Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mwanne Ismail Mchemba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Tabora Mjini

Primary Question

MHE. MWANNE I. MCHEMBA aliuliza:- Fomu ya PF3 hutolewa na polisi tukio linapotokea na kumletea usumbufu mgonjwa kwani anatakiwa kuwa na uthibitisho wa fomu hiyo ili daktari atoe ushauri wake na pia mgonjwa hawezi kupatiwa huduma yoyote mpaka awe na fomu hiyo hata kama ana maumivu makali au hali yake ni mbaya; Je, Serikali haioni sasa umuhimu wa kufanya marekebisho ya utaratibu ili kuwaondolea usumbufu wagonjwa?

Supplementary Question 1

MHE. MWANNE I. MCHEMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Waziri kwa kuwa wananchi wengi
wamekuwa waoga kwenda kwenye kituo cha polisi hususan wanawake na kwa kuwa maeneo mengi hayana vituo vya polisi hususan vijijini. Je, Serikali iko tayari sasa kugatua madaraka kwa Wenyeviti wa Mitaa, Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji ili waweze kupata matibabu pale wanapopata ajali?

Name

Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Magharibi

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge kwa kuona uhalisia unaotokea kwenye grass root. Niseme tu tumepokea wazo hilo, itabidi tuongee na wenzetu wa TAMISEMI kwa sababu likiamuliwa kufanyika katika msingi huo kuna vitu ambavyo lazima tujiridhishe navyo na aina ya maumivu ambayo yanaweza yakatumika kwenye ngazi ya viongozi wetu wa Serikali za Vijiji.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kitu ambacho huwa tunakiepusha na kulazimisha ipitie polisi hasa ni kwa wale ambao wanaweza wakafanya makosa makubwa kwa mfano, mtu aliyeenda kuiba akawa amejeruhiwa angetamani sana asipitie polisi aende moja kwa moja hospitalini. Kwa hiyo, huwa tunaona apitie polisi na wale
wengi wanaokwepa kupitia polisi tunakuwa tunajua watakuwa wana vitu wanavyovihofia.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kwa vitu ambavyo
vimefanyika katika ngazi ya familia labda mtu amepata ajali ya kawaida katika ngazi ya familia ama katika eneo na anafahamika, ana kumbukumbu nzuri za kutokuwa na vitendo vya kihalifu ni maeneo ambayo tunaweza tukaongelea tukaenda katika taswira hiyo aliyoisemea Mheshimiwa Mbunge.