Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mary Pius Chatanda

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Korogwe Mjini

Primary Question

MHE. MARY P. CHATANDA aliuliza:- Mwaka 2001, Chuo cha Ualimu Korogwe kwa kushirikiana na wananchi, walianza ujenzi wa maktaba ambayo bado haijakamilika; na kwa kuwa wanachuo na wananchi wa Korogwe wanahitaji sana maktaba hiyo:- Je, Serikali itakuwa tayari kusaidia juhudi zilizokwishaanza ili kukamilisha jengo hilo?

Supplementary Question 1

MHE. MARY P. CHATANDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Kwanza nampongeza Waziri wa Elimu na Naibu wake na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu kwa kazi nzuri ambayo wanaifanya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa basi, Mheshimiwa Naibu Waziri atakuwa tayari kufuatana nami ili aweze kuangalia lile jengo ili kusudi waweze kutoa kitu ambacho kinalingana na kazi ambayo inakusudiwa kumaliziwa?

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, jibu ni ndiyooo! (Makofi)