Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

George Malima Lubeleje

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpwapwa

Primary Question

MHE. GEORGE M. LUBELEJE aliuliza:- Rais wa Awamu ya Nne, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliahidi kujenga barabara ya Mbande – Kongwa – Mpwapwa kwa kiwango cha lami; na barabara hiyo tayari imeshafanyiwa upembuzi yakinifu. Je, ni lini sasa Serikali itaanza kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 1

MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niulize maswali mawili ya nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali ya nyongeza.
Kwa kuwa barabara ya barabara ya Mbande - Kongwa – Mpwapwa mpaka Kibakwe ni muhimu sana kwa maendeleo na uchumi wa Wilaya ya Mpwapwa na Kongwa; na kwa kuwa barabara hii inaunganisha Majimbo matatu; Jimbo la Kongwa, Mpwapwa pamoja na Kibakwe; na kwa kuwa ni ahadi ya Rais Mstaafu, Mheshimiwa Jakaya Kikwete na ahadi ya Mheshimiwa Rais John Magufuli ambaye ni Rais wetu sasa. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri atakubaliana na mimi kwamba ipo haja sasa ya kukamilisha barabara hii kwa kujengwa kwa kiwango cha lami?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Kwa kuwa barabara ya kutoka Mpwapwa – Gulwe kwenda Berege – Mima mpaka Iwondo haipitiki, ni mbaya sana kwa sababu ya mvua zinazonyesha. Je, Mheshimiwa Waziri ana maelezo gani kuhusu wananchi wa Jimbo la Mpwapwa?

Name

Eng. Edwin Amandus Ngonyani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa swali la kwanza ni kama nilivyojibu katika swali la msingi. Sana sana ninachoomba kuongezea ni kwamba dhamira yetu kama Serikali ni kubwa sana. Tuna nia ya kutekeleza ahadi za Marais hao; na kwa kweli mara fedha zitakapopatikana tutaendelea na kipande hiki kilichobakia.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa swali la pili, Wabunge wengi ni mashahidi kwamba maeneo mengi yaliyoharibiwa na mvua zinazoendelea, vijana wetu wa TANROAD wanafanya kazi kubwa. Naomba kwa upande wa TANROAD Dodoma waliangalie eneo hili ili kile wanachokifanya katika maeneo mengine na hapa wakifanye kwa ukamilifu ili wananchi waweze kupata mawasiliano ya uhakika.