Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mwita Mwikwabe Waitara

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Vijijini

Primary Question

MHE. MWITA M. WAITARA (K.n.y. MHE. ANATROPIA L. THEONEST) aliuliza:- Kuna mgogoro wa ardhi baina ya wananchi wa Kipunguni ‘A’ na Kipunguni Mashariki dhidi ya Mamlaka ya Uwanja wa Ndege Jijini Dar es Salaam. Wananchi hao wanapinga uthamini uliofanywa na fidia kidogo kwa kikundi cha watu wachache huku wengine wakizuiwa kuendeleza maeneo yao. (a) Je, ni lini Serikali itaenda kumaliza mgogoro huo uliodumu tangu mwaka 2007? (b) Je, Serikali ipo tayari kuwapa fidia ya kiwango cha soko wananchi waliozuiwa kuendeleza maeneo yao na kuendelea kubaki maskini kwa muda wote huo?

Supplementary Question 1

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.
Mheshimiwa Spika, huu ni mgogoro wa eneo ambalo limetathminiwa tangu mwaka 1997, huu ni mwaka 2017 miaka ishirini baadae.
Swali la kwanza, ni kwa nini Serikali inakataa kufanya tathmini upya katika maeneo haya hasa ukizingatia hali ya maisha ya sasa, kwamba hawa watu hata wakilipwa fidia leo hawawezi kufanya chochote kulingana na ugumu wa maisha ulivyo, kwa nini Serikali haipo tayari kufanya tathmini ya fidia ili walipwe kulingana na hali halisi ya maisha ya sasa?
Swali la pili, mgogoro huu pia umeathiri wananchi waliohamishwa kutoka Kipunguni ‘A’ kwenda Kipunguni ‘B’ Jimbo la Ukonga, Kipawa wakapelekwa Kata ya Buyuni Ukonga. Tunapozungumza hawa watu hawajalipwa fedha na walihamishwa kutoka Kipawa Kipunguni wakapelekwa Mbuyuni ambako hawakupewa tena maeneo. Sasa kuna mgogoro kati ya wananchi waliotoka Kipawa Kipunguni na wakazi wenyeji wa kule Buyuni.
Mheshimiwa Waziri yupo tayari baada ya Bunge hili au hata weekend yoyote tuambatane twende akawasikilize wananchi wenyewe awaone wanavyolalamika na kulia aone kama kuna sababu ya msingi sana ya kuchukua hatua mapema kwa kulipa fidia na kuondoa mgogoro uliopo katika eneo hilo. Nakushukuru sana. (Makofi)

Name

Eng. Edwin Amandus Ngonyani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Spika, sasa tumedhamiria kulipa fidia yote katika mwaka huu wa fedha unaoanza mwezi Julai, kwa sababu tumedhamiria tukisema tuanze kufanya uthamini upya itatuchelewesha kwa sababu kazi ya fidia nayo ni kazi ya muda mrefu.
Mheshimiwa Spika, ninawaomba sana ndugu zangu tulimalize hili suala na kwa kweli kwa namna fidia tulivyolipa ni kama tumekuja kulipa mara tatu zaidi ya ile thamani iliyokadiriwa mwanzo kwa sababu ya hiyo interest na interest ni kwa mujibu wa sheria, sehemu zote mbili kulipa kwa kufuata interest ya kila mwaka ama kuamua kufanya fidia upya zote ni njia sahihi na zote zinafuata sheria za nchi yetu.
Ninakuomba tulipe fidia kwa kufuata interest ambayo imekadiriwa kuanzia mwaka huo walipofanyiwa tathmini, najua Serikali tutaingia hasara kwa sababu tutalipa zaidi kuliko kama tungeweza kufanya evaluation upya, lakini Serikali imekubali ili tusipoteze muda tena tulimalize hilo once and for all.
Pili, nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge niko tayari baada ya kumaliza Bunge hili tupange twende tukalishughulikie suala hilo huko. (Makofi)