Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Cecil David Mwambe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ndanda

Primary Question

MHE. CECIL D. MWAMBE (K.n.y. MHE. MWITA M. WAITARA) aliuliza:- Baadhi ya wakazi wa Ukonga wanafuga kuku wa mayai na wengine wanatengeneza chakula cha mifugo, shughuli zinazowainulia kipato na kuweza kupata mahitaji muhimu ya kimaisha, lakini shughuli zao zimeathiriwa na watu wanaoingiza mayai toka nje ya nchi:- (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kuzuia uingizaji wa mayai toka nje kwa sababu unaharibu soko la ndani la bidhaa hiyo? (b) Je, Serikali ina mpango gani wa kusimamia malighafi ili chakula cha mifugo kiendane na bei ya mayai na kuku? (c) Je, Serikali ipo tayari kusimamia wananchi walipwe fidia kutoka kwa wawekezaji wanaoingiza vifaranga wasio na chanjo toka nje ambao wengi wao hufa na kusababisha hasara kwa wananchi wafugaji?

Supplementary Question 1

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, napenda kuuliza maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kadri ya muuliza maswali, kipengele namba (c) kinasema je, Serikali ipo tayari kusimamia wananchi walipwe fidia kutoka kwa wawekezaji wanaoingiza vifaranga wasio na chanjo toka nchi za nje?
Kimsingi kwenye jibu lake haja-commit, hajasema kama Serikali sasa hivi iko tayari kuhakikisha wafugaji wale wanaopata hasara wanalipwa fidia yao, kwa hiyo tunaomba Serikali itoe neno kwenye hili. Pia itueleze kama hali ni hii basi izuie kabisa watu wasiingize vifaranga ambavyo havina chanjo.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kutokana na kuongezeka kwa gharama za uzalishaji hasa wa chakula kama alivyosema yeye mwenyewe na tumeona gharama kubwa sana kwenye chakula cha mifugo. Kwa kipindi hiki ambapo kuna tatizo kubwa la chakula na njaa, Serikali haioni sasa umefika wakati iondoe angalau kodi fulani ili kuweza ku-compensate wakulima katika kupata chakula chenye bei nafuu na wananchi waweze kununua kuku kwa bei nafuu?
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

Name

William Tate Olenasha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngorongoro

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI:
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu fidia, kimsingi suala la fidia halitokei kwa sababu kama nilivyosema kwenye jibu la msingi, kimsingi ni kinyume cha sheria na taratibu kuingiza kuku na mayai kutoka nje, kwa hiyo wale ambao
wanaingizwa kwa taratibu ambazo sio rasmi, wanaingizwa kwa utaratibu wa njia za panya. Kwa hiyo, kimsingi Serikali imeweka utaratibu kuhakikisha kwamba hairuhusu uingizwaji, hivyo kutokea na ndiyo maana tumesema tayari
katika kipindi cha miaka minne tumeteketeza vifaranga zaidi ya 67,000. Hata hivyo, tunachotaka kutoka kwa Mheshimiwa Mbunge ni kuonesha ushirikiano kama wanaweza wakatuonesha watu ambao wanaingiza vifaranga na mayai kinyume na taratibu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na gharama ya vyakula vya mifugo, hasa kuku, kama nilivyosema vilevile ni kweli kwamba kuna gharama kubwa sana katika kutengeneza vyakula vya kuku kwa sababu kiinilishe kinachotumika ni maharage ya soya ambayo hatuzalishi hapa nchini. Kwa hiyo, hatua ambazo tunazichukua ni
pamoja na kuhamasisha wananchi walime zao la soya.
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile kupitia hotuba ya bajeti ya Wizara yetu kwa ajili ya mwaka wa fedha unaokuja, Serikali imechukua hatua kadhaa kupunguza kodi na tozo za mazao na bidhaa mbalimbali ili basi vyakula vya kuku na mazao mengine viweze kupatikana kwa bei nafuu. Kwa hiyo, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba suala la kodi na tozo litashughulikiwa.