Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Leonidas Tutubert Gama

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Songea Mjini

Primary Question

MHE. LEONIDAS T. GAMA aliuliza:- Wananchi wangu wa Jimbo la Songea Mjini katika eneo la Matogoro, Mahiro, Lihira na Chemchem walitoa maeneo ya kilimo na makazi kwa SOUWASA ili kutengeneza bwawa la maji kwa Mji wa Songea toka mwaka 2003 na jumla ya wananchi 872 walifanyiwa uthamini wa mali na nyumba zao. Mwaka 2015 uthamini ulifanyiwa marejeo (review) na jumla ya kiasi cha shilingi 1,466,957,000 iliidhinishwa na Serikali kama madai halali ya wananchi hao lakini hadi leo ni miaka 14 imepita wananchi hao hawajapewa stahili zao. (a) Je, Serikali haioni kuwa kitendo hiki cha kutowalipa wananchi haki zao ni kuwaongezea umaskini wa kipato, malazi na kukosa uwezo wa huduma za matibabu na elimu? (b) Je, ni lini Serikali itawalipa wananchi hao stahiki yao waliyotakiwa kulipwa miaka mingi iliyopita?

Supplementary Question 1

MHE. LEONIDAS T. GAMA: Mheshimiwa Spika, naomba nichukue nafasi hii kwa niaba ya wananchi wa Songea Mjini katika maeneo hayo niliyoyataja niishukuru sana Serikali kwa kutupa matumaini kwamba fidia hiyo italipwa kipindi cha bajeti ya fedha mwaka 2018/2019. Sasa naomba niulize maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, la kwanza, katika eneo hilo wapo wananchi 157 ambao wanadai kwa namna moja ama nyingine majina yao yaliondolea kwenye eno la fidia. Sasa naomba nimuulize Mheshimiwa Waziri, je, Serikali iko tayari kufuatilia ukweli juu ya wananchi hawa 157 ili ukweli ukijulikana walipwe fidia zao?
Mheshimiwa Spika, la pili, naomba nimuulize Mheshimiwa Waziri, kwa sababu wananchi wa aneo hilo pamoja na kupata maji kutoka hilo bwawa lililotengenezwa lakini bado kuna migogoro mingi kati yao na SOUWASA. Je, Mheshimiwa Waziri yuko tayari kwenda Songea ili kukutana na wananchi wa eneo hilo ili kuwasikiliza matatizo yao na kutatua? Naomba kuwasilisha.

Name

Eng. Gerson Hosea Lwenge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Spika, kwanza Serikali inaipokea hiyo shukurani aliyoitoa, lakini kuhusu wananchi 157 ambao inaonekana wako nje ya wale 872 tutakwenda kufuatilia na ninamuomba nimuahidi Mheshimiwa Mbunge baada ya Bunge hili nitakwenda Songea, nitakwenda kuona hali halisi na tuweze kuchukua hatua kwa Wananchi wale ambao bado wanadai hiyo fidia.