Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Hafidh Ali Tahir

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dimani

Primary Question

MHE. ALI HAFIDH TAHIR aliuliza:- Rais wa Tanzania wa Awamu ya Nne, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Kikwete wakati akitembelea Kijiji cha Kichako Punda Uwandani katika Shehia ya Maungani Jimbo la Dimani tarehe 25 Januari, 2008 aliahidi ujenzi wa Kituo cha Afya kwa wananchi wa Kichaka Punda Uwandani pamoja na kuweka umeme na maji kutoka Kijiji cha Jitimai hadi Skuli. (a) Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi hizo za muda mrefu? (b) Je, Serikali itakubaliana nami kuwa utekelezaji wa ahadi hizo utaongeza ari katika umoja uliopo ikiwa ni pamoja na kuimarisha Muungano?

Supplementary Question 1

MHE. ALI HAFIDH TAHIR: Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya majibu ambayo hayakuniridhisha ya Mheshimiwa Naibu Waziri, kwanza nilikuwa niseme maneno machache yafuatayo; Mheshimiwa Naibu Waziri anasema kwamba kwa sasa wananchi wa Kichaka Punda, anazungumzia kwa sasa, ahadi ambayo imewekwa na Mheshimiwa Rais aliyepita ilikuwa ni tarehe 25 Januari, 2008 na hakuna kilichofanywa, yeye anazungumzia, leo kwa sasa. Ahadi haijatekelezwa.
(a) Je, Mheshimiwa Naibu Waziri, anahakikisha kwamba Kituo cha Afya anachokuzungumzia anafahamu kwamba ni kibovu tangu tarehe 25 Januari, 2008 na hakuna marekebisho yeyote yaliyofanywa?
(b) Mheshimiwa Naibu Spika, suala la umeme kwenda Skuli ambapo Mheshimiwa Rais alimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mheshimiwa Abdallah Mwinyi na Naibu Waziri, Mheshimiwa Machano Othman, kwamba umeme huo mpaka sasa haujafika na unachokizungumzia sasa hivi ni nadharia. Utakuwa tayari mimi na wewe baada ya kikao hiki tufuatane ili ukahakikishe kwa vitendo kwamba hayo yote uliyoyazungumza siyo kweli?

Name

Luhaga Joelson Mpina

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisesa

Answer

NAIBU WAZIRI (MUUNGANO NA MAZINGIRA): Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nampongeza sana Mheshimiwa Hafidh Ali Tahir kwa jinsi ambavyo anafuatilia mahusiano ya Kimuungano na jinsi ambavyo ni Mwanamuungano wa kweli.
Mheshimiwa Naibu Spika, wakati najibu swali langu la msingi sikusema kwamba hiki Kituo cha Afya kimeshajengwa, nilisema kwamba Ofisi yangu itafuatilia kwa karibu kuhakikisha kwamba hii ahadi ya Mheshimiwa Rais, iliyotolewa inatekelezwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kusema kwamba kwa sababu sasa hivi ni kweli anazungumza jambo la tarehe 25 Januari, 2008 ambapo Mheshimiwa Rais aliahidi. Lakini tukubaliane tu kwamba leo ndiyo nalijibu swali hili na sasa tunaingia kwenye bajeti, tuhakikishe kwamba katika bajeti kwa maandalizi tunayoanza nayo sasa, hii ahadi ya Mheshimiwa Rais itatekelezwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, nakubaliana naye kabisa kwamba niko tayari, baada ya hili Bunge kwisha nitafanya ziara Zanzibar, pamoja na mambo mengine, nitaenda kuona hii ahadi ya Mheshimiwa Rais, pamoja na umeme. Kwa sababu sisi baada kuwasiliana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ndiyo ilituletea taarifa kwamba tayari umeme umeshapelekwa eneo hilo la kijiji ambacho Mheshimiwa Tahir anakizungumza hapa. Kwa hiyo, kwa mantiki hiyo basi, kama siyo kweli, basi katika ziara hiyo yatabainika hayo na hatua za kuhakikisha kwamba ni lazima ahadi ya Mheshimiwa Rais iwe imetekelezwa tutahakikisha kwamba imetekelezwa.

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Primary Question

MHE. ALI HAFIDH TAHIR aliuliza:- Rais wa Tanzania wa Awamu ya Nne, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Kikwete wakati akitembelea Kijiji cha Kichako Punda Uwandani katika Shehia ya Maungani Jimbo la Dimani tarehe 25 Januari, 2008 aliahidi ujenzi wa Kituo cha Afya kwa wananchi wa Kichaka Punda Uwandani pamoja na kuweka umeme na maji kutoka Kijiji cha Jitimai hadi Skuli. (a) Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi hizo za muda mrefu? (b) Je, Serikali itakubaliana nami kuwa utekelezaji wa ahadi hizo utaongeza ari katika umoja uliopo ikiwa ni pamoja na kuimarisha Muungano?

Supplementary Question 2

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kuniona. Kwa kuwa kulikuwa na maelekezo Serikalini kuhusu ushirikiano wa karibu kati ya Wizara za Kisekta za SMT na zile za SMZ ambayo yalikuwa yanahimiza ushirikiano wa karibu wa kitaalamu na utafiti na pale Wizara ya Maji ilikuwa imepangwa, Waziri wa Sekta ya Maji Bara na Zanzibar tarehe 8 Juni, 2014; mkutano ule ukaahirishwa kusubiri Bunge la Katiba:-
Je, kwa sasa hivi maelewano hayo yanaendeleaje kuimarishwa? Ahsante sana.

Name

January Yusuf Makamba

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bumbuli

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA): Mheshimiwa Naibu Spika, moja ya kazi ya Ofisi ya Makamu wa Rais ni kuratibu mahusiano kati ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mambo yasiyo ya Muungano. Mwezi wa kwanza tumetengeneza ratiba ya vile vikao ambavyo viliahirishwa na mambo ambayo yalibaki kufanyika katika kuhakikisha kwamba mahusiano hayo yanaimarishwa.
Kwa hiyo, moja ya kikao kilichopangwa kufanyika na ambacho tumeweka fedha kwenye bajeti ili kifanyike, ni pamoja na hicho unachoongelea Mheshimiwa Mbunge.
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda tu kuwapa faraja na taarifa wenzetu wa Zanzibar kwamba tumedhamiria kwa nguvu zote kuhakikisha kwamba Muungano wetu unaimarika katika mambo ya Muungano na yale yasiyo ya Muungano na kazi hiyo tutaifanya kwa nguvu ili kutimiza ahadi yetu kama tulivyowaahidi Watanzania. (Makofi)