza ni utaratibu gani ambao unapaswa kufuatwa ili Bunge liweze kujadili bajeti kwa mujibu wa sheria. Vinginevyo hapo tutajadiliana mpaka mwisho, tutafika mwisho kumbe tumevunja sheria moja kwa moja. Kwa hiyo, naomba jambo hilo liweze kutazamwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, naomba nichangie ni kuhusu Wizara ya TAMISEMI, eneo la kodi za majengo. Kama ambavyo mzungumzaji aliyepita amezungumza na Kamati imesema kwamba sasa hivi Serikali kupitia TRA inaenda kukusanya Kodi ya Majengo, lakini huko nyuma tulijaribu kwa Manispaa za Dar es Salaam kuwapa TRA, lakini haikuwa na mafanikio ambayo yalikuwa yanafikiriwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, haiwezekani Manispaa zetu zikanyang‟anywa mamlaka ya kukusanya kodi zake yenyewe. Kama kuna jambo ambalo Serikali inaliona ni makosa yaani labda kodi inayokusanywa ni kidogo ni vizuri Manispaa zikajengewa uwezo ziweze kuzikusanya kodi hizi, kuwanyang‟anya chanzo hiki cha mapato itakuwa ni kuua Manispaa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba nifahamu na Waziri atufahamishe, sasa hivi kuna Manispaa nyingi sana ambazo zinaongozwa na Vyama vya Upinzani, huu ni mkakati wa kuziua Manispaa hizi zisifanye kazi yake au ni nia njema? Naomba nipate ufafanuzi kuhusu jambo hili. Maana yake Manispaa yangu ya Kigoma Mjini iko chini ya Upinzani, je, mnataka kutunyang‟anya 50 percent ya mapato yetu na fedha hizi zisirudi? Manispaa za Dar es Salaam, Iringa, Mbeya na kadhalika, zote ziko chini ya Upinzani, lengo lenu ni kuzinyima zisifanye kazi zisionyeshe kwamba zinaweza zikatenda tofauti na Manispaa zinazoongozwa na Chama cha Mapinduzi? Naomba kupata ufafanuzi wa maeneo kama hayo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna jambo ambalo sasa hivi sehemu yake iko mahakamani na sitoligusia kwa sababu ni mambo ambayo yako mahakamani hatupaswi kuyazungumzia. Mwaka 2013, Serikali ilikopa fedha zaidi ya dola za Kimarekani milioni 600, kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo, kupitia hatifungani ambayo wataalam wote duniani wanasema ilikuwa ni ghali na kimsingi tunapaswa kuwa tumeanza kuilipa kuanzia mwezi Februari mwaka huu. Itakapofika mwaka 2020, hatifungani hii itakuwa tumepaswa kuwa tumeilipa yote na kiwango cha fedha kutokana na riba ambayo tumepewa tutakachoenda kulipa ni dola za Kimarekani milioni 897 zaidi ya shilingi trilioni mbili ambazo ndiyo nchi italipa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hatifungani hii imeonekana inarushwa, waliopelekwa mahakamani ni waliowezesha rushwa, mtoa rushwa hayupo mahakamani? Mpokea rushwa hayupo Mahakamani? Kwa sababu waliopata biashara hii ni Standard Bank ya Uingereza. Tungependa kuona TAKUKURU wakiishtaki Standard Bank ya Uingereza na kuna maslahi ya Taifa katika Jambo hili . Ukiishtaki benki hii unapata faida mbili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, faida ya kwanza ikigundulika walitoa rushwa, kwa ajili ya kupata biashara walioifanya Tanzania, Tanzania itafutiwa deni lote la shilingi trilioni mbili. Faida ya pili itakuwa ni salamu kwa makampuni mengine ya Kimataifa kutokuja kuhonga nchini ili kupata biashara. Sasa maslahi ya TAKUKURU ni nini? Maslahi ya TAKUKURU ni kupata picha za watu wamebeba ndoo wamepelekwa mahakamani au maslahi ya TAKUKURU ni nchi kuepuka deni kubwa kiasi hiki. Kwa hiyo, naomba Waziri atakapokuja kutueleza hapa alione hili kwa mapana yake tuna deni la trilioni mbili ambalo tukiweza kuwafikisha mahakamani Standard Bank, tukathibitisha waliohonga ili kupata biashara ile, linafutwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii ninavyozunguma na nitawasilisha mezani nyaraka kadhaa, mojawapo ni barua ya Watanzania 2000 duniani kote wameandika kwa taasisi ya Serious Proud Office ya Uingereza, kutaka kesi ile ifunguliwe upya. Hawa ni Watanzania wenye uzalendo wako nje wameandika kutaka kesi ile ifunguliwe upya, TAKUKURU haifanyi chochote. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba na Mwanasheria Mkuu wa Serikali yuko hapa, bahati nzuri amekuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu muda mrefu atazame hili jambo, lina maslahi mapana ya Taifa. Msifurahi tu kukamata watu wa Dola milioni sita, kuna trilioni mbili za kuokoa na tayari kuna Watanzania wameshatuanzishia hili? Nawaomba Serikali iungane Mkono na hawa Watanzania, TAKUKURU ianze uchunguzi dhidi ya benki hii ya Uingereza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, bahati mbaya sana ndani ya Ofisi ya TAKUKURU; kuna washauri wa kutoka Uingereza wanaoishauri TAKUKURU kuhusu kesi hiyo. Sasa mnaweza mkaona namna gani ambavyo mgongano wa maslahi unaingia katika jambo hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba jambo hili litazamwe na naamini kwamba Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU yuko hapa, hili ni jambo ambalo linaweza likaiokoa nchi na likatuma salamu na tukawa nchi ya kwanza katika Bara la Afrika; ambayo inatuma salamu kwa makampuni ya Kimataifa kwamba msije kuhonga watu wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na kuvutavuta miguu kwa Serikali, naomba Bunge lichukue jukumu hili. Sababu Serikali inaweza ikafanya, lakini ikaonekana Serikali za nchi maskini hizi ukizikopa hazilipi. Bunge lichukue hili jukumu. Kanuni ya 120(2) ya Bunge, naomba tuitumie Kanuni hiyo kuomba Bunge hili mara baada ya hoja hii kwisha; tuunde Kamati Teule kwenda kuchunguza jambo hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nawaambia nchi itapata faida kubwa sana; na tutakuwa na sifa Kimataifa kuzuia makampuni makubwa ya Kimataifa kuja kuhongahonga watu wetu, kupata biashara; kama hii biashara ambayo ilifanyika na tutaokoa trilioni mbili ya Pato la Taifa; kwa hiyo naomba jambo hilo liangaliwe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, kulikuwa na uchunguzi unaoendelea kuhusu IPTL Tegeta ESCROW. Taarifa zote ambazo TAKUKURU wanazitoa ya kupeleka watu Mahakamani, hili jambo haliguswi; kulikuwa kuna maazimio ya Bunge hapa kwamba suala hili lichunguzwe na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU alishatangazia umma uchunguzi umekwisha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini watu waliohusika na Tegeta ESCROW hawajafikishwa mahakamani mpaka sasa? Kinachoogopwa ni nini? Ni kwamba kuna majipu yanaonekana, mengine ya mgongoni hayaonekani, hamwezi kuyatumbua? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hili jambo tunapoteza bilioni nane kila mwezi tunailipa kampuni ya matapeli; ambayo iliiba fedha Benki Kuu; wakatumia fedha zile kuchukua mkopo wanazalisha umeme eight billion every month tunawalipa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini TAKUKURU hawajawafikisha watu hawa mahakamani mpaka sasa? Naomba jambo hili pia liweze kuangaliwa ili tuweze kuhakikisha kwamba nchi inapata faida inavyostahili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, yale ambayo sijayasema, nitayawasilisha kama hati za kuwasilisha mezani ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa. Nashukuru sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/2017.
MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Spika, leo na kesho tunajadili bajeti ya Wizara ambayo inabeba asilimia 46 ya Bajeti yote ya maendeleo ya nchi yetu.
Yaani katika fedha za Bajeti ya Maendeleo ambazo zinaombwa na Serikali mwaka huu, trilioni 10.5, trilioni nne point nane ni ya Wizara inayoongozwa na Mheshimiwa Profesa Mbarawa. Naamini kabisa kwamba, wakati tunapanga siku za kujadili hatukuwa tumezingatia hili, ilipaswa Wabunge wapate muda mwingi zaidi kwa kuwa na siku nyingi zaidi za kuijadili Wizara hii. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, pili, Wizara hii inaongoza taasisi ambayo kwa mujibu wa Taarifa ya PPRA ndio taasisi ya pili kwa thamani ya manunuzi nchini, TANROADS, baada ya TANESCO. Kwa hiyo, ni Wizara ambayo ni nyeti sana na naamini kabisa kwamba, Waheshimiwa Wabunge wataitendea haki na Serikali itaweza kutoa majibu yanayostahili kwa ajili ya hoja mbalimbali ambazo Wabunge wataweza kuzi-raise. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, napenda nisisitize hoja ambazo Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Waziri Kivuli wa Miundombinu, amezi-raise ziweze kupatiwa majibu na hasahasa hoja ya MV Dar-es-Salaam kwa sababu, ni hoja ambayo inakimbiwakimbiwa na ni muhimu tuweze kuona suala la MV Dar-es-Salaam likichukuliwa hatua, ndiyo tutaamini kweli kuna nia ya dhati ya kupambana na ufisadi katika nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Nsanzugwanko na Wabunge wengine wa Kigoma watakaopata nafasi watazungumzia barabara za Mkoa wa Kigoma. Tuna kilometa 258 ambazo zitaunganisha Nyakanazi na Manyovu kwa maana ya kutokea Kabondo – Kabingo – Kibondo – Kasulu mpaka Manyovu, kilometa 258.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri pamoja na Waziri wa Fedha walitwambia kwamba, mradi huu unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika. Katika vitabu vya bajeti hatuoni, siyo tu ni lini mradi huu utaanza, hatuoni fedha zimetengwa kiasi gani. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, pili, kuna confusion ya project number kwa sababu, barabara iliyokuwa inatoka Sumbawanga mpaka Nyakanazi ilikuwa na Project Number hiyo. Sasa hivi project number nyingine kwa Nyakanazi mpaka Manyovu kwa maana ya kwamba, Wizara ya Ujenzi bado haijarekebisha jambo hili. Kwetu sisi Kigoma, mkoa pekee ambao haujaunganishwa na mkoa mwingine wowote kwa lami moja kwa moja, barabara ya Nyakanazi ni barabara muhimu, ni barabara ya kimkakati na ndiyo siasa za Kigoma. Kwa hiyo, naomba jambo hili Waziri aweze kulitolea ufafanuzi wa kina, hasa hasa inaanza lini? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, barabara inayounganisha Tabora na Kigoma kuna takribani kilometa 200 pale kama 204 hivi ambazo bado hazijakamilika. Kwa hiyo, naomba Waziri aweze kutueleza taratibu, tumeona Urambo – Kaliua itaanza mwaka huu, lakini pale Kazirambwa mpaka Chagu hatujajua inaanza lini. Kwa hiyo, naomba mambo haya Waziri aweze kuyatazama ili Mkoa wa Kigoma uweze kuunganishwa. Pili, barabara ya kutokea Uvinza kwenda Mpanda na barabara ya kutokea Uvinza kwenda kwenye Daraja la Malagarasi, tunaomba tupate commitment hapa ya Serikali, inaanza lini? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, hasa tumeambiwa kwamba, barabara ya Mpanda mpaka Uvinza inaanza kilomita 30 kuanzia Mpanda. Naomba nimshauri Waziri kwamba, tuwe na Mkandarasi ambaye ataanzia Mpanda kuja Uvinza na tuwe na Mkandarasi ambaye ataanzia Kanyani mpakani kwenye njiapanda ya kwenda Uvinza mpaka Uvinza ili tuweze kuhakikisha kwamba, barabara hii inakamilika vizuri kwa pamoja. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kuna suala la reli. Kama ilivyo kwa barabara, reli kwa Kigoma ndiyo siasa na siyo Kigoma peke yake, kwa mikoa yote ambayo inategemea reli ya kati, reli ni kiungo muhimu sana cha usafiri. Hapa napenda nirejee maoni ambayo yalitolewa asubuhi kama swali na Mheshimiwa Sabreena na baadaye tukawa tumeyazungumza na majibu ambayo Waziri ameyatoa; kuna haja kubwa ya kuchukua hatua za haraka kuondoa ulanguzi wa tiketi katika Stesheni ya Reli, Kigoma. Ni jambo ambalo linaumiza sana watu, watu wanatoka mbali na njia pekee ni njia ya uwakala. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, hata ukisema tunatumia digital, tunatumia simu, bado simu zitatumia mawakala kwa sababu, ni lazima TRL iweze kukubaliana kuingia makubaliano na kampuni binafsi kama zile ambazo zinatumika kwa ajili ya uwakala, kwa hiyo, huwezi kukwepa uwakala.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba jambo hili watu wa TRL waweze kulitazama, lakini jambo la msingi sana katika eneo hili, lazima sasa tufahamu kwamba, RAHCO ndiyo TANROAD ya reli. RAHCO inapaswa kuachia assets zote ambazo hazihusiani na ujenzi wa reli, kuiachia TRL ili TRL iweze kuwa na balance sheet iliyo nzuri kwa kuweza kupata fedha za uendeshaji wa reli, kwa hiyo, naomba jambo hili liweze kutazamwa vizuri. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, pili, tuangalie namna gani ya kutumia Stesheni za Reli kama maeneo ya biashara; stesheni zetu za reli zote kuanzia Dar-es-Salaam mpaka Kigoma zimelala! Hamna shughuli yoyote inayofanyika! Kwa hiyo, naomba TRL waweze kupewa kibali maalum cha kuendeleza Stesheni za Reli ambazo sasa hivi ziko chini ya RAHCO. Kwa hiyo, naomba mabadiliko hayo yaweze kutazamwa.
Mheshimiwa Spika, naomba kupata maelezo ya Serikali kuhusu kipande cha reli kutokea Kigoma kwenda Tabora na Uvinza – Msongati kwa ajili ya standard gauge kwa sababu, naona sasa hivi mwelekeo wa Serikali ni kupeleka reli Isaka mpaka Kigali na mmesahau kabisa suala zima la Uvinza – Msongati na jambo hili kwetu ni siasa kwa sababu, tunataka Uvinza iwe ni hub kwa ajili ya maeneo ya Maziwa Makuu. Kwa hiyo, naomba jambo hilo liweze kutazamwa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo ningependa kulizungumza, naomba ufafanuzi wa Mheshimiwa Waziri kuhusu Uwanja wa Ndege wa Kigoma kwa sababu, tulizungumza na alikuja Kigoma na aliona. Ametenga fedha, lakini naomba nifahamu kiwango gani ambacho kinakwenda kupanua runway na kiwango gani ambacho kinaenda kujenga jengo la abiria kwa sababu, kwenye bajeti yake hakufafanua. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kuna baadhi ya mambo ambayo yame-miss katika bajeti; la kwanza, ni Bandari ya Ujiji kwa sababu tulishakubaliana na Mamlaka ya Bandari Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa Bandari Ndogo ya Ujiji na Mamlaka ya Bandari Tanzania wamesema wanaanza mwaka huu. Sasa sijaiona hiyo kwenye bajeti! Sasa ni kwa sababu, iko kwenye Bajeti ya Maendeleo ya Mamlaka ya Bandari ama namna gani? Naomba nipate maelezo hayo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, la mwisho kabisa, ni suala zima la Bandari ya Kigoma. Bandari ya Kigoma ndiyo Mji wa Kigoma! Bandari ya Kigoma ikilala mji unalala kwa sababu, biashara zinakuwa hazipo! Sasa hivi Bandari ya Kigoma inaendeshwa na Mamlaka ya Bandari, lakini huwezi ukafanikiwa kuiendesha Bandari ya Kigoma kama huna biashara kutokea Kongo, kama huna biashara kutokea Kalemii. Kwa hiyo, Serikali inapaswa kuwa strategic kuhusu Bandari ya Kigoma.
Mheshimiwa Spika, Bandari ya Kigoma inapaswa kuendeshwa na taasisi ambayo inao uwezo wa kupata mzigo kutoka Kongo. Kwa hiyo, Waziri naomba jambo hili alitazame, tulilizungumza Kigoma, tulijadiliana Kigoma, lakini sasa hivi kuna ushindani mkubwa sana, vinginevyo reli tunayojenga itakuwa haina maana yoyote kwa sababu, haitapata mzigo kutokea Kongo. Kwa hiyo, naomba jambo la uendeshaji wa Bandari ya Kigoma waweze kulitazama. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa, MV Liemba, naomba jambo hili tuweze kulimaliza, tumelizungumza muda mrefu sana. Waziri Mwakyembe anakumbuka, tulizungumza mpaka na watu wa Ujerumani, alikutana na Waziri wa Usafirishaji kutoka Ujerumani wakati akiwa ni Waziri wa Wizara hii. Jambo hili la MV Liemba yasije yakatokea mambo yaliyotokea kwa MV Bukoba! Kwa hiyo, naomba MV Liemba, kama meli ya kihistoria, iweze kutazamwa na iweze kushughulikiwa kwa namna ambavyo inatakiwa.
Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo, nakushukuru sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia kidogo tu Wizara hii ya Maji. Nina mambo matatu tu ya kuchangia leo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza ni mradi wa umwagiliaji wa Delta ya Lwiche ambapo jana nilizungumza na Waziri. Maana yake nilikuwa naitazama kwenye randama ya Fungu Na. 5, sijaiona vizuri; na baada ya Mheshimiwa Waziri kunihakikishia kwamba ipo, lakini bado sijaiona. Pili, katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri, pia sijaiona.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huu ni mradi mkubwa kwa ajili ya kulima mpunga katika Manispaa ya Kigoma Ujiji. Ni mradi ambao utawezesha umwagiliaji kwenye hekta 3,000 na kuweza kuzalisha tani 15,680 za mpunga. Kwa hiyo, ni mradi mkubwa ambao unaweza ukaisaidia nchi kuondokana na tatizo la chakula lakini ni mradi ambao unaweza kwa kiasi kikubwa kupunguza umaskini na kuleta ajira ya kutosha kwa watu wa Manispaa ya Kigoma na Vijiji ambavyo vinazunguka Manispaa ile.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba Waziri katika majibu yake, katika maelezo yake na katika ufuatiliaji wake aweze kuona ni kwa nini mradi huu hauonekani waziwazi licha ya ukubwa wake, katika vitabu vyake vya Wizara, kwa sababu bajeti nzima ya umwagiliaji mwaka huu ni shilingi bilioni 30.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huu peke yake una thamani ya Dola za Kimarekani milioni 15. Kwa hiyo, ni zaidi ya bajeti nzima ya umwagiliaji katika Wizara ya Maji na Umwagiliaji. Kwa hiyo, naomba jambo hili Mheshimiwa Waziri aweze kulifuatilia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, huu ni mradi ambao utafadhiliwa na Serikali ya Kuwait kupitia Kuwait Fund na tayari Wizara ya Mambo ya Nje imeshakubaliana na Serikali ya Kuwait na nadhani kutakuwa na tatizo la kimawasiliano kati ya Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Fedha na Wizara ya Maji. Naomba Mheshimiwa Waziri alifuatilie jambo hili ili mradi huu uweze kuanza haraka iwezekanavyo. Watu wa Wizara ya Kilimo tayari wameshamaliza kutengeneza feasibility study na ninaweza nikampatia Mheshimiwa Waziri pia aweze kuiona kwa sababu ninayo hapa. Naomba tu aweze kwenda kuifuatilia vizuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, nililokuwa napenda kufahamu, ni kuhusiana na mradi wa maji katika Manispaa ya Kigoma. Katika kitabu cha hotuba ya Mheshimiwa Waziri ukurasa wa 53 ibara ya 123, ameelezea kwa kina kuhusu mradi huu. Mheshimiwa Waziri anafahamu kwamba mradi huu ulikuwa uishe toka mwezi Machi, 2015. Mpaka sasa kwa mujibu wa taarifa ya Waziri, mradi huu umefikia asilimia 50. Kwa mujibu wa mkataba, mradi ulipaswa kwisha mwezi Machi, 2015. Waziri anasema mradi sasa utakamilika mwezi Oktoba, 2016.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa tuna tatizo! Tuna tatizo la Wakandarasi wanaopewa miradi ya maji; siyo Kigoma peke yake. Sehemu nyingi ya nchi, Wakandarasi katika Wizara ya maji ni watu ambao wamekuwa wakichelewesha kumaliza miradi. Mfano, mzuri ni Mkandarasi ambaye amepewa mradi huu wa maji wa Kigoma SPENCON.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaelezwa kwamba Mkandarasi huyu alitumia fedha za mradi wa maji Kigoma kwenda kulipa madeni aliyokopa kwenye miradi aliyokuwa nayo nchi ambazo ni tofauti na Tanzania, lakini katika hotuba ya Waziri, sioni uwajibikaji ambao unafanywa kwa huyu Mkandarasi, kwa sababu wananchi wamehangaika, hawana maji, Mkandarasi alipaswa awe amemaliza mradi huu, lakini mpaka sasa hivi mradi huu haujakwisha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, namwomba Mheshimiwa Waziri, pamoja na maelezo haya kwamba mradi utakamilika mwezi Oktoba lakini mradi huu umechelewa, tunapaswa kupata maelezo, ni hatua gani zimechukuliwa dhidi ya Mkandarasi ambaye alipewa mradi huu? Kwa sababu tusipochukua hatua kwa Wakandarasi wa namna hii, tutapiga kelele hapa, tutapendekeza kuongezeka kwa tozo mbalimbali, fedha zitapatikana, lakini kwa Wakandarasi wa aina hii maana yake ni kwamba fedha zile tunakwenda kuzipoteza na wananchi wetu wala hawatapata maji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba nipate maelezo ya Mheshimiwa Waziri kwamba ni hatua gani zinazochukuliwa kwa Wakandarasi wa namna hii. Mtu ambaye amepewa Mkataba, hajautekeleza, kwa nini tuwabembeleze Wakandarasi wa namna hii na wananchi wetu wanazidi kuumia?
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba jambo hili Mheshimiwa Waziri alitolee ufafanuzi wa kutosha kabisa kwa sababu ni jambo ambalo linawaudhi sana watu wa Kigoma, mradi huu wameusubiri kwa muda mrefu sana. Viongozi walikuwa wanakuja Kigoma, wanapokelewa na ndoo za maji kwa sababu ya kero ya maji katika mji wa Kigoma na mradi huu ndiyo ulikuwa unakwenda kumaliza kabisa kero hii ya maji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba nipate maelezo ya kutosha kabisa na siyo maelezo tu ya kueleza kwamba, mradi umefikia asilimia ngapi; mradi ulikuwa uishe mwezi Machi, 2015, mpaka sasa hivi mradi haujakwisha, una asilimia 50. Ni hatua gani ambazo zimechukuliwa dhidi ya Mkandarasi na dhidi ya watu ambao walikuwa wanasimamia mkataba huu ili kuhakikisha kwamba jambo hili linaweza likaisha? Nakubali kwamba liishe mwezi Oktoba lakini ni lazima tuchukue hatua dhidi ya Mkandarasi ambaye amechelewesha mradi huu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu ambalo nataka kulizungumzia ni suala la Wakala wa Maji Vijijini. Hili ni jambo ambalo lina muafaka. Mheshimiwa Mwambalaswa amezungumza hapa; Serikali, Kamati na Kambi ya Upinzani Bungeni, vyote vimekubaliana na jambo hili, hakuna sababu ya kulichelewesha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona faida kubwa ambayo tumeipata kwa kuwepo kwa REA na mafanikio makubwa ya REA yamepatikana baada ya Bunge hili kufanya maamuzi ya tozo ya mafuta ya taa kuielekeza REA. Ndiyo mafanikio ambayo tunayaona kwenye REA. Ni matunda ya kazi ya mapendekezo ya Wabunge katika Bunge hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Waheshimiwa Wabunge wanapendekeza tuwe na Wakala wa Maji Vijijini. Wakala huu uhangaike na maji tu. Tuupe fedha za kutosha, fedha ziwe ring fenced, uhangaike na maji tu. Kuendesha miradi ya maji kwa kutegemea Wizara peke yake, haitatusaidia sana. Tumeona muda wote huu tumefanya hivyo na hatujaona mafanikio makubwa. Kuna nyongeza imefanyika kwa watu kupata maji, lakini bado kasi yake haitoshi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana, tusimalize Mkutano huu wa Bajeti bila kutoka na Wakala wa Maji Vijijini. Wakala huu hauhitaji sheria, kwa sababu tuna mifano tayari. Unachukua tu templet ya uanzishwaji wa REA, unaiboresha, unatoa umeme, unaweka maji, unaweka utaratibu wa fedha zake kupatikana, tunaondoka hapa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapokuja kwenye Miswada ya kifedha itakayokuja baadaye, tuondoke na Wakala wa Maji Vijijini. Mheshimiwa Waziri ateue watu wazuri, awapeleke kule waendeshe Wakala huu tuondokane kabisa na kero ya maji kwa wananchi wetu. Ni aibu kubwa sana kwamba mpaka leo hii tunapozungumza, kuna baadhi ya wananchi wetu wanakunywa maji na mifugo katika sehemu nyingi za nchi yetu na sisi Waheshimiwa Wabunge tunajua.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana Waheshimiwa Wabunge wote, kwa sababu tuna consensus kwenye jambo hili, tuondoke na Wakala wa Maji Vijijini. Wakati Bunge linaahirishwa hapa, Waziri Mkuu anafunga Bunge, tunaondoka na Wakala wa Maji Vijijini. Tutakuwa tumepiga hatua kubwa, tutakuwa tumewasaidia wananchi wetu na tutaingia kwenye historia kama tulivyoingia kwenye historia ya kuhusu REA na kodi ya mafuta ya taa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana.
Mkataba wa Ubia wa Uchumi baina ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya.
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Spika, juzi nilisema hapa kwamba biashara ni vita. Nasikitika sana kwamba nature ya mjadala ambao unaendelea Bungeni ni kama watu ambao tunaenda vitani, halafu tunanyoosheana silaha.
Mheshimiwa Spika, inapokuja kwenye masuala ambayo nchi inakwenda kupambana na wengine, jambo la kwanza ambalo ni lazima tulifanye, wote lazima tuwe kitu kimoja. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, siridhishwi kabisa na nature ya mjadala, kwa sababu hatuoni aibu kutofautiana katika jambo ambalo huko tunakokwenda tunakwenda kupigwa na wenzetu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nitawaambia kitu kimoja, why Kenya has signed? Kwa wale ambao labda mtakuwa hamfahamu, why Kenya has signed an EPA kinyume na maagizo ambayo Wakuu wa nchi wa Afrika Mashariki wamekubaliana? Why has they signed? Maua! Biashara ya maua ndiyo imewafanya Kenya waseme to hell with EAC, sisi tunasaini. Maua tu.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kama una nchi kama Kenya yenye uchumi mkubwa zaidi ya Tanzania, inakuwa tayari kuhatarisha EAC kwa sababu ya maua, lazima tujiulize mara mbili mbili. Hii mnarushiana mishale hii, hili siyo jambo la chama kimoja hili. Siyo jambo la CCM, siyo jambo la CHADEMA, siyo jambo la CUF, siyo jambo la ACT-Wazalendo, hili ni jambo la Tanzania. Kwa hiyo, naomba tutakapoendelea na mjadala huu tuitazame nchi, tusijitazame sisi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kuna mambo sita muhimu ambayo yanatufanya sisi kama Tanzania tusite kuingia kwenye mkataba huu. Jambo la kwanza wanaita ni asymmetrical liberalization. EU wanasema sisi tuna-liberalize bidhaa zenu zote; nanyi tunawaruhusu kidogo kidogo, mta-liberalise asilimia 90 ya bidhaa zote na asilimia 10 ya bidhaa za kilimo. Wazungu wanasema, devils is in the details. Hiyo asilimia 10 ya bidhaa za kilimo ni nini?
Mheshimiwa Spika, ukienda kuangalia kwenye mkataba unakuta kwamba sisi tunaweza tukauza kila kitu kule, tukawabana wao waingize asilimia 10 tu, lakini ndani ya zile bidhaa 10 kuna bidhaa za mazao ya mihogo. Mazao ya mihogo ni nini? Starch kwamba sisi leo tunaweza tukawauzia wao mihogo (raw), wao wakatuletea starch. Ndivyo mkataba ambavyo upo. Kuna mazao mengi sana, ndiyo maana nasema, devils in the details.
Mheshimiwa Spika, wanatuambia kwamba hakuna export taxes, nini maana ya hii? Maana yake ni kwamba leo mkitaka msiuze korosho ambayo ni ghafi, mnataka muuze korosho iliyobanguliwa, EU wanasema usiweke kodi kwenye korosho ghafi. Sisi sera yetu ya kibiashara ni kwamba ili kuhakikisha watu wanabangua korosho, tunaweka kodi kwenye korosho ghafi.
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa mkataba huu, ili tufanye hivyo, lazima kwanza tuombe ruhusa kwa European Union. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lingine ni ngozi. Ni kwa nini nchi ya Ethiopia imekataa katakata hata ku-negotiate na European Union? Kwa sababu Ethiopia wamesema sisi tunataka kujenga kwanza uwezo wetu wa ndani, tukishaweza kushindana na ninyi, tutakuja ku-negotiate tuweze kuwa na mkataba, hiyo ni Article 14.2. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kuna jambo hapa ambalo limekuwa likiongelewa, lakini haliwekewi details; revenue loses. Kwa sababu, unapozuia export taxes na unaporuhusu bidhaa za European Union kuingia nchini bila kodi, maana yake ni kwamba, hutakuwa tena na import taxes ya bidhaa zote zinazotoka European Union, huta-charge excise duty kutoka bidhaa zote zinazotoka European Union, hauta-charge VAT kwenye bidhaa zote zinazotoka European Union…
Mheshimiwa Spika, nilikuwa naomba niongezewe muda kidogo.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kitakachotokea tutapoteza. Hata kwa East Africa nzima tutapoteza Euro bilioni 3.6, zaidi ya shilingi trilioni nane. Kwa Tanzania peke yake tutapoteza dola milioni 853. Hesabu hizi zimefanywa na European Union wenyewe. Sasa nini ambacho kilitakiwa kifanywe?
Mheshimiwa Spika, kulitakiwa kuwe na mfumo wa kuweza kufidia hiyo loss. EU wamekataa huo mfumo wa kufidia loss. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa sababu ya muda, naomba nipendekeze baadhi ya vitu. Moja, itakuwa ni faida kubwa kwa nchi yetu, kama mkataba wa namna hii ukisainiwa na Afrika nzima yaani kuwe na Continental Free Trade Agreement ambayo ndiyo iingie mahusiano na European Union. Kwa hiyo, nilikuwa nataka katika moja ya mapendekezo yetu, ushauri wetu kwa Serikali ni kwamba Tanzania itumie nguvu yake ya kidiplomasia ku-rally nchi nyingine za Kiafrika ili mkataba huu uondoke kwenye individual regional groups ambazo tayari zimeshasambaratika, tuwe na continental approach dhidi ya European Union. Faida yake kubwa hii ni kwamba, itasababisha tuwe na free trade area within Africa na tuwe na mahusiano na nchi hizo tukiwa na ukubwa kiasi hicho. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lingine ni lazima tu-negotiate; yaani moja ya maagizo ambayo Bunge linatakiwa litoe kwa Serikali, ni ku-negotiate compensation mechanism ya revenue losses, kwa sababu ukiingia mkataba wa namna hii, kuna trade diversion. Zile bidhaa ambazo tungeweza kuziagiza kutoka nchi nyingine, zikipewa preferential treatment, bidhaa za EU maana yake ni kwamba zinapotea. Kwa hiyo, ni lazima tuwe na compensation framework. Bila hiyo compensation framework, sisi ndio ambao tutaingia kwenye shida zaidi.
Mheshimiwa Spika, naomba nimalizie hii point ya mwisho tu.
Mheshimiwa Spika, Mawaziri wamshauri Rais. Kwa kuwa sasa hivi tupo kwenye hali ya juu sana ya majadiliano ya jambo hili, tunahitaji a political commissar ambaye akilala, akiamka anaangalia hii mikataba ya kibiashara ya Kimataifa tu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sasa hivi Wizara ya Viwanda na Biashara ina Waziri tu, haina Naibu Waziri. Waziri akihangaika na kututafutia viwanda, atapoteza focus ya kuhangaika kwenye negotiation.
Kwa hiyo, tuiombe Serikali, sisi hatuna mamlaka ya kumwagiza Rais, lakini tumshauri kwamba tunahitaji msaidizi wa Mheshimiwa Mwijage pale (political commissar) ambaye kazi yake yeye na apewe instrument maalum ya ku-deal na hili jambo ili kuhakikisha ya kwamba at all time tuna mtu ambaye yuko dedicated kwenye jambo hili tu, wakati Waziri anaangalia kwa ujumla wake masuala mengine ya viwanda na kadhalika, ili tuweze kuwa na nguvu ya kuweza kwenda kushindana na kujadiliana na wenzetu.
Mheshimiwa Spika, nakushukuru na ahsante sana.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia Bajeti hii ya Serikali, hii ni mara yangu ya kwanza nachangia mjadala wa bajeti toka mwaka 2016/2017.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza ambalo ningependa kushauri kwa Waheshimiwa Wabunge wenzangu ni kwamba mfumo wetu wa Bunge ni mfumo wa Kamati. Kamati za Bunge zinafanya kazi kwa niaba ya Wabunge wote. Kwa hiyo taarifa ambayo Kamati za Bunge zinaleta ndani ya Bunge, ndiyo taarifa ambazo zimefanyiwa kazi na kwa niaba ya Wabunge na Kamati husika. Kwa hiyo ni muhimu sana Waheshimiwa Wabunge kuwashauri tu kwamba turejee sana kazi ambazo wenzetu wamefanya kwa niaba yetu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili ni kwamba panapokuwa na jambo ambalo unaona kundi la Wabunge wenzako wana mashaka nalo, jitahidi sana kuwaelewa kwa sababu humu Bungeni tunategemeana. Leo hii ukija humu Bungeni ukaanza kuwa-counter Wabunge wa kutoka mikoa inayolima korosho, kesho utakuwa na jambo lako hutapata mtu wa kukuunga mkono, hiyo ndiyo Parliamentary Politics. Parliamentary Politics ni Wabunge kushirikiana. Kama unaona mwenzako ana jambo hulipendi, busara inakwambia kaa kimya usiwapinge wenzako, kwa sababu wao ndiyo ambao wana-feel the pinch ya jambo ambalo linakuwa limetokea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maana hiyo naenda kwenye korosho moja kwa moja. Ukurasa wa 43 wa Kitabu cha Kamati ya Bajeti, kimeeleza wasiwasi wake kutokana na mapendekezo ambayo Serikali inaleta kuhusu kuweka fedha za kutoka kwenye mazao kuziingiza kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nilikumbushe Bunge mwaka huu 2017/2018, kama siyo korosho na transit goods kwenye forex tungekuwa na dola inakwenda mpaka kwa Sh.4,000. Korosho na transit goods ndiyo zimetusaidia kuingiza mapato ya fedha za kigeni, kwa sababu mazao mengine yote mapato yameporomoka. Pamba mapato yameporomoka ya fedha za kigeni, kahawa mapato yameporomoka na mazao mengine kama jinsi ambavyo Kamati ya Bajeti imeweza kueleza. Kwa hiyo, korosho ni zao ambalo limetuokoa, limeingiza dola za Kimarekani milioni 514 mwaka uliopita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni muhimu sana tutazame nini kimesaidia korosho kuongeza uzalishaji na mauzo nje. Ni maamuzi tuliyoyafanya mwaka 2010 ya export levy asilimia 65 kwenda kuendeleza zao la korosho. Sasa hivi Serikali inataka kuchukua fedha hizo, itakuwa ni makosa makubwa sana kwa sababu unaenda kumshughulikia mtu anayefanya vizuri. Katika hali ya kawaida ilitakiwa Serikali ilete pendekezo asilimia 100 ya export levy iende kwenye korosho kwa sababu Mikoa inayolima korosho imeongezeka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la msingi la kuzingatia hapa na ambalo Wabunge wa Mikoa ya Kusini wamelieleza vizuri sana ni kwamba fedha ambayo imetengwa kisheria wameichukua hawajairudisha, hawajaitekeleza sheria inavyotaka, halafu badala ya kulipa kwanza hizo fedha ndiyo waje na mapendekezo mapya, wanakuja na mapendekezo ya kuchukua na zingine zitakazokuja forever, haiwezekani! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ya Bajeti imefanya uchambuzi hapa. Shilingi Bilioni 755 fedha ambazo ziko ring fenced, ambazo zina matumizi maalum ya kisheria, Wizara ya Fedha haijazipeleka kule ambako kunatakiwa. Kawaida hapa tayari sheria imevunjwa! Sasa Serikali inapata wapi moral authority ya kuja na hoja ya kwamba sasa hizi hela zote sasa ziende Mfuko Mkuu wa Hazina, ni makosa makubwa sana ambayo tunakwenda kuyafanya, nami naungana mkono na taarifa ya Kamati ya Bajeti kwamba suala hili lisitekelezwe kama jinsi ambavyo linapendekezwa na Serikali.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ni Treasury Single Account. Kwanza niseme kwamba wazo lenyewe siyo baya. Ni vizuri tuelewane hapo, wazo la Treasury Single Account si wazo baya, kwa sababu nimeenda kusoma kwenye taarifa za IMF na nitampatia nakala Mheshimiwa Waziri wa Fedha. Kuna working paper No. 10/143 iliyoandikwa na Sailendra Pattanayak nzuri sana inaeleza hili, lakini haielezi namna ambavyo Serikali yetu inataka kulifanya. Serikali yetu inataka fedha yote iingie Mfuko Mkuu wa Hazina na Serikali yetu inatuambia jambo hili ni la Jumuiya ya Afrika Mashariki, siyo kweli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimetazama protocol zote ambazo tumesaini za Jumuiya ya Afrika Mashariki hakuna jambo hilo. Jambo hili ungeliona Afrika Mashariki kama tungekuwa tunaanza kutekeleza monetary union. Hatujaletewa hapa Bungeni protocol ya monetary union. Kwa hiyo, hoja ambayo Serikali iliileta kwamba hili jambo ni la Afrika Mashariki ilikuwa ni hoja ya kutushawishi tu, lakini siyo kweli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hiyo hoja ni kweli Serikali ituletee hapa ni protocol ipi hiyo ya Afrika Mashariki ambayo inasema jambo hilo, siyo kweli! East Africa imetoa vigezo vya namna ya kuingia kwenye monetary union, ikiwemo nakisi ya bajeti na kadhalika, haijasema mtunzeje fedha zenu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi zingine wanachokifanya hawasemi hela zote ziingie kwenye akaunti moja ya Benki Kuu au ya reserve bank na kadhalika. Wanachokifanya wanajenga system ambayo Hazina na Benki Kuu watajua pale Bariadi kuna balance cash kiasi gani siku ile wakati business day imefungwa. Kwa hiyo Serikali itajua kama ni cash management Serikali itajua Bariadi Halmashauri ina hiki, sijui Itilima Halmashauri ina hiki, Misungwi ina hiki, Kigoma ina hiki, lakini kilicholetwa na Serikali ni kwamba Kigoma tukikusanya tupeleke Benki Kuu, siyo sahihi! Kwa hiyo, nadhani Wizara ya Fedha ilitazame hili. Siyo jambo baya, hatuwapingi, liandaliwe vizuri na tulifanye kwa mazingira yetu ya Tanzania.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hili jambo la stamp za electronic, msingi wa hoja siyo mbaya kwa sababu unaenda kudhibiti mapato, lakini tunatekeleza namna gani, lazima tulitekeleze kwa namna ambayo hatupeleki ushuru

kwa wananchi kinyemela. Kwa sababu kwa mazingira ambavyo lipo sasa hivi gharama kwa wananchi zitaongezeka. Waziri Mpango ametusomea hapa kwamba bidhaa za ndani soda, bia nini hazijaongezewa kodi, lakini ukitekeleza tu hii electronic stamp zinaongezeka kodi na baadhi ya bidhaa zitaongezeka kodi mpaka Sh.90 kama maji, soda na kadhalika. Kwa hiyo hatusemi kwamba ni jambo baya, liandaliwe utaratibu ambao likitekelezwa wananchi hawatapata madhara ambayo wanakwenda kuyapata. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mambo mengine mawili ya mwisho ambayo nitaenda kuchangia, Kamati ya Bajeti imezungumza kuhusu kodi, ushuru wa mafuta kwa ajili ya maji. Waheshimiwa Wabunge tulizungumza hapa wakati wa Wizara ya Maji na kuna consensus ya ndani ya Bunge kwamba tuongeze fedha kwenye ushuru, fedha Sh.50 ili tupate fedha za kutatua kero za maji kwa wananchi wetu, hakuna Mbunge ambaye hakuliunga mkono hili. Serikali haijaja na hilo wazo. Kamati ya Bajeti imependekeza kwamba Sheria ya Road and Fuel Tolls Act ibadilishwe tulete fedha hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri wa Fedha namwelewa ana wasiwasi wa masuala ya mfumuko wa bei na kadhalika, lakini namshauri Waziri wa Fedha akaangalie takwimu zake vizuri Dkt. Mpango. Ukiangalia mara ya mwisho tumepandisha ushuru huu kisawasawa ni mwaka 2007. Ushuru huu mwaka 2007 kwa dola (in dollar terms) ilikuwa ni senti za dola 0.42, leo ushuru huu kwa senti za dola leo 2018 ni senti za dola 0.34.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, katika hali ya kawaida in real terms utakuwa umefanya marekebisho ya ushuru na katika hali ya kawaida Mheshimiwa Waziri wa Fedha ushuru ungepaswa kupanda kwa Sh.160. Kamati ya Bajeti inaomba Sh.50 tu lakini ushuru unaweza ukapanda mpaka Sh.160 bila kuathiri mfumuko wa bei, kwa sababu tutakuwa tunafanya rationalization na exchange rate kwa sababu hayo mafuta tunayanunua kwa

dola. Kwa hiyo ni sahihi kabisa kuhakikisha ya kwamba tuna-relate huo ushuru kutokana na dollar terms.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mapendekezo yangu, Waziri ametueleza hapa kwamba kipaumbele ni kilimo. Kilimo hakijatengewa fedha za kutosha, umwagiliaji haujatengewa fedha za kutosha. Ukifanya 160 Mheshimiwa Dkt. Mpango, akisema Sh.60 ziende kwenye umwagiliaji unapata shilingi bilioni 190 ambazo hata kwa ambao tunataka michikichi watu wanaoleta mafuta ghafi wameongeza kodi ili tuweze kuzalisha hayo mawese kwa ndani, si tunahitaji uwezekezaji, hela hii hapa kwa ajili ya kuja kuwekeza. Watu wa alizeti hela hiyo hapo kwa ajili ya kuja kuwekeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, napendekeza katika Road and Fuel Act tufanye marekebisho hayo tuendane na mapendekezo ya Kamati ya Bajeti na tunaweza tukaenda mpaka Sh.160 tukapata fedha za umwagiliaji, nchi ikajitegemea kwa mafuta ya kula ya kutosha ndani ya muda mfupi ambao unatakiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho kabisa, kuna makosa tuliyafanya mwaka 2016/2017, lazima tukiri. Matatizo ya kibajeti tuliyonayo sasa hivi, matatizo ya ukwasi wa fedha tuliyonayo sasa hivi ni measures tulizozifanya kwenye bajeti ya kwanza ya mwaka 2016/2017. Lazima tuanze kurekebisha, tulipandisha bajeti kwa thirty one percent (31%) ndiyo maana leo bajeti hii tunaijadili hapa ukilinganisha na mwaka jana imepanda kwa asilimia mbili tu ili kurekebisha makosa ya mwaka 2016/2017.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya kosa tulilofanya mwaka ule ni kodi kwenye huduma za utalii. Kasi yetu ya kuongeza wageni wa utalii ilikuwa twelve percent (12%) kabla ya kuongeza hii kodi. Leo hii kasi yetu ni asilimia tatu. Nataka niwaambie jamani sasa hivi ukicheza na utalii, ukicheza na transit goods, Bandari ya Dar es Salaam na ukicheza na korosho ya kina Mzee Mkuchika shilingi itafika Sh.5000 au Sh.6000 kwa dola, sababu haya ndiyo maeneo yanayotupa forex sasa hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napendekeza kwamba ile kodi ya ile VAT kwenye tourism services iondolewe. Pili sasa hivi kwenye mapendekezo haya kwenye kukodisha ndege pia tumeweka VAT tena. Tumeleta mapendekezo kwenye Finance Bill ya sasa hivi, namwomba Mheshimiwa Waziri aitazame. Kwa kweli kama tukisimamia vizuri na ikiboreshwa iwe electronic stamp tutapata fedha za kuziba haya maeneo. Napendekeza maeneo hayo yaweze kuangaliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, michango kuhusu mambo mengine nimepeleka kwa maandishi na tutajadiliana zaidi kwenye Finance Bill wakati wa mjadala kuweza kuboresha zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuchangia hoja zifuatazo:-

(i) Uchunguzi wa mauaji ya raia (MKIRU - Mkuranga, Kibiti na Rufiji);

(ii) Suala la uraia wa watu wa Kigoma;
(iii) Kupotea kwa Ben Saanane, Azory Gwanda na Simon Kanguye bila taarifa yotote ya polisi kuhusu uchunguzi wa kupotea kwao. Pia uchunguzi kuhusu kupigwa risasi Tundu Lissu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zaidi ya Watanzania 380 wanatajwa kupotezwa ‘MKIRU’, Bunge lichunguze kama lilivyochunguza Operesheni Tokomeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, 12 Juni, 2017 mchana Bi, Ziada Salum wa kitongoji cha Maparoni Wilayani Kibiti alikuwa nyumbani kwake akipika chakula cha familia yake, wakati ambao Jeshi la Polisi lilifika na kumchukua kwa ajili ya kwenda kumhoji. Ni Miezi 11 leo tangu Bi. Ziada Salum achukuliwe, hajarudishwa mpaka leo, familia yake haijaarifiwa chochote, bado imekaa na matarajio kuwa ipo siku atarudi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwezi huo wa Juni, 2017, si Bi Ziada tu aliyechukuliwa na kutokurudishwa mpaka leo, kwa staili ya namna hiyo ni wengi mno. Wakiwemo kina mama wa familia moja, Rukia, Muhohi na Tatu, Muhohi wa kitongoji cha Msala, hapo hapo Wilayani Kibiti, wao wakichukuliwa kwenda kuhojiwa na Jeshi la Polisi 26 Juni, 2017 na mpaka leo hawajarudishwa. Kaka yao Nassoro Muhohi yeye alichukuliwa 27 Juni, 2017 kisha kuachiwa (najua kwa kumtaja hapa Bungeni anaweza kuchukuliwa tena na mara hii kupotea kabisa).

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitongoji hiki cha Msala kimewapoteza wengi, akiwemo Jumanne Rashid Pango, aliyechukuliwa naye siku moja pamoja na Rukia na Tatu Mhohi. Ni miezi zaidi ya 10 leo, watu hawa wote Jeshi la Polisi halijawarudisha, lakini pia halijatoa maelezo yoyote kwa ndugu zao juu ya walipo na lini watawarudisha?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kina Muhohi si ndugu pekee waliochukuliwa na Jeshi letu la Polisi na kutokurudishwa mpaka leo, katika Kata ya Mjawa, Wilayani Kibiti ndugu watatu wa familia moja nao walichukuliwa 2 Juni, 2017, hao ni Hamisi Omari Nyumba na mwanawe, Sadam Hamisi Nyumba pamoja na nduguye, Juma Omari Nyumba. Nao Jeshi la Polisi limebaki nao mpaka leo, halijawarudisha, hatujui kama bado wako hai ama ni sehemu ya miili iliyookotwa kwenye fukwe zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sio hao tu, 10 Julai, 2017, katika Kitongoji cha Nyantimba, Wilayani Rufiji, Jeshi la Polisi liliwachukua watu watatu, bwana Hamis Mketo, Bi Tabia Nyarwamba na Bi. Pili Mkali nao wakielezwa wanakwenda kuhojiwa, kama ilivyo kwa hao wengine, nao hawajarudishwa mpaka leo, zaidi ya miezi tisa sasa. Orodha niliyonayo hapa ni kadhia 68 za namna hii, kadhia 62 zikiwa zimezithibitisha, kadhia nane nikiwa naendelea na uchunguzi. Kwa sababu ya muda niishie kutaja hao tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kadhia za namna hii ni nyingi mno na yeyote kati yetu, akipata wasaa tu wa kwenda MKIRU (Mkuranga, Kibiti na Rufiji) ataelezwa mambo haya kwa undani, makadirio ni kuwa zipo kesi zaidi ya 380 za namna hii za watu kuchukuliwa na kutorudishwa kwa zaidi ya miezi 10 sasa, hizo ni tofauti na zile za watu waliokamatwa, kuteswa na kisha kuachiwa au wale waliojeruhiwa kwa kupigwa risasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo MKIRU tu, bali ukanda wote wa Kusini, wiki mbili zilizopita, Mbunge wa Kilwa Kusini Mheshimiwa Suleiman Bungara ‘Bwege’ (CUF) naye alieleza kadhia za watu 10 wa Jimboni kwake Kilwa, kuchukuliwa Msikitini na Jeshi letu la Polisi, kupigwa risasi wengine kutokurudishwa mpaka leo na kuhisiwa kuwa wameuawa, wengine kurudishwa wakiwa na vilema vya kukatwa masikio, kuchomwa ndevu kwa moto na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, najua haja ya kudhibiti hali mbaya ya usalama iliyojitokeza mwaka jana. Mauaji yale ya Askari Polisi na raia yaliyokuwa yakiendelea MKIRU yalipaswa kukomeshwa, lakini bado ukomeshwaji husika ulipaswa kufanyika ndani ya utaratibu wa kisheria tuliojiwekea kama Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa haya yanayoripotiwa sasa kutoka MKIRU, ni dhahiri kuwa utaratibu wa kisheria ulikiukwa, haki za binadamu zilivunjwa, raia wema na wasio na hatia waliuawa na jeshi ambalo lilipaswa kuwalinda na wananchi wengi wakiwa wamepotea tangu wachukuliwe kwenda kuhojiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mambo ya namna hii si mapya hapa nchini mwetu, hayana nia nzuri ya kudhibiti jambo baya, bali hutumika kuwaumiza wananchi. Mwaka 2013 nchi yetu ilikumbwa na janga kubwa la ujangili, tembo na faru wetu wakiuawa na magenge ya wahalifu. Kwa nia njema ya kudhibiti ujangili huo, Serikali kwa kutumia majeshi yetu, ilianzisha Operesheni ya kutokomeza Ujangili huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kipindi kifupi cha Operesheni husika, malalamiko juu ya wananchi kubakwa, kuteswa, kuuawa, kuporwa mali zao na mengine mengi mabaya ya unyanyasaji wa raia yaliripotiwa. Unyanyasaji na ukiukwaji huo wa haki za binaadam wa wananchi wetu uliripotiwa Wilayani Babati, Mkoani Manyara; Tarime, Mkoani Mara; Kasulu, Mkoani Kigoma; Meatu, Mkoani Simiyu; Ulanga, Mkoani Morogoro; Urambo na Kaliua, Mkoani Tabora; pamoja na maeneo mengine ya nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, malalamiko ya wananchi yaliletwa hapa Bungeni. Bunge letu lilichukua hatua juu ya malalamiko hayo. Kwanza kwa kuitaka Serikali kusitisha Operesheni Tokemeza na kisha kwa kuunda Kamati Teule ya Bunge, kuchunguza juu ya utekelezwaji wa Operesheni Tokomeza. Kamati Teule ilithibitisha ukweli wa madai ya wananchi kunyanyaswa, kuuawa, haki zao kubinywa na kadhalika na hatua kadhaa njema zilichukuliwa ili kurekebisha jambo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, malalamiko ya MKIRU ni makubwa mno, unyama unaoripotiwa kufanywa huko na vyombo vyetu vya ulinzi na usalalma hata hauelezeki, umehusisha kupotezwa kwa watoto, akinamama na wazee, haukujali jinsia wala rika, kadhia chache nilizozielezea hapa zimeonesha taswira ya maumivu na ukubwa wa jambo hilo, zaidi taarifa juu ya kupotea kwa watu zaidi ya 380 zikishtusha na kuamsha hisia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Mkutano Mkuu wa CCM wa mwaka 1987, Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere alisema yafuatayo:-

“Panapokuwa hapana haki, wala imani na matumaini ya kupata haki, hapawezi kuwa na amani wala utulivu wa kisiasa. Hatima yake patazuka fujo, utengano na mapambano”.

Mheshimiwa Mwenyekiti, watu hawa wa MKIRU na Kusini kwa ujumla ni ndugu zetu, kaka na dada zetu, ni Watanzania wenzetu ambao tuko humu Bungeni kuwawakilisha. Unyama huu unaosemwa kufanywa dhidi yao umewaondolea kabisa Haki yao ya uhai, umewaondolea Imani ya kupata ulinzi wa Vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama, Bunge letu lichunguze jambo hili kuwapa Matumaini ya kupata haki, ili wasibaki na vinyongo na ili wasichague fujo, utengano na mapambano kama njia ya kuponya majeraha yao na kudai Haki zao zilizominywa. Sisi Bunge tunao wajibu huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hivyo basi, kwa maelezo hayo niliyoyatoa, kwa mujibu wa Kanuni ya 120(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, naomba kutoa taarifa kwamba nitatoa hoja binafsi kutaka Bunge lako Tukufu Kamati Teule kufanya uchunguzi kuhusu kadhia za Mauaji, kupotea, kupigwa Risasi, kuteswa watu wa MKIRU na Kusini kwa ujumla. Ni imani yangu kuwa Wabunge wenzangu wataunga mkono jambo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wa kigoma si Watanzania? Uhamiaji na NIDA watueleze tukatafute nchi yetu? Jambo la pili ninalotaka kulizungumzia ni juu ya suala la uraia kwa watu wa mikoa ya mipakani mwa nchi, zaidi kwetu sisi watu wa Mkoa wa Kigoma. Nchi yetu inapakana na nchi majirani nane, zikiwemo nchi za Kenya na Uganda upande wa kaskazini; Msumbiji, Malawi na Zambia upande wa kusini; na Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa upande wa magharibi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi wa upande wa magharibi, hasa tunaopakana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Burundi ndio tunaosumbuka na haya masuala ya uraia kwa kiasi kikubwa kuliko watu wengine wa mikoa ya mipakani. Kiasi kwa sasa limekuwa ni jambo la kawaida kabisa kwa mtu yeyote mwenye asili ya Mkoa wa Kigoma, aliyekwaruzana au kusigana na Serikali kuitwa na kuhojiwa na Idara ya Uhamiaji au kutakiwa kuthibitisha uraia wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, orodha ya matukio ya namna hiyo ndefu sana, sina haja ya kuisema hapa, lakini wahanga wa karibuni wa kadhia za namna hiyo ni Abdul Nondo, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, UDSM na kiongozi wa Mtandao wa wanafunzi nchini, TSNP; pamoja na Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), ndugu Zacharia Kakobe, ambao wote waliitwa kuhojiwa na Idara ya Uhamiaji kwa sababu ya misigano waliyonayo na Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiacha hilo la watu wengi wenye asili ya Mkoa wa Kigoma, wenye mikwaruzano na Serikali kuitwa kuhojiwa na Idara ya Uhamiaji, sasa limeibuka tatizo kubwa zaidi na hili linatuhusu karibu wananchi wote wa Mkoa wa Kigoma, ugumu katika upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa kutoka NIDA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wa Kigoma tunasumbuliwa mno kupata vitambulisho, katika wakati ambao ni 13.4% tu ya Watanzania wote ndio wana vyeti vya kuzaliwa, haitegemewi kuwa hicho kitumike kuwa kikwazo cha sisi kunyimwa vitambulisho. Zaidi hata wananchi wanaokwenda na viapo nao wanasumbuliwa, wakati wanatumia gharama kubwa kuvipata viapo husika, wakivifuata mjini kwenye huduma ya Mawakili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wa Kigoma ni maskini, mkoa wetu ni moja ya mikoa masikini zaidi nchini, ni mkoa pekee hapa Tanzania ambao haujaunganika kwa mtandao wa barabara za lami na mikoa mingine nchini, haya pekee yalitosha kuifanya Serikali kututazama kwa jicho la huruma. Lakini sivyo, hata Utanzania wetu, uraia wa nchi yetu tunahojiwa, tukinyanyaswa na kutendewa kama watu wa daraja la pili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatuyaoni haya kwa Wadigo wa kule Horohoro, au Wamasai wa Longido, kama ambavyo hatuyaoni haya tunayotendewa watu wa Kigoma, kwa watu wa Nachingwea na Nanyumbu, au Nyasa na Tunduma. Kwa nini sisi tu watu wa Kigoma tunasumbuliwa zaidi kuhusu masuala ya uhamiaji? Kwa nini sisi watu wa Kigoma ndio tunapata zaidi tabu kupata vitambulisho vya Uraia kutoka NIDA? Kwa nini ni sisi tu? Naamini Waziri atakuja na majibu juu ya suala hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bunge tulipuuza kupotea kwa Saanane, tusipuuze kuchunguza kupotea kwa Azory na Kanguye. Mwaka jana Aprili, 11 nilizungumza humu Bungeni wakati nikichangia Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, juu ya kupotea kwa ndugu Ben Saanane, kijana wa Kitanzania, kupotea ambako kulihusishwa na Idara ya Usalama wa Taifa, ikielezwa kwamba alishikiliwa na kisha ‘kupotezwa’ na watu wanaohisiwa kuwa ni Maafisa wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika maelezo yangu yale, nilitoa wito kwa Bunge lichukue hatua kufanya uchunguzi juu ya jambo hilo, kwanza ili kupata ukweli juu ya matukio yaliyokuwa yameanza ya watu kupotea tu bila maelezo ya kina, pamoja na kulinda hadhi ya Idara ya Usalama wa Taifa ambayo ilitajwa kuhusika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni bahati mbaya kuwa wito wangu wa Bunge kufanya uchunguzi haukupata uungwaji mkono. Wakati natoa hotuba ile, ilkuwa ni miezi sita tangu ndugu Saanane apotezwe, leo ni mwaka mmoja na nusu, familia yake, ndugu na wazazi, wamebaki na simanzi ya kutojua nini kimetokea kwa kijana wao. Idara yetu ya Usalama wa Taifa imebaki na doa la kuhusishwa na kupotea kwake na nchi yetu imechafuka, kwa taswira yake kuwa ni nchi ya usalama na amani kupotea na Bunge letu likionekana dhaifu kwa kutokuchukua hatua ya kuchunguza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi ndani ya Bunge hili tunayo dhima na wajibu, tumekasimishwa na Watanzania wenzetu mamlaka na madaraka ya kuwasemea, kuisimamia Serikali kwa niaba yao, kuhakikisha juu ya usalama wao. Kwenye jambo hili la ndugu Saanane tumeshindwa kutimiza wajibu wetu, tumeshindwa kuhoji juu ya usalama wake, hasa ikiwa Idara yetu ya Usalama wa Taifa ndiyo inayotajwa juu ya kupotea kwake, hatujafanya kazi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kushindwa kwetu kuhakikisha tunachunguza suala la ndugu Saanane kumetoa mwanya wa matukio ya namna hiyo ya watu kupotezwa tu kuendelea bila kukoma, sasa karibu yataonekana ni matukio ya kawaida. Labda kwa kuwa Saanane ni kijana wa upinzani tuliona tu kuchunguza juu ya kupotea kwake, tukidhani ni jambo lingeishia tu kwa watu wa upinzani, lakini kupuuza kwetu kumepelekea kupotea kwa ndugu Simon Kanguye, huyu ni Diwani wa CCM na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibondo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mazingira ya kupotea kwa ndugu Kanguye hayana tofauti na mazingira ya kupotea kwa ndugu Saanane, yeye aliitwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, kukutana na DSO(Afisa Usalama wa Wilaya) wa Kibondo, tangu hapo hajaonekana, akiwa amepotea siku moja kabla ya ziara ya Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa hapo kwenye Hamashauri ya Kibondo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kanguye amepotea tangu Julai, 2017, miezi miwili na siku10 tangu Bunge likatae wito wangu wa kuchunguza kupotea kwa Ben Saanane. Naamini sisi Bunge tungechunguza juu ya kupotea kwa Ben labda asingepotea, labda angekuwa na familia yake, au barazani na Madiwani wenzake kule Kibondo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo ni miezi tisa na nusu tangu Kanguye apotee, mkewe na wanawe wamekwenda kila mahali kutaka msaada wa kupatikana kwake, mie huyu ni mjumbe mwenzangu wa RCC, nimehoji huko, sijapata majibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miezi minne tangu kupotea kwa Kanguye, akapotea Azory Gwanda, baba, mume na Mwandishi wa Habari za Uchunguzi, akiandikia hasa Magazeti ya Kampuni ya Mwananchi, kupotea kwake kumehusishwa na habari za Kibiti ambazo amechunguza na kuandika mno. Kama ilivyo kwa Saanane na Kanguye, maelezo ya kupotea kwa Azory (kwa mujibu wa mkewe) yamehusisha tena watu wetu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, waliomchukua 21 Novemba, 2017 nyumbani kwake na kutokuonekana mpaka leo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo ni miezi mitano na nusu tangu Azory apotee, mkewe, dada yetu Anna Pinoni aliyekuwa mjamzito,amejifungua Februari mwaka huu, binti yao sasa ana miezi mitatu, mnaweza kuwaza huzuni, upweke, mfadhaiko na msongo wa mawazo aliyonayo mama huyu. Kuachwa mjane, kuachwa na ujauzito na sasa kulea mtoto akiwa mpweke bila ya mzazi mwenzake. Mimi nikiwaza jambo hili naumia sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Bunge letu haliwezi kuwa msaada kwa Anna Pinoni, kuibana Serikali ieleze alipo mumewe, kuhakikisha anarudishwa kwake salama ili asibaki mjane binti yake asibaki yatima, basi litapoteza maana na uhalali wake kwa wananchi wanyonge. Hali ya mke wa Azory ndiyo aliyonayo mke wa Kanguye pamoja na watoto wao, ndiyo waliyonayo wazazi wa Ben Saanane.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi Wabunge hatukutimiza wajibu wakati wa suala la Ben Saanane, tuutimize sasa kwa kuchunguza matukio haya ya watu kupotezwa huku vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama vikihusishwa. Narudia wito wangu kwenu Wabunge wenzangu, kwa heshima na taadhima, tuunde Kamati Teule ya Bunge kuchunguza mambo haya, huu ni wajibu wetu kwa wananchi wenzetu. Tuutimize.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Kanuni ya 120(2) ya Kanuni za Bunge natoa taarifa kwamba nitatoa hoja binafsi kutaka Bunge lako Tukufu kuunda Kamati Teule kufanya uchunguzi kuhusu vitendo vya utekaji, upotezwaji na mauaji dhidi ya raia (likiwemo suala la Ben Saanane, Simon Kanguye na Azory Gwanda).

Mheshimiwa Mwenyekiti, naamini Waheshimiwa Wabunge wenzangu wataniunga mkono kwenye jambo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mauaji, utekaji na uteswaji unaendelea kwenye Wilaya za Kusini Pwani (Mkuranga, Kibiti, Rufiji – MKIRU). Natambua umuhimu wa kudhibiti usalama wa ndani yetu lakini nalaani mauaji ya raia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nalitaka Bunge kuunda Kamati Teule kuchunguza vifo vya raia Wilaya za MKIRU na Kilwa. Watu takribani 348 wamepotea/kufa ndani ya mwaka mmoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi za inayoitwa Task Force inayoteka, kutesa na kuua watu ni lazima ichunguzwe na Kamati Teule ya Bunge. Bunge haliwezi kuacha raia wake wanauawa hovyo kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia Wizara hii. Nina mambo mawili tu ya kuchangia.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la kwanza ni mambo ya jimboni; napenda nitoe shukrani za dhati kwa Mamlaka ya Bandari Tanzania kwa miradi ambayo imeanza kuifanya katika Mkoa wa Kigoma katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, Bandari ya Ujiji, Bandari ya Kibirizi na Bandari ya Nchi Kavu ya Katosho. Bandari ya Nchi Kavu ya Katosho umuhimu wake ni kuhakikisha kwamba Kigoma inakuwa ni kituo cha biashara kama ambavyo imekuwa siku zote kwamba eneo la Ujiji na Kigoma ni eneo la biashara la Maziwa Makuu na hivyo kuwezesha mizigo ambayo inatoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda Burundi au kwenda Mashariki ya Congo upande wa Kaskazini ya Mashariki ya Congo watu waweze kuichukua pale Kigoma, kuifanya Kigoma ni plot of destination. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo Mamlaka ya Bandari kwa kazi hizi ambazo wanaendelea kuzifanya na maeneo mengine nimeona bajeti wamepanga ya shilingi bilioni 548 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya Mamlaka ya Bandari nchi nzima, ni kazi ambayo ni nzuri kwa sababu maendeleo yake yanaendana na maendeleo ya jumla. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, niombe Wizara itupatie majibu ni kwa nini kama jinsi alivyoongea Mheshimiwa Nsanzugwanko jana, ni kwa nini Mradi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma unazidi kucheleshwa? Tunafahamu kwamba manunuzi yameshakamilika toka mwezi Januari, 2018, sasa hivi ni mwezi Mei, 2019, hatujaona chochote ambacho kinafanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kigoma, viwanja vingine tunaona vikijengwa, vingine vipya havikuwepo kabisa vinajengwa, kwa nini mradi ambao tayari una fedha kutoka European Investment Bank unaendelea kucheleweshwa mpaka sasa hivi? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine, tuna mradi mkubwa sana wa takribani dola milioni 40 wa upanuzi wa Bandari ya Kigoma ambao unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA). Juzi niliona Mheshimiwa Waziri wa Fedha akiwa amezungumza na watu wa JICA alivyokuwa kule Washington, lakini mpaka sasa hatujaona taarifa yoyote ile kuhusiana na mradi huu wa Kigoma. Nilivyofuatilia niliambiwa kwamba kuna masuala ya kikodi na kadhalika, nadhani kuna haja ya Serikali kuweza kuona vitu ambavyo msaada huu kutoka Japan wanaomba viingie bila kulipia kodi kama faida yake ni kubwa kuliko mradi wenyewe kwa ujumla wake, kwa sababu kuingiza dola milioni 40 katika Mji wa Kigoma kwa ajili ya ujenzi wa Bandari ya Kigoma nadhani una faida kubwa zaidi kuliko VAT ambayo wanaomba iwe exempted kwa ajili ya kuingiza vifaa vyao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo naamini kabisa kwamba Wizara na hasa Wizara ya Fedha na Mheshimiwa Waziri Mpango yupo hapa, watahakikisha jambo hili linakamilika sababu mwezi huu Mei ulitakiwa mradi uwe umeanza, mpaka sasa Wizara ya Fedha bado haijasaini mkataba na JICA kwa ajili ya mradi huu, zabuni zitangazwe ili uweze kuanza.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa lingine ni suala la kinchi la kiujumla. Mheshimiwa Silinde amezungumza hapa, toka tumeanza Awamu ya Tano fedha ambazo tumeziingiza Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi ni asilimia 46 ya bajeti yote ya maendeleo ya nchi yetu. Jumla ya fedha ambazo tumeziingiza Wizara hii ni trilioni 18.7 na fedha ambazo za ujumla za bajeti ya maendeleo ya nchi ni trilioni 40.6. Kwa hiyo 46 percent ya bajeti ya maendeleo anaishika Mheshimiwa Kamwelwe na Manaibu wake wawili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Wabunge wana haki ya kuuliza kiasi hiki cha fedha ambacho tumekiingiza mpaka sasa kimezalisha viwanda vingapi? Kwa sababu tunazungumza kuhusu forward and backward linkages, tunazungumza kuhusu namna gani ambavyo fedha tunazoziingiza kwenye miradi kama reli, miradi kama ndege ni namna gani ambazo zinachochea sekta nyingine za uchumi. Kwa hiyo, tungepata maelezo ya Serikali hapa kwamba tumeingiza trilioni 18.7, nini multiplier effect ya hili na Mheshimiwa Waziri Mpango analijua vizuri sana. Moja ya sekta ambayo ina-multiplier effect kubwa ni construction sekta. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa nini sisi ambao tunaingiza fedha nyingi namna hii bado kasi ya ukuaji wa uchumi iwe ni ndogo, leo hii tunabishania makisio ambayo haya IMF wameyatoa ya four percent na kadhalika, IMF Mheshimiwa Waziri Mpango hawajakanusha kuhusu makisio hayo, wamekanusha ripped report lakini makisio ni yale yale, lakini hata usipochukua makisio ya IMF chukua makisio ya Serikali ya six percent before Serikali ya Awamu ya Tano kuingia madarakani economy yetu ilikuwa inakua kwa seven percent for 10 years. Serikali ya Awamu ya Tano imeingia madarakani 18 trillion shillings zimeingizwa kwenye construction sector, growth rate iko chini kwa nini? Haya ndio masuala ambayo Wabunge tunapaswa kuiuliza Serikali, (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Kenya wamejenga ile SGR ya mkopo wenyewe ghari sana na wote tunajua, lakini mchango wa ujenzi building construction kwenye growth rate ilikuwa 1.5 percent, iweje sisi warithi growth rate ya seven percent halafu ndani ya miaka mitatu baada ya ku-inject all the money tushuke, nimesema waachane na four percent ya IMF, waende na six percent ya Serikali, why? Ni kwa sababu utekelezaji wetu wa mipango ya maendeleo ya miundombinu ni utekelezaji unaotoa fedha kwenda nje, hauingizi ndani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ndio maana mzunguko wa fedha ni mdogo sana kwa sababu wamewapa kazi wakandarasi wa nje, wanaagiza raw materials kutoka nje, every single cent amount ya nchi yetu inapelekwa nje, wanakusanya kodi kwa muuza nyanya, wanaenda kumlipa Mturuki anapeleka Uturuki, ndio maana uchumi haukui. Hata wajenge argument namna gani. Nimeona argument ya Serikali kwenda IMF kusema makisio haya ni makosa kwa sababu tuna miradi mikubwa, tuna SGR, tuna sijui Stiegler’s Gorge, argument ile haina maana kwa sababu all the money zinaenda nje na debt service yetu, huduma yetu ya Deni la Taifa ni kubwa...(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Zitto kuna taarifa hapo, Mheshimiwa Waziri wa Fedha.

T A A R I F A

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, naipokea taarifa ya Mheshimiwa Waziri Mpango. Ninachotaka kumwambia Mheshimiwa Waziri Mpango kwanza anajua kwamba mamlaka ya economic surveillance ya dunia ni moja, ni IMF na anafahamu kwa sababu amefanya kazi huko, Benki ya Dunia, African Development Bank na hata Wizara yetu ya Fedha makisio wanayoyatumia ni makisio ya IMF, sio makisio mengine yoyote na anafahamu, labda atakataa kwa sababu lazima a-defend Serikali hapa, lakini najua anafahamu hivyo. Hata hivyo, point yangu ni kwamba, wastani wa over a decade thus why tulikuwa sisi ni the fastest growing economy, wastani wa over a decade ni seven percent, sawa we can debate about that... (Makofi)

NAIBU SPIKA: Nashauri Waheshimiwa Wabunge ongeeni huku ili iwarahisishie kwenda na mazungumzo mnayotaka kuzungumza, mkianza kutazama wenyewe huko ndio hayo mnaanza kujibizana wenyewe, zungumza na mimi huku ili usipate wakati mgumu kuona mtu amekataa jambo lako.

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. Naomba nichukue takwimu za Mheshimiwa Waziri Mpango, yeye ni mchumi anajua, panapokuwa na depression, panapokuwa na mdororo wote wa uchumi kwa kutumia fiscal Policy Serikali ina-pump in money kwa ajili ya kuchochea uchumi, over the last three years, tume-pump 18.7 trillion kwenye construction. Naomba nijibiwe, hii fedha ambayo tumei-pump tumezalisha viwanda vingapi, tumezalisha ajira za kudumu ngapi, sekta ya kilimo imechochewa namna gani, ndio maana ya multiplier effect na ndio swali langu hili na wakati mwingine tunapozungumza wala hatuna nia mbaya, nia yetu ni kuhakikisha kwamba tunakwenda pamoja as a country, hakuna mtu ambaye hataki nchi yake iendelee, so there is no haja ya kuwa defensive. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukweli ni kwamba utekelezaji wa sera za kiuchumi wa nchi yetu over the last four years ni utekelezaji mbovu, ni utekelezaji fyongo, ndio maana pumping in of money, 20 percent ya development budget tunayoiingiza, haichochei uchumi inavyotakiwa.

T A A R I F A

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, sipokei taarifa ya dada yangu na namtakia mfungo mwema wa mwezi wa Ramadhani na ajiepushe sana kutumia maneno kupotosha kwa sababu mimi siwezi kutumia hayo dhidi yake.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna tofauti kubwa sana kati ya kasi ya ukuaji wa uchumi na uchumi. Sekta ya ujenzi ni ya pili kwenye kasi ya ukuaji, sio ya pili kwenye uchangiaji wa uchumi. Sekta ya ujenzi inachangia kidogo sana kwenye uchumi, ni ya pili kwenye ukuaji, we have to pump in all this money, lakini huo wa pili wake hauonekani kwenye uchumi wa ujumla wake na ndio argument yangu, kwamba almost half mama ya development budget.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Ongea na kiti mwache Mheshimiwa Dkt. Ashatu.

MHE KABWE. Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, nusu ya fedha zako za maendeleo unaziingiza kwenye sekta moja, Wizara moja unapaswa uone namna ambavyo sekta zingine zimeinuliwa na ndio maana maswali hapa nimeuliza. Serikali ije kutujibu hii investment ambayo tumefanya imezalisha viwanda vingapi?

Mheshimiwa Naibu Spika, construction sector impact yake sio long term inaanza na short term, mfano mzuri, anaweza akawa ni kijana anatengeneza screw za ujenzi wa reli, akapata kazi, screw tu ni moja ya kiwanda ambacho kinaweza kikatengeneza wakati huo na akiendelea maana yake wawe wamefanya transfer of technology, wameajiri, wame-train ataendelea na ile kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ninachokiomba, muundo wetu wa mipango ya kiuchumi na utekelezaji wa miradi yetu iangalie backward and forwarding linkages ili fedha ambayo tunaiingiza public investment ambayo tunaifanya iweze kuwa na faida zaidi kwa nchi yetu kwa ujumla wake. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimalizie mambo mawili…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Spika, kwa nini Serikali inachelewesha miradi ya maendeleo ya miundombinu ya Mkoa wa Kigoma?

Mheshimiwa Spika, kwanza nitoe shukrani zangu za dhati kwa Mamlaka ya Bandari Tanzania kwa kuendelea kuamini katika maendeleo ya Mkoa wa Kigoma na hususan Mji wa Kigoma kwa kuwekeza katika ujenzi wa Bandari Kavu ya Katosho pamoja na ujenzi wa Bandari ndogo za Kibirizi na Ujiji.

Mheshimiwa Spika, miradi hii mitatu ikikamilika itawezesha uwepo wa gati katika eneo la mji wa asili wa kibiashara wa Ujiji na kuwezesha ndoto yetu ya kurejesha hadhi ya Ujiji katika maendeleo ya nchi yetu. Mradi wa Bandari kavu ya Katosho utawezesha mizigo ya nchi za DRC, Zambia na Burundi inayopitia bandari ya Dar es Salaam kuchukuliwa Kigoma na hivyo kurahisisha biashara na hichi hizo jirani. Mamlaka ya Bandari pia wanajenga jengo la OSBC (One Stop Center) ambayo itarahisisha shughuli za ukusanyaji kodi, biashara na uhamiaji.

Mheshimiwa Spika, ni matarajio yetu kuwa TRC wanajiandaa nao ili ukamilikaji wa miradi hii uende sambamba na uwepo wa reli ya kusafirisha kwa urahisi mizigo ya Zambia, DRC na Burundi. Mambo haya yataingiza fedha kwenye mzunguko wa uchumi wa Mkoa wa Kigoma na kutoa ajira kwa wananchi wenzangu wa Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Mheshimiwa Spika, nampongeza Mkurugenzi Mkuu wa TPA kwa kuendeleza miradi hii na hii ni ishara ya imani yake kwa ukuaji na maendeleo ya mji wetu na mkoa wetu wa Kigoma.

Mheshimiwa Spika, vilevile napenda kumpongeza Meneja wa TANROADS Kigoma kwa kuwezesha mikataba ya Barabara ya Manyovu - Kasulu - Kibondo (mpaka Nyakanazi) kupitia ufadhili wa AFDB na barabara ya Uvinza - Darajani kupitia Kuwait Fund. Miradi hii ni muhimu kwa Mkoa wa Kigoma kwa kuwa itauunganisha Mkoa wa Kigoma na Mikoa mingine na kurahisisha usafirishaji wa mazao na bidhaa.

Mheshimiwa Spika, pamoja na shukrani hizo kwa watu wa TPA na TANROADS bado watu wa Kigoma wanalia kwa kuwa ipo miradi yao ya msingi inayokwamishwa na Serikali. Licha ya Jumuiya ya Kimataifa kuelewa umuhimu wa Mkoa wa Kigoma kijiografia na kiuchumi na hivyo kutoa fedha za miradi ya maendeleo itakayochochea shughuli za kiuchumi, Serikali ya CCM imekuwa inavuta miguu kutekeleza miradi hiyo. Nitawapa mifano michache ya namna Serikali ya CCM inavyohujumu Mkoa wetu wa Kigoma.

Mheshimiwa Spika, moja, Serikali ya Japan imeidhinisha mradi mkubwa wa kuboresha Bandari ya Kigoma wenye thamani ya dola za Marekani milioni 40 (karibu shilingi za Kitanzania bilioni 100), lakini kwa mwaka mzima sasa Wizara ya Fedha haitaki kusaini mkataba ili zabuni itangazwe na kazi ianze. Fedha hizi ni msaada, siyo mkopo.

Mheshimiwa Spika, pili, hoja ya Serikali ni kuwa Serikali ya Japan inataka msamaha wa Kodi ya VAT kwenye mradi huu, nayo haitaki. Sasa tunapewa mradi wa shilingi bilioni 100, bure, kisha tunataka na VAT kwenye vifaa vinavyofumika kwenye mradi huo huo kweli! Serikali inaweza kupata mapato mengi mno ya kodi ikiwa mradi huu wa upanuzi wa bandari ya Kigoma utafanyika. Kwa nini waukwamishe kwa mapato kiduchu tu ya VAT ya sasa? Kwa nini Serikali haioni picha kubwa?

Mheshmiwa Spika, tatu, Jumuiya ya Ulaya (EU) kupitia Benki yao ya Uwekezaji (European Investments Bank) wameidhinisha fedha, dola milioni 20 sawa na shilingi za Kitanzania bilioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la abiria katika uwanja wa ndege wa Kigoma na kuupanua uwanja ili ndege kubwa zitue kwa ajili ya kuunganisha nchi za maziwa makuu na Mji wetu. Tangu mwaka 2018 Januari, zabuni imetangazwa, mpaka leo kazi haijaanza wakati uwanja wa ndege wa Chato ambao haukuwa kwenye Bajeti ya Serikali wala mpango wa maendeleo umejengwa na kukamilika. Serikali inataka kuwaambia nini watu wa Kigoma? Wao sio Watanzania kuliko ndugu zao wa Tabora?

Mheshimiwa Spika, nne, hata miradi ambayo fedha tayari zipo, haifanywi. Kwa mfano, Manispaa ya Kigoma Ujiji tuna mradi mkubwa wa kuweka pavements kwenye mitaa yetu ili kutoa maarifa ya ufundi na kisha ajira kwa vijana. Lengo la mradi huu ni kutumia shughuli za ujenzi wa miundombinu kwa ajili ya kuongeza ajira kwa vijana na mzunguko wa fedha kwa wananchi kwa vijana na wanawake kupewa mafunzo ya ujenzi wa hizo barabara za mawe (pavements) na kisha kupitia vikundi vyao kupewa kazi hizo za ujenzi.

Mheshimiwa Spika, Serikali imegoma kusaini mkataba wa Mkandarasi Mshauri kwa ajili ya kufanya upembuzi na usanifu wa mradi huu pamoja na kuwa mfadhili wa mradi, Serikali ya Ubelgiji iko tayari na fedha ziko tayari. Mradi huu ambao ungehusu kata nane za Manispaa ya Kigoma Ujiji ungekuwa ni ‘Game Changer’ kwa uchumi wa Kigoma. Nao unakwamishwa. Kwa nini?

Mheshimiwa Spika, watu wa Kigoma ni wavumilivu sana. Wamevumilia kwa zaidi ya miaka hii 58 ya Uhuru wa Tanganyika na 55 ya uwepo wa Tanzania bila kuunganishwa na mkoa wowote, wakatengwa kiuchumi. Uvumilivu huo una kikomo, hasa ikiwa ni kwa miradi yao ya miundombinu na uchumi inahujumiwa namna hii. Serikali isiwafikishe huko.

Mheshimiwa Spika, Bajeti ya Wizara hii ilipaswa ichochee ukuaji wa uchumi, kwa nini uchumi unadumaa?

Mheshimiwa Spika, mgawo wa bajeti ya maendeleo kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano ni ufuatao: 2016/2017 shilingi trilioni 4.8 ambayo ilikuwa 40.3 % ya bajeti yote ya maendeleo ya shilingi trilioni 11.8. Mwaka 2017/2018 shilingi tirilioni 4.9 ambayo ilikuwa 40.8 % ya bajeti yote ya maendeleo ya shilingi trilioni 11.9. Mwaka 2018/2019 shilingi trilioni 4.1 ambayo ilikuwa 34.5 % ya bajeti yote ya maendeleo ya shilingi trilioni 12.0.

Mheshimiwa Spika, mpaka mwaka huu wa fedha unaoisha 2018/2019 Bunge litakuwa limeidhinisha kwa Wizara hii jumla ya shilingi trilioni 13.8 katika miaka mitatu ya bajeti. Ni wastani wa 38.5% ya bajeti yote ya maendeleo kwa miaka hii mitatu. Tukipitisha bajeti ya 2019/2020 tutakuwa tumewekeza jumla ya shilingi trilioni 40.6 na kati ya hizo shilingi 18.7 zitakuwa zimekwenda Wizara hii ya Miundombinu. Hii ni sawa na 46% ya Bajeti yote ya maendeleo kwa miaka minne kati ya mitano ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Mheshimiwa Spika, ni halali kabisa kwa Wabunge kuhoji: ajira ngapi za kudumu zimetengenezwa kutokana na uwekezaji huu? Sekta zipi nyingine za uchumi zimechochewa (multiplier effect) kutokana na uwekezaji huu? Kwa Mfano, viwanda vingapi vya chuma vimeanzishwa? Pato la Taifa limeongezeka kwa kiasi gani kutokana na uwekezaji huu? Watanzania wangapi wameondokana na umasikini? Mapato ya Serikali yameongezeka kwa kiasi gani?

Mheshimiwa Spika, kikawaida ni Bajeti ya Wizara hii ndiyo ambayo matumizi/manunuzi yake hutumika kuchochea shughuli za kiuchumi na kupeleka fedha kwa wananchi kupitia miradi mbalimbali ya ujenzi. Hali iko hivyo duniani kote, lakini hapa nchini kwetu hali ni tofauti, manunuzi mengi ya ujenzi yanayofanywa kupitia Wizara hii hayajachochea ukuaji wa uchumi, bali namna yalivyofanyika yamekuwa ni sababu ya kudumaza uchumi.

Mheshimiwa Spika, Serikali hii ilirithi Bajeti ya Serikali ya Awamu ya Nne ya Mwaka wa Fedha wa 2015/2016 ilipoingia madarakani Novemba 5, 2015. Katika wakati husika kasi ya mzunguko wa fedha nchini (M3) ilikuwa ni 15%. Hivyo kila shilingi nchini ilibadilisha na wastani wa mikono 15 kwenye matumizi ya kiuchumi. Ripoti ya BOT ya Mwezi Machi, 2019 (inayoelezea hali ya Februari, 2019) inaonyesha kuwa M3 kwa sasa ni 3% tu. Mzunguko wa fedha umepungua mno.

Mheshimiwa Spika, kwa miaka mitatu tumepitisha Tanzania Shillings 1.5 trillion kununua ndege. Fedha zote hizo zimekwenda nje ya nchi, hakuna hata shilingi moja kati ya hizo ambayo imerudi nchini. Hiyo ni moja ya sababu ya kupungua kwa mzunguko wa fedha nchini.

Mheshimiwa Spika, tuna ujenzi wa SGR. Mkataba wa Ubia Kati ya Kampuni ya Yapi Merkezi ya Uturuki na kampuni ya Construção Africa SA ya Ureno, naambiwa Kampuni hii imejitoa kwenye mkataba huu na kwamba kuna Kampuni nyingine iko kwenye huu mradi. Ikumbukwe ni hiyo kampuni ya Ureno ndiyo yenye uzoefu wa ujenzi wa reli. Je, mbia mpya wa Yapi Merkezi ni Nani? Uwezo wake ukoje? Tumefanya Due Diligence ili mambo ya Indo Power ya kwenye korosho yasijirudie? Taifa linapata nini?

Mheshimiwa Spika, tumerudia makosa tuliyoyafanya wakati wa ujenzi wa Bomba la Gesi kutoka Mtwara kuja Dar es Salaam. Mwezi Septemba, 2012, Wizara ya Fedha kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Benki ya Exim ya China walitiana saini makubaliano ya mkopo wa miaka 33 yenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 1.225 kwa riba ya 2% kwa ajili ya ujenzi wa bomba la gesi linalounganisha eneo la Msimbati na Mnazibay mpaka Dar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, Kampuni zilizoshinda zabuni ya ujenzi huu ni China Petroleum Technology and Development Corporation (CPTDC) na China Petroleum Pipeline Engineering Corporation (CPPEC), ambapo kila kitu kilichotumika kwenye ujenzi wa bomba hili kilitoka China na hakuna ushahidi wa kitaalam wa ujenzi huo ulioachwa nchini. Ndicho tunachofanya kwenye SGR. Mbaya zaidi kwa sasa tunatoa hela ndani kupeleka Uturuki na za nje tunazozikopa ni kutoka mabenki ya kibiashara yenye riba kubwa.

Mheshimiwa Spika, reli inahitaji chuma na chuma cha pua (Iron and Steel), mbao ngumu, wahandisi na mafundi mchundo wengi, vifaa vidogo kama screws na kadhalika. Je, Serikali imefungamanisha ajenda ya viwanda na ujenzi wa reli? Serikali inaweza kutuambia viwanda vingapi vya ugavi kwenye bidhaa za ujenzi wa reli vimejengwa?

Mheshimiwa Spika, viwanda vingapi vya mataruma vimejengwa nchini? Tunaagiza mataruma na hata screws za kufungia mataruma kutoka nje ya nchi. Ndiyo maana trilioni zote hizi tunazoipa Wizara kwa miaka hii mitatu hazisaidii ukuaji wa uchumi.
Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Dokta Ndugulile asisahau amendment ili tuweze kufanya hiyo amendment jioni kwa ajili ya kusaidia watu wa Kigamboni. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nina mambo matatu tu, mawili ni ya jimboni kwangu na moja ni la Kitaifa. Jambo la kwanza ni kuhusiana na mradi wa maji Kigoma. Tulikuwa tuna mradi wa maji ambao una thamani ya Dola za Kimarekani milioni 16 ambao ungeweza kutatua tatizo la maji la Manispaa ya Kigoma-Ujiji kwa asilimia mia moja na mradi ule ulikuwa uishe mwezi Machi, 2015. Bahati mbaya mpaka sasa mradi ule bado haujakamilika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Bunge la mwezi Februari, 2016 niliuliza swali hapa Bungeni na Wizara kupitia kwa Naibu Waziri wakasema kwamba mradi huu utakwisha mwezi Oktoba, 2016. Baadaye Mheshimiwa Waziri akafanya ziara katika Mkoa wa Kigoma na akatembelea mradi huu na akawa ametuahidi kwamba mradi huu utakamilika mwezi Desemba, 2016.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mchango wangu Bungeni mwezi Mei mwaka jana niliitahadharisha Serikali kwamba, mkandarasi aliyepewa kazi hii ya ujenzi wa mradi huu tayari amefilisika na anatumia fedha ambazo tunamlipa kulipia madeni yake katika maeneo mengine ambako anadaiwa; kwenye miradi mbalimbali duniani, lakini Serikali ikasema kwamba italishughulikia suala hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa masikitiko makubwa sana, mwezi Januari mwaka huu Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ametangaza rasmi kwamba mkandarasi huyu amefilisika. Imeleta taharuki kubwa kwa wananchi wa Manispaa ya Kigoma-Ujiji na hawaelewi sasa nini hatma ya mradi huu tena. Kwa hiyo, naomba Serikali iweze kutoa maelezo ya kina katika majibu yake kuhusiana na suala hili, kwa sababu ni mradi muhimu sana ni mradi ambao tumeuhangaikia, ni mradi ambao fedha za wafadhili zimetoka zaidi ya Shilingi bilioni 32 na tunashindwa kuelewa ni kwa nini Serikali haijachukua hatua zinazostahili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nasikia mkandarasi huyu hana mradi Kigoma peke yake, ana mradi pia Musoma na mradi huo pia na wenyewe unasuasua. Kwa hiyo, Waziri atakapokuwa analieleza hili, si kwa maslahi ya Kigoma peke yake, pia aangalie namna gani ambavyo tunaweza tukapambana na wakandarasi wa namna hii ambao wanachukua miradi hawaimalizi na kusababishia wananchi kero nyingi sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili ni suala la umwagiliaji. Mwaka jana nilizungumza kwenye Bajeti ya Wizara ya Kilimo na vile vile nilizungumza kwa maandishi kwenye Bajeti ya Wizara ya Maji na pia nilizungumza na Waziri mwenyewe na Waziri alikuja Kigoma na akatembelea Mradi wa Umwagiliaji wa mto Rwiche.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tarehe 5 Juni, 2015, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje alimuandikia barua Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Chakula wakati ule kuhusiana na mradi wa umwagiliaji wa mpunga katika bonde la Mto Rwiche. Barua ile ilikuwa na kumbukumbu namba CHC.325/395/01/42 ambapo Katibu Mkuu aliisaini na kuagiza jambo hili liweze kufanyiwa kazi. Katika barua ile Katibu Mkuu wa Wizara wa Mambo ya Nje aliambatisha barua kutoka Mfuko wa Maendeleo wa Quwait (Quwait Development Fund), barua ile ilikuwa ni ya tarehe 24 Mei, 2015.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kilichopaswa kufanywa upande wetu sisi ni kufanya detailed feasibility study ya mradi huu ili mradi huu uweze kufadhiliwa na Quwait Development Fund na hivyo tuweze kuwa na mradi mkubwa sana wa umwagiliaji na kuzalisha zao la mpunga katika Manispaa ya Kigoma katika bonde la mto Rwiche.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mpaka sasa na nilikuwa naangalia bajeti hapa ya Tume ya Umwagiliaji nimeona kwamba pamoja na kwamba tulipitisha bajeti ya Shilingi bilioni sita katika bajeti ya mwaka huu, fedha ambazo zimeshapelekwa Tume ya umwagiliaji ni asilimia 13 tu ya fedha ambazo zilitakiwa na sasa hivi tumeshafikia nusu ya mwaka wa fedha wa bajeti.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nipate maelezo ya Serikali na jambo hili linahusu Wizara tatu. Linahusu Wizara ya umwagiliaji, Wizara ya Mambo ya Nje na Wizara ya Fedha, kwa sababu Quwait Fund wana-desk pale Wizara ya Fedha. Tuweze kupata suluhisho la jambo hili kwa sababu mradi huu ni mradi mkubwa sana na ni mradi ambao unaweza ukatatua tatizo la chakula katika nchi yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama mnavyofahamu sasa hivi nchi yetu inakabiliwa na baa la njaa, chakula ni kichache hakitoshi, kwa hiyo, ni muhimu sana kuwa na miradi mingi ya umwagiliaji na mradi mmoja muhimu sana ni huu mradi wa bonde la Mto Rwiche. Nitakachokifanya kwa mara nyingine nitampatia Waziri barua zote hizi ili aweze kushauriana na Mawaziri wenzake; Waziri wa Fedha na Waziri wa Mambo ya Nje tuweze kupata suluhisho la jambo hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho ni la Kitaifa. Kamati ya Kilimo imependekeza kwamba tuongeze Sh. 100 kwenye bei ya mafuta ili tuweze kupata fedha za kutosha kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Maji. Sipishani kabisa wala sibishani na Kamati juu ya suala zima la kuongeza uwezo wa Mfuko wa Maendeleo ya Maji ili kuweza kutatua tatizo la maji kwa sabaabu ndilo tatizo kubwa ambalo wananchi wetu wanalo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo langu tu ni kwamba lazima tuwe aware kwamba kwa wiki tatu zilizopita bei ya mafuta kwenye soko la dunia imeongezeka kwa asimia 30. Kwa hiyo maamuzi yoyote ambayo tunayafanya, tuangalie namna gani ambayo tusipeleke mzigo kwa wananchi wa kawaida. Hata hivyo, tunalo suluhisho katika jambo hili, miaka takribani 10 iliyopita tulipitisha Sheria kwa ajili ya kutoa fedha kwenda REA, fedha kwenye mafuta ya taa, mafuta ya diesel na mafuta ya petrol.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kiwango kikubwa sasa hivi, REA imefanikisha malengo yake ya kuweza kufikisha umeme vijijini. Kwa hiyo tunachoweza kukifanya kwenye Sheria ya Fedha; na ningeomba tufanye marekebisho kidogo kwenye mapendekezo haya; ni kupunguza Sh. 50 kutoka kwenye fedha ambazo zinakwenda REA kutoka Sh. 100 mpaka Sh. 50 na tupunguze Sh. 100 kwenye fedha za mafuta ya taa zinazokwenda REA, fedha hizi sasa tuzipeleke kwenye maji. Kwa maana hiyo ni kwamba tutakuwa tumebakiza gharama za mafuta zitakuwa ni vile vile na sekta ya maji itakuwa imepata fedha za kutosha kwa ajili ya kuweza kutatua tatizo hili la maji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni muhimu kuweza kufanya hivi kwa sababu baadaye tunaweza tukajikuta tumesababisha mfumuko mkubwa wa bei bila kufanya mambo haya kwa uangalifu ambao unatakiwa. Kwa hiyo , naomba tu watu wa Kamati ya Maji, sipingi hoja yao, naiunga mkono lakini tuirekebishe kwa namna ambayo itaweza kuondoa mzigo wa….
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MWENYEKITI: Mheshimiwa Zitto muda wako umekwisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi jioni hii ya leo. Kwanza napenda niunge mkono Hotuba ya Kambi ya Upinzani Bungeni kama ilivyosoma na Dkt. Sware leo, naamini kabisa kwamba Serikali itaweza kuchukua maoni ambayo yameelezwa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na kuweza kuyafanyia kazi kwa manufaa ya Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nitajikita kwenye eneo moja tu la uvuvi leo; katika maeneo hayo mawili mifugo na uvuvi mimi nitazungumzia uvuvi peke yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uvuvi kwa mujibu wa takwimu za Serikali unachangia asilimia 2.2 katika Pato la Taifa (Gross Domestic Product). Kwa hiyo ukichukua Pato la Taifa la nchi yetu la shilingi trilioni 125 maana yake ni kwamba shughuli za uvuvi, yaani mnyororo wote wa thamani wa uvuvi unachangia shilingi trilioni 3 katika Pato la Taifa la shilingi trilioni 125. Ukichukua Watanzania watu wazima leo, ambao wana uzwezo wa kufanya kazi ambao ni takriban milioni 27 kwa population ya watu milioni 54, na kwa takwimu za Serikali kwamba asilimia 50 ya Watanzania wanajishughulisha na shughuli za uvuvi maana yake ni kwamba ukigawa Pato la trilioni 3 kwa mwaka linalotengenezwa na Sekta ya Uvuvi ina maana kila mvuvi nchi hii Pato lake kwa mwaka ni shilingi 230,000 tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukilinganisha na Pato la mtu per capita income ya Mtanzania ya takriban shilingi 2,000,000 unaweza ukaona ni namna gani ambavyo wavuvi katika nchi hii wana hali mbaya sana, wana umaskini wa hali ya juu sana. Tunahitaji mkakati maalum wa kuhakikisha dekta hii kwanza inakuwa inachangia kwa kiwango kikubwa kwa maana ya asilimia 5 kama ambavyo Mpango wa Maendeleo wa Taifa ulivyotaka, lakini tunaona Serikali kiwango cha bajeti ambacho kinawekwa kwenye sekta hii wala huwezi kuamini kwamba kuna nia ya dhati ya kuweza kuifanya Sekta ya Uvuvi iweze kukua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo langu la uchaguzi asilimia 30 ya wakazi wake wanategemea uvuvi katika Ziwa Tanganyika, na sasa hivi tumeanza anza pia kufuga samaki. Lakini sasa ukiangalia Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapin duzi ukurasa wa 22 Ibara ya 27 kuna ahadi 16 zinazohusiana na Sekta ya Uvuvi. Ahadi 16, ukurasa wa 22 Ibara ya 27 ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ambayo ndiyo tunapaswa kuwapima Serikali ya Chama Cha Mapinduzi. Katika ahadi 16 Serikali mpaka sasa tunakwenda kwenye bajeti ya nne haijatekeleza ahadi hata moja ambayo waliitoa kwa wananchi wakati wanaomba kura. Nitawapa mifano ya ahadi tatu tu ambazo mpaka sasa hazijatekelezwa. Chama Cha Mapinduzi waliahidi wakiunda Serikali watanunua meli tano za uvuvi zenye uwezo wa kuvua samaki bahari kuu na kuzalisha ajira 15,000, hakuna hata meli moja imenunuliwa mpaka sasa! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Chama Cha Mapinduzi kiliahidi kujenga bandari ya uvuvi ambayo itaweza kuzalisha ajira 30,000 hakuna hata dalili za kuanza kwa hiyo bandari ya uvuvi. Sasa tunashindwa kuelewa tutawapima namna gani mwaka 2020 sisi wavuvi? Tutawapima kwa nyavu za wannachi ambazo mnazichoma kila siku? Tutawapima kwa mitumbwi ambayo mnawavunjia wananchi kila siku? Tutawapima kwa umaskini ambao mmetengeneza kwa wavuvi katika nchi hii? Naomba Chama Cha Mapinduzi na Wizara ya Mifugo Uvuvi…

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Taarifa kidogo.

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naom ba Waziri ana nafasi ya kujibu dakiak zake, aniache nitiririke, a-relax, relax brother!

MWENYEKITI: Mheshimiwa Zitto subiri kidogo. Mheshimiwa Waziri, Taarifa.

T A A R I F A

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa Taarifa hii. Naomba nimpe taarifa; kwa kuwa amezungumza jambo kubwa sana linalohusu Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi, ingekuwa kama anachangia katika njia ya kawaida pasingekuwa na taabu, lakini anaposema kuwa mpaka kufika sasa mwaka wa nne Serikali ya Chama Cha Mapinduzi katika ahadi tulizozitoa upande wa Sekta ya Uvuvi hakuna tulichokifanya, nataka nimwambie asome vizuri hotuba ya Mheshimiwa Waziri ataona yale ambayo tumeyafanya katika kipindi kifupi baada ya Mheshimiwa Waziri Mpina na mimi Naibu wake kuingia katika Wizara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja, katika hayo ya uvuvi nataka nimkumbushe atazame liko jambo linalohusu TAFICO. Na nataka nikuambie kaka yangu Zitto ya kwamba huwezi kwenda katiak uvuvi wa bahari kuu bila ya kuanzisha Taasisi ya kusimamia, shirika la kusimamia. Tumeanzisha TAFICO, tumefufua TAFICO kwa lengo la kuhakikisha kuwa tunakwenda kusimamia uvuvi wa bahari kuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili nataka nimuelimishe kidogo katika eneo hili…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, umefahamika…

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

MWENYEKITI: Mheshimiwa ulishafahamika, Mheshimiwa Zitto, taarifa hiyo.

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa siipokei. Mimi nimetaja kurasa ya Ilani ya Chama ambacho yeye ndiyo anapaswa kuitekeleza. Ukurasa wa 22 Ibara ya 27 kuna ahadi 16, hakuna ahadi ya TAFICO. Kwahiyo huwezi kujitungia swali na ukajitengenezea jibu, ukajipa tiki, hakuna! Angalieni Ilani yenu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi watu wa uvuvi katika Ziwa Tanganyika tuna malalamiko mengi. Baadhi ya malalamiko yamejibiwa na Serikali lakini pia tutapenda kuona kama wale ambao waliumizwa na maamuzi ambayo sasa Serikali imeyageuza na namna gani ambavyo watakavyofanyiwa compensations zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza tuna tatizo la tozo, export, ushuru wa export. Nchi yetu inachimba na inavuna dhahabu. Wawekezaji wa dhahabu wanauza dhahabu nje, hakuna tozo ya export ya dhahabu. Kwanini tunaweka tozo ya export ya samaki? Tozo ya export ya dagaa Ilikuwa dola 1.5 kwa kilo sasa imekuwa dola moja, kiwango kikubwa, tena wanatoza kwa dola. Wavuvi wa Kalya, wavuvi wa Kagunga, wavuvi wa kila mahali wanatozwa kwa dola, ni kwanini? Kwa hiyo naomba tozo hii ya export iondolewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pili pamoja na nyavu kuchomwa na pamoja na Serikali kutoa maelezo mengine kuhusiana na suala la nyavu, kama nilivyosema tungependa tufahamu, sasa wale ambao wamechomewa nyavu zao na vyombo vyao ambao Serikali sasahivi imebadilisha sera yake, Serikali itawalipa namna gani? Kwa sababu ni watu ambao wameshaingizwa kwenye umaskini na ningependa kwakweli tuweze kuhakikisha ya kwamba jambo hili linashughulikiwa vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo ningependa kulisemea ni suala la leseni nyingi kwenye chombo kimoja. Sisi wavuvi boti ya kuvua ndiyo kama trekta kwa mkulima. Trekta kwa mkulima halina leseni sijui ya SUMATRA, n.k lakini mvuvi chombo chake cha kufanyia kazi anakata SUMATRA, lesseni ya boti, anakata leseni ya mwenye chombo, anakata leseni ya wavuvi, sisi ambao tunatumia vipe kule katika Ziwa Tanganyika unahitaji wavuvi sita kwenye kipe kimoja wote wanahitaji leseni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeeleza hapa kwamba inaangalia namna ambavyo italirekebisha jambo hili na pia hata leseni ambazo zinaweza kutumika kwenye zaidi ya halmashauri moja; na nimeona kwamba tayari GN namba 383 imeshatoka; lakini jambo ambalo naliomba Serikali ilifanyie kazi ni suala zima la kwamba hakuna haja ya chombo cha uvuvi kuwa na leseni kwa sababu leo hii hata road license tumetoa; road license tunailipa kwenye mafuta. Mvuvi anapokwenda kuvua ananunua mafuta! Kwa hiyo ina maana na yeye ameshalipia leseni yake moja kwa moja kama ambavyo mwenye trekta alivyo. Kwa hiyo kuna haja kubwa jambo hili liweze kuondolewa kwa sababu ni gharama kubwa kwa wavuvi na haliwezi kuwasaidia wavuvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho, pamoja na marekebisho kadhaa ambayo yamefanywa na mapendekezo ambayo tumeyatoa ya tozo n.k. naomba Serikali inipe maelezo kidogo. Ukiangalia takwimu kutoka kwenye kitabu cha Hali ya Uchumi wa Taifa utaona kwamba mwaka 2014 tuliuza nje bidhaa za mazao ya uvuvi ya thamani ya dola za Kimarekani million 832. Lakini tangu Serikali ya Awamu ya Tano ya Chama Cha Mapinduzi iingie madarakani mauzo nje ya mazao ya uvuvi yameporomoka mpaka dola milioni 182 kutoka dola milioni 832 mwaka 2014, mwaka mmoja kabla Serikali hii haijaingia madarakani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachokiona kila siku na sifa kubwa ambayo Wizara ya Mifugo na Uvuvi inapata ni kuonekana wakiwa na njiti za viberiti wakiwa na mafuta wanachoma nyavu za wavuvi ilhali exports zetu kwenye mazao ya uvuvi zinazidi kuporomoka. Tunaomba Wizara hii itakapokuja kujibu hoja za Wabunge hapa waweze kutoa maelezo ya kina ni nini ambacho kinasababisha mauzo nje ya mazao ya samaki yanaporomoka tangu Serikali hii ya Awamu ya Tano iingie madarakani, ni kwasababu ya uchomaji wavuvi wamepungua, ni kwa sababu ya tozo kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii Kigoma pale kupata mgebuka imekuwa ni tatizo kwa sababu ya amri ambazo Serikali imekuwa inazitoa, mara msitumie vipi, mara msivulie sijui neti, mara msifanye nini. Kwa hiyo, wavuvi wanakuwa hawaelewi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia, kuna tatizo kati ya msimamizi wa Wizara, dada anaitwa Judith, mimi simfahamu, nimezungumza na wavuvi, hana mahusiano mazuri na wavuvi wa eneo lote la ukanda wa Ziwa Tanganyika. Naomba Wizara ifanye consideration kutazama, kwa sababu kuna measures ambazo wamezichukua, basi angalau na msimamizi aweze kubadilika, kwa sababu malalamiko ya wavuvi ni makubwa na tunahitaji wavuvi nao wajione ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa muda ambao umenipatia na hongera sana kwa kazi uliyoifanya leo asubuhi. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa wa Mwaka 2018
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru kwa kupata nafasi ya kuchangia muswada huu ambao Serikali imeuleta mbele yetu.

Mheshimiwa Spika, wakati najiandaa kuchangia napenda niwakumbushe Waheshimiwa Wabunge wenzangu wakumbuke mwaka 1933 aliyekuwa kiongozi wa Ujerumani Adolf Hitler alipeleka ndani ya Bunge la Ujerumani muswada wa sheria ambao kiingereza unaitwa Enabling Act ambao Wabunge wa Chama chake cha Nazi na wa vyama vingine isipokuwa chama kimoja tu Chama cha SDP waliunga mkono. Ilichukua miezi sita tu muswada ule baada ya kuanza kutumika, Ujerumani haikuwa na chama cha siasa kwa sababu Hitler alitumia sheria ile ile ambayo ilitungwa na Bunge la Ujerumani kuhakikisha si tu vyama vimefutwa bali wanasiasa au wamekimbilia uhamishoni ama wameuawa kutokana na mazingira mabovu yaliyokuwa ndani ya sheria hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hii ndio hali ambayo Bunge lako tukufu inayo sasa hivi; kwamba tuna muswada hapa ambao kwa nature ya majadiliano unaonekana ni muswada kati ya chama kinachotawala na vyama vya upinzani, lakini utekelezaji na madhara yake yanakwenda zaidi ya ushindani wa chama kinachotawala na vyama vya upinzani. Hii ni kwa sababu sisi sote ni wanasiasa na tunajua mamlaka ambayo tunataka kumkabidhi Msajili wa Vyama vya Siasa kwa mujibu wa sheria hii ni mamlaka yatakayotengeneza hali ngumu sana ya kisiasa katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nikukumbushe, wewe ni Mwalimu wa Historia. Nchi yetu hii kabla ya Mfumo wa Vyama Vingi kuanza na wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere, kwa sababu watu hawakuwa huru kuzungumza kisiasa, kulikuwa na majaribio ya mapinduzi manane. Baada ya Mfumo wa Vyama Vingi kuanza, nchi yetu haina rekodi ya jaribio la mapinduzi hata moja kwa sababu watu wakiwa na hasira watakwenda Mwembeyanga, watakwenda Songea, watakwenda Kigoma, watazungumza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mazingira yanayojengwa sasa hivi, iwapo watu watakosa uhuru wa ku-vent out na milango ikafungwa, wakaamua kupita madirishani, tusilaumiane. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna hoja hapa ya; ni wakati gani na kwa namna gani Msajili wa Vyama vya Siasa anaweza akafuta chama. Katiba yetu imeelezwa vizuri na bahati nzuri nilishiriki vikao vya Kamati ya Katiba na Sheria, namshukuru Mwenyekiti aliniruhusu; na tunampongeza sana Mheshimiwa Chenge, alijitahidi kwa kadri ya uwezo wake kuweza kutupitisha katika kila kifungu na vifungu vya Kikatiba.

Mheshimiwa Spika, huwezi ukawa na Katiba inayoruhusu freedom of association halafu ukawa na mtu ambaye unampa mamlaka peke yake ya kuamua kwamba wakati huu sasa hii freedom of association inafutwa. Katika hali ya kuonesha kwamba inawezekana vyama vikafanya makosa vikatakiwa kufutwa, tulipendekeza ndani ya Kamati kwamba kuwepo na tribunal. Kwamba Msajili anapoona chama kimefanya makosa, sio yeye tu aamue, kuwe na tribunal, halafu vyama vipelekwe kule viweze kuwa tried na tribunal ile iweze kuamua. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Muswada huu pamoja na marekebisho, hakuna tribunal. Best examples zimetajwa na Mwenyekiti wa Kamati. Best examples zimetajwa kuna tribunal. Ghana ambayo imezungumziwa kwa kina sana katika Muswada huu, ina tribunal; Kenya ina tribunal; ni nini ambacho sisi tunakiona ni hatari kuweka tribunal ili kuhakikisha kwamba wote tuone haki inatendeka? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba na Wabunge wenzangu walitazame hili, tuone uwezekano wa kufanya mabadiliko. Badala ya mamlaka haya ambayo tumemkabidhi Msajili peke yake kuyafanya peke yake, yaundiwe tribunal ambayo itayafanya na bado hata hiyo tribunal inateuliwa na watu wa Serikalini humo humo tu; it’s not a problem, tunachokitaka, tuwe na uhuru wa kuweza kuzungumza na kuweza kutoa maoni yetu kwa jinsi ambavyo inastahili.

Mheshimiwa Spika, democracy siyo uadui. Nchi yetu imefaidika sana na democracy. Nitakupa takwimu kidogo tu. Kati ya mwaka 2007 na mwaka 2012, jumla ya Watanzania milioni moja waliondolewa kwenye poverty. Wewe unajua. Hiki ndicho kipindi ambacho demokrasia ilikuwa imeshamiri sana katika nchi yetu, hiki ndicho kipindi ambacho tulikuwa na uhuru mpana zaidi wa mawazo na ndicho kipindi ambacho Serikali inakuwa responsive kwa watu wake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, data za juzi za World Bank, ndani ya miaka mitatu toka utawala huu uingie madarakani, Watanzania milioni mbili wame-fall into poverty, kwa sababu kuna correlation kati ya demokrasia na maendeleo ya watu. Tunachopaswa kufanya leo, miaka 25 toka tumeingia katika Mfumo wa Vyama Vingi siyo kubana zaidi demokrasia, ni kuipanua zaidi demokrasia. Tungepaswa leo tuletewe Muswada ambao unapanua zaidi badala ya kudhibiti. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo tunadhibitiwa mpaka kwenye elimu ya uraia, kwamba unapokuwa na a sister party au any other organization ambayo mnafanya nayo kazi, tunaweka udhibiti. Siyo taasisi za nje tu, maana yake inawezekana watu wakadhani; na wakati naingia hapa nimekuta Mbunge mmoja kutoka Tabora Mjini anazungumza, anadhani kwamba ni taasisi za nje ndiyo zitakuja, zitaleta tatizo kwenye nchi yetu, hapana. Hata taasisi za ndani tunaweka udhibiti wa elimu ya uraia.

Mheshimiwa Spika, unapotunga sheria kuna jambo ambalo lilikuepo unataka kulitatua. Naomba Serikali inieleze, kabla ya kuweka vifungu hivi inavyovi-propose vya elimu ya uraia kudhibitiwa na Msajili, kulikuwa kuna tatizo gani katika nchi yetu? Kwa sababu a new bill ina lengo la kwenda kutibu tatizo ambalo limetokea. Naomba Serikali inieleze, kulikuwa kuna tatizo gani?

Mheshimiwa Spika, hatujaona tatizo lolote la elimu ya uraia, NGOs zimekuwa zikitoa elimu ya uraia, vyama vimekuwa vikitoa mafunzo kwa wanachama wake. Kwa nini sasa tutake kudhibiti katika Muswada huu ambao unakuja hapo mbele yetu? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba tuongozwe na maslahi mapana ya nchi yetu. Tusiongozwe na kubanana. Tusitunge sheria kwa kuwatazama watu. Kuna vifungu humu vya sheria vimetungwa kwa kutazama watu, ndiyo maana watu hawaogopi kubadilisha Katiba, hawaogopi kwenda kutunga kifungu ambacho kiko kinyume na Katiba. Tulikubaliana sisi ndani ya Kamati, Wajumbe wa Kamati, mimi nilikuwa mwalikwa kwamba the reference ya uraia itumike reference ya uraia ya ndani ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Schedule of Amendments iliyokuja, labda Mheshimiwa Jenista aseme amekosea. Ni tofauti kabisa na lile ambalo lilikubaliwa ndani ya Kamati. Kwamba leo wewe ukiwa umezaliwa na mzazi mmoja ambaye sio Mtanzania unaweza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, unaweza kuwa Makamu wa Rais, unaweza kuwa Mbunge, unaweza kuwa Waziri Mkuu, lakini huwezi kuanzisha chama cha siasa. It is ridiculous! (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na consensus ndani ya Kamati. Kitendo cha ile consensus ya ndani ya Kamati kutorejeshwa kwenye Schedule of Amendments lazima kuna watu wanaokuwa-targeted, huwezi kutunga sheria kwa ku-target watu. Naomba Bunge lako Tukufu lifanye amendment kwenye eneo hili. Tutumie provision ya Katiba katika hayo. Tunaelewa ni muhimu kuweza kuwa na Watanzania halisi katika uanzishaji na uendeshaji wa vyama, lakini tunayo guidance yetu ambayo ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la mwisho ni section 19(c), sijaiona kwenye Schedule of Amendments, lakini tulikuwa tumekubaliana kwamba ifanyiwe marekebisho kwenye Kamati. Kifungu cha 19(c) kinasema: “Msajili wa Vyama, wakati wowote ule akiona kwamba chama kiliundwa na kikasajiliwa, yeye akiamini fraudulently anakifuta chama kile. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mchakato wa kuanzisha chama haupati cheti cha usajili wa chama kama mchakato huo haukuidhinishwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama. Sasa mtu ambaye ndio ametoa cheti cha usajili, ameidhinisha, huyo huyo eti akiwaza tu kwamba hii ni fraudulent, anaweza akakifuta chama. Sasa who is fraudulent there? Ina maana ni Msajili mwenyewe kwa sababu yeye ndio ambaye ametoa ile certificate. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, chama cha kwanza ku-suffer kwenye hili itakuwa ni Chama cha Mapinduzi…

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Tulitoa mwongozo asubuhi kwamba tuvumiliane. Mheshimiwa Naibu Spika alipokuwa hapa, nafikiri alieleza vizuri. Karibu tunafika mwisho, tuvumiliane tu. (Makofi)

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa hiyo, nashauri kifungu hiki, tuliomba kwenye Kamati na Mheshimiwa Mtemi Chenge akapewa jukumu la kukitazama, sijakiona kwenye Schedule of Amendments, kama kipo mtaniwia radhi; kitazamwe, kifutwe, kwa sababu hakina maana yoyote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nasema, chama cha kwanza kuingia kwenye mgogoro huo kitakuwa ni Chama cha Mapinduzi kwa sababu hakikusajiliwa, hakikufuata mchakato ambao vyama vyote vilifuata kwenye usajili. Chama cha Mapinduzi kilitungwa kwa mujibu wa sheria. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo ninyi mpo madarakani, mna majority ndani ya Bunge, kesho mnapoteza majority hata ya Mbunge mmoja, the first act ya kiongozi yeyote atakayeingia madarakani, mmepoteza majority hata ya Mbunge mmoja, anakwenda kuwafuta, hamkufuata sheria. Sasa mnajitungia sheria hata ya kuwanyonga ninyi wenyewe? Naomba hiki Kifungu cha 19(c) kifutwe kwa sababu hakina maana yoyote. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Spika, la mwisho ni huu mjadala wa vikosi vya ulinzi, naomba Mbunge yeyote wa Chama cha Mapinduzi hapo alipo atazame kazi ya kwanza ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi ni nini? Mbunge yeyote yule wa CCM, najua kuna Wabunge ambao wameingia hawakupita kwenye hiyo michakato ya… (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Zitto, dakika zako zimekwisha. (Makofi)
Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti na mimi nashukuru kwa kupata nafasi ya kuchangia Kamati hizi ambazo ziko mbele yetu leo, nitaanza na upande wa Wizara ya Ulinzi. Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 1974 aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwalimu Nyerere, aliwaondoa watu wawili kutoka Jeshini, Mkuu wa Majeshi na Mnadhimu Mkuu na kuwapeleka kwenye shughuli za kiraia. Mkuu wa Majeshi akawa Waziri wa Vijana na Michezo na Mnadhimu Mkuu akawa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Sukari la Taifa. Huyu ambaye alienda kuwa Waziri na baadae Balozi tayari amefanyiwa taratibu za kijeshi za kustaafishwa na kupata mafao yake inavyostahili. Huyu ambaye alikwenda kuanzisha SUDECO mpaka leo tunavyozungumza, Jeshi halijamfanyia taratibu za kustafishwa kama mwanajeshi. Toka mwaka jana mwezi Februari nimekuwa nikileta swali hapa Bungeni kuhusiana na Kanali Kashmir kuhusu haki yake ya kustaafishwa kama mwanajeshi ili aweze kupata haki, swali hilo limekuwa likipigwa danadana, napata majibu kwamba Wizara ya Ulinzi haina majibu bado. Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba leo Waziri wa Ulinzi alieleze Bunge hili Tukufu, Mzee huyu ambaye sasa ana miaka 80 wanataka apoteze maisha kabla ya kupewa haki zake? Kwa sababu siyo yeye aliyetoka Jeshini kwenda uraiani, ameondolewa na Amiri Jeshi Mkuu Mwalimu Nyerere. Mwenzake aliyetoka naye Mkuu wa Majeshi wa zamani amestaafishwa rasmi wakati wa utawala wa Mzee Mkapa, tatizo ni nini kwa Kanali Kashmir? Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi kunaanza kujengeka hisia, Kanali Kashmir ni Mtanzania mwenye asili ya kiasia. Kuna hisia zinaendelea miongoni mwa Watanzania wenye jamii ya kiasia kwamba yeye anatengwa kwa rangi yake, wakati ni mtu ambaye alilitumikia Jeshi letu na aliitumikia nchi hii kwa uzalendo wa hali ya juu sana. Kwa hiyo naomba leo Waziri wamenikwepa kwenye maswali sasa at least Kamati imekuja na ninaiomba Kamati pia kama majibu ya Waziri hayakutosheleza imtembelee Kanali Kashmir apate haki yake na tumuombe Mungu ampe uhai mpaka hapo aweze kupata haki yake kabla Mwenyezi Mungu hajamchukua, ana umri wa miaka 80 sasa hivi. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ambalo ninataka kulizungumzia ni Sera ya Mambo ya Nje. Sasa hivi kuna tatizo kidogo, nakubaliana kabisa na ndugu yangu Mheshimiwa Chumi kwamba ni lazima Sera ya Mambo ya Nje ibadilike kuendana na wakati lakini kuna tatizo la kubadilisha misimamo bila kufuata misingi ya Sera ya Mambo ya Nje. Ni kweli tumempokea Mfalme wa Morocco hapa siyo nchi ya kutengeneza maadui lazima tutengeneze marafiki, lakini unapompokea si lazima uhoji kile ambacho umekuwa ukikisimamia kwa takribani mika 40? Mheshimiwa Mwenyekiti, Rais wetu hakwenda kwenye vikao vingine vyote vya AU, vikao viwili hakwenda, inawezekana kuna maelezo ya kwa nini Rais hakuhudhuria vikao vya AU, lakini kikao cha AU kinachohusiana na kuirudisha Morocco Rais amekwenda na humu ndani Wizara ya Mambo ya Nje haijatupa maelezo yoyote kuhusiana na haki za watu wa Saharawi. Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna Azimio la Umoja wa Mataifa Azimio Namba 2285 la mwaka 2016 linalotaka kura ya maoni ya watu wa Sahara Magharibi kuamua hatima yao. Sasa juzi wenzetu wa SADC wamepiga kura kukataa Morocco kurudishwa ndani ya African Union. Sisi tuko SADC, tunahitaji maelezo ya Serikali tulipigaje kura yetu? Haya siyo mambo ya kuchezea, tukiacha watu wafinyange finyange Sera ya Mambo ya Nje ambayo ndiyo imetengeneza nchi hii hatutakuwa na nchi, kwa sababu ukishavunja principles unabaki nani wewe? Mheshimiwa Mwenyekiti, the same thing to Israel mimi sipingani kabisa kufungua Ubalozi Israel, kuna watu wetu wengi Watanzania wanahitaji huduma za viza, wanahitaji huduma za kibalozi kwa ajili ya Hijja wanapokwenda Israel, lakini sisi ni waumini wa two state solution. Tumekwenda UNESCO, tumepiga kura, kura yetu inaendana kinyume na maamuzi yetu ya two state solution, kura tuliyopiga Paris tarehe 16 Oktoba mwaka jana. Tunaambiwa na Afisa wa Mambo ya Nje ambaye alipiga kura ile pamoja na Israel kinyume na maelekezo ya Wizara ya Mambo ya Nje kwamba amechukuliwa hatua, tunahitaji maelezo ya Serikali, hapa kwa sababu hizi ni matters of principle.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kufungua Ubalozi Misri waligombana na Israel wana Ubalozi, there is no problem about that, lakini tunachokitaka ni kuhakikisha kwamba yale mambo ambayo tunayasimamia yale tusiende kinyume nayo. Ninaomba Kamati ya Mambo ya Nje na wakina Mheshimiwa Msigwa Wajumbe huko wananisikia, haya ndiyo mambo ya kwenda kui-pin down Serikali kwenye Kamati, kwa sababu ni principle atakuja mtu hapa atavuruga tu, anaweza akaanza akasema kwamba apartheid was right, kwa sababu tu tumevuruga vuruga misingi ambayo tunayo. (Makofi) Jambo la mwisho napenda nimpongeze Rais kwa kufanya uteuzi wa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya, hii Waheshimiwa Wabunge ndiyo kazi ya Bunge. Tusingepiga kelele humu ndani na kuikumbusha Serikali kwamba kuna jambo hili... (Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji) MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Zitto,
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) wa Mwaka 2019
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kwa ruksa yako kabla sijaanza kuchangia, nitoe taarifa kwamba na nimeshamjulisha Waziri wa Mambo ya Ndani kwamba juzi usiku aliyekuwa msaidizi wangu Ndugu Raphael Ongangi ametekwa na watu wasiojulikana. Tumetoa taarifa Polisi lakini mpaka sasa hatujafahamu alipo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuanzia leo tumeanza kuona social media accounts zangu zote; Twitter, Facebook, Instagram na nyingine ziki-tweet mambo ambayo ni tofauti na ambayo mimi nayaamini. Kwa hiyo, hii inadhihirisha kwamba watu ambao wamemteka Ndugu Raphael, lengo lao wala halikuwa Raphael, lengo lao lilikuwa mimi. Nachowaomba ni kwamba wamuachie Raphael endelee na maisha yake, waniteke mimi ili niweze ku-deal nalo mimi mwenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, leo ni moja ya siku mbaya sana kwenye historia ya nchi yetu kwa sababu kwa mara nyingine tena ndani ya Bunge hili la Kumi na Moja na katika uhai wa Bunge la Kumi na Moja tunakwenda kutunga sheria ambazo zinaendelea kuminya haki za watu. Tulianza na Media Services Act, Sheria ya Vyama vya Siasa, Sheria ya Pensheni ambayo ilileta matatizo makubwa kwenye kikokotoo cha pensheni na haki za wafanyakazi, Sheria ya Takwimu na sasa tunaleta Sheria hii ambayo ni muendelezo wa juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kukandamiza haki za msingi za raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni bahati mbaya kwamba raia wengi wa nchi hii ni maskini kwa hiyo mambo ambayo wakiyazungumza na hata Wabunge wao wakiyazungumza, hayasikilizwi. Tulizungumza hapa Sheria ya Takwimu, kifungu cha 24(a) na (b) ambacho kilikuwa kinaweka matatizo makubwa na vizingiti na haki za watu kuweza kushughulika na mambo ya takwimu, hatukusikilizwa. Juzi Benki ya Dunia imezuia fedha zaidi ya Dola za Kimarekani bilioni 1.15, Benki ya Dunia wamesikilizwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kiufupi kwa maneno ya mtaani tungesema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Joseph Magufuli imeufyata mbele ya mabeberu. Hii ni kwa sababu sheria ambayo tuliikaa sisi ndani ya Bunge na ikapigiwa kelele na watu walewale waliosimama kuunga mkono Sheria ya Takwimu ambao leo wanasimama kuunga mkono mabadiliko haya, sheria ile imebadilishwa hata haijatimiza mwaka. Leo watu walewale wanasimama kuiambia Serikali ni Serikali sikivu. Wala usihangaike na takwimu, nina barua za Ikulu, barua kutoka Wizara ya Fedha kumuomba Rais aruhusu kabla ya Mkutano huu wa Bunge, Sheria ya Takwimu irekebishwe na mmetii, mmeileta imerekebishwa. Mnawasikiliza zaidi mabeberu kuliko wananchi wenu walioikataa sheria hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunafanya mabadiliko ya Sheria ya Makampuni, sheria ambayo ina muendelezo wa tafsiri ya nini kampuni dunia nzima. Sisi ni a Commonwealth country, nchi zote za Jumuiya ya Commonwealth zinatafsiri yake ya kampuni. Sheria ambayo tunaletewa leo hapa inaenda kuunganisha kampuni na mwenye kampuni kuwa kitu kimoja jambo ambalo tutachekwa duniani. Hakuna mtu atakayekuja nchi hii kuleta fedha yake kuwekeza ili kutengeneza ajira na kulipa kodi akiona kifungu cha 400A cha Sheria ya Makampuni ambayo Serikali inakileta hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kifungu hiki pamoja na marekebisho ambayo Serikali imeyaleta, mimi nafahamu Serikali inahangaika na ACACIA, wanataka kupambana na ACACIA; nendeni mkapambane na kampuni moja kwa taratibu zake za kiutalawa, msiharibu nchi yetu kwa sababu ya ugomvi wa kampuni moja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, section hiyo 400A inasema kwamba shareholders wakizuiwa kuingia nchini, kampuni inafutwa. Kweli sisi hatujui tofauti ya kampuni na shareholders? Hatujui kama kampuni ni a legal entity inayojitegemea na shareholders? Leo wewe ukiwa shareholder wa kampuni au ukiwa director wa kampuni, ukifanya makosa kampuni inaadhibiwa? Kwa nini mnatutia aibu duniani kwa kuleta sheria za hovyo hovyo namna hii, kwa nini? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, halafu mnampa Wizara kijana wetu Inno, kijana mzuri kabisa smart, mnampa Wizara kwenda kuhangaika na mambo ya kijingajinga kama haya? (Makofi)

KUHUSU UTARATIBU

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu utaratibu.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Jenista Mhagama.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 64(1)(f) na (g), Mheshimiwa Zitto unapitiliza, hatuwezi kukubali maneno ya namna hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, haya maneno ni ya kuudhi, kudhalilisha Bunge hili lakini unafahamu mfumo wa utendaji kazi ndani ya Serikali umetawaliwa na wataalam wabobezi na wazoefu wanayo heshima kubwa ndani ya nchi yetu na nje ya Taifa letu lakini maneno anayoyatumia Mheshimiwa Zitto Kabwe hapana, hapana. (Makofi)

WABUNGE FULANI: Yataje.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Naibu Spika, wote tumeyasikia, kwa heshima niliyonayo siwezi kuthubutu kuyarudia maneno haya na wote tumeyasikia.

WABUNGE FULANI: Aaaaa.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Naibu Spika, watu watacheka, watadhihaki, nasimama kama Chief Whip nasema Zitto Kabwe amepitiliza kwa kutumia lugha ya kuudhi ndani ya Bunge. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakuomba arekebishe maneno hayo, aendelee na mchango wake, atumie utaalam wake kuishauri Serikali lakini hatuwezi kukubali. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kila wakati tunakumbushana matumizi ya Kanuni yetu ya 64. Nyakati zote wale waliotangulia huwafundisha waliofuata na hii Kanuni ipo tangu Bunge lililopita. Kwa hiyo, Mheshimiwa Zitto hiki anachokifanya, anafanya kusudi kwa sababu Kanuni anazijua. (Makofi)

Mheshimiwa Zitto lazima ufike mahali pa kuheshimu watu wengine, kuheshimu mawazo ya watu wengine kama ya kwako ambavyo huwa yanaheshimika. Haiwezekani kikaletwa kitu hapa ama ikaletwa kama hivi tunao Muswada unaojadiliwa unasema kwamba Serikali imeleta jambo la hovyo, eeh, jambo la kijinga, haya ni mambo ya ajabu sana.

Waheshimiwa Wabunge, hii ina maana kwamba wewe peke yako mtu mmoja una akili sana kuzidi Kamati yetu ya Bunge ambayo ina watu zaidi ya 23. Wewe peke yako umezidi mawazo yote ya hizo taasisi zote zilizotajwa kwenye Muswada huu. (Makofi)

Unazungumza hapo kuhusu Serikali kwamba kwa mabadiliko haya Serikali, kwa lugha yako ya mtaani ambapo wewe unajua huo mtaa mnaokwendaga imeufyata. Mheshimiwa Zitto unafahamu lugha kama hiyo unapomwambia mtu mwingine ameufyata, unamaanisha nini?

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tusikilizane na nawakumbusha siku zote nikisimama Kanuni tulizojitungia wenyewe zinawataka mnisikilize, ndiyo maana ya neno Speaker, halina maana nyingine, maana yake when I am speaking you should not speak, that is what it means. (Makofi)

Mheshimiwa Esther Matiko na ukitajwa hapa huwa una malalamiko, unapenda sana kuongea, sikiliza na wenzio. Si lazima uzungumze kila wakati, unaweza kunyamaza pia. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, matumizi ya Kanuni hizi yanataka humu ndani tuheshimiane na kazi ya mtu anayekaa hapa mbele kuongoza mkutano wa Wabunge ni kuhakikisha humu ndani tunajadili kwa heshima na kwa mujibu wa Kanuni tulizojiwekea. Tusifike mahali pa kudharau mtu mwingine humu ndani, mheshimu, sema hoja yako kwa lugha ya staha. Ndiyo maana Kanuni ya 64 inakataza maneno ya dharau, maneno yasiyo na staha kwa mtu mwingine na maneno yanayoudhi, tafadhali. (Makofi)

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa maelekezo yako na natambua maoni ya Chief Whip wa Serikali. Nayarudia vile nilivyosema nikirekebisha ili niseme kwa lugha ambayo itaonekana kwamba ni ya staha.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tusikilizane. Nimetoa maelekezo, lugha ya kuchangia ni yenye staha, isiyoudhi watu wengine, isiyoleta dharau, Mheshimiwa Zitto Kabwe.

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru na ninatii maelekezo yako. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Sheria ya Makampuni ambayo inabadilishwa ina vifungu kadhaa lakini mimi focus yangu ni kifungu cha 400A peke yake ambacho nakiona kwamba ni kifungu ambacho kitahatarisha sana hali ya uwekezaji katika nchi yetu kwa sababu ni kifungu ambacho kinaweza kutumika vibaya kuwafanya watu wasiweke mitaji yao katika nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano kifungu hiki kinaunganisha kwa pamoja kama nilivyoeleza, mwenye kampuni na kampuni, kitu ambacho principally hakikubaliki. Mtu yeyote ambaye amesoma Sheria ya Makampuni, economics, accounts anajua kwamba kampuni na mwenye kampuni ni vitu viwili tofauti. Naomba eneo hilo liweze kurekebishwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pili, sheria inasema kwamba Msajili wa Makampuni anaweza akaifuta kampuni kwa sababu ilisajiliwa fraudulently. Hii inaondoa kabisa principle ya kinachoitwa conclusiveness of certificate of incorporation. Certificate of incorporation ikishatolewa ni conclusive, kwa hiyo, kama kulikuwa kuna tatizo kwenye usajili wake, taratibu za kisheria zinaweza zikafuatwa na uondoaji wa usajili ule ukaweza kufanyika kwa mujibu wa sheria. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, inazungumzia kuhusu misrepresentation kwenye usajili. Sheria ya sasa ya Makampuni, kifungu cha 472 tayari kinatoa adhabu kwa kosa hilo lakini kifungu ambacho Serikali inakileta kinasema kwamba kampuni hiyo itafutwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia ifahamike kwamba makampuni haya yanafanya kazi, yana creditors na mikopo na kadhalika, ikitokea Mkurugenzi mmoja amefanya kosa ukafuta kampuni unazungumzia nini maslahi ya creditors wa kampuni hiyo? Kwa hiyo, naomba jambo hili litazamwe upya na kifungu chote cha 400A cha Muswada huu kifutwe kwa sababu ni kifungu ambacho kitatuletea matatizo makubwa katika nchi yetu na hakuna mtu atakayekuja kufungua kampuni Tanzania. Tutajikuta tuna branches za makampuni ya kimataifa na hapatakuwa na kampuni itakayosajiliwa Tanzania kwa sababu ya kifungu hiki. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pointi yangu ya mwisho ni kuhusu trusts. Sheria hii inakwenda kutafsiri upya maana ya trust. Leo hii tukipitisha sheria hii Tulia Trust inafutwa, Mwalimu Nyerere Foundation inafutwa kwa sababu tafsiri mpya…

T A A R I F A

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: Taarifa.

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Tafsiri mpya ya trust ni ku-manage properties.

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: Taarifa.

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Tulia Trust inasaidia shule na kadhalika, sheria mpya inazuia. Sheria mpya inazuia Benjamin Mkapa Foundation kufanya kazi.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Zitto Kabwe, kuna taarifa, Mheshimiwa Mchengerwa.

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: Mheshimiwa Naibu Spika, michango ya ndugu zetu inatudhalilisha sisi wengine ambao tulitumia muda wetu mwingi kufanya kazi kwenye eneo hili.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: Waheshimiwa Wabunge, niwaombe watambue kwamba ni vyema wanapokuja kuchangia wakasoma vizuri taarifa ya Kamati lakini pia wakapitia marekebisho ambayo Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameyafanya kutokana na mapendekezo ya Wajumbe wa Kamati. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika sheria hii hakuna sehemu yoyote ambapo Msajili wa Makampuni au Msajili wa NGO ana mamlaka ya kufuta NGO au kampuni, akaamka tu mwenyewe akaenda kufuta, hayo maneno ni ya uongo na hayapo kabisa kwenye sheria hizi. Pia sheria hii inakwenda tu kuweka utaratibu wa namna gani ya kusajili trust pamoja na NGO na makampuni na ni utaratibu wa kawaida kama ambavyo unatumika katika nchi zote za Jumuiya ya Madola. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Zitto Kabwe, unaipokea taarifa hiyo?

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, siipokei taarifa hiyo kwa sababu Mheshimiwa Mwenyekiti wa Kamati hana credibility tena ndani ya Bunge, ameshawahi kukataa taarifa yake ya Kamati ndani ya Bunge. (Makofi)

T A A R I F A

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: Taarifa.

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Nina Muswada na Schedule of Amendments.

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: Taarifa.

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimalize, muda wenyewe umebakia dakika mbili tu, naomba nimalize.

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: Taarifa.

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimalize.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Mollel.

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: Mheshimiwa Naibu Spika, nataka tu nihoji credibility ya Mheshimiwa Zitto…

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nimpe taarifa kwamba hata yeye tuna-doubt credibility yake baada ya yeye kuwa Mwenyekiti wa PAC na madudu yaliyoko NSSF na akatulia na hakusema chochote na mpaka leo hasemi. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Zitto Kabwe.

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, hiyo hata kuijibu sihitaji kuijibu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nina Muswada na Schedule of Amendments, Muswada una-define trust kama ku-keep properties alone. Kwa hiyo, hata kazi ambazo zinafanywa na wastaafu wetu kuunda taasisi baada ya kustaafu zitazuiwa na sheria hii ambayo tunaitunga. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, point yangu ya mwisho, kuna suala zima la NGOs kusajiliwa upya kila baada ya miaka kumi. Naomba jambo hili tuliboreshe, tutofautishe certificate of incorporation na leseni ya kazi. Leseni inaweza ikawa- renewed kila baada ya muda, wanaweza wakaweka regime kwamba baada ya NGO kusajiliwa ipewe leseni ya kufanya kazi, ile leseni inaweza ikawa-renewed…

KUHUSU UTARATIBU

MHE. JOHN W. HECHE: Kuhusu utaratibu.

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Lakini siyo board corporate kila baada ya miaka kumi ife …

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Zitto, kuna Kanuni inavunjwa.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu utaratibu. Wakati Mheshimiwa Zitto anaongea hapa kuna mtu amesimama anatoa taarifa anasema Mheshimiwa Zitto alifanya madudu kwenye PAC na amekuwa na utaratibu wa kushambulia watu kila siku na inaachwa hivyohivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kutumia Kanuni ya 64(1)(f) aseme hayo madudu ambayo watu walifanya kwa sababu hili Bunge haliwezi kutumika kama chombo cha kudhalilisha watu na maneno ya mtaani tu yanaingizwa humu na yanaachwa, athibitishe.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, alikuwa akichangia Mheshimiwa Zitto akasimama Mheshimiwa Dkt. Mollel na akasimama Mheshimiwa Zitto kuendelea na mchango wake. Amesimama Mheshimiwa Heche akieleza kwamba Kanuni ya 64 utaratibu umevunjwa na Mbunge aliyezungumza kabla Mheshimiwa Zitto hajazungumza.

Waheshimiwa Wabunge, kwa ajili ya muda wetu ili mchangiaji aweze kumalizia; Kanuni hii inataka unapozungumza kuhusu utaratibu wa mtu ambaye ameshapita kabla mwingine hajasimama, Kanuni hii siyo unaweza kutumia sanasana ungeweza kusimama kuomba mwongozo baadaye kama jambo alilolifanya linaruhusiwa kwa taratibu zetu za Bunge. Sasa kwa sababu umesimama kuhusu utaratibu, anayeweza kuambiwa anavunja Kanuni ni Mheshimiwa Zitto kwa sababu alikuwa ameshasimama. Ndiyo maana nikasema Mheshimiwa Zitto kuna Kanuni inavunjwa.

Mheshimiwa Zitto, endelea. (Makofi)

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri kwamba Serikali ilete schedule of amendments kutofautisha kati ya cheti cha usajili kwa sababu cheti cha usajili kwa mujibu wa sheria ni perpetual na leseni ya kufanya kazi ili leseni iweze kuwa-renewed.

Mheshimiwa Naibu Spika, namalizia kwa kusema kwamba sheria hii ni sheria mbaya, Muswada huu wa sheria na naomba niwe on record ndani ya Bunge hili kwamba nimekataa kuunga mkono Muswada huu, ni sheria mbaya, leo ni one of the darkest days in our democracy. Tunakwenda kutunga sheria ya kuendelea kudhibiti watu na kuwanyima uhuru wao kama tulivyofanya kwenye Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Vyombo vya Habari na ni mwendelezo. Hii ndiyo imekuwa sifa kubwa ya Serikali ya Awamu ya Tano kukandamiza raia wake, kunyima haki raia wake na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu yana mwisho haya, mtaondoka madarakani na sheria hizi hizi zitatumika kuwanyonga ninyi. (Makofi)
Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: …..watu 20,000 wapelekwe kule wanafunzi waweze kusoma. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, chuo kikuu kingine napendekeza kijengwe Mtwara kwa ajili ya Mikoa ya Kusini. Na Chuo Kikuu cha Lake Tanganyika ama kijengwe Katavi au Kigoma au Tabora kwa ajili ya Mikoa ya Magharibi; hapa tutakuwa tumejenga uwezo wa kuwa na watu 60,000 zaidi kwenye vyuo vikuu vya umma na tukitanua vyuo vikuu ambavyo tunavyo sasa hivi, uwezo wa wanafunzi wote wanaostahili kuingia kwenye vyuo vikuu vya umma utakuwepo na hivyo tutaweza kuhakikisha ya kwamba tunaondokana na tatizo kubwa la ubora kwenye vyuo binafsi, ambalo tunalo sasa hivi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ambalo ninalipendekeza, na hili ni kwa Kamati zote ni kwamba Kamati zinatoa maoni yao hapa na mapendekezo, mapendekezo yanapitishwa. Mfumo tulionao hivi sasa na mapendekezo haya kufuatiliwa na Kamati yenyewe, na kulingana na wingi wa kazi za Kamati jambo hili limekuwa halifanyiki. Wabunge ambao ni wazoefu wa muda mrefu wanafahmu hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nadhani kuna haja ya kuhakikisha kwamba tunakuwa na Kamati Maalum ya Bunge ya Ufuatiliaji wa Mapendekezo ambayo yanakua yametolewa na Kamati za Bunge. Vinginevyo tutakuwa tunaongea hapa tunaonekana kama tunaimba tu. Kila mwaka tutakuja tutapokea taarifa, tutakuwa kama tunaimba tu na hatutakuwa na msaada wowote ambao tunakwenda nao. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ambalo nataka kulizungumza lipo kwenye Kamati ya UKIMWI. Kamati hii imeshughulikia suala ambalo sasa hivi ndiyo ajenda. Sasa hivi kila mtu anazungumzia vita dhidi ya dawa za kulevya, ambayo imeanzishwa na mmoja wa Wakuu wa Mikoa hapa nchini katika eneo lake, lakini imekuwa kama vita ya kitaifa hivi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini Waheshimiwa Wabunge wakijielekeza kusoma kwenye ukurasa wa 11 wa Taarifa ya Kamati ya UKIMWI, imeeleza kinagaubaga kwamba, mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya ambayo imeundwa kutokana na Sheria ya Bunge hapa haipewi uwezo kabisa wa kufanya kazi. Kwa hiyo, hata tukiendesha kampeni hizi namna gani, kila mtu atakuja na kampeni yake, lakini hatutaweza kuzifanya kampeni hizi kuwa endelelevu kwa sababu, vyombo ambavyo tumeviweka kwa ajili ya kupambana na tatizo hili sisi wenyewe hatuvipi uwezo wa kufanya kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ya Awamu ya Tano ina ajenda ya kubana matumizi. Inabana matumizi mpaka kwenye vyombo ambavyo vinapaswa kufanya kazi ambayo sasa yanatoka matamko ambayo dhahiri kabisa yanaenda kinyume na mfumo wetu wa utoaji haki. Sasa jambo hili tusiliangalie kishabiki, tusiangalie ni mtu gani amesema, amepingwa na nani anaungwa mkono na nani, tutakuwa tunakosea sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hii nchi hii kwa mujibu wa Katiba, you are innocent until proven guilty. Tunachojengewa sasa hivi moja ni kwamba once you are accused you are guilty, hili ni tatizo na hili ni tatizo ambalo Bunge hili lazima ilikemee, kwa sababu Waheshimiwa Wabunge hii ni kama mtego wa panya huu, leo hii kuna watu wamekamatwa, kesho Mkuu wa Mkoa mmoja ana chuki na Mbunge anasema nenda karipoti polisi una dawa, utasema nini? Na sisi kama hatukusimama kuhakikisha kwamba mfumo wa haki unafanya kazi hakuna atakayesimama kututetea atakapotufikia sisi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo naomba sana, kwanza hakuna mtu anayeweza kuthubutu kukataa kwamba tuna tatizo la dawa na ni lazima kulifanyia kazi, hakuna mtu ambaye anakataa. Lakini ni lazima sisi kama watunga sheria, sisi kama wasimamizi wa Serikali tusimame kidete tuseme kwamba ni lazima taratibu zetu za kisheria na Katiba ziweze kufuatwa, na hii itatusaidia sana. Maana matamko ambayo wakati mwingine yanaweza kuwa ni matamko ya kawaida yanatoka lakini madhara yake yanakuwa ni makubwa sana katika vita yenyewe ambayo tunakuwa tunapambana nayo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mimi rai yangu, na mengine nimeyotoa kwa maandishi kwa sababu nilidhani kwamba muda utakuwa ni mfupi sana; rai yangu kubwa ni hiyo; na kwamba kama vita hii ni vita ya zaidi ya mkoa mmoja, basi vita hii iendeshwe na viongozi wa kitaifa wenye mamlaka katika maeneo hayo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi Kigoma kule huwa tuna msemo, “ukiona kifaranga yuko juu ya chungu ujue chini kuna mama yake. Tukiendekeza hali hii tutakuja kupata matatizo makubwa sana; tulaani, lakini tuhakikishe haki inatendeka. Tushiriki kwenye kupambana, lakini tuhakikishe haki inatendeka. Hata siku moja tusionee mtu wala tusimfanye raia yeyote nchi hii aonekane kwamba anaonewa kwa sababu yeye hana madaraka, kwa sababu yeye ni mnyonge, kwa sababu yeye hana vyombo vya ulinzi na usalama vya kuweza kuagiza na kufanya vitu ambavyo anaweza kufanya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi yangu ni hayo. Nakushukuru sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, nami nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia hotuba ya Wizara hii muhimu sana, ambazo ni Wizara tatu kwa pamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa napenda niwashukuru sana Mamlaka ya Bandari kwa kazi ambayo wanaifanya Kigoma, nimeona zabuni ya bandari ya Kibirizi, ninaamini kabisa bandari ya Ujiji zabuni yake itakuwa ama imetoka leo au Jumatatu na pili bandari ya Kagunga imekamilika, kwa hiyo, napenda niwashukuru sana, nataraji kwamba hatua zitakazofata bandari ya Mwamgongo na bandari ya Mtanga zitaweza kufanyiwa kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pili nimeona ukurasa wa 102 wa hotuba ya Waziri kuhusiana na uwanja wa ndege wa Kigoma, nashukuru sana kwamba sasa zabuni itatangazwa tena na kuhakikisha kwamba tunapata mkandarasi kwa ajili ya kujenga jengo la abiria na njia zinazoenda pale. Hii ni ishara kwamba naungana mkono na juhudi za Mkoa wa Kigoma na Wabunge na wananchi wa Mkoa wa Kigoma kutaka kuubadilisha Mkoa wetu ule uweze kuwa na maendeleo ya kasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la kwanza ambalo nataka kuzungumzia ni reli, wenzangu wamezunguka hapa kuhusu reli na ukitazama hotuba ya Waziri wameendelea toka mwaka jana tumelalamika kuhusu jambo hili, kwamba wametoa tafsiri mpya ya reli ya kati. Reli ya kati tafsiri yake ni Kigoma - Dar es Salaam au Dar es Salaam - Kigoma, maeneo mengine yote ni matawi ya reli ya kati. Ukitoka Ruvu kwenda Tanga ni tawi, kutoka Tabora kwenda Mwanza ni tawi, kutoka Manyoni kwenda Singida ni tawi, ukitoka Kaliua kwenda Mpanda ni tawi, mengine yote hayo ni matawi. Reli ya kati ni Dar es Salaam – Kigoma na Kigoma - Dar es Salaam. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa standard gauge kwa hatua hizi wanazoziita hatua za awali unatoka Dar es Salaam kwenda Mwanza. Nilikuwa namuomba Waziri atafute andiko ambalo Mbunge wa zamani Mheshimiwa Ali Karavina aliandika, alikuwa Transport Economist Shirika la Reli wakati ule TRC, angalia takwimu ni wapi ambapo utapeleka reli upate fedha za kujenga maeneo mengine. Kwa sasabu lango la mashariki la nchi yetu ni Dar es Salaam, lango la magharibi la nchi yetu ni Kigoma.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, takwimu zinaonyesha kwamba mizigo ambayo Tanzania inahudumia kwa nchi za Maziwa Makuu, nchi ambazo zinaizunguka Tanzania ni tani milioni tano kwa mwaka, kwa taarifa ya hali ya uchumi ya mwaka 2015/2016. Katika hizo asilimia 34 ni Zambia, asilimia 34 Congo, asilimia 12 Rwanda, asilimia sita Burundi, asilimia 2.6 Uganda. Unapoanza na standard gauge matrilioni ya fedha, ukaipeleka Isaka na Mwanza maana yake ni kwamba unaenda kuhudumia mizigo asilimia 15 ya mizigo yote ambayo tunaipitisha unaacha kwenda kuhudumia mizigo asilimia 40, kwa maana ya Congo na Burundi ambayo yote inapita Kigoma. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, economics gani ambazo mmezitumia katika kuhakikisha kwamba reli inaelekea mahala ambapo hakuna mzigo, economics gani ambazo mmezitumia? Sipendi kusema kwamba Kigoma inatengwa siyo lugha ambayo mimi kama kiongozi napenda kuzungumza. Suala hili takwimu zote za kiuchumi zinaonesha reli inapaswa kwenda kule ambapo kuna faida. Hampeleki kule ambapo kuna faida hii maana yake nini? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, siyo hivyo tu Waziri, kuna fedha za Benki ya Dunia ukurasa wa 187 wa hotuba yako kwa ajili ya ukarabati wa reli, hata hizi bilioni 200 za ukarabati wa reli ambao upo sasa, hivi na zenyewe mmepeleka kule ambako mnapeleka standard gauge, mnashindwa hata kutudanganya kwa pipi? Hata kutudanganya Diamond aliimba nidanganye nidanganye nidanganye tu, mnashindwa! Angalau mngetupa hizi bilioni 200 mkakarabati reli ikafanya kazi mkapata fedha za kujenga huko ambako mnataka kupeleka standard gauge. Hili jambo naomba mlitazame vizuri, mliangalie kwa sababu haliendani kabisa.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata ukiangalia Waziri bandari zako, angalia takwimu za mwaka jana, bandari zipi ambazo zinakua, bandari ya Kigoma growth rate yake mwaka jana twelve percent, bandari zingine zote ni negative growth. Bandari ya Mwanza mwaka jana negative 41 percent mnapeleka reli huko, mnaacha kupeleka reli mahali ambapo mtapata fedha ili mpeleke reli sehemu nyingine. Hebu mtueleze hizi ni siasa, huu ni ukanda au ni uchumi katika maamuzi ambayo mmeyafanya kwa sababu hamueleweki.

Ninaomba jambo hili muweze kulitazama vizuri kwa sababu jambo hili linaleta hisia ya kwamba hamuendeshi nchi kwa mujibu wa Katiba. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Katiba Ibara ya 9(d) Serikali ihakikishe kwamba maendeleo ya uchumi ya Taifa yanakuzwa na kupangwa kwa ulinganifu na kwa pamoja. Hizi sentiments mnazisikia za watu wa Kusini, sentiments mnazisikia za watu wa Magharibi hazijengi umoja wa Taifa, hili jambo naomba mlitazame vizuri ili liweze kufanyiwa kazi inavyotakiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pili katika reli ambalo nataka kulizungumzia leo nataka kuongea na reli tu. Pili, what are offsets agreements katika uchumi huu wa reli? Tunatenga fedha nyingi sana kwa ajili ya ujenzi wa reli. Tunawezaje ku- link ujenzi huu, kipindi hiki cha ujenzi na ukuaji wa sekta ya viwanda. Forwards na backwards linkages kwenye mikataba mmezitazama namna gani? Waziri nakuomba google tu kwenye Ipad yako hapo kitabu cha Transport and Developing Countries kimeandikwa na Dr. David Hilling. Kinaeleza namna ambavyo in 18th century ujenzi tu wa reli ulivyoweza ku- transform uchumi wa Italy.

Nheshimiwa Naibu Spika, tunaweza kabisa juhudi zetu za ujenzi wa viwanda tukazi-link na ujenzi wa reli, tusifanye makosa tuliyoyafanya kwenye bomba la gesi la Mtwara, ambapo kila kitu kilichofunga lile bomba kilitoka China. Leo bomba linatumika only six percent hamna maendeleo yoyote ambayo tumekuja kuyapata kama nchi mpaka sasa. Kwa hiyo, naomba hili jambo mliangalie forward and backward linkages, iangalieni hiyo mikataba upya. Offsets agreements ni muhimu sana kwenye mikataba mikubwa namna hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la mwisho katika hili la reli ni suala la kwa nini wenzetu Ethiopia walikosa fedha kama sisi tunahangaika kutafuta fedha, wakatoa bond ya wananchi, sovereign bond ya wananchi, especially diaspora wakanunua kujenga The Millennium Dam ambayo inatengeneza ten thousand megawatts za umeme.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Hussein Bashe ameongea asubuhi hapa, ili tufaidike vizuri badala ya reli kuishia Morogoro, kipande hiki na kipindi hiki cha miezi hii reli ingefika Makurupora na mkaweka dry port pale Makutupora, kwa sababu mnakuwa na long haulage, unakuwa na economies of scale kwenye reli, lakini tunajua hatuna fedha, shirikisheni wananchi tupate fedha ya kufanya kipande hiki kwa kutoa bond, fifteen years. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, leteni sheria hapa kwenye Bunge, tutunge sheria ambayo kila mwaka tuta-allocate a certain amount of budget kwa ajili ya kulipia hizo percent ambazo tutaliwapa hao watu, ambao ni bond holders, after fifteen years tutakuwa tumefanya hiyo kazi, tumejenga reli na hamtakuwa mnahangaika. (Makofi)

Mheshimia Naibu Spika, ninyi mnajifungia ndani wenyewe, hamtaki kusikia mawazo ya watu wengine, watu wengine wakizungumza mnaona kama wanapinga, hakuna mtu ambaye anaweza kupinga maendeleo ya nchi kwa sababu ni maendeleo yetu wote. Kwa hiyo, nilikuwa nawaomba mtazame jambo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, angalieni uwezekano wa kuwa na railways bond angalau kipande ambacho mnataka kiishie Morogoro, kiishie Makutupora ili tuweze kupata fedha za kujenga maeneo mengine, vinginevyo hatutaweza kwenda huko tunakotaka kwenda. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, maelezo yangu mengine nimeyaandika kwa maandishi, nadhani nimeshaleta, mtaweza kuangalia namna gani mtakavyoweza kujibu. Nawashukuru sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuweza kuchangia hotuba hii ya Wizara muhimu sana. Pili, nampongeza sana Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, kwa hotuba ambayo imeweza kuchambua, kukosoa na kutoa mapendekezo ya namna gani ya kuboresha. Vile vile, nampongeza Mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda na Biashara kwa kuleta maoni ya Kamati na maoni ya Kamati ndiyo maoni ya Bunge, kwa sababu Kamati inafanya kazi kwa niaba ya Bunge. Naamini kabisa kwamba Mheshimiwa Waziri ataweza kuyafanyia kazi yote haya; hotuba ya Waziri kivuli na hotuba ya Mwenyekiti wa Kamati ili kuweza kuboresha kazi ambazo tunafanya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2016 mwezi kama huu tulipokutana kwa ajili ya kujadili hotuba ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Tanzania ilikuwa inauza nje bidhaa za viwanda za thamani ya Dola za Kimarekani bilioni
1.4 kwa mujibu wa taarifa ya Benki Kuu ya mwezi Machi, 2016. Bidhaa za viwanda ziliingizia Taifa mapato ya fedha za kigeni wakiwa ni wa pili baada ya utalii na wakiwa mbele ya dhahabu ambayo iliingiza Dola za Kimarekani bilioni 1.2; utalii bilioni mbili.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo tumekutana mwaka mmoja baadaye kwa kuchukua mwezi Machi, 2016 na mwezi Machi, 2017 bidhaa za viwanda ambazo tunauza nje, zimeshuka kwa Dola za Kimarekani milioni 500 kutoka 1.4 mpaka 0.9 million Dollars. Sasa tunaposimama hapa na kusema kazi inafanyika, Mheshimiwa Waziri atusaidie kwamba iwapo kazi inafanyika, kuna ongezeko la uzalishaji, ni kwa nini mauzo yetu nje yamepungua kwa kiwango kikubwa kiasi hiki?

Mheshimiwa Naibu Spika, haya ndiyo mambo ambayo ni vizuri sana Waheshimiwa Wabunge wazingatie. Kwa sababu bidhaa za viwanda zinazouzwa nje zinavyopungua, maana yake ni kwamba viwanda vyetu vya ndani vimepunguza uzalishaji; maana yake ni kwamba kuna watu wapoteza kazi; maana yake ni kwamba kuna mapato ya Serikali ambayo yamepotea. Sasa ndani ya miezi 12, tumepoteza mauzo nje kwa zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 500. Sijui ikifika 2020 kama kutakuwa kuna hata senti moja ambayo tutakuwa tunaipata kutokana na mauzo nje. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, tuna tatizo kubwa kwamba tuna viwanda ambavyo vimekuwepo, lakini uwezo wetu wa kulinda viwanda vyetu umekuwa ni mdogo sana. Mheshimiwa Waziri ni shahidi wa malalamiko ambayo anapelekewa kila mwezi ya watu ambao wanaingiza nguo kinyemela katika nchi yetu, wanaingiza mafuta ya kula kinyemela katika nchi yetu, wanaingiza battery kinyemela katika nchi yetu, zinakuwa na bei ndogo; na matokeo yake ni kwamba viwanda vya ndani vinashindwa kushindana nao katika soko na tunapoteza ajira. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nina mfano mzuri sana; jana niliangalia takwimu za kiwango gani cha battery tumeagiza kutoka China kwa miezi sita ya kwanza ya mwaka 2016. Ukienda Idara ya Customs ya China, utakuta kwamba kati ya Januari mpaka Septemba, mwaka 2016, kwa records za China, tuliagiza battery za thamani ya Dola za Kimarekani milioni 36.5, kwa takwimu za China.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukija kuangalia Idara yetu ya Forodha hapa, battery ambazo zimeingia nchini na ukilinganisha na TBS, battery ambazo wamezifanyia ukaguzi kuona ni ngapi zimeingia nchini ni za thamani ya Dola za Kimarekani milioni 5.3. Maana yake ni kwamba, kuna battery nyingi sana ambazo zinaingia nchini hazipiti katika njia za kawaida. Viwanda ambavyo vinazalisha battery hapa nchini kama Panasonic ambavyo vimeajiri watu, vinashindwa ku- compete na hizo battery zinazotoka especially China. matokeo yake ni kwamba tutaongea humu kuhusu viwanda lakini in real sense tunaviua hivyo viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, haya ni mambo ambayo tungetegemea kuona Mheshimiwa Waziri akihangaika nayo, kwa sababu wahenga wanasema “Ni bora ndege ambaye unae mkononi kuliko ndege ambaye yuko juu ya mti ambaye unataka kwenda kumtungua. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la tatu ambalo nataka kulizungumzia; sisi tuna miradi mikubwa mingi sana, miradi mingine ni ya mabilioni ya fedha. Kuna miradi ambayo inatoa fedha nje na kutengeneza ajira nje. Kwa mfano, manunuzi ya ndege, tunaposema tunanunua boeing, maana yake ni kwamba tunapeleka ajira Marekani. Kuna miradi ambayo inatengeneza ajira ndani na ingeweza kwa kiwango kikubwa kuchochote ukuaji wa Sekta ya Viwanda na mfano mzuri sana ni reli.

Mheshimiwa Naibu Spika, tuna mradi wa zaidi ya Dola za Kimarekani bilioni saba kwenye reli. Reli raw materials zake ni nini? Sehemu kubwa ni chuma. Unahitaji tani 50 za steel, chuma cha pua, kujenga kilomita moja ya reli. Sasa hivi sisi tumewapa Waturuki mkataba. Wataagiza kila chuma ambacho kinakuja kwenye reli yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Deo pale amezungumzia Mchuchuma na Liganga; siyo kama hatuna chuma; tunacho chuma Mchuchuma na Linganga. Kabla ya kuanza kufikiria kutandika haya matararuma ya reli, ilitakiwa tuwe tayari tumejenga uwezo wa kuzalisha kule ili fedha zote zibakie ndani ya nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nashindwa kuelewa; mimi kwa kweli sielewi. Hivi Mheshimiwa Mwijage mnakaa kwenye Cabinet Baraza zima, mkajadili hii mipango? Kwa sababu mkikaa, lazima kuna mtu atasema aah, huu ujenzi mimi miradi yangu fulani itaweza kufaidika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunajenga mabehewa. Mabehewa yana viti. Hivi wamefikiria namna gani ya kuendeleza zao la katani ili viti vya kwenye mabehewa viweze kuwa ni viti vya katani! (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tuna concrete, mmeandaa vipi watu ambao wanazalisha kokoto kwa ajili ya ku-supply kwenye reli? Hili ndiyo fungamanisho, kwa sababu una fedha, una dola shilingi bilioni saba zitakazoingia ndani ya nchi, over a period of five years or seven years, hizi fedha kama seventy percent zinatoka nje, tunafanya nini? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, angalieni interior decoration za mabehewa, ni ngozi. Mmekaa mkafikiria namna gani ya kufungamanisha Sekta ya Ngozi na mabehewa? Haya ndiyo mambo ambayo tungependa kuyaona tukiyajadili. Kwa sababu hizi huhitaji foreign direct investments, hizi ni fedha ambazo tayari mnaziingiza. Ni kiasi cha kuingia kwenye mikataba na kuweza kufanya. Kwa hiyo, sasa hivi sisi kwenye reli tutafaidika na nini? Ajira tu! Ajira za vibarua baada ya zile, hakuna kuchochewa kwa... (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Katibu Mkuu wa Mheshimiwa Waziri wa Viwanda ni Mwalimu wangu wa Economics. Mwaka wa tatu amenifundisha input, output modal. Sekta zote za uchumi, yaani unachukua sekta, njia hii na njia hii, ukiingiza kwenye transport unapata nini kwenye manufacturing? Unapata nini kwenye kilimo? Unapata nini kwenye nini?

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa sitaki kumwambia Profesa Mkenda kwamba nimrudishie degree yake. Kwa sababu yeye ndio Katibu Mkuu responsible wa hii Wizara; yeye pamoja na mwenzake Dkt. Meru. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, haya mambo ni mambo ambayo yanapaswa kutengenezewa mkakati, tusipoteze fedha. Kwa sababu ni fedha zetu! Tena tunasema tunajenga kwa fedha za ndani, lakini fedha za ndani zitaenda kutengeneza reli India au China au Uturuki, ziletwe hapa.

Mheshimiwa Naibu Spika, niliwaambia hapa wakati nachangia mchango wa Wizara ya Uchukuzi. Kumbukeni bomba la gesi, kila kitu ambacho kimejenga bomba la gesi kimetoka China. Nothing ambacho kimetoka hapa ndani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nawaomba Wizara wakae upya waangalie, fungamanisho ndiyo solution. Tutaweza kupiga hatua kubwa na kuchochea maendeleo makubwa kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tunatumia fedha za miradi yetu kwa ajili ya maendeleo.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi kwa leo ni hayo tu. Usia wangu ni huo tu, sina mengine ambayo nataka kuyachangia.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Maji na Umwagiliaji
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, leo sikupanga kuzungumza lakini nimeomba kuzungumza kutokana na hali halisi ya bajeti ya Wizara ya Maji.

Kwanza kabisa kwa mara nyingine binafsi kama Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, napenda kumshukuru sana Mheshimwa Rais kwa uteuzi wa Profesa Kitila Mkumbo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji. Ninaamini kabisa kwamba kutokana na uwezo wake, umahiri wake na weledi wake ataweza kuisaidia nchi na ujumbe utakwenda duniani kwamba ndani ya Vyama vya Upinzani kuna watu wazalendo na uwezo wa kufanya kazi, ninamtakia kila la heri Profesa Kitila. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo kubwa ambalo tunaliona na naomba Waheshimiwa Wabunge tuelewane katika hili, Mheshimiwa Rais alikuja hapa Bungeni, katika moja ya jambo ambalo lilikuwa ni very emotional kwa Watanzania ni pale Rais alipoahidi kuwatua akina mama ndoo kichwani.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeona Makamu wa Rais akizunguka kila kona ya nchi hii kufanya kazi hiyo, hata bajeti ya mwaka jana picha iliyokuwa mbele ya kwenye bajeti ilikuwa ni picha ya Makamu wa Rais anamtua mama ndoo kichwani, lakini kwa masikitiko makubwa sana bajeti ya Wizara ambayo ndiyo inawahusu Watanzania moja kwa moja imeshuka kutoka bilioni 915 za maendeleo mpaka bilioni 623 za maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, unatafsiri vipi uwekezaji wa rasilimali fedha namna hii kwenye ajenda ya kuwashusha na kuwaondolea kina mama ndoo kichwani. Waheshimiwa Wabunge nilikuwa nawaomba kwa siku tatu hizi za bajeti hii, najua tuna kero zetu kwenye majimbo, najua tuna matatizo kwenye mikoa yetu na kila mtu ataanza kuongelea mradi wake, iwapo hatutaungana pamoja na kutaka bajeti ya Wizara hii irudishwe angalau kwa mpango ule wa mwaka jana, hayo malalamiko yote mtakayoyatoa kwenye majimbo yenu hayatakuwa na maana yoyote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi kama Bunge tunayo hayo mamlaka, Kanuni za Bunge zinaturuhusu kuitaka Serikali ikapange upya bajeti hii, kama unaguswa na kero ya maji kwenye eneo lako, kama unaguswa na kero ya maji kwenye mkoa wako au jimbo lako au kijiji chako una njia moja tu ya kufanya ya kumsaidia Waziri bajeti hii iende ikaandikwe upya, tupate bajeti angalau ile ya mwaka jana iweze kurudi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hili jambo siyo la Vyama, wanaoumia na maji ni watu wa vyama vyote na watu wasio na vyama vilevile. Nimeomba dakika hizi tano kwa ajili ya kui-set hiyo trend na tuweze kuiambia Serikali, kuna mapendekezo mengi Kamati ya Maji imetoa maependekezo kuhusiana na Rural Water Agency, imetoa mapendekezo kuongeza fedha kwenye mafuta kwa ajili ya kuweza kuelekeza maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hiyo bajeti ya mwaka jana ya bilioni 915 ni asilimia 19.8 tu ya miradi ya maendeleo ndiyo imepelekwa kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ambayo imetueleza hapa. Hata Waziri mwenyewe kwenye hotuba yake ukurasa wa 120 ameeleza, tuchague, tupige kelele humu ndani, tulalamike, halafu tuonekane tumesemea watu wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, au tuchukue hatua ya kuhakikisha kwamba bajeti ya Wizara ya Maji inakwenda kurudishwa angalau kwenye kiwango cha mwaka jana. Naomba Waheshimiwa Wabunge huo ndio uwe mjadala wetu na huko ndiko ambako twende, tuweze kuwatua akina mama ndoo kichwani. Ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, Ibara 106 katika ukurasa wa 68 wa hotuba inayozungumzia mazao yanayozalisha mafuta ya kula, Mkoa wa Kigoma ni mzalishaji mkubwa wa mawese na uzalishaji wake unaweza kusaidia nchi kupunguza uagizaji kutoka nje. Mkoa wa Kigoma umeandaa mkakati wa kuendeleza zao la michikichi na kupitishwa na RCC ya Mkoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Serikali Kuu ishirikiane na Halmashauri za Serikali za Mitaa Mkoa wa Kigoma ili kuwezesha utekelezaji wa mkakati huu. Tunategemea kuwa wakulima wadogo 100,000 wenye hekta moja kila mmoja watahusika na uzalishaji wa mawese na hivyo kukuza viwanda mkoani Kigoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba zao la mawese lisisahaulike, ni ukombozi kwa Mkoa wa Kigoma. Kuna fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa ajili ya mazao ya mafuta ya kule. Wizara ishirikiane na Sekretarieti ya Mkoa wa Kigoma kufanikisha hili. Manispaa ya Kigoma Ujiji inaomba msaada wa kununua miche milioni moja ili kuweza kupanda kwenye msimu huu wa kilimo kuanzia Novemba. Tunaomba Wizara ishirikiane na sisi kufanikisha mradi huu wenye ukombozi mkubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu hifadhi ya jamii kwa wakulima, naishauri Serikali kupanga sera na baadaye sheria itakayowezesha wakulima kuwa na hifadhi ya jamii. Nimeona mafanikio ya wakulima scheme ya NSSF. Hata hivyo, tunaweza kuwa na wakulima wengi zaidi kwenye hifadhi ya jamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tutungie sheria suala hili ili mafao kwa wakulima yawe ya kisheria. Fao la bei itakuwa ni ukombozi mkubwa sana kwa mkulima. Hifadhi ya jamii inaendelea na kuwepo kwa fao la bei.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuwa mchangiaji wa mwisho leo katika Wizara hii.

Kwanza napenda kuwapongeza wachangiaji wote wa pande zote ambao wamechangia katika Wizara hii, wameonesha maeneo mbalimbali ambayo wanadhani kwamba yana haja ya kuboreshwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda niwapongeza kwa dhati kabisa Kamati ya Kilimo kwa kazi kubwa ambayo wameifanya ya uchambuzi wa bajeti hii na vilevile Waziri Kivuli wa Kilimo kwa maoni na mapendekezo ya Kambi ya Upinzani Bungeni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, takwimu nyingi zimeelezwa hapa kuhusiana na Wizara hii na takwimu hizo zinaonesha ni namna gani ambavyo Wizara hii ni muhimu sana na ingehitaji kuwekewa nguvu za kutosha katika namna ambavyo inatekelezwa. Mwaka 2009 pato la Taifa la nchi yetu lilikuwa ni dola za Kimarekani bilioni 21.4. Mwaka 2016, miaka saba baadaye, pato la Taifa la nchi yetu lilifikia dola za Kimarekani bilioni 52.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maana yake ni kwamba ndani ya kipindi cha miaka saba, tuliweza ku-double na zaidi pato la Taifa, lakini viwango vya umaskini wa Watanzania vimekuwa vikiongezeka kwa maana ya idadi ya watu maskini Tanzania imekuwa ikiongezeka licha ya pato la Taifa kuongeza zaidi ya mara mbili. Sababu ni nini? Sababu ni sekta ya kilimo. Hatuwekezi vya kutosha kwenye sekta ya kilimo na ndiyo maana malalamiko ya Wabunge yamekuwa ni mengi sana katika hili eneo. Kwa sababu kama una sekta ambayo watu asilimia 65.5 kwa mujibu wa takwimu za Serikali wanaitegemea, lakini sekta hii katika fedha zake za maendeleo inapelekewa asilimia tatu tu, ni dhahiri kabisa kwamba hatuwafanyii kazi Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu Wizara zote, tunaweza tukawa tunajadili na tukapitisha bajeti, lakini Wizara ambayo inawahusu Watanzania moja kwa moja ni Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi lakini mmeona dhahiri namna gani ambavyo Wizara hii bajeti yake, hata ile kidogo ambayo imetengwa, bado haiendi. Ukienda kuangalia vitabu vya maendeleo utaona kwamba katika kitabu cha maendeleo sehemu kubwa ya bajeti ambayo tuliitenga mwaka jana kwa ajili ya bajeti ya kilimo ilikuwa ni Storoge Capacity Expansion Project (Utunzaji wa Mazao yetu baada ya Uvuvi) mradi ambao ulikuwa ufadhiliwe locally na foreigners walikuwa ni Poland. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaposema kwamba ni bilioni tatu ambazo zimepelekwa kwenye Wizara hii maana yake ni kwamba mradi kama huu wote mwaka jana haukutekelezwa. Maana yake ni kwamba mwaka jana tumewalipa mishahara, tumewapa posho, tumewaweka ofisini wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo lakini hakuna kazi yoyote ya kimaendeleo ambayo ilifanyika. Hali kama hii kwa kweli inasikitisha sana na ni hali ambayo inabidi tuweze kuona ni namna gani ambavyo tutaweza kuirekebisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, licha ya kuangalia maeneo hayo ya bajeti ndogo ambayo inapelekwa ya Wizara ya Kilimo, lakini pili naomba tuweze kuangalia ni namna gani ambavyo mafanikio ambayo yamepatikana tunayalinda kivipi. Kwa mfano, napenda niwapongeze sana ndugu zangu wa Kusini kwa mavuno mazuri sana ya korosho na kwa fedha nyingi sana ambazo wamezipata kwenye korosho, lakini pamoja na ongezeko la mavuno ya korosho na ongezeko la bei ya korosho kwenye Soko la Dunia, sehemu kubwa ya mabadiliko haya ni ya bei.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwakani ikitokea kwamba bei ya korosho imeshuka, tutawafanya nini hawa wakulima na hapo ndipo inapokuja hoja ya msingi sana ya Hifadhi ya Jamii kwa Wakulima. Kuweka mfumo ambao utakuwa na fao la price stabilization ili pale ambapo bei za mazao ya kilimo zimekuwa kubwa sana, tuweze kuwa na sehemu ambayo itatunzwa, bei ikiporomoka chini ya gharama za uzalishaji kwa mkulima, mkulima yule atalipwa kumrudishia gharama za uzalishaji. Sasa hili ni eneo ambalo Waziri ameligusa, kuna paragraph moja amezungumza kuhusu Wakulima Scheme inaendeshwa na NSSF, lakini kuna haja kubwa ya kuweza kuangalia ni namna gani tutapanua hifadhi ya jamii kwa wakulima ili tuweze kuhakikisha kwamba wakulima wanakuwa na fao la bei. Siku bei zikiporomoka wakulima waweze kurudishwa katika zile bei ambazo angalau zitalinda hali yao ya uzalishaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho kabisa, naomba nirejee hoja ambayo Kambi ya Upinzani Bungeni imezungumza kuhusiana na tozo kwa wavuvi. Kuna malalamiko makubwa hasa kule kwetu upande wa Ziwa Tanganyika, SUMATRA inatoza leseni za usafiri kwa wavuvi na jana nimemsikia Waziri anasema kwamba kuna tozo ambazo zimeondolewa za kiwango fulani cha mitumbwi.

Naomba nipate ufafanuzi wa kutosha, kwa sababu SUMATRA hawatozi tozo ya leseni ya usafiri kwenye matreka, kwa sababu matrekta yanatumika kulima, lakini wanatoza tozo ya leseni ya wavuvi kwenye mitumbwi ya kuvulia. Sasa nataka nipate hapa haki inakuwa wapi, kwa sababu mvuvi hiki ndicho chombo chake cha kuzalisha, kwa nini atozwe, lakini mkulima chombo chake cha kuzalisha ambacho ni trekta yeye asiweze kutozwa? Kwa hiyo, naomba nipate maelezo haya ambayo pia Kambi ya Upinzani Bungeni imeyazungumza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa, nawapongeza sana tena Kamati ya Kilimo na naomba ninukuu sehemu ya hotuba ya Kamati ya Kilimo ambayo nadhani inahitaji majibu ya Serikali, ambayo inasema kwamba; “Kwa mwenendo huu wa bajeti unaashiria kwamba, kilimo si moja ya vipaumbele vya Serikali; Serikali haitambui umuhimu wa sekta za kilimo katika ustawi wa sekta zingine na kilimo si sekta mama ya ustawi wa wananchi ambao wengi wanajihusisha na shughuli za kilimo.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, hizi hoja za Kamati ya Kilimo, naomba zipate majibu ya uhakika kutoka Serikalini kwa sababu ndiyo hoja ambazo zinawahusu wakulima na wananchi wetu kwa ujumla. Nakushukuru sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Maji na Umwagiliaji
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, hivi karibuni kumetokea kero kubwa ya maji kwa wananchi wengi wa mijini kufuatia madeni ya umeme. Manispaa ya Kigoma-Ujiji imehusika moja kwa moja na suala hili kufuatia deni la shilingi bilioni 1.2. Hivi sasa kuna Mradi mkubwa wa Maji Kigoma. Naishauri Serikali kwamba mradi huu tutumie umeme wa jua kuendeshea mitambo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri mradi ufanyiwe marekebisho hayo, kwani kutumia umeme wa TANESCO siyo endelevu, kwani gharama ni kubwa. Kuna wafadhili wengi sana wanaowekeza kwenye nishati jadidifu, tuzungumze nao ili miradi inayoendelea sasa itumie nishati mbadala. Suala hili niliongea mwaka 2016/2017. Naomba Serikali litazameni hili, undeni kikosi kazi cha kulitazama hili la umeme wa jua kuendesha miradi ya maji mipya.

Mheshimiwa Naibu Spika, miradi mingi ya maji inayoendelea au kupangwa, inahitaji inputs ambazo nyingi zinaagizwa kutoka nje. Serikali inataka kuendeleza viwanda, ni vema kufungamanisha miradi hii na dira ya maendeleo ya viwanda. Tutazame orodha ya miradi na vituo vinavyotakiwa vikiwemo mabomba, madawa na kadhalika. Kisha tuone namna ya kuhamasisha sekta binafsi kujenga viwanda vya kuzalisha vifaa vinavyotakiwa kwenye miradi hii, hata ikibidi kuwapa guarantee sekta binafsi, tufanye hivi tuache kufanya miradi bila kutazama picha kubwa. Miradi.

mikubwa ya maji yaweza kuchochea maendeleo makubwa ya viwanda, kuongeza ajira na kutokomeza umaskini. Tusifanye kazi kwa kutazama eneo moja, bali tuwe multidisciplinary.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Maji na Umwagiliaji
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, hivi karibuni kumetokea kero kubwa ya maji kwa wananchi wengi wa mijini kufuatia madeni ya umeme. Manispaa ya Kigoma-Ujiji imehusika moja kwa moja na suala hili kufuatia deni la shilingi bilioni 1.2. Hivi sasa kuna Mradi mkubwa wa Maji Kigoma. Naishauri Serikali kwamba mradi huu tutumie umeme wa jua kuendeshea mitambo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri mradi ufanyiwe marekebisho hayo, kwani kutumia umeme wa TANESCO siyo endelevu, kwani gharama ni kubwa. Kuna wafadhili wengi sana wanaowekeza kwenye nishati jadidifu, tuzungumze nao ili miradi inayoendelea sasa itumie nishati mbadala. Suala hili niliongea mwaka 2016/2017. Naomba Serikali litazameni hili, undeni kikosi kazi cha kulitazama hili la umeme wa jua kuendesha miradi ya maji mipya.

Mheshimiwa Naibu Spika, miradi mingi ya maji inayoendelea au kupangwa, inahitaji inputs ambazo nyingi zinaagizwa kutoka nje. Serikali inataka kuendeleza viwanda, ni vema kufungamanisha miradi hii na dira ya maendeleo ya viwanda. Tutazame orodha ya miradi na vituo vinavyotakiwa vikiwemo mabomba, madawa na kadhalika. Kisha tuone namna ya kuhamasisha sekta binafsi kujenga viwanda vya kuzalisha vifaa vinavyotakiwa kwenye miradi hii, hata ikibidi kuwapa guarantee sekta binafsi, tufanye hivi tuache kufanya miradi bila kutazama picha kubwa. Miradi.

mikubwa ya maji yaweza kuchochea maendeleo makubwa ya viwanda, kuongeza ajira na kutokomeza umaskini. Tusifanye kazi kwa kutazama eneo moja, bali tuwe multidisciplinary.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. ZITTO R. Z. KABWE: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ya CCM, zililongwa mbali, zilitendwa mbali. Katibu Mkuu Hazina na sekta binafsi kushiriki kwenye sekta ya maji kinyume na sera ya Serikali na kauli ya Wizara ya Maji. Kiburi anapewa nani?

“Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na kuwepo kwa mahitaji makubwa ya kuboresha huduma za maji na umwagiliaji, mchango wa sekta binafsi kwenye uwekezaji katika kutoka huduma hizo bado si wa kuridhisha. Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi, ikiwa ni pamoja na kutunga Sera ya Taifa ya Ubia baina ya Sekta ya Umma, Sekta Binafsi ya mwaka 2009 na Sheria ya Ubia ya mwaka 2010 na Kanuni zake ili kuweka mazingira mazuri ya kuwavutia wawekezaji. Vilevile Wizara imeendelea kuwapatia wataalam wake mafunzo yanayohusu uwekezaji ikiwa ni pamoja na ubia baina ya sekta ya umma na sekta binafsi kwa lengo la kuwajengea uwezo wa namna ya kutekeleza miradi ya ubia.” Waziri wa Maji Bungeni, Mei 2018.

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati Waziri anaeleza hii kama changamoto, benki binafsi inanyang’anywa kazi ya mradi muhimu wa kupunguza gharama za uendeshaji wa miradi ya maji vijijini. Sekta binafsi itapata wapi matumaini ya kushiriki kwenye sekta ya maji?

Mheshimiwa Naibu Spika, Benki ya Dunia inapanga majaribio ya kutumia umeme wa jua kuendesha miradi ya maji vijijini kwa kutoa mkopo nafuu kwa Jumuiya ya Watumiaji wa Maji (COWSOs) kwa kushirikiana na taasisi za fedha nchini. Baada ya Benki ya Dunia kukamilisha mchakato wa kupata benki ya kufanya kazi hiyo ya kukopesha COWSOs, Serikali imeilazimisha benki hiyo kutoa kazi kwa benki nyingine ambayo kwa sasa inaelekea kuanguka kutokana na kuwa na mikopo chechefu mingi na changamoto za uendeshaji. Serikali inapotaka sekta binafsi kushiriki kwenye sekta ya maji au sekta yoyote nyingine na wakati huo huo kuweka vikwazo, huu ushuriki wa namna gani?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa nini Katibu Mkuu Hazina anataka benki iliyoshinda zabuni ya kutekeleza mradi huu muhimu iondolewe badala yake TIB wapewe kazi ambayo walishindwa na kuamua kujitoa na kwamba pia hawana uwezo wa kuifanya? Hii ni pilot tu kwa nini Hazina wasiache ifanyike ili ikiwa na mafanikio ndipo Benki ya Serikali iingie kwa mradi mkubwa? Nina zabuni ya mradi huu wa majaribio, Bunge likihitaji litawasilisha. Bunge liitake Serikali iache kuingilia mchakato huu ili tuweze kuona majaribio haya yana faida gani kwa nchi kabla ya ku-scale upya hii project.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2017.
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana nami kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue fursa hii kuwapongeza Wajumbe wote wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) kwa kazi kubwa ambayo wameifanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge wafahamu ya kwamba Kamati hizi mbili ndizo ambazo zinafanya kazi ya oversight kwa niaba ya Bunge letu, kwa hiyo ni Kamati ambazo taarifa zake ambazo tunazijadili mara moja kwa mwaka na bahati mbaya sana siku hizi kwa siku moja, ni taarifa ambazo ni nyeti mno kiasi kwamba zinahitaji tutulize akili zetu tujadiliane na tuweze kuwa na maamuzi ambayo yatawezesha tuweze kwenda vizuri kwa sababu kazi hizi ni kazi za Bunge, sio kazi za Serikali, kwa hiyo ni lazima Wabunge tuweze kufanya kazi hizi kwa ufanisi na kuweza kufanikisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ambayo ndiyo taarifa zake PAC na LAAC wameleta hapa ilizungumzia mambo mengi sana, miongoni mwa mambo ambayo yalizungumzwa ni suala la Deni la Taifa. Bahati mbaya sana na nadhani hii ni kwa mara ya kwanza tangu PAC itoe taarifa zake kwenye Bunge hii ni mara ya kwanza hatuoni chapter inayohusu Deni la Taifa. Chapter hii ni chapter muhimu ni chapter ya lazima Mama Mwenyekiti mwakani kosa hili lisirudiwe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ukitazama aliyosema CAG kuhusu Deni la Taifa inaonesha kwamba ndani ya kipindi kifupi sana Deni la Taifa limeongezeka kwa asilimia 168, lakini baya zaidi deni ambalo linatokana na masharti ya biashara limeongezeka kwa asilimia 17 ndani ya mwaka mmoja, madeni yanayotokana na masharti ya biashara, gharama zake ni kubwa sana na inawezekana uwezo wetu wa kuwalipa ukawa na matatizo makubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndani ya taarifa hii ya CAG inaonesha kwamba taarifa ambayo Serikali ilitoa kuhusu Deni la Taifa, deni la jumla ya shilingi trilioni 3.2 halikuwamo katika taarifa ya Deni la Taifa. Tulitarajia kwamba leo tungepata maelezo ni kwa nini trilioni 3.2 hazikuhusishwa katika taarifa ya pamoja ya Deni la Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo hivyo tu, kwa mujibu wa taarifa ya CAG uwiano asilimia 31 ya deni letu la nje ni commercial loans ni madeni ya kibiashara ambapo kama nilivyoeleza hapo mwanzo gharama ni kubwa mno na sasa hivi mwaka jana walikuja Waziri Mheshimiwa Philip Mpango na mwenzake Naibu wake wakaja Bungeni wakaomba ruhusa ya Bunge kukopa dola milioni 700 kwenye bajeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo nilikuwa taarifa ya Wizara ya Fedha kuhusiana na tathmini ya utekelezaji wa bajeti ya Serikali. Taarifa inasema katika mwaka wa fedha 2017/2018 Serikali imepanga kukopa dola za Kimarekani milioni mia saba zile walizoruhusiwa na Bunge. Taarifa hiyo inaendelea, Serikali imekamilisha majadiliano na Taasisi za kifedha kwa lengo la kukopa kiasi cha dola za Kimarekani bilioni 1.5 maana yake ni bilioni 1.46. Kwa ajili ya kugharamia mradi wa ujenzi ya reli ya kati kwa kiwango cha standard gauge kutoka Morogoro hadi Makutupora (Makofi).

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa Serikali inakamilisha taratibu za kusaini mikataba. Waziri Mpango ruhusa uliyopewa na Bunge dola za Kimarekani milioni mia saba. Ni wapi ulipata ruhusa ya kwenda kujadiliana kukopa ziada ya
1.5 bilioni? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wabunge wote ninyi ni mashahidi, kila siku tunaambiwa tunajenga standard gauge kwa fedha zetu za ndani. Leo Serikali inasema tunakopa kwa nini tunawalaghai wananchi, kwa nini hatuwaelezi wananchi ukweli kwamba hatuna uwezo wa kujenga kwa fedha za ndani, lakini tunakopa kuna ubaya gani? Maana yake kukopa siyo dhambi hamna mtu ambaye hana mikopo hapa, kwa nini tusiwaambie wananchi ukweli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini tunamuacha Rais anasema kwamba tunajenga kwa fedha zetu za ndani halafu tunakuja humu Bungeni taarifa za Serikali zinasema tunakopa mnamuaibisha Rais. Kwa hiyo, kuna haja ya kupata maelezo ya Serikali kuhusu masuala haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili Taasisi ya Kupambana na Rushwa PCCB imeundwa kwa mujibu wa sheria. Sheria Sura Na. 329, kifungu cha 47(2) cha sheria ile, kinaitaka PCCB kila mwaka ifunge mahesabu yake yakaguliwe na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, yapitiwe na PAC yaletwe Bungeni. Toka mwaka 2016 PCCB haijafunga mahesabu yake ya mwaka, haijakaguliwa, hawa ndiyo watu ambao wanapambana na rushwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi wamemshtaki Mhasibu wao kwa wizi wamejuaje ameiba wakati hawana audited accounts? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunahitaji maelezo ya Serikali, Taasisi hii ni special kiasi gani. Jeshi linakaguliwa, Mwamunyange alikuwa anakuja kwenye Kamati ya PAC na Makamanda wenzake wote kuelezea mahesabu ya Jeshi, kwa nini PCCB haikaguliwi? Naomba tupate maelezo ya kina kabisa ya Serikali kuhusiana na jambo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu Mama yangu Conchesta amelizungumza, LAAC wametoa taarifa nzuri sana ambayo inaelezea tatizo la asilimia 10. Waheshimiwa Wabunge tusidanganyane humu ndani, sote humu tumekuwa Wabunge wale ambao wamekuwa Wabunge sasa wana miaka kadhaa, wale ambao wamekuwa Wabunge muda mrefu wanajua, asilimia 10 kwa mazingira ya sasa hivi haitekelezeki. Waheshimiwa Wabunge fedha hizi za asilimia 10 siyo ndogo ni fedha nyingi ukiangalia bajeti ya ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti ambayo tumepitisha hapa ndani ya Bunge hii inayotumika sasa, jumla ya fedha ambazo Halmashauri zetu zinakusanya kwa mwaka ni bilioni mia sita themanini na saba (bil. 687), asilimia 10 yake ni bilioni sitini na nane, 10 percent hizi kama alivyosema mama yangu Mheshimiwa Conchesta tuzibadilishe. Tuanzishe benki na Halmashauri ziingize hizi fedha kwenye ile benki vijana na wanawake wakachukua mikopo kwenye ile benki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina hakika fedha hizi kwanza zitapelekwa kwa sababu wale mameneja wa matawi ya benki watahakikisha zinapelekwa lakini pili wananaochukua watalipa. Tutaokoa fedha nyingi sana na tutaweza kuleta maendeleo makubwa sana katika Nchi (Makofi).

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa tumepewa amri au maelekezo ya kwamba tuweke viwanda 100 kila Halmashauri kila Mkoa sijui kila Halmashauri au kila Mkoa. Serikali Kuu haina ardhi, ardhi ni ya Serikali za Mitaa, kosa kubwa tutakalolifanya ni kwenda kunyang’anya watu wetu ardhi walipwe fidia kidogo watu waje waweke viwanda, watu wale watapata hela kwa muda mfupi watazitumia zitakwisha. Hebu tubadilisheni kifikra, ardhi ya mwananchi inayotolewa kwa ajili ya uwekezaji iwe land for equity. Wananchi wapate hisa itawalipa ile kwa muda mrefu zaidi na itakuwa na mafanikio makubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna maeneo wamefanya, Mkoa wa Kigoma tumefanya Mji wa Ujiji City tumeingia mkataba na kampuni kutoka China 20 percent. Mradi mmoja wa hospitali utatupa five billion mapato ya ndani kwa mwaka mmoja. Sasa hivi mapato yetu ya ndani ni bilioni moja tu. Kwa hiyo napenda nishauri tulitazame hili, Waziri wa TAMISEMI aangalie namna ambavyo atalileta kisheria ili tulinde watu wetu tusiwafanye waje kuwa manamba wa wawekezaji bali wafaidike kutokana na uwekezaji ambao utakuwa unafanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, naunga mkono taarifa zote hizi mbili na nina maazimio ya marekebisho kidogo kwenye taarifa moja ya LAAC.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia hotuba zenye mafungu mbalimbali ya Wizara ya TAMISEMI, mafungu matatu na Wizara ya Ofisi ya Rais, Utawala Bora pamoja na Utumishi, na nitachangia maeneo kama matatu/manne tu kutokana na muda jinsi itakavyokuwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza ambalo nataka kulichangia ni la upande wa Fungu 30, Ofisi ya Rais Cabinet Secretariat ambapo ni pamoja na Fungu 20 ambapo ndipo Idara ya Usalama wa Taifa ipo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka jana tarehe 21 Julai, Rais alifanya ziara Mkoani kwetu Kigoma, siku moja kabla ya Rais kufika katika Wilaya ya Kibondo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Ndugu Simon Kanguye aliitwa Ofisini kwa Mkurugenzi akakutana na District Security Officer (DSO) wa Kibondo na toka siku hiyo Mwenyekiti huyu wa Halmashauri na Diwani hajulikani alipo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, familia imechukua hatua mbalimbali, wamelalamika sehemu mbalimbali, Wajumbe wenzake wa RCC Kigoma tumehoji kwenye vikao, Wajumbe wenzake, Mameya na Wenyeviti wamehoji kwenye ALAT, hakuna maelezo yoyote kutoka Serikalini kuhusiana na jambo hili.

T A A R I F A . . .

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niendelee.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi kama wawakilishi wa wananchi wa Kigoma tunalaumiwa kwa nini hatumtetei mwenzetu, mwenzetu yupo wapi toka Julai, miezi tisa leo. Naomba Serikali, Waziri wa TAMISEMI ndio Waziri mwenye Mameya wote, Wenyeviti wote wa Council, leo hii wananchi wa Kata ya Simon Kanguye hawana mwakilishi kwenye Baraza la Madiwani la Kibondo kwa sababu hawajui Diwani wao yupo wapi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mwenyekiti wa Council (Diwani) ni Diwani wa Chama cha Mapinduzi, wala siyo Diwani wa Opposition, mnapoteza mwakilishi wa wananchi na hamna maelezo yoyote. Naomba tupate maelezo haya kutoka Ofisi ya Rais, Utawala Bora ambayo ndio wanasimamia Idara ya Usalama wa Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa zote zipo Kibondo ya mtu aliyekwenda kumchukua tena ameenda kumtoa Ofisi ya Chama cha Mapinduzi, kumpeleka Ofisi ya Mkurugenzi, kumpeleka kwa DSO ambaye alikuwepo kwenye Ofisi ya Mkurugenzi na mpaka leo haonekani. Habari ambazo zinasambazwa Kibondo ni kwamba Mheshimiwa Kanguye tayari ameuawa, tunataka maelezo ya mtu wetu huyu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme kitu kimoja na wazee kama Mzee Mkuchika wanisikie vizuri. Sisi watu wa Kigoma ni watu wa Kigoma kwanza kabla ya kuwa Watanzania na naomba hili lieleweke kabisa. Haiwezekani tuonekane siyo raia, viongozi wetu na Madiwani wetu wakamatwe, wapotee na hakuna maelezo yoyote hatutakubali, kamwe hatutakubali na hatushindwi vita. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba kupata maelezo ya Mwenyekiti wa Council ya Kibondo, Simon Kanguye, familia yake inalia kila siku mchana huu nimetoka kuongea na mke wake na wadogo zake, hawana taarifa. Naomba Serikali itupe taarifa yupo wapi Mjumbe mwenzetu wa RCC Kigoma, kama mmemuua mtuambie watu watoe matanga, hatuwezi kuendelea na hali hii. Na ninarudia, watu wa Kigoma, ni watu wa Kigoma kwanza kabla ya kuwa Watanzania na ninaomba lieleweke hili. Kwenye hili watu wa Kigoma, Kakonko, Kibondo, Uvinza na wapi wote tupo pamoja. Mtueleze Mwenyekiti wa Council na Diwani wa Kibondo yupo wapi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ambalo napenda kulichangia, Halmashauri zetu kuna kazi inafanyika na nimesoma hotuba ya Waziri na bahati nzuri Waziri alikuwa Naibu Waziri kwa hiyo alijitahidi, alizunguka maeneo mengi kwa hiyo anafahamu eneo ambalo analifanyia kazi. Tuna tatizo kubwa sana la fedha za maendeleo kutokwenda kwenye Halmashauri zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwenye taarifa yake aliyoitoa hivi karibuni juzi, ameonesha kwamba asilimia 49 ya fedha zilizotengwa kwenye bajeti ya 2016/2017 hazikufika kwenye Halmashauri zetu. Mwaka jana tumetenga fedha zingine, nimesoma hotuba ya Waziri ukurasa wa saba anaonesha kwamba mpaka Februari fedha ambazo zimefika zote na sasa hivi Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI Selemani itabidi mnisamehe kidogo, mmechakachua hotuba sasa hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, siku zote hotuba za Mawaziri zinaonesha fedha za kawaida ngapi zimefika, fedha za maendeleo ngapi zimefika, kwenye hotuba hii ukurasa wa saba mmesema tu kwa ujumla fedha ngapi zimefika, fedha ngapi za maendeleo hazijafika hamjaeleza kwenye hotuba mpaka Februari mwaka huu. Lakini taarifa ya CAG inaonyesha almost 49 percent, nusu ya fedha zinazotengwa kwa maendeleo hazifiki. Sasa tunatunga bajeti kwa ajili ya nini? Kama budget credibility ipo namna hii, kama fedha zinatengwa haziendi tunatunga bajeti kwa ajili ya nini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni muingiliano. Bunge lililopita hapa tulisikia malalamiko ya Tunduma, kwamba Halmashauri haifanyi kazi kabisa Tunduma kwa sababu ya muingiliano kati ya Mkuu wa Wilaya na Madiwani. Pili, kuna muingiliano wa kisiasa vilevile kwenye maeneo kadhaa nchini. Kwa mfano, CAG anasema kwamba Halmashauri hazikusanyi mapato, Halmashauri yangu ni moja ya Halmashauri ambazo zina matatizo ya mapato, hayakusanywi, magumu kupatikana. Halmashauri nyingi sana only 17 percent ya mapato ndiyo imekusanywa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumekaa, tumetunga by- laws, tumeileta Serikalini, Waziri wa TAMISEMI amesaini by-laws, ushuru uanze kukusanywa, anakuja Kiongozi wa CCM Taifa Kigoma anasema kwamba msilipe huo ushuru. Fedha ambayo tumepanga kukusanya ndiyo inalipwa Tabora, ndiyo inalipwa Sumbawanga, ndiyo inalipwa Nzega, ndiyo inalipwa Kasulu, ndiyo inalipwa Kibondo, shilingi 50,000 kwa kizimba, lakini sisi tunakuja kuambiwa msikusanye, hii ni nini hii?

Mheshimiwa Mwenyekiti, watendaji nina barua hapa za mawasiliano kati ya TAMISEMI na Meya wa Halmashauri kuhusiana na namna ambavyo watendaji hawasimamii vizuri fedha za Halmashauri. Halmashauri yangu imepata hati chafu mwaka huu kwa sababu mapendekezo yote ambayo Meya ameyaandika na barua kutoka TAMISEMI, Katibu Mkuu Mhandisi Mussa Iyombe ameandika barua, Naibu Katibu Mkuu Zainab Chaula ameandika barua kuelekeza hatua za kuchukuliwa, hakuna hatua iliyochukuliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona hatua imechukuliwa baada ya juzi CAG kutoa taarifa na kusema kwamba watu wasimamishwe, ndiyo tumeona hatua imechukuliwa. Lakini toka mwaka 2016 Meya wa Halmashauri anaandika barua na nitaziweka Mezani hapo Waziri azione, hakuna hatua inayochukuliwa. Sasa mambo haya mtakuja kuwaumiza bure wananchi, kwa sababu wananchi siyo wanaoandika taarifa. Kuna hoja kumi hapa za hati chafu ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, kumi. Katika hizo hoja, tisa ni za watendaji, tutawajibuje wananchi, tutafanya nini katika mazingira kama haya? Haya ni matatizo ya viongozi wakubwa kuwapa viburi watendaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Rais alipokuwa Moshi aliwaambia watendaji, Madiwani wasiwapelekepeleke, wakiwapeleka atavunja Halmashauri. Madiwani wakikaa kwenye Kamati ya Fedha na Uongozi wanatoa maelekezo kwa watendaji hawafanyi, ndiyo barua hizi. Tumepata hati chafu Mheshimiwa Jafo kwa sababu Mkurugenzi hakuchukua taarifa ambayo imefanyiwa marekebisho kumpelekea CAG kwa wakati, mpaka leo anayo ofisini, tunafanya nini? Kwa hiyo, ninaomba haya mambo tuyaangalie upya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho kabisa ni mapato ya ndani ya Halmashauri. Mapato ya ndani ya Halmashauri yanaathiriwa sana na maamuzi… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Mungano na Mazingira kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi nashukuru. Nina mambo mawili tu ambayo napenda kuchangia. Kwanza, nimpongeze Mheshimiwa Makamba kwa kazi kubwa anayoifanya, tumemuona maeneo mbalimbali hasa maeneo ya mazingira na kule Zanzibar kutatua matatizo mbalimbali. Hata hivyo, kuna mambo ambayo nadhani juhudi zinazofanyika haziendani na matokeo yatakavyokuja kuwa. Na mimi nina mambo mawili tu ambayo nataka kuchangia kwa dakika hizi tano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza ni la Zanzibar, bidhaa kutoka Zanzibar kuingia katika soko la Tanzania Bara (soko la Tanganyika). Nimeona kwenye taarifa ambayo Waziri amezungumza, amesema kwamba miongoni mwa majukumu anayoyafanya ni kuondoa vikwazo vya biashara kati ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, Kamati imempongeza Waziri na Ofisi ya Makamu wa Rais, kwa kuzikutanisha sekta za biashara za pande mbili za Muungano kwa ajili ya kujadili upatikanaji wa fursa za masoko kwa Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini Mheshimiwa Waziri anafahamu kwamba katika stages za integration sisi tuko stage ya juu kabisa ya political federation. Kwa maana ya kwamba tumeshapita kwenye free trade area, customs union, common market, monitory union na sasa tuko kwenye political federation. Iweje leo tuanze kuzungumza kuondoa vikwazo vya biashara wakati katika hali ya kawaida ilitakiwa bidhaa zote zinazozalishwa Zanzibar ziingie kwenye soko la Bara bila vikwazo vya aina yoyote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, matatizo mengi ya Muungano yanasababishwa na Tanzania Bara kuzuia fursa za kiuchumi za Zanzibar. Leo hii Serikali inasema kwamba, inazuia kwa mfano, sukari kutoka Zanzibar kwa sababu ya kuzuia magendo, lakini hii hii Tanzania Bara ambayo inazalisha sukari Kagera na bado ina-import sukari kutoka nje, inaruhusu Kagera kuuza sukari Uganda. Kuna sukari kutoka Mumias Sugar inayoingia huku Tanzania Bara kwa sababu tupo kwenye East African Common Market, bidhaa zinatembea bila vikwazo vya aina yoyote, iweje Zanzibar izuiwe kuleta bidhaa zake huku? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ni suala la udhibiti wa bidhaa ambazo zinatoka nje wanasema kwamba sijui kuna sukari kutoka Brazil na kadhalika kwenye customs union kuna kitu kinaitwa rules of origin. Kwa hiyo, wataalam na maafisa wa Wizara ya Viwanda na Biashara wangekuwa kule Zanzibar wakatazama kinachozalishwa, wakatoa rules of origin bidhaa hii ikaingia huku kuuzwa.

Kwa hiyo, inavyoonesha hapa ni dhahiri kwamba uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano sasa hivi hauna nia ya dhati ya kuhakikisha kwamba Zanzibar inajitegemea kiuchumi ili Tanzania Bara iendelee kuitawala Zanzibar kiuchumi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nilikuwa naomba jambo hili liweze kupatiwa ufumbuzi kwa sababu hakuna sababu yoyote ile ya kuzuia bidhaa yoyote kutoka Zanzibar kuingia Tanzania Bara kwa sababu sisi…

T A A R I F A . . .

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni mazingira. Nafahamu kwamba sasa hivi tunashughulika na Stiglers’ Gorge na kadhalika, lakini tunafahamu kwamba kuna madhara makubwa sana ya mradi huu. Kwa sababu Waziri amesema wamefanya tathmini wanayo ofisini, tunaomba Bunge lipate tathmini ambayo Wizara imefanya kuhusiana na mradi wa Stiglers’ Gorge. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, muhimu zaidi ni kwamba, kuna miradi mingi sana iliyoainishwa kwenye Power System Master Plan ambayo ingeweza kuzalisha umeme sawasawa na huo umeme ambao tunaenda kuuzalisha Stiglers’ Gorge. Serikali haitekelezi miradi hiyo, inaamua kuingiza fedha za umma, tena tunajitamba kwamba tutatengeneza kwa fedha zetu za ndani, tunaenda kupoteza fedha nyingine kwenye mradi ambao utakuwa white elephant. Kwa sababu Stiglers’ Gorge iko down stream, kuna miradi ambayo ilipangwa ipo up stream ambayo ingeweza kuzalisha umeme huohuo ambao tunataka kuuzalisha kwenye Stiglers’ Gorge.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwakawa Fedha 2018/2018 – Wizara ya Kilimo
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na mkakati wa zao la michikichi Mkoa wa Kigoma. Mwezi Februari, 2017 Serikali ya Mkoa wa Kigoma kupitia kikao cha RCC ilipitisha mpango wa kuendeleza zao la michikichi. Mpango huu ulikuwa na shabaha ya kuongeza uzalishaji wa mafuta ya mawese nchini mpaka tani 400,000 kw mwaka kwa kulima hekta 100,000 za michikichi katika Wilaya tatu za Mkoa wa Kigoma. Mpango huu ungewezesha kufunguliwa kwa viwanda vya kati nane vya kusindika mawese na mazao ya mawese na mazao na kutengeneza ajira 6,400. Mpango huu ungewezesha familia 100,000 kulima michikichi kwa kila familia hekta moja(ekari 2.5) na kuongeza kipato cha familia kwa jumla ya shilingi za Kitanzania 13,000,000 kwa mwaka na hivyo kuwaondolea kwenye umaskini watu 600,000 na kuwafikisha kwenye kipato cha kati ndani ya miaka mitatu tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango huu pia ungewezesha Tanzania kutoagiza tena mafuta ghafi kutoka Malaysia na Indonesia na kuokoa shilingi dola milioni 294 (shilingi bilioni 646) ambazo Tanzania hutumia kila mwaka kuagiza mafuta hayo. Ukijumlisha uzalishaji wa alizeti na mawese nchini, mpango huu ungewezesha Tanzania kujitoshereza kwa mafuta ya kula na ziada nje ili kupata fedha za kigeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa mpango huu unahitaji dola milioni 45 tu na Benki ya Maendeleo ya Afrika ina facility hiyo ya uzalishaji wa mafuta ghafi ambapo Mkoa wa Kigoma uliomba Serikali iombe huko ili kupata mbegu, kutoa mafunzo ya ugani na kuandaa sheria ndogo za Mahakama za Serikali za Mitaa kuwezesha mkakati hu kutekelezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Kilimo haijachukua hatua yoyote katika kusaidia Mkoa wa Kigoma kutekeleza Mpango huu, hata barua kutoka Ofisi ya Rais, Mkoa wa Kigoma haijajibiwa na Wizara na Waziri wa Kilimo na Chakula hajakanyaga Mkoa wa Kigoma tangu aanze kazi licha ya kuwa ndiyo Mkoa pekee nchini haujawahi kupewa msaada wa chakula tangu dunia iumbwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naisihi Serikali iusaidie Mkoa wa Kigoma kutekeleza mkakati wa michikichi kupitia mpango wa kuendeleza zao la mchikichi ili nchi ipone kutoka kwenye kuagiza mawese na mafuta ya kuzalisha sabuni ambayo ni by product ya michikichi kupitia mafuta ya mise.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashauri Wizara za Fedha, Kilimo na Viwanda zikae na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ili kuweka mkakati wa utekelezaji wa mpango huu ili ifikapo mwaka 2022 Tanzania iwe muuzaji (net exporter) wa mafuta ya kula badala ya kuwa muagizaji (net importer). Ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia Wizara hii kwa mara ya tatu sasa, toka mwaka 2016, ni Wizara ambayo sijaacha kuichangia.

Mheshimiwa Spika, mwaka 2016 mchango wangu ulijikita kwenye kufungamanisha sekta ya kilimo na sekta ya viwanda. Moja ya jambo kubwa ambalo tulikuwa nalo wakati ule ilikuwa ni mgogoro wa sukari ambao sasa unazungumzwa na tulikuwa pia na mgogoro wa kuhusu mafuta ya kula ambao bado tunauzungumza.

Mheshimiwa Spika, Wabunge wa Mikoa ya Dodoma, Manyara na Kigoma ni Wabunge ambao tukipambana vilivyo tunaweza kabisa kuiondoa nchi yetu na aibu ya kuagiza mawese kutoa nje. Migogoro ambayo tunaizungumza kila siku hapa na mijadala ambayo tunayo na wewe mwenyewe juzi ulikuwa mkali sana ni kwa sababu ya mawese kutoka nje. Tuna uwezo wa kuzalisha mawese lakini Serikali haijaweka mkakati wowote ule wa kuhakikisha kwamba tunajitosheleza na tunaweza tukauza nje. Haijaweka mkakati wowote ule wa kuhakikisha kwamba tunaongeza uzalishaji wa alizeti, tuweze kuchakata hapa na tuondokane kabisa na hii aibu ya kuagiza mawese kutoka Malaysia, watu ambao walikuja kuchukua mbegu Kigoma. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, huu ni mwaka wa tatu sijaona katika mpango wowote wa Serikali kuhusiana na jambo hili na bado tunabishana na kulumbana na kushutumiana kwa uagizaji wa mawese. Hili ni jambo ambalo linapaswa liwe ni aibu hata kulizungumza katika Bunge hili kwa sababu tuna alizeti, tuna mawese Kigoma na maeneo mengine kama Kyela yangeweza kabisa kumaliza matatizo kama haya.

Mheshimiwa Spika, mwaka jana nilizungumza fungamanisho kuhusu miradi mikubwa inayoendelea nchini na viwanda na hasa hasa niliangalia suala la ujenzi wa reli na jinsi ambavyo tunaagiza malighafi za ujenzi wa reli kutoka nje. Leo umemsikia Waziri hapa anazungumza, bado tunalipa fidia Mchuchuma na Liganga. Leo umemsikia Waziri anazungumza kwamba wamekwenda wamefungua kiwanda cha nondo wapi, kiwanda cha nondo sehemu nyingine, nondo zote hizi malighafi zake ni kutoka nje na sisi tuna chuma Mchuchuma na Liganga miaka yote tunazungumza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wewe ni Mbunge tangu mwaka 2000 unakumbuka, tangu mwaka 2000 tunazungumza Mchuchuma na Liganga, leo Waziri anazungumza kulipa fidia Mchuchuma na Liganga. Sisi ni watu wa namna gani? Kuna takwimu moja inaonesha kwamba 40 percent ya Watanzania ni stunted, inawezekana humu 40 percent of us ni stunted, kwa sababu tunaongea vitu vilevile, miaka yote tunakumbushana, nothing happens. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo hii kweli inaingia akilini, tuna chuma na makaa ya mawe yamejaa pale Ludewa tunampa mkandarasi kazi ya kujenga reli, vyuma vinatoka Uturuki, India, China, kweli? Wenzetu Kenya wanajenga reli na wenyewe wanaagiza hukohuko wakati tungeweza kuwauzia. Zambia wanajenga reli kuunganisha Angola na Zambia, tungeweza kuwauzia chuma, kwa kweli mimi sioni what we are doing. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwaka 2016 Serikali ilikuja hapa na mpango unaitwa C2C, Cotton-to-Clothing, nimeangalia hotuba ya Waziri hapa, hata kulizungumza neno hilo ameona aibu. Unaondoaje umaskini bila viwanda vya nguo? Niambie nchi gani? Uingereza ambayo ni moja ya nchi kubwa umasikini wake umeondolewa na viwanda vya nguo na hawakuwa na pamba walikuwa wanaagiza pamba kutoka kwenye makoloni yao. Hata kuzungumza Mheshimiwa Mwijage Cotton-to-Clothing, agenda yenu wenyewe na ulikuja hapa ukatamba na vitabu kama ulivyovileta leo, where is it? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, eneo kubwa ambalo napenda kuliongelea, nimalizie dakika zangu za mwisho ni biashara ya nje. Tunazungumza viwanda lakini kwa miezi 24 iliyopita Serikali hii ya Awamu ya Tano imesababisha hasara ya nchi yetu ya mauzo nje ya thamani ya dola bilioni moja na siyo takwimu zangu, ni takwimu zao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, angalia ukurasa unaozungumzia China, ukurasa wa 51, mauzo yetu nje China yameporomoka. Nasoma takwimu, China mauzo nje yameporomoka kutoka dola milioni 356 mwaka 2016 mpaka dola milioni 217 mwaka 2017, kutoka takwimu za Serikali. Japan, mauzo yetu nje yameporomoka toka dola milioni 140 mpaka dola milioni 75.

Mheshimiwa Spika, lakini zaidi tumeshindwa hata kuuza mbaazi India. Waziri alikwenda India amesema amezungumza, mimi sina hakika kama Waziri kweli alikwenda kuzungumza na Waziri mwenzake lakini biashara ni diplomasia. Mwigaje huwezi wewe unazunguka kuna viwanda, Naibu wako anazunguka na viwanda, international trade ni Foreign Affairs. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, juzi Vice President alikuwa London, Modi alikuwa London, mmeshindwa kuseti appointment ya Vice President na Modi wakazungumza tukatatua tatizo la mbaazi? Mbaazi bei imeporomoka kutoka Sh.3,000 mpaka Sh.150 kwa kilo. Mwezi Machi nimezunguka kwenye kata 16 nchi hii nimekuta watu wanalia mbaazi zimo ndani. Waziri Mstaafu Nape alizungumza hapa, alimuuliza Naibu Waziri, Naibu Waziri akasema kwamba tutakula, no it is foreign trade! It is about forex! (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nchi hii tunaagiza nje vitu tunahitaji fedha za kigeni, mbaazi, choroko, giligilani, zilikuwa zinatupa dola milioni 224 kuuza India mwaka 2016, mwaka 2017 ikaporomoka dola milioni 131, mwaka 2018 sasa hivi dola milioni 75, what are you doing? Unapopoteza hizi forex utanunua mafuta na nini kwa sababu inabidi uagize. What will you buy mafuta with?

Mheshimiwa Spika, mimi nashindwa kuelewa what are we doing. Wizara ya Viwanda na Biashara that part ya biashara especially foreign trade hamna, tumepoteza one billion dollars in the span of 24 months, ni sawasawa na kupoteza kila siku shilingi za Kitanzania bilioni tatu in the last 24 months, you are still here Mwigaje, why don’t you just quit? Umeshindwa kazi. You can’t run Wizara ya Viwanda na Biashara as if you are running TAMISEMI, it is diplomacy, it is about going out getting markets. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo Malaysia kule a friend of Tanzania has been elected as a new Prime Minister, Mzee Mahathir, a very close friend of Mwalimu Nyerere, go there immediately, get the markets. Hamuwezi mkajidanganya na viwanda vya cherehani mkadhani kwamba you save this country! Foreign trade is power.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, haiwezekani sisi tukakosa soko India. The majority ya Wahindi ambao unawaona hapa Tanzania they are from Gujarat, Modi is from Gujarat, use that, talk to them! Hebu tuwaokoe hawa wakulima wa mbaazi, wakulima wa giligilani, giligilani imeshuka bei, mbaazi imeshuka bei, choroko imeshuka bei na dengu imeshuka bei, what are you doing?

Mheshimiwa Spika, ahsante.
Makadilio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Spika, katika ukurasa wa 21 wa Hotuba ya Waziri amezungumzia inaanzia ukurasa wa 20 kuhusu usimamizi wa Pori Tengefu la Kilombero na amesema kwamba kuna miradi kadhaa inaendelea katika pori hili ikiwemo Mradi wa Umeme wa Maji Rufiji (Rufiji Hydro Power Project) na ninanukuu Waziri anasema; “Pamoja na umuhimu huo bonde hilo linakabiliwa na changamoto za uvamizi kwa ajili ya shughuli za kibinadamu.” Moja ya shughuli ya kibinadamu zinazoendelea kule Mhifadhi Spika Job Ndugai ni pamoja na ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme megawati 2,100. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninapenda niwe very clear, hakuna mtu anayepinga nchi yetu kuongeza uwezo wa kuzalisha umeme. Lakini tunataka taratibu za kisheria, taratibu za utunzaji wa mazingira na kuhakikisha ya kwamba nchi haiathiriki kwa ujumla wake kutokana na mradi mmoja tu ambao tayari una mbadala mbalimbali kama jinsi ambavyo tukiwa tukielezwa hapa toka jana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Nape amezungumzia kwamba Selous inategemea watu takribani mikoa mitano na pamoja na kwamba ukikata miti ambayo inakatwa ambayo ni sawasawa na size ya Mkoa wa Dar es Salaam; Mkoa wa Dar es Salaam una square kilometers 1,360 na miti inayokwenda kukatwa ni square kilometers zaidi ya 1,400 kila Mbunge hapa afumbe macho aitazame Dar es Salaam yote, aione namna ambavyo ikiwa haina kitu kabisa jinsi ambavyo itakavyokuwa na mbaya zaidi eneo ambalo miti hii inakwenda kuondolea ndiyo eneo ambalo lina unyevunyevu ambao nyakati ambazo wanyama wanatafuta maji ndiko ambako wanakwenda. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sitaki kuangalia hiyo angle ya maisha ya watu, nataka kuangalia angle ya uchumi. Kwa mujibu wa mikakati ya nchi tunataka itakapofika mwaka 2025 tuwe na watalii milioni nane kwa mwaka katika nchi yetu wanaoingiza dola za Kimarekani bilioni 16 kwa mwaka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, watalii hawa hawatakuwa tena Northern Circuit, watalii hawa watakuwa ni Southern na Western Circuit, ukishaenda ukaiondoa Selous yote ukaondoa, maana yake ni kwamba huwezi kufikia hii mikakati. Ni namna gani ambayo tunalinganisha mikakati yetu na mipango ambayo tunaifanya, hasa ukizingatia tuna- alternative, tuna-alternative ya kuzalisha umeme, tuna- alternative ya bomba la gesi ambayo sasa hivi linatumia asilimia sita tu, na juzi hapa dada yangu Mbarouk amesema tusiite, dada yangu Mheshimiwa Subira alisema gharama ya kuzalisha umeme kwa maji ninafuu kuliko kwa gesi. Lakini ni lazima Serikali ikumbuke capital injection the investment unayokwenda kuifanya kwenye huo uzalishaji wa umeme kwa maji ni kubwa mno itakuchukua miaka 30 ku-recover mpaka urudi kuzalisha kwa senti mbili kwa dola kama jinsi ambavyo Serikali inasema. Kulikuwa kuna haja kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba ni kuombe, jambo hili la TFS kwenda kuangusha miti ile na kuuza yale magogo jambo hili lisamame kwa muda mpaka hiyo masuala ya Environmental Impact Assessment yatakapokuwa yamekamilika tuweze kuona mitigation measures ni zipi. Vinginevyo Serikali iangalie alternative ya uzalishaji wa umeme as upstream na kwenye power master plan ambayo tunayo inaonesha kuna orodha, Mheshimiwa Nassari ameitaja jana ya miradi mbalimbali ambayo imeorodheshwa ambayo itazalisha umeme sawasawa na huo ya Stiegler’s bila kuiathiri Stiegler’s. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nilikuwa naomba jambo hili tuweze kulitazama kwa namna hiyo tunakwenda kupoteza maana kabisa ya kukuza utalii katika nchi. Kama tusipokuwa makini na namna ambavyo tunashughulika na suala la Stiegler’s Gorge.

Mheshimiwa Spika wewe ulivyokuwa mwanafunzi, ulivyokuwa unafanyakazi wanyamapori, umekaa Selous, ulikuwa game warden Selous hebu itazame namna ambavyo tutaondoa hii miti na Selous itakavyokuwa imekufa na historia yako itakuwa imekufa kabisa, kwa hiyo lazima tulitazame jambo hili kwa mapana yake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine ni hili ambalo limezungumzwa na Kamati suala zima la vitalu. Nilikuwa namuomba Mheshimiwa tu ndugu yangu Kigwangalla kwa kuwa tumeona kwamba kuna tatizo la kisheria ambalo limetokea na kwamba maagizo ambayo ameyatoa kwa nia njema kabisa, lakini ni maagizo ambayo yametolewa kinyume na Sheria turejee kwenye status quo na nilikuwa nakuomba uagize Serikali turejee status quo wakati marekebisho mengine yanafanyika ili tusafiri sekta hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante sana
Makadilio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Spika, makosa ya matumizi ya takwimu, ukurasa 73 aya 164; Wizara inasema mapato yatokanayo na utalii yameongezeka kutoka dola milioni 2.mpaka dola bilioni 2.25 mwaka 2016 – 2017. Kamati pia katika taarifa yake ukurasa 11 imerudia kusema; mapato yatokanayo na utalii mwaka 2016/2017 yameongezeka hadi dola bilioni 2.3; hili ni kosa. Dola bilioni 2.3 sio mapato ya sekta bali ni forex (fedha za kigeni zinazoingia kwenye reserve kutoka utalii). Tusichanganye forex na revenues. Matumizi ya takwimu hizi ni muhimu kutiliwa maanani. Tutumie mapato ya fedha za kigeni ili kuwa sahihi. Pia utalii unachangia 25% ya forex na sio 25% ya GDP.

Mheshimiwa Spika, mradi wa umeme Rufiji katika ukurasa 71 wakati wa mjadala wa makadirio ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Serikali ilitoa commitment kuwa kabla ya mradi kuanza itafanyika ESIA. Hata hivyo TFS wametangaza zabuni ya kuvuna miti milioni mbili katika eneo lenye ukubwa sawa na Mkoa wa Dar es Salaam. Ni kweli kuwa hili eneo ni 3% tu ya Selous, lakini eneo husika ni eneo la mazalia ya wanyama. Kwa nini Serikali isisubiri ESIA iishe ili waanze utekelezaji? Kwa nini Serikali inafanya haraka hii?

Mheshimiwa Spika, narudia kusisitiza kuwa tutazame miradi mbadala iliyoainishwa kwenye Power System Master Plan (2016 update) ili kuepuka madhara ya mazingira katika Selous Game Reserve. Ni muhimu jambo hili tulitazame kitaifa ili kulinda maliasili zetu.

Mheshimiwa Spika, ni sahihi kuwa na uwezo mkubwa wa kuzalisha umeme lakini sio kwa kuharibu ekolojia. Kwa nini hatutumii bomba la gesi kikamilifu? Asilimia 25 ya bomba la gesi inazalisha umeme wote Stiegler’s. Kwa nini tuendelee na mradi huu?

Mheshimiwa Spika, nashauri ATCL wanahisa wake wawe TANAPA na NCAA. Hii ni kwa sababu wao ndio wafaidika wakuu wa Shirika la Ndege. Asilimia 15 ya makato yanayokwenda Hazina zitumike kama mtaji kwa ATCL.

Mheshimiwa Spika, suala la Loliondo lipate suluhisho ya kudumu kwani wananchi wanaumia sana. Mwaka 2017 boma 250 zilibomolewa na wananchi kupigwa sana. Waziri aliahidi kuwa OBC itanyang’anywa leseni ifikapo Januari, 2018. Hata hivyo mpaka leo OBC bado wapo. Kwa nini tusifuate sheria na kuiacha Loliondo kama village land?

Mheshimiwa Spika, CAG, ametoa hoja ya ukaguzi kuwa TANAPA na NCAA hukatwa mchango kwenye Mfuko Mkuu wa Hazina asilimia 15 na wakati huo huo kukatwa kodi asilimia 30 bila kuondoa makato yanayotambuliwa (allowance expense). Suala hili ni kinyume kabisa na principles za kodi kwani hiyo asilimia 15 ilipaswa kuondolewa kabla ya kutoza kodi. Ni muhimu sana Serikali ifuate ushauri wa CAG wa kurekebisha sheria ili kuwezesha makato yanayokwenda mfuko wa Hazina (Rejea CAG Pg. 98 – 99).
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
MHE. ZITTO R. Z. KABWE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi na kutokana na muda nimewasilisha kwa Mheshimiwa Waziri maelezo ya mchango wangu katika maeneo mbalimbali ambayo nachangia ili tuweze kupata majibu ya Serikali. Kwa hiyo, nitachangia maeneo machache tu kutokana na muda ambao umepatikana.

Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza, nchi yetu ilijenga heshima kubwa duniani siyo kwa sababu ya utajiri, siyo kwa sababu ya idadi ya watalii ambao tunao bali ni kwa sababu ya kupigania utu mahali popote pale duniani. Mwaka 1961 wakati tunapata uhuru, usiku wa kuamkia siku ya uhuru tuliweka Mwenge juu ya Mlima Kilimanjaro na Mwalimu Nyerere alitamka maneno yafuatayo:- (Makofi)

‘Tunataka kuwasha Mwenge na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete matumaini pale ambapo hakuna matumaini, upendo pale palipo na chuki, heshima pale palipojaa dharau.’ (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, huu ndio umekuwa msingi wa sera yetu ya mambo ya nje miaka nenda miaka rudi. Ndio mambo ambayo Waziri Mahiga, amekuwa akifundisha, ametumikia nchi yetu, amekuwa Balozi wa Umoja wa Mataifa lakini leo mambo ambayo yanatekelezwa tunashindwa kuelewa kabisa kama ni Mheshimiwa Dkt. Mahiga huyu tunayemjua au kuna Mheshimiwa Dkt. Mahiga mpya baada ya kuwa Waziri wa Mambo ya Nje. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimetazama kura zote UN Security Council, wakati Waziri Dkt. Mahiga anaiwakilisha nchi yetu. Kura zote zilizokuja kupigania wanyonge tulikuwa pamoja na wanyonge, lakini toka mwaka 2016 kura zote tunazopiga kwenye majukwaa ya kimataifa uanzie UNESCO Parish, mwezi Oktoba, 2017 na mpaka hivi majuzi ama tuna abstain tunaona aibu kusimama na wanyonge au tunapiga na watu ambao wanawakandamiza watu wengine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hakuna mtu anayekataza nchi yetu kuwa na mahusiano ya kibalozi na Israel. Hata Mwalimu Nyerere hakukataza kuwa na mahusiano na Israel lakini Mwalimu Nyerere alisema kwamba mahusiano hayo yasitufanye tuache kusimamia wanyonge. Mheshimiwa Waziri alikuwa Israel juzi, amekwenda Israel at the time, ambayo ndio inawaumiza Wapalestina kuliko wakati mwingine wowote miaka 70 ya Taifa la Israel. Amekwenda kutembelea miji ambayo inapakana na Gaza, kulikuwa na massacre. Nchi yetu leo inaona aibu kulaani mauaji ya watu wanyonge wanaokandamizwa, walionyang’anya ardhi yao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimesoma maelezo ya Wizara ukurasa wa nane mpaka wa tisa, propaganda kutaka kuridhisha watu ambao bado wanaamini misimamo ya Mwalimu Nyerere kwamba bado tuna misimamo hiyo, lakini ukitaka kujua hasa nini misimamo ya Serikali kwenye mambo ya kimataifa nenda angalia ukurasa wa 51 mpaka 60 ya hotuba ya Mheshimiwa Waziri. No mention of Palestina, no
mention of POLISARIO, Ame-mention kwenye preamble huku ili kuturidhisha kwamba misimamo yetu haijabadilika, lakini huku amekuja kuzungumzia mpaka mambo ya North Korea huko, nothing about watu ambao tumekuwa tukiwapigania.

Mheshimiwa Naibu Spika, juzi watu ambao tumewakomboa South Africa, baada ya massacre ya Gaza, wamemwondoa balozi wao, Waziri wetu anakunywa mvinyo na Netanyahu, the butchery ya Wapalestina. Anaenda kwenye television za Israel, television za Taifa anapongeza Israel, anashindwa kutoa neno moja la kulia na watu ambao, sasa mambo yote aliyokuwa anafundisha Mheshimiwa Dkt. Mahiga siku zote ya foreign yanaenda wapi? At this age anavunja heshima yake yote ya huku nyuma. Kwa sababu ya nini misaada ya Israel? POLISARIO, its true, amezungumza rafiki yangu Mheshimiwa Cosato kwamba Algeria wana ubalozi wana… mwisho. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
MHE. ZITTO Z. R. KABWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia bajeti ya Mafungu takribani sita ya Wizara ya Mambo ya Ndani. Kwanza nianze kurejea kwenye Katiba, Ibara ya 15 ambayo inasema kwamba kila mtu anayo haki ya kuwa huru na kuishi kama mtu huru. Ibara ya 15(2) inasema:

“Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kuwa huru na kuishi kwa uhuru itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kukamatwa, Kufungwa, kufungiwa, kuwekwa kizuizini, kuhamishwa kwa nguvu au kunyang’anywa uhuru wake vinginevyo.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ndiyo Katiba yetu ambayo inatuongoza na sote hapa tumeiapa kuilinda na kuitetea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda niwakumbushe na hasa niwakumbushe wana CCM. Kwenye hotuba ya Mwalimu Nyerere alipokuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mwaka 1987 kwenye Mkutano Mkuu alisema “Panapokuwa hapana haki wala imani na matumaini ya kupata haki, hapawezi kuwa na amani, utulivu wa kisiasa na hatima yake panazuka fujo, utengano na mapambano” haya ndiyo maneno ya Baba wa Taifa, amani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii tunazungumza kwa mara ya kwanza tokea Mbunge mwenzetu ashambuliwe kwa risasi. Tumekaa humu ndani kwa mara ya kwanza kwa maana ya bajeti, tunakwenda kupitisha zaidi ya shilingi bilioni 596, asilimia 63 ya bajeti yote ya Wizara ya Mambo ya Ndani inakwenda Jeshi la Polisi mpaka leo Jeshi la Polisi halijaweza kufanya uchunguzi na kujua ni nini ambacho kilitokea Mbunge mwenzetu akapigwa risasi hapa Dodoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tunakutana hapa tunataka tuwatengee fedha Jeshi la Polisi lakini tuna watu ambao wana miaka inakaribi miwili wamepotea hawajulikani wako wapi akina Ben Saanane. Mwandishi wa Habari, Azori Gwanda juzi mkewe amapata mtoto, mtoto hamuoni Baba yake na Jeshi la Polisi halina maelezo yoyote ambayo limeyatoa mpaka sasa hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati wa hotuba ya TAMISEMI na Utawala Bora nilizungumza kuhusu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Ndugu Kanguye ambae ni Diwani wa Chama cha Mapinduzi, wiki iliyopita Mama mzazi wa Ndugu Kanguye amefariki dunia, amefariki dunia akiwa hajui mwanawe yuko wapi. Waziri wa Utawala Bora alituambia kwamba siyo kazi ya Usalama wa Taifa kukamata tukasema sawa, hii Serikali moja, Wizara ya Mambo ya Ndani itakuja, Wizara ya Mambo ya Ndani imekuja haya watueleze! Kama siyo kazi ya Usalama wa Taifa ni kazi ya Polisi, Polisi watueleze kwamba Ndugu Kanguye yuko wapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, yote haya ni mlolongo wa mambo mengi ambayo yanaweza yakatuletea shida kubwa sana katika nchi. Mbunge wa Kilwa, Ndugu Bungara amezungumza kwa hisia na wakati mwingine muache watu wazungumze kwa hisia kwa sababu watu wanapozungumza kwa hisia ndiyo wanaongea yale mambo ambayo yanawahusu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tarehe 12 Juni, 2017, mama mmoja anaitwa Ziada Salum wa Kitongoji cha Maparani, Kibiti alichukuliwa na jeshi la Polisi saa 6.00 mchana na leo ni miezi 11 mama huyu hajaonekana yuko wapi. Siku hiyo hiyo kuna mtu anaitwa Rukia Muhoni na Tatu Muhoni ni ndugu hawa, walichukuliwa na Jeshi la Polisi mpaka leo hii tunavyozungumza miezi 11 hawajaonekana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina orodha hapa, nina watu 348 wa Wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji na hapa hatujajumlisha watu ambao wanatoka Kilwa. Kuna mtu jana hapa alizungumza kuna zaidi ya watu 1000 wamepotea, inawezekana orodha niliyonayo hapa na nitampatia Waziri, watu 348 na katika hao watu 68 wamethibitika wamekufa. Tunaomba Serikali itueleze nini kinaendelea Wilaya za Kusini ya Tanzania.
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, Manispaa ya Kigoma Ujiji ina changamoto kubwa ya mapato ya ndani. Mfano, mwaka 2016/2017 makadirio yalikuwa shilingi bilioni 3.3, lakini makusanyo yao yalikuwa bilioni 1.4 tu sawa na asilimia 42. Mwaka 2017/2018 makadirio ni billion 2.3 na mpaka sasa tumekusanya asilimia 33 tu na miezi imebaki miwili tu kabla ya mwaka wa fedha kwisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa ushuru wa masoko haukusanywi kwa sababu Katibu Mwenezi wa CCM amekataza wafanyabiashara kulipa tozo ya 50,000 kwa mwezi na Serikali ipo kimya. Serikali itoe kauli hapa Bungeni ili watendaji waende kukusanya ushuru. Shughuli zimesimama. Serikali ielekeze watendaji kukusanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, fedha za Mfuko wa Maendeleo wa Wanawake na Vijana asilimia 10. Kwa miaka 24 sasa MSM zimekuwa zinatenga asilimia 10 kutoka mapato ya ndani lakini changamoto bado ni nyingi na zile zile, nadhani tubadili mfumo. Napendekeza kuwa fedha hizi zitekelezwe kupitia mfumo wa Hifadhi ya Jamii ambapo vikundi vya vijana na wanawake wanufaishwe na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na kupitia fedha hizi MSM zichangie asilimia 50 ya michango ya mwezi na vijana na wanawake wachangie asilimia 50 iliyobaki. Hii ingejenga tabia ya kuweka akiba na pia kuwezesha vijana na wanawake hawa kuwa na bima ya afya kupitia mifuko hii. Hii pia ingewezesha kuwepo na fedha za uwekezaji wa miradi ya kimkakati kati ya MSM na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, mwaka 2016/ 2017, MSM zilikusanya shilingi bilioni 544 ambapo asilimia 10 ya hizi ni bilioni 54 ambazo zingewekwa akiba kwenye mifuko. Kwa kuwa vijana na wanawake wangechangia asilimia 50 ya michango yao, jumla ya fedha za michango zingefika bilioni 108. Hizi zingekuwa zinaongezeka kila mwaka (2017/ 2018 shilingi bilioni 687, mwaka 2018/2019 bilioni 735) na hivyo kujenga mfuko mkubwa ambao fedha zinatunzwa vizuri kuliko sasa ambapo fedha nyingi hupotea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napendekeza tufanye hili ili kulinda fedha hizi kwani zingekuwa na uhakika kwani mifuko ingefuatiliwa, ingejenga utamaduni wa kuweka akiba kwa watu wetu na ingewezesha watu wetu kupata bima ya afya na kupata mikopo yao kupitia mifuko hii. Wataalam walitazame hili jambo la kimaendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, usimamizi wa fedha MSM; kuna changamoto kubwa kuhusu uwezo wa watendaji wetu kufanya kazi na Madiwani, hawasikilizi, hawajali na dharau. Manispaa ya Kigoma Ujiji ni ushahidi tosha wa uzembe wa watendaji kupelekea kupata hati chafu. Rejea barua ya Meya wa Manispaa kwa TAMISEMI tarehe 30 Juni, 2017 kumb na. A20/448/Vol.11/7) na majibu kutoka TAMISEMI (15 Septemba, 2017) kumb. RALG(PCF.5211).

Mheshimiwa Mwenyekiti, barua hizi pamoja na barua nyingine zote zilionesha malalamiko dhidi ya watendaji. Manispaa iliomba Taasisi ya Wajibu ya Bw. L. Utouh kutusaidia kupata ufumbuzi. Watendaji hawakutekeleza kabisa ushauri. Ukisoma ukurasa wa 270-272 wa Taarifa ya CAG utaona sababu za hati chafu zote zinahusu ufuatiliaji wa watendaji. TAMISEMI haikumsikiliza Meya wa Manispaa. Nashauri uchunguzi unaofanywa sasa uwe mpana, utazame uwezo wa watendaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mapato ya ndani kwa mujibu wa CAG MSM zilishindwa kukusanya 17% ya makadirio (shilingi 104 bilioni) mwaka 2016/2017 wastani wa miaka ya nyuma ni 10% tu. Pia property tax kuchukuliwa na TRA ni changamoto. Hii maana yake ni kuwa fedha za vijana zitakuwa ndogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Serikali itoe maelezo kuonya wanasiasa kuingilia sheria. Katibu Mwenezi wa CCM Bwana Polepole alikuja Kigoma kuagiza ushuru usikusanywe na kuvunja sheria. Kwa nini TAMISEMI haikemei mambo haya? CAG ametaka tuongeze mapato lakini wanasiasa wanazuia?
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuweza kuchangia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nikupongeze kwa uongozi wako wa kuhakikisha kwamba tunaitekeleza ipasavyo Katiba yetu Ibara ya 63(3)(c). Wewe unafahamu siku za nyuma tulikuwa hatufanyi hivi, lakini tangu tumeanza Bunge hili kila mwezi Novemba tumekuwa tukikutana na kutekeleza matakwa ya kikatiba. Kwa hiyo, napenda nikupongeze wewe binafsi kwa uongozi wako katika jambo kama hili, nashukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nami pia niende kwenye baadhi ya mambo ambayo napenda kuchangia kwa ajili ya kuboresha mpango kama jinsi ambavyo wenzangu wametoka kuzungumza. Jambo la kwanza ni eneo la vipaumbele vya mpango.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukitazama tuna hotuba tatu sasa tangu tumeanza, kuanzia 2016 mpaka sasa. Ukichukua hotuba ya 2016, ukatazama vipaumbele vya mpango, wakati ule viliitwa miradi ya kielelezo, ukaenda 2017, 2018 jambo moja ambalo naliona ni kukosekana kwa sequencing. Unaanza na mambo fulani mwaka unaofuata una-drop baadhi, hata ambayo hayajatekelezwa kabisa, mwaka unaofuata una-drop mengine, hata ambayo hayajatekelezwa kabisa, matokeo yake ni kwamba kila mwaka tunakuwa tunaanza upya bila kufanya yale ambayo tungekuwa tumepaswa kuyafanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukitazama mwaka 2016 kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mpango ukurasa wa 18, jambo la kwanza kabisa Makaa ya Mawe Mchuchuma na Chuma cha Liganga. Ukienda mwaka 2017 ukurasa wa 29 lipo lakini kuna jambo la Mji wa Kilimo wa Mkulazi limegeuzwa kuwa shamba, halafu ukija 2018 hayapo kabisa na ni kwa sababu huko nyuma tumekuwa tukishindwa kuyatekeleza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukitazama hilo maana yake ni kwamba tunakuwa tunapiga mark time, tunakutana, tunajadiliana, tunatoa mawazo, mwezi Februari yanakuja tunayaidhinisha vizuri, tunaenda kwenye bajeti, tunaweka bajeti na nitakuja kwenye hiyo hoja ya bajeti credibility halafu hakuna kinachofanyika. Mfano dhahiri kabisa ni hili jambo la Mchuchuma na Liganga ambalo tangu 2016 linaonekana kwenye mpango kama mradi kielelezo, kufika sasa limeondolewa kabisa kama mradi kielelezo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba hili lifanyiwe marekebisho. Tujaribu kurudi 2016 tuangalie ile miradi vielelezo na tui-update utekelezeaji wake. Kuna ambayo imetekelezwa kama Reli ya Kati na kadhalika na ile ambayo imeachwa tuweze kuiboresha ili tutakapokuja mwezi Februari, tuwe na kitu ambacho tumeanza nacho kuanzia mwaka 2016.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili ni suala la credibility ya tunachokijadili hapa. Mwaka 2016 tulijadili na kukubaliana kwamba Serikali ikatenge shilingi trilioni 13.2 kwa ajili ya utekelezaji wa mpango wa maendeleo ambao tunaujadili kwa siku tano, wakaenda wakatoa trilioni 5 tu. 2017 tukasema zikatengwe shilingi trilioni 12, zikaenda zikatengwa trilioni 6 tu. Mwaka 2018 ndiyo tunapendekeza sasa zikatengwe tena shilingi trilioni 12. Hii inaonesha dhahiri kwamba kama hatutakuwa makini na kuanza kuhitaji uwajibikaji upande wa Serikali, tunapiga porojo. Kwa sababu kile ambacho tunakubaliana kukifanya wenzetu wakakifanye hakifanywi vile ambayo tumekubaliana kikafanywe. Hiyo ni problem ya credibility ya mpango na bajeti yenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la tatu, limezungumzwa kidogo na Mheshimiwa Bashe, tuna tatizo kwenye exports. Mwaka 2016 tuli-export bidhaa za dola za Kimarekani bilioni 9.8, kwa mujibu wa taarifa ya Serikali yenyewe. Sasa hivi kwa taarifa ambayo Mheshimiwa Waziri Mpango ametuletea leo exports zetu zime-drop kwa dola bilioni moja. Tayari mwezi wa Agosti tumepata negative balance of payment for the first time in the last three years. Sekta ambazo zimekuwa zikituokoa hasa mwaka jana ni tatu, utalii, transit trade bandarini pale na korosho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka jana korosho zimetuingizia fedha za kigeni zaidi ya kahawa, pamba, chai, tumbaku, karafuu, pareto, katani combined. Mwaka huu production inashuka sana, kwa hiyo tunakwenda kwenye balance of payment crisis. Serikali inafahamu hatuendi huku kwa sababu ya bahati mbaya labda natural calamities au nini, tunakwenda huko kwa sababu ya kwanza mipango mibovu lakini pili utekelezaji mbovu wa mipango hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nilitarajia leo tungeweza kuletewa kwamba tunaenda kwenye crisis maana mafuta yanaenda kupanda bei na Mheshimiwa Waziri Mpango anafahamu sasa hivi tuta-import sana kwa sababu ya miradi mikubwa ambayo tunaitekeleza. Tuna- import mataruma ya reli, aibu lakini ndiyo hivyo tuna import. Maana yake ni kwamba by Desemba tunaweza tukawa na crisis kubwa ya balance of payment. Ni nini mpango wa Serikali wa kuhakikisha tunaongeza huo uzalishaji? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali pia imezungumzia katika utekelezaji wa mwaka huu suala la ASDP II. Katika ASDP II kuna suala la mbegu za GMO, mbegu ambazo sote tunajua zinakwenda kuielekeza nchi yetu kuwa koloni la kampuni kubwa za mbegu duniani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nita-share na Mheshimiwa Waziri wa Fedha barua ambayo mtafiti mmoja wa Kitanzania amefanya, anaitwa Dkt. Richard Mbunda ambaye aliandika barua kwa Mheshimiwa Rais kuhusiana na suala hili kwamba tunaenda kuua mbegu za asili, tunaenda kuwaua wakulima wadogo, tunajikuta sisi kazi yetu ni ku-import mbegu kutoka kwa Monsanto na kampuni kubwa za mbegu na hatimaye ule uhuru wetu wa chakula (food sovereignty) tunakwenda kuiondoa. Napenda tupate kauli ya Serikali hasa sera yetu kwenye GMO ni nini, tunakubali kwenda kujinyonga na kuwa nchi ambayo inategemea kampuni kubwa kuleta mbegu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho ni jambo ambalo napenda Wizara ya Fedha ilitazame vizuri. Tuna tatizo la reporting accounting, nitaliandika vizuri kwenye mchago wa maandishi. Ukitazama taarifa ya Serikali ya sasa hivi tunarudi kwenye lile tatizo la 1.5 trilioni tena. Ukitazama kwenye report ambayo Serikali imetoa, page 10 na page 11 utaona taarifa ya mapato ambayo Serikali ime-report kuwa imeyakusanya mpaka mwezi Juni na taarifa ya matumizi ambayo Serikali imesema imetoa fedha hizo kwenda kwenye mafungu, kuna tofauti ya shilingi trilioni 2.1. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mbaya zaidi, ukitazama hotuba ya Mheshimiwa Waziri ya mwaka 2017, kama ingekuwa imezingatiwa hii na Treasury tatizo ninalolizungumza sasa ambalo PAC wanalifanyia kazi la 1.5 trilioni lisengekuwepo kwa sababu wali-report sahihi vile ambavyo wamekusanya na vile ambavyo wametoa, wakatazame ukurasa wa 11 na 12. CAG baadaye alionyesha kwamba kilichokuja kuripotiwa kuna hiyo tofauti ya 1.5 trilioni; sasa hivi 2018 tatizo limejirudia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi sitaki kusema kwamba kuna wizi, namjua Mheshimiwa Dkt. Mpango si mwizi na sisi watu wa Kigoma hatuna historia ya wizi lakini kuna tatizo kubwa la accounting. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kupata nafasi ya kuchangia Kamati zetu hizi mbili; Kamati ya Maliasili na Utalii na Kamati ya Kilimo ambazo zinabeba Wizara muhimu sana. Kamati ya Kilimo peke yake mchango wake kutoka kwenye idara ambazo inazisimamia katika Pato la Taifa ni takribani asilimia 33 na tunaambiwa sekta ya utalii peke yake inachangia asilimia 17 katika pato la Taifa. Kwa hiyo, tuna hoja nyeti sana ambazo naamini kwamba Wabunge tunazitendea haki pia.

Mheshimiwa Spika, nitaanza na jambo la uelewa kidogo, jana na juzi tumekuwa na mjadala hapa kuhusiana na masuala ya biashara ya korosho na kulikuwa na ubishani kidogo kuhusu masuala ya kangomba na kadhalika. Kuna jambo ambalo naomba Waheshimiwa Wabunge tulitazame, leo hii sisi tumeweka nguvu kubwa Kagera kuzuia kahawa yetu isiende Uganda. Kahawa yetu ikishakatiza tu mpaka wa Uganda, kule Uganda hawana shida yoyote. Ndiyo maana leo ukitazama mauzo ya kahawa nje, pamoja na kwamba Uganda eneo lake la kahawa ni dogo lakini wanauza tani 306,000 za kahawa kwenye soko la dunia wakati sisi tunasuasua kati ya tani 100,000 na 137,000, sina uhakika sasa hivi tumeuza kiasi gani, lakini Uganda mara zote wanauza nje mara mbili. Uganda sasa hivi ni namba nane duniani na namba moja Afrika kwa kuuza kahawa nje. Kahawa ile ambayo Waganda wanauza, sehemu yake inatoka Tanzania, Burundi, Rwanda na kadhalika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sisi leo anaweza akasimama Mkuu wa Wilaya akaita na vyombo vya habari kutangaza kwamba eti amezuia korosho kutoka Msumbiji kuja Tanzania. Nadhani ifike wakati viongozi wetu ngazi za chini na naomba radhi, nitatumia neno tuache ushamba. Re-export ni biashara kubwa duniani, sisi tunapaswa kuweka incentives kama kuna watu wana bidhaa zao ambazo zinauzwa wakazileta tukaziuza sisi zita-appear kwenye balace of payment yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ndiyo maana leo United Arab Emirates wanauza nje bidhaa za thamani ya Dola za Kimarekani bilioni 295. Katika hizo re-export ni Dola za Kimarekani bilioni 137 yaani ni bidhaa za nchi zingine zikifika pale Dubai au Abu Dhabi na kadhalika, wanazifanyia repackaging wanauza nje, inaitwa re-export. Kwa hiyo, naiomba Serikali izungumze na hawa Wakuu wetu wa Wilaya wa mipakani huko waachane na hayo mambo, waache tabia za kishamba, kama mali inakuja kwetu acha iingie tutaiuza sisi dola zitaingia kwetu. Kwa hiyo, naomba hili jambo tulitazame vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini pili na naomba hili nimu- address Waziri wetu wa Kilimo, rasimisha kangomba, ndiyo njia pekee ya kuhakikisha kwamba tunaondoa ulanguzi. Vyama vyetu vya Ushirika havina incentive ya kuwawezesha wakulima wetu wapate mikopo midogomidogo ya kuweza kushughulika na kero zao ndogondogo. Ndiyo maana ukienda Kagera kule na rafiki yangu Naibu Waziri wa Kilimo anajua kuna Obutura, ndiyo kangomba hiyo ni majina tu tofautitofauti, rasimisheni haya mambo, wapeni leseni. (Makofi)

Wapeni mizani, wataacha kufanya kazi ya ulanguzi na itatusaidia korosho, kahawa au pamba nyingi kukusanywa na tutakuwa hatuna mambo haya.

Mheshimiwa Spika, haiwezekani leo mtu ambaye anafanya brokerage Dar es Salaam Stock Exchange anaonekana ni mtaalam kwelikweli, halafu unakwenda unamdhalilisha kangomba unamuita mlanguzi, unamuita nini, haya mambo yamepitwa na wakati. Rasimisheni, wapeni leseni na mizani tuweze kufanya kazi vizuri, matatizo mengine yatakuwa yamekwisha bila shida yoyote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine ninalotaka kulizungumzia, sasa hivi tuna wakati mgumu sana, ni kweli tuna miradi mikubwa inafanyika, ni kweli kabisa lakini wachumi wenzangu hapa watanisaidia. Duniani kote pale ambapo hali ya uchumi ni mbaya, kuna recession (mdororo), Serikali hutekeleza miradi mikubwa ili watu wapate fedha kuongeza aggregate demand ili uzalishaji uweze kurudi. Sisi hapa kwetu tuna miradi mikubwa kwelikweli lakini aggregate demand haionekani, haiongezeki ni kwa nini? Kwa sababu katika hali ya kawaida ilitakiwa leo Watanzania wawe na furaha kwelikweli kwa sababu tuna miradi inayoingiza fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ni kwa sababu miradi yetu inatoa fedha kupeleka nje, miradi yetu ni outflows siyo inflows ndiyo maana kuna shida, ndiyo maana liquidity ni problem katika nchi yetu. Ndiyo maana tunazungumzia sijui inflation kwamba imeshuka na nini, ni inflation ambayo inatokana
na watu kutokuwa na fedha za kununua bidhaa, ndiyo maana inflation iko very low. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ndiyo maana ndani ya miaka mitatu, kwa mujibu wa taarifa ya World Bank na jana Mheshimiwa Komu amezungumza hapa, Watanzania milioni mbili wameingia kwenye poverty. Kwa sababu mifumo na maamuzi yetu ya kiuchumi sio ambayo yanakwenda kuwasaidia wale wadogo. Fine, tuna miradi mikubwa tutashangilia lakini hii miradi mikubwa haitengenezwi kwa namna ambayo itamfanya mpaka mtu wa chini aweze kupata hali nzuri ya uchumi.

Mheshimiwa Spika, suala lingine naomba nipate maelezo ya Serikali, tunaambiwa kwamba Tanzania Agricultural Development Bank imepata mkopo kutoka African Development Bank ndiyo fedha ambazo zinatumika kwa ajili ya kununua korosho. Sisi ni watu wazima humu ndani, leo hii nenda kwenye website ya African Development Bank angalia kama kuna credit inayokwenda Tanzania Agricultural Development Bank, hutaona. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo hii dakika chache kabla sijaanza kuongea nimetazama na nimekuta mara ya mwihso ni credit ya tarehe 24 Januari, 2019. Serikali itueleze hizi bilioni 900 zimetoka wapi? Mmekwenda Benki Kuu kuondoa kwenye deposits za Mashirika ya Umma kwa ajili ya kupeleka Agricultural Development Bank na kwenye Bodi ya Mazao Mchanganyiko kwa ajili ya kununua korosho? Haitakuwa mbaya lakini mtuambie badala ya kudanganya.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu mlituambia tutanunua korosho, tutazibangua, tutauza nje, tunauza korosho ghafi kama vile walivyokuwa wanafanya watu wengine. Naomba sasa hivi tuondokane na hiki kitu cha kudanganyana na kutoelezana ukweli. Naomba Serikali itueleze leo fedha zile zimetoka wapi kwa sababu fedha za African Development Bank pale hazipo, sasa mtueleze Benki Kuu mmezichukua kutoka kwa nani, kutoka kwenye akaunti zipi na taratibu zipi ambazo zitatengenezwa kwa ajili ya kuzirejesha fedha hizo, kwa sababu tunajua Benki yetu hii ya Kilimo haina mtaji huo wala hizo deposits za kuweza kununua hizo fedha ambazo zinatakiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la mwisho ambalo ninapenda kulichangia ni hili suala la TFS. Kamati ya Utalii imezungumzia kuifanya TFS iwe Mamlaka kutoka kuwa Wakala, naunga mkono ukurasa wa 13 wa Kamati hiyo kwa sababu wanashughulikia misitu mingi sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, yale matatizo ambayo yalitokea Iringa juzi ya miti ile ya watu wa REA na makampuni yanayotutengezea umeme kuzuiwa kwa ajili ya ushuru wa Halmshauri na kadhalika, ile ni double payment kwa sababu TFS already imeshalipa zile cess lakini pili, Mkuu wa Mkoa akaagiza tena kwamba Halmashauri zilipwe tena, matokeo yake ni nini, sisi ndiyo ambayo tunaathirika tunakosa nguzo kwa ajili ya umeme. Tukiipa TFS mamlaka ya kutosha ikawa mamlaka inaweza ikasaidia kuondokana na hizi kero nyingine ambazo zimetokea. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo, nakubaliana na mapendekezo ya Kamati zote mbili ambazo zimeleta taarifa zake hapa na naamini kabisa kwamba zitaweza kufanyiwa kazi na Serikali italeta taratibu za utekelezaji wake. Ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi nashukuru kwa kupata nafasi ya kuchangia Makadirio ya Bajeti ya Wizara hizi ambazo ziko chini ya Ofisi Rais, TAMISEMI na Utumishi na Utawala Bora. Nianze na jambo la Utawala Bora ambalo Mheshimiwa Prof. Tibaijuka ameligusia kidogo. Naomba nilipanue zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na utamaduni hivi sasa, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka kukamata watu. Hatujui kama kesi hizo wanabambikiwa au ni kesi halali, lakini baadaye tunaona kwamba watu wale wanakubaliana na Ofisi ya DPP, wanalipa fedha kesi zinakwisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nchi yetu ipate ufafanuzi, kwa sababu namna ambavyo jambo hili linafanywa, kwanza inawezekana kuna uonevu mkubwa sana kwamba kuna watu ambao wanabambikiwa kesi, wanapewa money laundering offences, wanawekwa ndani ili wakazungumze na DPP halafu waende Mahakamani wakiri walipe faini ya kile kiwango ambacho wameshtakiwa nacho. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano dhahiri ni wa juzi, ambapo taarifa ambayo VODACOM wameitoa, kwa sababu VODACOM ni listed Company; hawa watu wengine inawezekana negotiations zinafanyika na DPP zinaishia kimya kimya hatujui, lakini kwa VODACOM kwa sababu ni listed Company waliweka taarifa yao ile public kwa sababu wako listed kwenye Dar es Salaam Stock exchange na Johannesburg Stock exchange.

Mheshimiwa Mwenyekiti, VODACOM wanasema, VODACOM Tanzania has reached an agreement with Director of Public Prosecutions (DPP) for five detained employees to be released. The agreement include payment of five point two billion Tanzania Shillings by VODACOM to Tanzania in order to settle charges initiated by DPP.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba nipate uelewa. Nchi yetu haina sheria wala kanuni zinazowezesha pale ambapo mtu anakuwa ametuhumiwa kujadiliana na prosecuter ili ama kupunguza adhabu au kufuta adhabu au kulipa faini. Haya makubaliano ya DPP na watuhumiwa yanaendeshwa kwa sheria ipi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumepewa revenue book, kila Mbunge amepewa. Ukitazama revenue books hizi, kuna kila senti ambapo kila Idara ya Serikali inaingiza. Nimeangalia Vote 35 - The National Prosecutions Services, kwa miaka mitatu yote ya nyuma na hata mwaka huu, wanatarajiwa kuingiza shilingi milioni 14 tu. Mwaka 2018 peke yake DPP wamefanya transactions za zaidi ya shilingi bilioni 23 kwa watu ambao wanakamatwa na ku-settle kesi kati yao na DPP wanaenda Mahakamani kesi zinafutwa. Naomba kufahamu, kwa sheria ipi? Fedha zinakwenda wapi? Nani anazikagua hizo fedha? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili jambo ni jambo ambalo tukilikalia kimya tunatengeneza a gangstar republic, kwamba dola inaweza ikaenda ikamkata mtu, ikamzushia, ikamwambia ukitaka utoke, toa hela; watu wanatoa hela, wanatoka. Hatuwezi kuendesha nchi kama gangstars. Naomba tupate maelezo ya jambo hili, ni namna gani ambavyo linakwenda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili…

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti,...

MBUNGE FULANI: Tulia wewe…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Stella Manyanya.

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Naomba kwa mujibu wa kauni ya 64 1(a) na kuendelea, naomba kufuatia maelezo ambayo Mheshimiwa Zitto anayazungumza, badala tu ya kuyaweka kwa ujumla jumla na kwa sababu vyombo anavyovizungumzia ni vizito na vinavyoheshimika katika nchi hii, ni vyema akatoa kwa vielelezo vikaja mbele ya kiti chako ili hata watakapokuja ku-respond wajue ni kitu gani anakizungumzia kwa uhakika. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Zitto.

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ambalo nataka kulizungumzia ni TAKUKURU. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, TAKUKURU ndiyo Taasisi ambayo tumeipa dhamana ya kupambana na Rushwa. Nimeona kwenye bajeti ya mwaka huu tunawaombea shilingi bilioni 75, lakini taarifa ambazo ninazo za uhakika ni kwamba kwa takribani miaka minane iliyopita TAKUKURU hesabu zake hazijawahi kukaguliwa na auditor yeyote yule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nifahamu kutoka Ofisi ya Utawala Bora, ni kwa nini TAKUKURU, licha ya kwamba sheria tuliyoitunga mwaka 2007 inataka wafunge mahesabu na wakaguliwe, kwa nini TAKUKURU hawakaguliwi na kila mwaka tunawatengea mabilioni ya fedha, tunawaamini kwamba wanapambana na rushwa, lakini wao wenyewe fedha ambazo tunawapa hazikaguliwi na wala hili Bunge haliwezi kuziona? Ni kwa nini jambo hilo linaendelea kufanyika? Naomba Serikali iweze kutoa maelezo ya hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu, utawala bora pia na hili jambo ni la muhimu sana; kuna watu kwenye nchi ambao ni lazima mhakikishe ya kwamba hawakugusiki na mambo machafu au hata hisia. Nimesoma hotuba ya Ofisi ya Rais hapa ukurasa wa 87 ambapo Bunge linajulishwa kuwa kwa mujibu wa GN Na. 252 ya mwaka 2018, sasa Wakala wa Ndege za Serikali umehamishiwa Ofisi ya Rais kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, unafahamu kwamba mwaka 2017/2018 tulitenga fedha shilingi bilioni 509, mwaka uliofuata shilingi bilioni 497 na mwaka huu zinaombwa shilingi bilioni 500 kwa ajili ya ununuzi wa ndege za ATCL. Sisi wote tunajua ATCL hawamiliki ndege zile. Ndege zile zinamilikiwa na Wakala wa Ndege wa Serikali. ATCL inakodishiwa ndege zile. Halafu tumepitisha huko, tunategemea kwamba CAG atakwenda kukagua Wizara ya Ujenzi na kadhalika, ghafla tunaambiwa kwamba Wakala wa Ndege za Serikali hayuko tena Ujenzi, iko Ofisi ya Rais. Serikali inaenda kuficha nini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, maana yake mtu mwingine anafanya procurement, una mtu mwingine anamiliki ndege, una mtu mwingine anaziendesha zile ndege; Serikali inataka kuficha nini? Kwa nini mnafanya mambo bila kutumia maarifa mnajaza jambo kama hili lenye ma-procurement ya hela nyingi, chini ya Ofisi ya Rais? Likitokea doa hata kidogo, mmnamgusa Rais moja kwa moja. Nasi hatulaza damu, tutasema moja kwa moja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana hivi vitu huwa vinatenganishwa ili angalau Mkuu wa Nchi anakuwa juu aweze ku-deal na hawa wa chini. Mnalundika procurement yote, zenye utata hatujui zilitangazwa lini, negotiations zilikuwaje, ndege zinadondoka kila siku. Juzi hapa KQ Dreamliner yao imekwama, imetua Dar es Salaam. Ikianguka yetu hapa, twende tukamlaumu Rais? Hivi si ni vitu vya kawaida tu ambavyo wataalam mnapaswa kukaa na muepushe! Hata mwenyewe akitaka, mnamwambia mzee hatuwezi kufanya, tukifanya tutakuletea shida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nipate maelezo ya Serikali ni kwa nini maamuzi haya yamefanywa? Maamuzi haya mmefanya wakati Bunge linaendelea, maana yake ilikuwa Bunge linaendelea, ni Juni 2018, tayari tumeshapitisha Bajeti inayokwenda kununua hizo ndege kwa ajili ya kwenda Wizara ya Ujenzi, halafu pia mambo yote hayo yamepelekwa Ofisi ya Rais na tunajua hapa kuna controversies za Vote 20 ambazo naomba nipate maelezo haya ya Serikali... (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Katiba na Sheria
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kupata nafasi ya kuchangia mafungu mbalimbali katika Wizara ya Katiba na Sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kumpongeza Mzee wangu Mheshimiwa Balozi Mahiga kwa uteuzi wake wa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Naamini kwamba uzoefu wake katika Mambo ya Nje utaweza kusaidia kwa kiwango kikubwa kazi kubwa iliyoko katika Wizara hii. Kwa hiyo, nampongeza sana Mheshimiwa Mahiga. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nitoe shukrani za dhati kwa Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufanikisha ufunguzi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Kigoma. Mahakama hiyo itaweza kutusaidia sana watu wa Kigoma kuweza kupunguza mwendo wa kwenda Tabora kwa ajili ya kufuatilia kesi mbalimbali. Kwa hiyo, naomba salamu zangu kwa Jaji Mkuu ziweze kufika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina mambo mawili tu ambayo ningependa kuya-address. Jambo la kwanza linahusiana na mashauri mbalimbali ambayo Serikali yetu inakabiliwa nayo katika Mahakama mbalimbali za Kimataifa na namna gani bora ya kuweza kuhakikisha kwamba maslahi ya Taifa kwa maana ya public interest yanazingatiwa katika kukamilisha mambo haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mara kadhaa siku za nyuma nimekuwa nikishauriana kwanza Waziri, Mheshimiwa Kabudi na baadaye Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwamba kuna baadhi ya kesi ambazo sisi tumeshtakiwa lakini tuna vithibitisho vya kuhakikisha kwamba sisi tusishitakiwe katika kesi kama zile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kesi mojawapo ni ambayo inafanyika sasa na imeshaamuliwa kati ya Tanzania na Benki ya Standard Chartered ya Hong Kong ambayo mwaka jana ilikuwa ni audit query kwenye Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na mwaka huu nimeona Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ameweka Jedwali la Utekelezaji na ameeleza kwamba TANESCO kwa kushirikiana na Serikali iko katika mchakato wa kutekeleza Deed of Indemnity iliyotumiwa na Bwana Harbinder Singh Sethi kwa niaba ya IPTL na Benki ya Tanzania kwa ajili ya Serikali ya Tanzania kutatua madai yanayotarajiwa na Standard Chartered Bank - Hong Kong ikiwa TANESCO itashindwa. Hii ni kesi ya zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 148.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa suala ambalo napenda Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Serikali nzima iweze kulieleza kwamba public interest yetu hapa ni fedha ambazo zilichotwa kutoka Benki Kuu kurejeshwa. Ndiyo public interest yetu hapa, public interest siyo kuwaweka watu ndani na fedha zile zikosekane. Sasa kwa sababu tuna Deed of Indemnity na tayari mazungumzo yanaendelea, Serikali inaweza kulifahamisha Bunge ni hatua gani inazichukua ili watu ambao wamewaweka ndani waweze kushirikiana na Serikali, Deed of Indemnity ifanye kazi tuondokane na haya madai ambayo sisi tunadaiwa. Kwa hiyo, naomba hili Mwanasheria Mkuu wa Serikali na wenzake waweze kutupatia majibu kwa sababu ni jambo ambalo linaweza kuokoa mabilioni ya fedha iwapo tutalifanya kwa maarifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni kesi ambayo sitaki kuizungumzia kwa undani, ya Standard Bank ya Mzee Kitilya ya zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 6. Wote tunafahamu kwamba kuna Benki ya Kimataifa ambayo iwapo raia wetu wangetumika kama mashahidi nchi yetu tungeweza kukwepa mkopo wa Dola za Kimarekani milioni 600 ambao sisi tunaamini kwamba ulipatikana kwa njia za rushwa. Hata hivyo, Serikali yetu badala ya kufanya kazi na raia wake inawaweka ndani raia wake, inarefusha kesi wakati kuna deni hapa ambalo kila mwaka tunalipa riba na thamani ya shilingi inaporomoka na gharama ya deni inaongezeka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashindwa kuelewa Serikali hapa hekima yake ni ipi? Hekima yake ni kuhangaika na Dola milioni 6 na kuwaweka watu ndani au hekima ni kuokoa mkopo wa Dola za Kimarekani milioni 600 ambao kama tuki- prove kwamba ulipatikana kwa rushwa mkopo ule nchi yetu haitaweza kuulipa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba nipate maelezo ya Serikali inatumia hekima gani katika hili? Au inaona raha tu kumweka Kitilya ndani au inataka kumkomoa Kitilya na wenzake? Kwa nini hatufanyi maamuzi ambayo public interest ni kubwa zaidi kuliko kuumiza watu kama ambavyo tunafanya? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, ni jambo ambalo nililizungumza kwenye bajeti ya mzee wangu Mheshimiwa Mkuchika, suala la Ofisi ya DPP. Majibu ambayo Mheshimiwa Mkuchika aliyatoa pamoja na kwamba aliongea kwa busara sana lakini sikuridhika nayo kwa sababu mateso ambayo wananchi wanapata kutokana na ubambikiwaji wa kesi na majadiliano ya pembeni ambayo hayafuati sheria kwa sababu hatuna sheria ya pre-bargain tunawaonea raia wetu sana. Naomba Serikali iweze kutazama na ni jambo rahisi sana.

KUHUSU UTARATIBU

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nachokiona ni kwamba mfumo wetu wa jinai (criminal justice system) ni mfumo ambao umejaa uonevu, unaweka mazingira ambapo tunawatesa raia wetu na unapaswa kufumuliwa. Ili mfumo huu ufumuliwe sawasawa lazima tuanze na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka (DPP). (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nachokiomba na nitatumia Kanuni ya 120(2)(a) ya Kanuni za Bunge kwamba mara baada ya mjadala huu kukamilika, nitatoa taarifa kwamba Bunge liunde Kamati Teule kwa ajili ya kuchunguza, kufanya probe ya makubaliano ambayo Ofisi ya DPP inafanya na watu ambao walikuwa watuhumiwa na kutoa fedha, kwa sababu fedha zingine zinatolewa pembeni, wanazungumza unaambiwa mpelekee mtu fulani, malalamiko mtaani ni makubwa sana. Ukiyasikia malalamiko hayo unaumia, mtu yoyote anayependa justice anaumia. Haiwezekani mfumo wetu wa mashtaka ndiyo ukawa mfumo wa kukomoa watu, ikawa kama ni Kangaroo Court ikawa watu wanaonewa, unakamatwa...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Kilimo
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Spika, Serikali imetangaza dhamira yake ya kuanzisha Bima ya Mazao ili kukabiliana na majanga. Ni wazo zuri na naliunga mkono japo litazamwe kwa makini isije kuwa ni gharama kwa mkulima na faida kwa makampuni ya bima. Hata hivyo, napenda kurudia wito wangu kuwa kuna haja ya kuwa na Skimu ya Hifadhi ya Jamii kwa Wakulima. Bima ya Mazao yaweza kuwa moja ya mafao yatakayotolewa na mfumo huo.

Mheshimiwa Spika, nasaha yangu kwa Serikali ni kuanzisha Skimu ya Hifadhi ya Jamii ya Wakulima ili kuwavutia kuweka akiba, kupata bima ya afya, Fao la Bei na mikopo nafuu ya pembejeo. Fao la Bei husaidia bei ya mazao ikianza kushuka. Kwa sasa bei za mazao zikishuka wakulima watarudi kwenye umaskini kwani hawana fidia ya bei kushuka (Fao la Bei). Kukiwa na price stabilisation mkulima anakuwa na hakika hata bei ikishuka chini ya kiwango cha gharama zake za uzalishaji Skimu ya Hifadhi ya Jamii itamfidia na hivyo kuendelea na shughuli zake msimu unaofuata.

Mheshimiwa Spika, mwezi Januari, 2018 niliandika Kuhusu Skimu hii kwenye zao la korosho, nanukuu:

“Mwaka huu peke yake iwapo wakulima 600,000 wa korosho wangekuwa kwenye hifadhi ya jamii, wangeweza kuweka akiba ya TZS 144 bilioni (14% ya Mapato yote ya korosho katika msimu mpaka sasa). Ingekuwa tumefanya hivi tangu 2015/2016 na 2016/2017, leo skimu ya Hifadhi ya Jamii ya Wakulima wa Korosho peke yake ingekuwa na thamani ya zaidi ya shilingi 300 bilioni. Hizi zingeweza kuwekezwa kwenye biashara ya pembejeo za kilimo, kuboresha mashamba, viwanda vya kuongeza thamani (processing factories). Pia ingetatua kabisa tatizo la afya kwa kuwapa wakulima wote Bima ya Afya bila kuathiri akiba zao.” Mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa Spika, kupitia Skimu wakulima wanaweza kuingia kwenye mpango wa nyumba bora kwa kupewa mikopo ya muda mrefu ya nyumba na hivyo kufuta kabisa umaskini. Mkulima wa Tanzania anaathiriwa sana na mitaji ya pembejeo, uhakika wa bei za mazao yao na gharama za matibabu wanapoumwa wao na familia zao. Yote haya yanajibiwa na hifadhi ya jamii. Zaidi ya yote mkulima anakuwa na akiba ya uzeeni, pale ambapo hataweza tena kulima anakuwa analipwa pensheni ya kila mwezi. Haya ndio mapinduzi tunayoyataka kwenye nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, nawasihi Wabunge kulitazama hili na kufanya kazi na Serikali ili kuleta mabadiliko makubwa kwa wananchi. Serikali ianze na wakulima wa baadhi ya mazao kama vile tumbaku, kahawa, pamba, karafuu, chai na mkonge. Baada ya kutekeleza na kujifunza kwa wakulima hawa tunaweza kupanua wigo kwenda kwa wakulima wote nchini.

Mheshimiwa Spika, skimu ya namna hii pia yaweza kutekelezwa kwa wafugaji na wavuvi pia. Mfano wakulima wa korosho wapatao 600,000 nchini wakiwa kwenye Hifadhi ya Jamii (kwa kutumia ushuru wa korosho - exports levy), tutaweza kufikia watu 3.6m wenye Bima ya Afya katika mikoa yote inayolima korosho ambao ni sawa na wananchi wote wa Lindi, Mtwara, Tunduru na baadhi ya Wilaya za Mkoa wa Pwani. Kupitia Skimu na mafao yake wakulima hawatakopwa mazao yao, pembejeo zitafika kwa wakati na wakati wa hali mbaya ya bei, watafidiwa gharama zao za uzalishaji.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Fedha na Mipango
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi nami ya kuchangia bajeti, makadirio ya bajeti ya Wizara ya Fedha, mafungu yote saba ya Wizara hii. Na nitakuwa na maeneo matatu ya kuchangia, kama nitapata muda nitaongeza eneo la nne na ningependa kuanza na upande wa makusanyo ya kodi.

Mheshimiwa Spika, kwa muda wa miaka minne sasa tumekuwa tukielezwa kwamba tumeongeza sana uwezo wetu wa makusanyo ya kodi, lakini ukitazama takwimu za Serikali yenyewe kuhusiana na uwezo wetu wa kukusanya kodi ukilinganisha na huku ambako tunatoka story hii sio story ya kweli. Ni story ambayo inapaswa tuelezwe upya, ili tuweze kuona changamoto ni nini na tuweze kutatua namna gani.

Mheshimiwa Spika, kwa mfano wakati Serikali ya Awamu ya Tano inaingia madarakani mwaka 2015, kipimo cha makusayo ya kodi kwa kutumia Pato la Taifa, yaani tax GDP ratio ilikuwa tumefikia asilimia 15 na lengo letu na Waziri Mpango atakumbuka kwamba katika Mpango wa Maendeleo wa Kwanza ilikuwa na lengo la asilimia 16 ambalo ndio sasa lengo la bajeti ambayo inakwisha sasa hivi na Mpango wa Maendeleo wa Pili tufike asilimia 19 ya pato la Taifa.

Mheshimiwa Spika, lakini kwa mujibu wa Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali tax GDP ratio ya mwaka wa fedha 2017/2018 ni asilimia 12 tu. Na hii inatuweka sisi kuwa hata chini ya nchi kama Burundi ambayo tax GDP ratio ni asilimia 13, Kenya asilimia 18.1, Uganda asilimia 16, Rwanda asilimia 16. Katika nchi za Afrika Mashariki sisi ni wa mwisho ukitumia kiashiria cha kupima makusanyo ya ndani kulingana na Pato la Taifa yaani shughuli za uchumi katika nchi. Hii inathibitisha ya kwamba hatuendi mbele katika makusanyo ya kodi, bali tunarudi nyuma, lakini kwa sababu tunaangalia tarakimu tumetoka bilioni 800 mpaka trilioni 1.2 au trilioni 1.3 tunajiona kana kwamba tunakusanya sana, lakini ukiangalia bilioni 800 ya Pato la Taifa kwa mwaka husika na trilioni 1.3 ya Pato la Taifa la mwaka huo maana yake ni kwamba tunashuka sana.

Mheshimiwa Spika, nimepita library asubuhi, nimejaribu kuangalia miaka mitatu ya mwisho ya Serikali ya Awamu ya Nne ongezeko la makusanyo ya kodi lilikuwa ni asilimia ngapi kulingana na miaka mitatu ya mwanzo mpaka huu mwaka wa fedha tunaoumaliza sasa ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Mheshimiwa Spika, miaka mitatu ya mwisho ya Serikali ya Awamu ya Nne wastani wa ongezeko la makusanyo ya kodi lilikuwa ni asilimia 16. Wastani wa makusanyo ya Serikali ya Awamu ya Tano toka wameanza mpaka bajeti hii ambayo tunaimalizia ni asilimia 11.3; kwa hiyo, hakuna sababu yoyote ya kujidanganya kwamba tuna makusanyo makubwa ilhali makusanyo si mazuri.

Mheshimiwa Spika, na makusanyo si mazuri kwa sababu biashara zinafungwa; sekta binafsi ndio inayotengeneza kodi, sekta ya umma haitengenezi kodi. Zaidi ya asilimia 95 ya watu wanaoajiriwa, ajira rasmi katika nchi yetu, wanatoka sekta binafsi, kwa miaka mitatu iliyopita tumeinyonga sekta binafsi.

Mheshimiwa Spika, leo tunavyozungumza, nitakupa mifano tu ya siku za karibuni; Kampuni ya Mwananchi imepunguza wafanyakazi zaidi ya 100 ndani ya wiki mbili zilizopita. Kampuni ya New Habari Corporation ya akina Mheshimiwa Bashe imepunguza kutoka wafanyakazi 300 wamebakiwa na wafanyakazi 43. Tunavyozungumza sasa Kampuni inayonunua tumbaku asilimia 40 ya tumbaku ya nchi hii, Kampuni ya TLTC, Kiwanda cha Morogoro wamefunga na wame-retrench wakati wa season watu 3,000 walipoteza kazi. Katika mazingira kama haya mtapata wapi kodi? Kwa sababu sehemu kubwa ya kodi ni kodi za wafanyakazi.

Mheshimiwa Spika, wala tusijidanganye tukadhani kwamba wenye mitaji wanalipa kodi kubwa, angalieni takwimu za Serikali 2/3 ya makusanyo ya kodi za mapato ni kodi za wafanyakazi. Kwa hiyo, ni lazima mjenge mazingira ya kazi watu wapate kazi ili Serikali ipate pesa, lakini Serikali inanyonga, biashara zinafungwa, wapi Serikali itapata pesa? Ndio maana takwimu hizi zinaonekana hivi kwamba tax GDP ratio imeshuka na hata ongezeko la hizo kitarakimu ambazo tunaambiwa bado ukilinganisha na Serikali iliyopita, zimeshuka sana ni lazima tufanye marekebisho ya uhakika ya kuhakikisha ya kwamba, tunakusanya kodi ya kutosha.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili ambalo nataka nilizungumzie nalo kwa kina kidogo ni usimamizi wa Deni la Taifa. Siendi kwenye mjadala kama deni ni himilivu au si himilivu, usimamizi wa Deni la Taifa ni tatizo. Tazama record za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa miaka miwili iliyopita, wanatoa maelezo yanayoonesha ya kwamba moja, kuna upotoshaji mkubwa katika taarifa za Deni la Taifa kwa sababu mfumo wa malipo ya Deni la Taifa na mfumo wa utunzaji wa kumbukumbu za Deni la Taifa havisomani. Matokeo yake ni kwamba tuna madeni ambayo hayako recorded.

Mheshimiwa Spika, kwa mfano kwenye Taarifa ya CAG ya mwaka jana kuna zaidi ya shilingi trilioni mbili ambazo record yake haionekani, lakini Mdhibiti amekwenda kwa waliotukopesha, kuna fedha ambazo waliotukopesha wanasema tumezitoa, ukienda Hazina wanasema hizo mbona hatujazipata kwa sababu ya mfumo mbovu wa usimamizi wa deni. Kwa hiyo, hata deni ambalo tunaambiwa hapa na Mheshimiwa Waziri Mpango ndugu yangu kwamba, ni kiasi hiki, ni asilimia hii ya Pato la Taifa sijui ya mauzo nje, na kadhalika, ni deni ambalo record yake sio sahihi.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba kwa ruhusa yako, for the first time in the history of this country, ruhusu Ukaguzi Maalum wa Deni la Taifa tuweze kupata takwimu sahihi kwa sababu takwimu za sasa hivi sio sahihi na mimi hapo nimesoma ripoti mbili tu ya mwaka jana na ya mwaka huu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ambayo inaonesha kuna tatizo kubwa sana katika utunzaji wa kumbukumbu; wanatunza kumbukumbu za deni kwenye madaftari ya shule, ma-counter book, unawezaje kutunza kumbukumbu za deni kwenye ma-counter book? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, aah, ndio ukweli huo Mheshimiwa Mwakyembe na Mheshimiwa Spika, mwambie Mheshimiwa Mwakyembe tumeingia wote Bungeni humu, tuko sawa kwa hiyo, aniheshimu wakati naongea kwa hiyo, atulie kidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba hili jambo uruhusu Ukaguzi Maalum wa Deni la Taifa kwa maslahi ya nchi tuweze kujua kwamba tunadaiwa kiasi gani na tunadaiwa na nani? Kwa sababu inawezekana tukawa tunalipa madeni ambayo ni hewa, hayapo. Kuna kitu kinaitwa odious debts, debts ambazo zimekuwa created, hazipo na hii inawezekana kabisa ipo katika mfumo wetu kwa sababu haufanyi kazi sawasawa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la mwisho ni jambo ambalo naishukuru sana Kamati ya Bajeti na naipongeza sana imefanya kazi nzuri sana ya Bunge. Kuna fedha ambazo zinakusanywa kinyume na Katiba na sheria. Kwa mujibu wa Ibara ya 138 ya Katiba, Bunge lako hili unaloliongoza ndilo lenye mamlaka ya kutamka kodi. Ibara ya 138 ya Katiba; hakuna kodi ya aina yoyote itakayotozwa isipokuwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge au kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa kisheria na uliotiliwa nguvu kisheria na sheria iliyotungwa na Bunge.

Mheshimiwa Spika, lini hapa Bungeni tulikaa tukapanga ushuru wa vitambulisho vya wamachinga? Wapi kwenye revenue book unaona hayo mapato? Tutawa- account namba gani hawa? Haipo kwenye sheria…

SPIKA: Ahsante sana, muda hauko upande wako.

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Spika, naomba dakika moja tu ya kiti, dakika moja ya kiti. Ahsante sana.

Mheshimiwa Spika, haipo kwenye sheria ya utaratibu wala kwenye revenue book, hakuna mahali ambapo fedha zinazokusanywa kwa wananchi wetu zimo, sasa tunatuvunjaje sheria na Katiba namna hii? Kwamba Bunge halijakaa kutunga, Serikali inatekeleza, watu wetu wanaumizwa, nimesikia Tunduma huko leo wafanyabiashara wameshindwa kufanya biashara kwa sababu wameambiwa hawana vitambulisho, haimo kwenye revenue book, kwenye sheria, tunavunja Katiba kwa nini? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba maoni yaliyotolewa na Kamati ya… (Makofi)

SPIKA: Nakushukuru sana.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. ZITTO Z. KABWE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuweza kutoa mchango wangu katika Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2019/2020.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2018 Serikali ilikuja na pendekezo kwenye Bunge lako Tukufu la kuweza kutoa unafuu kwa wanawake milioni 13 wa nchi hii katika matumizi yao ya taulo za kike kila mwezi. Mwaka huu Serikali imeona kwamba pendekezo lile halijaleta yale matokeo ambayo ilikuwa inayataka. Ukurasa wa 38 Waziri wa Fedha anasema, kwa kuwa pendekezo lile halijawezesha kupatikana kwa bidhaa hiyo, muhimu kwa bei nafuu kwa walengwa na badala yake pendekezo lile limefaidisha wafanyabiashara.

Mheshimiwa Naibu Spika, inawezekana kabisa kwamba Serikali ikawa concerned kwamba bei ya taulo za kike haikushuka kutokana na mapendekezo ambayo Serikali iliyaleta, lakini Serikali inapaswa kujitafakari; je, mwaka mmoja ambao utekelezaji umefanyika unatosha kuweza kupima matokeo ya sera ile ambayo iliyefanya mwaka 2018? Katika hilo naomba niikumbushe Serikali kwamba mwaka 2018 Serikali ilikuja na pendekezo la kuongeza kodi kwenye mafuta ghafi yanayotoka nje ili kulinda wazalishaji wa mbegu za mafuta hapa nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika na Bunge lako Tukufu kwa pamoja, nataka tutazame nini matokeo ya pendekezo lile ambalo Serikali ililileta? Mwaka 2017 kabla ya kodi zile kupandishwa katika uzalishaji wa mazao ya mafuta tulikuwa tunazalisha tani 6,600,000 mwaka 2017 kabla ya kupandisha kodi ili kudhibiti uagizaji wa mafuta kutoka nje. Mwaka 2018 tumezalisha tani 1,600,000 ni ukurasa 135 wa taarifa ya hali ya uchumi; pungufu la negative seventy six per cent (-76%) kwamba pendekezo ambalo Serikali ililileta mwaka 2018, matokeo yake ukurasa wa 135 wa Taarifa ya Hali ya Uchumi. Matokeo ya kuweka kodi hayakuzalisha tegemeo la uzalishaji wa mbegu kuongezeka, lakini Serikali mwaka huu haijaja na pendekezo la kufuta lile pendekezo la mwaka 2018. Matokeo yake imeendeleza pendekezo lile.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu kuna transition period. Huwezi ukaweka pendekezo la kikodi sasa ukategemea matokeo ya haraka hapo hapo. Kodi imeanza tarehe 1 mwezi Julai, kuna watu walikuwa wana stock ambazo walizinunua hazikuwa na hiyo exemption. Lazima wataendelea kuziuza kwa fedha zile. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, Mheshimiwa Waziri wa Fedha anafahamu, tumepata mtikisiko hapa katikati wa fedha yetu kuporomoka thamani dhidi ya dola za Kimarekani. Taulo za kike zote tunazoagiza nchi hii zinatoka nje. Factor ya exchange rate tumeitazama?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, mimi natoa rai kwa Serikali kwamba siyo sahihi kuja kufuta ile exemption tuliyoiweka mwaka 2018. Serikali inapaswa kutazama vizuri, kutoa muda wa kutosha, kama namna ambavyo imetoa muda kwenye mafuta licha ya kwamba uzalishaji umeshuka, tutazame pia tutoe muda kwenye eneo hili la taulo za kike. Uamuzi wa mwaka 2018 uliipa sifa nchi yetu, tulikuwa ni a pioneer country katika kulinda wanawake wa nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, India wametufuata, wametuiga sisi, Australia wametufuata, wametuiga sisi na nchi nyingine mbalimbali. Mwaka huu South Africa wametuiga sisi. Sisi tunarudi nyuma kwa sababu tu ndani ya mwaka mmoja, bei haikushuka, hapana, siyo sahihi. Naisihi Serikali itazame upya pendekezo hili na itazame upya pendekezo hili kwa kuwa tayari ndani ya bajeti ya mwaka huu Serikali imependekeza kuondoa ushuru kwenye malighafi zinazozalisha taulo za watoto. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, malighafi za taulo za watoto ndiyo malighafi za taulo za kike. Meza ambayo inapaswa kufanya kwenye taulo za watoto, ndiyo meza hiyo hiyo inatakiwa kufanywa kwenye taulo za kike. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naisihi Serikali, moja, pendekezo…

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango.

TAARIFA

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kumpa taarifa msemaji kwamba tozo anayosema imepunguzwa kwenye malighafi za diapers, tozo hiyo pia kwa miaka minne mfululizo imeondolewa kwenye malighafi za kutengeneza taulo za kike. Kwa hiyo, hili jambo lipo, siyo kwamba ni jambo geni ambalo linatakiwa kupendekezwa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Zitto Kabwe unaipokea taarifa hiyo?

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. Kwa hiyo, VAT exemption kwenye taulo za kike mwaka huu, labda kuwe na sababu nyingine, lakini kwa sababu ya bei kutokushuka, naomba Serikali itazame upya kwa sababu ni jambo ambalo linaweza kutatuliwa administratively. Tuna tatizo kwamba retailers, wauzaji wa mwisho margin yao kwenye taulo za kike ni kubwa sana na jambo hili linaweza likatekelezwa administratively kwa kuhakikisha kwamba wanakaa na kuweza kupata suluhisho la kudumu.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili ni suala zima la uwekezaji katika nchi yetu. Serikali inazungumza kwamba pato letu la Taifa linakua kwa 7%. Sitaki kuingia kwenye ubishani kati ya Serikali ya takwimu zao na takwimu za taasisi nyingine. Hata hivyo tumeona kuwa ndani ya mwaka mmoja, kwa mujibu wa taarifa ya hali ya uchumi, uwekezaji nchini umeporomoka kwa asilimia 44.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2017 thamani ya uwekezaji ndani ya nchi yetu ilikuwa ni dola za Kimarekani bilioni 5.2. Sasa hivi imeshuka mpaka dola za Kimarekani bilioni 2.8. Mauzo yetu nje yameporomoka sana na urari umekuwa hasi na tumewahi kuwa na urari wa bidhaa kati ya biashara ya ndani na nje ukiwa chanya miaka ya nyuma iliyopita. Mheshimiwa Waziri Dkt. Mpango anafahamu na ni wote wawili; Waziri na Naibu Waziri anafahamu.

Mheshimiwa Naibu Spika, pato la Taifa, unachukua consumption, unachukua investment, unachukua government expenditure, unachukua export minus imports. Investment negative forty four (-44) growth ya matumizi ya Serikali kwa maana ya bajeti ya Serikali inaongezeka kwa 2% tu sasa hivi. Export minus imports negative, kwa sababu tuna-import zaidi kuliko ku-export, pato la Taifa litakuwaje katika mazingira kama hayo? Ni lazima Serikali ifanye kazi ya bidii kuhakikisha ya kwamba tunaongeza zaidi exports nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia, licha ya miradi ambayo inazungumzwa, hali ya uchumi wa wananchi, uzalishaji wa wananchi unashuka sana. Angalieni mazao yetu ya kilimo, ukiangalia Taarifa ya Hali ya Uchumi unaona na baadhi ya maeneo tunaona uzalishaji unashuka kwa sababu tu ya sera za Serikali ambazo siyo sahihi. Naomba Serikali iweze kutazama kwa umakini. Haiwezekani ukawa na growth kubwa kama foreign direct investment na export zetu zinazidi kushuka mwaka hadi mwaka kwa sababu unakosa inflows kwenye nchi ambalo ni jambo la muhimu sana kwa ajili ya kuweza kuhakikisha kwamba uchumi unaweza kukua.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi kuna continental free trade area, Waafrika tunatakiwa tuwe katika uchumi wa pamoja.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Ni ya pili? Samahani, nashukuru sana, ahsante.
Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari za Mwaka 2016
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa kupata nafasi hii ya kuchangia muswada huu muhimu sana. Kama ambavyo Mheshimiwa Waziri wa Habari amesema ni muswada wa kihistoria, na ni wa kihistoria kwelikweli; kwa namna ambavyo umeletwa na kwa namna ambavyo umechukua muda mrefu sana huko nyuma, katika dil-ly-dal-ly za kati ya muswada unaandikwa au hauandikwi.
Napenda nimpongeze sana Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa maelezo ambayo ameyatoa, na yale maeneo mengine ambayo hakuyagusia wengine tutayagusia. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, unapoandika sheria mpya, maana yake ni kwamba sheria ambayo ipo wakati huo au mazingira ya wakati huo, hayatoshelezi hali ambayo inatakiwa kuwapo, ndiyo sababu hasa ya kuandika sheria hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sheria hii ambayo tunaijadili leo, lengo lake ni kujibu malalamiko ya muda mrefu kuhusiana na Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini katika mambo yote ya Sheria ya Magazeti ni jambo lipi ambalo lilikuwa linalalamikiwa sana, ni suala la mamlaka ya Waziri kufungia gazeti lolote au chombo chochote cha habari, muda wowote ambao yeye anataka. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 kifungu cha 25, kinasema; “Minister may prohibit publication of the newspaper.”
Mheshimiwa Mwenyekiti, tulitarajia kwamba sheria hii mpya, ingekuja na provision bora zaidi miaka 40 baada ya sheria ya mwaka 1976 kutungwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kifungu cha 55 cha sheria mpya ambayo tumeletewa hapa, ambacho kinasema powers of the Minister; The Minister shall have powers to prohibit or otherwise sanction the publication of any content, not only any newspapers, any content that jeopardises national security or public safety. Na national security or public safety haijawa defined mahali popote katika sheria hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sheria ya mwaka 1976 kifungu ambacho kinamuwezesha Waziri kufungia gazeti kimeweka hata masharti ya namna ya kulifungia, sheria ya mwaka 2016 kifungu hicho kimetoa tu powers na Waziri anaweza akaamua kufanya anavyotaka. Kwa hiyo, hakuna ubora wowote kati ya sheria hii na sheria mpya ambayo tunataka tuitunge hivi sasa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ndio maana tunasema na tunatoa wito kwa Serikali kwamba kuna haja ya kufanyia kazi zaidi muswada huu kwa sababu hatuoni tofauti kubwa. Kwa sababu kunaweza kukawa na mambo mengi ambayo yanaelezwa kwamba yana faida. Ukiangalia muswada uliochapishwa mwezi Septemba uliokuja kwenye Kamati ni mbaya zaidi kuliko muswada ambao umetoka kwenye Kamati pamoja na amendment hizi. Kwa hiyo, kama tungetoa muda zaidi maana yake ni kwamba tungepata sheria iliyo bora zaidi kuliko hii sheria ambayo tumeletewa ndani ya Bunge hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sheria ya mwaka 1976 haimpi mamlaka Waziri au Serikali kukitaka chombo chochote cha binafsi kuchapisha habari yoyote wanayotaka, hakuna kifungu chochote, sheria ya mwaka 2016, miaka 40 baadaye, kifungu cha 7(1)(b)(iv) kinampa mamlaka Waziri wa Habari kuweza kuagiza habari gani ichapishwe na chombo chochote kile. Muswada huu unatengeneza Mhariri Mkuu wa Taifa ambaye ni Waziri wa Habari. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sheria ya mwaka 1976 haikuwa na accreditation kwa journalists (ithibati kwa waandishi wa habari). Ndiyo maana leo tunaye Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, ametoka Makerere karudi nchini, Mwalimu Nyerere akamteua kuwa Mhariri Mkuu wa magazeti ya Serikali. Hakuwa na elimu yoyote ya uandishi wa habari hakuwa amefanyiwa ithibati yoyote ile. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 1966 Mheshimiwa Mkapa anapewa uhariri hakuna accreditation, mwaka 1976 Sheria ya Magazeti inatungwa hakuna accreditation, mwaka 2016 kuna accreditation. Leo hii tungekuwa na sheria hii pasingekuwa na Mheshimiwa Mkapa leo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri wa Katiba na Sheria Ndugu Mwakyembe yuko hapa, amemaliza kidato cha sita hakuweza kwenda Chuo Kikuu kwa sababu ya uwezo wa wazazi, akaenda kujitolea kwenye Magazeti ya Chama cha Mapinduzi ya Uhuru, akaajiriwa baadaye baada ya kuonekana ana uwezo, akawa mwandishi wa gazeti la Uhuru, leo hii Mheshimiwa Harrison Mwakyembe ni Daktari wa Sheria, ni Waziri wetu wa Sheria; angekuwa amefanyiwa accreditation kama Serikali hii ya sasa inavyotaka tusingekuwa na Mheshimiwa Harrison Mwakyembe leo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Watanzania wengi sana hawajui, mwaka 1996 tumepata ajali mbaya sana hapa nchini ya MV Bukoba. Ajali ya MV Bukoba imetokea watu wengi walikuwa hawajui na hawajui ilifikaje kwenye public. Aliyetoa taarifa ya ajali ya MV Bukoba hakuwa mwandishi wa habari, alikuwa ni kijana mmachinga, kapewa taarifa na ndugu yake yuko ndani ya meli ile akatoa taarifa ile kwenye chombo cha habari cha Habari Corporation wakati ule, sasa hivi New Habari Corporation.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa chombo kile kilikuwa hakina mwandishi Mwanza kikamtumia mmachinga yule kuwa mwandishi wake kutoa taarifa kuhusu MV Bukoba, Serikali ikasikia kuhusu MV Bukoba kwa mmachinga si kwa mwandishi wa habari. (Makofi)
Baada ya ajali ile mwandishi yule akachukuliwa akaajiriwa na gazeti la Mtanzania likampa elimu kama ambavyo Uhuru ilivyompa elimu Mheshimiwa Dkt. Mwakyembe. Leo hii yule mwandishi anayeitwa Mbarak Islam ni mmoja wa wahariri wa uchunguzi bora zaidi hapa nchini. Kwa sheria hii leo tusingekuwa na Mbarak Islam. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuweka requirements za accreditation ni lengo la dola kutaka kudhibiti waandishi wa habari. (Makofi)
Waheshimiwa Wabunge uandishi wa habari ni passion! Uandishi wa habari ni passion! Uandishi wa habari sio tu kwamba ni kama mkemia, daktari, uandishi wa habari ni passion.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuweka accreditation kwa waandishi wa habari Waheshimiwa Wabunge tutaua vipaji vya vijana wetu wengi sana wana…
MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge tuvumiliane.
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: …kwenye sheria hii kwa ajili ya accreditation.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nawaambia ndugu zangu Wabunge, tunapotunga sheria hii mtazameni Mheshimiwa Harrison Mwakyembe; tunapotunga sheria hii mtazameni Mheshimiwa Benjamin William Mkapa; tunapotunga sheria hii mtazameni Mbarak Islam na tunapotunga sheria hii watazameni maelfu ya vijana wa Kitanzania wenye uwezo wa kuandika, lakini hawataweza kuandika kwa sababu ya accreditation ambayo mnataka kuiweka kwenye sheria hii. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kusihi hata kama tutahitaji accreditation, hata kama accreditation itahitajika hauhitaji kuwa na Bodi ya Accreditation na Baraza la Habari. Majukumu yanayofanywa na Accreditation Board yanaweza yakafanywa na Baraza la Habari ili angalau kama tunataka accreditation, angalau tupeleke majukumu hayo ya accreditation kwa waandishi wa habari wao wenyewe na sio kuweka majukumu ya accreditation ndani ya mikono ya dola. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ndugu zangu, mimi ninaomba niwasihi, tunaandika sheria itakayodumu muda mrefu sana. Naomba niwasihi sana, tutafanya makosa makubwa sana kutumia hasira zetu, maana Waziri leo amesema kwamba hakuna mtu hapa ambaye hajaguswa na kuandikwa vibaya na vyombo vya habari. Hata Mitume imetusihi usifanye maamuzi ukiwa na furaha sana au ukiwa na hasira, tukiandika sheria hii kwa hasira ambazo tunazo labda kwa sababu tuliandikwa vibaya tutatunga sheria mbaya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ni shuhuda wa kuandikwa vibaya sana na vyombo vya habari, mimi hapa ninayezungumza na ninyi, lakini nitakuwa wa mwisho kunyima uhuru waandishi wa habari kuandika na ndiyo maana tunataka pawepo na taratibu ambazo utakwenda kulalamika, utashughulikiwa, lakini sio kwa namna ambavyo tumeweka kwenye sheria hii. Nawasihi ndugu zangu Wabunge tuangalie upya sheria hii ili tuweze kuandika sheria ambayo haitatuleta madhara hapo badaye. (Makofi)
Mheshikmiwa Mwenyekiti, nashukuru sana.
Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Maliasili wa Mwaka 2017.
MHE. ZITTO Z. R. KABWE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa muda ambao umenipa maana uliniambia dakika saba baadaye ukasema tano, kutokana na mambo ambayo nimeyapanga kuzungumza nitaangalia yale
ambayo nitakayoweza kuzungumza na mengine labda nitaweka kwa maandishi.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la kwanza ambalo napenda nilizungumze ni nasaha tu kwa Bunge. Kazi ambayo tunaifanya hapa ni kubwa sana lakini aina ya mjadala yaani quality of debate ambayo tunayo hailingani na uzito wa jambo ambalo tunalifanya hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, napenda kuwasihi Wabunge wa pande zote mbili, bahati nzuri nina hiyo moral authority maana pande zote mbili mimi niko mwenyewe, mwenzangu naona wewe uko UKAWA. Kwa hiyo, nawasihi tufanye jambo hili kwa utulivu ili tuweze kutunga sheria ambayo itakuwa na manufaa kwa nchi. Hii kubishana, kurushiana maneno na kadhalika yanatupotezea muda muhimu sana sisi kama nchi kuweza kufanya kazi hiyo kwa pamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, kwa ujumla hii seti ina sheria tatu. Sheria moja ndiyo kubwa sana ile ya mabadiliko ya The Mining Act, kwa hiyo, tunaweza tukahitaji muda wa kutosha sana kule. Sheria mbili hizi, hii ya re- negotiation na hii ya sovereignty ni statements of intent. Ni mambo ambayo tulipaswa tuyafanye toka mwaka 1962, hatujafanya. Kwa hiyo, tunakuja hapa kwa ajili ya ku-correct hayo makosa ambayo tumeyafanya huko nyuma. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nadhani hizi sheria mbili ya re-negotiation ya mikataba na Bunge kuwa na mamlaka ya kutazama mikataba na Sheria ya Sovereignty ya kuweka maliasili yetu kuwa yetu, hizi tuzimalize tupate muda wa kutosha tuje kujadili ile ambayo ni kubwa ambayo hata nimeona Mheshimiwa Musukuma anachangia sheria ambayo haipo hapa kwenye mjadala. Hizo 16% na kadhalika ziko kule siyo hapa, hizi ni statement of intents, tuzikamilishe tumalize tupate muda wa kushughulika na jambo kubwa zaidi ambalo liko kwenye Mining Act ambayo sijui itakuja lini kama ni kesho au siku gani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, la tatu ambalo napenda kuzungumzia ni je, sheria hizi mbili ni za kimapinduzi (revolutionary)? Yes. Kwa sababu gani? Kwa mara ya kwanza tumekuwa nchi ya kwanza ya kiafrika kutamka kwenye sheria kwamba chochote kilichopo chini na juu ya ardhi ya nchi yetu ni chetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni transformative? No! Kwa sababu licha ya kutamka hivyo hatujagusa mfumo wa uzalishaji. Mfumo wa uzalishaji bado ni ule ule ambao tunazungumza kwamba tunataka kuutatua. Kwa mfano, Wabunge hapa mnazungumzia umiliki wa 16% na baadaye muende mpaka 50% siyo jambo jipya. Sheria iliyopita ina umiliki, hii sheria ambayo tunataka kui-amend ina umiliki.

Mheshimiwa Naibu Spika, Sheria ya mwaka 1979 ilikuwa ina umiliki na mpaka sasa kuna migodi ya Almasi, Mwadui tunamiliki 25%, kwa hiyo siyo jambo jipya. Jambo jipya ni nini? Jambo jipya tubadilishe mfumo wa uzalishaji. Mwekezaji awe mkandarasi, awe contractor. Sisi tuna madini, unajua una mashapo kadhaa Buzwagi akija Acacia, unakubaliana naye achimbe kwa niaba yako, aondoe gharama zake, kile kinachobakia mgawane kwa makubaliano maalum, hiyo ndio transformative, hatufanyi hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hili siyo jambo jipya, tunalifanya hili kwenye mikataba ya gesi sasa hivi. Ndiyo maana hamuoni malalamiko makubwa ya kimapato kwenye gesi kwa sababu kwenye gesi mwekezaji ni mkandarasi.
Muswada wa Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi wa Mwaka 2017.
MHE. ZITTO Z. R. KABWE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa muda ambao umenipa maana uliniambia dakika saba baadaye ukasema tano, kutokana na mambo ambayo nimeyapanga kuzungumza nitaangalia yale
ambayo nitakayoweza kuzungumza na mengine labda nitaweka kwa maandishi.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la kwanza ambalo napenda nilizungumze ni nasaha tu kwa Bunge. Kazi ambayo tunaifanya hapa ni kubwa sana lakini aina ya mjadala yaani quality of debate ambayo tunayo hailingani na uzito wa jambo ambalo tunalifanya hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, napenda kuwasihi Wabunge wa pande zote mbili, bahati nzuri nina hiyo moral authority maana pande zote mbili mimi niko mwenyewe, mwenzangu naona wewe uko UKAWA. Kwa hiyo, nawasihi tufanye jambo hili kwa utulivu ili tuweze kutunga sheria ambayo itakuwa na manufaa kwa nchi. Hii kubishana, kurushiana maneno na kadhalika yanatupotezea muda muhimu sana sisi kama nchi kuweza kufanya kazi hiyo kwa pamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, kwa ujumla hii seti ina sheria tatu. Sheria moja ndiyo kubwa sana ile ya mabadiliko ya The Mining Act, kwa hiyo, tunaweza tukahitaji muda wa kutosha sana kule. Sheria mbili hizi, hii ya re- negotiation na hii ya sovereignty ni statements of intent. Ni mambo ambayo tulipaswa tuyafanye toka mwaka 1962, hatujafanya. Kwa hiyo, tunakuja hapa kwa ajili ya ku-correct hayo makosa ambayo tumeyafanya huko nyuma. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nadhani hizi sheria mbili ya re-negotiation ya mikataba na Bunge kuwa na mamlaka ya kutazama mikataba na Sheria ya Sovereignty ya kuweka maliasili yetu kuwa yetu, hizi tuzimalize tupate muda wa kutosha tuje kujadili ile ambayo ni kubwa ambayo hata nimeona Mheshimiwa Musukuma anachangia sheria ambayo haipo hapa kwenye mjadala. Hizo 16% na kadhalika ziko kule siyo hapa, hizi ni statement of intents, tuzikamilishe tumalize tupate muda wa kushughulika na jambo kubwa zaidi ambalo liko kwenye Mining Act ambayo sijui itakuja lini kama ni kesho au siku gani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, la tatu ambalo napenda kuzungumzia ni je, sheria hizi mbili ni za kimapinduzi (revolutionary)? Yes. Kwa sababu gani? Kwa mara ya kwanza tumekuwa nchi ya kwanza ya kiafrika kutamka kwenye sheria kwamba chochote kilichopo chini na juu ya ardhi ya nchi yetu ni chetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni transformative? No! Kwa sababu licha ya kutamka hivyo hatujagusa mfumo wa uzalishaji. Mfumo wa uzalishaji bado ni ule ule ambao tunazungumza kwamba tunataka kuutatua. Kwa mfano, Wabunge hapa mnazungumzia umiliki wa 16% na baadaye muende mpaka 50% siyo jambo jipya. Sheria iliyopita ina umiliki, hii sheria ambayo tunataka kui-amend ina umiliki.

Mheshimiwa Naibu Spika, Sheria ya mwaka 1979 ilikuwa ina umiliki na mpaka sasa kuna migodi ya Almasi, Mwadui tunamiliki 25%, kwa hiyo siyo jambo jipya. Jambo jipya ni nini? Jambo jipya tubadilishe mfumo wa uzalishaji. Mwekezaji awe mkandarasi, awe contractor. Sisi tuna madini, unajua una mashapo kadhaa Buzwagi akija Acacia, unakubaliana naye achimbe kwa niaba yako, aondoe gharama zake, kile kinachobakia mgawane kwa makubaliano maalum, hiyo ndio transformative, hatufanyi hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hili siyo jambo jipya, tunalifanya hili kwenye mikataba ya gesi sasa hivi. Ndiyo maana hamuoni malalamiko makubwa ya kimapato kwenye gesi kwa sababu kwenye gesi mwekezaji ni mkandarasi.
Muswada wa Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma wa Mwaka 2017
MHE. ZITTO Z. R. KABWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia muswada huu muhimu sana. Nadhani katika mambo ambayo tunaweza tukasema kwamba tumeyafanya katika Bunge hili la Kumi na Moja ni pamoja na muswada huu kwa sababu ni Muswada ambao una mabadiliko makubwa sana ambayo tunakwenda kuyafanya katika mfumo mzima wa hifadhi ya jamii ya nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo moja la jumla ambalo napenda nilizungumze, ni kwamba hapa tumekaa tunazungumzia jambo la 9% tu ya work force ya Tanzania. Kwa sababu mfumo wetu wa hifadhi ya jamii katika nchi yetu unagusia watu tu ambao wameajiriwa katika sekta rasmi ambao ni watu 2,100,000. Watu 700,000 walioajiriwa na Serikali na Mashirika yake na watu 1,400,000 ambao wameajiriwa na sekta binafsi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kuna haja huko siku za usoni tunakokwenda tujaribu kuona ni namna gani ambavyo tutakuwa na utekelezaji wa kisera na kisheria katika hifadhi ya jamii ili tuweze kuwafikia Watanzania wengi zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii napenda kutoa mfano huu sana kwa watu wa korosho. Leo hii korosho ine bei nzuri sana na wananchi wamepata fedha nyingi sana, lakini kesho na keshokutwa bei ya Soko la Dunia ikiporomoka, watu watalia kwa sababu hatuna mfumo wa hifadhi ya jamii kwa wakulima ambapo tungeweza kuwapa wakulima fao la bei pale ambapo bei zimekuwa zimetetereka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo jambo la msingi sana ambalo ni lazima tulitazame lazima tuondoke kuzungumzia 9% ya watu, tuje kuzungumzia Watanzania wengi zaidi ambao hawaguswi kabisa na schemes za hifadhi ya jamii ambazo tunazo katika nchi yetu hivi sasa

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili ambalo napenda kulizungumzia, limegusiwa kidogo na Mheshimiwa Masele, Mbunge wa Shinyanga Mjini kuhusiana na SHIB (Fao la Matibabu). Katika sheria hii mpya kuna hiyo provision ya sickness benefit ambayo ndani ya sheria haijaelezwa inakuwa namna gan? Kwa sababu ni miongoni mwa vifungu viwili
ambavyo Serikali inasema Waziri na SSRA watavitolea ufafanuzi wakati mafao mengine yote ndani ya sheria yamewekewa ufafanuzi wa namna gani ambavyo itatekelezwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kustaajabisha kidogo, ukienda kwenye consequential amendments ambazo Serikali inazo ndani ya muswada huu, section 97, Serikali inafanya amendment ya Sheria ya NSSF. Sheria ya NSSF section 21 inatoa health insurance benefit kwa wanachama wa NSSF. Sheria hii ambayo Serikali inaileta hapa, inaondoa health insurance benefit kwa wanachama wa NSSF. Hili ni jambo la hatari, kwa sababu sasa hivi NSSF ina zaidi ya wanachama 600,000. Kwa hiyo, Serikali hii inakwenda kutunga sheria kuwaondoa watu 600,000 kwenye takwa la kisheria la health insurance. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naelewa mkanganyiko ambao Serikali imeupata kwamba inataka health insurance zote ziwe provided for na NHIF, inaeleweka. Tunachopaswa kukifanya kwenye sheria ni kuweka provision inayosema kwamba fao hilo la health insurance litatolewa na NHIF, kwa NSSF kuchukua ile michango ambayo imefanyiwa mahesabu na actuarial kwamba ni percent ngapi ya michango ambayo inalipia health insurance, michango ile ipelekwe NHIF.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ukiwa na kadi ya NSSF wewe ni mwanachama wa NSSF, automatically unakuwa mwanachama wa NHIF. Hii ndiyo njia bora zaidi ambayo Serikali ilipaswa kufanya na inapaswa kufanya. Nawashauri Waheshimiwa Wabunge, kama amendment hii haitaletwa, tusiipitishe sheria hii kwa sababu tunakwenda kuwaondoa watu 600,000 kutoka kwenye health insurance. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo moja tu ambalo ni vizuri pia Serikali ifahamu kufuatia hoja ambayo Mheshimiwa Bilago, Mbunge wa Kakonko amezungumza kwamba tunapotunga Sheria za Pensheni, wale ambao tayari wanafaidika na sheria sasa hivi, hawapaswi kufanywa kuwa worse off. Wale wapya ambao wanaingia wakati sheria inatungwa, ndio wanapaswa kuendana na yale masharti mapya. Kwa hiyo, ni muhimu sana jambo hili liweze kueleweka vizuri ili tusiweze kuwafanya watu wetu kuwa katika hali mbaya zaidi badala ya kuwaboresha zaidi. (Makofi)

Jambo la mwisho na ambalo limezungumzwa na Msemaji wa Kambi ya Upinzani, ni jambo ambalo sisi kama Taifa ni lazima tuli-face, hatuna namna ya kulikwepa kama ambavyo tumelikwepa kwa miaka minne iliyopita, ni hiki kinachoitwa fao la kujitoa au kujitoa kwenye mafao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huko nje vijana wengi sana wanataka fao hili liwepo kwamba hiyo ni innovation ambayo ipo Tanzania. Inaeleweka kabisa dhamira ya Serikali yoyote, dhamira ya dola yoyote ni kujenga mazingira ambayo una mfumo madhubuti wa hifadhi ya jamii. Mfumo ambao hautakufanya baadaye uwe na wazee ambao hawana pension. Lazima ujenga hayo mazingira. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekuja na innovation ya unemployment benefit. Tumeijadili sana hii kwenye Kamati na Serikali imeongeza kifungu cha 35 kuifafanua. Maelezo ambayo Serikali imetupa ya kwamba wafanyakazi ambao wanatoka kwenye mafao, ambao wamekosa kazi walipwe asilimia 33 ya mshahara kwa muda wa miezi sita. Baada ya miezi sita fedha ile inayobakia iingie kwenye supplementary scheme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hayo ndiyo maelezo ambayo Serikali imeyaeleza kwenye Kamati, haijayaweka kwenye sheria kama mafao mengine namna ambavyo yamefafanuliwa kwenye sheria, ila ndiyo maelezo ambayo tumepewa na masharti yamewekwa kwenye section 35. Mimi nadhani tulitazame hili jambo vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inalazimisha Mwajiri kuchangia asilimia 10 ya mshahara wa mfanyakazi kwenye mfuko…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2018
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia Muswada huu wa Fedha na nina mambo matatu tu. Nina suala la Treasury Single Account kama jinsi linavyopendekezwa, suala la kodi kwenye maji kama ambavyo Kamati ya Bajeti inavyopendekeza na nina suala la Sheria ya Korosho. Naomba nianze na hili la Sheria ya Korosho.

Mheshimiwa Spika, kwanza naomba Bunge lako Tukufu lifahamu, kwamba hakuna zao lingine lolote Tanzania lina Export Levy. Naomba hili lieleweke vizuri, kwa sababu inaonekana kama kuna misinformation ambayo inasambaa ili ionekane kwamba watu wa korosho wanahitaji special treatment.

Mheshimiwa Spika, sasa hivi nimetoka kusoma kwenye tovuti ya TRA, inasema exports are free of duty and taxes except for three items; raw hides and skins, raw cashewnuts and these are wet blue hides and skins na wameweka charge zao pale. Kwa hiyo, naomba hili liwe very clear.

Mheshimiwa Spika, Tanzania hii ni zao moja tu lina Export Levy. Pamba haina Export Levy, kahawa haina Export Levy, chai haina Export Levy na tumbaku haina Export Levy. Soma Tobacco Industry Act, Cotton Industry Act, Tea Industry Act, Coffee Industry Act. So, naomba hili liwe very clear. Why Korosho Export Levy? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hii kodi imeanzishwa na Wadau wa Korosho wenyewe. Hii kodi haikuanzishwa na Serikali. Wadau wa Korosho walikaa wakaamua kwenye Mkutano wao kwamba tunataka tuongeze thamani ya korosho humu ndani. Tufanyeje Serikali haina hela? Wakakubaliana na exporters. Ninyi exporters lipeni, walianzia 3%, sasa hivi imefika 15%. Ndiyo ule msingi wa kesi ambayo Mheshimiwa Attorney General aliizungumza hapa na kuli-mislead Bunge kabisa. Mimi namheshimu sana, nimesoma naye Chuo Kikuu, nilikuwa naye Human Rights Association ya Chuo Kikuu. Nimeshangaa sana.

Mheshimiwa Spika, kesi ile ilikuwa inahusu Bodi ya Korosho na hao wadau wa korosho. Wadau wenyewe ndio walioanzisha hii, wakaja kutuomba Bungeni mwaka 2010 tulikaa wewe ukiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maliaslili na Utalii. Mmoja wa watu tulikaa nao kwenye kikao kikiongozwa na Marehemu Abdallah Kigoda, ni Mheshimiwa Waziri wa Utawala Bora yuko hapa. Wameomba wenyewe, jamani tutozeni hii kodi ili tuendeleze sekta.

Mheshimiwa Spika, sasa Serikali wanataka nini? Ndiyo maana watu wa pamba hawana, hawakuomba; tumbaku hawana, hawakuomba; na chai hawana, hawakuomba. Hivi hatuoni aibu! Watu wameomba wenyewe watozwe ili waendeleze zao lao, halafu sisi tunasema aah, tunazichukua zote asilimia 100, haiwezekani. Ni ubinadamu tu, tusiwe wakatili jamani. Kwa nini tuwe katili kwa jambo ambalo watu wameomba wenyewe? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali zuri sana. Hicho ndicho ambacho Section 17A ilikijibu kufuatia hukumu ya Mahakama. Kwa sababu katika mazao yote, Bodi zimepewa powers za kuweka regulations za makusanyo. Kukawa na mgogoro kati ya Bodi na Trust Fund. Trust Fund ikaenda Serikalini ikaomba, TRA wakauliza hivyo hivyo. Ndiyo Trust Fund ikasema, basi ninyi mtachukua 35%.

Mheshimiwa Spika, ndiyo maana hili ndiyo zao pekee lina Export Levy. Kwa nini hamna kwenye pamba, hatuuzi pamba ghafi nje? Kwa nini hamna kwenye kahawa, hatuuzi kahawa ghafi nje? Kwa nini hamna kwenye chai, hatuuzi chai ghafi nje? The genesis of this matter ni kwamba wameomba wadau. Wakaiomba TRA iwe Wakala wao na wanamlipa TRA asilimia 35. Hii ndiyo hali halisi ya jambo hili.

Mheshimiwa Spika, naomba niendelee na hoja zangu za mwisho. Sasa nakuja na suala la Treasury Single Account. Wazo la Treasury Single Account ni wazo zuri sana. Nimeshiriki kwa ruhusa yako kwenye Kamati ya Bajeti na tumelijadili, ni wazo zuri sana, lakini lina jambo la Kikatiba. Treasury Single Account ina jambo la Kikatiba; na tukifanya makosa tukaipitisha leo, Bunge hili litakuwa linakwenda kuvunja Katiba. Section 136 ya Katiba inaelezea namna ambavyo Mheshimiwa Spika, Section 136(1)(b). Inaelezea namna ambavyo matumizi yanaidhinishwa na Bunge. Naombeni ile tuliyopitisha juzi, Appropriation Act. Hii Appropriation Act ndiyo ambayo inakuwa referred to na Section 136(b) ya Katiba.

Mheshimiwa Spika, tukishatimiza wajibu wetu, tumepitisha Appropriation Act. Pendekezo la Serikali linataka moja, fedha ambazo sisi hatuhusiki nazo, un-voted ziingie Mfuko Mkuu wa Serikali, hazitajwi na Katiba. Hatuhusiki nazo, hazimo kwenye Appropriation Act.

Mheshimiwa Spika, nenda Section 143(2) kuhusiana na namna ambavyo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali anapaswa kuwa, ni kwamba fedha zote zinazotoka Mfuko Mkuu wa Hazina kwenda kwenye mafungu ambayo Bunge limepitisha Appropriation Act, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali anaidhinisha. (Makofi)

Serikali inataka ichukue fedha ambazo ziko Mfuko Mkuu wa Hazina iziiingize kwenye Treasury Single Account halafu ndiyo iende ikazigawe. Huwezi kufanya hivyo bila ku-ammend Public Audit Act ili sasa impe mamlaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ku-approve fedha zinazotoka Mfuko Mkuu wa Hazina kwa ujumla wake bila Appropriation Act, halafu wakati mnazitoa kutoka Treasury Single Account kwenda kwenye mafungu aweze kuzi- approve kwa kupitia Appropriation Act. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pendekezo hili la Serikali linamfanya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuwa redundant. Ataona 32 trillion kwa ujumla wake kuingia Mfuko Mkuu ile TSA…

T A A R I F A . . .

KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Spika, kubwa sana na naomba radhi kwa Wabunge wengine wapya. Wabunge wapya wawe wanapata semina sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa Wabunge wazoefu wanajua, unapoleta Finance Act unaingiza na sheria nyingine ambazo hazihusiani kabisa na fedha na ndiyo kama Cashewnut Industry na mengine yote ambayo tunafanya. Ni rafiki yangu, nitakaa naye pembeni nitamwelewesha kwa sababu pia amesoma maeneo ambayo siyo… (Makofi/Kicheko)

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Spika, ndiyo maana Kamati ya Bajeti imeomba jambo hili lipewe muda zaidi. Hiyo amendment ambayo imeletwa na Serikali, yaani haina hata maana, kwa sababu wanasema ni un-spent funds. Haina hata maana. Ukisoma Taarifa ya Kamati ya Bajeti ndiyo maana tuliiomba hii Taarifa mapema, watakuonesha, kwenye Bank of Tanzania Act kuna other sections, section 35, 36 ambazo bado zina-refer unvoted revenue ambapo ilipaswa zifanyiwe amendment.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, huwezi kuwa na TSA leo, hujafanya amendment ya Public Audit Act. Hamna kwenye hii sheria. Huwezi kuwa na TSA leo hujafanya amendment ya Katiba yetu kwa ajili ya ku-widen mamlaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuwatazama. Mnaweza mkaamua, mkaipitisha, mkaweka tarehe na mapendekezo tarehe 30 Septemba ni karibu mno. Toeni miezi sita, mwaka mmoja ili kipindi hiki cha katikati matayarisho hayo yaweze kufanyika. Kwa sababu hili jambo ni zuri, lakini lina mambo ambayo hayajafanyiwa kazi, Public Audit Act lazima iwe amended, Bank of Tanzania Act inapaswa kuwa amended in totality kwa mujibu wa Kamati. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nimalize. Hili la maji wengine wataliongea.

Waheshimiwa Wabunge wenzangu, sisi humu kama Bunge, wanaotufanyia kazi ni Kamati za Bunge ambazo Mheshimiwa Spika ameziunda, ndiyo wanaokaa mpaka saa nane usiku kufanya analysis. Kamati inapoleta taarifa yake ndani ya Bunge, wewe ukai-reject Taarifa ya Kamati, umelikataa Bunge.

Mheshimiwa Spika, naomba hili jambo kwa mara nyingine uwape Semina Waheshimiwa Wabunge. Kamati ndiyo Bunge, zinafanya kazi kwa niaba yetu. Kama Kamati ya Bajeti imeleta mapendekezo, imeyafanyia kazi, imeita watu, imeita watafiti, watu wamekaa mpaka saa nane usiku, ikaingia humu ndani mkai-disregard, sijui tutakuwa ni Bunge la namba gani.

Mheshimiwa Spika, ahsante.
Muswada wa Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira wa Mwaka 2018
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nina maeneo machache ambayo ningependa kuchangia kwenye Muswada huu na mengine nimeshachangia kwa maandishi kwa ajili ya Serikali kuweza kuyafanyia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza ni Kifungu cha 32(2), ambacho kinaainisha taasisi mbalimbali ambazo Muswada unaruhusu ziweze kuundwa kwa ajili ya kuendesha miradi ya maji katika maeneo ya vijijini na zimetajwa (a) mpaka (f). Ushauri wangu ni kwamba, jambo hili tulitazame vizuri kwa sababu kwenye sera tuna Jumuiya za Watumiaji Maji (COWSOs) na nadhani ingekuwa ni vizuri zaidi Muswada huu ungeimarisha ushirika wa watu wanaotumia maji na baadaye ukaruhusu kama kuna makubaliano kati ya wananchi na sekta binafsi, basi na nitakuja kutoa mapendekezo hapo mbele ule Wakala wa Maji Vijijini ufanye usimamizi wa hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mapendekezo yangu ni kwamba, ile (a) Water Consumer Association (b) Water Trust (d) Non Government Organisation (e) A Company; ziondolewe na badala yake ile (a) iwe ni Water Users Association tuweze kuweka zile COWSOs na ibakie na cooperative na nitakuja kueleza huko mbele kwenye vifungu ni kwa nini napendekeza hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, ni suala zima na hiyo inajengewa hoja kwa nguvu zaidi na Ibara hiyo hiyo ya 32 pale inaposema: “Not withstanding the provisions of Section 32(3) and Section 33(1), where a water scheme operated or to be operated by a community organization is developed through grant, donation, whatever, such scheme shall be public.” Kwa hiyo, inaenda kujibu hoja ambayo nimeisema hapo mwanzo for it to be public inabidi tuimarishe zaidi ushirika wa watumiaji maji halafu baadaye tutaweza kuona ni namna gani ambavyo sekta binafsi itapaswa kushiriki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na pia hiyo inaimarishwa zaidi na ibara ya 36 ambapo inazungumzia sasa namna gani ambayo RUWA na nimeambiwa kwamba, Kamati imerekebisha iitwe RUWASA itakavyoingia, kwamba, katika ngazi za chini za wananchi kule hizi cooperatives ziwe ni kama primary cooperatives na pale ambapo itahitajika ziunganishwe pamoja ziwe ni kama cooperative union kwamba, ni umbrella kwa ajili ya kupata ile scale na kadhalika kama ambavyo imeelezwa kwenye Muswada.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo ningependa Serikali ilitazame kwenye account and audit of community organisations; sasa kwa mujibu wa Kifungu cha 40(1): “The accounts of community organisations shall be audited in accordance with a Public Audit Act.” Ukienda kuitazama Public Audit Act unaona kwamba, imeainisha majukumu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali katika kukagua taasisi mbalimbali. Iwapo tutampa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu kazi ya kwenda kukagua vikundi vya watumiaji maji kule vijijini ni kazi ambayo hataiweza kabisa, ni kazi kubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ushauri wangu ni kwamba, kama tutakuwa tumekubali kuweka ushirika na kuweka zile COWSOs, then tuna kitu kinaitwa COASCO ambayo ni Shirika la Ukaguzi wa Ushirika. Kwa hiyo, COASCO ingeweza sasa kuifanya hii kazi ambayo Section 40 imeiainisha kwa hiyo, naomba hilo eneo pia, Serikali ilitazame na kulifanyia maboresho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Section 43 inazungumzia majukumu mbalimbali ya RUWASA. Napendekeza kwamba, tuongeze kwamba, RUWASA itakuwa ni mtekelezaji, yaani implementor wa Sera ya Maji Vijijini ili tuwe na chombo kimoja ambacho ndio kinaangalia overall implementation ya hiyo sera ya maji vijijini kwa sababu, naona hapa wameangalia zaidi miradi tu na sio kuangalia sera kwa upana wake. Jambo la msingi kabisa ni kwamba, tunahitaji huu Wakala ufanye kazi ya kusuluhisha migogoro ya kimikataba kati ya Community Water Users Associations na sekta binafsi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, kama kwenye kijiji wananchi wameamua kuwa na mradi wao, lakini wameingia PPP na sekta binafsi, sekta binafsi kuendesha ule mradi, Mkataba ule wa uendeshaji wa ule mradi kati ya wananchi na kampuni binafsi ni vema arbiter wa hiyo mikataba awe ni RUWASA. Kwa hiyo, napendekeza kazi hiyo pia, iweze kutazamwa kwa sababu, tusipoweka hivyo tutapata matatizo makubwa sana huko mbele kwenye utekelezaji; kutakuwa na mambo ya kwenda Mahakamani wananchi wetu vijijini huko hawatakuwa na uwezo wa kwenda Mahakamani wanapokuwa wamepishana na kampuni binafsi ambazo zitakuwa zinatoa huduma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kifungu cha 49 na nimeona kuna ammendment ya Mheshimiwa Anthony Komu, naiomba Serikali ilitazame kwa uzito wake. Hii ni muhimu sana kwa Waheshimiwa Wabunge wote kwamba, kifungu hiki kinaeleza obligation ya RUWASA kupeleka taarifa kwenye mamlaka za mkoa, kama RCC it is fine, lakini katika ngazi za wilaya wameweka ni District Administrative Forums. Hili haliwezekani kwa sababu, wenye watu ni Mabaraza ya Madiwani. Mabaraza ya Madiwani ni lazima wawe wanapokea taarifa hizi kila mwaka za utekelezaji wa miradi ya maji kwenye Halmashauri zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, napendekeza kwamba, ni muhimu ile ammendment ambayo imeletwa na Mheshimiwa Anthony Komu, Serikali iweze kuitazama ili kuondoa neno District Consultative Councils na badala yake kuweka Local Government Authorities na kama ikiwezekana kabisa waweke Mabaraza ya Madiwani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo ningependa tulitazame kwa makini ni hili eneo la National Water Funds. Mheshimiwa Mwenyekiti na Wabunge wote wanajua kwamba, sehemu kubwa ya umaskini ambao Watanzania wanao umeshikwa na mtego wa maji. Watu wa Vijijini wanatumia gharama kubwa sana kupata maji, wastani sasa hivi na Kambi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Bobali ameeleza hapa mfano wa kule Newala, wastani wa nchi nzima mwananchi wa kijijini ananunua pipa la maji kwa Sh.7,000 anatumia asilimia 16 ya kipato chake cha mwaka kwa ajili ya maji. Mwananchi wa mjini ananunua pipa moja la maji shilingi 300.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hebu tutazame hiyo; mwananchi wa kijijini pipa la maji ananunua kwa shilingi 7,000, mwananchi wa mjini pipa la maji ananunua kwa shilingi 300, asilimia 16 ya kipato cha mtu wa kijijini anakitumia kwa ajili ya maji tu wakati mtu wa mjini anatumia asilimia moja tu. Kwa hiyo, maji ni mtego wa umasikini. Kwa hiyo, napenda nikubaliane na maoni ambayo Kamati na Kambi ya Upinzani wameeleza kwamba, hii National Water Fund iwe restricted kwa ajili ya maji vijijini tu, 100 percent ya resources za National Water Fund ziende vijijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi kwa taarifa ambazo nimeelezwa na Wajumbe wa Kamati ya Kilimo na Maji, 70 percent ya hizi fedha zinakwenda kwenye Mamlaka za Maji Mijini. Watu wa mijini ambao wanatumia maji kwa gharama nafuu zaidi ndio wanapewa resources nyingi zaidi kuliko watu wa vijijini ambao gharama za maji kwao ni kubwa sana. Kwa hiyo, naomba eneo hilo litazamwe ili tuweze kuimarisha watu wetu wa vijijini zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo hayo, naomba nichukue fursa hii kuomba maoni ambayo yametolewa na Kambi ya Upinzani Bungeni yaweze kuzingatiwa katika hali nzima ya kuweza kuona ni namna gani ambavyo RUWASA itaweza kufanya kazi zake, lakini pia tuweze kuona ni namna gani ambavyo Mabaraza ya Madiwani yataweza kushiriki katika mfumo mzima huu ili tuweze kuwaondoa wananchi wetu katika mtego huu wa umaskini, mtego wa kutokupatikana kwa maji safi na salama. Hali ya umaskini inazidi kuwa mbaya, lakini sehemu kubwa ya umaskini inasababishwa na watu kutokuwa na maji safi na salama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. (Makofi)
Sheria ya Fedha ya Mwaka 2019
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, leo tunakamilisha kazi ambayo tumeifanya kwa takribani miezi au siku 50 za kazi lakini tuko hapa zaidi ya takriban miezi mitatu ambapo mapato yote ambayo tumeainisha kwenye volume one revenue estimates, sasa tunayatungia sheria of course bado kuna mapato ambayo sijayaona addendum ikiwa imekuja hapa ya vitambulisho vya Wamachinga ambayo bado hayajaweza kuoneshwa hasa kwenye taarifa hii ya mapato ya Serikali, mapato hayo yameelekezwa wapi, naamini kwamba by kesho wakati tunapitisha kwa sababu Sheria ya Fedha ndio hasa inaenda ku-effect revenue book ambayo tulipewa hapa, kwa hiyo naamini kwamba addendum itaweza kuja.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna sehemu moja ya mapato ambayo kikawaida hatuioni kwenye Finance Act lakini tunakuwa tumeipitisha na hatuioni kwa sababu haionekani kama ni kodi na hii ni eneo hasa la mikopo. Katika eneo hili ningependa tuangalie uwezekano wa Finance Bill zinazokuja tuwe tunaweka katika Finance Act kwa sababu ya kuweza kutoa ruhusa ya kisheria kwa Serikali yaani Bunge kutoa ruhusa ya kisheria kwa Serikali kuweza kwenda kukopa ili tuwe tunaweka ukomo wa mikopo ambayo Serikali inakwenda kuchukua hasa mikopo ya nje ambayo inakuja kujenga na kuongeza deni la Taifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano, mwaka huu tunatarajia kukopa kwa mujibu wa mfumo wa bajeti, sura ya bajeti ya mwaka 2019/2020 jumla ya shilingi trilioni 2.3 kama mikopo ya kibiashara. Ukitazama kwenye ukurasa wa 104 wa Hotuba ya Bajeti tunakuta kwamba mikopo yenye masharti ya kibiashara tunakwenda kukopa jumla ya shilingi trilioni 2.3, lakini sasa ukiangalia kwa mfano Serikali sasa hivi inahangaika kutafuta mikopo kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo. Kwa mfano, Mheshimiwa Waziri wa Fedha na timu yake walipokuwa kule DC Washington kwenye mkutano wa majira ya kipupwe ya mikutano ya Bretton Wood Institutions walikutana na watu wa Benki ya Standard Chartered kwa ajili ya kuomba mkopo wa dola za Kimarekani bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kati, kipande cha kuanzia Morogoro mpaka Dodoma na baadaye kwenda mpaka Isaka.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tunaenda kukopa fedha hizi kwa ajili ya reli hii, lakini reli hii ni reli ambayo inakwenda kunufaisha nchi nyingine, hainufaishi nchi yetu kwa sababu ya mwelekeo wa reli yenyewe. Nilikuwa natazama hapa namna gani ambavyo bandari zetu zinakua kwa kuongeza mizigo, nimekuta kwamba bandari ambayo ni fastest growing inayokua kuliko bandari zote katika nchi yetu ni Bandari ya Kigoma, ambayo mwaka jana imekuwa kwa asilimia 43.7. Bandari nyingine inayofuata ni Bandari ya Tanga, lakini Bandari ya Mwanza ambako ndio reli inakwenda mwaka jana imekuwa kwa negative 31.8 percent.

Mheshimiwa Naibu Spika, juzi nilishangaa Rais wa Congo alipokuja hapa nchini, Serikali ilimpeleka kuangalia SGR na alivyoenda kule wanazungumzia kuifanya Rwanda kuwa Logistic hub, SGR iende mpaka Rwanda, Congo waende kuchukua mizigo Rwanda, maana yake ni kwamba tunaiua Tanzania, tunaiua Bandari ya Kigoma na Bandari ya Kigoma itakuwa haina maana yoyote, nami hili naona ni uhujumu kwa nchi yetu na jambo hili linapaswa kuzuiwa. Njia pekee ya kulizuia jambo hili ni kuhakikisha kwamba mikopo ambayo tunakwenda kukopa huko nje kujenga reli kwa ajili ya kupeleka kwenye nchi nyingine, Bunge likatae ili lielekeze mikopo ambayo inakusanywa iende sehemu ambayo italeta maendeleo kwa ajili ya nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili ambalo nilipenda kulizungumza, kuna mazungumzo hapa kuhusiana na suala zima la pamba ni dhahiri kwamba Waheshimiwa Wabunge wana wasiwasi kwamba tunaenda kupata matatizo ambayo tuliyapata kwenye zao la korosho na Waheshimiwa Wabunge wamezungumza kwa undani sana namna gani ambapo tunaweza tukatatua tatizo hili na mimi sina haja ya kurudia eneo hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo moja tu ambalo naomba niwakumbushe na naiomba Serikali ilichukue kama wazo, kuna haja kubwa kwamba haiwezekani kila mwaka tunakuja hapa Bungeni tunalalamika kuhusu kuporomoka kwa bei ya mazao na namna gani ya kuwalipa wakulima. Mwaka jana tulikuwa na mgogoro mkubwa wa korosho haujakwisha, mpaka leo mmesikia mijadala kuhusu korosho. Mwaka huu sasa tuna mgogoro wa pamba ambapo bei iliyotangazwa na Serikali na bei ya soko la dunia haviendani. Sasa napendekeza kwamba, Serikali ilete Muswada wa Sheria wa kuunda Mfuko wa Price Stabilization ili kuweza kuhakikisha kwamba tunakuwa tunachanga change kidogokidogo, bei za soko la dunia zikiporomoka tuweze kuwafidia wakulima kiwango kile ambacho kimeporomoka na hatutakuwa tena na mgogoro wa bei za mazao yetu ya kilimo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo naomba Serikali ichukue wazo hili, tumekuwa tukilizungumza mara kwa mara iende ikalifanyie kazi na mfumo ambao unaweza kusaidia hili ni kuanzisha mfumo wa hifadhi ya jamii kwa wakulima ambapo ndani yake kunakuwa na fao la bei ambalo linaweza likatatua matatizo kama haya ambayo tunayapata kwenye pamba sasa hivi na tuliyapata mwaka jana kwenye korosho. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja yangu ya mwisho inahusiana na mapendekezo ambayo Serikali iliyaleta kuhusu sanitary pads. Serikali imeeleza hatua mbalimbali ambazo imechukua, Kamati ya Bajeti na napenda niipongeze sana Kamati ya Bajeti imezungumza na Serikali na Serikali imeweza kuongeza makampuni ambayo yatapata ile nafuu ya kodi ya mapato ya miaka miwili kwamba ni makampuni ambayo yapo hivi sasa na makampuni yatakayoanzishwa hapo baadaye.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, wakati tunazungumza hapa Serikali ilitueleza na ni hoja ambayo Mheshimiwa Bashe pia ameizungumza kwamba kuna duty remission ambayo imekuwepo toka mwaka 2009, miaka 10 ambapo uingizaji wa raw materials, malighafi za kuzalisha sanitary pads hapa nchini kodi yake ya ushuru wa forodha ni asilimia sifuri na kwenye Kamati ya Bajeti Serikali imetuletea ushahidi wa namna gani ambavyo hilo limekuwa likitekelezwa na hapa nina orodha ya makampuni ya Tanzania ambayo yanafaidika na nafuu hiyo na ni makampuni mawili tu sitaki kuyataja kwa majina kutokana na daftari la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mheshimiwa Naibu Spika, hii inaonesha nini? Hii inaonesha kwamba Serikali inashindwa kutimiza wajibu wake wa kuwaelewesha Watanzania nafuu gani ambazo zipo zinaweza zikatekelezwa ili kuweza kuhakikisha kwamba bei ya sanitary pad inapungua na ndio maana mpaka baada ya Serikali kubanwa sana ndio tumeweza kufahamu kwamba kuna duty remission hii ambayo ingeweza kusaidia, Serikali ingeieleza toka mwaka jana, Serikali ingechukua hatua za kueleza wadau wote katika sekta, leo hii pengine tungekuwa tunajadili masuala mengine kuhusiana na suala la sanitary pads.

Naitaka Serikali ihakikishe kwamba hii nafuu inafahamika kwa wazalishaji kwa sababu ni nafuu ambayo ni kubwa, ni nafuu ambayo ingefahamika toka mwaka jana inawezekana leo tusingekuwa na kelele ambazo tunazo mpaka hivi sasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, naomba niombe Serikali iendelee kufikiria wazo ambalo Kamati ya Bajeti imelitoa la kuona ni namna gani ambavyo VAT katika bidhaa hizi muhimu na sio kwa wanawake peke yake na hata kwa watoto zile diapers waziwekee zero rating kwa bidhaa zinazozalishwa ndani na bidhaa zinazozalishwa nje, ukichukua measures zote hizi ya import duty ya zero rating na hatua za kiutawala za bei elekezi, nina hakika kabisa kwamba tutaweza kuuza au wananchi wetu wataweza kununua sanitary pads kwa chini ya Sh.1,500/=, inawezekana inahitajika Serikali itmize wajibu wake, wajibu wa kuongoza na sio wajibu wa kutawala.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. (Makofi)