Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Amb Dr. Diodorus Buberwa Kamala

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkenge

Primary Question

MHE.BALOZI DKT. DIODORUS B. KAMALA aliuliza:- Kupitia vikao vya Jumuiya ya Afrika Mashariki, mwaka 2015 Serikali ya Kenya iliruhusiwa na Jumuiya hiyo kuuza ndani ya nchi hiyo bila kutozwa kodi bidhaa za ngozi na nguo zinazozalishwa nchini humo kwenye maeneo huru ya uwekezaji (Export Processing Zones [EPZ]). Je, ni sababu zipi za msingi zilizotumika kufanya uamuzi huo?

Supplementary Question 1

MHE. BALOZI DKT. DIODORUS B. KAMALA: Mheshimiwa
Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu lakini ninayo maswali mawili madogo ya nyongeza.
Kwa kuwa Kenya iliruhusiwa kuuza bidhaa zake zinazozalishwa EPZ asilimia 20 bila kodi jambo ambalo alitakiwi, lakini kwa nini wakati huo huo baada ya muda mfupi Kenya hiyo hiyo ikaruhusiwa mitumba inayotaka nje badala ya kutozwa senti 40 kwa kilo watoze senti 20 kwa kilo?
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa nchi za Ethiopia, Afrika ya Kusini, India, Morocco na nyinginezo zinatoa mkakati maalum wa kusaidia viwanda vya nguo na ngozi ili watu waweze kuwekeza kwenye sekta hizo kwa kutoa garantees walau ya miezi ya sita na baadaye Serikali inajiondoa na wazalishaji wanaendelea na kwa kufanya hivyo Ethiopia na nchi nyingine zimefanya vizuri Je, Tanzania tuko tayari walau kujifunza kidogo kutoka katika nchi hizo?

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza suala la nguo pamoja na mitumba ni suala ambalo ni nyeti na suala ambalo linahusu viwanda vyetu vya Afrika Mashariki kwa ujumla. Kimsingi ni kwamba kufuatia maombi hayo kumekuwa na mambo mengine ambayo yameendelea ambayo yameendelea kujadiliwa na nchi. Lakini kubwa zaidi ni kama nilivyosema awali kwamba swala hilo lilikuwa limejadiliwa na Wakuu wetu wananchi.
Kwa hiyo, mabadiliko mengine yoyote yale ni muhimu lazima yarudi tena kwa wakuu wetu wa nchi na misingi hiyo naamini kwamba Serikali kwa kushirikiana na nchi ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kwa ujumla wake tutapata ufumbuzi wa mambo ambayo yanayoonekana labda pengine yanakuja kuwa ni kikwazo hasa katika kuhakikisha kwamba bidhaa zinazotoka kwenye nchi zetu zinalindwa vilevile.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili kuhusiana na kujifunza kutoka nchi nyingine za Morocco na kadhalika. Kimsingi wajasiriamali hawa wawekezaji wanapokuja kwenye nchi wanakuja na mitaji lakini wanakutana na sheria mbalimbali ambazo kwa upande mmoja zinakuwa zinasaidia kuwezesha uwekezaji huo, lakini upande mwingine inaweza ikatokea kwamba kuna vikwazo na sisi tumekuwa tukiendelea kujifunza na kuona namna bora zaidi ya kuwasaidia wawekezaji wetu ili waweze kukua na kuendeleza viwanda vinavyowekezwa na ajira kwa ujumla.
Kwa hiyo, ni wazo jema tutaendelea kujifunza na vilevile kuona namna bora kadri inavyoonekana kila siku ya kuweza kuwasaidia wawekezaji wetu.