Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Maria Ndilla Kangoye

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARIA N. KANGOYE aliuliza:- Serikali kupitia Ilani ya CCM ya 2015 – 2020, ahadi namba 25(d) iliwaahidi vijana wafugaji kuwa itatoa dhamana ya mikopo kwenye asasi za fedha. (a) Je, Serikali imeandaa mkakati gani wa kuwawezesha vijana wafugaji kuunda vyama vya ushirika ili waweze kunufaika na ahadi hiyo ya CCM? (b) Je, Serikali inayo orodha ya vikundi vya vijana wafugaji ambao wamejiunga na vyama vya ushirika ambao wameweza kunufaika na utaratibu wowote ulioandaliwa na Serikali?

Supplementary Question 1

MHE. MARIA N. KANGOYE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipatia fursa ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza kwa niaba ya vijana wa Kitanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, ninapenda kujua ni nini mpango wa Serikali wa kuwapatia vijana wafugaji elimu ya malisho katika ufugaji endelevu? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, katika majibu ya Serikali kwa swali langu la msingi kipengele (b) ni dhahiri kwamba Mkoani Mwanza hakuna vikundi vya vijana/ wafugaji ambao wamejiunga na vyama hivi vya ushirika.
Je, ni lini Mheshimiwa Naibu Waziri atakuwa tayari kuambatana na mimi kwenda Mkoani Mwanza kukutana na maafisa vijana pamoja na maafisa ufugaji ili tuweze kutafuta namna ya kuwawezesha vijana hawa kujiunga na vyama hivyo vya ushirika?

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza, mpango wa Serikali ni nini wa kuwapatia elimu vijana wa nchi hii juu ya malisho.
Kwanza, kupitia mpango mkakati kabambe kwa maana ya Tanzania Livestock Masterplan ambao tunakwenda kuuzindua sasa katika eneo hili la malisho tumeweka msisitizo mkubwa sana. Nataka niwaambie vijana nchi nzima ya kwamba malisho ni uchumi, leo mbegu kilo moja ya malisho inauzwa takribani 15,000.
Mheshimiwa Mwenyekiti, licha ya ng’ombe mwenyewe na mazao yake, lakini uwepo wa malisho mtu ama kijana akijikita katika malisho anao uwezo na uhakika wa kupata kipato chake kitakachomsaidia katika kuendesha maisha yake. Hivyo, Serikali katika kuhakikisha hili tayari tunao mpango wa kuhakikisha mbegu za malisho zinapatikana madukani ili ziweze kuuzwa kama zinavyouzwa mbegu zingine kwa maana ya mbegu za mahindi, mpunga na nyinginezo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili la Mheshimiwa Maria Kangoye ni kwenda Mwanza kukutana na kuwahamasisha vijana juu ya shughuli za ufugaji na uandaaji wa malisho; nataka nimhakikishie Mheshimiwa Kangoye niko tayari hata baada tu ya kumaliza Bunge hili kuambatana naye kuelekea Mwanza.