Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Risala Said Kabongo

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. RISALA S. KABONGO aliuliza:- Vijiji vya Ngiresi, Sokoni II na Oldadai Kata ya Sokoni II Jimbo la Arumeru Magharibi vinakabiliwa na tatizo la ukosefu wa maji ya bomba, kwa muda mrefu licha ya kwamba vijiji hivyo kuna vyanzo vingi vya maji na mabomba yanayopeleka maji Arusha Mjini:- (a) Je, Mamlaka ya Maji Jiji la Arusha inashindwa kutekeleza maombi ya wananchi wa vijiji hivyo ya kupatiwa maji kutoka kwenye mabomba kwa utaratibu wa kulipia? (b) Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza na kuboresha vyanzo vya maji katika Jiji la Arusha na Halmashauri zake kutokana na ongezeko kubwa la wakazi wake?

Supplementary Question 1

MHE RISALA S. KABONGO: Mheshimiwa, Naibu Spika nakushukuru. Nakushukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yako.
Kwa kuwa, mradi huu ni Mkubwa na ni wa miaka mitano; je, Serikali inavipa vipaumbele gani vijiji hivi vya Oldadai na Sokoni II na Ngilesi, kwa kuwa wamekuwa na kero kubwa na ya muda mrefu ya kupata maji?
Eneo la pili, nitaomba Mheshimiwa Waziri, atakapopata nafasi baada ya Bunge hili, aweze kutembelea maeneo haya na kujionea hali halisi katika vyanzo hivi ambavyo vinatunza maji yanayosaidia katika Mkoa wa Arusha. Ahsante. (Makofi)

Name

Eng. Gerson Hosea Lwenge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa ni kweli tumepata ufadhili wa mradi mkubwa ambao utekelezaji wake utachukua miaka mitatu. Jana tulikuwa na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, amekuja ofisini kwangu pamoja na Meya, pamoja na Mbunge na tumekubaliana kwamba, tutatengeneza mpango wa muda mfupi ili hivyo vijiji unavyovisema tuweze kuvitafutia angalau wapate maji wakati tunatekeleza huu mradi mkubwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, hivi sasa kulikuwa na Mradi wa Vijiji Kumi, tumekubaliana kwamba Jiji la Arusha litakabidhi kwenye mamlaka yetu ya Arusha ili kusudi waweze kuunganisha kwenye mtandao baadhi ya maeneo ambayo Arusha hayapati maji.
Mheshimiwa Naibu Spika, nakubaliana pia kwamba na mimi nitakuja kuangalia utekelezaji wa mpago huu. (Makofi)

Name

Joseph Leonard Haule

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Mikumi

Primary Question

MHE. RISALA S. KABONGO aliuliza:- Vijiji vya Ngiresi, Sokoni II na Oldadai Kata ya Sokoni II Jimbo la Arumeru Magharibi vinakabiliwa na tatizo la ukosefu wa maji ya bomba, kwa muda mrefu licha ya kwamba vijiji hivyo kuna vyanzo vingi vya maji na mabomba yanayopeleka maji Arusha Mjini:- (a) Je, Mamlaka ya Maji Jiji la Arusha inashindwa kutekeleza maombi ya wananchi wa vijiji hivyo ya kupatiwa maji kutoka kwenye mabomba kwa utaratibu wa kulipia? (b) Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza na kuboresha vyanzo vya maji katika Jiji la Arusha na Halmashauri zake kutokana na ongezeko kubwa la wakazi wake?

Supplementary Question 2

MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa nafasi hii. Suala la Arumeru Magharibi linafanana sana na tatizo ambalo lipo Mikumi, je, Serikali ina mpango gani wa kuondoa kero ya maji katika Kata ya Mikumi, Ruaha, Uleling’ombe na maeneo ya Tindiga?

Name

Eng. Isack Aloyce Kamwelwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Katavi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Naibu Spika na Waheshimiwa Wabunge, Mheshimiwa Waziri katika majibu yake ametoa taarifa kwamba tunaingia katika progamu ya pili kupitia sera ya mwaka 2002 ya kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2020 asilimia 85 ya Watanzania wote watakuwa wanapata maji katika vijiji na asilimia 95 katika miji.
Mheshimiwa Mbunge, kwa upande wa Jimbo lako la Mikumi na Kata zake, tutahakikisha kwamba tunazipa kipaumbele kuhakikisha zinapata maji katika hii progamu ya pili. Na ninakuomba sana baada ya Bunge hili tuwasiliane ili tuweze kupata taarifa iliyo nzuri zaidi tuanze utekelezaji.

Name

Shabani Omari Shekilindi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lushoto

Primary Question

MHE. RISALA S. KABONGO aliuliza:- Vijiji vya Ngiresi, Sokoni II na Oldadai Kata ya Sokoni II Jimbo la Arumeru Magharibi vinakabiliwa na tatizo la ukosefu wa maji ya bomba, kwa muda mrefu licha ya kwamba vijiji hivyo kuna vyanzo vingi vya maji na mabomba yanayopeleka maji Arusha Mjini:- (a) Je, Mamlaka ya Maji Jiji la Arusha inashindwa kutekeleza maombi ya wananchi wa vijiji hivyo ya kupatiwa maji kutoka kwenye mabomba kwa utaratibu wa kulipia? (b) Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza na kuboresha vyanzo vya maji katika Jiji la Arusha na Halmashauri zake kutokana na ongezeko kubwa la wakazi wake?

Supplementary Question 3

MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa kuniona. Kwa kuwa tatizo la Arumeru Mashariki linafanana kabisa na tatizo la maji la Lushoto.
Je, ni lini Serikali itaondoa adha hii kwa wananchi wa Lushoto?

Name

Eng. Isack Aloyce Kamwelwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Katavi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza Wilaya ya Lushoto mlalo wake wa ardhi ni mzuri kuruhusu ujenzi wa mabwawa. Tumeweka mpango wa kujenga mabwawa katika awamu hii ya programu ya pili ambayo yatasaidia kwenye irrigation pamoja na kuhakikisha kwamba tunapata maji ya kunywa kwa wananchi wa Jimbo lake.