Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Omar Abdallah Kigoda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Handeni Mjini

Primary Question

MHE. OMARI A. KIGODA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani juu ya barabara ya Handeni – Mzika – Dumila na ile ya Handeni – Kiberashi, hasa ikizingatiwa kuwa upembuzi yakinifu umeshafanyika tangu kipindi cha uongozi wa Awamu ya Nne?

Supplementary Question 1

MHE. OMARI A. KIGODA: Mheshimiwa Naibu Spika, asante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali langu la kwanza, kwa kuwa, Wakandarasi wakipewa kazi huwa wanapewa na time frame ya kumaliza ile kazi, hii barabara imeshafanyika kwa asilimia 69, naomba Mheshimiwa Waziri anipe jibu asilimia 31 iliyobaki atakabidhiwa lini na Mkandarasi?
Swali la pili, kwa kuwa, Wataalam wamethibitisha tairi za super single zinazofungwa kwenye malori zina uharibifu mkubwa sana wa barabara zetu. Je, ni lini Serikali itatoa maamuzi kuhusu hizo tairi ambazo zinaharibu barabara zetu zinazo-cost hela nyingi sana za wananchi? Ahsante sana.

Name

Eng. Edwin Amandus Ngonyani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, time frame ya kukamilisha barabara hii hivi sasa iko katika majadiliano kutokana na kuchelewa kwa Serikali kumlipa Mkandarasi kulikotokea katika kipindi kilichopita na hivyo, alivyorudi sasa tutapata muda kamili wa kukamilisha barabara hii kutokana na majadiliano yanayoendelea hivi sasa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa suala la matairi ya super single, Serikali hivi sasa inangalia uwezekano wa kubadilisha kanuni zinazotumika kwa sasa ama kupunguza kiwango cha uzito utakaotumika kwa super single badala ya kutumia kile kiwango cha matairi mawili, kipungue chini ya matairi mawili ama kupiga marufuku kabisa. Kwa hiyo, hilo tunalishughulikia na mara Kanuni hizo na baada ya kujadiliana na wadau kutakapokamilika, tutalijulisha Bunge lako maamuzi yatakayotokea.