Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Abdallah Ally Mtolea

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Temeke

Primary Question

MHE. ABDALLAH A. MTOLEA aliuliza:- Serikali inajitahidi kujenga barabara ili kupunguza foleni pamoja na kurahisisha usarifi na usafirishaji, lakini barabara zinawekwa matuta ambayo siyo rafiki kwa vyombo vya usafiri jambo linalosababisha baadhi ya watumiaji wa barabara hizo kuzikimbia, kwa mfano, matuta yaliyowekwa katika barabara ya Msata – Bagamoyo:- Je, matuta ni sehemu ya alama za barabarani?

Supplementary Question 1

MHE. ABDALLAH A. MTOLEA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali ambapo imekiri uwepo wa matuta hayo ambayo siyo rafiki barabarani na wameanza kuchukua jitihada, nilitaka kujua ni lini sasa Serikali itakuwa imemaliza kuyapitia na kuyarekebisha matuta yaliyopo kwenye barabara ya Msata – Bagamoyo?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; hivi karibuni Jeshi la Polisi kwa kupitia Kitengo chake cha Usalama Barabarani, wamekuwa wakifanya kazi nzuri ya kuwadhibiti madereva wakorofi. Je, pamoja na kazi nzuri hii ya Jeshi la Polisi bado tunaona kuna tija ya kuendelea kuweka matuta kwenye barabara kuu?

Name

Elias John Kwandikwa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ushetu

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyojibu katika jibu langu la msingi, tunaendelea kuyatoa matuta yote ambayo yameonekana kwamba hayafai kulingana na mwongozo ambao tumeutoa. Nimhakikishie tu Mheshimiwa Mtolea kwamba muda siyo mrefu tutakamilisha kazi hii kwa sababu mpaka hivi ninavyoongea, tuko karibu asilimia 90 ya matuta yote ambayo tuliyatambua kwamba ni hatarishi. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge uvute subira kwa sababu kuyatoa matuta haya pia ni gharama; tutaendelea kuyatoa matuta yote sehemu hiyo uliyosema kutoka Msata kwenda Bagamoyo na maeneo mengine nchini. Kwa hiyo, vuta subira kasi yetu ni nzuri, tutayatoa matuta yote.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali lake la pili, kwanza namshukuru sana Mheshimiwa Mtolea kwa kutambua na kuona udhibiti wa madereva tunaoufanya Serikali kupitia Mambo ya Ndani na sisi upande wa ujenzi. Mimi kama Makamu wa Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani, tunahakikisha kwamba kwanza wananchi wanabaki salama, watumiaji wengine wa barabara wanabaki salama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Mheshimiwa tutaendelea kufanya udhibiti ili kuhakikisha kwamba wananchi wanakuwa salama kwanza, halafu tuendelee na hatua nyingine. Kwa hiyo, ni muhimu sana kuhakikisha watu wetu wanakuwa salama. Kwa hiyo, tutaendela kudhibiti na kuhakikisha kwamba wananchi wanakuwa salama.