Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Zainab Mndolwa Amir

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ZAINAB M. AMIR aliuliza:- Mboga za majani ni lishe bora kwa afya ya binadamu na wakulima wengi wa mbogamboga katika Jiji la Dar es Salaam wanatumia maji yasiyo salama kwa ajili ya kumwagilia na huenda maji hayo yana kemikali zinazoweza kusababisha mbogamboga hizo kudhuru afya za wananchi badala ya kuziimarisha:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuwapatia maji safi na salama wakulima hao wa mbogamboga?

Supplementary Question 1

MHE. ZAINAB M. AMIR: Mheshimiwa Spika, ahsante. Namshukuru Naibu Waziri kwa majibu yake mazuri. Kutokana na umuhimu wa mboga za majani kwa afya ya binadamu na ukizingatia maeneo mengi ya Dar es Salaam mboga hizo hulimwa mabondeni na kipindi cha mvua kuna mafuriko yanayoharibu mboga hizo. Je, ni lini Serikali itatenga maeneo maalum ambayo wakulima hawa watalima? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, je, Serikali ina mkakati gani wa kuwapatia wakulima hao mikopo ambayo itasaidia kulimo kilimo chenye tija na chenye kuzingatia afya ya mlaji? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

Name

Jumaa Hamidu Aweso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Pangani

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Spika, moja ya mikakati ya Serikali ni kuhakikisha kwamba inawatengea wananchi, hasa wajasiriamali wakiwemo wakulima wa mbogamboga na hili linafanywa na halmashauri au manispaa husika. Kwa hiyo ni suala zima la ufuatiliaji ili kuhakikisha kwamba wananchi wetu wanaweza kupata maeneo sahihi ili wananchi wa Dar es Salaam waweze kunufaika na kilimo cha mbogamboga.
Mheshimiwa Spika, swali la pili kuhusu suala zima la mikopo; bila ya nyezo huwezi kutoka, kuna namna bora ya kuhakikisha kwamba tunawasaidia wananchi wetu ili waweze kupata mikopo. Hili linatokana na halmashauri husika kwa kutenga asilimia tano za vijana na akinamama, ila kubwa sasa nimwombe Mheshimiwa Mbunge kushirikiana nao kusimamia fedha hizo ili waweze kupata na ziweze kuwasaidia wakulima wetu.
Mheshimiwa Spika, ahsante sana.