Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Rose Kamili Sukum

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ROSE K. SUKUM aliuliza:- Serikali hupeleka fedha kwenye Halmashauri baada ya kupokea mpango kazi wa maendeleo au matumizi ya kawaida kwa Halmashauri husika. Kama ikitokea fedha zaidi zimepelekwa katika Halmashauri, maana yake kuna Halmashauri imepelekewa kidogo:- (a) Je, kwa nini fedha za ziada zisirudishwe Hazina na badala yake zinaombwa kutumiwa na Halmashauri ambayo haikuwa na mahitaji nazo? (b) Je, Halmashauri ambazo zinakuwa zimepelekewa fedha kidogo zinafidiwa vipi ili kukidhi maombi ya mpango kazi wake? (c) Je, kwa Halmashauri inayotumia fedha hizo bila ya kusubiri maelekezo kama ilivyo pale inapokuwa ziada kuwekwa kwenye Akaunti ya Amana kama Memorandum ya Fedha ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa Kifungu Na. 9(2)(e) kinavyoelekeza, endapo itabainika, wanachukuliwa hatua gani?

Supplementary Question 1

MHE. ROSE K. SUKUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri wa TAMISEMI, lakini nina maswai mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Naibu Waziri amekiri kwamba Afisa Masuhuli anayetumia fedha bila idhini ya TAMISEMI au ya Hazina, hastahili kutumia hizo fedha. Je, ni kwa nini ofisi yake haikutekeleza wajibu huo kwa Maafisa Masuhuli ambao wametumia hizo fedha bila idhini yake au bila idhini ya Ofisi yake pamoja na Hazina? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wewe mwenyewe umekiri kwamba fedha endapo itabainika imeongezwa, lakini (b) yake umesema kwamba hakuna bajeti inayoidhinishwa ikazidi kupelekwa kwenye Halmashauri: sasa ni ipi tuipokee kutoka kwako endapo fedha zimeongezeka? Unasema kwamba haziongezeki, nami nina uhakika kwamba fedha zinaongezeka; sasa naomba kuuliza. Je, kwa wale ambao wameongezewa fedha na wale ambao wamepunguziwa wanafidiwaje?
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Naibu Waziri atupatie majibu ambayo yanastahili.

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema hapa kwamba kwa Afisa Masuhuli yeyote ambaye atakiuka utaratibu wa fedha, maana yake atachukuliwa hatua. Kwa sababu, Mheshimiwa Sukum hakunipa mfano halisi, lakini naomba nimhakikishie, kuna maamuzi mbalimbali ya kinidhamu tumeyachukua kwa Watendaji mbalimbali. Hata baadhi ya Wakurugenzi wengine ambao wameenda nje ya system sasa kutokuwa Wakurugenzi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hiyo ni kwa sababu mwanzo katika njia moja ama nyingine walikiuka utaratibu wa fedha na kufanya ufisadi mkubwa katika fedha hizo na ndiyo maana Serikali ilichukua hatua. Ni kwa sababu hatuwezi ku-publicize hapa kwamba nani na nani, lakini tumechukua hatua mbalimbali kwa baadhi ya Wakurugenzi ambao ni Maafisa Masuhuli, walioko katika maeneo hayo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake lingine kwamba fedha sehemu nyingine zinaongezeka na nyingine zinapungua, nimezungumza wazi, hapa kila Mbunge akisimama anazungumza kwamba fedha haziji, fedha haziji. Ndiyo nimesema, kwa uzoefu tuliokuwa nao, mara nyingi sana fedha zile tunazozipanga, ndiyo maana hata Mheshimiwa Kawambwa hapa anaomba fedha za wodi yake hazijafika. Uzoefu uliokuwepo ni kwamba fedha zinazokwenda ni chache kuliko kile kilichopangwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kunatokea na special
case kwamba kuna baadhi ya fedha zimeongezeka, ni lazima utaratibu ufuatwe kama nilivyoelekeza katika maelezo yangu ya awali, kwamba lazima atoe taarifa aidha Hazina au Ofisi ya Rais, TAMISEMI kwa Katibu Mkuu kwa ajili ya ufuatiliaji, fedha hizo zirudishwe katika Mfuko Mkuu wa Hazina.

Name

Sophia Hebron Mwakagenda

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ROSE K. SUKUM aliuliza:- Serikali hupeleka fedha kwenye Halmashauri baada ya kupokea mpango kazi wa maendeleo au matumizi ya kawaida kwa Halmashauri husika. Kama ikitokea fedha zaidi zimepelekwa katika Halmashauri, maana yake kuna Halmashauri imepelekewa kidogo:- (a) Je, kwa nini fedha za ziada zisirudishwe Hazina na badala yake zinaombwa kutumiwa na Halmashauri ambayo haikuwa na mahitaji nazo? (b) Je, Halmashauri ambazo zinakuwa zimepelekewa fedha kidogo zinafidiwa vipi ili kukidhi maombi ya mpango kazi wake? (c) Je, kwa Halmashauri inayotumia fedha hizo bila ya kusubiri maelekezo kama ilivyo pale inapokuwa ziada kuwekwa kwenye Akaunti ya Amana kama Memorandum ya Fedha ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa Kifungu Na. 9(2)(e) kinavyoelekeza, endapo itabainika, wanachukuliwa hatua gani?

Supplementary Question 2

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa kuwa, Halmashauri mara nyingi tatizo la fedha ni shida kubwa sana. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri anaweza kutuambia ni jinsi gani atahakikisha Ofisi yake inatimiza yale malengo ya fedha iliyoahidi kwenda kwenye Halmashauri?
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuhusu usimamizi, aseme
kwa kina atazisimamiaje Halmashauri zake zisifanye ufisadi kwa kuwa, imekuwa ikijirudia mara kwa mara na kutuletea matatizo katika Halmashauri zetu?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa tunazungumzia suala zima la fedha na fedha hizi zinatafutwa kwa gharama kubwa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi.
Naomba nimhakikishie, nilikuwa nikifanya ziara katika Halmashauri zote na nashukuru Mungu sasa nimebakiza chini ya Halmashauri 10 kuzipitia Tanzania nzima. Ajenda yetu ya kwanza ni suala la uadilifu katika usimamizi wa fedha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumewaambia na nimetoa maelekezo katika maeneo yote kwamba Wakurugenzi na Waweka Hazina sasa lazima wanapokwenda katika Kikao cha Kamati ya Fedha ambapo Madiwani na Wabunge ni Wajumbe hapo, lazima watoe taarifa ya transactions katika Halmashauri zao, fedha zilizopokelewa na matumizi yake yalikuwaje. Siyo kupokea lile kabrasha la mapato na matumizi ambapo Mbunge au Diwani anashindwa kujua ndani kilichokuwemo. Kwa hiyo, tumetoa maelekezo haya vya kutosha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nawaomba sana Waheshimiwa Wabunge ambao sisi ni Wajumbe wa Kamati ya Fedha kwamba tukiingia katika vikao vyetu, tuweze kuzisaidia Halmshauri hizi kwa sababu sisi ndio wafanya maamuzi ambao tunawawakilisha wananchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niwasihi Wabunge wote kwamba kwa moyo mkunjufu na moyo wa dhati tuzisimamie Halmashauri zetu, compliance iwepo na wananchi wetu wapate huduma na maendeleo.