Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Shally Josepha Raymond

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SHALLY J. RAYMOND aliuliza:- Kuna miundombinu ya kusambaza maji safi na salama iliyokamilika lakini inatoa huduma chini ya kiwango cha ujenzi wake (below design and built capacity). (a) Je, ni miradi mingapi ya maji safi na salama inayotoa huduma chini ya uwezo wa usanifu na ujenzi wake kutokana na vyanzo kupungua au kukauka maji? (b) Je, ni hatua zipi zinachukuliwa kuepusha miradi mingine kukumbwa na matatizo kama hayo?

Supplementary Question 1

MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Katika jibu lake la msingi amekiri kwamba kuna miradi 114 ambayo imekuwa haiendelei au imeharibika kabisa na katika miradi hiyo 114 mmojawapo ninaoufahamu mimi ni ule wa Kili Water kule Mkoani Kilimanjaro.
Mheshimiwa Spika, ni lini sasa Serikali itahakikisha imeukarabati mradi huo ili kuondoa adha ya Wanawake wa Tambarare ya Rombo kubeba ndoo za maji Alfajiri na mapema walio katika Kata ya kule Ngoyoni, Mamsera chini pamoja na wale ambao wako kule pembeni ya Ziwa Chala?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, tambarare yote ya Mkoa wa Kilimanjaro imekumbwa na adha hii ikiweko Wilaya ya Mwanga, Same Mjini mpaka kule Hedaru. Ni lini sasa Serikali itakamilisha ule mradi wa maji wa Ziwa la Nyumba ya Mungu ambao utapeleka maji kupitia Mwanga, Same, Hedaru mpaka Mombo?

Name

Eng. Gerson Hosea Lwenge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Spika, kwanza naomba nichukue fursa hii kwa niaba ya Serikali kumpongeza sana Mbunge kwa maana kwamba anafuatilia kuona namna gani miradi hii inawea kuathiri matumizi ya wananchi kwa maana kwamba maji yamekuwa yanapungua kwa namna hali ya hewa inavyobadilika. Kwa hiyo ni jambo ambalo ni la msingi lakini pia ni lazima tuchukue hatua. Hatua mojawapo ni lazima sisi sote tuhakikishe kwamba tunalinda vyanzo vya maji lakini pia tupande miti ambayo ni rafiki lakini pia tuvune maji ya mvua kwasababu rasilimali za maji zinapungua mwaka hadi mwaka kama hatuchukui hatua yoyote ya kukabiliana na tatizo hilo. (Makofi)
Sasa kuhusu mradi ambao unasema ni lini utakarabatiwa, Mkoa wa Kilimanjaro Serikali kwa mwaka huu wa 2017/2018 tumetengea shilingi bilioni 8.95 kwa ajili ya kumaliza miradi inayoendelea lakini pia kukarabati miradi ambayo ipo haifanyi kazi katika kiwango kwahiyo watumie fddha zile katika kuangalia vipaumbele na kuona kama wanaweza kukarabati kwa mwaka huu wa fedha vinginevyo wapange katika mwaka wa fedha unaofuata.
Kuhusu swali lake la pili, mradi wa Nyumba ya Mungu kupeleka maji Mwanga mpaka Same, sasa hivi mkandari huko mwanzo alikuwa anusua sua lakini sasa hivi anakwenda kwa kasi na nina uhakika kwamba mradi ule utakuja kukamilika lakini pia tumeanza na awamu nyingine ya kupeleka maji kule Same nayo Mkandarasi yupo site na kazi inakwenda vizuri. Serikali inafuatilia kwa nguvu zote ili miradi hii iweze kukamilika.