Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Jasson Samson Rweikiza

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Vijijini

Primary Question

MHE. JASSON S. RWEIKIZA aliuliza:- Kuna mradi mkubwa wa maji wa siku nyingi pale Maruku (Kyolelo) ambao miundombinu yake mikubwa kama matanki, mabomba chini ya ardhi na vyanzo vyake ni vizuri lakini kutokana na uchakavu mradi huo hautoi maji; mradi huo ulikuwa ukihudumia vijiji vitano katika Kata za Kanyangeneko na Maruku; kukarabati miundombinu iliyochakaa inaweza kugharimu kiasi kidogo cha fedha kama shilingi milioni 500 kwa kuhudumia vijiji vitano wakati mradi mmoja kwa kijiji kimoja wa miradi inayoendelea unagharimu zaidi ya shilingi milioni 800. Je, Serikali haioni ni busara kuukarabati mradi huu haraka?

Supplementary Question 1

MHE. JASSON S. RWEIKIZA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Spika, nafahamu kwamba lengo la Serikali ya CCM ni kuwapatia Wananchi wengi maji safi na salama kwa gharama nafuu na ndiyo maana kuna miradi ya vijiji vingi nchi nzima kila Halmashauri ya kupeleka maji kwa wananchi na miradi hii inagharimu takribani kila mradi shilingi milioni 700 au 800. Mradi huu ninaoulizia swali, ulikuwa unahudumia vijiji sita; vijiji hivyo ni Maruku, Butairuka, Bwizanduru, Bulinda, Butayaibega na Buguruka. Mradi huu kama ungekarabatiwa haraka ungegharimu kama shilingi milioni 500 au 400 kwahiyo ni gharama nafuu na maji yangepatikana kwenye vijiji vyote hivi pamoja na Chuo cha Kilimo cha Maruku, shule kadhaa zipo pale za sekondari na za msingi. Sasa Serikali haioni kama ni busara mradi huu ukarabatiwe haraka wananchi wapate maji safi na salama?

Name

Eng. Gerson Hosea Lwenge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Spika, kwanza ni kweli kwamba kuna umuhimu wa huo mradi kukarabatiwa ili uweze kutoa maji kwa namna jinsi ulivyokuwa umepangwa na kwenye jibu la msingi nimeeleza kwamba nia hiyo ipo na tayari Serikali imetenga fedha shilingi bilioni katika kuetekeleza miradi ya Halmshauri ya Bukoba lakini vipaumbele ni mradi upi wanaanza nao, wanaamua kule kule kwenye Halmshauri na kwa kuwa Waheshimiwa Wabunge ni sehemu ya Baraza la Madiwani katika kuweka vipaumbele na kwa sababu mradi huu tayari umeshakubaliwa na Serikali, kwa hiyo mimi ningeshauri kwamba uupe kipaumbele ili tukarabati na hivyo vijiji anavyosema viweze kupata maji.

Name

Ridhiwani Jakaya Kikwete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chalinze

Primary Question

MHE. JASSON S. RWEIKIZA aliuliza:- Kuna mradi mkubwa wa maji wa siku nyingi pale Maruku (Kyolelo) ambao miundombinu yake mikubwa kama matanki, mabomba chini ya ardhi na vyanzo vyake ni vizuri lakini kutokana na uchakavu mradi huo hautoi maji; mradi huo ulikuwa ukihudumia vijiji vitano katika Kata za Kanyangeneko na Maruku; kukarabati miundombinu iliyochakaa inaweza kugharimu kiasi kidogo cha fedha kama shilingi milioni 500 kwa kuhudumia vijiji vitano wakati mradi mmoja kwa kijiji kimoja wa miradi inayoendelea unagharimu zaidi ya shilingi milioni 800. Je, Serikali haioni ni busara kuukarabati mradi huu haraka?

Supplementary Question 2

MHE. RIDHIWANI J. KIKWETE: Mheshimiwa Spika, nikushukuru na mimi kupata nafasi ya kuuliza swali la nyongeza kuwa matatizo waliyonayo wananchi wa Bukoba Vijijini yanafanana moja kwa moja na matatizo waliyonayo Wananchi wa Chalinze na kwa kipindi kirefu sana wamesubiri maji na sasa hivi hawaoni kinachoendelea. Sasa swali langu, Mheshimiwa Waziri ni lini mkandarasi yule utamfukuza ili wananchi wa Chalinze wajue wanaanza upya? Swali langu la kwanza na swali la pili, nini mpango mkakati sasa wa kuwakwamua wananchi wa Chalinze? Ahsante sana.

Name

Eng. Gerson Hosea Lwenge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Spika, ni kweli pale Chalinze kuna mradi Awamu ya Tatu ambao unatekelezwa na Kampuni moja kutoka India (OIA) na utendaji wake wa kazi hauridhishi na tulikuwa tumetoa muda kwamba mpaka mwezi wa kumi awe amefikisha mahali ambapo Serikali inaweza kumruhusu au kufuta mkandarasi yule. Tunafuatilia kazi hiyo kwa karibu sana, naomba nikuhakikishie Bunge hili kwamba ikifikia mwezi wa kumi na hakuna kazi ya maana inayoendelea pale, tutachukua hatua zaidi za kimkataba.